1 00:00:00,000 --> 00:00:03,000 Kama ujuavyo, moja ya raha kubwa za kusafiri 2 00:00:03,000 --> 00:00:05,000 na moja ya furaha za utafiti wa mahusiano ya kikabila 3 00:00:05,000 --> 00:00:07,000 ni fursa ya kuishi miongoni mwao 4 00:00:07,000 --> 00:00:09,000 hao wasiosahau namna za kijadi 5 00:00:09,000 --> 00:00:12,000 ambao wangali wakihisi ya kale kwenye upepo, 6 00:00:12,000 --> 00:00:15,000 na kuyagusa juu ya mawe yaliyosafishwa na mvua, 7 00:00:15,000 --> 00:00:17,000 na kuyaonja kwenye majani machungu ya mimea. 8 00:00:17,000 --> 00:00:21,000 Kujua kwamba wanaoabudu chuipamba bado wana safari kupita mbingu za mbali, 9 00:00:21,000 --> 00:00:25,000 au imani za wazee wa Kiinuiti zinaleta maana, 10 00:00:25,000 --> 00:00:27,000 au kwamba huko Himalaya, 11 00:00:28,000 --> 00:00:32,000 Mabudha bado wanaifuata pumzi ya Dharma, 12 00:00:32,000 --> 00:00:35,000 ni katika kukumbuka utambuzi wa msingi wa anthropolojia, 13 00:00:35,000 --> 00:00:37,000 na kwamba mtazamo wa ulimwengu tunamoishi 14 00:00:38,000 --> 00:00:40,000 haupo kihalisia, 15 00:00:40,000 --> 00:00:41,000 bali ni nadharia tu ya ukweli, 16 00:00:41,000 --> 00:00:45,000 ni matokeo ya jozi moja tu ya machaguo kadhaa 17 00:00:45,000 --> 00:00:49,000 ambayo mababu zetu walifanya, japo kwa mafanikio, vizazi kadhaa vilivyopita. 18 00:00:50,000 --> 00:00:54,000 Na kwa hakika, sote tunashabihiana katika kufuata kanuni za maumbile 19 00:00:54,000 --> 00:00:56,000 Sote tunazaliwa. Sote tunazaa watoto. 20 00:00:56,000 --> 00:00:58,000 Tunapitia kafara za kusimikwa, 21 00:00:58,000 --> 00:01:00,000 Tunalazimika kukabiliana na ukatili wa kutenganishwa kwa kifo 22 00:01:00,000 --> 00:01:04,000 haitushangazi kwamba sote tunaimba, sote tunacheza, 23 00:01:04,000 --> 00:01:06,000 sote tuna sanaa. 24 00:01:06,000 --> 00:01:09,000 Lakini kinachosisimua zaidi ni namna pekee za mapigo ya wimbo, 25 00:01:09,000 --> 00:01:11,000 mahadhi ya dansi kwa kila utamaduni. 26 00:01:11,000 --> 00:01:14,000 Na iwapo ni Wapenani wa misitu ya Borneo 27 00:01:14,000 --> 00:01:17,000 au makuhani wa Voodoo nchini Haiti 28 00:01:18,000 --> 00:01:22,000 au majemedari wa jangwa la Kaisut Kaskazini mwa Kenya, 29 00:01:24,000 --> 00:01:26,000 au matabibu wa Kikurandero wa milima ya Andes, 30 00:01:27,000 --> 00:01:32,000 au nyumba ya kuhamishika iliyopo katikati ya Sahara 31 00:01:32,000 --> 00:01:34,000 Huyu ndiye mwenzi ambaye nilisafiri nae jangwani 32 00:01:34,000 --> 00:01:35,000 mwezi mmoja uliopita 33 00:01:35,000 --> 00:01:38,000 au mchunga mbuzipori wa miteremko ya Qomolangma, 34 00:01:38,000 --> 00:01:40,000 Everest, mungu mke wa ulimwengu. 35 00:01:40,000 --> 00:01:43,000 Watu wote hawa wanatufundisha kwamba kuna namna nyingine za kuwa, 36 00:01:43,000 --> 00:01:44,000 namna tofauti za kufikiria 37 00:01:44,000 --> 00:01:46,000 namna mbalimbali za kujiwekeza katika Dunia. 38 00:01:46,000 --> 00:01:48,000 Na hili ndilo wazo, ambalo ukilifikiria, 39 00:01:48,000 --> 00:01:50,000 laweza kukupa tumaini, 40 00:01:50,000 --> 00:01:53,000 Sasa, kwa pamoja tamaduni nyingi mbalimbali za ulimwengu 41 00:01:53,000 --> 00:01:57,000 zinafanya mtandao wa maisha ya kiroho na kiutamaduni 42 00:01:57,000 --> 00:01:59,000 unaoifunika dunia, 43 00:01:59,000 --> 00:02:01,000 na ni muhimu kwa ustawi wa dunia 44 00:02:01,000 --> 00:02:04,000 hali kadhalika mtandao wa kibaiolojia wa maisha unaoujua kama biosifia. 45 00:02:04,000 --> 00:02:07,000 Na waweza kufikiria kwamba mtandao huu wa kiutamaduni kwenye maisha 46 00:02:07,000 --> 00:02:08,000 kuwa ni ethnosifia 47 00:02:08,000 --> 00:02:10,000 na waweza kuainisha ethnosifia 48 00:02:10,000 --> 00:02:13,000 kuwa ni jumla ya mawazo na ndoto, imani, 49 00:02:13,000 --> 00:02:16,000 mitazamo, hamasa, vipawa vilivyohuishwa 50 00:02:16,000 --> 00:02:20,000 na mawazo ya binadamu tokea mapambazuko ya ufahamu. 51 00:02:20,000 --> 00:02:23,000 Ethnosifia ni urithi mkuu wa utu, 52 00:02:23,000 --> 00:02:25,000 ni ishara ya kila namna tulivyo 53 00:02:25,000 --> 00:02:29,000 na kila namna tuwezavyo kuwa viumbe wadadisi ajabu 54 00:02:30,000 --> 00:02:33,000 Na kwa namna ambavyo biosifia imeharibiwa, 55 00:02:33,000 --> 00:02:35,000 ndivyo pia ethnosifia 56 00:02:35,000 --> 00:02:37,000 --na iwapo kwa kiwango kikubwa zaidi. 57 00:02:37,000 --> 00:02:39,000 Hakuna mwanabaiolojia, kwa mfano, awezaye kusema 58 00:02:39,000 --> 00:02:42,000 kwamba 50% ya viumbe wote au zaidi wamefikia au wapo 59 00:02:42,000 --> 00:02:44,000 katika hatari ya kuteketea kwakuwa si kweli, 60 00:02:44,000 --> 00:02:46,000 na pia kwamba -- tishio kubwa la maafa 61 00:02:46,000 --> 00:02:49,000 katika uwanja wa mtandao wa kibailojia 62 00:02:49,000 --> 00:02:52,000 nadra sana unaangalia kwa mtazamo tunaodhania kuwa bora zaidi 63 00:02:52,000 --> 00:02:54,000 kwenye uwanja wa mtandao wa utamaduni. 64 00:02:54,000 --> 00:02:57,000 Na kielelezo kikubwa cha muelekeo huo ni kupotea kwa lugha. 