Ngozi Okonjo-Iweala anazungumzia kufanya biashara Afrika
-
0:05 - 0:08Asante sana Chris. Kila mtu aliyekuja hapa
-
0:08 - 0:12alisema kuwa anaogopa. Sijui kama na mimi ninaogopa,
-
0:12 - 0:16lakini hii ni mara yangu ya kwanza kuhutubia hadhara kama hii.
-
0:16 - 0:20Na sina teknolojia yeyote ya kisasa kwa ajili yenu ili muweze kuiangalia.
-
0:20 - 0:23Hakuna kielezopicha, kwa hiyo itabidi mnivumilie.
-
0:23 - 0:26(Kicheko).
-
0:26 - 0:32Ninachotaka kufanya asubuhi hii ni kuwasimulia hadithi kadhaa
-
0:32 - 0:35na kuongelea kuhusu Afrika iliyo tofauti.
-
0:35 - 0:39Tayari asubuhi hii kulikuwa na madokezo kuhusu Afrika
-
0:39 - 0:44unayoyasikia kila mara: Afrika ya VVU/UKIMWI,
-
0:44 - 0:50Afrika ya malaria, Afrika ya umaskini, Afrika ya migongano,
-
0:50 - 0:53na Afrika ya maafa.
-
0:53 - 0:57Ingawa kuna ukweli kwamba mambo hayo yanatokea,
-
0:57 - 1:01kuna Afrika ambayo hamuisikii sana.
-
1:01 - 1:05Na saa nyingine nashangazwa na kujiuliza kwanini.
-
1:05 - 1:09Hii ni Afrika ambayo inabadilika, ambayo Chris ameidokezea.
-
1:09 - 1:11Hii ni Afrika yenye fursa.
-
1:11 - 1:14Hii ni Afrika ambayo watu wanataka kuchukua hatua juu ya
-
1:14 - 1:16maisha na uwezo wao.
-
1:16 - 1:19Na hii ndio Afrika ambayo watu wanatafuta kuingia ubia
-
1:19 - 1:23kufanya hivyo. Na hili haswa ndilo ninalotaka kuzungumzia leo.
-
1:23 - 1:25Ningependa kuanza kwa kuwaambia
-
1:25 - 1:27habari kuhusu mabadiliko hayo Afrika.
-
1:28 - 1:33Mnamo 15 Septemba 2005, Bwana Diepreye Alamieyeseigha,
-
1:33 - 1:37Gavana wa jimbo moja lenye utajiri wa mafuta huko Nigeria,
-
1:37 - 1:44alikamatwa na Polisi wa mji wa London alipokuwa matembizini mjini London.
-
1:44 - 1:49Alikamatwa kwasababu kulikuwa na hamisho la kiasi cha dola za kimarekani milioni 8
-
1:49 - 1:52ambazo zilienda katika akaunti hewa
-
1:52 - 1:55ambazo alikuwa akizimiliki yeye pamoja na familia yake.
-
1:56 - 1:58Kukamatwa kwake kuliwezekana kwasababu kulikuwa na ushirikiano
-
1:58 - 2:01baina ya Polisi wa mji wa London
-
2:01 - 2:04na Tume ya Uhalifu wa Kiuchumi na Fedha ya Nigeria --
-
2:04 - 2:11inayoongozwa na mtu wenye uwezo na ujasiri: Bwana Nuhu Ribadu.
-
2:11 - 2:14Alamieyeseigha alikamatwa mjini London.
-
2:14 - 2:18Kutokana na udhaifu, alifanikiwa kutoroka akiwa amevalia kama mwanamke
-
2:18 - 2:21na kukimbia kutoka London kurudi Nigeria ambako,
-
2:21 - 2:25kwa mujibu wa katiba, wale walio madarakani
-
2:25 - 2:27kama magavana, rais – kama ilivyo kwenye nchi nyingi --
-
2:27 - 2:32wana kinga na hawawezi kushtakiwa. Lakini nini kilitokea:
-
2:32 - 2:36watu walikasirishwa sana na tabia hii na iliwezekana
-
2:36 - 2:42kwa sheria za jimbo lake kumvua madaraka.
