Uponyaji na Ukombozi wa PAPO HAPO Kupitia Zoom!
-
0:00 - 0:08Kwa Jina Kuu la Yesu Kristo!
-
0:08 - 0:15Pona kwa Jina La Yesu
-
0:15 - 0:22Kila Roho isiyo ya Mungu , Toka kwa jina La Yesu!
-
0:22 - 0:25Toka sasa!
-
0:25 - 0:31Yesu Kristo , tunakuomba nguvu zako za uponyaji gusa kila mahali palipo haribika .
-
0:31 - 0:42Mahali popote viungo vilipoharibika ! nasema anza kufanya kazi sasa!
-
0:42 - 0:49Kwa Jina la Yesu Kristo
-
0:49 - 1:00Sasa, roho mchafu , nasema toka kwa jina La Yesu Kristo!
-
1:00 - 1:08Asante Yesu , kwa uhuru.
-
1:08 - 1:12Kwa Kuu Jina La Yesu .
-
1:12 - 1:17sasa mku huru . Kaka nataka ujiangalie .
-
1:17 - 1:21Roho wa Mungu amegusa sehemu ya mwili iliyo kua na maumivu .
-
1:21 - 1:25Jiangalie na ufurahie . furahia utukufu wa Mungu
-
1:25 - 1:29Dada yetu , Mungu amekukomboa na kumweka mume wako huru
-
1:29 - 1:36Unaweza amka na kufurahia sasa, uko huru kwa jina la Yesu.
-
1:37 - 1:43Tafadhali tuambie nchi uliyotokea , na mtu aliye keti kando yako
-
1:43 - 1:51Jina langu ni Shadreck: Mwanamke alikaa kando yangu ni mke wangu mpendwa , Naomi . Tunatokea Zambia.
-
1:51 - 1:56Yote yalianza miaka sita iliyopita , nilipokua kazini (kwenye chimbo chini ya ardhi)
-
1:56 - 2:01kwa sababu taaluma yangu ni ukarabati wa vifaa vizito,
-
2:01 - 2:04maana yake natengeneza mashine za kazi nzito.
-
2:04 - 2:09Nilipokua nafanya kazi ndani ya chimbo hilo , kwa ghafla nikasikia uchungu mkali mno.
-
2:09 - 2:15kutokea bega langu la kushoto kwenda chini kwenye mguu wangu wa kushoto
-
2:15 - 2:22Sikuweza kutembea - nikaviangusha chini vifaa vya kazi
-
2:22 - 2:25sababu sikuweza kufanya kitu chochote wakati huo
-
2:25 - 2:30Huo ulikua mwanzo wa zamu yangu kazini , nilitakiwa kufanya kazi kwa mda wa masaa nane.
-
2:30 - 2:34Hayo yalitokea dakika chache baada ya kuanza zamu yangu kazini
-
2:34 - 2:41Ilinilazimu kukaa chini na sikuweza kufanya kitu chochote mpaka masaa yangu ya zamu kazini yakaisha,
-
2:41 - 2:46Nilitarajia kua labda uchungu huo ulikua tu mojawapo ya vitu vya kupita.
-
2:46 - 2:50Siku iliyofuata , uchungu ulikua bado upo.
-
2:50 - 2:54Nilienda hospitalini wakanipa dawa ya maumivi (Vituliza maumivu )
-
2:54 - 3:01Baada ya siku tatu nilidhani labda maumivu yangetoweka, lakini ndipo yalipozidi kuwa makali,
-
3:01 - 3:06Singeweza hata kutembea - kutembea ilikua tatizo hata kuinama sikuweza.
-
3:06 - 3:10Hata kulala- nilikua sina raha.
-
3:10 - 3:15Singeweza kuchukua chochote sakafuni , hata kama kingekua kidogo kama chupa.
-
3:15 - 3:19Kingeanguka sakafuni, ningeomba mtu mwingine kunichukulia.
-
3:19 - 3:26NIlipokua nikioga , ilinilazimu kuketia stuli (Kigoda) sababu ilikua vigumu kwangu kuinama.
