Kama ujuavyo, moja ya raha kubwa za kusafiri na moja ya furaha za utafiti wa mahusiano ya kikabila ni fursa ya kuishi miongoni mwao hao wasiosahau namna za kijadi ambao wangali wakihisi ya kale kwenye upepo, na kuyagusa juu ya mawe yaliyosafishwa na mvua, na kuyaonja kwenye majani machungu ya mimea. Kujua kwamba wanaoabudu chuipamba bado wana safari kupita mbingu za mbali, au imani za wazee wa Kiinuiti zinaleta maana, au kwamba huko Himalaya, Mabudha bado wanaifuata pumzi ya Dharma, ni katika kukumbuka utambuzi wa msingi wa anthropolojia, na kwamba mtazamo wa ulimwengu tunamoishi haupo kihalisia, bali ni nadharia tu ya ukweli, ni matokeo ya jozi moja tu ya machaguo kadhaa ambayo mababu zetu walifanya, japo kwa mafanikio, vizazi kadhaa vilivyopita. Na kwa hakika, sote tunashabihiana katika kufuata kanuni za maumbile Sote tunazaliwa. Sote tunazaa watoto. Tunapitia kafara za kusimikwa, Tunalazimika kukabiliana na ukatili wa kutenganishwa kwa kifo haitushangazi kwamba sote tunaimba, sote tunacheza, sote tuna sanaa. Lakini kinachosisimua zaidi ni namna pekee za mapigo ya wimbo, mahadhi ya dansi kwa kila utamaduni. Na iwapo ni Wapenani wa misitu ya Borneo au makuhani wa Voodoo nchini Haiti au majemedari wa jangwa la Kaisut Kaskazini mwa Kenya, au matabibu wa Kikurandero wa milima ya Andes, au nyumba ya kuhamishika iliyopo katikati ya Sahara Huyu ndiye mwenzi ambaye nilisafiri nae jangwani mwezi mmoja uliopita au mchunga mbuzipori wa miteremko ya Qomolangma, Everest, mungu mke wa ulimwengu. Watu wote hawa wanatufundisha kwamba kuna namna nyingine za kuwa, namna tofauti za kufikiria namna mbalimbali za kujiwekeza katika Dunia. Na hili ndilo wazo, ambalo ukilifikiria, laweza kukupa tumaini, Sasa, kwa pamoja tamaduni nyingi mbalimbali za ulimwengu zinafanya mtandao wa maisha ya kiroho na kiutamaduni unaoifunika dunia, na ni muhimu kwa ustawi wa dunia hali kadhalika mtandao wa kibaiolojia wa maisha unaoujua kama biosifia. Na waweza kufikiria kwamba mtandao huu wa kiutamaduni kwenye maisha kuwa ni ethnosifia na waweza kuainisha ethnosifia kuwa ni jumla ya mawazo na ndoto, imani, mitazamo, hamasa, vipawa vilivyohuishwa na mawazo ya binadamu tokea mapambazuko ya ufahamu. Ethnosifia ni urithi mkuu wa utu, ni ishara ya kila namna tulivyo na kila namna tuwezavyo kuwa viumbe wadadisi ajabu Na kwa namna ambavyo biosifia imeharibiwa, ndivyo pia ethnosifia --na iwapo kwa kiwango kikubwa zaidi. Hakuna mwanabaiolojia, kwa mfano, awezaye kusema kwamba 50% ya viumbe wote au zaidi wamefikia au wapo katika hatari ya kuteketea kwakuwa si kweli, na pia kwamba -- tishio kubwa la maafa katika uwanja wa mtandao wa kibailojia nadra sana unaangalia kwa mtazamo tunaodhania kuwa bora zaidi kwenye uwanja wa mtandao wa utamaduni. Na kielelezo kikubwa cha muelekeo huo ni kupotea kwa lugha. Wakati nyote mliopo humu ndani mlipozaliwa, kulikuwepo lugha 6,000 zikitumika duniani. Kwa sasa, lugha si mkusanyiko wa maneno au mkusanyiko wa kanuni za sarufi. Lugha ni mwanga wa roho ya binadamu. Ni chombo ambacho hupitisha uhai wa tamaduni fulani kuja kwenye ulimwengu wa vitu. Kila lugha ni mkuzo wa msitu wa akili, mgawanyiko