0:00:00.000,0:00:03.000 Kama ujuavyo, moja ya raha kubwa za kusafiri 0:00:03.000,0:00:05.000 na moja ya furaha za utafiti wa mahusiano ya kikabila 0:00:05.000,0:00:07.000 ni fursa ya kuishi miongoni mwao 0:00:07.000,0:00:09.000 hao wasiosahau namna za kijadi 0:00:09.000,0:00:12.000 ambao wangali wakihisi ya kale kwenye upepo, 0:00:12.000,0:00:15.000 na kuyagusa juu ya mawe yaliyosafishwa na mvua, 0:00:15.000,0:00:17.000 na kuyaonja kwenye majani machungu ya mimea. 0:00:17.000,0:00:21.000 Kujua kwamba wanaoabudu chuipamba bado wana safari kupita mbingu za mbali, 0:00:21.000,0:00:25.000 au imani za wazee wa Kiinuiti zinaleta maana, 0:00:25.000,0:00:27.000 au kwamba huko Himalaya, 0:00:28.000,0:00:32.000 Mabudha bado wanaifuata pumzi ya Dharma, 0:00:32.000,0:00:35.000 ni katika kukumbuka utambuzi wa msingi wa anthropolojia, 0:00:35.000,0:00:37.000 na kwamba mtazamo wa ulimwengu tunamoishi 0:00:38.000,0:00:40.000 haupo kihalisia, 0:00:40.000,0:00:41.000 bali ni nadharia tu ya ukweli, 0:00:41.000,0:00:45.000 ni matokeo ya jozi moja tu ya machaguo kadhaa 0:00:45.000,0:00:49.000 ambayo mababu zetu walifanya, japo kwa mafanikio, vizazi kadhaa vilivyopita. 0:00:50.000,0:00:54.000 Na kwa hakika, sote tunashabihiana katika kufuata kanuni za maumbile 0:00:54.000,0:00:56.000 Sote tunazaliwa. Sote tunazaa watoto. 0:00:56.000,0:00:58.000 Tunapitia kafara za kusimikwa, 0:00:58.000,0:01:00.000 Tunalazimika kukabiliana na ukatili wa kutenganishwa kwa kifo 0:01:00.000,0:01:04.000 haitushangazi kwamba sote tunaimba, sote tunacheza, 0:01:04.000,0:01:06.000 sote tuna sanaa. 0:01:06.000,0:01:09.000 Lakini kinachosisimua zaidi ni namna pekee za mapigo ya wimbo, 0:01:09.000,0:01:11.000 mahadhi ya dansi kwa kila utamaduni. 0:01:11.000,0:01:14.000 Na iwapo ni Wapenani wa misitu ya Borneo 0:01:14.000,0:01:17.000 au makuhani wa Voodoo nchini Haiti 0:01:18.000,0:01:22.000 au majemedari wa jangwa la Kaisut Kaskazini mwa Kenya, 0:01:24.000,0:01:26.000 au matabibu wa Kikurandero wa milima ya Andes, 0:01:27.000,0:01:32.000 au nyumba ya kuhamishika iliyopo katikati ya Sahara 0:01:32.000,0:01:34.000 Huyu ndiye mwenzi ambaye nilisafiri nae jangwani 0:01:34.000,0:01:35.000 mwezi mmoja uliopita 0:01:35.000,0:01:38.000 au mchunga mbuzipori wa miteremko ya Qomolangma, 0:01:38.000,0:01:40.000 Everest, mungu mke wa ulimwengu. 0:01:40.000,0:01:43.000 Watu wote hawa wanatufundisha kwamba kuna namna nyingine za kuwa, 0:01:43.000,0:01:44.000 namna tofauti za kufikiria 0:01:44.000,0:01:46.000 namna mbalimbali za kujiwekeza katika Dunia. 0:01:46.000,0:01:48.000 Na hili ndilo wazo, ambalo ukilifikiria, 0:01:48.000,0:01:50.000 laweza kukupa tumaini, 0:01:50.000,0:01:53.000 Sasa, kwa pamoja tamaduni nyingi mbalimbali za ulimwengu 0:01:53.000,0:01:57.000 zinafanya mtandao wa maisha ya kiroho na kiutamaduni 0:01:57.000,0:01:59.000 unaoifunika dunia, 0:01:59.000,0:02:01.000 na ni muhimu kwa ustawi wa dunia 0:02:01.000,0:02:04.000 hali kadhalika mtandao wa kibaiolojia wa maisha unaoujua kama biosifia. 0:02:04.000,0:02:07.000 Na waweza kufikiria kwamba mtandao huu wa kiutamaduni kwenye maisha 0:02:07.000,0:02:08.000 kuwa ni ethnosifia 0:02:08.000,0:02:10.000 na waweza kuainisha ethnosifia 0:02:10.000,0:02:13.000 kuwa ni jumla ya mawazo na ndoto, imani, 0:02:13.000,0:02:16.000 mitazamo, hamasa, vipawa vilivyohuishwa 0:02:16.000,0:02:20.000 na mawazo ya binadamu tokea mapambazuko ya ufahamu. 0:02:20.000,0:02:23.000 Ethnosifia ni urithi mkuu wa utu, 0:02:23.000,0:02:25.000 ni ishara ya kila namna tulivyo 0:02:25.000,0:02:29.000 na kila namna tuwezavyo kuwa viumbe wadadisi ajabu 0:02:30.000,0:02:33.000 Na kwa namna ambavyo biosifia imeharibiwa, 0:02:33.000,0:02:35.000 ndivyo pia ethnosifia 0:02:35.000,0:02:37.000 --na iwapo kwa kiwango kikubwa zaidi. 0:02:37.000,0:02:39.000 Hakuna mwanabaiolojia, kwa mfano, awezaye kusema 0:02:39.000,0:02:42.000 kwamba 50% ya viumbe wote au zaidi wamefikia au wapo 0:02:42.000,0:02:44.000 katika hatari ya kuteketea kwakuwa si kweli, 0:02:44.000,0:02:46.000 na pia kwamba -- tishio kubwa la maafa 0:02:46.000,0:02:49.000 katika uwanja wa mtandao wa kibailojia 0:02:49.000,0:02:52.000 nadra sana unaangalia kwa mtazamo tunaodhania kuwa bora zaidi 0:02:52.000,0:02:54.000 kwenye uwanja wa mtandao wa utamaduni. 