Ramsey Musallam: Sheria 3 za kuamsha kujifunza
-
0:01 - 0:03Ninafundisha somo la kemia
-
0:03 - 0:04(Mlipuko)
-
0:04 - 0:08Sawa,Sawa.
-
0:08 - 0:10Ni zaidi ya milipuko,
-
0:10 - 0:11Kemia ipo kila mahali.
-
0:11 - 0:14Umeshawahi kuwa katika mgahawa
-
0:14 - 0:16ukiwa unajaribu kufanya hivi?
-
0:16 - 0:19Baadhi ya watu wanaitikia ndio.
-
0:19 - 0:21Hivi karibuni, niliwaonyesha wanafunzi wangu,
-
0:21 - 0:25niliwaambia waelezee kwa nini imetokea.
-
0:25 - 0:28Maswali na mazungumzo yaliyofuata
-
0:28 - 0:30yalikuwa ya kusisimua.
-
0:30 - 0:31angalia video hii ambayo Maddie
-
0:31 - 0:35kutoka darasa langu la tatu aliyonitumia jioni.
-
0:45 - 0:48(Vicheko)
-
0:48 - 0:51Ni dhahiri,kama mwalimu wa kemia wa Maddie
-
0:51 - 0:54Nilifurahi kwamba alienda nyumbani na kuendelea
-
0:54 - 0:56na zoezi hili la ajabu
-
0:56 - 0:58ambalo tulilifanya darasani.
-
0:58 - 1:01Lakini kilichonisisimua zaidi ilikuwa ni kuwa udadisi wa Maddie
-
1:01 - 1:03ulimpeleka kwenye hatua nyingine.
-
1:03 - 1:05ukiangalia ndani ya kikopo hiki,
-
1:05 - 1:06unaweza ukaona mshumaa.
-
1:06 - 1:09Maddie anatumia joto kuifanya hali hii
-
1:09 - 1:12kuwa tukio jingine jipya.
-
1:12 - 1:15Maswali na udadisi kama wa Maddie
-
1:15 - 1:18ndio sumaku zinazotuvuta kwa walimu wetu,
-
1:18 - 1:21na zinazidi teknolojia zote
-
1:21 - 1:24ubunifu mpya wa elimu.
-
1:24 - 1:28Lakini kama teknolojia kabla ya udadisi wa wanafunzi,
-
1:28 - 1:31tunaweza tukawa tunajinyima wenyewe
-
1:31 - 1:35zana muhimu kama walimu: maswali ya wanafunzi wetu.
-
1:35 - 1:40Kwa mfano,kupitia mhadhaa unaochosha
-
1:40 - 1:42kwa kutumia mtandao
-
1:42 - 1:43unaweza ukaokoa muda wa ufundishaji,
-
1:43 - 1:46lakini kama ni lengo la wanafunzi wetu.
-
1:46 - 1:49ni jambo lile lile la kudhalilisha
-
1:49 - 1:52ambalo limefungwa vizuri.
-
1:52 - 1:54Lakini kama tuna ujasiri
-
1:54 - 1:57wa kuwachanganya wanafunzi wetu,
-
1:57 - 1:59na kuamsha maswali ya kweli,
-
1:59 - 2:02ingawa maswali hayo sisi kama walimu yana taarifa
-
2:02 - 2:05ambazo tunaweza kuzitumia kwa ajili ya kutengeneza
-
2:05 - 2:09mfumo wa taarifa zilizochanganyika
-
2:09 - 2:14ukiondoa maneno ya karne ya 21 kuhusu hali hii,
-
2:14 - 2:18Ukweli ni kuwa nimefundisha sasa kwa miaka 13,
-
2:18 - 2:21na ilibidi kuwe na tukio la kutisha
-
2:21 - 2:24kunitoa katika miaka 10 ya ufundishaji wa mazoea
-
2:24 - 2:27na kunifanya nijue kuwa maswali ya wanafunzi
-
2:27 - 2:30ndio mbegu za kujifunza hasa,
-
2:30 - 2:33na sio mtaala ambao umeshaandaliwa
-
2:33 - 2:36ambao unawapa tu taarifa chache
-
2:36 - 2:39Mwezi Mei 2010,nikiwa na miaka 35,
-
2:39 - 2:42nikiwa na mtoto wa miaka 2 nyumbani na mtoto wa pili njiani
-
2:42 - 2:45niligundulika kuwa na kuongezeka kwa mishipa ya damu
-
2:45 - 2:48katika eneo la mshipa mkubwa wa damu wa aorta katika moyo
-
2:48 - 2:51ilisababisha nifanyiwe upasuaji wa moyo.Hii ni barua pepe
-
2:51 - 2:52kutoka kwa Daktari,pale.
-
2:52 - 2:56nilipoipata barua hii, nilikuwa
-
2:56 - 2:58nimechanganyikiwa kabisa?
-
2:58 - 3:02lakini nilipata mida ya faraja
-
3:02 - 3:06nikiwa na hakika aliyokuwa nayo daktari wangu.
-
3:06 - 3:09Alipata ujasiri huu?
-
3:09 - 3:13Kwa hiyo nilipomuuliza,akaniambia vitu vitatu.
-
3:13 - 3:16akasema kwanza,udadisi wake ulimsukuma
-
3:16 - 3:19kuuliza maswali magumu kuhusu upasuaji,
-
3:19 - 3:22kuhusu uzuri na ubaya wake.
-
3:22 - 3:25Pili,aliikubali,na hakuogopa,
-
3:25 - 3:27mchakato wa kujaribu jaribu,
-
3:27 - 3:30mchakato usiokwepeka wa kujarijaribu.
