Kama ujuavyo, moja ya raha kubwa za kusafiri
na moja ya furaha za utafiti wa mahusiano ya kikabila
ni fursa ya kuishi miongoni mwao
hao wasiosahau namna za kijadi
ambao wangali wakihisi ya kale kwenye upepo,
na kuyagusa juu ya mawe yaliyosafishwa na mvua,
na kuyaonja kwenye majani machungu ya mimea.
Kujua kwamba wanaoabudu chuipamba bado wana safari kupita mbingu za mbali,
au imani za wazee wa Kiinuiti zinaleta maana,
au kwamba huko Himalaya,
Mabudha bado wanaifuata pumzi ya Dharma,
ni katika kukumbuka utambuzi wa msingi wa anthropolojia,
na kwamba mtazamo wa ulimwengu tunamoishi
haupo kihalisia,
bali ni nadharia tu ya ukweli,
ni matokeo ya jozi moja tu ya machaguo kadhaa
ambayo mababu zetu walifanya, japo kwa mafanikio, vizazi kadhaa vilivyopita.
Na kwa hakika, sote tunashabihiana katika kufuata kanuni za maumbile
Sote tunazaliwa. Sote tunazaa watoto.
Tunapitia kafara za kusimikwa,
Tunalazimika kukabiliana na ukatili wa kutenganishwa kwa kifo
haitushangazi kwamba sote tunaimba, sote tunacheza,
sote tuna sanaa.
Lakini kinachosisimua zaidi ni namna pekee za mapigo ya wimbo,
mahadhi ya dansi kwa kila utamaduni.
Na iwapo ni Wapenani wa misitu ya Borneo
au makuhani wa Voodoo nchini Haiti
au majemedari wa jangwa la Kaisut Kaskazini mwa Kenya,
au matabibu wa Kikurandero wa milima ya Andes,
au nyumba ya kuhamishika iliyopo katikati ya Sahara
Huyu ndiye mwenzi ambaye nilisafiri nae jangwani
mwezi mmoja uliopita
au mchunga mbuzipori wa miteremko ya Qomolangma,
Everest, mungu mke wa ulimwengu.
Watu wote hawa wanatufundisha kwamba kuna namna nyingine za kuwa,
namna tofauti za kufikiria
namna mbalimbali za kujiwekeza katika Dunia.
Na hili ndilo wazo, ambalo ukilifikiria,
laweza kukupa tumaini,
Sasa, kwa pamoja tamaduni nyingi mbalimbali za ulimwengu
zinafanya mtandao wa maisha ya kiroho na kiutamaduni
unaoifunika dunia,
na ni muhimu kwa ustawi wa dunia
hali kadhalika mtandao wa kibaiolojia wa maisha unaoujua kama biosifia.
Na waweza kufikiria kwamba mtandao huu wa kiutamaduni kwenye maisha
kuwa ni ethnosifia
na waweza kuainisha ethnosifia
kuwa ni jumla ya mawazo na ndoto, imani,
mitazamo, hamasa, vipawa vilivyohuishwa
na mawazo ya binadamu tokea mapambazuko ya ufahamu.
Ethnosifia ni urithi mkuu wa utu,
ni ishara ya kila namna tulivyo
na kila namna tuwezavyo kuwa viumbe wadadisi ajabu
Na kwa namna ambavyo biosifia imeharibiwa,
ndivyo pia ethnosifia
--na iwapo kwa kiwango kikubwa zaidi.
Hakuna mwanabaiolojia, kwa mfano, awezaye kusema
kwamba 50% ya viumbe wote au zaidi wamefikia au wapo
katika hatari ya kuteketea kwakuwa si kweli,
na pia kwamba -- tishio kubwa la maafa
katika uwanja wa mtandao wa kibailojia
nadra sana unaangalia kwa mtazamo tunaodhania kuwa bora zaidi
kwenye uwanja wa mtandao wa utamaduni.
