Wade Davis na Tamaduni Zilizo Hatarini Kupotea
-
0:00 - 0:03Kama ujuavyo, moja ya raha kubwa za kusafiri
-
0:03 - 0:05na moja ya furaha za utafiti wa mahusiano ya kikabila
-
0:05 - 0:07ni fursa ya kuishi miongoni mwao
-
0:07 - 0:09hao wasiosahau namna za kijadi
-
0:09 - 0:12ambao wangali wakihisi ya kale kwenye upepo,
-
0:12 - 0:15na kuyagusa juu ya mawe yaliyosafishwa na mvua,
-
0:15 - 0:17na kuyaonja kwenye majani machungu ya mimea.
-
0:17 - 0:21Kujua kwamba wanaoabudu chuipamba bado wana safari kupita mbingu za mbali,
-
0:21 - 0:25au imani za wazee wa Kiinuiti zinaleta maana,
-
0:25 - 0:27au kwamba huko Himalaya,
-
0:28 - 0:32Mabudha bado wanaifuata pumzi ya Dharma,
-
0:32 - 0:35ni katika kukumbuka utambuzi wa msingi wa anthropolojia,
-
0:35 - 0:37na kwamba mtazamo wa ulimwengu tunamoishi
-
0:38 - 0:40haupo kihalisia,
-
0:40 - 0:41bali ni nadharia tu ya ukweli,
-
0:41 - 0:45ni matokeo ya jozi moja tu ya machaguo kadhaa
-
0:45 - 0:49ambayo mababu zetu walifanya, japo kwa mafanikio, vizazi kadhaa vilivyopita.
-
0:50 - 0:54Na kwa hakika, sote tunashabihiana katika kufuata kanuni za maumbile
-
0:54 - 0:56Sote tunazaliwa. Sote tunazaa watoto.
-
0:56 - 0:58Tunapitia kafara za kusimikwa,
-
0:58 - 1:00Tunalazimika kukabiliana na ukatili wa kutenganishwa kwa kifo
-
1:00 - 1:04haitushangazi kwamba sote tunaimba, sote tunacheza,
-
1:04 - 1:06sote tuna sanaa.
-
1:06 - 1:09Lakini kinachosisimua zaidi ni namna pekee za mapigo ya wimbo,
-
1:09 - 1:11mahadhi ya dansi kwa kila utamaduni.
-
1:11 - 1:14Na iwapo ni Wapenani wa misitu ya Borneo
-
1:14 - 1:17au makuhani wa Voodoo nchini Haiti
-
1:18 - 1:22au majemedari wa jangwa la Kaisut Kaskazini mwa Kenya,
-
1:24 - 1:26au matabibu wa Kikurandero wa milima ya Andes,
-
1:27 - 1:32au nyumba ya kuhamishika iliyopo katikati ya Sahara
-
1:32 - 1:34Huyu ndiye mwenzi ambaye nilisafiri nae jangwani
-
1:34 - 1:35mwezi mmoja uliopita
-
1:35 - 1:38au mchunga mbuzipori wa miteremko ya Qomolangma,
-
1:38 - 1:40Everest, mungu mke wa ulimwengu.
-
1:40 - 1:43Watu wote hawa wanatufundisha kwamba kuna namna nyingine za kuwa,
-
1:43 - 1:44namna tofauti za kufikiria
-
1:44 - 1:46namna mbalimbali za kujiwekeza katika Dunia.
-
1:46 - 1:48Na hili ndilo wazo, ambalo ukilifikiria,
-
1:48 - 1:50laweza kukupa tumaini,
-
1:50 - 1:53Sasa, kwa pamoja tamaduni nyingi mbalimbali za ulimwengu
-
1:53 - 1:57zinafanya mtandao wa maisha ya kiroho na kiutamaduni
-
1:57 - 1:59unaoifunika dunia,
-
1:59 - 2:01na ni muhimu kwa ustawi wa dunia
-
2:01 - 2:04hali kadhalika mtandao wa kibaiolojia wa maisha unaoujua kama biosifia.
-
2:04 - 2:07Na waweza kufikiria kwamba mtandao huu wa kiutamaduni kwenye maisha
-
2:07 - 2:08kuwa ni ethnosifia
-
2:08 - 2:10na waweza kuainisha ethnosifia
-
2:10 - 2:13kuwa ni jumla ya mawazo na ndoto, imani,
-
2:13 - 2:16mitazamo, hamasa, vipawa vilivyohuishwa
-
2:16 - 2:20na mawazo ya binadamu tokea mapambazuko ya ufahamu.
-
2:20 - 2:23Ethnosifia ni urithi mkuu wa utu,
-
2:23 - 2:25ni ishara ya kila namna tulivyo
-
2:25 - 2:29na kila namna tuwezavyo kuwa viumbe wadadisi ajabu
-
2:30 - 2:33Na kwa namna ambavyo biosifia imeharibiwa,
-
2:33 - 2:35ndivyo pia ethnosifia
-
2:35 - 2:37--na iwapo kwa kiwango kikubwa zaidi.
-
2:37 - 2:39Hakuna mwanabaiolojia, kwa mfano, awezaye kusema
-
2:39 - 2:42kwamba 50% ya viumbe wote au zaidi wamefikia au wapo
-
2:42 - 2:44katika hatari ya kuteketea kwakuwa si kweli,
-
2:44 - 2:46na pia kwamba -- tishio kubwa la maafa
-
2:46 - 2:49katika uwanja wa mtandao wa kibailojia
-
2:49 - 2:52nadra sana unaangalia kwa mtazamo tunaodhania kuwa bora zaidi
-
2:52 - 2:54kwenye uwanja wa mtandao wa utamaduni.