-
2:43 - 2:45Leo, Alams – kama tumuitavyo kwa kifupi – yuko jela.
-
2:46 - 2:51Hii ni hadithi kuhusu ukweli kwamba watu wa Afrika
-
2:51 - 2:56hawako tayari tena kuvumilia rushwa kutoka kwa viongozi wao.
-
2:57 - 3:02Hii ni hadithi kuhusu ukweli kwamba watu wanataka rasilimali zao
-
3:02 - 3:07zidhibitiwe vizuri kwa manufaa yao, na sio kupelekwa sehemu
-
3:07 - 3:10ambako itawanufaisha mabwanyenye wachache.
-
3:10 - 3:14Kwa hiyo, unaposikia kuhusu Afrika ya rushwa --
-
3:14 - 3:18rushwa kila mara – Ninataka mfahamu kuwa watu
-
3:18 - 3:21na serikali wanajitahidi sana kupambana na tatizo hili
-
3:21 - 3:25katika baadhi ya nchi, na kwamba mafanikio yanaanza kuonekana.
-
3:25 - 3:28Inamaana kuwa tatizo limekwisha? Jibu ni hapana.
-
3:28 - 3:32Bado kuna safari ndefu, lakini pia kuna nia.
-
3:32 - 3:36Mafanikio yanaandikwa juu ya mapigano ya jambo hili muhimu.
-
3:36 - 3:38Kwa hiyo mnaposikia kuhusu rushwa,
-
3:38 - 3:41msifikiri kwamba hakuna linalotendeka kuhusu hili --
-
3:41 - 3:44na kwamba hamuwezi kufanya kazi katika nchi yeyote Afrika
-
3:44 - 3:47kwasababu ya rushwa. Hiyo si kweli.
-
3:47 - 3:53Kuna nia ya kupambana na rushwa, na katika nchi nyingi, mapambano hayo yanaendelea
-
3:53 - 3:57na mafanikio yanaonekana. Katika nchi nyingine, kama yangu,
-
3:57 - 4:00ambako kumekuwa na historia ndefu ya kidikteta nchini Nigeria,
-
4:00 - 4:04mapambano bado yanaendelea, na bado tuna safari ndefu.
-
4:04 - 4:08Ukweli wa mambo ni kwamba mapambano bado yanaendelea.
-
4:09 - 4:11Matokeo yanaonekana:
-
4:11 - 4:15tathmini huru ya Benki ya Dunia na mashirika mengine
-
4:15 - 4:19inaonyesha kuwa mwelekeo juu ya rushwa unapungua
-
4:19 - 4:22na utawala unarekebika.
-
4:22 - 4:26Utafiti uliofanywa na Tume ya Uchumi ya Afrika unaonyesha
-
4:26 - 4:30wazi mwelekeo mzuri wa utawala katika nchi 28 za Afrika.
-
4:30 - 4:32Ngoja niseme kitu kimoja zaidi
-
4:32 - 4:34kabla sijamaliza kuzungumzia kuhusu utawala bora.
-
4:34 - 4:37Na ni kitu ambacho watu wanazungumzia kuhusu rushwa, rushwa.
-
4:37 - 4:39Kila mara wanapo zungumzia kuhusu hili
-
4:39 - 4:41mara moja unafikiria Afrika.
-
4:41 - 4:45Hiyo ndio picha: Nchi za Afrika. Lakini ngoja niseme hili:
-
4:45 - 4:51iwapo Alams alifanikiwa kuhamisha dola za kimarekani milioni 8 kwenye akaunti mjini London --
-
4:53 - 4:57kama watu wengine waliochukukua pesa wakikadiria kuwa
-
4:57 - 5:01kati ya bilioni 20 na 40 za pesa za nchi zinazoendelea
-
5:01 - 5:04ziko nje ya nchi katika nchi zilizoendelea – kama wanaweza kufanyi hivi,
-
5:04 - 5:07hiyo ni nini? Hiyo siyo rushwa?