Na kielelezo kikubwa cha muelekeo huo ni kupotea kwa lugha.
Wakati nyote mliopo humu ndani mlipozaliwa,
kulikuwepo lugha 6,000 zikitumika duniani.
Kwa sasa, lugha si mkusanyiko wa maneno
au mkusanyiko wa kanuni za sarufi.
Lugha ni mwanga wa roho ya binadamu.
Ni chombo ambacho hupitisha uhai wa tamaduni fulani
kuja kwenye ulimwengu wa vitu.
Kila lugha ni mkuzo wa msitu wa akili,
mgawanyiko wa vijito, wazo, bioanuwai ya mambo ya kiroho,
Miongoni mwa lugha hizo 6,000 mpaka leo tunapokuwa hapa Monterey,
takriban nusu yake hazitamkwi kwenye masikio ya watoto.
Hazifundishwi kwa watoto wachanga tena,
maana yake ni kwamba, kwa hakika, labda kama kuna mambo yatabadilika,
zimeshakufa.
Hakuna upweke unaozidi ule wa kugubikwa na ukimya,
wa kuwa mtu wa mwisho kabisa kuongea lugha yako,
kutokuwa na namna ya kurithisha busara za mababu
au kutarajia ahadi za watoto?
Na zaidi, kinachotisha ni hatima ya mtu fulani
sehemu fulani ya Dunia takriban kila wiki mbili,
kwa sababu kila wiki mbili, kuna mzee anafariki dunia
na anakwenda kaburini na silabi za mwisho
za lugha ya kale.
Na najua kuna baadhi yenu mngesema,"Naam, si ingekuwa vema?
Si ingekuwa bora zaidi
iwapo sote tungeongea lugha moja?" Nami nasema "Vema,
tuifanye lugha hiyo Kiyoruba. Tuifanye iwe Kikantoni.
Tuifanye Kikogi."
Na wote mara mtagundua nini kitatokea
kutoweza kuongea lugha yako mwenyewe.
Na ninachotaka kufanya nanyi leo
ni kuwapeleka kwenye safari ya ethnosifia --
safari fupi ya kupitia ethnosifia
kujaribu kukupa picha ya nini kinapotea.
Naam, kuna wengi wetu wanaosahau
ninaposema "kuna namna mbalimbali za kuwa,"
Namaanisha kweli kuna namna mbalimbali za kuwa.
Chukulia kwa mfano, mtoto huyu wa Barasana huko kaskazini magharibi Amazoni
watu wa majoka ya anakonda
wanaoamini miujiza itokanayo na mto wa maziwa
kutoka mashariki kwenye matumbo ya nyoka walotukuka.
Naam, hawa ni watu ambao kwa kutambua
hawawezi kutofautisha rangi ya bluu na rangi ya kijani
kwakuwa paa la mbingu
linalinganishwa na paa la msitu
ambamo watu hawa wanategemea.
Wana kanuni ya ajabu kuhusu ndoa na lugha
ijulikanayo kama ndoa baina ya lugha tofauti:
unalazimika kumuoa azungumzaye lugha tofauti na yako.
Na hii inatokana na imani za kale,
na bado hali ya kushangaza ipo kwenye nyumba hizi ndefu
ambako kuna lugha sita au saba zinazozungumzwa
kutokana na kuoana,
hutomsikia yeyote akijifunza lugha.
Wanasikiliza tu na kuanza kuongea.
Au, moja ya makabila ya kushangaza niliyowahi kuishi nayo,
ni Waorani wa Kaskazini-Mashariki ya Ecuador,
ni watu wa ajabu ambao walitembelewa kwa mara ya kwanza mwaka 1958.
Mnamo mwaka 1957, wamishonari watano walijaribu kuwatembelea
na wakafanya kosa kubwa.
