[Script Info] Title: [Events] Format: Layer, Start, End, Style, Name, MarginL, MarginR, MarginV, Effect, Text Dialogue: 0,0:00:05.00,0:00:08.00,Default,,0000,0000,0000,,Asante sana Chris. Kila mtu aliyekuja hapa Dialogue: 0,0:00:08.00,0:00:12.00,Default,,0000,0000,0000,,alisema kuwa anaogopa. Sijui kama na mimi ninaogopa, Dialogue: 0,0:00:12.00,0:00:16.00,Default,,0000,0000,0000,,lakini hii ni mara yangu ya kwanza kuhutubia hadhara kama hii. Dialogue: 0,0:00:16.00,0:00:20.00,Default,,0000,0000,0000,,Na sina teknolojia yeyote ya kisasa kwa ajili yenu ili muweze kuiangalia. Dialogue: 0,0:00:20.00,0:00:23.00,Default,,0000,0000,0000,,Hakuna kielezopicha, kwa hiyo itabidi mnivumilie. Dialogue: 0,0:00:23.00,0:00:26.00,Default,,0000,0000,0000,,(Kicheko). Dialogue: 0,0:00:26.00,0:00:32.00,Default,,0000,0000,0000,,Ninachotaka kufanya asubuhi hii ni kuwasimulia hadithi kadhaa Dialogue: 0,0:00:32.00,0:00:35.00,Default,,0000,0000,0000,,na kuongelea kuhusu Afrika iliyo tofauti. Dialogue: 0,0:00:35.00,0:00:39.00,Default,,0000,0000,0000,,Tayari asubuhi hii kulikuwa na madokezo kuhusu Afrika Dialogue: 0,0:00:39.00,0:00:44.00,Default,,0000,0000,0000,,unayoyasikia kila mara: Afrika ya VVU/UKIMWI, Dialogue: 0,0:00:44.00,0:00:50.00,Default,,0000,0000,0000,,Afrika ya malaria, Afrika ya umaskini, Afrika ya migongano, Dialogue: 0,0:00:50.00,0:00:53.00,Default,,0000,0000,0000,,na Afrika ya maafa. Dialogue: 0,0:00:53.00,0:00:57.00,Default,,0000,0000,0000,,Ingawa kuna ukweli kwamba mambo hayo yanatokea, Dialogue: 0,0:00:57.00,0:01:01.00,Default,,0000,0000,0000,,kuna Afrika ambayo hamuisikii sana. Dialogue: 0,0:01:01.00,0:01:05.00,Default,,0000,0000,0000,,Na saa nyingine nashangazwa na kujiuliza kwanini. Dialogue: 0,0:01:05.00,0:01:09.00,Default,,0000,0000,0000,,Hii ni Afrika ambayo inabadilika, ambayo Chris ameidokezea. Dialogue: 0,0:01:09.00,0:01:11.00,Default,,0000,0000,0000,,Hii ni Afrika yenye fursa. Dialogue: 0,0:01:11.00,0:01:14.00,Default,,0000,0000,0000,,Hii ni Afrika ambayo watu wanataka kuchukua hatua juu ya Dialogue: 0,0:01:14.00,0:01:16.00,Default,,0000,0000,0000,,maisha na uwezo wao. Dialogue: 0,0:01:16.00,0:01:19.00,Default,,0000,0000,0000,,Na hii ndio Afrika ambayo watu wanatafuta kuingia ubia Dialogue: 0,0:01:19.00,0:01:23.00,Default,,0000,0000,0000,,kufanya hivyo. Na hili haswa ndilo ninalotaka kuzungumzia leo. Dialogue: 0,0:01:23.00,0:01:25.00,Default,,0000,0000,0000,,Ningependa kuanza kwa kuwaambia Dialogue: 0,0:01:25.00,0:01:27.00,Default,,0000,0000,0000,,habari kuhusu mabadiliko hayo Afrika. Dialogue: 0,0:01:28.00,0:01:33.00,Default,,0000,0000,0000,,Mnamo 15 Septemba 2005, Bwana Diepreye Alamieyeseigha, Dialogue: 