0:02:54.000,0:02:57.000 Na kielelezo kikubwa cha muelekeo huo ni kupotea kwa lugha. 0:02:57.000,0:03:00.000 Wakati nyote mliopo humu ndani mlipozaliwa, 0:03:00.000,0:03:03.000 kulikuwepo lugha 6,000 zikitumika duniani. 0:03:03.000,0:03:06.000 Kwa sasa, lugha si mkusanyiko wa maneno 0:03:06.000,0:03:08.000 au mkusanyiko wa kanuni za sarufi. 0:03:08.000,0:03:10.000 Lugha ni mwanga wa roho ya binadamu. 0:03:10.000,0:03:13.000 Ni chombo ambacho hupitisha uhai wa tamaduni fulani 0:03:13.000,0:03:14.000 kuja kwenye ulimwengu wa vitu. 0:03:14.000,0:03:17.000 Kila lugha ni mkuzo wa msitu wa akili, 0:03:17.000,0:03:21.000 mgawanyiko wa vijito, wazo, bioanuwai ya mambo ya kiroho, 0:03:21.000,0:03:25.000 Miongoni mwa lugha hizo 6,000 mpaka leo tunapokuwa hapa Monterey, 0:03:25.000,0:03:29.000 takriban nusu yake hazitamkwi kwenye masikio ya watoto. 0:03:29.000,0:03:32.000 Hazifundishwi kwa watoto wachanga tena, 0:03:32.000,0:03:34.000 maana yake ni kwamba, kwa hakika, labda kama kuna mambo yatabadilika, 0:03:34.000,0:03:35.000 zimeshakufa. 0:03:35.000,0:03:39.000 Hakuna upweke unaozidi ule wa kugubikwa na ukimya, 0:03:39.000,0:03:41.000 wa kuwa mtu wa mwisho kabisa kuongea lugha yako, 0:03:41.000,0:03:44.000 kutokuwa na namna ya kurithisha busara za mababu 0:03:44.000,0:03:47.000 au kutarajia ahadi za watoto? 0:03:47.000,0:03:50.000 Na zaidi, kinachotisha ni hatima ya mtu fulani 0:03:50.000,0:03:52.000 sehemu fulani ya Dunia takriban kila wiki mbili, 0:03:52.000,0:03:54.000 kwa sababu kila wiki mbili, kuna mzee anafariki dunia 0:03:54.000,0:03:56.000 na anakwenda kaburini na silabi za mwisho 0:03:56.000,0:03:58.000 za lugha ya kale. 0:03:58.000,0:04:00.000 Na najua kuna baadhi yenu mngesema,"Naam, si ingekuwa vema? 0:04:00.000,0:04:01.000 Si ingekuwa bora zaidi 0:04:01.000,0:04:04.000 iwapo sote tungeongea lugha moja?" Nami nasema "Vema, 0:04:04.000,0:04:07.000 tuifanye lugha hiyo Kiyoruba. Tuifanye iwe Kikantoni. 0:04:07.000,0:04:08.000 Tuifanye Kikogi." 0:04:08.000,0:04:10.000 Na wote mara mtagundua nini kitatokea 0:04:10.000,0:04:13.000 kutoweza kuongea lugha yako mwenyewe. 0:04:13.000,0:04:16.000 Na ninachotaka kufanya nanyi leo 0:04:16.000,0:04:20.000 ni kuwapeleka kwenye safari ya ethnosifia -- 0:04:20.000,0:04:22.000 safari fupi ya kupitia ethnosifia 0:04:22.000,0:04:26.000 kujaribu kukupa picha ya nini kinapotea. 0:04:27.000,0:04:34.000 Naam, kuna wengi wetu wanaosahau 0:04:34.000,0:04:36.000 ninaposema "kuna namna mbalimbali za kuwa," 0:04:36.000,0:04:38.000 Namaanisha kweli kuna namna mbalimbali za kuwa. 0:04:39.000,0:04:44.000 Chukulia kwa mfano, mtoto huyu wa Barasana huko kaskazini magharibi Amazoni 0:04:44.000,0:04:45.000 watu wa majoka ya anakonda 0:04:45.000,0:04:47.000 wanaoamini miujiza itokanayo na mto wa maziwa 0:04:47.000,0:04:50.000 kutoka mashariki kwenye matumbo ya nyoka walotukuka. 0:04:50.000,0:04:53.000 Naam, hawa ni watu ambao kwa kutambua 0:04:53.000,0:04:55.000 hawawezi kutofautisha rangi ya bluu na rangi ya kijani 0:04:55.000,0:04:57.000 kwakuwa paa la mbingu 0:04:57.000,0:04:58.000 linalinganishwa na paa la msitu 0:04:58.000,0:05:00.000 ambamo watu hawa wanategemea. 0:05:00.000,0:05:03.000 Wana kanuni ya ajabu kuhusu ndoa na lugha 0:05:03.000,0:05:05.000 ijulikanayo kama ndoa baina ya lugha tofauti: 0:05:05.000,0:05:08.000 unalazimika kumuoa azungumzaye lugha tofauti na yako. 0:05:08.000,0:05:10.000 Na hii inatokana na imani za kale, 0:05:10.000,0:05:12.000 na bado hali ya kushangaza ipo kwenye nyumba hizi ndefu 0:05:12.000,0:05:14.000 ambako kuna lugha sita au saba zinazozungumzwa 0:05:14.000,0:05:16.000 kutokana na kuoana, 0:05:16.000,0:05:19.000 hutomsikia yeyote akijifunza lugha. 0:05:19.000,0:05:22.000 Wanasikiliza tu na kuanza kuongea. 0:05:22.000,0:05:24.000 Au, moja ya makabila ya kushangaza niliyowahi kuishi nayo, 0:05:24.000,0:05:28.000 ni Waorani wa Kaskazini-Mashariki ya Ecuador, 0:05:28.000,0:05:31.000 ni watu wa ajabu ambao walitembelewa kwa mara ya kwanza mwaka 1958. 0:05:31.000,0:05:35.000 Mnamo mwaka 1957, wamishonari watano walijaribu kuwatembelea 0:05:35.000,0:05:36.000 na wakafanya kosa kubwa. 