-
5:08 - 5:12Katika nchi hii, kama ukipokea vitu vya wizi, haushitakiwi?
-
5:13 - 5:16Kwa hiyo tukiongelea kuhusu aina hii ya rushwa, hebu pia tufikirie kuhusu
-
5:16 - 5:19nini kinatokea katika upande mwingine wa dunia --
-
5:19 - 5:23ambako pesa hizo zinakwenda na nini kifanyike ili kuweza kuzuia hili.
-
5:23 - 5:26Kuna jambo ninalifanyia kazi kwa sasa, pamoja na Benki ya Dunia,
-
5:26 - 5:29kuhusu kurudisha rasilimali, tunajaribu tuwezalo
-
5:29 - 5:32kurudisha pesa ambazo zimepelekwa nje ya nchi --
-
5:32 - 5:35pesa za nchi zinazoendelea -- ili ziweze kurudishwa.
-
5:35 - 5:38Kama tutaweza kurudisha dola bilioni 20 ambazo ziko nje,
-
5:38 - 5:41litakuwa jambo zuri sana kwa baadhi ya nchi hizi
-
5:41 - 5:44kuliko misaada yote ikiwekwa pamoja.
-
5:44 - 5:51(Makofi).
-
5:51 - 5:55Kitu cha pili ninachotaka kuzungumzia ni nia ya mageuzi.
-
5:55 - 5:59Afrika, baada – wamechoka, tumechoka
-
5:59 - 6:04kuwa kitovu cha misaada kutoka kwa kila mtu.
-
6:04 - 6:08Tunashukuru, ila tunajua kuwa
-
6:08 - 6:12tunaweza kuchukua hatua juu ya uwezo wetu na kama tuna nia ya kufanya mabadiliko.
-
6:13 - 6:17Na kinachotokea katika nchi nyingi za Afrika sasa ni utambuzi kwamba
-
6:17 - 6:21hakuna anayeweza kufanya lolote ila sisi wenyewe. Ni lazima tufanye.
-
6:21 - 6:25Tunaweza kuwakaribisha washirika ambao wanaweza kutuunga mkono, lakini lazima tuanze wenyewe.
-
6:25 - 6:28Ni lazima turekebishe uchumi wetu, tubadilishe uongozi,
-
6:28 - 6:34tuwe na demokrasia zaidi, tuwe wazi kupokea mabadiliko na taarifa.
-
6:34 - 6:36Na hiki ndicho tumeanza kukifanya
-
6:36 - 6:39katika mojawapo kati ya nchi kubwa kabisa katika bara, Nigeria.
-
6:39 - 6:42Hakika, kama hauko Nigeria, hauko Afrika.
-
6:42 - 6:43Ninataka kuwaambia kuwa.
-
6:43 - 6:44(Kicheko).
-
6:44 - 6:46Mmoja kati ya waafrika wanne walio kusini mwa jangwa la Sahara ni Mnigeria,
-
6:48 - 6:53na ina watu milioni 140 – watu wenye pilika --
-
6:54 - 6:58lakini watu wenye kuvutia. Hauwezi kuchoka.
-
6:58 - 6:59(Kicheko).
-
6:59 - 7:01Tulichoanza kufanya ni kujua kwamba
-
7:01 - 7:03tunaweza kuchukua hatua na kujibadili wenyewe.
-
7:04 - 7:06Na kwa msaada wa kiongozi
-
7:06 - 7:09ambaye alikuwa na nia, kwa wakati ule, ya kufanya mabadiliko,
-
7:09 - 7:11tunaandaa mpango madhubuti wa mabadiliko
-
7:11 - 7:13ambao tumeuandika wenyewe.
-
7:13 - 7:16Si Shirika la Kimataifa la Fedha. Wala Benki ya Dunia,
-
7:16 - 7:19ambako nilifanya kazi kwa miaka 21 na kufikia cheo cha makamu wa rais.
-
7:20 - 7:22Hakuna mtu anaweza kukufanyia. Inabidi ufanye mwenyewe.
