< Return to Video

Uponyaji na Ukombozi wa PAPO HAPO Kupitia Zoom!

  • 0:00 - 0:08
    Kwa Jina Kuu la Yesu Kristo!
  • 0:08 - 0:15
    Pona kwa Jina La Yesu
  • 0:15 - 0:22
    Kila Roho isiyo ya Mungu , Toka kwa jina La Yesu!
  • 0:22 - 0:25
    Toka sasa!
  • 0:25 - 0:31
    Yesu Kristo , tunakuomba nguvu zako za uponyaji gusa kila mahali palipo haribika .
  • 0:31 - 0:42
    Mahali popote viungo vilipoharibika ! nasema anza kufanya kazi sasa!
  • 0:42 - 0:49
    Kwa Jina la Yesu Kristo
  • 0:49 - 1:00
    Sasa, roho mchafu , nasema toka kwa jina La Yesu Kristo!
  • 1:00 - 1:08
    Asante Yesu , kwa uhuru.
  • 1:08 - 1:12
    Kwa Kuu Jina La Yesu .
  • 1:12 - 1:17
    sasa mku huru . Kaka nataka ujiangalie .
  • 1:17 - 1:21
    Roho wa Mungu amegusa sehemu ya mwili iliyo kua na maumivu .
  • 1:21 - 1:25
    Jiangalie na ufurahie . furahia utukufu wa Mungu
  • 1:25 - 1:29
    Dada yetu , Mungu amekukomboa na kumweka mume wako huru
  • 1:29 - 1:36
    Unaweza amka na kufurahia sasa, uko huru kwa jina la Yesu.
  • 1:37 - 1:43
    Tafadhali tuambie nchi uliyotokea , na mtu aliye keti kando yako
  • 1:43 - 1:51
    Jina langu ni Shadreck: Mwanamke alikaa kando yangu ni mke wangu mpendwa , Naomi . Tunatokea Zambia.
  • 1:51 - 1:56
    Yote yalianza miaka sita iliyopita , nilipokua kazini (kwenye chimbo chini ya ardhi)
  • 1:56 - 2:01
    kwa sababu taaluma yangu ni ukarabati wa vifaa vizito,
  • 2:01 - 2:04
    maana yake natengeneza mashine za kazi nzito.
  • 2:04 - 2:09
    Nilipokua nafanya kazi ndani ya chimbo hilo , kwa ghafla nikasikia uchungu mkali mno.
  • 2:09 - 2:15
    kutokea bega langu la kushoto kwenda chini kwenye mguu wangu wa kushoto
  • 2:15 - 2:22
    Sikuweza kutembea - nikaviangusha chini vifaa vya kazi
  • 2:22 - 2:25
    sababu sikuweza kufanya kitu chochote wakati huo
  • 2:25 - 2:30
    Huo ulikua mwanzo wa zamu yangu kazini , nilitakiwa kufanya kazi kwa mda wa masaa nane.
  • 2:30 - 2:34
    Hayo yalitokea dakika chache baada ya kuanza zamu yangu kazini
  • 2:34 - 2:41
    Ilinilazimu kukaa chini na sikuweza kufanya kitu chochote mpaka masaa yangu ya zamu kazini yakaisha,
  • 2:41 - 2:46
    Nilitarajia kua labda uchungu huo ulikua tu mojawapo ya vitu vya kupita.
  • 2:46 - 2:50
    Siku iliyofuata , uchungu ulikua bado upo.
  • 2:50 - 2:54
    Nilienda hospitalini wakanipa dawa ya maumivi (Vituliza maumivu )
  • 2:54 - 3:01
    Baada ya siku tatu nilidhani labda maumivu yangetoweka, lakini ndipo yalipozidi kuwa makali,
  • 3:01 - 3:06
    Singeweza hata kutembea - kutembea ilikua tatizo hata kuinama sikuweza.
  • 3:06 - 3:10
    Hata kulala- nilikua sina raha.
  • 3:10 - 3:15
    Singeweza kuchukua chochote sakafuni , hata kama kingekua kidogo kama chupa.
  • 3:15 - 3:19
    Kingeanguka sakafuni, ningeomba mtu mwingine kunichukulia.
  • 3:19 - 3:26
    NIlipokua nikioga , ilinilazimu kuketia stuli (Kigoda) sababu ilikua vigumu kwangu kuinama.
  • 3:26 - 3:32
    Hali ilikua mbaya , huku nikitafuta matibabu ya kiafya kwa miaka mbili.
  • 3:32 - 3:37
    Nilikua mara kwa mara nikienda Hospitalini kuona wauguzi
  • 3:37 - 3:50
    Tabibu wa kwanza aliniambia aliona kukunjika kwa uti wa mgongo kusiko kua kwa kawaida.
  • 3:50 - 3:53
    Yeye ndiye aliye gundua ulemavu huo wa uti wa mgongo(Skoliosisi)
  • 3:53 - 3:59
    Sikuweza kufanya chochote kazini na karibu nipoteze kazi.
  • 3:59 - 4:01
    Sababu singeweza kufanya chochote sikua nasaidia katika uzalishaji kazini
  • 4:01 - 4:09
    Ilinibiddi nihamishwe kutoka idara yangu kwenda idara ingine
  • 4:09 - 4:16
    Nilipofika idara yangu mpya hawakujua kamwe kwamba nilikuwa nikikabili tatizo hilo zito.
  • 4:16 - 4:19
    Waliona tu nikienda hospitalini.
  • 4:19 - 4:22
    Kila mara , sababu niliwekwa chini ya matibabu.
  • 4:22 - 4:29
    Niliwekwa chini ya matibabu ya mifupa ya mwili , ikanilazimu kwenda kwa matibabu mara tatu kwa wiki.
  • 4:29 - 4:35
    Hata kama walinifanyia hayo yote sikupata nafuu.
  • 4:35 - 4:40