65 00:02:57,000 --> 00:03:00,000 Wakati nyote mliopo humu ndani mlipozaliwa, 66 00:03:00,000 --> 00:03:03,000 kulikuwepo lugha 6,000 zikitumika duniani. 67 00:03:03,000 --> 00:03:06,000 Kwa sasa, lugha si mkusanyiko wa maneno 68 00:03:06,000 --> 00:03:08,000 au mkusanyiko wa kanuni za sarufi. 69 00:03:08,000 --> 00:03:10,000 Lugha ni mwanga wa roho ya binadamu. 70 00:03:10,000 --> 00:03:13,000 Ni chombo ambacho hupitisha uhai wa tamaduni fulani 71 00:03:13,000 --> 00:03:14,000 kuja kwenye ulimwengu wa vitu. 72 00:03:14,000 --> 00:03:17,000 Kila lugha ni mkuzo wa msitu wa akili, 73 00:03:17,000 --> 00:03:21,000 mgawanyiko wa vijito, wazo, bioanuwai ya mambo ya kiroho, 74 00:03:21,000 --> 00:03:25,000 Miongoni mwa lugha hizo 6,000 mpaka leo tunapokuwa hapa Monterey, 75 00:03:25,000 --> 00:03:29,000 takriban nusu yake hazitamkwi kwenye masikio ya watoto. 76 00:03:29,000 --> 00:03:32,000 Hazifundishwi kwa watoto wachanga tena, 77 00:03:32,000 --> 00:03:34,000 maana yake ni kwamba, kwa hakika, labda kama kuna mambo yatabadilika, 78 00:03:34,000 --> 00:03:35,000 zimeshakufa. 79 00:03:35,000 --> 00:03:39,000 Hakuna upweke unaozidi ule wa kugubikwa na ukimya, 80 00:03:39,000 --> 00:03:41,000 wa kuwa mtu wa mwisho kabisa kuongea lugha yako, 81 00:03:41,000 --> 00:03:44,000 kutokuwa na namna ya kurithisha busara za mababu 82 00:03:44,000 --> 00:03:47,000 au kutarajia ahadi za watoto? 83 00:03:47,000 --> 00:03:50,000 Na zaidi, kinachotisha ni hatima ya mtu fulani 84 00:03:50,000 --> 00:03:52,000 sehemu fulani ya Dunia takriban kila wiki mbili, 85 00:03:52,000 --> 00:03:54,000 kwa sababu kila wiki mbili, kuna mzee anafariki dunia 86 00:03:54,000 --> 00:03:56,000 na anakwenda kaburini na silabi za mwisho 87 00:03:56,000 --> 00:03:58,000 za lugha ya kale. 88 00:03:58,000 --> 00:04:00,000 Na najua kuna baadhi yenu mngesema,"Naam, si ingekuwa vema? 89 00:04:00,000 --> 00:04:01,000 Si ingekuwa bora zaidi 90 00:04:01,000 --> 00:04:04,000 iwapo sote tungeongea lugha moja?" Nami nasema "Vema, 91 00:04:04,000 --> 00:04:07,000 tuifanye lugha hiyo Kiyoruba. Tuifanye iwe Kikantoni. 92 00:04:07,000 --> 00:04:08,000 Tuifanye Kikogi." 93 00:04:08,000 --> 00:04:10,000 Na wote mara mtagundua nini kitatokea 94 00:04:10,000 --> 00:04:13,000 kutoweza kuongea lugha yako mwenyewe. 95 00:04:13,000 --> 00:04:16,000 Na ninachotaka kufanya nanyi leo 96 00:04:16,000 --> 00:04:20,000 ni kuwapeleka kwenye safari ya ethnosifia -- 97 00:04:20,000 --> 00:04:22,000 safari fupi ya kupitia ethnosifia 98 00:04:22,000 --> 00:04:26,000 kujaribu kukupa picha ya nini kinapotea. 99 00:04:27,000 --> 00:04:34,000 Naam, kuna wengi wetu wanaosahau 100 00:04:34,000 --> 00:04:36,000 ninaposema "kuna namna mbalimbali za kuwa," 101 00:04:36,000 --> 00:04:38,000 Namaanisha kweli kuna namna mbalimbali za kuwa. 102 00:04:39,000 --> 00:04:44,000 Chukulia kwa mfano, mtoto huyu wa Barasana huko kaskazini magharibi Amazoni 103 00:04:44,000 --> 00:04:45,000 watu wa majoka ya anakonda 104 00:04:45,000 --> 00:04:47,000 wanaoamini miujiza itokanayo na mto wa maziwa 105 00:04:47,000 --> 00:04:50,000 kutoka mashariki kwenye matumbo ya nyoka walotukuka. 106 00:04:50,000 --> 00:04:53,000 Naam, hawa ni watu ambao kwa kutambua 107 00:04:53,000 --> 00:04:55,000 hawawezi kutofautisha rangi ya bluu na rangi ya kijani 108 00:04:55,000 --> 00:04:57,000 kwakuwa paa la mbingu 109 00:04:57,000 --> 00:04:58,000 linalinganishwa na paa la msitu 110 00:04:58,000 --> 00:05:00,000 ambamo watu hawa wanategemea. 111 00:05:00,000 --> 00:05:03,000 Wana kanuni ya ajabu kuhusu ndoa na lugha 112 00:05:03,000 --> 00:05:05,000 ijulikanayo kama ndoa baina ya lugha tofauti: 113 00:05:05,000 --> 00:05:08,000 unalazimika kumuoa azungumzaye lugha tofauti na yako. 114 00:05:08,000 --> 00:05:10,000 Na hii inatokana na imani za kale, 115 00:05:10,000 --> 00:05:12,000 na bado hali ya kushangaza ipo kwenye nyumba hizi ndefu 116 00:05:12,000 --> 00:05:14,000 ambako kuna lugha sita au saba zinazozungumzwa 117 00:05:14,000 --> 00:05:16,000 kutokana na kuoana, 118 00:05:16,000 --> 00:05:19,000 hutomsikia yeyote akijifunza lugha. 119 00:05:19,000 --> 00:05:22,000 Wanasikiliza tu na kuanza kuongea. 120 00:05:22,000 --> 00:05:24,000 Au, moja ya makabila ya kushangaza niliyowahi kuishi nayo, 121 00:05:24,000 --> 00:05:28,000 ni Waorani wa Kaskazini-Mashariki ya Ecuador, 122 00:05:28,000 --> 00:05:31,000 ni watu wa ajabu ambao walitembelewa kwa mara ya kwanza mwaka 1958. 123 00:05:31,000 --> 00:05:35,000 Mnamo mwaka 1957, wamishonari watano walijaribu kuwatembelea 124 00:05:35,000 --> 00:05:36,000 na wakafanya kosa kubwa. 