0,0:01:33.00,0:01:37.00,Default,,0000,0000,0000,,Gavana wa jimbo moja lenye utajiri wa mafuta huko Nigeria, Dialogue: 0,0:01:37.00,0:01:44.00,Default,,0000,0000,0000,,alikamatwa na Polisi wa mji wa London alipokuwa matembizini mjini London. Dialogue: 0,0:01:44.00,0:01:49.00,Default,,0000,0000,0000,,Alikamatwa kwasababu kulikuwa na hamisho la kiasi cha dola za kimarekani milioni 8 Dialogue: 0,0:01:49.00,0:01:52.00,Default,,0000,0000,0000,,ambazo zilienda katika akaunti hewa Dialogue: 0,0:01:52.00,0:01:55.00,Default,,0000,0000,0000,,ambazo alikuwa akizimiliki yeye pamoja na familia yake. Dialogue: 0,0:01:56.00,0:01:58.00,Default,,0000,0000,0000,,Kukamatwa kwake kuliwezekana kwasababu kulikuwa na ushirikiano Dialogue: 0,0:01:58.00,0:02:01.00,Default,,0000,0000,0000,,baina ya Polisi wa mji wa London Dialogue: 0,0:02:01.00,0:02:04.00,Default,,0000,0000,0000,,na Tume ya Uhalifu wa Kiuchumi na Fedha ya Nigeria -- Dialogue: 0,0:02:04.00,0:02:11.00,Default,,0000,0000,0000,,inayoongozwa na mtu wenye uwezo na ujasiri: Bwana Nuhu Ribadu. Dialogue: 0,0:02:11.00,0:02:14.00,Default,,0000,0000,0000,,Alamieyeseigha alikamatwa mjini London. Dialogue: 0,0:02:14.00,0:02:18.00,Default,,0000,0000,0000,,Kutokana na udhaifu, alifanikiwa kutoroka akiwa amevalia kama mwanamke Dialogue: 0,0:02:18.00,0:02:21.00,Default,,0000,0000,0000,,na kukimbia kutoka London kurudi Nigeria ambako, Dialogue: 0,0:02:21.00,0:02:25.00,Default,,0000,0000,0000,,kwa mujibu wa katiba, wale walio madarakani Dialogue: 0,0:02:25.00,0:02:27.00,Default,,0000,0000,0000,,kama magavana, rais – kama ilivyo kwenye nchi nyingi -- Dialogue: 0,0:02:27.00,0:02:32.00,Default,,0000,0000,0000,,wana kinga na hawawezi kushtakiwa. Lakini nini kilitokea: Dialogue: 0,0:02:32.00,0:02:36.00,Default,,0000,0000,0000,,watu walikasirishwa sana na tabia hii na iliwezekana Dialogue: 0,0:02:36.00,0:02:42.00,Default,,0000,0000,0000,,kwa sheria za jimbo lake kumvua madaraka. Dialogue: 0,0:02:43.00,0:02:45.00,Default,,0000,0000,0000,,Leo, Alams – kama tumuitavyo kwa kifupi – yuko jela. Dialogue: 0,0:02:46.00,0:02:51.00,Default,,0000,0000,0000,,Hii ni hadithi kuhusu ukweli kwamba watu wa Afrika Dialogue: 0,0:02:51.00,0:02:56.00,Default,,0000,0000,0000,,hawako tayari tena kuvumilia rushwa kutoka kwa viongozi wao. Dialogue: 0,0:02:57.00,0:03:02.00,Default,,0000,0000,0000,,Hii ni hadithi kuhusu ukweli kwamba watu wanataka rasilimali zao Dialogue: 0,0:03:02.00,0:03:07.00,Default,,0000,0000,0000,,zidhibitiwe vizuri kwa manufaa yao, na sio kupelekwa sehemu Dialogue: 0,0:03:07.00,0:03:10.00,Default,,0000,0000,0000,,ambako itawanufaisha mabwanyenye wachache. Dialogue: 0,0:03:10.00,0:03:14.00,Default,,0000,0000,0000,,Kwa hiyo, unaposikia