    Sababu saa zingine singeweza kutembea hata mita mia moja
  • 4:40 - 4:44
    Ningetembea mita mia moja , ingenilazimu kuketi chini nipumzike.
  • 4:44 - 4:53
    Nililazimika kutumwa kwa picha ya MRI kuona picha kamili ya shida hiyo
  • 4:53 - 5:05
    Kwa Picha hiyo ya MRI ilionesha uti wa mgongo upande wa chini ulikunjika visivyo.
  • 5:05 - 5:16
    Hii ndiyo repoti ya hospitalini niliyopewa.
  • 5:16 - 5:23
    Ripoti hii nilipewa Sinozam Friendship Hospital na inasema report ya MRI
  • 5:23 - 5:31
    Jina langu na miaka iko hapo . inaonesha utafiti uliofanywa.
  • 5:31 - 5:37
    Ambayo ni MRI ya uti wa mgongo upande wa chini .
  • 5:37 - 5:43
    Hii ndiyo repoti iliyo kuja na haikua ya kuridhisha.
  • 5:43 - 5:50
    'Taswira: Uharibifu mdogo wa uti wa mgongo wa L2',
  • 5:50 - 5:56
    ikimaanisha kuwa kulikuwa na hali isiyo ya kawaida kwenye sehemu ya chini ya mgongo wangu.
  • 5:56 - 6:03
    Hii shida ilisababisha shida nyingi , nilifikiria iwapo nikipoteza kazi
  • 6:03 - 6:09
    Singeweza kufanya lolote , hata kutafuta kazi kwingine.
  • 6:09 - 6:16
    Hali ilikua mbaya ilinibidi nitafute suluhisho mbadala.
  • 6:16 - 6:25
    Nikiwa katika mchakato huu, nilikutana na Huduma ya Maombi ya God's Heart TV.
  • 6:25 - 6:31
    Nilitaka kujua nitakavyo weza kua miongoni mwa watu wapokeao maombi.
  • 6:31 - 6:35
    Nilingundua kua baada ya kuwasilisha ombi langu la kupokea maombi , nilipokea mwaliko.
  • 6:35 - 6:42
    Nilitumia mwaliko huo kujiunga na ibada ya maombi tarehe 24th mwezi wa tisa 2023
  • 6:42 - 6:47
    Kama mlivyo ona kwenye video fupi hapo awali nilipokua nikiombewa.
  • 6:47 - 6:53
    Alipokua anatuombea Ndugu Chris sikusikia chochote wakati huo
  • 6:53 - 7:00
    lakini niligundua kuwa mke wangu alikuwa ameanguka sakafuni na niliombwa nimsimamishe.
  • 7:00 - 7:04
    Kisha mtu wa Mungu akatuombea. Aliniomba nifanye mazoezi mwenyewe,
  • 7:04 - 7:08
    Nilikua mwoga kwa mara ya kwanza sababu sikusikia kitu ama kujua
  • 7:08 - 7:12
    Kua kitu cha tofauti kimetendeka mwilini mwangu
  • 7:12 - 7:17
    Nikajarubu kuinama na kufanya mazoezi na sikusikia uchungu
  • 7:17 - 7:23
    Lakini hiyo haikutosha , nilipopokea maombi niligundua kua
  • 7:23 - 7:29
    Kusumbuka na uchungu wote ulikua umeisha
  • 7:29 - 7:34
    Niliweza kuketi , kufanya mazoezi , kukimbia na kuinama
  • 7:34 - 7:40
    Usiku huo nililala kama mtoto, nilipoamka nilijiskia huru.
  • 7:40 - 7:55
    Naweza kuinua mikono, kuinama , kufanya mazoezi , kuchukua kitu sakafuni
  • 7:55 - 8:02
    Niko huru kabisa - hakuna chochote kinachozuia harakati zangu za mwili kwa sasa.
  • 8:02 - 8:08
    Jina langu ni Naomi , natoka Zambia
  • 8:08 - 8:16
    Shida nilio kua nayo kabla ya kupokea maombi kutoka kwa Ndugu Chris.
  • 8:16 - 8:23
    Nilikua na uchungu mwilini wote , nilihisi uchungu siku zote.
  • 8:23 - 8:33
    Kichwa kuuma , mabega kuuma na ndoto mbaya
  • 8:33 - 8:41
    Wakati wa ibada ya maombi , mtu wa mungu alituombea.
  • 8:41 - 8:47
    Aliniwekelea mkono na nikajipata sakafuni.
  • 8:47 - 8:52
    Tangu wakati huo, maumivu ambayo nilikuwa nikisikia hayakuwepo tena.
  • 8:52 - 9:01
    Nimekombolewa kutoka kwenye maumivu na ndoto mbaya; ndoto mbaya nilizokuwa nazo zimetoweka!
  • 9:01 - 9:07
    Namshukuru huyu Yesu ameniweka huru na niko hapa kama ushuhuda ulio hai.
  • 9:07 - 9:18
    Ushauri wangu kwa watazamaji ni kuja kwa Mungu na moyo safi, uliojaa imani.
  • 9:18 - 9:23
    Mwamini Mungu, kwa sababu tunamtumikia Mungu aliye hai ambaye hashindwi kamwe.
  • 9:23 - 9:30
    Unapokumbana na matatizo yoyote katika maisha yako, tafuta uso wa Mungu.
  • 9:30 - 9:39
    Ushauri wangu kwa watazamaji wanaotazama ni kwamba umbali sio kikwazo.
  • 9:39 - 9:42
    Sharti pekee linalohitajika ni kuamini tu.
  • 9:42 - 9:49
    Ikiwa utaamini, leo masuala yako yote, shida na magonjwa yatakuwa jambo la zamani.
Title:
Uponyaji na Ukombozi wa PAPO HAPO Kupitia Zoom!
Description:

Baada ya miaka sita ya maumivu ya mgongo kwa muda mrefu kutokana na 'scoliosis', Shadreck kutoka Zambia alipokea muujiza wa papo hapo baada ya kujiunga na Huduma ya Maombi ya PAmoja na Ndugu Chris. Mkewe pia alikombolewa kutokana na roho iliyomsababishia ndoto mbaya na maumivu ya mwili kwa ujumla. Utiwe moyo katika imani yako na ushuhuda wao!

Je, unataka kujiunga na Huduma ya Maombi Shirikishi na Ndugu Chris ili kupokea maombi kupitia Zoom? Tuma ombi lako la maombi hapa - https://www.godsheart.tv/zoom

#Ushuhuda

➡️ Pata Kutiwa Moyo Kila Siku kwenye WhatsApp - https://godsheart.tv/whatsapp/
➡️ Saidia TV ya Moyo wa Mungu kifedha - https://godsheart.tv/financial/
➡️ Habari kuhusu Maombi Shirikishi - https://godsheart.tv/interactive-prayer/
➡️ Jitolee kama Mtafsiri wa TV ya Moyo wa Mungu - https://godsheart.tv/translate/
➡️ Shiriki shaushuhuda wako - https://godsheart.tv/testimony
➡️ Jiunge na Ibada yetu ya Maombi ya Moja kwa Moja Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi - https://www.youtube.com/godshearttv/live

more » « less
Video Language:
English
Team:
God's Heart TV
Duration:
10:19

Swahili subtitles

Revisions Compare revisions