WEBVTT 00:00:00.000 --> 00:00:03.000 Kama ujuavyo, moja ya raha kubwa za kusafiri 00:00:03.000 --> 00:00:05.000 na moja ya furaha za utafiti wa mahusiano ya kikabila 00:00:05.000 --> 00:00:07.000 ni fursa ya kuishi miongoni mwao 00:00:07.000 --> 00:00:09.000 hao wasiosahau namna za kijadi 00:00:09.000 --> 00:00:12.000 ambao wangali wakihisi ya kale kwenye upepo, 00:00:12.000 --> 00:00:15.000 na kuyagusa juu ya mawe yaliyosafishwa na mvua, 00:00:15.000 --> 00:00:17.000 na kuyaonja kwenye majani machungu ya mimea. 00:00:17.000 --> 00:00:21.000 Kujua kwamba wanaoabudu chuipamba bado wana safari kupita mbingu za mbali, 00:00:21.000 --> 00:00:25.000 au imani za wazee wa Kiinuiti zinaleta maana, 00:00:25.000 --> 00:00:27.000 au kwamba huko Himalaya, 00:00:28.000 --> 00:00:32.000 Mabudha bado wanaifuata pumzi ya Dharma, 00:00:32.000 --> 00:00:35.000 ni katika kukumbuka utambuzi wa msingi wa anthropolojia, 00:00:35.000 --> 00:00:37.000 na kwamba mtazamo wa ulimwengu tunamoishi 00:00:38.000 --> 00:00:40.000 haupo kihalisia, 00:00:40.000 --> 00:00:41.000 bali ni nadharia tu ya ukweli, 00:00:41.000 --> 00:00:45.000 ni matokeo ya jozi moja tu ya machaguo kadhaa 00:00:45.000 --> 00:00:49.000 ambayo mababu zetu walifanya, japo kwa mafanikio, vizazi kadhaa vilivyopita. NOTE Paragraph 00:00:50.000 --> 00:00:54.000 Na kwa hakika, sote tunashabihiana katika kufuata kanuni za maumbile 00:00:54.000 --> 00:00:56.000 Sote tunazaliwa. Sote tunazaa watoto. 00:00:56.000 --> 00:00:58.000 Tunapitia kafara za kusimikwa, 00:00:58.000 --> 00:01:00.000 Tunalazimika kukabiliana na ukatili wa kutenganishwa kwa kifo 00:01:00.000 --> 00:01:04.000 haitushangazi kwamba sote tunaimba, sote tunacheza, 00:01:04.000 --> 00:01:06.000 sote tuna sanaa. NOTE Paragraph 00:01:06.000 --> 00:01:09.000 Lakini kinachosisimua zaidi ni namna pekee za mapigo ya wimbo, 00:01:09.000 --> 00:01:11.000 mahadhi ya dansi kwa kila utamaduni. 00:01:11.000 --> 00:01:14.000 Na iwapo ni Wapenani wa misitu ya Borneo 00:01:14.000 --> 00:01:17.000 au makuhani wa Voodoo nchini Haiti 00:01:18.000 --> 00:01:22.000 au majemedari wa jangwa la Kaisut Kaskazini mwa Kenya, 00:01:24.000 --> 00:01:26.000 au matabibu wa Kikurandero wa milima ya Andes, 00:01:27.000 --> 00:01:32.000 au nyumba ya kuhamishika iliyopo katikati ya Sahara 00:01:32.000 --> 00:01:34.000 Huyu ndiye mwenzi ambaye nilisafiri nae jangwani 00:01:34.000 --> 00:01:35.000 mwezi mmoja uliopita 00:01:35.000 --> 00:01:38.000 au mchunga mbuzipori wa miteremko ya Qomolangma, 00:01:38.000 --> 00:01:40.000 Everest, mungu mke wa ulimwengu. NOTE Paragraph 00:01:40.000 --> 00:01:43.000 Watu wote hawa wanatufundisha kwamba kuna namna nyingine za kuwa, 00:01:43.000 --> 00:01:44.000 namna tofauti za kufikiria 00:01:44.000 --> 00:01:46.000 namna mbalimbali za kujiwekeza katika Dunia. 00:01:46.000 --> 00:01:48.000 Na hili ndilo wazo, ambalo ukilifikiria, 00:01:48.000 --> 00:01:50.000 laweza kukupa tumaini, 00:01:50.000 --> 00:01:53.000 Sasa, kwa pamoja tamaduni nyingi mbalimbali za ulimwengu 00:01:53.000 --> 00:01:57.000 zinafanya mtandao wa maisha ya kiroho na kiutamaduni 00:01:57.000 --> 00:01:59.000 unaoifunika dunia, 00:01:59.000 --> 00:02:01.000 na ni muhimu kwa ustawi wa dunia 00:02:01.000 --> 00:02:04.000 hali kadhalika mtandao wa kibaiolojia wa maisha unaoujua kama biosifia. 00:02:04.000 --> 00:02:07.000 Na waweza kufikiria kwamba mtandao huu wa kiutamaduni kwenye maisha 00:02:07.000 --> 00:02:08.000 kuwa ni ethnosifia 00:02:08.000 --> 00:02:10.000 na waweza kuainisha ethnosifia 00:02:10.000 --> 00:02:13.000 kuwa ni jumla ya mawazo na ndoto, imani, 00:02:13.000 --> 00:02:16.000 mitazamo, hamasa, vipawa vilivyohuishwa 00:02:16.000 --> 00:02:20.000 na mawazo ya binadamu tokea mapambazuko ya ufahamu. 00:02:20.000 --> 00:02:23.000 Ethnosifia ni urithi mkuu wa utu, 00:02:23.000 --> 00:02:25.000 ni ishara ya kila namna tulivyo 00:02:25.000 --> 00:02:29.000 na kila namna tuwezavyo kuwa viumbe wadadisi ajabu NOTE Paragraph 00:02:30.000 --> 00:02:33.000 Na kwa namna ambavyo biosifia imeharibiwa, 00:02:33.000 --> 00:02:35.000 ndivyo pia ethnosifia 00:02:35.000 --> 00:02:37.000 --na iwapo kwa kiwango kikubwa zaidi. 00:02:37.000 --> 00:02:39.000 Hakuna mwanabaiolojia, kwa mfano, awezaye kusema 00:02:39.000 --> 00:02:42.000 kwamba 50% ya viumbe wote au zaidi wamefikia au wapo 00:02:42.000 --> 00:02:44.000 katika hatari ya kuteketea kwakuwa si kweli, 00:02:44.000 --> 00:02:46.000 na pia kwamba -- tishio kubwa la maafa 00:02:46.000 --> 00:02:49.000 katika uwanja wa mtandao wa kibailojia 00:02:49.000 --> 00:02:52.000 nadra sana unaangalia kwa mtazamo tunaodhania kuwa bora zaidi 00:02:52.000 --> 00:02:54.000 kwenye uwanja wa mtandao wa utamaduni. 