0:05:36.000,0:05:37.000 Walidondosha kutoka hewani 0:05:37.000,0:05:39.000 picha zao za ukubwa nchi nane kwa kumi 0:05:39.000,0:05:41.000 kitu ambacho tunaweza kusema ni ishara ya urafiki, 0:05:41.000,0:05:43.000 wakasahau kwamba watu hawa wa misitu ya kitropiki 0:05:43.000,0:05:46.000 hawakuwahi kuona kitu chochote chenye vina viwili kabla 0:05:46.000,0:05:48.000 Wakaziokota picha hizi toka ardhini 0:05:48.000,0:05:51.000 wakajaribu kuangalia kwa nyuma ili kupata umbile kamili 0:05:51.000,0:05:53.000 hawakuona kitu, na wakaamini kwamba hizi ni kadi za wito 0:05:53.000,0:05:56.000 toka kwa shetani, kwahiyo wakawachoma mikuki wamishonari na kuwaua. 0:05:57.000,0:05:59.000 Lakini Waorani si kwamba tu waliwachoma wageni. 0:05:59.000,0:06:00.000 Walichomana wao kwa wao. 0:06:00.000,0:06:03.000 54% ya vifo vyao vilitokana na kuchomana mikuki wao kwa wao. 0:06:03.000,0:06:06.000 Tulifuatilia vizazi nane vilivyopita, 0:06:06.000,0:06:08.000 na tukapata matukio mawili tu ya vifo vya asilia 0:06:08.000,0:06:10.000 na tulipowauliza zaidi watu habari hizi, 0:06:10.000,0:06:12.000 wakakiri kwamba mmoja wao alikuwa mzee sana 0:06:12.000,0:06:16.000 na angekufa kwa uzee, kwahiyo tukamchoma mkuki tu (Kicheko) 0:06:16.000,0:06:19.000 Lakini pia wana ujuzi wa ajabu 0:06:19.000,0:06:20.000 wa msituni ambao unashangaza sana. 0:06:20.000,0:06:23.000 Wawindaji huweza kunusa harufu ya mkojo wa mnyama toka umbali wa hatua 40 0:06:23.000,0:06:26.000 na wakakwambia ni kiumbe gani ameuacha mkojo huo. 0:06:26.000,0:06:28.000 Miaka ya 80, nilikuwa na kazi moja ya kusisimua 0:06:28.000,0:06:30.000 nilipoulizwa na Profesa wangu wa Harvard 0:06:30.000,0:06:32.000 iwapo ningependa kwenda Haiti, 0:06:33.000,0:06:35.000 kupeleleza vikundi vya siri 0:06:35.000,0:06:37.000 vilivyokuwa ngome kubwa ya Duvalier 0:06:37.000,0:06:38.000 na majasusi wa Tonton Macoutes 0:06:38.000,0:06:41.000 na kupata sumu itumikayo kutengeneza mizuka. 0:06:41.000,0:06:44.000 ili kupata mantiki kutokana na uvumi 0:06:44.000,0:06:47.000 ilinibidi nijaribu kuelewa kuhusu imani hii ya ajabu 0:06:47.000,0:06:50.000 ya Vodoun, na Voodoo si kikundi cha uchawi wa nguvu za kiza 0:06:50.000,0:06:53.000 Kinyume chake, ni mtazamo fulani wa ulimwengu nje ya maumbile. 0:06:53.000,0:06:54.000 inashangaza. 0:06:54.000,0:06:55.000 Iwapo nikikutaka utaje dini kuu za dunia, 0:06:55.000,0:06:56.000 utasema nini? 0:06:56.000,0:06:59.000 Ukristu, Uislamu, Ubudha, Ujudea, na kadhalika. 0:06:59.000,0:07:01.000 Huwa kuna bara moja linasahaulika, 0:07:01.000,0:07:03.000 kwa mtazamo kwamba nchi za Afrika, kusini mwa Sahara 0:07:03.000,0:07:05.000 hazikuwa na imani za kidini. Vema, kwa hakika, walikuwa nazo 0:07:05.000,0:07:07.000 na Voodoo ni mchujo tu 0:07:08.000,0:07:09.000 wa mawazo haya makuu ya kidini 0:07:09.000,0:07:12.000 yaliyokuja wakati wa uhamisho wa kikatili wa kipindi cha utumwa. 0:07:12.000,0:07:14.000 Lakini, kinachofanya voodoo kuwa ya kipekee 0:07:14.000,0:07:16.000 ni huu uhusiano wa kuishi 0:07:16.000,0:07:17.000 kati ya wazima na wafu. 0:07:17.000,0:07:18.000 Kwahiyo, wanaoishi wanazaa mizimu. 0:07:18.000,0:07:21.000 Mizimu inaswaliwa kutoka kwenye Maji Makuu, 0:07:21.000,0:07:23.000 kuitikia mapigo ya muziki 0:07:23.000,0:07:25.000 na kusambaratisha roho za wazima kwa muda 0:07:25.000,0:07:29.000 ili kwa kipindi maalum na kifupi, makuhani wanakuwa mungu. 0:07:29.000,0:07:31.000 Ndiyo maana Mavoodoo wanapenda kusema 0:07:31.000,0:07:34.000 kwamba "Nyie watu weupe mnakwenda kanisani na kuongea kuhusu Mungu. 0:07:34.000,0:07:36.000 Sisi tunacheza hekaluni na kuwa Mungu." 0:07:36.000,0:07:39.000 Na ni kwa sababu mnaingiliwa, mnachukuliwa na mizimu, 0:07:39.000,0:07:40.000 unawezaje kuathirika? 0:07:40.000,0:07:43.000 Kwahiyo unaona maonyesho haya ya kushangaza: 0:07:43.000,0:07:45.000 kuhani wa Voodoo akiwa katika hali ya kupandisha mori 0:07:45.000,0:07:48.000 akifukiza uvumba bila hofu, 0:07:48.000,0:07:51.000 ni kitendo cha kushangaza cha uwezo wa akili 0:07:51.000,0:07:52.000 kuathiri mwili unaoibeba 0:07:52.000,0:07:55.000 unapozimuliwa na hali ya kupandisha mori. 0:07:56.000,0:07:58.000 Na sasa, katika watu wote niliowahi kuishi nao, 0:07:58.000,0:08:00.000 wa ajabu zaidi ni Wakogi 0:08:00.000,0:08:03.000 wa Sierra Nevada ya Santa Marta kaskazini mwa Colombia. 