-
7:22 - 7:26Tukaandaa mpango ambao kwanza, utafanya: kuiondoa serikali
-
7:26 - 7:30kwenye shughuli zisizo na manufaa -- zisizoihusu --
-
7:30 - 7:32Serikali haitakiwi kufanya biashara
-
7:32 - 7:33ya uzalishaji na utoaji huduma
-
7:33 - 7:36kwasababu haina ufanisi na haina ujuzi.
-
7:36 - 7:40Kwa hiyo tuliamua kubinafsisha mashirika yetu mengi.
-
7:40 - 7:44(Makofi).
-
7:45 - 7:49Sisi -- matokeo yake, tuliamua kuwa na soko huria.
-
7:49 - 7:52Unaweza kuamini kuwa kabla ya mabadiliko haya --
-
7:52 - 7:56ambayo yalianza mwishoni mwa mwaka 2003, wakati nilipoondoka Washington
-
7:56 - 7:58kwenda kushika nafasi ya Waziri wa Fedha --
-
8:00 - 8:04tulikuwa na kampuni ya simu ambayo iliweza kutoa huduma za simu za mezani
-
8:04 - 8:094,500 katika historia yake ya miaka 30?
-
8:09 - 8:11(Kicheko).
-
8:11 - 8:14Kuwa na simu katika nchi yangu lilikuwa ni jambo la kifahari sana.
-
8:14 - 8:16Usingeweza kupata. Ilibidi uhonge.
-
8:16 - 8:18Ilibidi ufanye kila uwezalo ili kupata simu.
-
8:18 - 8:21Rais Obasanjo aliunga mkono na kuzindua
-
8:21 - 8:25kulegezwa kwa masharti katika sekta ya mawasiliano
-
8:26 - 8:34tumepanda kutoka simu 4,500 za mezani kufikia simu milioni 32 zenye GSM, na zinaongezeka.
-
8:34 - 8:39Soko la mawasiliano la Nigeria ni la pili kwa ukuaji duniani kote,♪
-
8:39 - 8:44ikiwa imetanguliwa na China. Tunapata uwekezaji wa takriban dola bilioni 1 kwa mwaka
-
8:44 - 8:50katika mawasiliano. Na hakuna mtu anayejua, isipokuwa kwa wajanja wachache.
-
8:50 - 8:53(Kicheko).
-
8:53 - 8:57Wajanja wa kwanza kuja
-
8:57 - 8:59walikuwa ni kampuni ya MTN ya Afrika Kusini.
-
8:59 - 9:03Katika miaka mitatu niliyokuwa Waziri wa Fedha,
-
9:03 - 9:06wamepata wastani wa dola milioni 360 kwa mwaka.
-
9:08 - 9:14milioni 360 katika soko – katika nchi ambayo ni maskini,
-
9:14 - 9:18yenye wastani wa pato la taifa chini ya dola 500.
-
9:19 - 9:21Kwahiyo soko lipo hapo.
-
9:21 - 9:24Walilifanya hili siri, lakini baadae wengine nao walianza kujua.
-
9:25 - 9:28Wanageria wenyewe walianzisha
-
9:28 - 9:30makampuni ya mawasiliano ya simu zisizotumia waya
-
9:30 - 9:32na wengine kama watatu wane hivi wameingia.
-
9:32 - 9:35Lakini bado kuna soko kubwa sana,
-
9:35 - 9:38na watu hawajui kuhusu hili, au hawataki kujua.
-
9:40 - 9:42Kwa hiyo ubinafsishaji ni jambo mojawapo tulilofanya.
-
9:43 - 9:49Kitu kingine tulichofanya ni kusimamia vizuri masuala yetu ya fedha.
-
9:50 - 9:52Kwasababu hakuna atakayekusaidia na kukuongoza
-
9:53 - 9:56iwapo hudhibiti fedha zako vizuri.
-
9:56 - 10:00Na Nigeria, ikiwa na sekta ya mafuta, ilikuwa na sifa
-
10:00 - 10:05ya rushwa na kutosimamia vizuri masuala ya fedha za umma.