wa vijito, wazo, bioanuwai ya mambo ya kiroho, Miongoni mwa lugha hizo 6,000 mpaka leo tunapokuwa hapa Monterey, takriban nusu yake hazitamkwi kwenye masikio ya watoto. Hazifundishwi kwa watoto wachanga tena, maana yake ni kwamba, kwa hakika, labda kama kuna mambo yatabadilika, zimeshakufa. Hakuna upweke unaozidi ule wa kugubikwa na ukimya, wa kuwa mtu wa mwisho kabisa kuongea lugha yako, kutokuwa na namna ya kurithisha busara za mababu au kutarajia ahadi za watoto? Na zaidi, kinachotisha ni hatima ya mtu fulani sehemu fulani ya Dunia takriban kila wiki mbili, kwa sababu kila wiki mbili, kuna mzee anafariki dunia na anakwenda kaburini na silabi za mwisho za lugha ya kale. Na najua kuna baadhi yenu mngesema,"Naam, si ingekuwa vema? Si ingekuwa bora zaidi iwapo sote tungeongea lugha moja?" Nami nasema "Vema, tuifanye lugha hiyo Kiyoruba. Tuifanye iwe Kikantoni. Tuifanye Kikogi." Na wote mara mtagundua nini kitatokea kutoweza kuongea lugha yako mwenyewe. Na ninachotaka kufanya nanyi leo ni kuwapeleka kwenye safari ya ethnosifia -- safari fupi ya kupitia ethnosifia kujaribu kukupa picha ya nini kinapotea. Naam, kuna wengi wetu wanaosahau ninaposema "kuna namna mbalimbali za kuwa," Namaanisha kweli kuna namna mbalimbali za kuwa. Chukulia kwa mfano, mtoto huyu wa Barasana huko kaskazini magharibi Amazoni watu wa majoka ya anakonda wanaoamini miujiza itokanayo na mto wa maziwa kutoka mashariki kwenye matumbo ya nyoka walotukuka. Naam, hawa ni watu ambao kwa kutambua hawawezi kutofautisha rangi ya bluu na rangi ya kijani kwakuwa paa la mbingu linalinganishwa na paa la msitu ambamo watu hawa wanategemea. Wana kanuni ya ajabu kuhusu ndoa na lugha ijulikanayo kama ndoa baina ya lugha tofauti: unalazimika kumuoa azungumzaye lugha tofauti na yako. Na hii inatokana na imani za kale, na bado hali ya kushangaza ipo kwenye nyumba hizi ndefu ambako kuna lugha sita au saba zinazozungumzwa kutokana na kuoana, hutomsikia yeyote akijifunza lugha. Wanasikiliza tu na kuanza kuongea. Au, moja ya makabila ya kushangaza niliyowahi kuishi nayo, ni Waorani wa Kaskazini-Mashariki ya Ecuador, ni watu wa ajabu ambao walitembelewa kwa mara ya kwanza mwaka 1958. Mnamo mwaka 1957, wamishonari watano walijaribu kuwatembelea na wakafanya kosa kubwa. Walidondosha kutoka hewani picha zao za ukubwa nchi nane kwa kumi kitu ambacho tunaweza kusema ni ishara ya urafiki, wakasahau kwamba watu hawa wa misitu ya kitropiki hawakuwahi kuona kitu chochote chenye vina viwili kabla Wakaziokota picha hizi toka ardhini wakajaribu kuangalia kwa nyuma ili kupata umbile kamili hawakuona kitu, na wakaamini kwamba hizi ni kadi za wito toka kwa shetani, kwahiyo wakawachoma mikuki wamishonari na kuwaua. Lakini Waorani si kwamba tu waliwachoma wageni. Walichomana wao kwa wao. 54% ya vifo vyao vilitokana na kuchomana mikuki wao kwa wao. Tulifuatilia vizazi nane vilivyopita, na tukapata matukio mawili tu ya vifo vya asilia na tulipowauliza zaidi watu habari hizi, wakakiri kwamba mmoja wao alikuwa mzee sana na angekufa kwa uzee, kwahiyo tukamchoma mkuki tu (Kicheko) Lakini pia wana ujuzi wa ajabu wa msituni ambao unashangaza