-
3:26 - 3:32Hali ilikua mbaya , huku nikitafuta matibabu ya kiafya kwa miaka mbili.
-
3:32 - 3:37Nilikua mara kwa mara nikienda Hospitalini kuona wauguzi
-
3:37 - 3:50Tabibu wa kwanza aliniambia aliona kukunjika kwa uti wa mgongo kusiko kua kwa kawaida.
-
3:50 - 3:53Yeye ndiye aliye gundua ulemavu huo wa uti wa mgongo(Skoliosisi)
-
3:53 - 3:59Sikuweza kufanya chochote kazini na karibu nipoteze kazi.
-
3:59 - 4:01Sababu singeweza kufanya chochote sikua nasaidia katika uzalishaji kazini
-
4:01 - 4:09Ilinibiddi nihamishwe kutoka idara yangu kwenda idara ingine
-
4:09 - 4:16Nilipofika idara yangu mpya hawakujua matatizo ya kiafya yaliyo nikumba.
-
4:16 - 4:19Waliona tu nikienda hospitalini.
-
4:19 - 4:22Kila mara , sababu niliwekwa chini ya matibabu.
-
4:22 - 4:29Niliwekwa chini ya matibabu ya mifupa ya mwili , ikanilazimu kwenda kwa matibabu mara tatu kwa wiki.
-
4:29 - 4:35Hata kama walinifanyia hayo yote sikupata nafuu.
-
4:35 - 4:40Sababu saa zingine singeweza kutembea hata mita mia moja
-
4:40 - 4:44Ningetembea mita mia moja , ingenilazimu kuketi chini nipumzike.
-
4:44 - 4:53Nililazimika kutumwa kwa picha ya MRI kuona picha kamili ya shida hiyo
-
4:53 - 5:05Kwa Picha hiyo ya MRI ilionesha uti wa mgongo upande wa chini ulikunjika visivyo.
-
5:05 - 5:16Hii ndiyo repoti ya hospitalini niliyopewa.
-
5:16 - 5:23Ripoti hii nilipewa Sinozam Friendship Hospital na inasema report ya MRI
-
5:23 - 5:31Jina langu na miaka iko hapo . inaonesha utafiti uliofanywa.
-
5:31 - 5:37Ambayo ni MRI ya uti wa mgongo upande wa chini .
-
5:37 - 5:43Hii ndiyo repoti iliyo kuja na haikua ya kuridhisha.
-
5:43 - 5:50Kuonesha : Mild wedge-formed deformation of L2 vertebral bone’,
-
5:50 - 5:56Inamanisha hali isyokua ya kawaida pande ya chini ya uti wa mgongo.
-
5:56 - 6:03Hii shida ilisababisha shida nyingi , nilifikiria iwapo nikipoteza kazi
-
6:03 - 6:09Singeweza kufanya lolote , hata kutafuta kazi kwingine.
-
6:09 - 6:16Hali ilikua mbaya ilinibidi nitafute suluhisho mbadala.
-
6:16 - 6:25Katika hali hiyo , nilipata kujua maombi yafanyikayo God's Heart TV
-
6:25 - 6:31Nilitaka kujua nitakavyo weza kua miongoni mwa watu wapokeao maombi.
-
6:31 - 6:35Nilingundua kua baada ya kusalimisha ombi langu la kupokea maombi , nilipokea mwaliko.
-
6:35 - 6:42Nilitumia mwaliko huo kujiunga na ibada ya maombi tarehe 24th mwezi wa tisa 2023
-
6:42 - 6:47Kama mlivyo ona kwenye video fupi hapo awali nilipokua nikiombewa.
-
6:47 - 6:53Alipokua anatuombea Ndugu Chris sikusikia chochote wakati huo
-
6:53 - 7:00Lakini niligundua kua mke wangu alikua ameanguka sakafuni na niliomwa kumwokota.