-
2:54 - 2:57Na kielelezo kikubwa cha muelekeo huo ni kupotea kwa lugha.
-
2:57 - 3:00Wakati nyote mliopo humu ndani mlipozaliwa,
-
3:00 - 3:03kulikuwepo lugha 6,000 zikitumika duniani.
-
3:03 - 3:06Kwa sasa, lugha si mkusanyiko wa maneno
-
3:06 - 3:08au mkusanyiko wa kanuni za sarufi.
-
3:08 - 3:10Lugha ni mwanga wa roho ya binadamu.
-
3:10 - 3:13Ni chombo ambacho hupitisha uhai wa tamaduni fulani
-
3:13 - 3:14kuja kwenye ulimwengu wa vitu.
-
3:14 - 3:17Kila lugha ni mkuzo wa msitu wa akili,
-
3:17 - 3:21mgawanyiko wa vijito, wazo, bioanuwai ya mambo ya kiroho,
-
3:21 - 3:25Miongoni mwa lugha hizo 6,000 mpaka leo tunapokuwa hapa Monterey,
-
3:25 - 3:29takriban nusu yake hazitamkwi kwenye masikio ya watoto.
-
3:29 - 3:32Hazifundishwi kwa watoto wachanga tena,
-
3:32 - 3:34maana yake ni kwamba, kwa hakika, labda kama kuna mambo yatabadilika,
-
3:34 - 3:35zimeshakufa.
-
3:35 - 3:39Hakuna upweke unaozidi ule wa kugubikwa na ukimya,
-
3:39 - 3:41wa kuwa mtu wa mwisho kabisa kuongea lugha yako,
-
3:41 - 3:44kutokuwa na namna ya kurithisha busara za mababu
-
3:44 - 3:47au kutarajia ahadi za watoto?
-
3:47 - 3:50Na zaidi, kinachotisha ni hatima ya mtu fulani
-
3:50 - 3:52sehemu fulani ya Dunia takriban kila wiki mbili,
-
3:52 - 3:54kwa sababu kila wiki mbili, kuna mzee anafariki dunia
-
3:54 - 3:56na anakwenda kaburini na silabi za mwisho
-
3:56 - 3:58za lugha ya kale.
-
3:58 - 4:00Na najua kuna baadhi yenu mngesema,"Naam, si ingekuwa vema?
-
4:00 - 4:01Si ingekuwa bora zaidi
-
4:01 - 4:04iwapo sote tungeongea lugha moja?" Nami nasema "Vema,
-
4:04 - 4:07tuifanye lugha hiyo Kiyoruba. Tuifanye iwe Kikantoni.
-
4:07 - 4:08Tuifanye Kikogi."
-
4:08 - 4:10Na wote mara mtagundua nini kitatokea
-
4:10 - 4:13kutoweza kuongea lugha yako mwenyewe.
-
4:13 - 4:16Na ninachotaka kufanya nanyi leo
-
4:16 - 4:20ni kuwapeleka kwenye safari ya ethnosifia --
-
4:20 - 4:22safari fupi ya kupitia ethnosifia
-
4:22 - 4:26kujaribu kukupa picha ya nini kinapotea.
-
4:27 - 4:34Naam, kuna wengi wetu wanaosahau
-
4:34 - 4:36ninaposema "kuna namna mbalimbali za kuwa,"
-
4:36 - 4:38Namaanisha kweli kuna namna mbalimbali za kuwa.
-
4:39 - 4:44Chukulia kwa mfano, mtoto huyu wa Barasana huko kaskazini magharibi Amazoni
-
4:44 - 4:45watu wa majoka ya anakonda
-
4:45 - 4:47wanaoamini miujiza itokanayo na mto wa maziwa
-
4:47 - 4:50kutoka mashariki kwenye matumbo ya nyoka walotukuka.
-
4:50 - 4:53Naam, hawa ni watu ambao kwa kutambua
-
4:53 - 4:55hawawezi kutofautisha rangi ya bluu na rangi ya kijani
-
4:55 - 4:57kwakuwa paa la mbingu
-
4:57 - 4:58linalinganishwa na paa la msitu
-
4:58 - 5:00ambamo watu hawa wanategemea.
-
5:00 - 5:03Wana kanuni ya ajabu kuhusu ndoa na lugha
-
5:03 - 5:05ijulikanayo kama ndoa baina ya lugha tofauti:
-
5:05 - 5:08unalazimika kumuoa azungumzaye lugha tofauti na yako.
-
5:08 - 5:10Na hii inatokana na imani za kale,
-
5:10 - 5:12na bado hali ya kushangaza ipo kwenye nyumba hizi ndefu
-
5:12 - 5:14ambako kuna lugha sita au saba zinazozungumzwa
-
5:14 - 5:16kutokana na kuoana,
-
5:16 - 5:19hutomsikia yeyote akijifunza lugha.
-
5:19 - 5:22Wanasikiliza tu na kuanza kuongea.
-
5:22 - 5:24Au, moja ya makabila ya kushangaza niliyowahi kuishi nayo,
-
5:24 - 5:28ni Waorani wa Kaskazini-Mashariki ya Ecuador,
-
5:28 - 5:31ni watu wa ajabu ambao walitembelewa kwa mara ya kwanza mwaka 1958.
-
5:31 - 5:35Mnamo mwaka 1957, wamishonari watano walijaribu kuwatembelea
-
5:35 - 5:36na wakafanya kosa kubwa.