sana. Wawindaji huweza kunusa harufu ya mkojo wa mnyama toka umbali wa hatua 40 na wakakwambia ni kiumbe gani ameuacha mkojo huo. Miaka ya 80, nilikuwa na kazi moja ya kusisimua nilipoulizwa na Profesa wangu wa Harvard iwapo ningependa kwenda Haiti, kupeleleza vikundi vya siri vilivyokuwa ngome kubwa ya Duvalier na majasusi wa Tonton Macoutes na kupata sumu itumikayo kutengeneza mizuka. ili kupata mantiki kutokana na uvumi ilinibidi nijaribu kuelewa kuhusu imani hii ya ajabu ya Vodoun, na Voodoo si kikundi cha uchawi wa nguvu za kiza Kinyume chake, ni mtazamo fulani wa ulimwengu nje ya maumbile. inashangaza. Iwapo nikikutaka utaje dini kuu za dunia, utasema nini? Ukristu, Uislamu, Ubudha, Ujudea, na kadhalika. Huwa kuna bara moja linasahaulika, kwa mtazamo kwamba nchi za Afrika, kusini mwa Sahara hazikuwa na imani za kidini. Vema, kwa hakika, walikuwa nazo na Voodoo ni mchujo tu wa mawazo haya makuu ya kidini yaliyokuja wakati wa uhamisho wa kikatili wa kipindi cha utumwa. Lakini, kinachofanya voodoo kuwa ya kipekee ni huu uhusiano wa kuishi kati ya wazima na wafu. Kwahiyo, wanaoishi wanazaa mizimu. Mizimu inaswaliwa kutoka kwenye Maji Makuu, kuitikia mapigo ya muziki na kusambaratisha roho za wazima kwa muda ili kwa kipindi maalum na kifupi, makuhani wanakuwa mungu. Ndiyo maana Mavoodoo wanapenda kusema kwamba "Nyie watu weupe mnakwenda kanisani na kuongea kuhusu Mungu. Sisi tunacheza hekaluni na kuwa Mungu." Na ni kwa sababu mnaingiliwa, mnachukuliwa na mizimu, unawezaje kuathirika? Kwahiyo unaona maonyesho haya ya kushangaza: kuhani wa Voodoo akiwa katika hali ya kupandisha mori akifukiza uvumba bila hofu, ni kitendo cha kushangaza cha uwezo wa akili kuathiri mwili unaoibeba unapozimuliwa na hali ya kupandisha mori. Na sasa, katika watu wote niliowahi kuishi nao, wa ajabu zaidi ni Wakogi wa Sierra Nevada ya Santa Marta kaskazini mwa Colombia. Wazawa wa ustaarabu wa kikatili wa kale ambao uliwahi kuenea uwanda wote wa Colombia katika pwani ya Caribbean wakati wa uvamizi, watu hawa walikimbilia kwenye safu ya milima ya kivolkano inayopanda juu ya pwani ya Caribbean Katika bara lililomwaga damu, hawa ni watu pekee ambao hawakushindwa vita na Waspanishi Mpaka leo, bado wanatawaliwa na makuhani wa kafara lakini mafunzo yao ya ukuhani ni ya ajabu sana Makuhani vijana wanachukuliwa toka kwenye familia zao katika umri wa miaka mitatu au minne, na kufichwa kwenye ulimwengu wa giza kwenye vibanda vya mawe chini ya malundo ya barafu kwa miaka 18. Vipindi viwili vya miaka tisa imepangwa hivyo makusudi kuigiza miezi tisa ya kukua waliokaa ndani ya tumbo la mama, na sasa kilimwengu wapo kwenye tumbo la mama mkuu. Na kwa muda wote huu, wanafundishwa maadili muhimu ya utamaduni wao, maadili ambayo yanatunza maombi ya sala zao na sala zao pekee ndizo zinatunza maumbile -- au twaweza kusema uwiano wa mazingira. Na mwisho wa mafunzo haya ya ajabu, siku moja wanatolewa nje ghafla na kwa mara ya kwanza katika maisha yao, wakiwa na umri wa miaka 18 wanaona jua likichomoza. Na katika kipindi hicho cha ufahamu wa mwanga wa kwanza wakati Jua linapoangaza milima yenye mandhari ya kupendeza, mara