0:08:03.000,0:08:06.000 Wazawa wa ustaarabu wa kikatili wa kale 0:08:06.000,0:08:09.000 ambao uliwahi kuenea uwanda wote wa Colombia katika pwani ya Caribbean 0:08:09.000,0:08:10.000 wakati wa uvamizi, 0:08:10.000,0:08:13.000 watu hawa walikimbilia kwenye safu ya milima ya kivolkano 0:08:13.000,0:08:15.000 inayopanda juu ya pwani ya Caribbean 0:08:15.000,0:08:17.000 Katika bara lililomwaga damu, 0:08:17.000,0:08:20.000 hawa ni watu pekee ambao hawakushindwa vita na Waspanishi 0:08:20.000,0:08:23.000 Mpaka leo, bado wanatawaliwa na makuhani wa kafara 0:08:23.000,0:08:25.000 lakini mafunzo yao ya ukuhani ni ya ajabu sana 0:08:26.000,0:08:28.000 Makuhani vijana wanachukuliwa toka kwenye familia zao 0:08:28.000,0:08:30.000 katika umri wa miaka mitatu au minne, 0:08:30.000,0:08:32.000 na kufichwa kwenye ulimwengu wa giza 0:08:32.000,0:08:36.000 kwenye vibanda vya mawe chini ya malundo ya barafu kwa miaka 18. 0:08:36.000,0:08:37.000 Vipindi viwili vya miaka tisa 0:08:37.000,0:08:40.000 imepangwa hivyo makusudi kuigiza miezi tisa ya kukua 0:08:40.000,0:08:42.000 waliokaa ndani ya tumbo la mama, 0:08:42.000,0:08:45.000 na sasa kilimwengu wapo kwenye tumbo la mama mkuu. 0:08:45.000,0:08:46.000 Na kwa muda wote huu, 0:08:47.000,0:08:50.000 wanafundishwa maadili muhimu ya utamaduni wao, 0:08:50.000,0:08:52.000 maadili ambayo yanatunza maombi ya sala zao 0:08:52.000,0:08:55.000 na sala zao pekee ndizo zinatunza maumbile -- 0:08:55.000,0:08:57.000 au twaweza kusema uwiano wa mazingira. 0:08:58.000,0:08:59.000 Na mwisho wa mafunzo haya ya ajabu, 0:08:59.000,0:09:01.000 siku moja wanatolewa nje ghafla 0:09:01.000,0:09:04.000 na kwa mara ya kwanza katika maisha yao, wakiwa na umri wa miaka 18 0:09:04.000,0:09:08.000 wanaona jua likichomoza. Na katika kipindi hicho cha ufahamu 0:09:08.000,0:09:11.000 wa mwanga wa kwanza wakati Jua linapoangaza milima 0:09:11.000,0:09:12.000 yenye mandhari ya kupendeza, 0:09:13.000,0:09:15.000 mara vitu vyote walivyojifunza kwa nadharia 0:09:15.000,0:09:18.000 vinatimia kwa utukufu mkubwa. Na kuhani anarudi nyuma 0:09:18.000,0:09:20.000 na kusema "Mnaona? Ni hakika kama nilivyowaambia. 0:09:20.000,0:09:23.000 Ni nzuri sana. Ni jukumu lenu kuilinda." 0:09:23.000,0:09:25.000 Wanajiita kaka wakubwa 0:09:25.000,0:09:28.000 na wanasema sisi, ambao ni kaka wadogo, 0:09:28.000,0:09:31.000 tunaohusika na kuiharibu dunia, 0:09:32.000,0:09:34.000 Na sasa, kiwango cha ufahamu kinakuwa muhimu sana. 0:09:34.000,0:09:36.000 Tunapofikiria kuhusu wazawa wa asilia na mandhari ya nchi, 0:09:36.000,0:09:38.000 tunakuwa aidha tunamfuata Rousseau 0:09:38.000,0:09:41.000 na nadharia ya ukatili halali, 0:09:41.000,0:09:43.000 ambao una maanisha kwamba ubaguzi wa rangi ni urahisi, 0:09:43.000,0:09:46.000 au badala yake, tumfuate Thoreau 0:09:46.000,0:09:48.000 na kusema watu hawa wapo karibu zaidi na Dunia kuliko sisi, 0:09:48.000,0:09:50.000 Vema, wazawa asilia hawana unyovu wa moyo 0:09:50.000,0:09:52.000 wala hawasumbuliwi na mawazo ya kukumbuka nyumbani 0:09:52.000,0:09:54.000 Hakuna fursa kubwa 0:09:54.000,0:09:56.000 kwenye mabwawa ya malaria huko Asmat 0:09:56.000,0:09:59.000 au kwenye upepo mkali wa Tibet, lakini wameweza, hata hivyo, 0:09:59.000,0:10:03.000 kwa kupitia ibada fulani, wameweza kutengeneza mtazamo wa Dunia 0:10:03.000,0:10:06.000 ambao unazingatia kujijua au kuwa karibu na kujijua, 0:10:06.000,0:10:08.000 lakini kwa kutumia ufahamu wa juu zaidi: 0:10:08.000,0:10:11.000 wazo la kwamba Dunia yenyewe yaweza kuwepo 0:10:12.000,0:10:14.000 kwakuwa imepewa pumzi kwa ufahamu wa binadamu. 0:10:14.000,0:10:16.000 Naam, hiyo ina maana gani? 0:10:16.000,0:10:18.000 Ina maana kwamba mtoto mdogo wa huko Andes 0:10:18.000,0:10:20.000 aliyelelewa kuamini kwamba milima ni mizimu ya Apu 0:10:20.000,0:10:22.000 inayoleta hatima yake 0:10:22.000,0:10:25.000 atakuwa binadamu tofauti kabisa 0:10:25.000,0:10:28.000 na atakuwa na uhusiano tofauti na maliasili hiyo 0:10:28.000,0:10:30.000 au sehemu ile ambako mtoto wa kutoka Montana 0:10:30.000,0:10:33.000 amelelewa kuamini kwamba mlima ni mkusanyiko wa mawe 0:10:33.000,0:10:34.000 yanayosubiri kuchimbuliwa. 0:10:34.000,0:10:38.000 Ama ni makao ya mizimu au malundo ya madini si jambo muhimu. 