125 00:05:36,000 --> 00:05:37,000 Walidondosha kutoka hewani 126 00:05:37,000 --> 00:05:39,000 picha zao za ukubwa nchi nane kwa kumi 127 00:05:39,000 --> 00:05:41,000 kitu ambacho tunaweza kusema ni ishara ya urafiki, 128 00:05:41,000 --> 00:05:43,000 wakasahau kwamba watu hawa wa misitu ya kitropiki 129 00:05:43,000 --> 00:05:46,000 hawakuwahi kuona kitu chochote chenye vina viwili kabla 130 00:05:46,000 --> 00:05:48,000 Wakaziokota picha hizi toka ardhini 131 00:05:48,000 --> 00:05:51,000 wakajaribu kuangalia kwa nyuma ili kupata umbile kamili 132 00:05:51,000 --> 00:05:53,000 hawakuona kitu, na wakaamini kwamba hizi ni kadi za wito 133 00:05:53,000 --> 00:05:56,000 toka kwa shetani, kwahiyo wakawachoma mikuki wamishonari na kuwaua. 134 00:05:57,000 --> 00:05:59,000 Lakini Waorani si kwamba tu waliwachoma wageni. 135 00:05:59,000 --> 00:06:00,000 Walichomana wao kwa wao. 136 00:06:00,000 --> 00:06:03,000 54% ya vifo vyao vilitokana na kuchomana mikuki wao kwa wao. 137 00:06:03,000 --> 00:06:06,000 Tulifuatilia vizazi nane vilivyopita, 138 00:06:06,000 --> 00:06:08,000 na tukapata matukio mawili tu ya vifo vya asilia 139 00:06:08,000 --> 00:06:10,000 na tulipowauliza zaidi watu habari hizi, 140 00:06:10,000 --> 00:06:12,000 wakakiri kwamba mmoja wao alikuwa mzee sana 141 00:06:12,000 --> 00:06:16,000 na angekufa kwa uzee, kwahiyo tukamchoma mkuki tu (Kicheko) 142 00:06:16,000 --> 00:06:19,000 Lakini pia wana ujuzi wa ajabu 143 00:06:19,000 --> 00:06:20,000 wa msituni ambao unashangaza sana. 144 00:06:20,000 --> 00:06:23,000 Wawindaji huweza kunusa harufu ya mkojo wa mnyama toka umbali wa hatua 40 145 00:06:23,000 --> 00:06:26,000 na wakakwambia ni kiumbe gani ameuacha mkojo huo. 146 00:06:26,000 --> 00:06:28,000 Miaka ya 80, nilikuwa na kazi moja ya kusisimua 147 00:06:28,000 --> 00:06:30,000 nilipoulizwa na Profesa wangu wa Harvard 148 00:06:30,000 --> 00:06:32,000 iwapo ningependa kwenda Haiti, 149 00:06:33,000 --> 00:06:35,000 kupeleleza vikundi vya siri 150 00:06:35,000 --> 00:06:37,000 vilivyokuwa ngome kubwa ya Duvalier 151 00:06:37,000 --> 00:06:38,000 na majasusi wa Tonton Macoutes 152 00:06:38,000 --> 00:06:41,000 na kupata sumu itumikayo kutengeneza mizuka. 153 00:06:41,000 --> 00:06:44,000 ili kupata mantiki kutokana na uvumi 154 00:06:44,000 --> 00:06:47,000 ilinibidi nijaribu kuelewa kuhusu imani hii ya ajabu 155 00:06:47,000 --> 00:06:50,000 ya Vodoun, na Voodoo si kikundi cha uchawi wa nguvu za kiza 156 00:06:50,000 --> 00:06:53,000 Kinyume chake, ni mtazamo fulani wa ulimwengu nje ya maumbile. 157 00:06:53,000 --> 00:06:54,000 inashangaza. 158 00:06:54,000 --> 00:06:55,000 Iwapo nikikutaka utaje dini kuu za dunia, 159 00:06:55,000 --> 00:06:56,000 utasema nini? 160 00:06:56,000 --> 00:06:59,000 Ukristu, Uislamu, Ubudha, Ujudea, na kadhalika. 161 00:06:59,000 --> 00:07:01,000 Huwa kuna bara moja linasahaulika, 162 00:07:01,000 --> 00:07:03,000 kwa mtazamo kwamba nchi za Afrika, kusini mwa Sahara 163 00:07:03,000 --> 00:07:05,000 hazikuwa na imani za kidini. Vema, kwa hakika, walikuwa nazo 164 00:07:05,000 --> 00:07:07,000 na Voodoo ni mchujo tu 165 00:07:08,000 --> 00:07:09,000 wa mawazo haya makuu ya kidini 166 00:07:09,000 --> 00:07:12,000 yaliyokuja wakati wa uhamisho wa kikatili wa kipindi cha utumwa. 167 00:07:12,000 --> 00:07:14,000 Lakini, kinachofanya voodoo kuwa ya kipekee 168 00:07:14,000 --> 00:07:16,000 ni huu uhusiano wa kuishi 169 00:07:16,000 --> 00:07:17,000 kati ya wazima na wafu. 170 00:07:17,000 --> 00:07:18,000 Kwahiyo, wanaoishi wanazaa mizimu. 171 00:07:18,000 --> 00:07:21,000 Mizimu inaswaliwa kutoka kwenye Maji Makuu, 172 00:07:21,000 --> 00:07:23,000 kuitikia mapigo ya muziki 173 00:07:23,000 --> 00:07:25,000 na kusambaratisha roho za wazima kwa muda 174 00:07:25,000 --> 00:07:29,000 ili kwa kipindi maalum na kifupi, makuhani wanakuwa mungu. 175 00:07:29,000 --> 00:07:31,000 Ndiyo maana Mavoodoo wanapenda kusema 176 00:07:31,000 --> 00:07:34,000 kwamba "Nyie watu weupe mnakwenda kanisani na kuongea kuhusu Mungu. 177 00:07:34,000 --> 00:07:36,000 Sisi tunacheza hekaluni na kuwa Mungu." 178 00:07:36,000 --> 00:07:39,000 Na ni kwa sababu mnaingiliwa, mnachukuliwa na mizimu, 179 00:07:39,000 --> 00:07:40,000 unawezaje kuathirika? 180 00:07:40,000 --> 00:07:43,000 Kwahiyo unaona maonyesho haya ya kushangaza: 181 00:07:43,000 --> 00:07:45,000 kuhani wa Voodoo akiwa katika hali ya kupandisha mori 182 00:07:45,000 --> 00:07:48,000 akifukiza uvumba bila hofu, 183 00:07:48,000 --> 00:07:51,000 ni kitendo cha kushangaza cha uwezo wa akili 184 00:07:51,000 --> 00:07:52,000 kuathiri mwili unaoibeba 185 00:07:52,000 --> 00:07:55,000 unapozimuliwa na hali ya kupandisha mori. 186 00:07:56,000 --> 00:07:58,000 Na sasa, katika watu wote niliowahi kuishi nao, 187 00:07:58,000 --> 00:08:00,000 wa ajabu zaidi ni Wakogi 188 00:08:00,000 --> 00:08:03,000 wa Sierra Nevada ya Santa Marta kaskazini mwa Colombia. 