-
10:05 - 10:09Je tulijaribu kufanya nini? Tulianzisha sheria ya fedha
-
10:10 - 10:12ambayo ilitenganisha bajeti yetu na bei ya mafuta.
-
10:12 - 10:16Zamani tulikuwa tumezoea kubajeti kutokana na kipato ambacho tulikipata kutokana na mafuta,
-
10:16 - 10:21kwasababu mafuta ndiyo sekta kuu ya mapato
-
10:21 - 10:24katika uchumi: asilimia 70 ya mapato yetu yanatokana na mafuta.
-
10:24 - 10:28Tulitenganisha hilo, na tulipofanya hivyo tulianza kubajeti
-
10:28 - 10:31kwa bei ambayo ilikuwa chini kidogo ya bei ya mafuta
-
10:31 - 10:35na kuhifadhi chochote cha ziada juu ya bei hiyo.
-
10:36 - 10:39Hatukuweza kujua kama tungeweza kufanikisha, ilikuwa ni utata sana.®
-
10:39 - 10:42Lakini kitu ambacho kilitokea haraka ilikuwa ni mabadiliko
-
10:42 - 10:45ambayo yalikuwepo kwa maendeleo yetu ya uchumi --
-
10:45 - 10:49ambapo, hata kama bei ya mafuta ingekuwa juu, tungekuwa haraka sana.
-
10:49 - 10:51Wakati zilipoanguka, tulianguka.
-
10:51 - 10:55Na tulikuwa tunashindwa kulipia chochote, hata mishahara, katika uchumi.
-
10:56 - 11:00Hii ilisawazisha. Tuliweza kuweka akiba, kabla sijaondoka,
-
11:00 - 11:06dola bilioni 27. Ambapo – hii ilienda kwenye hazina yetu --
-
11:06 - 11:10wakati nilipofika mwaka 2003, tulikuwa na dola billion 7 kwenye akiba.
-
11:11 - 11:14Na wakati naondoka, tulikuwa na karibu dola bilioni 30. Na
-
11:14 - 11:17tunavyoongea sasa, tuna dola bilioni 40 kwenye akiba
-
11:18 - 11:22hii ni kutokana na usimamizi mzuri wa fedha zetu.
-
11:23 - 11:26Hii inasaidia kutuliza uchumi wetu, kuufanya uwe imara.
-
11:26 - 11:29Thamani ya fedha yetu ilikuwa ikibadilika kila mara
-
11:29 - 11:33kwa sasa ipo angalau imara na kusimamiwa, ili wafanyabiashara
-
11:33 - 11:38wawe na uhakika wa bei katika uchumi.
-
11:40 - 11:44Tuliweza kudhibiti mfumuko bei kutoka asilimia 28 mpaka karibu asilimia 11.
-
11:46 - 11:52Na pato letu la taifa liliongezeka kutoka wastani wa asilimia 2.3 kwa muongo uliopita
-
11:52 - 11:55mpaka kufikia asilimia 6.5 sasa.
-
11:56 - 11:59Kwa hiyo mabadiliko yote tuliyoweza kufanya
-
11:59 - 12:02yameweza kuonekana kwa vitendo ambavyo vinaweza kuonekana katika uchumi.
-
12:02 - 12:06Na kitu cha muhimu zaidi, ni kwasababu tunataka kuondokana na mafuta
-
12:06 - 12:08na kupanua wigo zaidi – na kuna fursa nyingi sana
-
12:08 - 12:11katika nchi hii kubwa, kama ilivyo katika nchi nyingine za Afrika --
-
12:13 - 12:16kilichotia fora zaidi ni huu ukuaji haukutoka
-
12:16 - 12:19kwenye sekta mafuta pekee, bali sekta nyingine pia.
-
12:19 - 12:22Kilimo kilikuwa kwa wastani wa asilimi 8.
-
12:22 - 12:26Sekta ya mawasiliano ilikuwa, makazi na ujenzi,
-
12:26 - 12:31na ninaweza kuendelea zaidi na zaidi. Na hii ni kuwaonyesha kwamba
-
12:31 - 12:33uchumi wako unaporekebishika,
-
12:33 - 12:37fursa katika sekta nyingine zipo nyingi.