-
5:36 - 5:37Walidondosha kutoka hewani
-
5:37 - 5:39picha zao za ukubwa nchi nane kwa kumi
-
5:39 - 5:41kitu ambacho tunaweza kusema ni ishara ya urafiki,
-
5:41 - 5:43wakasahau kwamba watu hawa wa misitu ya kitropiki
-
5:43 - 5:46hawakuwahi kuona kitu chochote chenye vina viwili kabla
-
5:46 - 5:48Wakaziokota picha hizi toka ardhini
-
5:48 - 5:51wakajaribu kuangalia kwa nyuma ili kupata umbile kamili
-
5:51 - 5:53hawakuona kitu, na wakaamini kwamba hizi ni kadi za wito
-
5:53 - 5:56toka kwa shetani, kwahiyo wakawachoma mikuki wamishonari na kuwaua.
-
5:57 - 5:59Lakini Waorani si kwamba tu waliwachoma wageni.
-
5:59 - 6:00Walichomana wao kwa wao.
-
6:00 - 6:0354% ya vifo vyao vilitokana na kuchomana mikuki wao kwa wao.
-
6:03 - 6:06Tulifuatilia vizazi nane vilivyopita,
-
6:06 - 6:08na tukapata matukio mawili tu ya vifo vya asilia
-
6:08 - 6:10na tulipowauliza zaidi watu habari hizi,
-
6:10 - 6:12wakakiri kwamba mmoja wao alikuwa mzee sana
-
6:12 - 6:16na angekufa kwa uzee, kwahiyo tukamchoma mkuki tu (Kicheko)
-
6:16 - 6:19Lakini pia wana ujuzi wa ajabu
-
6:19 - 6:20wa msituni ambao unashangaza sana.
-
6:20 - 6:23Wawindaji huweza kunusa harufu ya mkojo wa mnyama toka umbali wa hatua 40
-
6:23 - 6:26na wakakwambia ni kiumbe gani ameuacha mkojo huo.
-
6:26 - 6:28Miaka ya 80, nilikuwa na kazi moja ya kusisimua
-
6:28 - 6:30nilipoulizwa na Profesa wangu wa Harvard
-
6:30 - 6:32iwapo ningependa kwenda Haiti,
-
6:33 - 6:35kupeleleza vikundi vya siri
-
6:35 - 6:37vilivyokuwa ngome kubwa ya Duvalier
-
6:37 - 6:38na majasusi wa Tonton Macoutes
-
6:38 - 6:41na kupata sumu itumikayo kutengeneza mizuka.
-
6:41 - 6:44ili kupata mantiki kutokana na uvumi
-
6:44 - 6:47ilinibidi nijaribu kuelewa kuhusu imani hii ya ajabu
-
6:47 - 6:50ya Vodoun, na Voodoo si kikundi cha uchawi wa nguvu za kiza
-
6:50 - 6:53Kinyume chake, ni mtazamo fulani wa ulimwengu nje ya maumbile.
-
6:53 - 6:54inashangaza.
-
6:54 - 6:55Iwapo nikikutaka utaje dini kuu za dunia,
-
6:55 - 6:56utasema nini?
-
6:56 - 6:59Ukristu, Uislamu, Ubudha, Ujudea, na kadhalika.
-
6:59 - 7:01Huwa kuna bara moja linasahaulika,
-
7:01 - 7:03kwa mtazamo kwamba nchi za Afrika, kusini mwa Sahara
-
7:03 - 7:05hazikuwa na imani za kidini. Vema, kwa hakika, walikuwa nazo
-
7:05 - 7:07na Voodoo ni mchujo tu
-
7:08 - 7:09wa mawazo haya makuu ya kidini
-
7:09 - 7:12yaliyokuja wakati wa uhamisho wa kikatili wa kipindi cha utumwa.
-
7:12 - 7:14Lakini, kinachofanya voodoo kuwa ya kipekee
-
7:14 - 7:16ni huu uhusiano wa kuishi
-
7:16 - 7:17kati ya wazima na wafu.
-
7:17 - 7:18Kwahiyo, wanaoishi wanazaa mizimu.
-
7:18 - 7:21Mizimu inaswaliwa kutoka kwenye Maji Makuu,
-
7:21 - 7:23kuitikia mapigo ya muziki
-
7:23 - 7:25na kusambaratisha roho za wazima kwa muda
-
7:25 - 7:29ili kwa kipindi maalum na kifupi, makuhani wanakuwa mungu.
-
7:29 - 7:31Ndiyo maana Mavoodoo wanapenda kusema
-
7:31 - 7:34kwamba "Nyie watu weupe mnakwenda kanisani na kuongea kuhusu Mungu.
-
7:34 - 7:36Sisi tunacheza hekaluni na kuwa Mungu."
-
7:36 - 7:39Na ni kwa sababu mnaingiliwa, mnachukuliwa na mizimu,
-
7:39 - 7:40unawezaje kuathirika?
-
7:40 - 7:43Kwahiyo unaona maonyesho haya ya kushangaza:
-
7:43 - 7:45kuhani wa Voodoo akiwa katika hali ya kupandisha mori
-
7:45 - 7:48akifukiza uvumba bila hofu,
-
7:48 - 7:51ni kitendo cha kushangaza cha uwezo wa akili
-
7:51 - 7:52kuathiri mwili unaoibeba
-
7:52 - 7:55unapozimuliwa na hali ya kupandisha mori.
-
7:56 - 7:58Na sasa, katika watu wote niliowahi kuishi nao,
-
7:58 - 8:00wa ajabu zaidi ni Wakogi
-
8:00 - 8:03wa Sierra Nevada ya Santa Marta kaskazini mwa Colombia.
