Mimi ni Leigh Rice, kiongozi wa wanafunzi wa utume wa Pasifiki ya kusini
Nipo bandari ya Moresby leo na nimefurahi kuwa na Mchungaji Kove Tau
kiongozi wa kanisa katika mji huu wenye watu laki 8.
Kutambua usomaji wa Biblia ndiyo moyo wa kufanya wanafunzi wetu.
Washiriki ukaribisha familia, marafiki, wafanyakazi wenzao, wanafunzi wenzao
kuja pamoja kusoma Biblia.
Tulimwomba kaka Peter kuja na kufanya mafunzo kwa ajili yetu
Peter alitufundisha njia ya Yesu, iliyo rahisi
mtu yoyote awezafanya, inajitambulisha,
bila gharama.
Tuliamua kubuni tena namna tunavyofanya utume katika makanisa yetu.
Tunafuata mifano ya kitabu cha Matendo,
jinsi kanisa la agano jipya lilivyokua.
Tulibadilisha madarasa yetu ya Shule ya Sabato
kuwa vikundi vya ugunduzi kusoma Biblia.
Tulitengeneza madarasa yetu ya Shule ya Sabato
kulingana na maeneo watu waishipo.
Tulileta makanisa nyumbani mwao na zikawa makanisa.
Jina langu ni Nathani
Nilifurahia sana kuona njia hii
ambapo twaweza shirikiana Neno la Mungu
Nilisikia wazo hilo na kuamua
kwamba natakiwa leta wazo hili nyumbani.
Sasa, hapa ndipo tukutanapo kila Sabato.
Tulipoanza ugunduzi wa usomaji Biblia familia na majirani
ilikuwa na matokeo makubwa katika maisha yetu ya kiroho
Familia na wanangu, vijana wote watatu
waliweza kujadili Biblia wao wenyewe
na tulifurahia hilo sana.
Tukianzia Injili ya Marko, tukisoma kisa kimoja baada ya kingine
na kuendelea na maombi pia.
Mtu wa pili uisoma
na kisha mwingine katika kikundi hukisema kisa kwa maneno yake mwenyewe
Hii yote hujengwa katika maswali rahisi matano
Nini ni kipya?
Nini chakushangaza?
Waelewa nini?
Nini utatii au kufanya katika maisha yako?
Na nini utamshirikisha mtu mwingine wiki hii?
Baada ya majadiliano, tunaomba
''Baba twakushukuru kwa kuwa nasi,
Tafadhali tusaidie tunapomfuata Yesu wiki hii
Nafanya kazi [ALAS] kampuni ya ujenzi
kama msimamizi wa ujenzi.
Baada ya kuendesha kikundi kile nyumbani
Niliamua kuleta wazo lile kazini mwangu
lilikuwa na mabadiliko sana kwa vijana wangu
Namjua kipofu mmoja. Namwita ''Vinegar''
Nilitambua anaishi kwenye nyumba ndogo ya muda
Nikawa na wazo hili la kujenga nyumba
Nilitaka kujadiliana hilo na vijana wangu.
Walifurahia na kujitolea kuniunga mkono kunisaidia
Naamini Yesu ni Mkombozi wangu.
Namwamini.
Siku moja atarudi na nitaondoka naye.
Kila Sabato kuna batizo mbili au tatu
kila kanisa.
Kwa taarifa, robo hii,
huu ulikuwa ubatizo mkubwa
uliowahikutokea katika jimbo la kati la Papua
Naona mwendelezo wa kielelezo vile tufanyavyo kanisani.
Sababu makanisa sasa huona
kwamba twapaswa kulileta kanisa pale jamii ilipo
Mungu hutumia watu wa kawaida
kubeba mipango Yake ya Kipekee.