-
12:38 - 12:41Tuna frusa katika kilimo, kama nilivyosema.
-
12:41 - 12:45Tuna fursa katika madini. Tuna madini mengi
-
12:45 - 12:48ambako hakuna mtu amewekeza katika utafutaji. Tumegundua
-
12:48 - 12:51kuwa bila kuwa na sera sahihi za kuwezesha,
-
12:51 - 12:54hilo halitawezekana. Sasa tuna sheria ya uchimbaji madini
-
12:54 - 12:57ambayo inalinganishwa na sheria nyingine bora duniani.
-
12:58 - 13:00Tuna fursa katika makazi na usimamizi wa majumba.
-
13:00 - 13:03Kulikuwa hakuna chochote katika nchi ya watu milioni 140 --
-
13:04 - 13:09hakuna maduka makubwa kama myajuavyo hapa.
-
13:10 - 13:13Hii inaweza kuwa fursa kwa mtu fulani
-
13:13 - 13:15ambayo ilitia chachu ya kufikiria kwa watu.
-
13:16 - 13:19Sasa tuna mazingira ambayo biashara katika maduka haya makubwa
-
13:19 - 13:22yanapata faida mara nne ya ilivyokadiriwa.
-
13:23 - 13:26Kwa hiyo mambo makubwa kwenye ujenzi, mali isiyohamishika,
-
13:26 - 13:28Masoko ya rehani. Huduma za fedha
-
13:29 - 13:33tulikuwa na Benki 89. Nyingi hazifanyi biashara iliyokusudiwa.
-
13:33 - 13:37Tulizizatiti kutoka 89 kufikia Benki 25 kwa
-
13:37 - 13:42waongeze mtaji wao -- gawio la mtaji.
-
13:42 - 13:47Ilikuwa kutoka dola milioni 25 mpaka dola milioni 150.
-
13:47 - 13:51Benki, Benki hizi sasa zimejizatiti na kuimarishwa
-
13:51 - 13:55mfumo wa Benki umevutia wamekezaji wengi kutoka nje.
-
13:55 - 13:59Benki ya Barclays kutoka Uingereza inaingiza milioni 500.
-
13:59 - 14:03Standard Chartered imeingiza milioni 140.
-
14:03 - 14:06Ninaweza kuendelea zaidi. Dola zaidi na zaidi, ndani ya mfumo.
-
14:06 - 14:08Tunafanya hivyo hivyo kwenye sekta ya bima.
-
14:08 - 14:11Kwa hiyo kwenye huduma za fedha, kuna fursa kubwa zaidi.
-
14:11 - 14:17Kwenye utalii, katika nchi nyingi za Kiafrika, ni fursa kubwa.
-
14:17 - 14:20Na hii ndiyo sababu kubwa ya kuwa watu wengi wanaifahamu Afrika Mashariki kwa:
-
14:21 - 14:24wanyama pori, tembo na kadhalika.
-
14:24 - 14:26Lakini kusimimamia soko la utalii ili
-
14:26 - 14:29liweze kuwanufaisha watu ni muhimu sana.
-
14:30 - 14:33Sasa ninachojaribu kusema ni nini? Najaribu kuwaambia
-
14:33 - 14:36kuna wimbi jipya katika bara.
-
14:36 - 14:41Wimbi la uwazi na demokrasia ambapo tangu mwaka 2000,
-
14:41 - 14:43zaidi ya theluthi mbili ya nchi za Afrika zimefanya
-
14:43 - 14:45uchaguzi wa kidemokrasia wa vyama vingi.
-
14:46 - 14:49Si zote zilikuwa kamilifu, au zitakuwa,
-
14:49 - 14:51lakini mwelekeo uko wazi.
-
14:51 - 14:55Ninajaribu kuwaelezea kwamba toka miaka mitatu iliyopita
-
14:55 - 14:58wastani wa ukuaji wa uchumi katika bara umeongezeka
-
14:58 - 15:02kutoka karibu asilimia 2.5 mpaka asilimia 5 kwa mwaka.