0:10:38.000,0:10:41.000 Kinachosisimua ni nadharia inayo ainisha uhusiano huo 0:10:41.000,0:10:43.000 kati ya mtu na ulimwengu asilia 0:10:43.000,0:10:45.000 Nilikulia katika misitu ya British Columbia 0:10:45.000,0:10:47.000 na kuamini kwamba misitu hiyo ipo kwa ajili ya kukatwa, 0:10:47.000,0:10:49.000 Hiyo imenifanya kuwa mtu tofauti 0:10:49.000,0:10:51.000 sana na rafiki zangu miongoni mwa Kwakiutl 0:10:51.000,0:10:53.000 ambao wanaamini kwamba misitu ni makao ya Hukuk 0:10:53.000,0:10:54.000 na lango la peponi 0:10:54.000,0:10:57.000 na mizimu mumiani iishiyo miisho ya kaskazini mwa ulimwengu, 0:10:57.000,0:11:01.000 mizimu wanayokumbana nayo wakati wa simiko la Hamatsa 0:11:01.000,0:11:03.000 Na sasa, ukianza kuzingatia wazo 0:11:03.000,0:11:05.000 kwamba tamaduni hizi zinaweza kujenga mitazamo tofauti 0:11:05.000,0:11:06.000 waweza kuanza kuelewa 0:11:06.000,0:11:11.000 baadhi ya uvumbuzi wao wa ajabu. Chukulia mfano mmea huu hapa, 0:11:11.000,0:11:13.000 Ni picha niliyoipiga Kaskazini mwa Amazoni mwezi Aprili 0:11:13.000,0:11:16.000 Hii ni ayahuasca, wengi wenu mmekwisha sikia habari zake, 0:11:16.000,0:11:19.000 moja kati ya michanyato mikali kabisa ya kuzingulia 0:11:19.000,0:11:21.000 kati ya vifaa vyote vya mashamani 0:11:21.000,0:11:23.000 kinachoifanya ayahuasca kuwa ya kushangaza zaidi 0:11:23.000,0:11:27.000 si kiwango cha hali ya juu cha dawa inayotengenezwa 0:11:27.000,0:11:31.000 bali maudhui yake. Inatengenezwa kutokana na vitu viwili 0:11:31.000,0:11:33.000 Kwa upande mmoja ni mti wa liana 0:11:33.000,0:11:35.000 ambao ni jamii ya beta-carbolines 0:11:35.000,0:11:38.000 harmine, harmoline, ambayo ni nishai 0:11:38.000,0:11:40.000 Kuinywa peke yake 0:11:40.000,0:11:42.000 ni afadhali uvute moshi mzito wa bluu 0:11:42.000,0:11:44.000 unaingia kwenye ufahamu wako 0:11:44.000,0:11:47.000 ambao umechanganywa na majani ya jamii ya kahawa 0:11:47.000,0:11:49.000 yaitwayo Psychotria viridis. 0:11:49.000,0:11:52.000 Mmea huu una tindikali za tryptamines, 0:11:52.000,0:11:56.000 inafanana sana na kisisimuzi cha mfumo wa ufahamu cha dimethyltryptamine-5, 0:11:56.000,0:11:57.000 methoxydimethyltryptamine.[br] 0:11:57.000,0:11:59.000 Iwapo ungaliwaona Mayonami 0:11:59.000,0:12:01.000 wakiingiza vitu kwenye pua zao, 0:12:01.000,0:12:04.000 mchanyato wanaoutengeneza kwa mimea mbalimbali 0:12:04.000,0:12:08.000 ambayo pia ina methoxydimethyltryptamine. 0:12:08.000,0:12:10.000 Kuingiza unga huo kwenye pua yako 0:12:10.000,0:12:14.000 ni kama vile kuzibuliwa kama risasi toka kwenye bomba la bunduki 0:12:14.000,0:12:21.000 lililosakafiwa kwa michoro ya baroque na ukatua kwenye bahari ya umeme, (Kicheko) 0:12:21.000,0:12:23.000 Haifanyi upotoshaji wa hali halisi; 0:12:23.000,0:12:24.000 inayeyusha ufahamu wa hali halisi. 0:12:24.000,0:12:27.000 Kwa kweli, nilikuwa nabishana na mwalimu wangu Profesa Richard Evan Shultes -- 0:12:27.000,0:12:29.000 mtu ambaye alianzisha zama za uchunguzi wa madawa yanayobadili ufahamu 0:12:29.000,0:12:31.000 kwa uvumbuzi wake wa uyoga wa ajabu 0:12:31.000,0:12:33.000 nchini Mexico mnamo miaka ya 1930. 0:12:33.000,0:12:35.000 Nilikuwa nabisha kwamba huwezi kuainisha tryptamines hizi 0:12:35.000,0:12:38.000 kama vilevinishai kwakuwa wakati umezinguliwa nazo 0:12:38.000,0:12:42.000 hatokuwepo mtu mwingine akisubiri kushuhudia muweweseko wake. (Kicheko) 0:12:42.000,0:12:45.000 Lakini kuhusu tryptamines haziwezi kunywewa 0:12:45.000,0:12:47.000 kwakuwa zimeathiriwa na kimeng'enya 0:12:47.000,0:12:50.000 vinavyopatikana kiasilia katika utumbo wa binadamu na huitwa monoamine oxidase 0:12:50.000,0:12:53.000 Vinaweza kunywewa tu iwapo vitachanganywa na 0:12:53.000,0:12:56.000 kemikali nyinginezo zinazoweza kuathiri vimeng'enya vya MAO 0:12:56.000,0:12:57.000 Na sasa, vitu vya kushangaza 0:12:57.000,0:13:01.000 ni hizo beta-carbolines zinazopatikana kwenye liana 0:13:01.000,0:13:04.000 ni vidhibiti vya MAO kwa namna fulani muhimu 0:13:05.000,0:13:08.000 kuizimua tryptamine. Na hapo unajiuliza swali 0:13:08.000,0:13:12.000 Ilikuwaje kwenye mimea mbalimbali zaidi ya 80,000, 0:13:12.000,0:13:16.000 watu hawa walichagua hii miwili ambayo haifanani maumbile 0:13:16.000,0:13:17.000 lakini ambayo ikichanganywa kwa namna hii, 0:13:17.000,0:13:19.000 inatengeneza mchanganyiko wa kemikali 0:13:19.000,0:13:21.000 kamilifu ambayo ni zaidi ya jumla ya kila kimojawapo? 