-
7:00 - 7:04Mtumishi wa mungu alituombea , na akaniamrisha nijifanyishe mazoezi ya mwili
-
7:04 - 7:08Nilikua mwoga kwa mara ya kwanza sababu sikusikia kitu ama kujua
-
7:08 - 7:12Kua kitu cha tofauti kimetendeka mwilini mwangu
-
7:12 - 7:17Nikajarubu kuinama na kufanya mazoezi na sikusikia uchungu
-
7:17 - 7:23Lakini hiyo haikutosha , nilipopokea maombi niligundua kua
-
7:23 - 7:29Kusumbuka na uchungu wote ulikua umeisha
-
7:29 - 7:34Niliweza kuketi , kufanya mazoezi , kukimbia na kuinama
-
7:34 - 7:40Usiku huo nililala kama mtoto, nilipoamka nilijiskia huru.
-
7:40 - 7:55Naweza kuinua mikono, kuinama , kufanya mazoezi , kuchukua kitu sakafuni
-
7:55 - 8:02Niko huru kabisa- hakuna kitu kinachosumbua kufanya chochote mwilini
-
8:02 - 8:08Jina langu ni Naomi , natoka Zambia
-
8:08 - 8:16Shida nilio kua nayo kabla ya kupokea maombi kutoka kwa Ndugu Chris.
-
8:16 - 8:23Nilikua na uchungu mwilini wote , nilihisi uchungu siku zote.
-
8:23 - 8:33Kichwa kuuma , mabega kuuma na ndoto mbaya
-
8:33 - 8:41Wakati wa ibada ya maombi , mtu wa mungu alituombea.
-
8:41 - 8:47Aliniwekelea mkono na nikajipata sakafuni.
-
8:47 - 8:52Kutokea wakati huo , uchungu niliokua na hisi haupo tena
-
8:52 - 9:01, kutoka kwa uchungu na ndoto za kutisha, Ndoto mbaya nilizokua nazo zimetoweka
-
9:01 - 9:07Namshukuru huyu Yesu ameniweka huru na niko hapa kama ushuhuda ulio hai.
-
9:07 - 9:18Ushauri wangu kwa watazamaji ni kumwendea Mungu na moyo safi , na mwenye kuamini
-
9:18 - 9:23Amini Mungu , sababu tunamtumikia Mungu asiye shindwa,
-
9:23 - 9:30Unapopata shida yeyote kwa maisha , utafute uso wa Mungu
-
9:30 - 9:39Ushauri wangu kwa watazamaji ni kwamba umbali wako sio kikwazo.
-
9:39 - 9:42Unatakiwa tu kuamini
-
9:42 - 9:49Unapoamini leo shida zako zote na magonjwa inakua jambo la zamani.
- Title:
- Uponyaji na Ukombozi wa PAPO HAPO Kupitia Zoom!
- Description:
-
Baada ya miaka sita ya uchungu wa uti wa mgongo , Shadreck kutoka zambia alipokea muuzija baada ya kujiunga na ibada ya maombi iliofanywa na Ndugu Chris.Bibi yake pia alikombolewa na roho iliyomsababishia ndoto mbaya na uchungu mwilini mwake, Himizwa kiimani na ushuhuda huu
- Video Language:
- English
- Team:
- God's Heart TV
- Duration:
- 10:19
georgejbudeba edited Swahili subtitles for INSTANT Healing & Deliverance Through Zoom! | ||
georgejbudeba edited Swahili subtitles for INSTANT Healing & Deliverance Through Zoom! | ||
georgejbudeba edited Swahili subtitles for INSTANT Healing & Deliverance Through Zoom! | ||
georgejbudeba edited Swahili subtitles for INSTANT Healing & Deliverance Through Zoom! | ||
georgejbudeba edited Swahili subtitles for INSTANT Healing & Deliverance Through Zoom! | ||
georgejbudeba edited Swahili subtitles for INSTANT Healing & Deliverance Through Zoom! | ||
georgejbudeba edited Swahili subtitles for INSTANT Healing & Deliverance Through Zoom! | ||
georgejbudeba edited Swahili subtitles for INSTANT Healing & Deliverance Through Zoom! |