00:02:54.000 --> 00:02:57.000 Na kielelezo kikubwa cha muelekeo huo ni kupotea kwa lugha. NOTE Paragraph 00:02:57.000 --> 00:03:00.000 Wakati nyote mliopo humu ndani mlipozaliwa, 00:03:00.000 --> 00:03:03.000 kulikuwepo lugha 6,000 zikitumika duniani. 00:03:03.000 --> 00:03:06.000 Kwa sasa, lugha si mkusanyiko wa maneno 00:03:06.000 --> 00:03:08.000 au mkusanyiko wa kanuni za sarufi. 00:03:08.000 --> 00:03:10.000 Lugha ni mwanga wa roho ya binadamu. 00:03:10.000 --> 00:03:13.000 Ni chombo ambacho hupitisha uhai wa tamaduni fulani 00:03:13.000 --> 00:03:14.000 kuja kwenye ulimwengu wa vitu. 00:03:14.000 --> 00:03:17.000 Kila lugha ni mkuzo wa msitu wa akili, 00:03:17.000 --> 00:03:21.000 mgawanyiko wa vijito, wazo, bioanuwai ya mambo ya kiroho, NOTE Paragraph 00:03:21.000 --> 00:03:25.000 Miongoni mwa lugha hizo 6,000 mpaka leo tunapokuwa hapa Monterey, 00:03:25.000 --> 00:03:29.000 takriban nusu yake hazitamkwi kwenye masikio ya watoto. 00:03:29.000 --> 00:03:32.000 Hazifundishwi kwa watoto wachanga tena, 00:03:32.000 --> 00:03:34.000 maana yake ni kwamba, kwa hakika, labda kama kuna mambo yatabadilika, 00:03:34.000 --> 00:03:35.000 zimeshakufa. 00:03:35.000 --> 00:03:39.000 Hakuna upweke unaozidi ule wa kugubikwa na ukimya, 00:03:39.000 --> 00:03:41.000 wa kuwa mtu wa mwisho kabisa kuongea lugha yako, 00:03:41.000 --> 00:03:44.000 kutokuwa na namna ya kurithisha busara za mababu 00:03:44.000 --> 00:03:47.000 au kutarajia ahadi za watoto? 00:03:47.000 --> 00:03:50.000 Na zaidi, kinachotisha ni hatima ya mtu fulani 00:03:50.000 --> 00:03:52.000 sehemu fulani ya Dunia takriban kila wiki mbili, 00:03:52.000 --> 00:03:54.000 kwa sababu kila wiki mbili, kuna mzee anafariki dunia 00:03:54.000 --> 00:03:56.000 na anakwenda kaburini na silabi za mwisho 00:03:56.000 --> 00:03:58.000 za lugha ya kale. NOTE Paragraph 00:03:58.000 --> 00:04:00.000 Na najua kuna baadhi yenu mngesema,"Naam, si ingekuwa vema? 00:04:00.000 --> 00:04:01.000 Si ingekuwa bora zaidi 00:04:01.000 --> 00:04:04.000 iwapo sote tungeongea lugha moja?" Nami nasema "Vema, 00:04:04.000 --> 00:04:07.000 tuifanye lugha hiyo Kiyoruba. Tuifanye iwe Kikantoni. 00:04:07.000 --> 00:04:08.000 Tuifanye Kikogi." 00:04:08.000 --> 00:04:10.000 Na wote mara mtagundua nini kitatokea 00:04:10.000 --> 00:04:13.000 kutoweza kuongea lugha yako mwenyewe. NOTE Paragraph 00:04:13.000 --> 00:04:16.000 Na ninachotaka kufanya nanyi leo 00:04:16.000 --> 00:04:20.000 ni kuwapeleka kwenye safari ya ethnosifia -- 00:04:20.000 --> 00:04:22.000 safari fupi ya kupitia ethnosifia 00:04:22.000 --> 00:04:26.000 kujaribu kukupa picha ya nini kinapotea. 00:04:27.000 --> 00:04:34.000 Naam, kuna wengi wetu wanaosahau 00:04:34.000 --> 00:04:36.000 ninaposema "kuna namna mbalimbali za kuwa," 00:04:36.000 --> 00:04:38.000 Namaanisha kweli kuna namna mbalimbali za kuwa. NOTE Paragraph 00:04:39.000 --> 00:04:44.000 Chukulia kwa mfano, mtoto huyu wa Barasana huko kaskazini magharibi Amazoni 00:04:44.000 --> 00:04:45.000 watu wa majoka ya anakonda 00:04:45.000 --> 00:04:47.000 wanaoamini miujiza itokanayo na mto wa maziwa 00:04:47.000 --> 00:04:50.000 kutoka mashariki kwenye matumbo ya nyoka walotukuka. 00:04:50.000 --> 00:04:53.000 Naam, hawa ni watu ambao kwa kutambua 00:04:53.000 --> 00:04:55.000 hawawezi kutofautisha rangi ya bluu na rangi ya kijani 00:04:55.000 --> 00:04:57.000 kwakuwa paa la mbingu 00:04:57.000 --> 00:04:58.000 linalinganishwa na paa la msitu 00:04:58.000 --> 00:05:00.000 ambamo watu hawa wanategemea. 00:05:00.000 --> 00:05:03.000 Wana kanuni ya ajabu kuhusu ndoa na lugha 00:05:03.000 --> 00:05:05.000 ijulikanayo kama ndoa baina ya lugha tofauti: 00:05:05.000 --> 00:05:08.000 unalazimika kumuoa azungumzaye lugha tofauti na yako. 00:05:08.000 --> 00:05:10.000 Na hii inatokana na imani za kale, 00:05:10.000 --> 00:05:12.000 na bado hali ya kushangaza ipo kwenye nyumba hizi ndefu 00:05:12.000 --> 00:05:14.000 ambako kuna lugha sita au saba zinazozungumzwa 00:05:14.000 --> 00:05:16.000 kutokana na kuoana, 00:05:16.000 --> 00:05:19.000 hutomsikia yeyote akijifunza lugha. 00:05:19.000 --> 00:05:22.000 Wanasikiliza tu na kuanza kuongea. NOTE Paragraph 00:05:22.000 --> 00:05:24.000 Au, moja ya makabila ya kushangaza niliyowahi kuishi nayo, 00:05:24.000 --> 00:05:28.000 ni Waorani wa Kaskazini-Mashariki ya Ecuador, 00:05:28.000 --> 00:05:31.000 ni watu wa ajabu ambao walitembelewa kwa mara ya kwanza mwaka 1958. 00:05:31.000 --> 00:05:35.000 Mnamo mwaka 1957, wamishonari watano walijaribu kuwatembelea 00:05:35.000 --> 00:05:36.000 na wakafanya kosa kubwa. 