-
8:03 - 8:06Wazawa wa ustaarabu wa kikatili wa kale
-
8:06 - 8:09ambao uliwahi kuenea uwanda wote wa Colombia katika pwani ya Caribbean
-
8:09 - 8:10wakati wa uvamizi,
-
8:10 - 8:13watu hawa walikimbilia kwenye safu ya milima ya kivolkano
-
8:13 - 8:15inayopanda juu ya pwani ya Caribbean
-
8:15 - 8:17Katika bara lililomwaga damu,
-
8:17 - 8:20hawa ni watu pekee ambao hawakushindwa vita na Waspanishi
-
8:20 - 8:23Mpaka leo, bado wanatawaliwa na makuhani wa kafara
-
8:23 - 8:25lakini mafunzo yao ya ukuhani ni ya ajabu sana
-
8:26 - 8:28Makuhani vijana wanachukuliwa toka kwenye familia zao
-
8:28 - 8:30katika umri wa miaka mitatu au minne,
-
8:30 - 8:32na kufichwa kwenye ulimwengu wa giza
-
8:32 - 8:36kwenye vibanda vya mawe chini ya malundo ya barafu kwa miaka 18.
-
8:36 - 8:37Vipindi viwili vya miaka tisa
-
8:37 - 8:40imepangwa hivyo makusudi kuigiza miezi tisa ya kukua
-
8:40 - 8:42waliokaa ndani ya tumbo la mama,
-
8:42 - 8:45na sasa kilimwengu wapo kwenye tumbo la mama mkuu.
-
8:45 - 8:46Na kwa muda wote huu,
-
8:47 - 8:50wanafundishwa maadili muhimu ya utamaduni wao,
-
8:50 - 8:52maadili ambayo yanatunza maombi ya sala zao
-
8:52 - 8:55na sala zao pekee ndizo zinatunza maumbile --
-
8:55 - 8:57au twaweza kusema uwiano wa mazingira.
-
8:58 - 8:59Na mwisho wa mafunzo haya ya ajabu,
-
8:59 - 9:01siku moja wanatolewa nje ghafla
-
9:01 - 9:04na kwa mara ya kwanza katika maisha yao, wakiwa na umri wa miaka 18
-
9:04 - 9:08wanaona jua likichomoza. Na katika kipindi hicho cha ufahamu
-
9:08 - 9:11wa mwanga wa kwanza wakati Jua linapoangaza milima
-
9:11 - 9:12yenye mandhari ya kupendeza,
-
9:13 - 9:15mara vitu vyote walivyojifunza kwa nadharia
-
9:15 - 9:18vinatimia kwa utukufu mkubwa. Na kuhani anarudi nyuma
-
9:18 - 9:20na kusema "Mnaona? Ni hakika kama nilivyowaambia.
-
9:20 - 9:23Ni nzuri sana. Ni jukumu lenu kuilinda."
-
9:23 - 9:25Wanajiita kaka wakubwa
-
9:25 - 9:28na wanasema sisi, ambao ni kaka wadogo,
-
9:28 - 9:31tunaohusika na kuiharibu dunia,
-
9:32 - 9:34Na sasa, kiwango cha ufahamu kinakuwa muhimu sana.
-
9:34 - 9:36Tunapofikiria kuhusu wazawa wa asilia na mandhari ya nchi,
-
9:36 - 9:38tunakuwa aidha tunamfuata Rousseau
-
9:38 - 9:41na nadharia ya ukatili halali,
-
9:41 - 9:43ambao una maanisha kwamba ubaguzi wa rangi ni urahisi,
-
9:43 - 9:46au badala yake, tumfuate Thoreau
-
9:46 - 9:48na kusema watu hawa wapo karibu zaidi na Dunia kuliko sisi,
-
9:48 - 9:50Vema, wazawa asilia hawana unyovu wa moyo
-
9:50 - 9:52wala hawasumbuliwi na mawazo ya kukumbuka nyumbani
-
9:52 - 9:54Hakuna fursa kubwa
-
9:54 - 9:56kwenye mabwawa ya malaria huko Asmat
-
9:56 - 9:59au kwenye upepo mkali wa Tibet, lakini wameweza, hata hivyo,
-
9:59 - 10:03kwa kupitia ibada fulani, wameweza kutengeneza mtazamo wa Dunia
-
10:03 - 10:06ambao unazingatia kujijua au kuwa karibu na kujijua,
-
10:06 - 10:08lakini kwa kutumia ufahamu wa juu zaidi:
-
10:08 - 10:11wazo la kwamba Dunia yenyewe yaweza kuwepo
-
10:12 - 10:14kwakuwa imepewa pumzi kwa ufahamu wa binadamu.
-
10:14 - 10:16Naam, hiyo ina maana gani?
-
10:16 - 10:18Ina maana kwamba mtoto mdogo wa huko Andes
-
10:18 - 10:20aliyelelewa kuamini kwamba milima ni mizimu ya Apu
-
10:20 - 10:22inayoleta hatima yake
-
10:22 - 10:25atakuwa binadamu tofauti kabisa
-
10:25 - 10:28na atakuwa na uhusiano tofauti na maliasili hiyo
-
10:28 - 10:30au sehemu ile ambako mtoto wa kutoka Montana
-
10:30 - 10:33amelelewa kuamini kwamba mlima ni mkusanyiko wa mawe
-
10:33 - 10:34yanayosubiri kuchimbuliwa.
-
10:34 - 10:38Ama ni makao ya mizimu au malundo ya madini si jambo muhimu.