Walidondosha kutoka hewani
picha zao za ukubwa nchi nane kwa kumi
kitu ambacho tunaweza kusema ni ishara ya urafiki,
wakasahau kwamba watu hawa wa misitu ya kitropiki
hawakuwahi kuona kitu chochote chenye vina viwili kabla
Wakaziokota picha hizi toka ardhini
wakajaribu kuangalia kwa nyuma ili kupata umbile kamili
hawakuona kitu, na wakaamini kwamba hizi ni kadi za wito
toka kwa shetani, kwahiyo wakawachoma mikuki wamishonari na kuwaua.
Lakini Waorani si kwamba tu waliwachoma wageni.
Walichomana wao kwa wao.
54% ya vifo vyao vilitokana na kuchomana mikuki wao kwa wao.
Tulifuatilia vizazi nane vilivyopita,
na tukapata matukio mawili tu ya vifo vya asilia
na tulipowauliza zaidi watu habari hizi,
wakakiri kwamba mmoja wao alikuwa mzee sana
na angekufa kwa uzee, kwahiyo tukamchoma mkuki tu (Kicheko)
Lakini pia wana ujuzi wa ajabu
wa msituni ambao unashangaza sana.
Wawindaji huweza kunusa harufu ya mkojo wa mnyama toka umbali wa hatua 40
na wakakwambia ni kiumbe gani ameuacha mkojo huo.
Miaka ya 80, nilikuwa na kazi moja ya kusisimua
nilipoulizwa na Profesa wangu wa Harvard
iwapo ningependa kwenda Haiti,
kupeleleza vikundi vya siri
vilivyokuwa ngome kubwa ya Duvalier
na majasusi wa Tonton Macoutes
na kupata sumu itumikayo kutengeneza mizuka.
ili kupata mantiki kutokana na uvumi
ilinibidi nijaribu kuelewa kuhusu imani hii ya ajabu
ya Vodoun, na Voodoo si kikundi cha uchawi wa nguvu za kiza
Kinyume chake, ni mtazamo fulani wa ulimwengu nje ya maumbile.
inashangaza.
Iwapo nikikutaka utaje dini kuu za dunia,
utasema nini?
Ukristu, Uislamu, Ubudha, Ujudea, na kadhalika.
Huwa kuna bara moja linasahaulika,
kwa mtazamo kwamba nchi za Afrika, kusini mwa Sahara
hazikuwa na imani za kidini. Vema, kwa hakika, walikuwa nazo
na Voodoo ni mchujo tu
wa mawazo haya makuu ya kidini
yaliyokuja wakati wa uhamisho wa kikatili wa kipindi cha utumwa.
Lakini, kinachofanya voodoo kuwa ya kipekee
ni huu uhusiano wa kuishi
kati ya wazima na wafu.
Kwahiyo, wanaoishi wanazaa mizimu.
Mizimu inaswaliwa kutoka kwenye Maji Makuu,
kuitikia mapigo ya muziki
na kusambaratisha roho za wazima kwa muda
ili kwa kipindi maalum na kifupi, makuhani wanakuwa mungu.
Ndiyo maana Mavoodoo wanapenda kusema
kwamba "Nyie watu weupe mnakwenda kanisani na kuongea kuhusu Mungu.
Sisi tunacheza hekaluni na kuwa Mungu."
Na ni kwa sababu mnaingiliwa, mnachukuliwa na mizimu,
unawezaje kuathirika?
Kwahiyo unaona maonyesho haya ya kushangaza:
kuhani wa Voodoo akiwa katika hali ya kupandisha mori
akifukiza uvumba bila hofu,
ni kitendo cha kushangaza cha uwezo wa akili
kuathiri mwili unaoibeba
unapozimuliwa na hali ya kupandisha mori.
Na sasa, katika watu wote niliowahi kuishi nao,
wa ajabu zaidi ni Wakogi
wa Sierra Nevada ya Santa Marta kaskazini mwa Colombia.