189 00:08:03,000 --> 00:08:06,000 Wazawa wa ustaarabu wa kikatili wa kale 190 00:08:06,000 --> 00:08:09,000 ambao uliwahi kuenea uwanda wote wa Colombia katika pwani ya Caribbean 191 00:08:09,000 --> 00:08:10,000 wakati wa uvamizi, 192 00:08:10,000 --> 00:08:13,000 watu hawa walikimbilia kwenye safu ya milima ya kivolkano 193 00:08:13,000 --> 00:08:15,000 inayopanda juu ya pwani ya Caribbean 194 00:08:15,000 --> 00:08:17,000 Katika bara lililomwaga damu, 195 00:08:17,000 --> 00:08:20,000 hawa ni watu pekee ambao hawakushindwa vita na Waspanishi 196 00:08:20,000 --> 00:08:23,000 Mpaka leo, bado wanatawaliwa na makuhani wa kafara 197 00:08:23,000 --> 00:08:25,000 lakini mafunzo yao ya ukuhani ni ya ajabu sana 198 00:08:26,000 --> 00:08:28,000 Makuhani vijana wanachukuliwa toka kwenye familia zao 199 00:08:28,000 --> 00:08:30,000 katika umri wa miaka mitatu au minne, 200 00:08:30,000 --> 00:08:32,000 na kufichwa kwenye ulimwengu wa giza 201 00:08:32,000 --> 00:08:36,000 kwenye vibanda vya mawe chini ya malundo ya barafu kwa miaka 18. 202 00:08:36,000 --> 00:08:37,000 Vipindi viwili vya miaka tisa 203 00:08:37,000 --> 00:08:40,000 imepangwa hivyo makusudi kuigiza miezi tisa ya kukua 204 00:08:40,000 --> 00:08:42,000 waliokaa ndani ya tumbo la mama, 205 00:08:42,000 --> 00:08:45,000 na sasa kilimwengu wapo kwenye tumbo la mama mkuu. 206 00:08:45,000 --> 00:08:46,000 Na kwa muda wote huu, 207 00:08:47,000 --> 00:08:50,000 wanafundishwa maadili muhimu ya utamaduni wao, 208 00:08:50,000 --> 00:08:52,000 maadili ambayo yanatunza maombi ya sala zao 209 00:08:52,000 --> 00:08:55,000 na sala zao pekee ndizo zinatunza maumbile -- 210 00:08:55,000 --> 00:08:57,000 au twaweza kusema uwiano wa mazingira. 211 00:08:58,000 --> 00:08:59,000 Na mwisho wa mafunzo haya ya ajabu, 212 00:08:59,000 --> 00:09:01,000 siku moja wanatolewa nje ghafla 213 00:09:01,000 --> 00:09:04,000 na kwa mara ya kwanza katika maisha yao, wakiwa na umri wa miaka 18 214 00:09:04,000 --> 00:09:08,000 wanaona jua likichomoza. Na katika kipindi hicho cha ufahamu 215 00:09:08,000 --> 00:09:11,000 wa mwanga wa kwanza wakati Jua linapoangaza milima 216 00:09:11,000 --> 00:09:12,000 yenye mandhari ya kupendeza, 217 00:09:13,000 --> 00:09:15,000 mara vitu vyote walivyojifunza kwa nadharia 218 00:09:15,000 --> 00:09:18,000 vinatimia kwa utukufu mkubwa. Na kuhani anarudi nyuma 219 00:09:18,000 --> 00:09:20,000 na kusema "Mnaona? Ni hakika kama nilivyowaambia. 220 00:09:20,000 --> 00:09:23,000 Ni nzuri sana. Ni jukumu lenu kuilinda." 221 00:09:23,000 --> 00:09:25,000 Wanajiita kaka wakubwa 222 00:09:25,000 --> 00:09:28,000 na wanasema sisi, ambao ni kaka wadogo, 223 00:09:28,000 --> 00:09:31,000 tunaohusika na kuiharibu dunia, 224 00:09:32,000 --> 00:09:34,000 Na sasa, kiwango cha ufahamu kinakuwa muhimu sana. 225 00:09:34,000 --> 00:09:36,000 Tunapofikiria kuhusu wazawa wa asilia na mandhari ya nchi, 226 00:09:36,000 --> 00:09:38,000 tunakuwa aidha tunamfuata Rousseau 227 00:09:38,000 --> 00:09:41,000 na nadharia ya ukatili halali, 228 00:09:41,000 --> 00:09:43,000 ambao una maanisha kwamba ubaguzi wa rangi ni urahisi, 229 00:09:43,000 --> 00:09:46,000 au badala yake, tumfuate Thoreau 230 00:09:46,000 --> 00:09:48,000 na kusema watu hawa wapo karibu zaidi na Dunia kuliko sisi, 231 00:09:48,000 --> 00:09:50,000 Vema, wazawa asilia hawana unyovu wa moyo 232 00:09:50,000 --> 00:09:52,000 wala hawasumbuliwi na mawazo ya kukumbuka nyumbani 233 00:09:52,000 --> 00:09:54,000 Hakuna fursa kubwa 234 00:09:54,000 --> 00:09:56,000 kwenye mabwawa ya malaria huko Asmat 235 00:09:56,000 --> 00:09:59,000 au kwenye upepo mkali wa Tibet, lakini wameweza, hata hivyo, 236 00:09:59,000 --> 00:10:03,000 kwa kupitia ibada fulani, wameweza kutengeneza mtazamo wa Dunia 237 00:10:03,000 --> 00:10:06,000 ambao unazingatia kujijua au kuwa karibu na kujijua, 238 00:10:06,000 --> 00:10:08,000 lakini kwa kutumia ufahamu wa juu zaidi: 239 00:10:08,000 --> 00:10:11,000 wazo la kwamba Dunia yenyewe yaweza kuwepo 240 00:10:12,000 --> 00:10:14,000 kwakuwa imepewa pumzi kwa ufahamu wa binadamu. 241 00:10:14,000 --> 00:10:16,000 Naam, hiyo ina maana gani? 242 00:10:16,000 --> 00:10:18,000 Ina maana kwamba mtoto mdogo wa huko Andes 243 00:10:18,000 --> 00:10:20,000 aliyelelewa kuamini kwamba milima ni mizimu ya Apu 244 00:10:20,000 --> 00:10:22,000 inayoleta hatima yake 245 00:10:22,000 --> 00:10:25,000 atakuwa binadamu tofauti kabisa 246 00:10:25,000 --> 00:10:28,000 na atakuwa na uhusiano tofauti na maliasili hiyo 247 00:10:28,000 --> 00:10:30,000 au sehemu ile ambako mtoto wa kutoka Montana 248 00:10:30,000 --> 00:10:33,000 amelelewa kuamini kwamba mlima ni mkusanyiko wa mawe 249 00:10:33,000 --> 00:10:34,000 yanayosubiri kuchimbuliwa. 250 00:10:34,000 --> 00:10:38,000 Ama ni makao ya mizimu au malundo ya madini si jambo muhimu. 