kuhusu Afrika ya rushwa -- Dialogue: 0,0:03:14.00,0:03:18.00,Default,,0000,0000,0000,,rushwa kila mara – Ninataka mfahamu kuwa watu Dialogue: 0,0:03:18.00,0:03:21.00,Default,,0000,0000,0000,,na serikali wanajitahidi sana kupambana na tatizo hili Dialogue: 0,0:03:21.00,0:03:25.00,Default,,0000,0000,0000,,katika baadhi ya nchi, na kwamba mafanikio yanaanza kuonekana. Dialogue: 0,0:03:25.00,0:03:28.00,Default,,0000,0000,0000,,Inamaana kuwa tatizo limekwisha? Jibu ni hapana. Dialogue: 0,0:03:28.00,0:03:32.00,Default,,0000,0000,0000,,Bado kuna safari ndefu, lakini pia kuna nia. Dialogue: 0,0:03:32.00,0:03:36.00,Default,,0000,0000,0000,,Mafanikio yanaandikwa juu ya mapigano ya jambo hili muhimu. Dialogue: 0,0:03:36.00,0:03:38.00,Default,,0000,0000,0000,,Kwa hiyo mnaposikia kuhusu rushwa, Dialogue: 0,0:03:38.00,0:03:41.00,Default,,0000,0000,0000,,msifikiri kwamba hakuna linalotendeka kuhusu hili -- Dialogue: 0,0:03:41.00,0:03:44.00,Default,,0000,0000,0000,,na kwamba hamuwezi kufanya kazi katika nchi yeyote Afrika Dialogue: 0,0:03:44.00,0:03:47.00,Default,,0000,0000,0000,,kwasababu ya rushwa. Hiyo si kweli. Dialogue: 0,0:03:47.00,0:03:53.00,Default,,0000,0000,0000,,Kuna nia ya kupambana na rushwa, na katika nchi nyingi, mapambano hayo yanaendelea Dialogue: 0,0:03:53.00,0:03:57.00,Default,,0000,0000,0000,,na mafanikio yanaonekana. Katika nchi nyingine, kama yangu, Dialogue: 0,0:03:57.00,0:04:00.00,Default,,0000,0000,0000,,ambako kumekuwa na historia ndefu ya kidikteta nchini Nigeria, Dialogue: 0,0:04:00.00,0:04:04.00,Default,,0000,0000,0000,,mapambano bado yanaendelea, na bado tuna safari ndefu. Dialogue: 0,0:04:04.00,0:04:08.00,Default,,0000,0000,0000,,Ukweli wa mambo ni kwamba mapambano bado yanaendelea. Dialogue: 0,0:04:09.00,0:04:11.00,Default,,0000,0000,0000,,Matokeo yanaonekana: Dialogue: 0,0:04:11.00,0:04:15.00,Default,,0000,0000,0000,,tathmini huru ya Benki ya Dunia na mashirika mengine Dialogue: 0,0:04:15.00,0:04:19.00,Default,,0000,0000,0000,,inaonyesha kuwa mwelekeo juu ya rushwa unapungua Dialogue: 0,0:04:19.00,0:04:22.00,Default,,0000,0000,0000,,na utawala unarekebika. Dialogue: 0,0:04:22.00,0:04:26.00,Default,,0000,0000,0000,,Utafiti uliofanywa na Tume ya Uchumi ya Afrika unaonyesha Dialogue: 0,0:04:26.00,0:04:30.00,Default,,0000,0000,0000,,wazi mwelekeo mzuri wa utawala katika nchi 28 za Afrika. Dialogue: 0,0:04:30.00,0:04:32.00,Default,,0000,0000,0000,,Ngoja niseme kitu kimoja zaidi Dialogue: 0,0:04:32.00,0:04:34.00,Default,,0000,0000,0000,,kabla sijamaliza kuzungumzia kuhusu utawala bora. Dialogue: 0,0:04:34.00,0:04:37.00,Default,,0000,0000,0000,,Na ni kitu ambacho watu wanazungumzia kuhusu rushwa, rushwa. Dialogue: 