Mimi ni Leigh Rice, kiongozi wa wanafunzi wa utume wa Pasifiki ya kusini Nipo bandari ya Moresby leo na nimefurahi kuwa na Mchungaji Kove Tau kiongozi wa kanisa katika mji huu wenye watu laki 8. Kutambua usomaji wa Biblia ndiyo moyo wa kufanya wanafunzi wetu. Washiriki ukaribisha familia, marafiki, wafanyakazi wenzao, wanafunzi wenzao kuja pamoja kusoma Biblia. Tulimwomba kaka Peter kuja na kufanya mafunzo kwa ajili yetu Peter alitufundisha njia ya Yesu, iliyo rahisi mtu yoyote awezafanya, inajitambulisha, bila gharama. Tuliamua kubuni tena namna tunavyofanya utume katika makanisa yetu. Tunafuata mifano ya kitabu cha Matendo, jinsi kanisa la agano jipya lilivyokua. Tulibadilisha madarasa yetu ya Shule ya Sabato kuwa vikundi vya ugunduzi kusoma Biblia. Tulitengeneza madarasa yetu ya Shule ya Sabato kulingana na maeneo watu waishipo. Tulileta makanisa nyumbani mwao na zikawa makanisa. Jina langu ni Nathani Nilifurahia sana kuona njia hii ambapo twaweza shirikiana Neno la Mungu Nilisikia wazo hilo na kuamua kwamba natakiwa leta wazo hili nyumbani. Sasa, hapa ndipo tukutanapo kila Sabato. Tulipoanza ugunduzi wa usomaji Biblia familia na majirani ilikuwa na matokeo makubwa katika maisha yetu ya kiroho Familia na wanangu, vijana wote watatu waliweza kujadili Biblia wao wenyewe na tulifurahia hilo sana. Tukianzia Injili ya Marko, tukisoma kisa kimoja baada ya kingine na kuendelea na maombi pia. Mtu wa pili uisoma na kisha mwingine katika kikundi hukisema kisa kwa maneno yake mwenyewe Hii yote hujengwa katika maswali rahisi matano Nini ni kipya? Nini chakushangaza? Waelewa nini? Nini utatii au kufanya katika maisha yako? Na nini utamshirikisha mtu mwingine wiki hii? Baada ya majadiliano, tunaomba ''Baba twakushukuru kwa kuwa nasi, Tafadhali tusaidie tunapomfuata Yesu wiki hii Nafanya kazi [ALAS] kampuni ya ujenzi kama msimamizi wa ujenzi. Baada ya kuendesha kikundi kile nyumbani Niliamua kuleta wazo lile kazini mwangu lilikuwa na mabadiliko sana kwa vijana wangu Namjua kipofu mmoja. Namwita ''Vinegar'' Nilitambua anaishi kwenye nyumba ndogo ya muda Nikawa na wazo hili la kujenga nyumba Nilitaka kujadiliana hilo na vijana wangu. Walifurahia na kujitolea kuniunga mkono kunisaidia Naamini Yesu ni Mkombozi wangu. Namwamini. Siku moja atarudi na nitaondoka naye. Kila Sabato kuna batizo mbili au tatu kila kanisa. Kwa taarifa, robo hii, huu ulikuwa ubatizo mkubwa uliowahikutokea katika jimbo la kati la Papua Naona mwendelezo wa kielelezo vile tufanyavyo kanisani. Sababu makanisa sasa huona kwamba twapaswa kulileta kanisa pale jamii ilipo Mungu hutumia watu wa kawaida kubeba mipango Yake ya Kipekee.