0:13:21.000,0:13:24.000 Vema, tunatumia maneno rahisi, kwamba walikuwa wakijaribu kubahatisha, 0:13:24.000,0:13:25.000 jambo ambalo halina ukweli wowote. 0:13:26.000,0:13:29.000 Lakini ukiwauliza Wahindi watakwambia, "Mimea inaongea nasi." 0:13:29.000,0:13:30.000 Vema, hiyo ina maana gani? 0:13:30.000,0:13:34.000 Kabila hili la Cofan wana aina 17 za ayahuasca, 0:13:34.000,0:13:37.000 na wanaweza kuitofautisha kutoka mbali huko msituni, 0:13:38.000,0:13:42.000 na zote hizi kwetu sisi zinaonekana kuwa sawa. 0:13:42.000,0:13:44.000 Halafu unawauliza waliwezaje kuziainisha 0:13:44.000,0:13:47.000 na wanasema " Nilidhani unajua masuala ya mimea, 0:13:47.000,0:13:49.000 nina maana, hujui chochote?" Na nikasema "Hapana." 0:13:49.000,0:13:52.000 Naam, inakuwa kwamba unachukua moja ya kila hizo aina 17 0:13:52.000,0:13:55.000 usiku wa mbalamwezi na zinakuimbia kwa mlio tofauti 0:13:55.000,0:13:57.000 Sasa, hiyo haiwezi kukupatia Ph.D. ya Harvard, 0:13:57.000,0:14:01.000 lakini hii inavutia zaidi ya kuhesabu chavua. 0:14:01.000,0:14:02.000 Na sasa, 0:14:02.000,0:14:05.000 (Makofi)[br] 0:14:05.000,0:14:07.000 na tatizo -- na tatizo ni kwamba hata sisi 0:14:07.000,0:14:09.000 tunaotetea hatima ya wazawa asilia 0:14:09.000,0:14:10.000 tunawaona kama wanavutia 0:14:10.000,0:14:12.000 lakini wamebanwa na mipaka ya historia 0:14:12.000,0:14:15.000 wakati ulimwengu halisi, yaani ulimwengu wetu, unasonga mbele. 0:14:15.000,0:14:17.000 Vema, ukweli ni kwamba karne ya 20, miaka 300 kuanzia sasa, 0:14:17.000,0:14:20.000 haitakumbukwa kwa vita vyake 0:14:20.000,0:14:21.000 au uvumbuzi wa kiteknolojia 0:14:21.000,0:14:23.000 bali ni zama ambazo tulikaa 0:14:24.000,0:14:26.000 na kuunga mkono waziwazi au tu kukubali 0:14:26.000,0:14:29.000 uharibifu mkubwa wa urithi mkubwa wa kibaiolojia au kiutamaduni 0:14:29.000,0:14:32.000 duniani. Kwa sasa, tatizo si mabadiliko. 0:14:32.000,0:14:34.000 Tamaduni zote wakati wote 0:14:34.000,0:14:37.000 zimejihusisha na mchezo 0:14:37.000,0:14:38.000 wa masuala mapya ya kimaisha. 0:14:39.000,0:14:41.000 Na tatizo si teknolojia peke yake. 0:14:42.000,0:14:44.000 Wahindi Wekundu Sioux hawajaacha kuwa Sioux 0:14:44.000,0:14:45.000 walipoacha upinde na mshale 0:14:45.000,0:14:47.000 kama vile ambavyo Mmarekani kuacha kuwa Mmarekani 0:14:47.000,0:14:49.000 alipoacha farasi na mkokoteni wake 0:14:49.000,0:14:50.000 Si mabadiliko ya teknolojia 0:14:50.000,0:14:54.000 yanayotishia uhai wa ethnosifia. Ni ubabe. 0:14:54.000,0:14:56.000 Sura katili ya miliki. 0:14:56.000,0:14:58.000 Na chochote unachokiangalia duniani, 0:14:58.000,0:15:01.000 utaona kwamba hizi si tamaduni tu zinazopotea. 0:15:01.000,0:15:03.000 Hawa ni watu halisi wanaoishi 0:15:03.000,0:15:06.000 wakiondolewa uhai kwa nguvu zinazojulikana 0:15:06.000,0:15:08.000 lakini ziko nje ya uwezo wao kuzimudu. 0:15:08.000,0:15:10.000 Iwapo ni uharibifu mbaya wa misitu 0:15:11.000,0:15:13.000 kwenye nchi ya Wapenani -- 0:15:13.000,0:15:16.000 watu waishio kwa kuhamahama huko Asia ya Kusinimashariki, kutoka Sarawak -- 0:15:16.000,0:15:20.000 watu walioshi huru mwituni mpaka kizazi kimoja kilichopita, 0:15:20.000,0:15:23.000 na sasa wote wamezuiliwa na kutumikishwa 0:15:23.000,0:15:25.000 kwenye kingo za mito, 0:15:25.000,0:15:29.000 ambako utaona mito yenyewe imechafuliwa kwa tope 0:15:29.000,0:15:31.000 yanayoonekana kubeba takriban nusu ya ukubwa wa kisiwa cha Borneo 0:15:31.000,0:15:32.000 kwenda Bahari ya China ya Kusini, 0:15:32.000,0:15:34.000 ambako meli za Kijapani zinasubiri 0:15:34.000,0:15:38.000 tayari kubeba magogo mabichi yaliyozolewa toka misituni. 0:15:38.000,0:15:39.000 Au suala la Wayanomami, 0:15:39.000,0:15:41.000 ni ugonjwa ambao umeingia, 0:15:41.000,0:15:43.000 wakati wa uvumbuzi wa dhahabu. 0:15:43.000,0:15:45.000 Au tukienda kwenye milima ya Tibet, 0:15:45.000,0:15:47.000 ambako ninafanya utafiti mwingi kwa sasa, 0:15:48.000,0:15:51.000 utaona sura ya kutisha ya ubeberu wa kisiasa. 0:15:51.000,0:15:53.000 Kama ujuavyo, mauaji ya halaiki, kumaliza maisha ya watu 0:15:53.000,0:15:55.000 kunalaaniwa ulimwenguni kote, lakini mauaji ya kiutamaduni, 0:15:56.000,0:15:59.000 uharibifu wa utaratibu wa maisha ya watu, siyo tu kwamba unalaaniwa, 0:15:59.000,0:16:02.000 unashangiliwa -- na makundi mengi 0:16:02.000,0:16:04.000 kuwa kama mkakati wa maendeleo. 