-
10:38 - 10:41Kinachosisimua ni nadharia inayo ainisha uhusiano huo
-
10:41 - 10:43kati ya mtu na ulimwengu asilia
-
10:43 - 10:45Nilikulia katika misitu ya British Columbia
-
10:45 - 10:47na kuamini kwamba misitu hiyo ipo kwa ajili ya kukatwa,
-
10:47 - 10:49Hiyo imenifanya kuwa mtu tofauti
-
10:49 - 10:51sana na rafiki zangu miongoni mwa Kwakiutl
-
10:51 - 10:53ambao wanaamini kwamba misitu ni makao ya Hukuk
-
10:53 - 10:54na lango la peponi
-
10:54 - 10:57na mizimu mumiani iishiyo miisho ya kaskazini mwa ulimwengu,
-
10:57 - 11:01mizimu wanayokumbana nayo wakati wa simiko la Hamatsa
-
11:01 - 11:03Na sasa, ukianza kuzingatia wazo
-
11:03 - 11:05kwamba tamaduni hizi zinaweza kujenga mitazamo tofauti
-
11:05 - 11:06waweza kuanza kuelewa
-
11:06 - 11:11baadhi ya uvumbuzi wao wa ajabu. Chukulia mfano mmea huu hapa,
-
11:11 - 11:13Ni picha niliyoipiga Kaskazini mwa Amazoni mwezi Aprili
-
11:13 - 11:16Hii ni ayahuasca, wengi wenu mmekwisha sikia habari zake,
-
11:16 - 11:19moja kati ya michanyato mikali kabisa ya kuzingulia
-
11:19 - 11:21kati ya vifaa vyote vya mashamani
-
11:21 - 11:23kinachoifanya ayahuasca kuwa ya kushangaza zaidi
-
11:23 - 11:27si kiwango cha hali ya juu cha dawa inayotengenezwa
-
11:27 - 11:31bali maudhui yake. Inatengenezwa kutokana na vitu viwili
-
11:31 - 11:33Kwa upande mmoja ni mti wa liana
-
11:33 - 11:35ambao ni jamii ya beta-carbolines
-
11:35 - 11:38harmine, harmoline, ambayo ni nishai
-
11:38 - 11:40Kuinywa peke yake
-
11:40 - 11:42ni afadhali uvute moshi mzito wa bluu
-
11:42 - 11:44unaingia kwenye ufahamu wako
-
11:44 - 11:47ambao umechanganywa na majani ya jamii ya kahawa
-
11:47 - 11:49yaitwayo Psychotria viridis.
-
11:49 - 11:52Mmea huu una tindikali za tryptamines,
-
11:52 - 11:56inafanana sana na kisisimuzi cha mfumo wa ufahamu cha dimethyltryptamine-5,
-
11:56 - 11:57methoxydimethyltryptamine.
-
11:57 - 11:59Iwapo ungaliwaona Mayonami
-
11:59 - 12:01wakiingiza vitu kwenye pua zao,
-
12:01 - 12:04mchanyato wanaoutengeneza kwa mimea mbalimbali
-
12:04 - 12:08ambayo pia ina methoxydimethyltryptamine.
-
12:08 - 12:10Kuingiza unga huo kwenye pua yako
-
12:10 - 12:14ni kama vile kuzibuliwa kama risasi toka kwenye bomba la bunduki
-
12:14 - 12:21lililosakafiwa kwa michoro ya baroque na ukatua kwenye bahari ya umeme, (Kicheko)
-
12:21 - 12:23Haifanyi upotoshaji wa hali halisi;
-
12:23 - 12:24inayeyusha ufahamu wa hali halisi.
-
12:24 - 12:27Kwa kweli, nilikuwa nabishana na mwalimu wangu Profesa Richard Evan Shultes --
-
12:27 - 12:29mtu ambaye alianzisha zama za uchunguzi wa madawa yanayobadili ufahamu
-
12:29 - 12:31kwa uvumbuzi wake wa uyoga wa ajabu
-
12:31 - 12:33nchini Mexico mnamo miaka ya 1930.
-
12:33 - 12:35Nilikuwa nabisha kwamba huwezi kuainisha tryptamines hizi
-
12:35 - 12:38kama vilevinishai kwakuwa wakati umezinguliwa nazo
-
12:38 - 12:42hatokuwepo mtu mwingine akisubiri kushuhudia muweweseko wake. (Kicheko)
-
12:42 - 12:45Lakini kuhusu tryptamines haziwezi kunywewa
-
12:45 - 12:47kwakuwa zimeathiriwa na kimeng'enya
-
12:47 - 12:50vinavyopatikana kiasilia katika utumbo wa binadamu na huitwa monoamine oxidase
-
12:50 - 12:53Vinaweza kunywewa tu iwapo vitachanganywa na
-
12:53 - 12:56kemikali nyinginezo zinazoweza kuathiri vimeng'enya vya MAO
-
12:56 - 12:57Na sasa, vitu vya kushangaza
-
12:57 - 13:01ni hizo beta-carbolines zinazopatikana kwenye liana
-
13:01 - 13:04ni vidhibiti vya MAO kwa namna fulani muhimu
-
13:05 - 13:08kuizimua tryptamine. Na hapo unajiuliza swali
-
13:08 - 13:12Ilikuwaje kwenye mimea mbalimbali zaidi ya 80,000,
-
13:12 - 13:16watu hawa walichagua hii miwili ambayo haifanani maumbile
-
13:16 - 13:17lakini ambayo ikichanganywa kwa namna hii,
-
13:17 - 13:19inatengeneza mchanganyiko wa kemikali
-
13:19 - 13:21kamilifu ambayo ni zaidi ya jumla ya kila kimojawapo?
-
13:21 - 13:24Vema, tunatumia maneno rahisi, kwamba walikuwa wakijaribu kubahatisha,
-
13:24 - 13:25jambo ambalo halina ukweli wowote.
-
13:26 - 13:29Lakini ukiwauliza Wahindi watakwambia, "Mimea inaongea nasi."
-
13:29 - 13:30Vema, hiyo ina maana gani?