00:05:36.000 --> 00:05:37.000 Walidondosha kutoka hewani 00:05:37.000 --> 00:05:39.000 picha zao za ukubwa nchi nane kwa kumi 00:05:39.000 --> 00:05:41.000 kitu ambacho tunaweza kusema ni ishara ya urafiki, 00:05:41.000 --> 00:05:43.000 wakasahau kwamba watu hawa wa misitu ya kitropiki 00:05:43.000 --> 00:05:46.000 hawakuwahi kuona kitu chochote chenye vina viwili kabla 00:05:46.000 --> 00:05:48.000 Wakaziokota picha hizi toka ardhini 00:05:48.000 --> 00:05:51.000 wakajaribu kuangalia kwa nyuma ili kupata umbile kamili 00:05:51.000 --> 00:05:53.000 hawakuona kitu, na wakaamini kwamba hizi ni kadi za wito 00:05:53.000 --> 00:05:56.000 toka kwa shetani, kwahiyo wakawachoma mikuki wamishonari na kuwaua. 00:05:57.000 --> 00:05:59.000 Lakini Waorani si kwamba tu waliwachoma wageni. 00:05:59.000 --> 00:06:00.000 Walichomana wao kwa wao. 00:06:00.000 --> 00:06:03.000 54% ya vifo vyao vilitokana na kuchomana mikuki wao kwa wao. 00:06:03.000 --> 00:06:06.000 Tulifuatilia vizazi nane vilivyopita, 00:06:06.000 --> 00:06:08.000 na tukapata matukio mawili tu ya vifo vya asilia 00:06:08.000 --> 00:06:10.000 na tulipowauliza zaidi watu habari hizi, 00:06:10.000 --> 00:06:12.000 wakakiri kwamba mmoja wao alikuwa mzee sana 00:06:12.000 --> 00:06:16.000 na angekufa kwa uzee, kwahiyo tukamchoma mkuki tu (Kicheko) 00:06:16.000 --> 00:06:19.000 Lakini pia wana ujuzi wa ajabu 00:06:19.000 --> 00:06:20.000 wa msituni ambao unashangaza sana. 00:06:20.000 --> 00:06:23.000 Wawindaji huweza kunusa harufu ya mkojo wa mnyama toka umbali wa hatua 40 00:06:23.000 --> 00:06:26.000 na wakakwambia ni kiumbe gani ameuacha mkojo huo. NOTE Paragraph 00:06:26.000 --> 00:06:28.000 Miaka ya 80, nilikuwa na kazi moja ya kusisimua 00:06:28.000 --> 00:06:30.000 nilipoulizwa na Profesa wangu wa Harvard 00:06:30.000 --> 00:06:32.000 iwapo ningependa kwenda Haiti, 00:06:33.000 --> 00:06:35.000 kupeleleza vikundi vya siri 00:06:35.000 --> 00:06:37.000 vilivyokuwa ngome kubwa ya Duvalier 00:06:37.000 --> 00:06:38.000 na majasusi wa Tonton Macoutes 00:06:38.000 --> 00:06:41.000 na kupata sumu itumikayo kutengeneza mizuka. 00:06:41.000 --> 00:06:44.000 ili kupata mantiki kutokana na uvumi 00:06:44.000 --> 00:06:47.000 ilinibidi nijaribu kuelewa kuhusu imani hii ya ajabu 00:06:47.000 --> 00:06:50.000 ya Vodoun, na Voodoo si kikundi cha uchawi wa nguvu za kiza 00:06:50.000 --> 00:06:53.000 Kinyume chake, ni mtazamo fulani wa ulimwengu nje ya maumbile. 00:06:53.000 --> 00:06:54.000 inashangaza. 00:06:54.000 --> 00:06:55.000 Iwapo nikikutaka utaje dini kuu za dunia, 00:06:55.000 --> 00:06:56.000 utasema nini? 00:06:56.000 --> 00:06:59.000 Ukristu, Uislamu, Ubudha, Ujudea, na kadhalika. NOTE Paragraph 00:06:59.000 --> 00:07:01.000 Huwa kuna bara moja linasahaulika, 00:07:01.000 --> 00:07:03.000 kwa mtazamo kwamba nchi za Afrika, kusini mwa Sahara 00:07:03.000 --> 00:07:05.000 hazikuwa na imani za kidini. Vema, kwa hakika, walikuwa nazo 00:07:05.000 --> 00:07:07.000 na Voodoo ni mchujo tu 00:07:08.000 --> 00:07:09.000 wa mawazo haya makuu ya kidini 00:07:09.000 --> 00:07:12.000 yaliyokuja wakati wa uhamisho wa kikatili wa kipindi cha utumwa. 00:07:12.000 --> 00:07:14.000 Lakini, kinachofanya voodoo kuwa ya kipekee 00:07:14.000 --> 00:07:16.000 ni huu uhusiano wa kuishi 00:07:16.000 --> 00:07:17.000 kati ya wazima na wafu. 00:07:17.000 --> 00:07:18.000 Kwahiyo, wanaoishi wanazaa mizimu. 00:07:18.000 --> 00:07:21.000 Mizimu inaswaliwa kutoka kwenye Maji Makuu, 00:07:21.000 --> 00:07:23.000 kuitikia mapigo ya muziki 00:07:23.000 --> 00:07:25.000 na kusambaratisha roho za wazima kwa muda 00:07:25.000 --> 00:07:29.000 ili kwa kipindi maalum na kifupi, makuhani wanakuwa mungu. 00:07:29.000 --> 00:07:31.000 Ndiyo maana Mavoodoo wanapenda kusema 00:07:31.000 --> 00:07:34.000 kwamba "Nyie watu weupe mnakwenda kanisani na kuongea kuhusu Mungu. 00:07:34.000 --> 00:07:36.000 Sisi tunacheza hekaluni na kuwa Mungu." 00:07:36.000 --> 00:07:39.000 Na ni kwa sababu mnaingiliwa, mnachukuliwa na mizimu, 00:07:39.000 --> 00:07:40.000 unawezaje kuathirika? 00:07:40.000 --> 00:07:43.000 Kwahiyo unaona maonyesho haya ya kushangaza: 00:07:43.000 --> 00:07:45.000 kuhani wa Voodoo akiwa katika hali ya kupandisha mori 00:07:45.000 --> 00:07:48.000 akifukiza uvumba bila hofu, 00:07:48.000 --> 00:07:51.000 ni kitendo cha kushangaza cha uwezo wa akili 00:07:51.000 --> 00:07:52.000 kuathiri mwili unaoibeba 00:07:52.000 --> 00:07:55.000 unapozimuliwa na hali ya kupandisha mori. NOTE Paragraph 00:07:56.000 --> 00:07:58.000 Na sasa, katika watu wote niliowahi kuishi nao, 00:07:58.000 --> 00:08:00.000 wa ajabu zaidi ni Wakogi 00:08:00.000 --> 00:08:03.000 wa Sierra Nevada ya Santa Marta kaskazini mwa Colombia. 