-
15:02 - 15:06Hii ni bora zaidi ya ufanisi wa nchi nyingi za OECD.
-
15:07 - 15:11Kwahiyo ni wazi kwamba mambo yanabadilika.
-
15:11 - 15:13Migogoro imepungua barani;
-
15:14 - 15:16kutoka migogoro 12 kwa muongo uliopita,
-
15:16 - 15:18kufikia migogoro mitatu au minne,
-
15:18 - 15:21Mojawapo ya migogoro mibaya zaidi, kwa hakika, ni ule wa Darfur.
-
15:21 - 15:24Na kama ujuavyo, kuna athari kwa majirani, iwapo
-
15:24 - 15:26kuna jambo linatokea upande mmoja wa bara,
-
15:26 - 15:29inaonekana kama bara zima limeathirika.
-
15:29 - 15:32Lakini ni vema muelewe kwamba hili bara --
-
15:32 - 15:38ni bara lenye nchi nyingi na si nchi moja.
-
15:38 - 15:40Na iwapo tuna migogoro mitatu minne hivi,
-
15:40 - 15:43ina maana kuwa kuna fursa nyingi za kuwekeza
-
15:43 - 15:50katika uchumi ulio imara, unaokua na wenye kusisimua
-
15:50 - 15:53ambako kuna fursa nyingi sana.
-
15:54 - 15:58Ningependa kutoa dokezo moja kuhusu uwekezaji huu.
-
15:59 - 16:01Namna nzuri ya kuisaidia Afrika sasa
-
16:02 - 16:05ni kuwasaidia waweze kusimama wenyewe.
-
16:05 - 16:09Na namna nzuri ya kufanya hivyo ni kusaidia kuleta ajira.
-
16:10 - 16:14Hakuna tatizo katika kupambana na malaria na kuwekeza pesa kwenye hilo
-
16:14 - 16:18na kuokoa maisha ya watoto. Sina maana hiyo. Hilo ni sawa.
-
16:19 - 16:23Lakini fikiria tofauti itakayokuwa kwenye familia: iwapo wazazi wanaweza kuwa na ajira
-
16:23 - 16:25na wakahakikisha watoto wao wanakwenda shule,
-
16:25 - 16:28kwamba wanaweza kununua dawa za kupambana na magonjwa wao wenyewe.
-
16:28 - 16:32Kama tunaweza kuwekeza kwenye maeneo ambayo nyinyi wenyewe mnapata faida
-
16:32 - 16:37wakati huo huo mkitengeneza ajira na kuwasaidia watu wasimame wenyewe,
-
16:37 - 16:42hii siyo fursa nzuri? Hii si ndiyo njia ya kufuata?
-
16:42 - 16:45Na nataka kusema jambo kuhusu watu bora zaidi wa kuwawekezea
-
16:45 - 16:47katika bara hili ni wanawake.
-
16:48 - 16:55(Makofi).
-
16:55 - 17:00Nina CD hapa. Samahani sikusema kwa wakati muafaka.
-
17:00 - 17:02Lakini, ningependa mngekuwa mmeiangalia.
-
17:02 - 17:05Inasema, "Afrika: Iko wazi kwa Biashara."
-
17:06 - 17:09Na video hii imeshinda tuzo
-
17:09 - 17:11kama makala bora ya mwaka.
-
17:11 - 17:13Elewa kwamba mwanamke aliyetengeneza makala hii
-
17:13 - 17:18atakuwa Tanzania, ambako watakuwa na kongamano mwezi Juni.
-
17:19 - 17:24Lakini hii inakuonyesha kwamba Waafrika, na hususani wanawake wa Afrika, ambao
-
17:24 - 17:29pamoja na matatizo yote wameweza kuanzisha biashara, nyingine ni za kiwango cha kimataifa.
-
17:29 - 17:32Mmoja kati ya wanawake katika video hii, Adenike Ogunlesi,
-
17:32 - 17:34anashona nguo za watoto
-
17:34 - 17:39kitu ambacho alianza kama kujifurahisha na ikakua na kuwa biashara.