vitu vyote walivyojifunza kwa nadharia vinatimia kwa utukufu mkubwa. Na kuhani anarudi nyuma na kusema "Mnaona? Ni hakika kama nilivyowaambia. Ni nzuri sana. Ni jukumu lenu kuilinda." Wanajiita kaka wakubwa na wanasema sisi, ambao ni kaka wadogo, tunaohusika na kuiharibu dunia, Na sasa, kiwango cha ufahamu kinakuwa muhimu sana. Tunapofikiria kuhusu wazawa wa asilia na mandhari ya nchi, tunakuwa aidha tunamfuata Rousseau na nadharia ya ukatili halali, ambao una maanisha kwamba ubaguzi wa rangi ni urahisi, au badala yake, tumfuate Thoreau na kusema watu hawa wapo karibu zaidi na Dunia kuliko sisi, Vema, wazawa asilia hawana unyovu wa moyo wala hawasumbuliwi na mawazo ya kukumbuka nyumbani Hakuna fursa kubwa kwenye mabwawa ya malaria huko Asmat au kwenye upepo mkali wa Tibet, lakini wameweza, hata hivyo, kwa kupitia ibada fulani, wameweza kutengeneza mtazamo wa Dunia ambao unazingatia kujijua au kuwa karibu na kujijua, lakini kwa kutumia ufahamu wa juu zaidi: wazo la kwamba Dunia yenyewe yaweza kuwepo kwakuwa imepewa pumzi kwa ufahamu wa binadamu. Naam, hiyo ina maana gani? Ina maana kwamba mtoto mdogo wa huko Andes aliyelelewa kuamini kwamba milima ni mizimu ya Apu inayoleta hatima yake atakuwa binadamu tofauti kabisa na atakuwa na uhusiano tofauti na maliasili hiyo au sehemu ile ambako mtoto wa kutoka Montana amelelewa kuamini kwamba mlima ni mkusanyiko wa mawe yanayosubiri kuchimbuliwa. Ama ni makao ya mizimu au malundo ya madini si jambo muhimu. Kinachosisimua ni nadharia inayo ainisha uhusiano huo kati ya mtu na ulimwengu asilia Nilikulia katika misitu ya British Columbia na kuamini kwamba misitu hiyo ipo kwa ajili ya kukatwa, Hiyo imenifanya kuwa mtu tofauti sana na rafiki zangu miongoni mwa Kwakiutl ambao wanaamini kwamba misitu ni makao ya Hukuk na lango la peponi na mizimu mumiani iishiyo miisho ya kaskazini mwa ulimwengu, mizimu wanayokumbana nayo wakati wa simiko la Hamatsa Na sasa, ukianza kuzingatia wazo kwamba tamaduni hizi zinaweza kujenga mitazamo tofauti waweza kuanza kuelewa baadhi ya uvumbuzi wao wa ajabu. Chukulia mfano mmea huu hapa, Ni picha niliyoipiga Kaskazini mwa Amazoni mwezi Aprili Hii ni ayahuasca, wengi wenu mmekwisha sikia habari zake, moja kati ya michanyato mikali kabisa ya kuzingulia kati ya vifaa vyote vya mashamani kinachoifanya ayahuasca kuwa ya kushangaza zaidi si kiwango cha hali ya juu cha dawa inayotengenezwa bali maudhui yake. Inatengenezwa kutokana na vitu viwili Kwa upande mmoja ni mti wa liana ambao ni jamii ya beta-carbolines harmine, harmoline, ambayo ni nishai Kuinywa peke yake ni afadhali uvute moshi mzito wa bluu unaingia kwenye ufahamu wako ambao umechanganywa na majani ya jamii ya kahawa yaitwayo Psychotria viridis. Mmea huu una tindikali za tryptamines, inafanana sana na kisisimuzi cha mfumo wa ufahamu cha dimethyltryptamine-5, methoxydimethyltryptamine. Iwapo ungaliwaona Mayonami wakiingiza vitu kwenye pua zao, mchanyato wanaoutengeneza kwa mimea mbalimbali ambayo pia ina methoxydimethyltryptamine. Kuingiza unga huo kwenye pua yako ni kama vile kuzibuliwa kama risasi toka kwenye bomba la bunduki lililosakafiwa kwa michoro