0,0:04:37.00,0:04:39.00,Default,,0000,0000,0000,,Kila mara wanapo zungumzia kuhusu hili Dialogue: 0,0:04:39.00,0:04:41.00,Default,,0000,0000,0000,,mara moja unafikiria Afrika. Dialogue: 0,0:04:41.00,0:04:45.00,Default,,0000,0000,0000,,Hiyo ndio picha: Nchi za Afrika. Lakini ngoja niseme hili: Dialogue: 0,0:04:45.00,0:04:51.00,Default,,0000,0000,0000,,iwapo Alams alifanikiwa kuhamisha dola za kimarekani milioni 8 kwenye akaunti mjini London -- Dialogue: 0,0:04:53.00,0:04:57.00,Default,,0000,0000,0000,,kama watu wengine waliochukukua pesa wakikadiria kuwa Dialogue: 0,0:04:57.00,0:05:01.00,Default,,0000,0000,0000,,kati ya bilioni 20 na 40 za pesa za nchi zinazoendelea Dialogue: 0,0:05:01.00,0:05:04.00,Default,,0000,0000,0000,,ziko nje ya nchi katika nchi zilizoendelea – kama wanaweza kufanyi hivi, Dialogue: 0,0:05:04.00,0:05:07.00,Default,,0000,0000,0000,,hiyo ni nini? Hiyo siyo rushwa? Dialogue: 0,0:05:08.00,0:05:12.00,Default,,0000,0000,0000,,Katika nchi hii, kama ukipokea vitu vya wizi, haushitakiwi? Dialogue: 0,0:05:13.00,0:05:16.00,Default,,0000,0000,0000,,Kwa hiyo tukiongelea kuhusu aina hii ya rushwa, hebu pia tufikirie kuhusu Dialogue: 0,0:05:16.00,0:05:19.00,Default,,0000,0000,0000,,nini kinatokea katika upande mwingine wa dunia -- Dialogue: 0,0:05:19.00,0:05:23.00,Default,,0000,0000,0000,,ambako pesa hizo zinakwenda na nini kifanyike ili kuweza kuzuia hili. Dialogue: 0,0:05:23.00,0:05:26.00,Default,,0000,0000,0000,,Kuna jambo ninalifanyia kazi kwa sasa, pamoja na Benki ya Dunia, Dialogue: 0,0:05:26.00,0:05:29.00,Default,,0000,0000,0000,,kuhusu kurudisha rasilimali, tunajaribu tuwezalo Dialogue: 0,0:05:29.00,0:05:32.00,Default,,0000,0000,0000,,kurudisha pesa ambazo zimepelekwa nje ya nchi -- Dialogue: 0,0:05:32.00,0:05:35.00,Default,,0000,0000,0000,,pesa za nchi zinazoendelea -- ili ziweze kurudishwa. Dialogue: 0,0:05:35.00,0:05:38.00,Default,,0000,0000,0000,,Kama tutaweza kurudisha dola bilioni 20 ambazo ziko nje, Dialogue: 0,0:05:38.00,0:05:41.00,Default,,0000,0000,0000,,litakuwa jambo zuri sana kwa baadhi ya nchi hizi Dialogue: 0,0:05:41.00,0:05:44.00,Default,,0000,0000,0000,,kuliko misaada yote ikiwekwa pamoja. Dialogue: 0,0:05:44.00,0:05:51.00,Default,,0000,0000,0000,,(Makofi). Dialogue: 0,0:05:51.00,0:05:55.00,Default,,0000,0000,0000,,Kitu cha pili ninachotaka kuzungumzia ni nia ya mageuzi. Dialogue: 0,0:05:55.00,0:05:59.00,Default,,0000,0000,0000,,Afrika, baada – wamechoka, tumechoka Dialogue: 0,0:05:59.00,0:06:04.00,Default,,0000,0000,0000,,kuwa kitovu cha misaada kutoka kwa kila mtu. Dialogue: 0,0:06:04.00,0:06:08.00,Default,,0000,0000,0000,,Tunashukuru, ila tunajua kuwa Dialogue: 