251 00:10:38,000 --> 00:10:41,000 Kinachosisimua ni nadharia inayo ainisha uhusiano huo 252 00:10:41,000 --> 00:10:43,000 kati ya mtu na ulimwengu asilia 253 00:10:43,000 --> 00:10:45,000 Nilikulia katika misitu ya British Columbia 254 00:10:45,000 --> 00:10:47,000 na kuamini kwamba misitu hiyo ipo kwa ajili ya kukatwa, 255 00:10:47,000 --> 00:10:49,000 Hiyo imenifanya kuwa mtu tofauti 256 00:10:49,000 --> 00:10:51,000 sana na rafiki zangu miongoni mwa Kwakiutl 257 00:10:51,000 --> 00:10:53,000 ambao wanaamini kwamba misitu ni makao ya Hukuk 258 00:10:53,000 --> 00:10:54,000 na lango la peponi 259 00:10:54,000 --> 00:10:57,000 na mizimu mumiani iishiyo miisho ya kaskazini mwa ulimwengu, 260 00:10:57,000 --> 00:11:01,000 mizimu wanayokumbana nayo wakati wa simiko la Hamatsa 261 00:11:01,000 --> 00:11:03,000 Na sasa, ukianza kuzingatia wazo 262 00:11:03,000 --> 00:11:05,000 kwamba tamaduni hizi zinaweza kujenga mitazamo tofauti 263 00:11:05,000 --> 00:11:06,000 waweza kuanza kuelewa 264 00:11:06,000 --> 00:11:11,000 baadhi ya uvumbuzi wao wa ajabu. Chukulia mfano mmea huu hapa, 265 00:11:11,000 --> 00:11:13,000 Ni picha niliyoipiga Kaskazini mwa Amazoni mwezi Aprili 266 00:11:13,000 --> 00:11:16,000 Hii ni ayahuasca, wengi wenu mmekwisha sikia habari zake, 267 00:11:16,000 --> 00:11:19,000 moja kati ya michanyato mikali kabisa ya kuzingulia 268 00:11:19,000 --> 00:11:21,000 kati ya vifaa vyote vya mashamani 269 00:11:21,000 --> 00:11:23,000 kinachoifanya ayahuasca kuwa ya kushangaza zaidi 270 00:11:23,000 --> 00:11:27,000 si kiwango cha hali ya juu cha dawa inayotengenezwa 271 00:11:27,000 --> 00:11:31,000 bali maudhui yake. Inatengenezwa kutokana na vitu viwili 272 00:11:31,000 --> 00:11:33,000 Kwa upande mmoja ni mti wa liana 273 00:11:33,000 --> 00:11:35,000 ambao ni jamii ya beta-carbolines 274 00:11:35,000 --> 00:11:38,000 harmine, harmoline, ambayo ni nishai 275 00:11:38,000 --> 00:11:40,000 Kuinywa peke yake 276 00:11:40,000 --> 00:11:42,000 ni afadhali uvute moshi mzito wa bluu 277 00:11:42,000 --> 00:11:44,000 unaingia kwenye ufahamu wako 278 00:11:44,000 --> 00:11:47,000 ambao umechanganywa na majani ya jamii ya kahawa 279 00:11:47,000 --> 00:11:49,000 yaitwayo Psychotria viridis. 280 00:11:49,000 --> 00:11:52,000 Mmea huu una tindikali za tryptamines, 281 00:11:52,000 --> 00:11:56,000 inafanana sana na kisisimuzi cha mfumo wa ufahamu cha dimethyltryptamine-5, 282 00:11:56,000 --> 00:11:57,000 methoxydimethyltryptamine. 283 00:11:57,000 --> 00:11:59,000 Iwapo ungaliwaona Mayonami 284 00:11:59,000 --> 00:12:01,000 wakiingiza vitu kwenye pua zao, 285 00:12:01,000 --> 00:12:04,000 mchanyato wanaoutengeneza kwa mimea mbalimbali 286 00:12:04,000 --> 00:12:08,000 ambayo pia ina methoxydimethyltryptamine. 287 00:12:08,000 --> 00:12:10,000 Kuingiza unga huo kwenye pua yako 288 00:12:10,000 --> 00:12:14,000 ni kama vile kuzibuliwa kama risasi toka kwenye bomba la bunduki 289 00:12:14,000 --> 00:12:21,000 lililosakafiwa kwa michoro ya baroque na ukatua kwenye bahari ya umeme, (Kicheko) 290 00:12:21,000 --> 00:12:23,000 Haifanyi upotoshaji wa hali halisi; 291 00:12:23,000 --> 00:12:24,000 inayeyusha ufahamu wa hali halisi. 292 00:12:24,000 --> 00:12:27,000 Kwa kweli, nilikuwa nabishana na mwalimu wangu Profesa Richard Evan Shultes -- 293 00:12:27,000 --> 00:12:29,000 mtu ambaye alianzisha zama za uchunguzi wa madawa yanayobadili ufahamu 294 00:12:29,000 --> 00:12:31,000 kwa uvumbuzi wake wa uyoga wa ajabu 295 00:12:31,000 --> 00:12:33,000 nchini Mexico mnamo miaka ya 1930. 296 00:12:33,000 --> 00:12:35,000 Nilikuwa nabisha kwamba huwezi kuainisha tryptamines hizi 297 00:12:35,000 --> 00:12:38,000 kama vilevinishai kwakuwa wakati umezinguliwa nazo 298 00:12:38,000 --> 00:12:42,000 hatokuwepo mtu mwingine akisubiri kushuhudia muweweseko wake. (Kicheko) 299 00:12:42,000 --> 00:12:45,000 Lakini kuhusu tryptamines haziwezi kunywewa 300 00:12:45,000 --> 00:12:47,000 kwakuwa zimeathiriwa na kimeng'enya 301 00:12:47,000 --> 00:12:50,000 vinavyopatikana kiasilia katika utumbo wa binadamu na huitwa monoamine oxidase 302 00:12:50,000 --> 00:12:53,000 Vinaweza kunywewa tu iwapo vitachanganywa na 303 00:12:53,000 --> 00:12:56,000 kemikali nyinginezo zinazoweza kuathiri vimeng'enya vya MAO 304 00:12:56,000 --> 00:12:57,000 Na sasa, vitu vya kushangaza 305 00:12:57,000 --> 00:13:01,000 ni hizo beta-carbolines zinazopatikana kwenye liana 306 00:13:01,000 --> 00:13:04,000 ni vidhibiti vya MAO kwa namna fulani muhimu 307 00:13:05,000 --> 00:13:08,000 kuizimua tryptamine. Na hapo unajiuliza swali 308 00:13:08,000 --> 00:13:12,000 Ilikuwaje kwenye mimea mbalimbali zaidi ya 80,000, 309 00:13:12,000 --> 00:13:16,000 watu hawa walichagua hii miwili ambayo haifanani maumbile 310 00:13:16,000 --> 00:13:17,000 lakini ambayo ikichanganywa kwa namna hii, 311 00:13:17,000 --> 00:13:19,000 inatengeneza mchanganyiko wa kemikali 312 00:13:19,000 --> 00:13:21,000 kamilifu ambayo ni zaidi ya jumla ya kila kimojawapo? 313 00:13:21,000 --> 00:13:24,000 Vema, tunatumia maneno rahisi, kwamba walikuwa wakijaribu kubahatisha, 314 00:13:24,000 --> 00:13:25,000 jambo ambalo halina ukweli wowote. 