ya baroque na ukatua kwenye bahari ya umeme, (Kicheko) Haifanyi upotoshaji wa hali halisi; inayeyusha ufahamu wa hali halisi. Kwa kweli, nilikuwa nabishana na mwalimu wangu Profesa Richard Evan Shultes -- mtu ambaye alianzisha zama za uchunguzi wa madawa yanayobadili ufahamu kwa uvumbuzi wake wa uyoga wa ajabu nchini Mexico mnamo miaka ya 1930. Nilikuwa nabisha kwamba huwezi kuainisha tryptamines hizi kama vilevinishai kwakuwa wakati umezinguliwa nazo hatokuwepo mtu mwingine akisubiri kushuhudia muweweseko wake. (Kicheko) Lakini kuhusu tryptamines haziwezi kunywewa kwakuwa zimeathiriwa na kimeng'enya vinavyopatikana kiasilia katika utumbo wa binadamu na huitwa monoamine oxidase Vinaweza kunywewa tu iwapo vitachanganywa na kemikali nyinginezo zinazoweza kuathiri vimeng'enya vya MAO Na sasa, vitu vya kushangaza ni hizo beta-carbolines zinazopatikana kwenye liana ni vidhibiti vya MAO kwa namna fulani muhimu kuizimua tryptamine. Na hapo unajiuliza swali Ilikuwaje kwenye mimea mbalimbali zaidi ya 80,000, watu hawa walichagua hii miwili ambayo haifanani maumbile lakini ambayo ikichanganywa kwa namna hii, inatengeneza mchanganyiko wa kemikali kamilifu ambayo ni zaidi ya jumla ya kila kimojawapo? Vema, tunatumia maneno rahisi, kwamba walikuwa wakijaribu kubahatisha, jambo ambalo halina ukweli wowote. Lakini ukiwauliza Wahindi watakwambia, "Mimea inaongea nasi." Vema, hiyo ina maana gani? Kabila hili la Cofan wana aina 17 za ayahuasca, na wanaweza kuitofautisha kutoka mbali huko msituni, na zote hizi kwetu sisi zinaonekana kuwa sawa. Halafu unawauliza waliwezaje kuziainisha na wanasema " Nilidhani unajua masuala ya mimea, nina maana, hujui chochote?" Na nikasema "Hapana." Naam, inakuwa kwamba unachukua moja ya kila hizo aina 17 usiku wa mbalamwezi na zinakuimbia kwa mlio tofauti Sasa, hiyo haiwezi kukupatia Ph.D. ya Harvard, lakini hii inavutia zaidi ya kuhesabu chavua. Na sasa, (Makofi) na tatizo -- na tatizo ni kwamba hata sisi tunaotetea hatima ya wazawa asilia tunawaona kama wanavutia lakini wamebanwa na mipaka ya historia wakati ulimwengu halisi, yaani ulimwengu wetu, unasonga mbele. Vema, ukweli ni kwamba karne ya 20, miaka 300 kuanzia sasa, haitakumbukwa kwa vita vyake au uvumbuzi wa kiteknolojia bali ni zama ambazo tulikaa na kuunga mkono waziwazi au tu kukubali uharibifu mkubwa wa urithi mkubwa wa kibaiolojia au kiutamaduni duniani. Kwa sasa, tatizo si mabadiliko. Tamaduni zote wakati wote zimejihusisha na mchezo wa masuala mapya ya kimaisha. Na tatizo si teknolojia peke yake. Wahindi Wekundu Sioux hawajaacha kuwa Sioux walipoacha upinde na mshale kama vile ambavyo Mmarekani kuacha kuwa Mmarekani alipoacha farasi na mkokoteni wake Si mabadiliko ya teknolojia yanayotishia uhai wa ethnosifia. Ni ubabe. Sura katili ya miliki. Na chochote unachokiangalia duniani, utaona kwamba hizi si tamaduni tu zinazopotea. Hawa ni watu halisi wanaoishi wakiondolewa uhai kwa nguvu zinazojulikana lakini ziko nje ya uwezo wao kuzimudu. Iwapo ni uharibifu mbaya wa misitu kwenye nchi ya Wapenani -- watu waishio kwa kuhamahama huko Asia ya Kusinimashariki, kutoka Sarawak -- watu walioshi huru