Wazawa wa ustaarabu wa kikatili wa kale
ambao uliwahi kuenea uwanda wote wa Colombia katika pwani ya Caribbean
wakati wa uvamizi,
watu hawa walikimbilia kwenye safu ya milima ya kivolkano
inayopanda juu ya pwani ya Caribbean
Katika bara lililomwaga damu,
hawa ni watu pekee ambao hawakushindwa vita na Waspanishi
Mpaka leo, bado wanatawaliwa na makuhani wa kafara
lakini mafunzo yao ya ukuhani ni ya ajabu sana
Makuhani vijana wanachukuliwa toka kwenye familia zao
katika umri wa miaka mitatu au minne,
na kufichwa kwenye ulimwengu wa giza
kwenye vibanda vya mawe chini ya malundo ya barafu kwa miaka 18.
Vipindi viwili vya miaka tisa
imepangwa hivyo makusudi kuigiza miezi tisa ya kukua
waliokaa ndani ya tumbo la mama,
na sasa kilimwengu wapo kwenye tumbo la mama mkuu.
Na kwa muda wote huu,
wanafundishwa maadili muhimu ya utamaduni wao,
maadili ambayo yanatunza maombi ya sala zao
na sala zao pekee ndizo zinatunza maumbile --
au twaweza kusema uwiano wa mazingira.
Na mwisho wa mafunzo haya ya ajabu,
siku moja wanatolewa nje ghafla
na kwa mara ya kwanza katika maisha yao, wakiwa na umri wa miaka 18
wanaona jua likichomoza. Na katika kipindi hicho cha ufahamu
wa mwanga wa kwanza wakati Jua linapoangaza milima
yenye mandhari ya kupendeza,
mara vitu vyote walivyojifunza kwa nadharia
vinatimia kwa utukufu mkubwa. Na kuhani anarudi nyuma
na kusema "Mnaona? Ni hakika kama nilivyowaambia.
Ni nzuri sana. Ni jukumu lenu kuilinda."
Wanajiita kaka wakubwa
na wanasema sisi, ambao ni kaka wadogo,
tunaohusika na kuiharibu dunia,
Na sasa, kiwango cha ufahamu kinakuwa muhimu sana.
Tunapofikiria kuhusu wazawa wa asilia na mandhari ya nchi,
tunakuwa aidha tunamfuata Rousseau
na nadharia ya ukatili halali,
ambao una maanisha kwamba ubaguzi wa rangi ni urahisi,
au badala yake, tumfuate Thoreau
na kusema watu hawa wapo karibu zaidi na Dunia kuliko sisi,
Vema, wazawa asilia hawana unyovu wa moyo
wala hawasumbuliwi na mawazo ya kukumbuka nyumbani
Hakuna fursa kubwa
kwenye mabwawa ya malaria huko Asmat
au kwenye upepo mkali wa Tibet, lakini wameweza, hata hivyo,
kwa kupitia ibada fulani, wameweza kutengeneza mtazamo wa Dunia
ambao unazingatia kujijua au kuwa karibu na kujijua,
lakini kwa kutumia ufahamu wa juu zaidi:
wazo la kwamba Dunia yenyewe yaweza kuwepo
kwakuwa imepewa pumzi kwa ufahamu wa binadamu.
Naam, hiyo ina maana gani?
Ina maana kwamba mtoto mdogo wa huko Andes
aliyelelewa kuamini kwamba milima ni mizimu ya Apu
inayoleta hatima yake
atakuwa binadamu tofauti kabisa
na atakuwa na uhusiano tofauti na maliasili hiyo
au sehemu ile ambako mtoto wa kutoka Montana
amelelewa kuamini kwamba mlima ni mkusanyiko wa mawe
yanayosubiri kuchimbuliwa.
Ama ni makao ya mizimu au malundo ya madini si jambo muhimu.