-
13:30 - 13:34Kabila hili la Cofan wana aina 17 za ayahuasca,
-
13:34 - 13:37na wanaweza kuitofautisha kutoka mbali huko msituni,
-
13:38 - 13:42na zote hizi kwetu sisi zinaonekana kuwa sawa.
-
13:42 - 13:44Halafu unawauliza waliwezaje kuziainisha
-
13:44 - 13:47na wanasema " Nilidhani unajua masuala ya mimea,
-
13:47 - 13:49nina maana, hujui chochote?" Na nikasema "Hapana."
-
13:49 - 13:52Naam, inakuwa kwamba unachukua moja ya kila hizo aina 17
-
13:52 - 13:55usiku wa mbalamwezi na zinakuimbia kwa mlio tofauti
-
13:55 - 13:57Sasa, hiyo haiwezi kukupatia Ph.D. ya Harvard,
-
13:57 - 14:01lakini hii inavutia zaidi ya kuhesabu chavua.
-
14:01 - 14:02Na sasa,
-
14:02 - 14:05(Makofi)
-
14:05 - 14:07na tatizo -- na tatizo ni kwamba hata sisi
-
14:07 - 14:09tunaotetea hatima ya wazawa asilia
-
14:09 - 14:10tunawaona kama wanavutia
-
14:10 - 14:12lakini wamebanwa na mipaka ya historia
-
14:12 - 14:15wakati ulimwengu halisi, yaani ulimwengu wetu, unasonga mbele.
-
14:15 - 14:17Vema, ukweli ni kwamba karne ya 20, miaka 300 kuanzia sasa,
-
14:17 - 14:20haitakumbukwa kwa vita vyake
-
14:20 - 14:21au uvumbuzi wa kiteknolojia
-
14:21 - 14:23bali ni zama ambazo tulikaa
-
14:24 - 14:26na kuunga mkono waziwazi au tu kukubali
-
14:26 - 14:29uharibifu mkubwa wa urithi mkubwa wa kibaiolojia au kiutamaduni
-
14:29 - 14:32duniani. Kwa sasa, tatizo si mabadiliko.
-
14:32 - 14:34Tamaduni zote wakati wote
-
14:34 - 14:37zimejihusisha na mchezo
-
14:37 - 14:38wa masuala mapya ya kimaisha.
-
14:39 - 14:41Na tatizo si teknolojia peke yake.
-
14:42 - 14:44Wahindi Wekundu Sioux hawajaacha kuwa Sioux
-
14:44 - 14:45walipoacha upinde na mshale
-
14:45 - 14:47kama vile ambavyo Mmarekani kuacha kuwa Mmarekani
-
14:47 - 14:49alipoacha farasi na mkokoteni wake
-
14:49 - 14:50Si mabadiliko ya teknolojia
-
14:50 - 14:54yanayotishia uhai wa ethnosifia. Ni ubabe.
-
14:54 - 14:56Sura katili ya miliki.
-
14:56 - 14:58Na chochote unachokiangalia duniani,
-
14:58 - 15:01utaona kwamba hizi si tamaduni tu zinazopotea.
-
15:01 - 15:03Hawa ni watu halisi wanaoishi
-
15:03 - 15:06wakiondolewa uhai kwa nguvu zinazojulikana
-
15:06 - 15:08lakini ziko nje ya uwezo wao kuzimudu.
-
15:08 - 15:10Iwapo ni uharibifu mbaya wa misitu
-
15:11 - 15:13kwenye nchi ya Wapenani --
-
15:13 - 15:16watu waishio kwa kuhamahama huko Asia ya Kusinimashariki, kutoka Sarawak --
-
15:16 - 15:20watu walioshi huru mwituni mpaka kizazi kimoja kilichopita,
-
15:20 - 15:23na sasa wote wamezuiliwa na kutumikishwa
-
15:23 - 15:25kwenye kingo za mito,
-
15:25 - 15:29ambako utaona mito yenyewe imechafuliwa kwa tope
-
15:29 - 15:31yanayoonekana kubeba takriban nusu ya ukubwa wa kisiwa cha Borneo
-
15:31 - 15:32kwenda Bahari ya China ya Kusini,
-
15:32 - 15:34ambako meli za Kijapani zinasubiri
-
15:34 - 15:38tayari kubeba magogo mabichi yaliyozolewa toka misituni.
-
15:38 - 15:39Au suala la Wayanomami,
-
15:39 - 15:41ni ugonjwa ambao umeingia,
-
15:41 - 15:43wakati wa uvumbuzi wa dhahabu.
-
15:43 - 15:45Au tukienda kwenye milima ya Tibet,
-
15:45 - 15:47ambako ninafanya utafiti mwingi kwa sasa,
-
15:48 - 15:51utaona sura ya kutisha ya ubeberu wa kisiasa.
-
15:51 - 15:53Kama ujuavyo, mauaji ya halaiki, kumaliza maisha ya watu
-
15:53 - 15:55kunalaaniwa ulimwenguni kote, lakini mauaji ya kiutamaduni,
-
15:56 - 15:59uharibifu wa utaratibu wa maisha ya watu, siyo tu kwamba unalaaniwa,
-
15:59 - 16:02unashangiliwa -- na makundi mengi
-
16:02 - 16:04kuwa kama mkakati wa maendeleo.
-
16:04 - 16:07Na huwezi kuelewa uchungu wa Tibet
-
16:07 - 16:09mpaka usafiri kwa barabara.
-
16:09 - 16:13Niliwahi kusafiri maili 6,000 kutoka Chengdu huko Magharibi mwa China
-
16:13 - 16:16kwa barabara kupitia kusinimashariki Tibet mpaka Lhasa
-
16:16 - 16:20nikiwa na mwenzi ambaye ni kijana, na mpaka nilipofika Lhasa
-
16:20 - 16:23ndipo nikaelewa ukweli kuhusu takwimu
-
16:23 - 16:24unazozisikia.