0,0:06:08.00,0:06:12.00,Default,,0000,0000,0000,,tunaweza kuchukua hatua juu ya uwezo wetu na kama tuna nia ya kufanya mabadiliko. Dialogue: 0,0:06:13.00,0:06:17.00,Default,,0000,0000,0000,,Na kinachotokea katika nchi nyingi za Afrika sasa ni utambuzi kwamba Dialogue: 0,0:06:17.00,0:06:21.00,Default,,0000,0000,0000,,hakuna anayeweza kufanya lolote ila sisi wenyewe. Ni lazima tufanye. Dialogue: 0,0:06:21.00,0:06:25.00,Default,,0000,0000,0000,,Tunaweza kuwakaribisha washirika ambao wanaweza kutuunga mkono, lakini lazima tuanze wenyewe. Dialogue: 0,0:06:25.00,0:06:28.00,Default,,0000,0000,0000,,Ni lazima turekebishe uchumi wetu, tubadilishe uongozi, Dialogue: 0,0:06:28.00,0:06:34.00,Default,,0000,0000,0000,,tuwe na demokrasia zaidi, tuwe wazi kupokea mabadiliko na taarifa. Dialogue: 0,0:06:34.00,0:06:36.00,Default,,0000,0000,0000,,Na hiki ndicho tumeanza kukifanya Dialogue: 0,0:06:36.00,0:06:39.00,Default,,0000,0000,0000,,katika mojawapo kati ya nchi kubwa kabisa katika bara, Nigeria. Dialogue: 0,0:06:39.00,0:06:42.00,Default,,0000,0000,0000,,Hakika, kama hauko Nigeria, hauko Afrika. Dialogue: 0,0:06:42.00,0:06:43.00,Default,,0000,0000,0000,,Ninataka kuwaambia kuwa. Dialogue: 0,0:06:43.00,0:06:44.00,Default,,0000,0000,0000,,(Kicheko). Dialogue: 0,0:06:44.00,0:06:46.00,Default,,0000,0000,0000,,Mmoja kati ya waafrika wanne walio kusini mwa jangwa la Sahara ni Mnigeria, Dialogue: 0,0:06:48.00,0:06:53.00,Default,,0000,0000,0000,,na ina watu milioni 140 – watu wenye pilika -- Dialogue: 0,0:06:54.00,0:06:58.00,Default,,0000,0000,0000,,lakini watu wenye kuvutia. Hauwezi kuchoka. Dialogue: 0,0:06:58.00,0:06:59.00,Default,,0000,0000,0000,,(Kicheko).\N Dialogue: 0,0:06:59.00,0:07:01.00,Default,,0000,0000,0000,,Tulichoanza kufanya ni kujua kwamba Dialogue: 0,0:07:01.00,0:07:03.00,Default,,0000,0000,0000,,tunaweza kuchukua hatua na kujibadili wenyewe. Dialogue: 0,0:07:04.00,0:07:06.00,Default,,0000,0000,0000,,Na kwa msaada wa kiongozi Dialogue: 0,0:07:06.00,0:07:09.00,Default,,0000,0000,0000,,ambaye alikuwa na nia, kwa wakati ule, ya kufanya mabadiliko, Dialogue: 0,0:07:09.00,0:07:11.00,Default,,0000,0000,0000,,tunaandaa mpango madhubuti wa mabadiliko Dialogue: 0,0:07:11.00,0:07:13.00,Default,,0000,0000,0000,,ambao tumeuandika wenyewe. Dialogue: 0,0:07:13.00,0:07:16.00,Default,,0000,0000,0000,,Si Shirika la Kimataifa la Fedha. Wala Benki ya Dunia, Dialogue: 0,0:07:16.00,0:07:19.00,Default,,0000,0000,0000,,ambako nilifanya kazi kwa miaka 21 na kufikia cheo cha makamu wa rais. Dialogue: 0,0:07:20.00,0:07:22.00,Default,,0000,0000,0000,,Hakuna mtu anaweza kukufanyia. Inabidi ufanye mwenyewe. Dialogue: 0,0:07:22.00,0:07:26.00,Default,,0000,0000,0000,,Tukaandaa mpango