Kinachosisimua ni nadharia inayo ainisha uhusiano huo
kati ya mtu na ulimwengu asilia
Nilikulia katika misitu ya British Columbia
na kuamini kwamba misitu hiyo ipo kwa ajili ya kukatwa,
Hiyo imenifanya kuwa mtu tofauti
sana na rafiki zangu miongoni mwa Kwakiutl
ambao wanaamini kwamba misitu ni makao ya Hukuk
na lango la peponi
na mizimu mumiani iishiyo miisho ya kaskazini mwa ulimwengu,
mizimu wanayokumbana nayo wakati wa simiko la Hamatsa
Na sasa, ukianza kuzingatia wazo
kwamba tamaduni hizi zinaweza kujenga mitazamo tofauti
waweza kuanza kuelewa
baadhi ya uvumbuzi wao wa ajabu. Chukulia mfano mmea huu hapa,
Ni picha niliyoipiga Kaskazini mwa Amazoni mwezi Aprili
Hii ni ayahuasca, wengi wenu mmekwisha sikia habari zake,
moja kati ya michanyato mikali kabisa ya kuzingulia
kati ya vifaa vyote vya mashamani
kinachoifanya ayahuasca kuwa ya kushangaza zaidi
si kiwango cha hali ya juu cha dawa inayotengenezwa
bali maudhui yake. Inatengenezwa kutokana na vitu viwili
Kwa upande mmoja ni mti wa liana
ambao ni jamii ya beta-carbolines
harmine, harmoline, ambayo ni nishai
Kuinywa peke yake
ni afadhali uvute moshi mzito wa bluu
unaingia kwenye ufahamu wako
ambao umechanganywa na majani ya jamii ya kahawa
yaitwayo Psychotria viridis.
Mmea huu una tindikali za tryptamines,
inafanana sana na kisisimuzi cha mfumo wa ufahamu cha dimethyltryptamine-5,
methoxydimethyltryptamine.
Iwapo ungaliwaona Mayonami
wakiingiza vitu kwenye pua zao,
mchanyato wanaoutengeneza kwa mimea mbalimbali
ambayo pia ina methoxydimethyltryptamine.
Kuingiza unga huo kwenye pua yako
ni kama vile kuzibuliwa kama risasi toka kwenye bomba la bunduki
lililosakafiwa kwa michoro ya baroque na ukatua kwenye bahari ya umeme, (Kicheko)
Haifanyi upotoshaji wa hali halisi;
inayeyusha ufahamu wa hali halisi.
Kwa kweli, nilikuwa nabishana na mwalimu wangu Profesa Richard Evan Shultes --
mtu ambaye alianzisha zama za uchunguzi wa madawa yanayobadili ufahamu
kwa uvumbuzi wake wa uyoga wa ajabu
nchini Mexico mnamo miaka ya 1930.
Nilikuwa nabisha kwamba huwezi kuainisha tryptamines hizi
kama vilevinishai kwakuwa wakati umezinguliwa nazo
hatokuwepo mtu mwingine akisubiri kushuhudia muweweseko wake. (Kicheko)
Lakini kuhusu tryptamines haziwezi kunywewa
kwakuwa zimeathiriwa na kimeng'enya
vinavyopatikana kiasilia katika utumbo wa binadamu na huitwa monoamine oxidase
Vinaweza kunywewa tu iwapo vitachanganywa na
kemikali nyinginezo zinazoweza kuathiri vimeng'enya vya MAO
Na sasa, vitu vya kushangaza
ni hizo beta-carbolines zinazopatikana kwenye liana
ni vidhibiti vya MAO kwa namna fulani muhimu
kuizimua tryptamine. Na hapo unajiuliza swali
Ilikuwaje kwenye mimea mbalimbali zaidi ya 80,000,
watu hawa walichagua hii miwili ambayo haifanani maumbile
lakini ambayo ikichanganywa kwa namna hii,
inatengeneza mchanganyiko wa kemikali
kamilifu ambayo ni zaidi ya jumla ya kila kimojawapo?