0:16:04.000,0:16:07.000 Na huwezi kuelewa uchungu wa Tibet 0:16:07.000,0:16:09.000 mpaka usafiri kwa barabara. 0:16:09.000,0:16:13.000 Niliwahi kusafiri maili 6,000 kutoka Chengdu huko Magharibi mwa China 0:16:13.000,0:16:16.000 kwa barabara kupitia kusinimashariki Tibet mpaka Lhasa 0:16:16.000,0:16:20.000 nikiwa na mwenzi ambaye ni kijana, na mpaka nilipofika Lhasa 0:16:20.000,0:16:23.000 ndipo nikaelewa ukweli kuhusu takwimu 0:16:23.000,0:16:24.000 unazozisikia. 0:16:24.000,0:16:28.000 majengo matakatifu takriban 6,000 yamebomolewa kuwa vumbi na majivu. 0:16:28.000,0:16:31.000 watu milioni 1.2 wameuawa na makada 0:16:31.000,0:16:32.000 wakati wa Mapinduzi ya Utamaduni 0:16:33.000,0:16:35.000 Baba wa kijana huyu alitawazwa kuwa naibu wa Lama. 0:16:35.000,0:16:37.000 Kwa sababu hiyo aliuawa mara tu 0:16:37.000,0:16:39.000 ya uvamizi wa China. 0:16:39.000,0:16:41.000 Mjomba wake alitoroka pamoja na mhashamu kwenda uhamishoni 0:16:41.000,0:16:44.000 nchini Nepal 0:16:44.000,0:16:46.000 Mama yake alifungwa kwa sababu tu -- 0:16:46.000,0:16:48.000 alikuwa tajiri. 0:16:49.000,0:16:51.000 Yeye alipenyezwa kwa siri kuingizwa jela akiwa na umri wa miaka miwili 0:16:51.000,0:16:53.000 kujificha kwenye sketi za mamaake 0:16:53.000,0:16:55.000 kwakuwa hakuweza kustahimili kuishi bila mwanae. 0:16:55.000,0:16:57.000 Dada yake aliyefanya kitendo hicho cha kishujaa 0:16:57.000,0:16:58.000 alipelekwa kwenye kambi ya elimu 0:16:58.000,0:17:00.000 Siku moja kwa bahati mbaya alikumbana na kundi la askari 0:17:01.000,0:17:03.000 wa Mao, na kwa kosa hilo, 0:17:03.000,0:17:06.000 akahukumiwa kifungo cha miaka saba na kazi ngumu. 0:17:06.000,0:17:09.000 Machungu ya Tibet hayavumiliki, 0:17:09.000,0:17:12.000 lakini ujasiri wa watu hawa ni kitu cha kusisimua. 0:17:13.000,0:17:16.000 Na mwisho wake, inakuja mwisho kwenye uchaguzi, 0:17:16.000,0:17:19.000 Tunataka kuishi kwenye ulimwengu unaochosha wa utamaduni mmoja 0:17:19.000,0:17:22.000 au tunapenda kuwa na mtandao wa tamaduni mbalimbali? 0:17:22.000,0:17:25.000 Margaret Mead, mtaalam maarufu wa mambo ya kale, kabla ya kifo chake alisema 0:17:25.000,0:17:28.000 wasiwasi wake mkubwa ni kwamba tunazidi kuelekea kwenye 0:17:28.000,0:17:30.000 hii hali ya mtazamo mmoja wa kilimwengu 0:17:30.000,0:17:35.000 si tu kwamba tutaona uwezo mkubwa wa ufahamu wa binadamu 0:17:35.000,0:17:39.000 ukipunguzwa kuwa mawazo finyu, 0:17:39.000,0:17:40.000 bali tutazinduka siku moja 0:17:40.000,0:17:43.000 tukiwa tumesahau kwamba kuna uwezekano tofauti wa mambo. 0:17:44.000,0:17:47.000 Na ni taadhima kubwa kukumbuka kwamba kizazi chetu kimekuwepo kwa 0:17:47.000,0:17:49.000 takriban miaka 600,000 0:17:49.000,0:17:52.000 Mapinduzi ya Kilimo -- yaliyoanzisha ukulima, 0:17:52.000,0:17:54.000 tulipo salim amri kwenye imani ya mbegu 0:17:54.000,0:17:56.000 ushairi wa shaman ulisambaratishwa 0:17:56.000,0:17:57.000 kwa maandiko ya ukuhani 0:17:57.000,0:18:00.000 tukajenga daraja za umiliki ziada -- 0:18:00.000,0:18:02.000 ni miaka 10,000 iliyopita tu. 0:18:02.000,0:18:04.000 Maendeleo ya viwanda kama tuyajuavyo 0:18:04.000,0:18:06.000 yana si zaidi ya miaka 300. 0:18:06.000,0:18:08.000 Na sasa, historia hiyo ya juu juu hainishawishi 0:18:08.000,0:18:11.000 kwamba tuna majibu ya matatizo yetu yote 0:18:11.000,0:18:13.000 yatakayo tufariji katika hatima ya milenia 0:18:13.000,0:18:15.000 Wakati hizi tamaduni mbalimbali ulimwenguni 0:18:15.000,0:18:18.000 zikiulizwa maana ya kuwa binadamu, 0:18:18.000,0:18:20.000 zitakujibu kwa sauti 10,000 tofauti. 0:18:20.000,0:18:26.000 Na kwa kupitia wimbo huo ndipo tutatambua uwezekano 0:18:26.000,0:18:29.000 wa kuona kwamba sisi ni viumbe wenye ufahamu, 0:18:29.000,0:18:32.000 kufahamu fika kuhakikisha watu wote na bustani zote 0:18:32.000,0:18:38.000 zinapata namna ya kustawi. Na kuna vipindi vya matumaini. 0:18:38.000,0:18:41.000 Hii ni picha niliyoipiga kwenye ncha ya kaskazini mwa kisiwa cha Baffin 0:18:41.000,0:18:43.000 nilipokwenda kuwinda nyangumi wenye pembe nikiwa na Wainuiti, 0:18:44.000,0:18:47.000 na mtu huyu, Olaya, alinisimulia hadithi ya ajabu kuhusu babu yake. 0:18:48.000,0:18:50.000 Serikali ya Canada haikuwa ikiwatendea haki 0:18:50.000,0:18:52.000 Wainuiti, katika miaka ya 1950, 0:18:52.000,0:18:55.000 ili kujenga utaifa, tuliwahamishia kwenye vijiji. 