ambao kwanza, utafanya: kuiondoa serikali Dialogue: 0,0:07:26.00,0:07:30.00,Default,,0000,0000,0000,,kwenye shughuli zisizo na manufaa -- zisizoihusu -- Dialogue: 0,0:07:30.00,0:07:32.00,Default,,0000,0000,0000,,Serikali haitakiwi kufanya biashara Dialogue: 0,0:07:32.00,0:07:33.00,Default,,0000,0000,0000,,ya uzalishaji na utoaji huduma Dialogue: 0,0:07:33.00,0:07:36.00,Default,,0000,0000,0000,,kwasababu haina ufanisi na haina ujuzi. Dialogue: 0,0:07:36.00,0:07:40.00,Default,,0000,0000,0000,,Kwa hiyo tuliamua kubinafsisha mashirika yetu mengi. Dialogue: 0,0:07:40.00,0:07:44.00,Default,,0000,0000,0000,,(Makofi). Dialogue: 0,0:07:45.00,0:07:49.00,Default,,0000,0000,0000,,Sisi -- matokeo yake, tuliamua kuwa na soko huria. Dialogue: 0,0:07:49.00,0:07:52.00,Default,,0000,0000,0000,,Unaweza kuamini kuwa kabla ya mabadiliko haya -- Dialogue: 0,0:07:52.00,0:07:56.00,Default,,0000,0000,0000,,ambayo yalianza mwishoni mwa mwaka 2003, wakati nilipoondoka Washington Dialogue: 0,0:07:56.00,0:07:58.00,Default,,0000,0000,0000,,kwenda kushika nafasi ya Waziri wa Fedha -- Dialogue: 0,0:08:00.00,0:08:04.00,Default,,0000,0000,0000,,tulikuwa na kampuni ya simu ambayo iliweza kutoa huduma za simu za mezani Dialogue: 0,0:08:04.00,0:08:09.00,Default,,0000,0000,0000,,4,500 katika historia yake ya miaka 30? Dialogue: 0,0:08:09.00,0:08:11.00,Default,,0000,0000,0000,,(Kicheko). Dialogue: 0,0:08:11.00,0:08:14.00,Default,,0000,0000,0000,,Kuwa na simu katika nchi yangu lilikuwa ni jambo la kifahari sana. Dialogue: 0,0:08:14.00,0:08:16.00,Default,,0000,0000,0000,,Usingeweza kupata. Ilibidi uhonge. Dialogue: 0,0:08:16.00,0:08:18.00,Default,,0000,0000,0000,,Ilibidi ufanye kila uwezalo ili kupata simu. Dialogue: 0,0:08:18.00,0:08:21.00,Default,,0000,0000,0000,,Rais Obasanjo aliunga mkono na kuzindua Dialogue: 0,0:08:21.00,0:08:25.00,Default,,0000,0000,0000,,kulegezwa kwa masharti katika sekta ya mawasiliano Dialogue: 0,0:08:26.00,0:08:34.00,Default,,0000,0000,0000,,tumepanda kutoka simu 4,500 za mezani kufikia simu milioni 32 zenye GSM, na zinaongezeka. Dialogue: 0,0:08:34.00,0:08:39.00,Default,,0000,0000,0000,,Soko la mawasiliano la Nigeria ni la pili kwa ukuaji duniani kote,♪ Dialogue: 0,0:08:39.00,0:08:44.00,Default,,0000,0000,0000,,ikiwa imetanguliwa na China. Tunapata uwekezaji wa takriban dola bilioni 1 kwa mwaka Dialogue: 0,0:08:44.00,0:08:50.00,Default,,0000,0000,0000,,katika mawasiliano. Na hakuna mtu anayejua, isipokuwa kwa wajanja wachache. Dialogue: 0,0:08:50.00,0:08:53.00,Default,,0000,0000,0000,,(Kicheko). Dialogue: 0,0:08:53.00,0:08:57.00,Default,,0000,0000,0000,,Wajanja wa kwanza kuja Dialogue: 0,0:08:57.00,0:08:59.00,Default,,0000,0000,0000,,walikuwa