Vema, tunatumia maneno rahisi, kwamba walikuwa wakijaribu kubahatisha,
jambo ambalo halina ukweli wowote.
Lakini ukiwauliza Wahindi watakwambia, "Mimea inaongea nasi."
Vema, hiyo ina maana gani?
Kabila hili la Cofan wana aina 17 za ayahuasca,
na wanaweza kuitofautisha kutoka mbali huko msituni,
na zote hizi kwetu sisi zinaonekana kuwa sawa.
Halafu unawauliza waliwezaje kuziainisha
na wanasema " Nilidhani unajua masuala ya mimea,
nina maana, hujui chochote?" Na nikasema "Hapana."
Naam, inakuwa kwamba unachukua moja ya kila hizo aina 17
usiku wa mbalamwezi na zinakuimbia kwa mlio tofauti
Sasa, hiyo haiwezi kukupatia Ph.D. ya Harvard,
lakini hii inavutia zaidi ya kuhesabu chavua.
Na sasa,
(Makofi)
na tatizo -- na tatizo ni kwamba hata sisi
tunaotetea hatima ya wazawa asilia
tunawaona kama wanavutia
lakini wamebanwa na mipaka ya historia
wakati ulimwengu halisi, yaani ulimwengu wetu, unasonga mbele.
Vema, ukweli ni kwamba karne ya 20, miaka 300 kuanzia sasa,
haitakumbukwa kwa vita vyake
au uvumbuzi wa kiteknolojia
bali ni zama ambazo tulikaa
na kuunga mkono waziwazi au tu kukubali
uharibifu mkubwa wa urithi mkubwa wa kibaiolojia au kiutamaduni
duniani. Kwa sasa, tatizo si mabadiliko.
Tamaduni zote wakati wote
zimejihusisha na mchezo
wa masuala mapya ya kimaisha.
Na tatizo si teknolojia peke yake.
Wahindi Wekundu Sioux hawajaacha kuwa Sioux
walipoacha upinde na mshale
kama vile ambavyo Mmarekani kuacha kuwa Mmarekani
alipoacha farasi na mkokoteni wake
Si mabadiliko ya teknolojia
yanayotishia uhai wa ethnosifia. Ni ubabe.
Sura katili ya miliki.
Na chochote unachokiangalia duniani,
utaona kwamba hizi si tamaduni tu zinazopotea.
Hawa ni watu halisi wanaoishi
wakiondolewa uhai kwa nguvu zinazojulikana
lakini ziko nje ya uwezo wao kuzimudu.
Iwapo ni uharibifu mbaya wa misitu
kwenye nchi ya Wapenani --
watu waishio kwa kuhamahama huko Asia ya Kusinimashariki, kutoka Sarawak --
watu walioshi huru mwituni mpaka kizazi kimoja kilichopita,
na sasa wote wamezuiliwa na kutumikishwa
kwenye kingo za mito,
ambako utaona mito yenyewe imechafuliwa kwa tope
yanayoonekana kubeba takriban nusu ya ukubwa wa kisiwa cha Borneo
kwenda Bahari ya China ya Kusini,
ambako meli za Kijapani zinasubiri
tayari kubeba magogo mabichi yaliyozolewa toka misituni.
Au suala la Wayanomami,
ni ugonjwa ambao umeingia,
wakati wa uvumbuzi wa dhahabu.
Au tukienda kwenye milima ya Tibet,
ambako ninafanya utafiti mwingi kwa sasa,
utaona sura ya kutisha ya ubeberu wa kisiasa.
Kama ujuavyo, mauaji ya halaiki, kumaliza maisha ya watu
kunalaaniwa ulimwenguni kote, lakini mauaji ya kiutamaduni,
uharibifu wa utaratibu wa maisha ya watu, siyo tu kwamba unalaaniwa,
unashangiliwa -- na makundi mengi
kuwa kama mkakati wa maendeleo.