-
16:24 - 16:28majengo matakatifu takriban 6,000 yamebomolewa kuwa vumbi na majivu.
-
16:28 - 16:31watu milioni 1.2 wameuawa na makada
-
16:31 - 16:32wakati wa Mapinduzi ya Utamaduni
-
16:33 - 16:35Baba wa kijana huyu alitawazwa kuwa naibu wa Lama.
-
16:35 - 16:37Kwa sababu hiyo aliuawa mara tu
-
16:37 - 16:39ya uvamizi wa China.
-
16:39 - 16:41Mjomba wake alitoroka pamoja na mhashamu kwenda uhamishoni
-
16:41 - 16:44nchini Nepal
-
16:44 - 16:46Mama yake alifungwa kwa sababu tu --
-
16:46 - 16:48alikuwa tajiri.
-
16:49 - 16:51Yeye alipenyezwa kwa siri kuingizwa jela akiwa na umri wa miaka miwili
-
16:51 - 16:53kujificha kwenye sketi za mamaake
-
16:53 - 16:55kwakuwa hakuweza kustahimili kuishi bila mwanae.
-
16:55 - 16:57Dada yake aliyefanya kitendo hicho cha kishujaa
-
16:57 - 16:58alipelekwa kwenye kambi ya elimu
-
16:58 - 17:00Siku moja kwa bahati mbaya alikumbana na kundi la askari
-
17:01 - 17:03wa Mao, na kwa kosa hilo,
-
17:03 - 17:06akahukumiwa kifungo cha miaka saba na kazi ngumu.
-
17:06 - 17:09Machungu ya Tibet hayavumiliki,
-
17:09 - 17:12lakini ujasiri wa watu hawa ni kitu cha kusisimua.
-
17:13 - 17:16Na mwisho wake, inakuja mwisho kwenye uchaguzi,
-
17:16 - 17:19Tunataka kuishi kwenye ulimwengu unaochosha wa utamaduni mmoja
-
17:19 - 17:22au tunapenda kuwa na mtandao wa tamaduni mbalimbali?
-
17:22 - 17:25Margaret Mead, mtaalam maarufu wa mambo ya kale, kabla ya kifo chake alisema
-
17:25 - 17:28wasiwasi wake mkubwa ni kwamba tunazidi kuelekea kwenye
-
17:28 - 17:30hii hali ya mtazamo mmoja wa kilimwengu
-
17:30 - 17:35si tu kwamba tutaona uwezo mkubwa wa ufahamu wa binadamu
-
17:35 - 17:39ukipunguzwa kuwa mawazo finyu,
-
17:39 - 17:40bali tutazinduka siku moja
-
17:40 - 17:43tukiwa tumesahau kwamba kuna uwezekano tofauti wa mambo.
-
17:44 - 17:47Na ni taadhima kubwa kukumbuka kwamba kizazi chetu kimekuwepo kwa
-
17:47 - 17:49takriban miaka 600,000
-
17:49 - 17:52Mapinduzi ya Kilimo -- yaliyoanzisha ukulima,
-
17:52 - 17:54tulipo salim amri kwenye imani ya mbegu
-
17:54 - 17:56ushairi wa shaman ulisambaratishwa
-
17:56 - 17:57kwa maandiko ya ukuhani
-
17:57 - 18:00tukajenga daraja za umiliki ziada --
-
18:00 - 18:02ni miaka 10,000 iliyopita tu.
-
18:02 - 18:04Maendeleo ya viwanda kama tuyajuavyo
-
18:04 - 18:06yana si zaidi ya miaka 300.
-
18:06 - 18:08Na sasa, historia hiyo ya juu juu hainishawishi
-
18:08 - 18:11kwamba tuna majibu ya matatizo yetu yote
-
18:11 - 18:13yatakayo tufariji katika hatima ya milenia
-
18:13 - 18:15Wakati hizi tamaduni mbalimbali ulimwenguni
-
18:15 - 18:18zikiulizwa maana ya kuwa binadamu,
-
18:18 - 18:20zitakujibu kwa sauti 10,000 tofauti.
-
18:20 - 18:26Na kwa kupitia wimbo huo ndipo tutatambua uwezekano
-
18:26 - 18:29wa kuona kwamba sisi ni viumbe wenye ufahamu,
-
18:29 - 18:32kufahamu fika kuhakikisha watu wote na bustani zote
-
18:32 - 18:38zinapata namna ya kustawi. Na kuna vipindi vya matumaini.
-
18:38 - 18:41Hii ni picha niliyoipiga kwenye ncha ya kaskazini mwa kisiwa cha Baffin
-
18:41 - 18:43nilipokwenda kuwinda nyangumi wenye pembe nikiwa na Wainuiti,
-
18:44 - 18:47na mtu huyu, Olaya, alinisimulia hadithi ya ajabu kuhusu babu yake.
-
18:48 - 18:50Serikali ya Canada haikuwa ikiwatendea haki
-
18:50 - 18:52Wainuiti, katika miaka ya 1950,
-
18:52 - 18:55ili kujenga utaifa, tuliwahamishia kwenye vijiji.
-
18:55 - 18:59Babu yake alikataa kwenda.
-
18:59 - 19:03Nduguze, kwa kuhofia maisha yake, wakampokonya silaha zake zote,
-
19:03 - 19:04na vifaa vyake vyote.
-
19:05 - 19:07Na sasa, uelewe kwamba Wainuiti hawakuogopa baridi;
-
19:07 - 19:08walijinufaisha nayo.