mwituni mpaka kizazi kimoja kilichopita, na sasa wote wamezuiliwa na kutumikishwa kwenye kingo za mito, ambako utaona mito yenyewe imechafuliwa kwa tope yanayoonekana kubeba takriban nusu ya ukubwa wa kisiwa cha Borneo kwenda Bahari ya China ya Kusini, ambako meli za Kijapani zinasubiri tayari kubeba magogo mabichi yaliyozolewa toka misituni. Au suala la Wayanomami, ni ugonjwa ambao umeingia, wakati wa uvumbuzi wa dhahabu. Au tukienda kwenye milima ya Tibet, ambako ninafanya utafiti mwingi kwa sasa, utaona sura ya kutisha ya ubeberu wa kisiasa. Kama ujuavyo, mauaji ya halaiki, kumaliza maisha ya watu kunalaaniwa ulimwenguni kote, lakini mauaji ya kiutamaduni, uharibifu wa utaratibu wa maisha ya watu, siyo tu kwamba unalaaniwa, unashangiliwa -- na makundi mengi kuwa kama mkakati wa maendeleo. Na huwezi kuelewa uchungu wa Tibet mpaka usafiri kwa barabara. Niliwahi kusafiri maili 6,000 kutoka Chengdu huko Magharibi mwa China kwa barabara kupitia kusinimashariki Tibet mpaka Lhasa nikiwa na mwenzi ambaye ni kijana, na mpaka nilipofika Lhasa ndipo nikaelewa ukweli kuhusu takwimu unazozisikia. majengo matakatifu takriban 6,000 yamebomolewa kuwa vumbi na majivu. watu milioni 1.2 wameuawa na makada wakati wa Mapinduzi ya Utamaduni Baba wa kijana huyu alitawazwa kuwa naibu wa Lama. Kwa sababu hiyo aliuawa mara tu ya uvamizi wa China. Mjomba wake alitoroka pamoja na mhashamu kwenda uhamishoni nchini Nepal Mama yake alifungwa kwa sababu tu -- alikuwa tajiri. Yeye alipenyezwa kwa siri kuingizwa jela akiwa na umri wa miaka miwili kujificha kwenye sketi za mamaake kwakuwa hakuweza kustahimili kuishi bila mwanae. Dada yake aliyefanya kitendo hicho cha kishujaa alipelekwa kwenye kambi ya elimu Siku moja kwa bahati mbaya alikumbana na kundi la askari wa Mao, na kwa kosa hilo, akahukumiwa kifungo cha miaka saba na kazi ngumu. Machungu ya Tibet hayavumiliki, lakini ujasiri wa watu hawa ni kitu cha kusisimua. Na mwisho wake, inakuja mwisho kwenye uchaguzi, Tunataka kuishi kwenye ulimwengu unaochosha wa utamaduni mmoja au tunapenda kuwa na mtandao wa tamaduni mbalimbali? Margaret Mead, mtaalam maarufu wa mambo ya kale, kabla ya kifo chake alisema wasiwasi wake mkubwa ni kwamba tunazidi kuelekea kwenye hii hali ya mtazamo mmoja wa kilimwengu si tu kwamba tutaona uwezo mkubwa wa ufahamu wa binadamu ukipunguzwa kuwa mawazo finyu, bali tutazinduka siku moja tukiwa tumesahau kwamba kuna uwezekano tofauti wa mambo. Na ni taadhima kubwa kukumbuka kwamba kizazi chetu kimekuwepo kwa takriban miaka 600,000 Mapinduzi ya Kilimo -- yaliyoanzisha ukulima, tulipo salim amri kwenye imani ya mbegu ushairi wa shaman ulisambaratishwa kwa maandiko ya ukuhani tukajenga daraja za umiliki ziada -- ni miaka 10,000 iliyopita tu. Maendeleo ya viwanda kama tuyajuavyo yana si zaidi ya miaka 300. Na sasa, historia hiyo ya juu juu hainishawishi kwamba tuna majibu ya matatizo yetu yote yatakayo tufariji katika hatima ya milenia Wakati hizi tamaduni mbalimbali ulimwenguni zikiulizwa maana ya kuwa binadamu, zitakujibu kwa sauti 10,000 tofauti. Na kwa kupitia wimbo huo ndipo tutatambua uwezekano wa kuona kwamba sisi ni viumbe