315 00:13:26,000 --> 00:13:29,000 Lakini ukiwauliza Wahindi watakwambia, "Mimea inaongea nasi." 316 00:13:29,000 --> 00:13:30,000 Vema, hiyo ina maana gani? 317 00:13:30,000 --> 00:13:34,000 Kabila hili la Cofan wana aina 17 za ayahuasca, 318 00:13:34,000 --> 00:13:37,000 na wanaweza kuitofautisha kutoka mbali huko msituni, 319 00:13:38,000 --> 00:13:42,000 na zote hizi kwetu sisi zinaonekana kuwa sawa. 320 00:13:42,000 --> 00:13:44,000 Halafu unawauliza waliwezaje kuziainisha 321 00:13:44,000 --> 00:13:47,000 na wanasema " Nilidhani unajua masuala ya mimea, 322 00:13:47,000 --> 00:13:49,000 nina maana, hujui chochote?" Na nikasema "Hapana." 323 00:13:49,000 --> 00:13:52,000 Naam, inakuwa kwamba unachukua moja ya kila hizo aina 17 324 00:13:52,000 --> 00:13:55,000 usiku wa mbalamwezi na zinakuimbia kwa mlio tofauti 325 00:13:55,000 --> 00:13:57,000 Sasa, hiyo haiwezi kukupatia Ph.D. ya Harvard, 326 00:13:57,000 --> 00:14:01,000 lakini hii inavutia zaidi ya kuhesabu chavua. 327 00:14:01,000 --> 00:14:02,000 Na sasa, 328 00:14:02,000 --> 00:14:05,000 (Makofi) 329 00:14:05,000 --> 00:14:07,000 na tatizo -- na tatizo ni kwamba hata sisi 330 00:14:07,000 --> 00:14:09,000 tunaotetea hatima ya wazawa asilia 331 00:14:09,000 --> 00:14:10,000 tunawaona kama wanavutia 332 00:14:10,000 --> 00:14:12,000 lakini wamebanwa na mipaka ya historia 333 00:14:12,000 --> 00:14:15,000 wakati ulimwengu halisi, yaani ulimwengu wetu, unasonga mbele. 334 00:14:15,000 --> 00:14:17,000 Vema, ukweli ni kwamba karne ya 20, miaka 300 kuanzia sasa, 335 00:14:17,000 --> 00:14:20,000 haitakumbukwa kwa vita vyake 336 00:14:20,000 --> 00:14:21,000 au uvumbuzi wa kiteknolojia 337 00:14:21,000 --> 00:14:23,000 bali ni zama ambazo tulikaa 338 00:14:24,000 --> 00:14:26,000 na kuunga mkono waziwazi au tu kukubali 339 00:14:26,000 --> 00:14:29,000 uharibifu mkubwa wa urithi mkubwa wa kibaiolojia au kiutamaduni 340 00:14:29,000 --> 00:14:32,000 duniani. Kwa sasa, tatizo si mabadiliko. 341 00:14:32,000 --> 00:14:34,000 Tamaduni zote wakati wote 342 00:14:34,000 --> 00:14:37,000 zimejihusisha na mchezo 343 00:14:37,000 --> 00:14:38,000 wa masuala mapya ya kimaisha. 344 00:14:39,000 --> 00:14:41,000 Na tatizo si teknolojia peke yake. 345 00:14:42,000 --> 00:14:44,000 Wahindi Wekundu Sioux hawajaacha kuwa Sioux 346 00:14:44,000 --> 00:14:45,000 walipoacha upinde na mshale 347 00:14:45,000 --> 00:14:47,000 kama vile ambavyo Mmarekani kuacha kuwa Mmarekani 348 00:14:47,000 --> 00:14:49,000 alipoacha farasi na mkokoteni wake 349 00:14:49,000 --> 00:14:50,000 Si mabadiliko ya teknolojia 350 00:14:50,000 --> 00:14:54,000 yanayotishia uhai wa ethnosifia. Ni ubabe. 351 00:14:54,000 --> 00:14:56,000 Sura katili ya miliki. 352 00:14:56,000 --> 00:14:58,000 Na chochote unachokiangalia duniani, 353 00:14:58,000 --> 00:15:01,000 utaona kwamba hizi si tamaduni tu zinazopotea. 354 00:15:01,000 --> 00:15:03,000 Hawa ni watu halisi wanaoishi 355 00:15:03,000 --> 00:15:06,000 wakiondolewa uhai kwa nguvu zinazojulikana 356 00:15:06,000 --> 00:15:08,000 lakini ziko nje ya uwezo wao kuzimudu. 357 00:15:08,000 --> 00:15:10,000 Iwapo ni uharibifu mbaya wa misitu 358 00:15:11,000 --> 00:15:13,000 kwenye nchi ya Wapenani -- 359 00:15:13,000 --> 00:15:16,000 watu waishio kwa kuhamahama huko Asia ya Kusinimashariki, kutoka Sarawak -- 360 00:15:16,000 --> 00:15:20,000 watu walioshi huru mwituni mpaka kizazi kimoja kilichopita, 361 00:15:20,000 --> 00:15:23,000 na sasa wote wamezuiliwa na kutumikishwa 362 00:15:23,000 --> 00:15:25,000 kwenye kingo za mito, 363 00:15:25,000 --> 00:15:29,000 ambako utaona mito yenyewe imechafuliwa kwa tope 364 00:15:29,000 --> 00:15:31,000 yanayoonekana kubeba takriban nusu ya ukubwa wa kisiwa cha Borneo 365 00:15:31,000 --> 00:15:32,000 kwenda Bahari ya China ya Kusini, 366 00:15:32,000 --> 00:15:34,000 ambako meli za Kijapani zinasubiri 367 00:15:34,000 --> 00:15:38,000 tayari kubeba magogo mabichi yaliyozolewa toka misituni. 368 00:15:38,000 --> 00:15:39,000 Au suala la Wayanomami, 369 00:15:39,000 --> 00:15:41,000 ni ugonjwa ambao umeingia, 370 00:15:41,000 --> 00:15:43,000 wakati wa uvumbuzi wa dhahabu. 371 00:15:43,000 --> 00:15:45,000 Au tukienda kwenye milima ya Tibet, 372 00:15:45,000 --> 00:15:47,000 ambako ninafanya utafiti mwingi kwa sasa, 373 00:15:48,000 --> 00:15:51,000 utaona sura ya kutisha ya ubeberu wa kisiasa. 374 00:15:51,000 --> 00:15:53,000 Kama ujuavyo, mauaji ya halaiki, kumaliza maisha ya watu 375 00:15:53,000 --> 00:15:55,000 kunalaaniwa ulimwenguni kote, lakini mauaji ya kiutamaduni, 376 00:15:56,000 --> 00:15:59,000 uharibifu wa utaratibu wa maisha ya watu, siyo tu kwamba unalaaniwa, 377 00:15:59,000 --> 00:16:02,000 unashangiliwa -- na makundi mengi 378 00:16:02,000 --> 00:16:04,000 kuwa kama mkakati wa maendeleo. 