-
19:08 - 19:11Mikokoteni ya kuteleza kwenye barafu ilitengenezwa kwa samaki
-
19:11 - 19:12na kufunikwa kwa ngozi ya swala.
-
19:12 - 19:17Kwahiyo babu yake mtu huyu hakutishika na usiku wa huko Aktika
-
19:17 - 19:19au upepo mkali ulokuwa ukipuliza
-
19:19 - 19:22Alitoka nje, akavua suruali yake
-
19:23 - 19:26na kunyea mkononi. Na kinyesi kilipoanza kuganda,
-
19:26 - 19:29akafinyanga katika umbile la upanga.
-
19:29 - 19:31Akatemea mate kwenye upande wa makali ya upanga huo wa kinyesi
-
19:31 - 19:34na baadae inaganda na kuwa ngumu, na aliitumia kumuua mbwa.
-
19:34 - 19:37Akamchuna mbwa na kuboresha silaha yake,
-
19:37 - 19:40akachukua ubavu wa mbwa na kutengeneza mkokoteni wa kuteleza,
-
19:41 - 19:42akamfunga mbwa wa pili,
-
19:42 - 19:46na kutokomea kwenye uwanda wa barafu, kisu cha kinyesi kibindoni.
-
19:46 - 19:50Halafu unazungumzia kujikwamua bila kitu chochote (Kicheko)
-
19:50 - 19:51Na hii, kwa namna mbalimbali,
-
19:51 - 19:53(Makofi)
-
19:53 - 19:55hii ni ishara ya ujasiri wa Wainuiti
-
19:55 - 19:58na wazawa wote asilia ulimwenguni kote.
-
19:58 - 20:00Serikali ya Canada mnamo Aprili 1999
-
20:00 - 20:03waliwarudishia mamlaka Wainuiti
-
20:03 - 20:06kwenye eneo kubwa kuliko California na Texas yakiunganishwa pamoja.
-
20:06 - 20:08Ni nchi yetu mpya. Inaitwa Nunavut.
-
20:09 - 20:12Ni jimbo linalojitegemea. Wanasimamia maliasili zote za madini.
-
20:12 - 20:14Ni mfano wa ajabu jinsi ambavyo taifa
-
20:14 - 20:18linafikia -- au kutafuta muafaka na watu wake.
-
20:19 - 20:22Na mwisho, hatimaye, naona ni wazi kabisa
-
20:22 - 20:23walau wengi wetu tulosafiri
-
20:23 - 20:25kwenye sehemu hizi za mbali kwenye dunia,
-
20:27 - 20:28tumegundua si mbali tena.
-
20:28 - 20:30Ni makazi ya mtu fulani.
-
20:30 - 20:32Yanaonyesha matawi ya mawazo ya binadamu
-
20:32 - 20:36kwamba nenda nyuma kwenye mwanzo wa nyakati. Na kwetu sote,
-
20:36 - 20:39ndoto za watoto hawa, kama vile ndoto za watoto wetu wenyewe,
-
20:39 - 20:42zimekuwa sehemu ya jiografia ya matumaini.
-
20:42 - 20:46Kwahiyo, tunachojaribu kufanya National Geographic hatimaye,
-
20:46 - 20:50ni, tunaamini kwamba wanasiasa hawafanikishi lolote.
-
20:50 - 20:51Huo ni ukosoaji wa hoja --
-
20:51 - 20:53(Makofi)
-
20:53 - 20:55tunadhani kwamba wakosoaji hawana ushawishi,
-
20:55 - 20:58lakini tunaamini kwamba kuhadithia kutaibadili dunia,
-
20:58 - 21:01na kwahiyo sisi ni miongoni mwa taasisi bora zaidi za masimulizi
-
21:01 - 21:04duniani. Tunapata watembezi milioni 35 kwenye tovuti yetu kila mwezi.
-
21:04 - 21:07Nchi 156 zinarusha matangazo ya televisheni yetu.
-
21:08 - 21:10Majarida yetu yanasomwa na mamilioni.
-
21:10 - 21:13Na tunachokifanya ni safari nyingi
-
21:13 - 21:15kwenda kwenye ethnosifia ambako tunawapeleka watazamaji wetu
-
21:15 - 21:17kwenye sehemu ambako kuna maajabu ya kiutamaduni
-
21:18 - 21:20ambayo hawatoweza kuvumilia bali kushangazwa
-
21:20 - 21:22na wanachokiona, na natumaini, kwahiyo,
-
21:22 - 21:25kukubali taratibu, mmoja mmoja,
-
21:25 - 21:27kiini cha uvumbuzi wa elimu ya mambo ya kale:
-
21:27 - 21:31kwamba ulimwengu unastahili kuwepo kwa namna mbalimbali
-
21:31 - 21:32na kwamba tunaweza kupata namna ya kuishi
-
21:32 - 21:35katika ulimwengu wa tamaduni tofauti
-
21:35 - 21:37ambako busara zote za watu
-
21:37 - 21:40zitachangia ustawi wetu sote
-
21:40 - 21:41Asante sana.
-
21:41 - 21:43(Makofi)
- Title:
- Wade Davis na Tamaduni Zilizo Hatarini Kupotea
- Speaker:
- Wade Davis
- Description:
-
Kwa kutumia picha za kushangaza na simulizi za kusisimua, Wade Davis mwandishi wa National Geographic anaadhimisha umaridadi wa mchanganyiko wa tamaduni za kiasili ulimwenguni, ambazo ziko hatarini kupotea duniani katika kasi ya kutisha.
- Video Language:
- English
- Team:
- closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 21:44
TED edited Swahili subtitles for Dreams from endangered cultures | ||
TED edited Swahili subtitles for Dreams from endangered cultures | ||
TED added a translation |