00:08:03.000 --> 00:08:06.000 Wazawa wa ustaarabu wa kikatili wa kale 00:08:06.000 --> 00:08:09.000 ambao uliwahi kuenea uwanda wote wa Colombia katika pwani ya Caribbean 00:08:09.000 --> 00:08:10.000 wakati wa uvamizi, 00:08:10.000 --> 00:08:13.000 watu hawa walikimbilia kwenye safu ya milima ya kivolkano 00:08:13.000 --> 00:08:15.000 inayopanda juu ya pwani ya Caribbean 00:08:15.000 --> 00:08:17.000 Katika bara lililomwaga damu, 00:08:17.000 --> 00:08:20.000 hawa ni watu pekee ambao hawakushindwa vita na Waspanishi 00:08:20.000 --> 00:08:23.000 Mpaka leo, bado wanatawaliwa na makuhani wa kafara 00:08:23.000 --> 00:08:25.000 lakini mafunzo yao ya ukuhani ni ya ajabu sana 00:08:26.000 --> 00:08:28.000 Makuhani vijana wanachukuliwa toka kwenye familia zao 00:08:28.000 --> 00:08:30.000 katika umri wa miaka mitatu au minne, 00:08:30.000 --> 00:08:32.000 na kufichwa kwenye ulimwengu wa giza 00:08:32.000 --> 00:08:36.000 kwenye vibanda vya mawe chini ya malundo ya barafu kwa miaka 18. 00:08:36.000 --> 00:08:37.000 Vipindi viwili vya miaka tisa 00:08:37.000 --> 00:08:40.000 imepangwa hivyo makusudi kuigiza miezi tisa ya kukua 00:08:40.000 --> 00:08:42.000 waliokaa ndani ya tumbo la mama, 00:08:42.000 --> 00:08:45.000 na sasa kilimwengu wapo kwenye tumbo la mama mkuu. 00:08:45.000 --> 00:08:46.000 Na kwa muda wote huu, 00:08:47.000 --> 00:08:50.000 wanafundishwa maadili muhimu ya utamaduni wao, 00:08:50.000 --> 00:08:52.000 maadili ambayo yanatunza maombi ya sala zao 00:08:52.000 --> 00:08:55.000 na sala zao pekee ndizo zinatunza maumbile -- 00:08:55.000 --> 00:08:57.000 au twaweza kusema uwiano wa mazingira. 00:08:58.000 --> 00:08:59.000 Na mwisho wa mafunzo haya ya ajabu, 00:08:59.000 --> 00:09:01.000 siku moja wanatolewa nje ghafla 00:09:01.000 --> 00:09:04.000 na kwa mara ya kwanza katika maisha yao, wakiwa na umri wa miaka 18 00:09:04.000 --> 00:09:08.000 wanaona jua likichomoza. Na katika kipindi hicho cha ufahamu 00:09:08.000 --> 00:09:11.000 wa mwanga wa kwanza wakati Jua linapoangaza milima 00:09:11.000 --> 00:09:12.000 yenye mandhari ya kupendeza, 00:09:13.000 --> 00:09:15.000 mara vitu vyote walivyojifunza kwa nadharia 00:09:15.000 --> 00:09:18.000 vinatimia kwa utukufu mkubwa. Na kuhani anarudi nyuma 00:09:18.000 --> 00:09:20.000 na kusema "Mnaona? Ni hakika kama nilivyowaambia. 00:09:20.000 --> 00:09:23.000 Ni nzuri sana. Ni jukumu lenu kuilinda." 00:09:23.000 --> 00:09:25.000 Wanajiita kaka wakubwa 00:09:25.000 --> 00:09:28.000 na wanasema sisi, ambao ni kaka wadogo, 00:09:28.000 --> 00:09:31.000 tunaohusika na kuiharibu dunia, NOTE Paragraph 00:09:32.000 --> 00:09:34.000 Na sasa, kiwango cha ufahamu kinakuwa muhimu sana. 00:09:34.000 --> 00:09:36.000 Tunapofikiria kuhusu wazawa wa asilia na mandhari ya nchi, 00:09:36.000 --> 00:09:38.000 tunakuwa aidha tunamfuata Rousseau 00:09:38.000 --> 00:09:41.000 na nadharia ya ukatili halali, 00:09:41.000 --> 00:09:43.000 ambao una maanisha kwamba ubaguzi wa rangi ni urahisi, 00:09:43.000 --> 00:09:46.000 au badala yake, tumfuate Thoreau 00:09:46.000 --> 00:09:48.000 na kusema watu hawa wapo karibu zaidi na Dunia kuliko sisi, 00:09:48.000 --> 00:09:50.000 Vema, wazawa asilia hawana unyovu wa moyo 00:09:50.000 --> 00:09:52.000 wala hawasumbuliwi na mawazo ya kukumbuka nyumbani 00:09:52.000 --> 00:09:54.000 Hakuna fursa kubwa 00:09:54.000 --> 00:09:56.000 kwenye mabwawa ya malaria huko Asmat 00:09:56.000 --> 00:09:59.000 au kwenye upepo mkali wa Tibet, lakini wameweza, hata hivyo, 00:09:59.000 --> 00:10:03.000 kwa kupitia ibada fulani, wameweza kutengeneza mtazamo wa Dunia 00:10:03.000 --> 00:10:06.000 ambao unazingatia kujijua au kuwa karibu na kujijua, 00:10:06.000 --> 00:10:08.000 lakini kwa kutumia ufahamu wa juu zaidi: 00:10:08.000 --> 00:10:11.000 wazo la kwamba Dunia yenyewe yaweza kuwepo 00:10:12.000 --> 00:10:14.000 kwakuwa imepewa pumzi kwa ufahamu wa binadamu. NOTE Paragraph 00:10:14.000 --> 00:10:16.000 Naam, hiyo ina maana gani? 00:10:16.000 --> 00:10:18.000 Ina maana kwamba mtoto mdogo wa huko Andes 00:10:18.000 --> 00:10:20.000 aliyelelewa kuamini kwamba milima ni mizimu ya Apu 00:10:20.000 --> 00:10:22.000 inayoleta hatima yake 00:10:22.000 --> 00:10:25.000 atakuwa binadamu tofauti kabisa 00:10:25.000 --> 00:10:28.000 na atakuwa na uhusiano tofauti na maliasili hiyo 00:10:28.000 --> 00:10:30.000 au sehemu ile ambako mtoto wa kutoka Montana 00:10:30.000 --> 00:10:33.000 amelelewa kuamini kwamba mlima ni mkusanyiko wa mawe 00:10:33.000 --> 00:10:34.000 yanayosubiri kuchimbuliwa. 00:10:34.000 --> 00:10:38.000 Ama ni makao ya mizimu au malundo ya madini si jambo muhimu. 