0:18:55.000,0:18:59.000 Babu yake alikataa kwenda. 0:18:59.000,0:19:03.000 Nduguze, kwa kuhofia maisha yake, wakampokonya silaha zake zote, 0:19:03.000,0:19:04.000 na vifaa vyake vyote. 0:19:05.000,0:19:07.000 Na sasa, uelewe kwamba Wainuiti hawakuogopa baridi; 0:19:07.000,0:19:08.000 walijinufaisha nayo. 0:19:08.000,0:19:11.000 Mikokoteni ya kuteleza kwenye barafu ilitengenezwa kwa samaki 0:19:11.000,0:19:12.000 na kufunikwa kwa ngozi ya swala. 0:19:12.000,0:19:17.000 Kwahiyo babu yake mtu huyu hakutishika na usiku wa huko Aktika 0:19:17.000,0:19:19.000 au upepo mkali ulokuwa ukipuliza 0:19:19.000,0:19:22.000 Alitoka nje, akavua suruali yake 0:19:23.000,0:19:26.000 na kunyea mkononi. Na kinyesi kilipoanza kuganda, 0:19:26.000,0:19:29.000 akafinyanga katika umbile la upanga. 0:19:29.000,0:19:31.000 Akatemea mate kwenye upande wa makali ya upanga huo wa kinyesi 0:19:31.000,0:19:34.000 na baadae inaganda na kuwa ngumu, na aliitumia kumuua mbwa. 0:19:34.000,0:19:37.000 Akamchuna mbwa na kuboresha silaha yake, 0:19:37.000,0:19:40.000 akachukua ubavu wa mbwa na kutengeneza mkokoteni wa kuteleza, 0:19:41.000,0:19:42.000 akamfunga mbwa wa pili, 0:19:42.000,0:19:46.000 na kutokomea kwenye uwanda wa barafu, kisu cha kinyesi kibindoni. 0:19:46.000,0:19:50.000 Halafu unazungumzia kujikwamua bila kitu chochote (Kicheko) 0:19:50.000,0:19:51.000 Na hii, kwa namna mbalimbali, 0:19:51.000,0:19:53.000 (Makofi) 0:19:53.000,0:19:55.000 hii ni ishara ya ujasiri wa Wainuiti 0:19:55.000,0:19:58.000 na wazawa wote asilia ulimwenguni kote. 0:19:58.000,0:20:00.000 Serikali ya Canada mnamo Aprili 1999 0:20:00.000,0:20:03.000 waliwarudishia mamlaka Wainuiti 0:20:03.000,0:20:06.000 kwenye eneo kubwa kuliko California na Texas yakiunganishwa pamoja. 0:20:06.000,0:20:08.000 Ni nchi yetu mpya. Inaitwa Nunavut. 0:20:09.000,0:20:12.000 Ni jimbo linalojitegemea. Wanasimamia maliasili zote za madini. 0:20:12.000,0:20:14.000 Ni mfano wa ajabu jinsi ambavyo taifa 0:20:14.000,0:20:18.000 linafikia -- au kutafuta muafaka na watu wake. 0:20:19.000,0:20:22.000 Na mwisho, hatimaye, naona ni wazi kabisa 0:20:22.000,0:20:23.000 walau wengi wetu tulosafiri 0:20:23.000,0:20:25.000 kwenye sehemu hizi za mbali kwenye dunia, 0:20:27.000,0:20:28.000 tumegundua si mbali tena. 0:20:28.000,0:20:30.000 Ni makazi ya mtu fulani. 0:20:30.000,0:20:32.000 Yanaonyesha matawi ya mawazo ya binadamu 0:20:32.000,0:20:36.000 kwamba nenda nyuma kwenye mwanzo wa nyakati. Na kwetu sote, 0:20:36.000,0:20:39.000 ndoto za watoto hawa, kama vile ndoto za watoto wetu wenyewe, 0:20:39.000,0:20:42.000 zimekuwa sehemu ya jiografia ya matumaini. 0:20:42.000,0:20:46.000 Kwahiyo, tunachojaribu kufanya National Geographic hatimaye, 0:20:46.000,0:20:50.000 ni, tunaamini kwamba wanasiasa hawafanikishi lolote. 0:20:50.000,0:20:51.000 Huo ni ukosoaji wa hoja -- 0:20:51.000,0:20:53.000 (Makofi)[br] 0:20:53.000,0:20:55.000 tunadhani kwamba wakosoaji hawana ushawishi, 0:20:55.000,0:20:58.000 lakini tunaamini kwamba kuhadithia kutaibadili dunia, 0:20:58.000,0:21:01.000 na kwahiyo sisi ni miongoni mwa taasisi bora zaidi za masimulizi 0:21:01.000,0:21:04.000 duniani. Tunapata watembezi milioni 35 kwenye tovuti yetu kila mwezi. 0:21:04.000,0:21:07.000 Nchi 156 zinarusha matangazo ya televisheni yetu. 0:21:08.000,0:21:10.000 Majarida yetu yanasomwa na mamilioni. 0:21:10.000,0:21:13.000 Na tunachokifanya ni safari nyingi 0:21:13.000,0:21:15.000 kwenda kwenye ethnosifia ambako tunawapeleka watazamaji wetu 0:21:15.000,0:21:17.000 kwenye sehemu ambako kuna maajabu ya kiutamaduni 0:21:18.000,0:21:20.000 ambayo hawatoweza kuvumilia bali kushangazwa 0:21:20.000,0:21:22.000 na wanachokiona, na natumaini, kwahiyo, 0:21:22.000,0:21:25.000 kukubali taratibu, mmoja mmoja, 0:21:25.000,0:21:27.000 kiini cha uvumbuzi wa elimu ya mambo ya kale: 0:21:27.000,0:21:31.000 kwamba ulimwengu unastahili kuwepo kwa namna mbalimbali 0:21:31.000,0:21:32.000 na kwamba tunaweza kupata namna ya kuishi 0:21:32.000,0:21:35.000 katika ulimwengu wa tamaduni tofauti 0:21:35.000,0:21:37.000 ambako busara zote za watu 0:21:37.000,0:21:40.000 zitachangia ustawi wetu sote 0:21:40.000,0:21:41.000 Asante sana. 0:21:41.000,0:21:43.000 (Makofi)