379 00:16:04,000 --> 00:16:07,000 Na huwezi kuelewa uchungu wa Tibet 380 00:16:07,000 --> 00:16:09,000 mpaka usafiri kwa barabara. 381 00:16:09,000 --> 00:16:13,000 Niliwahi kusafiri maili 6,000 kutoka Chengdu huko Magharibi mwa China 382 00:16:13,000 --> 00:16:16,000 kwa barabara kupitia kusinimashariki Tibet mpaka Lhasa 383 00:16:16,000 --> 00:16:20,000 nikiwa na mwenzi ambaye ni kijana, na mpaka nilipofika Lhasa 384 00:16:20,000 --> 00:16:23,000 ndipo nikaelewa ukweli kuhusu takwimu 385 00:16:23,000 --> 00:16:24,000 unazozisikia. 386 00:16:24,000 --> 00:16:28,000 majengo matakatifu takriban 6,000 yamebomolewa kuwa vumbi na majivu. 387 00:16:28,000 --> 00:16:31,000 watu milioni 1.2 wameuawa na makada 388 00:16:31,000 --> 00:16:32,000 wakati wa Mapinduzi ya Utamaduni 389 00:16:33,000 --> 00:16:35,000 Baba wa kijana huyu alitawazwa kuwa naibu wa Lama. 390 00:16:35,000 --> 00:16:37,000 Kwa sababu hiyo aliuawa mara tu 391 00:16:37,000 --> 00:16:39,000 ya uvamizi wa China. 392 00:16:39,000 --> 00:16:41,000 Mjomba wake alitoroka pamoja na mhashamu kwenda uhamishoni 393 00:16:41,000 --> 00:16:44,000 nchini Nepal 394 00:16:44,000 --> 00:16:46,000 Mama yake alifungwa kwa sababu tu -- 395 00:16:46,000 --> 00:16:48,000 alikuwa tajiri. 396 00:16:49,000 --> 00:16:51,000 Yeye alipenyezwa kwa siri kuingizwa jela akiwa na umri wa miaka miwili 397 00:16:51,000 --> 00:16:53,000 kujificha kwenye sketi za mamaake 398 00:16:53,000 --> 00:16:55,000 kwakuwa hakuweza kustahimili kuishi bila mwanae. 399 00:16:55,000 --> 00:16:57,000 Dada yake aliyefanya kitendo hicho cha kishujaa 400 00:16:57,000 --> 00:16:58,000 alipelekwa kwenye kambi ya elimu 401 00:16:58,000 --> 00:17:00,000 Siku moja kwa bahati mbaya alikumbana na kundi la askari 402 00:17:01,000 --> 00:17:03,000 wa Mao, na kwa kosa hilo, 403 00:17:03,000 --> 00:17:06,000 akahukumiwa kifungo cha miaka saba na kazi ngumu. 404 00:17:06,000 --> 00:17:09,000 Machungu ya Tibet hayavumiliki, 405 00:17:09,000 --> 00:17:12,000 lakini ujasiri wa watu hawa ni kitu cha kusisimua. 406 00:17:13,000 --> 00:17:16,000 Na mwisho wake, inakuja mwisho kwenye uchaguzi, 407 00:17:16,000 --> 00:17:19,000 Tunataka kuishi kwenye ulimwengu unaochosha wa utamaduni mmoja 408 00:17:19,000 --> 00:17:22,000 au tunapenda kuwa na mtandao wa tamaduni mbalimbali? 409 00:17:22,000 --> 00:17:25,000 Margaret Mead, mtaalam maarufu wa mambo ya kale, kabla ya kifo chake alisema 410 00:17:25,000 --> 00:17:28,000 wasiwasi wake mkubwa ni kwamba tunazidi kuelekea kwenye 411 00:17:28,000 --> 00:17:30,000 hii hali ya mtazamo mmoja wa kilimwengu 412 00:17:30,000 --> 00:17:35,000 si tu kwamba tutaona uwezo mkubwa wa ufahamu wa binadamu 413 00:17:35,000 --> 00:17:39,000 ukipunguzwa kuwa mawazo finyu, 414 00:17:39,000 --> 00:17:40,000 bali tutazinduka siku moja 415 00:17:40,000 --> 00:17:43,000 tukiwa tumesahau kwamba kuna uwezekano tofauti wa mambo. 416 00:17:44,000 --> 00:17:47,000 Na ni taadhima kubwa kukumbuka kwamba kizazi chetu kimekuwepo kwa 417 00:17:47,000 --> 00:17:49,000 takriban miaka 600,000 418 00:17:49,000 --> 00:17:52,000 Mapinduzi ya Kilimo -- yaliyoanzisha ukulima, 419 00:17:52,000 --> 00:17:54,000 tulipo salim amri kwenye imani ya mbegu 420 00:17:54,000 --> 00:17:56,000 ushairi wa shaman ulisambaratishwa 421 00:17:56,000 --> 00:17:57,000 kwa maandiko ya ukuhani 422 00:17:57,000 --> 00:18:00,000 tukajenga daraja za umiliki ziada -- 423 00:18:00,000 --> 00:18:02,000 ni miaka 10,000 iliyopita tu. 424 00:18:02,000 --> 00:18:04,000 Maendeleo ya viwanda kama tuyajuavyo 425 00:18:04,000 --> 00:18:06,000 yana si zaidi ya miaka 300. 426 00:18:06,000 --> 00:18:08,000 Na sasa, historia hiyo ya juu juu hainishawishi 427 00:18:08,000 --> 00:18:11,000 kwamba tuna majibu ya matatizo yetu yote 428 00:18:11,000 --> 00:18:13,000 yatakayo tufariji katika hatima ya milenia 429 00:18:13,000 --> 00:18:15,000 Wakati hizi tamaduni mbalimbali ulimwenguni 430 00:18:15,000 --> 00:18:18,000 zikiulizwa maana ya kuwa binadamu, 431 00:18:18,000 --> 00:18:20,000 zitakujibu kwa sauti 10,000 tofauti. 432 00:18:20,000 --> 00:18:26,000 Na kwa kupitia wimbo huo ndipo tutatambua uwezekano 433 00:18:26,000 --> 00:18:29,000 wa kuona kwamba sisi ni viumbe wenye ufahamu, 434 00:18:29,000 --> 00:18:32,000 kufahamu fika kuhakikisha watu wote na bustani zote 435 00:18:32,000 --> 00:18:38,000 zinapata namna ya kustawi. Na kuna vipindi vya matumaini. 436 00:18:38,000 --> 00:18:41,000 Hii ni picha niliyoipiga kwenye ncha ya kaskazini mwa kisiwa cha Baffin 437 00:18:41,000 --> 00:18:43,000 nilipokwenda kuwinda nyangumi wenye pembe nikiwa na Wainuiti, 438 00:18:44,000 --> 00:18:47,000 na mtu huyu, Olaya, alinisimulia hadithi ya ajabu kuhusu babu yake. 439 00:18:48,000 --> 00:18:50,000 Serikali ya Canada haikuwa ikiwatendea haki 440 00:18:50,000 --> 00:18:52,000 Wainuiti, katika miaka ya 1950, 441 00:18:52,000 --> 00:18:55,000 ili kujenga utaifa, tuliwahamishia kwenye vijiji. 