ni kampuni ya MTN ya Afrika Kusini. Dialogue: 0,0:08:59.00,0:09:03.00,Default,,0000,0000,0000,,Katika miaka mitatu niliyokuwa Waziri wa Fedha, Dialogue: 0,0:09:03.00,0:09:06.00,Default,,0000,0000,0000,,wamepata wastani wa dola milioni 360 kwa mwaka. Dialogue: 0,0:09:08.00,0:09:14.00,Default,,0000,0000,0000,,milioni 360 katika soko – katika nchi ambayo ni maskini, Dialogue: 0,0:09:14.00,0:09:18.00,Default,,0000,0000,0000,,yenye wastani wa pato la taifa chini ya dola 500. Dialogue: 0,0:09:19.00,0:09:21.00,Default,,0000,0000,0000,,Kwahiyo soko lipo hapo. Dialogue: 0,0:09:21.00,0:09:24.00,Default,,0000,0000,0000,,Walilifanya hili siri, lakini baadae wengine nao walianza kujua. Dialogue: 0,0:09:25.00,0:09:28.00,Default,,0000,0000,0000,,Wanageria wenyewe walianzisha Dialogue: 0,0:09:28.00,0:09:30.00,Default,,0000,0000,0000,,makampuni ya mawasiliano ya simu zisizotumia waya Dialogue: 0,0:09:30.00,0:09:32.00,Default,,0000,0000,0000,,na wengine kama watatu wane hivi wameingia. Dialogue: 0,0:09:32.00,0:09:35.00,Default,,0000,0000,0000,,Lakini bado kuna soko kubwa sana, Dialogue: 0,0:09:35.00,0:09:38.00,Default,,0000,0000,0000,,na watu hawajui kuhusu hili, au hawataki kujua. Dialogue: 0,0:09:40.00,0:09:42.00,Default,,0000,0000,0000,,Kwa hiyo ubinafsishaji ni jambo mojawapo tulilofanya. Dialogue: 0,0:09:43.00,0:09:49.00,Default,,0000,0000,0000,,Kitu kingine tulichofanya ni kusimamia vizuri masuala yetu ya fedha. Dialogue: 0,0:09:50.00,0:09:52.00,Default,,0000,0000,0000,,Kwasababu hakuna atakayekusaidia na kukuongoza Dialogue: 0,0:09:53.00,0:09:56.00,Default,,0000,0000,0000,,iwapo hudhibiti fedha zako vizuri. Dialogue: 0,0:09:56.00,0:10:00.00,Default,,0000,0000,0000,,Na Nigeria, ikiwa na sekta ya mafuta, ilikuwa na sifa Dialogue: 0,0:10:00.00,0:10:05.00,Default,,0000,0000,0000,,ya rushwa na kutosimamia vizuri masuala ya fedha za umma. Dialogue: 0,0:10:05.00,0:10:09.00,Default,,0000,0000,0000,,Je tulijaribu kufanya nini? Tulianzisha sheria ya fedha Dialogue: 0,0:10:10.00,0:10:12.00,Default,,0000,0000,0000,,ambayo ilitenganisha bajeti yetu na bei ya mafuta. Dialogue: 0,0:10:12.00,0:10:16.00,Default,,0000,0000,0000,,Zamani tulikuwa tumezoea kubajeti kutokana na kipato ambacho tulikipata kutokana na mafuta, Dialogue: 0,0:10:16.00,0:10:21.00,Default,,0000,0000,0000,,kwasababu mafuta ndiyo sekta kuu ya mapato Dialogue: 0,0:10:21.00,0:10:24.00,Default,,0000,0000,0000,,katika uchumi: asilimia 70 ya mapato yetu yanatokana na mafuta. Dialogue: 0,0:10:24.00,0:10:28.00,Default,,0000,0000,0000,,Tulitenganisha hilo, na tulipofanya hivyo tulianza kubajeti Dialogue: 0,0:10:28.00,0:10:31.00,Default,,0000,0000,0000,,kwa bei ambayo ilikuwa chini kidogo ya bei ya mafuta Dialogue: 0,0:10:31.00,0:10:35.00,Default,,0000,0000,0000,,na kuhifadhi chochote cha ziada juu ya bei hiyo. Dialogue: 0,0:10:36.00,0:10:39.00,Default,,0000,0000,0000,,Hatukuweza kujua kama tungeweza kufanikisha, ilikuwa ni utata sana.