-
17:39 - 17:42Akichanganya vitambaa vya Kiafrika ambavyo tunavyo,
-
17:43 - 17:44na vitambaa vingine kutoka sehemu nyingine.
-
17:44 - 17:49Na hivyo, atatengeneza suruali kwa kutumia vitambaa vizito,
-
17:49 - 17:53ikiwa imechanganywa na vitambaa vya kiafrika. Ni ubunifu mzuri sana.
-
17:55 - 17:58Amefikai hatua ambapo anapata zabuni kutoka Wal-Mart.
-
17:59 - 18:00(Kicheko).
-
18:01 - 18:03Kwa nguo 10,000
-
18:04 - 18:08Kwa hiyo hii inawaonyesha kuwa tuna watu wenye uwezo wa kufanya mambo.
-
18:08 - 18:13Wanawake wana juhudi, wako makini; wanachapa kazi.
-
18:13 - 18:15Naweza kuendelea kwa kutoa mifano:
-
18:15 - 18:19Beatrice Gakuba wa Rwanda, alifungua biashara ya maua
-
18:19 - 18:24na sasa anayasafirisha kwenye mnada wa udachi huko Amsterdam kila asubuhi,
-
18:24 - 18:28na ameajiri wanawake na wanaume takriban 200 kumsaidia kazi.
-
18:29 - 18:33Hata hivyo, wengi wao, wana kiu ya kupata mtaji wa kupanua biashara zao,
-
18:34 - 18:37kwasababu hakuna anayeamini nje ya nchi zetu
-
18:37 - 18:42tunaweza kufanya mambo ya maana. Hakuna mtu anayefikiria kwa mtazamo wa masoko.
-
18:42 - 18:45Hakuna anyefikiria kuna fursa
-
18:45 - 18:48Nimesimama hapa kuwaambia wale waliochelewa jahazi kwa sasa,
-
18:48 - 18:50watalikosa milele.
-
18:50 - 18:56Kwa hiyo iwapo unataka kuwa Afrika, fikiria kuwekeza.
-
18:57 - 19:03Wafikirie akina Beatrice, wafikirie kina Adenike wa dunia hii.
-
19:03 - 19:06ambao wanafanya mambo makubwa ambayo yanawasogeza
-
19:06 - 19:09katika uchumi wa dunia, wakati huo huo wakihakikisha
-
19:09 - 19:12wanawake wenzao na wanaume wanapata ajira.
-
19:12 - 19:14na kwamba watoto katika familia hizo wanapata elimu
-
19:14 - 19:17kwa sababu wazazi wao wanapata kipato cha kuridhisha
-
19:18 - 19:22Kwa hiyo nina wakaribisha kuja kutafuta fursa
-
19:23 - 19:27Mtakapo kwenda Tanzania, sikilizeni kwa makini,
-
19:27 - 19:31kwasababu nina hakika mtasikia kuhusu fursa mbalimbali zilizopo
-
19:31 - 19:36ili muweze kushiriki katika kufanya mambo mazuri
-
19:36 - 19:41kwa bara hili, kwa watu wake na kwenu wenyewe
-
19:41 - 19:42Asanteni sana.
-
19:42 - 19:50(Makofi)
- Title:
- Ngozi Okonjo-Iweala anazungumzia kufanya biashara Afrika
- Speaker:
- Ngozi Okonjo-Iweala
- Description:
-
Tunajua mtazamo potofu kuhusu Afrika -- njaa na magonjwa, vita na rushwa. Lakini, anasema Ngozi Okojo-Iweala, kuna mambo mengi yanayotokea katika nchi za Afrika ambayo hayazungumzwi: moja kati ya mabadiliko hayo, kukua kwa uchumi na fursa za kibiashara.
- Video Language:
- English
- Team:
- closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 19:49
TED edited Swahili subtitles for Want to help Africa? Do business here | ||
TED edited Swahili subtitles for Want to help Africa? Do business here | ||
TED added a translation |