00:10:38.000 --> 00:10:41.000 Kinachosisimua ni nadharia inayo ainisha uhusiano huo 00:10:41.000 --> 00:10:43.000 kati ya mtu na ulimwengu asilia 00:10:43.000 --> 00:10:45.000 Nilikulia katika misitu ya British Columbia 00:10:45.000 --> 00:10:47.000 na kuamini kwamba misitu hiyo ipo kwa ajili ya kukatwa, 00:10:47.000 --> 00:10:49.000 Hiyo imenifanya kuwa mtu tofauti 00:10:49.000 --> 00:10:51.000 sana na rafiki zangu miongoni mwa Kwakiutl 00:10:51.000 --> 00:10:53.000 ambao wanaamini kwamba misitu ni makao ya Hukuk 00:10:53.000 --> 00:10:54.000 na lango la peponi 00:10:54.000 --> 00:10:57.000 na mizimu mumiani iishiyo miisho ya kaskazini mwa ulimwengu, 00:10:57.000 --> 00:11:01.000 mizimu wanayokumbana nayo wakati wa simiko la Hamatsa NOTE Paragraph 00:11:01.000 --> 00:11:03.000 Na sasa, ukianza kuzingatia wazo 00:11:03.000 --> 00:11:05.000 kwamba tamaduni hizi zinaweza kujenga mitazamo tofauti 00:11:05.000 --> 00:11:06.000 waweza kuanza kuelewa 00:11:06.000 --> 00:11:11.000 baadhi ya uvumbuzi wao wa ajabu. Chukulia mfano mmea huu hapa, 00:11:11.000 --> 00:11:13.000 Ni picha niliyoipiga Kaskazini mwa Amazoni mwezi Aprili 00:11:13.000 --> 00:11:16.000 Hii ni ayahuasca, wengi wenu mmekwisha sikia habari zake, 00:11:16.000 --> 00:11:19.000 moja kati ya michanyato mikali kabisa ya kuzingulia 00:11:19.000 --> 00:11:21.000 kati ya vifaa vyote vya mashamani 00:11:21.000 --> 00:11:23.000 kinachoifanya ayahuasca kuwa ya kushangaza zaidi 00:11:23.000 --> 00:11:27.000 si kiwango cha hali ya juu cha dawa inayotengenezwa 00:11:27.000 --> 00:11:31.000 bali maudhui yake. Inatengenezwa kutokana na vitu viwili 00:11:31.000 --> 00:11:33.000 Kwa upande mmoja ni mti wa liana 00:11:33.000 --> 00:11:35.000 ambao ni jamii ya beta-carbolines 00:11:35.000 --> 00:11:38.000 harmine, harmoline, ambayo ni nishai 00:11:38.000 --> 00:11:40.000 Kuinywa peke yake 00:11:40.000 --> 00:11:42.000 ni afadhali uvute moshi mzito wa bluu 00:11:42.000 --> 00:11:44.000 unaingia kwenye ufahamu wako 00:11:44.000 --> 00:11:47.000 ambao umechanganywa na majani ya jamii ya kahawa 00:11:47.000 --> 00:11:49.000 yaitwayo Psychotria viridis. 00:11:49.000 --> 00:11:52.000 Mmea huu una tindikali za tryptamines, 00:11:52.000 --> 00:11:56.000 inafanana sana na kisisimuzi cha mfumo wa ufahamu cha dimethyltryptamine-5, 00:11:56.000 --> 00:11:57.000 methoxydimethyltryptamine. 00:11:57.000 --> 00:11:59.000 Iwapo ungaliwaona Mayonami 00:11:59.000 --> 00:12:01.000 wakiingiza vitu kwenye pua zao, 00:12:01.000 --> 00:12:04.000 mchanyato wanaoutengeneza kwa mimea mbalimbali 00:12:04.000 --> 00:12:08.000 ambayo pia ina methoxydimethyltryptamine. 00:12:08.000 --> 00:12:10.000 Kuingiza unga huo kwenye pua yako 00:12:10.000 --> 00:12:14.000 ni kama vile kuzibuliwa kama risasi toka kwenye bomba la bunduki 00:12:14.000 --> 00:12:21.000 lililosakafiwa kwa michoro ya baroque na ukatua kwenye bahari ya umeme, (Kicheko) 00:12:21.000 --> 00:12:23.000 Haifanyi upotoshaji wa hali halisi; 00:12:23.000 --> 00:12:24.000 inayeyusha ufahamu wa hali halisi. NOTE Paragraph 00:12:24.000 --> 00:12:27.000 Kwa kweli, nilikuwa nabishana na mwalimu wangu Profesa Richard Evan Shultes -- 00:12:27.000 --> 00:12:29.000 mtu ambaye alianzisha zama za uchunguzi wa madawa yanayobadili ufahamu 00:12:29.000 --> 00:12:31.000 kwa uvumbuzi wake wa uyoga wa ajabu 00:12:31.000 --> 00:12:33.000 nchini Mexico mnamo miaka ya 1930. 00:12:33.000 --> 00:12:35.000 Nilikuwa nabisha kwamba huwezi kuainisha tryptamines hizi 00:12:35.000 --> 00:12:38.000 kama vilevinishai kwakuwa wakati umezinguliwa nazo 00:12:38.000 --> 00:12:42.000 hatokuwepo mtu mwingine akisubiri kushuhudia muweweseko wake. (Kicheko) NOTE Paragraph 00:12:42.000 --> 00:12:45.000 Lakini kuhusu tryptamines haziwezi kunywewa 00:12:45.000 --> 00:12:47.000 kwakuwa zimeathiriwa na kimeng'enya 00:12:47.000 --> 00:12:50.000 vinavyopatikana kiasilia katika utumbo wa binadamu na huitwa monoamine oxidase 00:12:50.000 --> 00:12:53.000 Vinaweza kunywewa tu iwapo vitachanganywa na 00:12:53.000 --> 00:12:56.000 kemikali nyinginezo zinazoweza kuathiri vimeng'enya vya MAO 00:12:56.000 --> 00:12:57.000 Na sasa, vitu vya kushangaza 00:12:57.000 --> 00:13:01.000 ni hizo beta-carbolines zinazopatikana kwenye liana 00:13:01.000 --> 00:13:04.000 ni vidhibiti vya MAO kwa namna fulani muhimu 00:13:05.000 --> 00:13:08.000 kuizimua tryptamine. Na hapo unajiuliza swali 00:13:08.000 --> 00:13:12.000 Ilikuwaje kwenye mimea mbalimbali zaidi ya 80,000, 00:13:12.000 --> 00:13:16.000 watu hawa walichagua hii miwili ambayo haifanani maumbile 00:13:16.000 --> 00:13:17.000 lakini ambayo ikichanganywa kwa namna hii, 00:13:17.000 --> 00:13:19.000 inatengeneza mchanganyiko wa kemikali 00:13:19.000 --> 00:13:21.000 kamilifu ambayo ni zaidi ya jumla ya kila kimojawapo? NOTE Paragraph 00:13:21.000 --> 00:13:24.000 Vema, tunatumia maneno rahisi, kwamba walikuwa wakijaribu kubahatisha, 00:13:24.000 --> 00:13:25.000 jambo ambalo halina ukweli wowote. 