Octoba 17- Nyumba ya Mwanaume Kipofu
-
0:15 - 0:19Mimi ni Leigh Rice, kiongozi wa wanafunzi wa utume wa Pasifiki ya kusini
-
0:19 - 0:22Nipo bandari ya Moresby leo na nimefurahi kuwa na Mchungaji Kove Tau
-
0:22 - 0:25kiongozi wa kanisa katika mji huu wenye watu laki 8.
-
0:28 - 0:32Kutambua usomaji wa Biblia ndiyo moyo wa kufanya wanafunzi wetu.
-
0:33 - 0:37Washiriki ukaribisha familia, marafiki, wafanyakazi wenzao, wanafunzi wenzao
-
0:37 - 0:39kuja pamoja kusoma Biblia.
-
0:42 - 0:45Tulimwomba kaka Peter kuja na kufanya mafunzo kwa ajili yetu
-
0:47 - 0:52Peter alitufundisha njia ya Yesu, iliyo rahisi
-
0:52 - 0:56mtu yoyote awezafanya, inajitambulisha,
-
0:56 - 0:57bila gharama.
-
1:00 - 1:04Tuliamua kubuni tena namna tunavyofanya utume katika makanisa yetu.
-
1:05 - 1:07Tunafuata mifano ya kitabu cha Matendo,
-
1:07 - 1:09jinsi kanisa la agano jipya lilivyokua.
-
1:10 - 1:12Tulibadilisha madarasa yetu ya Shule ya Sabato
-
1:12 - 1:15kuwa vikundi vya ugunduzi kusoma Biblia.
-
1:16 - 1:19Tulitengeneza madarasa yetu ya Shule ya Sabato
-
1:20 - 1:23kulingana na maeneo watu waishipo.
-
1:24 - 1:28Tulileta makanisa nyumbani mwao na zikawa makanisa.
-
1:33 - 1:34Jina langu ni Nathani
-
1:34 - 1:37Nilifurahia sana kuona njia hii
-
1:37 - 1:41ambapo twaweza shirikiana Neno la Mungu
-
1:43 - 1:45Nilisikia wazo hilo na kuamua
-
1:45 - 1:48kwamba natakiwa leta wazo hili nyumbani.
-
1:49 - 1:52Sasa, hapa ndipo tukutanapo kila Sabato.
-
1:56 - 2:02Tulipoanza ugunduzi wa usomaji Biblia familia na majirani
-
2:02 - 2:07ilikuwa na matokeo makubwa katika maisha yetu ya kiroho
-
2:08 - 2:13Familia na wanangu, vijana wote watatu
-
2:13 - 2:16waliweza kujadili Biblia wao wenyewe
-
2:16 - 2:18na tulifurahia hilo sana.
-
2:23 - 2:28Tukianzia Injili ya Marko, tukisoma kisa kimoja baada ya kingine
-
2:28 - 2:30na kuendelea na maombi pia.
-
2:30 - 2:32Mtu wa pili uisoma
-
2:32 - 2:35na kisha mwingine katika kikundi hukisema kisa kwa maneno yake mwenyewe
-
2:37 - 2:40Hii yote hujengwa katika maswali rahisi matano
-
2:40 - 2:41Nini ni kipya?
-
2:41 - 2:43Nini chakushangaza?
-
2:43 - 2:45Waelewa nini?
-
2:45 - 2:48Nini utatii au kufanya katika maisha yako?
-
2:48 - 2:50Na nini utamshirikisha mtu mwingine wiki hii?
-
2:51 - 2:52Baada ya majadiliano, tunaomba
-
2:52 - 2:54''Baba twakushukuru kwa kuwa nasi,
-
2:54 - 2:56Tafadhali tusaidie tunapomfuata Yesu wiki hii
-
2:58 - 3:01Nafanya kazi [ALAS] kampuni ya ujenzi
-
3:01 - 3:04kama msimamizi wa ujenzi.
-
3:04 - 3:07Baada ya kuendesha kikundi kile nyumbani
-
3:07 - 3:11Niliamua kuleta wazo lile kazini mwangu
-
3:12 - 3:16lilikuwa na mabadiliko sana kwa vijana wangu
-
3:21 - 3:25Namjua kipofu mmoja. Namwita ''Vinegar''
-
3:25 - 3:30Nilitambua anaishi kwenye nyumba ndogo ya muda
-
3:30 - 3:33Nikawa na wazo hili la kujenga nyumba
-
3:34 - 3:37Nilitaka kujadiliana hilo na vijana wangu.
-
3:37 - 3:42Walifurahia na kujitolea kuniunga mkono kunisaidia
-
3:43 - 3:46Naamini Yesu ni Mkombozi wangu.
-
3:46 - 3:48Namwamini.
-
3:48 - 3:51Siku moja atarudi na nitaondoka naye.
-
3:52 - 3:55Kila Sabato kuna batizo mbili au tatu
-
3:55 - 3:57kila kanisa.
-
3:57 - 3:59Kwa taarifa, robo hii,
-
3:59 - 4:02huu ulikuwa ubatizo mkubwa
-
4:02 - 4:05uliowahikutokea katika jimbo la kati la Papua
-
4:05 - 4:09Naona mwendelezo wa kielelezo vile tufanyavyo kanisani.
-
4:09 - 4:10Sababu makanisa sasa huona
-
4:10 - 4:14kwamba twapaswa kulileta kanisa pale jamii ilipo
-
4:26 - 4:28Mungu hutumia watu wa kawaida
-
4:28 - 4:31kubeba mipango Yake ya Kipekee.
- Title:
- Octoba 17- Nyumba ya Mwanaume Kipofu
- Description:
-
Kanisa huko Papua New Guinea laamua kutengeneza upya njia ya kufanya utume. Walifuata mfano wa kitabu cha Matendo, jinsi kanisa la agano jipya lilivyokua. Matokeo yalishangaza!
- Video Language:
- English
- Team:
- Team Adventist
- Project:
- Mission Spotlight DVD
- Duration:
- 04:35
Davlup edited Swahili subtitles for October 17 - A House for the Blind Man |