wenye ufahamu, kufahamu fika kuhakikisha watu wote na bustani zote zinapata namna ya kustawi. Na kuna vipindi vya matumaini. Hii ni picha niliyoipiga kwenye ncha ya kaskazini mwa kisiwa cha Baffin nilipokwenda kuwinda nyangumi wenye pembe nikiwa na Wainuiti, na mtu huyu, Olaya, alinisimulia hadithi ya ajabu kuhusu babu yake. Serikali ya Canada haikuwa ikiwatendea haki Wainuiti, katika miaka ya 1950, ili kujenga utaifa, tuliwahamishia kwenye vijiji. Babu yake alikataa kwenda. Nduguze, kwa kuhofia maisha yake, wakampokonya silaha zake zote, na vifaa vyake vyote. Na sasa, uelewe kwamba Wainuiti hawakuogopa baridi; walijinufaisha nayo. Mikokoteni ya kuteleza kwenye barafu ilitengenezwa kwa samaki na kufunikwa kwa ngozi ya swala. Kwahiyo babu yake mtu huyu hakutishika na usiku wa huko Aktika au upepo mkali ulokuwa ukipuliza Alitoka nje, akavua suruali yake na kunyea mkononi. Na kinyesi kilipoanza kuganda, akafinyanga katika umbile la upanga. Akatemea mate kwenye upande wa makali ya upanga huo wa kinyesi na baadae inaganda na kuwa ngumu, na aliitumia kumuua mbwa. Akamchuna mbwa na kuboresha silaha yake, akachukua ubavu wa mbwa na kutengeneza mkokoteni wa kuteleza, akamfunga mbwa wa pili, na kutokomea kwenye uwanda wa barafu, kisu cha kinyesi kibindoni. Halafu unazungumzia kujikwamua bila kitu chochote (Kicheko) Na hii, kwa namna mbalimbali, (Makofi) hii ni ishara ya ujasiri wa Wainuiti na wazawa wote asilia ulimwenguni kote. Serikali ya Canada mnamo Aprili 1999 waliwarudishia mamlaka Wainuiti kwenye eneo kubwa kuliko California na Texas yakiunganishwa pamoja. Ni nchi yetu mpya. Inaitwa Nunavut. Ni jimbo linalojitegemea. Wanasimamia maliasili zote za madini. Ni mfano wa ajabu jinsi ambavyo taifa linafikia -- au kutafuta muafaka na watu wake. Na mwisho, hatimaye, naona ni wazi kabisa walau wengi wetu tulosafiri kwenye sehemu hizi za mbali kwenye dunia, tumegundua si mbali tena. Ni makazi ya mtu fulani. Yanaonyesha matawi ya mawazo ya binadamu kwamba nenda nyuma kwenye mwanzo wa nyakati. Na kwetu sote, ndoto za watoto hawa, kama vile ndoto za watoto wetu wenyewe, zimekuwa sehemu ya jiografia ya matumaini. Kwahiyo, tunachojaribu kufanya National Geographic hatimaye, ni, tunaamini kwamba wanasiasa hawafanikishi lolote. Huo ni ukosoaji wa hoja -- (Makofi) tunadhani kwamba wakosoaji hawana ushawishi, lakini tunaamini kwamba kuhadithia kutaibadili dunia, na kwahiyo sisi ni miongoni mwa taasisi bora zaidi za masimulizi duniani. Tunapata watembezi milioni 35 kwenye tovuti yetu kila mwezi. Nchi 156 zinarusha matangazo ya televisheni yetu. Majarida yetu yanasomwa na mamilioni. Na tunachokifanya ni safari nyingi kwenda kwenye ethnosifia ambako tunawapeleka watazamaji wetu kwenye sehemu ambako kuna maajabu ya kiutamaduni ambayo hawatoweza kuvumilia bali kushangazwa na wanachokiona, na natumaini, kwahiyo, kukubali taratibu, mmoja mmoja, kiini cha uvumbuzi wa elimu ya mambo ya kale: kwamba ulimwengu unastahili kuwepo kwa namna mbalimbali na kwamba tunaweza kupata namna ya kuishi katika ulimwengu wa tamaduni tofauti ambako busara zote za watu zitachangia ustawi wetu sote Asante sana. (Makofi)