00:13:26.000 --> 00:13:29.000 Lakini ukiwauliza Wahindi watakwambia, "Mimea inaongea nasi." NOTE Paragraph 00:13:29.000 --> 00:13:30.000 Vema, hiyo ina maana gani? 00:13:30.000 --> 00:13:34.000 Kabila hili la Cofan wana aina 17 za ayahuasca, 00:13:34.000 --> 00:13:37.000 na wanaweza kuitofautisha kutoka mbali huko msituni, 00:13:38.000 --> 00:13:42.000 na zote hizi kwetu sisi zinaonekana kuwa sawa. 00:13:42.000 --> 00:13:44.000 Halafu unawauliza waliwezaje kuziainisha 00:13:44.000 --> 00:13:47.000 na wanasema " Nilidhani unajua masuala ya mimea, 00:13:47.000 --> 00:13:49.000 nina maana, hujui chochote?" Na nikasema "Hapana." 00:13:49.000 --> 00:13:52.000 Naam, inakuwa kwamba unachukua moja ya kila hizo aina 17 00:13:52.000 --> 00:13:55.000 usiku wa mbalamwezi na zinakuimbia kwa mlio tofauti 00:13:55.000 --> 00:13:57.000 Sasa, hiyo haiwezi kukupatia Ph.D. ya Harvard, 00:13:57.000 --> 00:14:01.000 lakini hii inavutia zaidi ya kuhesabu chavua. NOTE Paragraph 00:14:01.000 --> 00:14:02.000 Na sasa, 00:14:02.000 --> 00:14:05.000 (Makofi) 00:14:05.000 --> 00:14:07.000 na tatizo -- na tatizo ni kwamba hata sisi 00:14:07.000 --> 00:14:09.000 tunaotetea hatima ya wazawa asilia 00:14:09.000 --> 00:14:10.000 tunawaona kama wanavutia 00:14:10.000 --> 00:14:12.000 lakini wamebanwa na mipaka ya historia 00:14:12.000 --> 00:14:15.000 wakati ulimwengu halisi, yaani ulimwengu wetu, unasonga mbele. 00:14:15.000 --> 00:14:17.000 Vema, ukweli ni kwamba karne ya 20, miaka 300 kuanzia sasa, 00:14:17.000 --> 00:14:20.000 haitakumbukwa kwa vita vyake 00:14:20.000 --> 00:14:21.000 au uvumbuzi wa kiteknolojia 00:14:21.000 --> 00:14:23.000 bali ni zama ambazo tulikaa 00:14:24.000 --> 00:14:26.000 na kuunga mkono waziwazi au tu kukubali 00:14:26.000 --> 00:14:29.000 uharibifu mkubwa wa urithi mkubwa wa kibaiolojia au kiutamaduni 00:14:29.000 --> 00:14:32.000 duniani. Kwa sasa, tatizo si mabadiliko. 00:14:32.000 --> 00:14:34.000 Tamaduni zote wakati wote 00:14:34.000 --> 00:14:37.000 zimejihusisha na mchezo 00:14:37.000 --> 00:14:38.000 wa masuala mapya ya kimaisha. NOTE Paragraph 00:14:39.000 --> 00:14:41.000 Na tatizo si teknolojia peke yake. 00:14:42.000 --> 00:14:44.000 Wahindi Wekundu Sioux hawajaacha kuwa Sioux 00:14:44.000 --> 00:14:45.000 walipoacha upinde na mshale 00:14:45.000 --> 00:14:47.000 kama vile ambavyo Mmarekani kuacha kuwa Mmarekani 00:14:47.000 --> 00:14:49.000 alipoacha farasi na mkokoteni wake 00:14:49.000 --> 00:14:50.000 Si mabadiliko ya teknolojia 00:14:50.000 --> 00:14:54.000 yanayotishia uhai wa ethnosifia. Ni ubabe. 00:14:54.000 --> 00:14:56.000 Sura katili ya miliki. 00:14:56.000 --> 00:14:58.000 Na chochote unachokiangalia duniani, 00:14:58.000 --> 00:15:01.000 utaona kwamba hizi si tamaduni tu zinazopotea. 00:15:01.000 --> 00:15:03.000 Hawa ni watu halisi wanaoishi 00:15:03.000 --> 00:15:06.000 wakiondolewa uhai kwa nguvu zinazojulikana 00:15:06.000 --> 00:15:08.000 lakini ziko nje ya uwezo wao kuzimudu. 00:15:08.000 --> 00:15:10.000 Iwapo ni uharibifu mbaya wa misitu 00:15:11.000 --> 00:15:13.000 kwenye nchi ya Wapenani -- 00:15:13.000 --> 00:15:16.000 watu waishio kwa kuhamahama huko Asia ya Kusinimashariki, kutoka Sarawak -- 00:15:16.000 --> 00:15:20.000 watu walioshi huru mwituni mpaka kizazi kimoja kilichopita, 00:15:20.000 --> 00:15:23.000 na sasa wote wamezuiliwa na kutumikishwa 00:15:23.000 --> 00:15:25.000 kwenye kingo za mito, 00:15:25.000 --> 00:15:29.000 ambako utaona mito yenyewe imechafuliwa kwa tope 00:15:29.000 --> 00:15:31.000 yanayoonekana kubeba takriban nusu ya ukubwa wa kisiwa cha Borneo 00:15:31.000 --> 00:15:32.000 kwenda Bahari ya China ya Kusini, 00:15:32.000 --> 00:15:34.000 ambako meli za Kijapani zinasubiri 00:15:34.000 --> 00:15:38.000 tayari kubeba magogo mabichi yaliyozolewa toka misituni. 00:15:38.000 --> 00:15:39.000 Au suala la Wayanomami, 00:15:39.000 --> 00:15:41.000 ni ugonjwa ambao umeingia, 00:15:41.000 --> 00:15:43.000 wakati wa uvumbuzi wa dhahabu. NOTE Paragraph 00:15:43.000 --> 00:15:45.000 Au tukienda kwenye milima ya Tibet, 00:15:45.000 --> 00:15:47.000 ambako ninafanya utafiti mwingi kwa sasa, 00:15:48.000 --> 00:15:51.000 utaona sura ya kutisha ya ubeberu wa kisiasa. 00:15:51.000 --> 00:15:53.000 Kama ujuavyo, mauaji ya halaiki, kumaliza maisha ya watu 00:15:53.000 --> 00:15:55.000 kunalaaniwa ulimwenguni kote, lakini mauaji ya kiutamaduni, 00:15:56.000 --> 00:15:59.000 uharibifu wa utaratibu wa maisha ya watu, siyo tu kwamba unalaaniwa, 00:15:59.000 --> 00:16:02.000 unashangiliwa -- na makundi mengi 00:16:02.000 --> 00:16:04.000 kuwa kama mkakati wa maendeleo. 