442 00:18:55,000 --> 00:18:59,000 Babu yake alikataa kwenda. 443 00:18:59,000 --> 00:19:03,000 Nduguze, kwa kuhofia maisha yake, wakampokonya silaha zake zote, 444 00:19:03,000 --> 00:19:04,000 na vifaa vyake vyote. 445 00:19:05,000 --> 00:19:07,000 Na sasa, uelewe kwamba Wainuiti hawakuogopa baridi; 446 00:19:07,000 --> 00:19:08,000 walijinufaisha nayo. 447 00:19:08,000 --> 00:19:11,000 Mikokoteni ya kuteleza kwenye barafu ilitengenezwa kwa samaki 448 00:19:11,000 --> 00:19:12,000 na kufunikwa kwa ngozi ya swala. 449 00:19:12,000 --> 00:19:17,000 Kwahiyo babu yake mtu huyu hakutishika na usiku wa huko Aktika 450 00:19:17,000 --> 00:19:19,000 au upepo mkali ulokuwa ukipuliza 451 00:19:19,000 --> 00:19:22,000 Alitoka nje, akavua suruali yake 452 00:19:23,000 --> 00:19:26,000 na kunyea mkononi. Na kinyesi kilipoanza kuganda, 453 00:19:26,000 --> 00:19:29,000 akafinyanga katika umbile la upanga. 454 00:19:29,000 --> 00:19:31,000 Akatemea mate kwenye upande wa makali ya upanga huo wa kinyesi 455 00:19:31,000 --> 00:19:34,000 na baadae inaganda na kuwa ngumu, na aliitumia kumuua mbwa. 456 00:19:34,000 --> 00:19:37,000 Akamchuna mbwa na kuboresha silaha yake, 457 00:19:37,000 --> 00:19:40,000 akachukua ubavu wa mbwa na kutengeneza mkokoteni wa kuteleza, 458 00:19:41,000 --> 00:19:42,000 akamfunga mbwa wa pili, 459 00:19:42,000 --> 00:19:46,000 na kutokomea kwenye uwanda wa barafu, kisu cha kinyesi kibindoni. 460 00:19:46,000 --> 00:19:50,000 Halafu unazungumzia kujikwamua bila kitu chochote (Kicheko) 461 00:19:50,000 --> 00:19:51,000 Na hii, kwa namna mbalimbali, 462 00:19:51,000 --> 00:19:53,000 (Makofi) 463 00:19:53,000 --> 00:19:55,000 hii ni ishara ya ujasiri wa Wainuiti 464 00:19:55,000 --> 00:19:58,000 na wazawa wote asilia ulimwenguni kote. 465 00:19:58,000 --> 00:20:00,000 Serikali ya Canada mnamo Aprili 1999 466 00:20:00,000 --> 00:20:03,000 waliwarudishia mamlaka Wainuiti 467 00:20:03,000 --> 00:20:06,000 kwenye eneo kubwa kuliko California na Texas yakiunganishwa pamoja. 468 00:20:06,000 --> 00:20:08,000 Ni nchi yetu mpya. Inaitwa Nunavut. 469 00:20:09,000 --> 00:20:12,000 Ni jimbo linalojitegemea. Wanasimamia maliasili zote za madini. 470 00:20:12,000 --> 00:20:14,000 Ni mfano wa ajabu jinsi ambavyo taifa 471 00:20:14,000 --> 00:20:18,000 linafikia -- au kutafuta muafaka na watu wake. 472 00:20:19,000 --> 00:20:22,000 Na mwisho, hatimaye, naona ni wazi kabisa 473 00:20:22,000 --> 00:20:23,000 walau wengi wetu tulosafiri 474 00:20:23,000 --> 00:20:25,000 kwenye sehemu hizi za mbali kwenye dunia, 475 00:20:27,000 --> 00:20:28,000 tumegundua si mbali tena. 476 00:20:28,000 --> 00:20:30,000 Ni makazi ya mtu fulani. 477 00:20:30,000 --> 00:20:32,000 Yanaonyesha matawi ya mawazo ya binadamu 478 00:20:32,000 --> 00:20:36,000 kwamba nenda nyuma kwenye mwanzo wa nyakati. Na kwetu sote, 479 00:20:36,000 --> 00:20:39,000 ndoto za watoto hawa, kama vile ndoto za watoto wetu wenyewe, 480 00:20:39,000 --> 00:20:42,000 zimekuwa sehemu ya jiografia ya matumaini. 481 00:20:42,000 --> 00:20:46,000 Kwahiyo, tunachojaribu kufanya National Geographic hatimaye, 482 00:20:46,000 --> 00:20:50,000 ni, tunaamini kwamba wanasiasa hawafanikishi lolote. 483 00:20:50,000 --> 00:20:51,000 Huo ni ukosoaji wa hoja -- 484 00:20:51,000 --> 00:20:53,000 (Makofi) 485 00:20:53,000 --> 00:20:55,000 tunadhani kwamba wakosoaji hawana ushawishi, 486 00:20:55,000 --> 00:20:58,000 lakini tunaamini kwamba kuhadithia kutaibadili dunia, 487 00:20:58,000 --> 00:21:01,000 na kwahiyo sisi ni miongoni mwa taasisi bora zaidi za masimulizi 488 00:21:01,000 --> 00:21:04,000 duniani. Tunapata watembezi milioni 35 kwenye tovuti yetu kila mwezi. 489 00:21:04,000 --> 00:21:07,000 Nchi 156 zinarusha matangazo ya televisheni yetu. 490 00:21:08,000 --> 00:21:10,000 Majarida yetu yanasomwa na mamilioni. 491 00:21:10,000 --> 00:21:13,000 Na tunachokifanya ni safari nyingi 492 00:21:13,000 --> 00:21:15,000 kwenda kwenye ethnosifia ambako tunawapeleka watazamaji wetu 493 00:21:15,000 --> 00:21:17,000 kwenye sehemu ambako kuna maajabu ya kiutamaduni 494 00:21:18,000 --> 00:21:20,000 ambayo hawatoweza kuvumilia bali kushangazwa 495 00:21:20,000 --> 00:21:22,000 na wanachokiona, na natumaini, kwahiyo, 496 00:21:22,000 --> 00:21:25,000 kukubali taratibu, mmoja mmoja, 497 00:21:25,000 --> 00:21:27,000 kiini cha uvumbuzi wa elimu ya mambo ya kale: 498 00:21:27,000 --> 00:21:31,000 kwamba ulimwengu unastahili kuwepo kwa namna mbalimbali 499 00:21:31,000 --> 00:21:32,000 na kwamba tunaweza kupata namna ya kuishi 500 00:21:32,000 --> 00:21:35,000 katika ulimwengu wa tamaduni tofauti 501 00:21:35,000 --> 00:21:37,000 ambako busara zote za watu 502 00:21:37,000 --> 00:21:40,000 zitachangia ustawi wetu sote 503 00:21:40,000 --> 00:21:41,000 Asante sana. 504 00:21:41,000 --> 00:21:43,000 (Makofi)