-
3:30 - 3:33na tatu,kupitia kutafakari sana,
-
3:33 - 3:35alikusanya taarifa alizohitaji
-
3:35 - 3:37kusanifu na kupitia upya mchakato,
-
3:37 - 3:41na kwa mkono wa taratibu,akaokoa maisha yangu.
-
3:41 - 3:44Nilichukua mengi kutoka maneno haya ya hekima,
-
3:44 - 3:46na kabla ya kwenda darasani majira ya kipupwe
-
3:46 - 3:50niliandika sheria tatu zangu mwenyewe
-
3:50 - 3:52ambazo nazitumia wakati napangillia masomo mpaka leo.
-
3:52 - 3:56Sheria ya kwanza: udadisi kwanza
-
3:56 - 3:59Maswali yanaweza kuwa dirisha la mazungumzo mazuri sana,
-
3:59 - 4:02lakini kinyume chake si sahihi
-
4:02 - 4:06Sheria ya pili: Kubaliana na hali ya fujo
-
4:06 - 4:08Sote ni walimu.Tunajua kujifunza ni vurugu tupu.
-
4:08 - 4:11na kwa sababu tu njia za kisayansi zimetengewa
-
4:11 - 4:15ukurasa wa tano wa kipengele 1.2 ya sura ya kwanza
-
4:15 - 4:18ambazo huwa tunaziruka,sawa,
-
4:18 - 4:21kujari jaribu bado kunaweza kuwa ni sehemu isiyo rasmi
-
4:21 - 4:23kwa vile tuvifanyavyo kila siku
-
4:23 - 4:27Katika kanisa la Moyo Mtakatifu ,chumba 206.
-
4:27 - 4:31Sheria namba tatu: Fanya zoezi la kutafakari.
-
4:31 - 4:33Tukifanyacho ni muhimu.inastahili kuangaliwa nasi,
-
4:33 - 4:36lakini instahili mapitio yetu.
-
4:36 - 4:39Je tunaweza kuwa madaktari wa madarasa yetu?
-
4:39 - 4:42Kama vile tuyafanyayosiku moja yataokoa maisha ya watu.
-
4:42 - 4:44Wanafunzi wetu,wanstahili kabisa.
-
4:44 - 4:46na kila hali ni tofauti.
-
4:46 - 4:47(Mlipuko)
-
4:47 - 4:49Sawa. Samahani
-
4:49 - 4:51Mwalimu wa Kemia ndani yangu alitaka kuta hicho
-
4:51 - 4:54nje yangu kabla hatujaendelea.
-
4:54 - 4:56Kwa hiyo hawa ni mabinti zangu.
-
4:56 - 4:59Kulia kwangu tuna Emmalou -- Familia ya kusini
-
4:59 - 5:02Na kushoto,Riley.
-
5:02 - 5:05Riley atakuwa binti mkubwa wiki chache zijazo.
-
5:05 - 5:06Atakuwa na miaka minne,
-
5:06 - 5:09na yeyote amjuaye mtoto wa miaka minne
-
5:09 - 5:12anajua kuwa wanapenda kuuliza "kwa nini"?
-
5:12 - 5:13Ndiyo. Kwa nini.
-
5:13 - 5:16Naweza kumfundisha mtoto huyo chochote
-
5:16 - 5:19kwa sababu ni mdadisi wa kila kitu.
-
5:19 - 5:21Sote tulikuwa hivyo katika umri huo.
-
5:21 - 5:24Lakini changamoto kubwa ni kwa walimu wa mbeleni wa Riley
-
5:24 - 5:27ambao bado hajakutana nao.
-
5:27 - 5:30Watawezaje kuukuza udadisi huu?
-
5:30 - 5:35Naweza nikasema kuwa Riley ni kama fumbo la watoto wote,
-
5:35 - 5:39Na nadhani kuacha shule kunakuja katika njia mbalimbali
-
5:39 - 5:42Kwa mwanafunzi wa mwaka wa mwisho, anayeacha shule kabla ya mwaka kwisha.
-
5:42 - 5:47au dawati tupu katika shule za sekondari za mijini.
-
5:47 - 5:50lakini,ikiwa sisi kama walimu tunaacha
-
5:50 - 5:52kazi nyepesi ya kusambaza taarifa
-
5:52 - 5:55na kukubaliana na dhana mpya
-
5:55 - 5:58ya wapandaji wa udadisi na uulizaji maswali,
-
5:58 - 6:00tunaweza kusababisha maana zaidi
-
6:00 - 6:03kuwepo kwao shuleni,na kuwasha cheche za tafakari.
-
6:03 - 6:04Asante sana.
-
6:04 - 6:10(Makofi).
- Title:
- Ramsey Musallam: Sheria 3 za kuamsha kujifunza
- Speaker:
- Ramsey Musallam
- Description:
-
Ilihitajika hali ya kutishia maisha kumtoa mwalimu wa kemia Ramsey Musallam kutoka miaka kumi ya ufundishaji wa mazoea kuelewa kazi halisi ya mkufunzi: kupandikiza udadisi. katika mazungumzo haya ya kufurahisha na ya binafsi,Musallam anatoa sheria tatu za kuamsha tafakari na kujifunza, na kuwafanya wanafunzi kuwa na shauku jinsi dunia inavyofanya kazi.
- Video Language:
- English
- Team:
- closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 06:29
Joachim Mangilima approved Swahili subtitles for 3 rules to spark learning | ||
Nelson Simfukwe accepted Swahili subtitles for 3 rules to spark learning | ||
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for 3 rules to spark learning | ||
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for 3 rules to spark learning | ||
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for 3 rules to spark learning | ||
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for 3 rules to spark learning | ||
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for 3 rules to spark learning | ||
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for 3 rules to spark learning |