00:16:04.000 --> 00:16:07.000 Na huwezi kuelewa uchungu wa Tibet 00:16:07.000 --> 00:16:09.000 mpaka usafiri kwa barabara. 00:16:09.000 --> 00:16:13.000 Niliwahi kusafiri maili 6,000 kutoka Chengdu huko Magharibi mwa China 00:16:13.000 --> 00:16:16.000 kwa barabara kupitia kusinimashariki Tibet mpaka Lhasa 00:16:16.000 --> 00:16:20.000 nikiwa na mwenzi ambaye ni kijana, na mpaka nilipofika Lhasa 00:16:20.000 --> 00:16:23.000 ndipo nikaelewa ukweli kuhusu takwimu 00:16:23.000 --> 00:16:24.000 unazozisikia. 00:16:24.000 --> 00:16:28.000 majengo matakatifu takriban 6,000 yamebomolewa kuwa vumbi na majivu. 00:16:28.000 --> 00:16:31.000 watu milioni 1.2 wameuawa na makada 00:16:31.000 --> 00:16:32.000 wakati wa Mapinduzi ya Utamaduni 00:16:33.000 --> 00:16:35.000 Baba wa kijana huyu alitawazwa kuwa naibu wa Lama. 00:16:35.000 --> 00:16:37.000 Kwa sababu hiyo aliuawa mara tu 00:16:37.000 --> 00:16:39.000 ya uvamizi wa China. 00:16:39.000 --> 00:16:41.000 Mjomba wake alitoroka pamoja na mhashamu kwenda uhamishoni 00:16:41.000 --> 00:16:44.000 nchini Nepal 00:16:44.000 --> 00:16:46.000 Mama yake alifungwa kwa sababu tu -- 00:16:46.000 --> 00:16:48.000 alikuwa tajiri. 00:16:49.000 --> 00:16:51.000 Yeye alipenyezwa kwa siri kuingizwa jela akiwa na umri wa miaka miwili 00:16:51.000 --> 00:16:53.000 kujificha kwenye sketi za mamaake 00:16:53.000 --> 00:16:55.000 kwakuwa hakuweza kustahimili kuishi bila mwanae. 00:16:55.000 --> 00:16:57.000 Dada yake aliyefanya kitendo hicho cha kishujaa 00:16:57.000 --> 00:16:58.000 alipelekwa kwenye kambi ya elimu 00:16:58.000 --> 00:17:00.000 Siku moja kwa bahati mbaya alikumbana na kundi la askari 00:17:01.000 --> 00:17:03.000 wa Mao, na kwa kosa hilo, 00:17:03.000 --> 00:17:06.000 akahukumiwa kifungo cha miaka saba na kazi ngumu. 00:17:06.000 --> 00:17:09.000 Machungu ya Tibet hayavumiliki, 00:17:09.000 --> 00:17:12.000 lakini ujasiri wa watu hawa ni kitu cha kusisimua. NOTE Paragraph 00:17:13.000 --> 00:17:16.000 Na mwisho wake, inakuja mwisho kwenye uchaguzi, 00:17:16.000 --> 00:17:19.000 Tunataka kuishi kwenye ulimwengu unaochosha wa utamaduni mmoja 00:17:19.000 --> 00:17:22.000 au tunapenda kuwa na mtandao wa tamaduni mbalimbali? 00:17:22.000 --> 00:17:25.000 Margaret Mead, mtaalam maarufu wa mambo ya kale, kabla ya kifo chake alisema 00:17:25.000 --> 00:17:28.000 wasiwasi wake mkubwa ni kwamba tunazidi kuelekea kwenye 00:17:28.000 --> 00:17:30.000 hii hali ya mtazamo mmoja wa kilimwengu 00:17:30.000 --> 00:17:35.000 si tu kwamba tutaona uwezo mkubwa wa ufahamu wa binadamu 00:17:35.000 --> 00:17:39.000 ukipunguzwa kuwa mawazo finyu, 00:17:39.000 --> 00:17:40.000 bali tutazinduka siku moja 00:17:40.000 --> 00:17:43.000 tukiwa tumesahau kwamba kuna uwezekano tofauti wa mambo. NOTE Paragraph 00:17:44.000 --> 00:17:47.000 Na ni taadhima kubwa kukumbuka kwamba kizazi chetu kimekuwepo kwa 00:17:47.000 --> 00:17:49.000 takriban miaka 600,000 00:17:49.000 --> 00:17:52.000 Mapinduzi ya Kilimo -- yaliyoanzisha ukulima, 00:17:52.000 --> 00:17:54.000 tulipo salim amri kwenye imani ya mbegu 00:17:54.000 --> 00:17:56.000 ushairi wa shaman ulisambaratishwa 00:17:56.000 --> 00:17:57.000 kwa maandiko ya ukuhani 00:17:57.000 --> 00:18:00.000 tukajenga daraja za umiliki ziada -- 00:18:00.000 --> 00:18:02.000 ni miaka 10,000 iliyopita tu. 00:18:02.000 --> 00:18:04.000 Maendeleo ya viwanda kama tuyajuavyo 00:18:04.000 --> 00:18:06.000 yana si zaidi ya miaka 300. 00:18:06.000 --> 00:18:08.000 Na sasa, historia hiyo ya juu juu hainishawishi 00:18:08.000 --> 00:18:11.000 kwamba tuna majibu ya matatizo yetu yote 00:18:11.000 --> 00:18:13.000 yatakayo tufariji katika hatima ya milenia 00:18:13.000 --> 00:18:15.000 Wakati hizi tamaduni mbalimbali ulimwenguni 00:18:15.000 --> 00:18:18.000 zikiulizwa maana ya kuwa binadamu, 00:18:18.000 --> 00:18:20.000 zitakujibu kwa sauti 10,000 tofauti. NOTE Paragraph 00:18:20.000 --> 00:18:26.000 Na kwa kupitia wimbo huo ndipo tutatambua uwezekano 00:18:26.000 --> 00:18:29.000 wa kuona kwamba sisi ni viumbe wenye ufahamu, 00:18:29.000 --> 00:18:32.000 kufahamu fika kuhakikisha watu wote na bustani zote 00:18:32.000 --> 00:18:38.000 zinapata namna ya kustawi. Na kuna vipindi vya matumaini. NOTE Paragraph 00:18:38.000 --> 00:18:41.000 Hii ni picha niliyoipiga kwenye ncha ya kaskazini mwa kisiwa cha Baffin 00:18:41.000 --> 00:18:43.000 nilipokwenda kuwinda nyangumi wenye pembe nikiwa na Wainuiti, 00:18:44.000 --> 00:18:47.000 na mtu huyu, Olaya, alinisimulia hadithi ya ajabu kuhusu babu yake. 00:18:48.000 --> 00:18:50.000 Serikali ya Canada haikuwa ikiwatendea haki 00:18:50.000 --> 00:18:52.000 Wainuiti, katika miaka ya 1950, 00:18:52.000 --> 00:18:55.000 ili kujenga utaifa, tuliwahamishia kwenye vijiji. 