Na huwezi kuelewa uchungu wa Tibet
mpaka usafiri kwa barabara.
Niliwahi kusafiri maili 6,000 kutoka Chengdu huko Magharibi mwa China
kwa barabara kupitia kusinimashariki Tibet mpaka Lhasa
nikiwa na mwenzi ambaye ni kijana, na mpaka nilipofika Lhasa
ndipo nikaelewa ukweli kuhusu takwimu
unazozisikia.
majengo matakatifu takriban 6,000 yamebomolewa kuwa vumbi na majivu.
watu milioni 1.2 wameuawa na makada
wakati wa Mapinduzi ya Utamaduni
Baba wa kijana huyu alitawazwa kuwa naibu wa Lama.
Kwa sababu hiyo aliuawa mara tu
ya uvamizi wa China.
Mjomba wake alitoroka pamoja na mhashamu kwenda uhamishoni
nchini Nepal
Mama yake alifungwa kwa sababu tu --
alikuwa tajiri.
Yeye alipenyezwa kwa siri kuingizwa jela akiwa na umri wa miaka miwili
kujificha kwenye sketi za mamaake
kwakuwa hakuweza kustahimili kuishi bila mwanae.
Dada yake aliyefanya kitendo hicho cha kishujaa
alipelekwa kwenye kambi ya elimu
Siku moja kwa bahati mbaya alikumbana na kundi la askari
wa Mao, na kwa kosa hilo,
akahukumiwa kifungo cha miaka saba na kazi ngumu.
Machungu ya Tibet hayavumiliki,
lakini ujasiri wa watu hawa ni kitu cha kusisimua.
Na mwisho wake, inakuja mwisho kwenye uchaguzi,
Tunataka kuishi kwenye ulimwengu unaochosha wa utamaduni mmoja
au tunapenda kuwa na mtandao wa tamaduni mbalimbali?
Margaret Mead, mtaalam maarufu wa mambo ya kale, kabla ya kifo chake alisema
wasiwasi wake mkubwa ni kwamba tunazidi kuelekea kwenye
hii hali ya mtazamo mmoja wa kilimwengu
si tu kwamba tutaona uwezo mkubwa wa ufahamu wa binadamu
ukipunguzwa kuwa mawazo finyu,
bali tutazinduka siku moja
tukiwa tumesahau kwamba kuna uwezekano tofauti wa mambo.
Na ni taadhima kubwa kukumbuka kwamba kizazi chetu kimekuwepo kwa
takriban miaka 600,000
Mapinduzi ya Kilimo -- yaliyoanzisha ukulima,
tulipo salim amri kwenye imani ya mbegu
ushairi wa shaman ulisambaratishwa
kwa maandiko ya ukuhani
tukajenga daraja za umiliki ziada --
ni miaka 10,000 iliyopita tu.
Maendeleo ya viwanda kama tuyajuavyo
yana si zaidi ya miaka 300.
Na sasa, historia hiyo ya juu juu hainishawishi
kwamba tuna majibu ya matatizo yetu yote
yatakayo tufariji katika hatima ya milenia
Wakati hizi tamaduni mbalimbali ulimwenguni
zikiulizwa maana ya kuwa binadamu,
zitakujibu kwa sauti 10,000 tofauti.
Na kwa kupitia wimbo huo ndipo tutatambua uwezekano
wa kuona kwamba sisi ni viumbe wenye ufahamu,
kufahamu fika kuhakikisha watu wote na bustani zote
zinapata namna ya kustawi. Na kuna vipindi vya matumaini.
Hii ni picha niliyoipiga kwenye ncha ya kaskazini mwa kisiwa cha Baffin
nilipokwenda kuwinda nyangumi wenye pembe nikiwa na Wainuiti,
na mtu huyu, Olaya, alinisimulia hadithi ya ajabu kuhusu babu yake.