00:18:55.000 --> 00:18:59.000 Babu yake alikataa kwenda. 00:18:59.000 --> 00:19:03.000 Nduguze, kwa kuhofia maisha yake, wakampokonya silaha zake zote, 00:19:03.000 --> 00:19:04.000 na vifaa vyake vyote. 00:19:05.000 --> 00:19:07.000 Na sasa, uelewe kwamba Wainuiti hawakuogopa baridi; 00:19:07.000 --> 00:19:08.000 walijinufaisha nayo. 00:19:08.000 --> 00:19:11.000 Mikokoteni ya kuteleza kwenye barafu ilitengenezwa kwa samaki 00:19:11.000 --> 00:19:12.000 na kufunikwa kwa ngozi ya swala. 00:19:12.000 --> 00:19:17.000 Kwahiyo babu yake mtu huyu hakutishika na usiku wa huko Aktika 00:19:17.000 --> 00:19:19.000 au upepo mkali ulokuwa ukipuliza 00:19:19.000 --> 00:19:22.000 Alitoka nje, akavua suruali yake 00:19:23.000 --> 00:19:26.000 na kunyea mkononi. Na kinyesi kilipoanza kuganda, 00:19:26.000 --> 00:19:29.000 akafinyanga katika umbile la upanga. 00:19:29.000 --> 00:19:31.000 Akatemea mate kwenye upande wa makali ya upanga huo wa kinyesi 00:19:31.000 --> 00:19:34.000 na baadae inaganda na kuwa ngumu, na aliitumia kumuua mbwa. 00:19:34.000 --> 00:19:37.000 Akamchuna mbwa na kuboresha silaha yake, 00:19:37.000 --> 00:19:40.000 akachukua ubavu wa mbwa na kutengeneza mkokoteni wa kuteleza, 00:19:41.000 --> 00:19:42.000 akamfunga mbwa wa pili, 00:19:42.000 --> 00:19:46.000 na kutokomea kwenye uwanda wa barafu, kisu cha kinyesi kibindoni. 00:19:46.000 --> 00:19:50.000 Halafu unazungumzia kujikwamua bila kitu chochote (Kicheko) NOTE Paragraph 00:19:50.000 --> 00:19:51.000 Na hii, kwa namna mbalimbali, 00:19:51.000 --> 00:19:53.000 (Makofi) 00:19:53.000 --> 00:19:55.000 hii ni ishara ya ujasiri wa Wainuiti 00:19:55.000 --> 00:19:58.000 na wazawa wote asilia ulimwenguni kote. 00:19:58.000 --> 00:20:00.000 Serikali ya Canada mnamo Aprili 1999 00:20:00.000 --> 00:20:03.000 waliwarudishia mamlaka Wainuiti 00:20:03.000 --> 00:20:06.000 kwenye eneo kubwa kuliko California na Texas yakiunganishwa pamoja. 00:20:06.000 --> 00:20:08.000 Ni nchi yetu mpya. Inaitwa Nunavut. 00:20:09.000 --> 00:20:12.000 Ni jimbo linalojitegemea. Wanasimamia maliasili zote za madini. 00:20:12.000 --> 00:20:14.000 Ni mfano wa ajabu jinsi ambavyo taifa 00:20:14.000 --> 00:20:18.000 linafikia -- au kutafuta muafaka na watu wake. NOTE Paragraph 00:20:19.000 --> 00:20:22.000 Na mwisho, hatimaye, naona ni wazi kabisa 00:20:22.000 --> 00:20:23.000 walau wengi wetu tulosafiri 00:20:23.000 --> 00:20:25.000 kwenye sehemu hizi za mbali kwenye dunia, 00:20:27.000 --> 00:20:28.000 tumegundua si mbali tena. 00:20:28.000 --> 00:20:30.000 Ni makazi ya mtu fulani. 00:20:30.000 --> 00:20:32.000 Yanaonyesha matawi ya mawazo ya binadamu 00:20:32.000 --> 00:20:36.000 kwamba nenda nyuma kwenye mwanzo wa nyakati. Na kwetu sote, 00:20:36.000 --> 00:20:39.000 ndoto za watoto hawa, kama vile ndoto za watoto wetu wenyewe, 00:20:39.000 --> 00:20:42.000 zimekuwa sehemu ya jiografia ya matumaini. NOTE Paragraph 00:20:42.000 --> 00:20:46.000 Kwahiyo, tunachojaribu kufanya National Geographic hatimaye, 00:20:46.000 --> 00:20:50.000 ni, tunaamini kwamba wanasiasa hawafanikishi lolote. 00:20:50.000 --> 00:20:51.000 Huo ni ukosoaji wa hoja -- 00:20:51.000 --> 00:20:53.000 (Makofi) 00:20:53.000 --> 00:20:55.000 tunadhani kwamba wakosoaji hawana ushawishi, 00:20:55.000 --> 00:20:58.000 lakini tunaamini kwamba kuhadithia kutaibadili dunia, 00:20:58.000 --> 00:21:01.000 na kwahiyo sisi ni miongoni mwa taasisi bora zaidi za masimulizi 00:21:01.000 --> 00:21:04.000 duniani. Tunapata watembezi milioni 35 kwenye tovuti yetu kila mwezi. 00:21:04.000 --> 00:21:07.000 Nchi 156 zinarusha matangazo ya televisheni yetu. 00:21:08.000 --> 00:21:10.000 Majarida yetu yanasomwa na mamilioni. 00:21:10.000 --> 00:21:13.000 Na tunachokifanya ni safari nyingi 00:21:13.000 --> 00:21:15.000 kwenda kwenye ethnosifia ambako tunawapeleka watazamaji wetu 00:21:15.000 --> 00:21:17.000 kwenye sehemu ambako kuna maajabu ya kiutamaduni 00:21:18.000 --> 00:21:20.000 ambayo hawatoweza kuvumilia bali kushangazwa 00:21:20.000 --> 00:21:22.000 na wanachokiona, na natumaini, kwahiyo, 00:21:22.000 --> 00:21:25.000 kukubali taratibu, mmoja mmoja, 00:21:25.000 --> 00:21:27.000 kiini cha uvumbuzi wa elimu ya mambo ya kale: 00:21:27.000 --> 00:21:31.000 kwamba ulimwengu unastahili kuwepo kwa namna mbalimbali 00:21:31.000 --> 00:21:32.000 na kwamba tunaweza kupata namna ya kuishi 00:21:32.000 --> 00:21:35.000 katika ulimwengu wa tamaduni tofauti 00:21:35.000 --> 00:21:37.000 ambako busara zote za watu 00:21:37.000 --> 00:21:40.000 zitachangia ustawi wetu sote NOTE Paragraph 00:21:40.000 --> 00:21:41.000 Asante sana. 00:21:41.000 --> 00:21:43.000 (Makofi)