Serikali ya Canada haikuwa ikiwatendea haki
Wainuiti, katika miaka ya 1950,
ili kujenga utaifa, tuliwahamishia kwenye vijiji.
Babu yake alikataa kwenda.
Nduguze, kwa kuhofia maisha yake, wakampokonya silaha zake zote,
na vifaa vyake vyote.
Na sasa, uelewe kwamba Wainuiti hawakuogopa baridi;
walijinufaisha nayo.
Mikokoteni ya kuteleza kwenye barafu ilitengenezwa kwa samaki
na kufunikwa kwa ngozi ya swala.
Kwahiyo babu yake mtu huyu hakutishika na usiku wa huko Aktika
au upepo mkali ulokuwa ukipuliza
Alitoka nje, akavua suruali yake
na kunyea mkononi. Na kinyesi kilipoanza kuganda,
akafinyanga katika umbile la upanga.
Akatemea mate kwenye upande wa makali ya upanga huo wa kinyesi
na baadae inaganda na kuwa ngumu, na aliitumia kumuua mbwa.
Akamchuna mbwa na kuboresha silaha yake,
akachukua ubavu wa mbwa na kutengeneza mkokoteni wa kuteleza,
akamfunga mbwa wa pili,
na kutokomea kwenye uwanda wa barafu, kisu cha kinyesi kibindoni.
Halafu unazungumzia kujikwamua bila kitu chochote (Kicheko)
Na hii, kwa namna mbalimbali,
(Makofi)
hii ni ishara ya ujasiri wa Wainuiti
na wazawa wote asilia ulimwenguni kote.
Serikali ya Canada mnamo Aprili 1999
waliwarudishia mamlaka Wainuiti
kwenye eneo kubwa kuliko California na Texas yakiunganishwa pamoja.
Ni nchi yetu mpya. Inaitwa Nunavut.
Ni jimbo linalojitegemea. Wanasimamia maliasili zote za madini.
Ni mfano wa ajabu jinsi ambavyo taifa
linafikia -- au kutafuta muafaka na watu wake.
Na mwisho, hatimaye, naona ni wazi kabisa
walau wengi wetu tulosafiri
kwenye sehemu hizi za mbali kwenye dunia,
tumegundua si mbali tena.
Ni makazi ya mtu fulani.
Yanaonyesha matawi ya mawazo ya binadamu
kwamba nenda nyuma kwenye mwanzo wa nyakati. Na kwetu sote,
ndoto za watoto hawa, kama vile ndoto za watoto wetu wenyewe,
zimekuwa sehemu ya jiografia ya matumaini.
Kwahiyo, tunachojaribu kufanya National Geographic hatimaye,
ni, tunaamini kwamba wanasiasa hawafanikishi lolote.
Huo ni ukosoaji wa hoja --
(Makofi)
tunadhani kwamba wakosoaji hawana ushawishi,
lakini tunaamini kwamba kuhadithia kutaibadili dunia,
na kwahiyo sisi ni miongoni mwa taasisi bora zaidi za masimulizi
duniani. Tunapata watembezi milioni 35 kwenye tovuti yetu kila mwezi.
Nchi 156 zinarusha matangazo ya televisheni yetu.
Majarida yetu yanasomwa na mamilioni.
Na tunachokifanya ni safari nyingi
kwenda kwenye ethnosifia ambako tunawapeleka watazamaji wetu
kwenye sehemu ambako kuna maajabu ya kiutamaduni
ambayo hawatoweza kuvumilia bali kushangazwa
na wanachokiona, na natumaini, kwahiyo,
kukubali taratibu, mmoja mmoja,
kiini cha uvumbuzi wa elimu ya mambo ya kale:
kwamba ulimwengu unastahili kuwepo kwa namna mbalimbali
na kwamba tunaweza kupata namna ya kuishi
katika ulimwengu wa tamaduni tofauti
ambako busara zote za watu
zitachangia ustawi wetu sote
Asante sana.
(Makofi)