® Dialogue: 0,0:10:39.00,0:10:42.00,Default,,0000,0000,0000,,Lakini kitu ambacho kilitokea haraka ilikuwa ni mabadiliko Dialogue: 0,0:10:42.00,0:10:45.00,Default,,0000,0000,0000,,ambayo yalikuwepo kwa maendeleo yetu ya uchumi -- Dialogue: 0,0:10:45.00,0:10:49.00,Default,,0000,0000,0000,,ambapo, hata kama bei ya mafuta ingekuwa juu, tungekuwa haraka sana. Dialogue: 0,0:10:49.00,0:10:51.00,Default,,0000,0000,0000,,Wakati zilipoanguka, tulianguka. Dialogue: 0,0:10:51.00,0:10:55.00,Default,,0000,0000,0000,,Na tulikuwa tunashindwa kulipia chochote, hata mishahara, katika uchumi. Dialogue: 0,0:10:56.00,0:11:00.00,Default,,0000,0000,0000,,Hii ilisawazisha. Tuliweza kuweka akiba, kabla sijaondoka, Dialogue: 0,0:11:00.00,0:11:06.00,Default,,0000,0000,0000,,dola bilioni 27. Ambapo – hii ilienda kwenye hazina yetu -- Dialogue: 0,0:11:06.00,0:11:10.00,Default,,0000,0000,0000,,wakati nilipofika mwaka 2003, tulikuwa na dola billion 7 kwenye akiba. Dialogue: 0,0:11:11.00,0:11:14.00,Default,,0000,0000,0000,,Na wakati naondoka, tulikuwa na karibu dola bilioni 30. Na Dialogue: 0,0:11:14.00,0:11:17.00,Default,,0000,0000,0000,,tunavyoongea sasa, tuna dola bilioni 40 kwenye akiba Dialogue: 0,0:11:18.00,0:11:22.00,Default,,0000,0000,0000,,hii ni kutokana na usimamizi mzuri wa fedha zetu. Dialogue: 0,0:11:23.00,0:11:26.00,Default,,0000,0000,0000,,Hii inasaidia kutuliza uchumi wetu, kuufanya uwe imara. Dialogue: 0,0:11:26.00,0:11:29.00,Default,,0000,0000,0000,,Thamani ya fedha yetu ilikuwa ikibadilika kila mara Dialogue: 0,0:11:29.00,0:11:33.00,Default,,0000,0000,0000,,kwa sasa ipo angalau imara na kusimamiwa, ili wafanyabiashara Dialogue: 0,0:11:33.00,0:11:38.00,Default,,0000,0000,0000,,wawe na uhakika wa bei katika uchumi. Dialogue: 0,0:11:40.00,0:11:44.00,Default,,0000,0000,0000,,Tuliweza kudhibiti mfumuko bei kutoka asilimia 28 mpaka karibu asilimia 11. Dialogue: 0,0:11:46.00,0:11:52.00,Default,,0000,0000,0000,,Na pato letu la taifa liliongezeka kutoka wastani wa asilimia 2.3 kwa muongo uliopita Dialogue: 0,0:11:52.00,0:11:55.00,Default,,0000,0000,0000,,mpaka kufikia asilimia 6.5 sasa. Dialogue: 0,0:11:56.00,0:11:59.00,Default,,0000,0000,0000,,Kwa hiyo mabadiliko yote tuliyoweza kufanya Dialogue: 0,0:11:59.00,0:12:02.00,Default,,0000,0000,0000,,yameweza kuonekana kwa vitendo ambavyo vinaweza kuonekana katika uchumi. Dialogue: 0,0:12:02.00,0:12:06.00,Default,,0000,0000,0000,,Na kitu cha muhimu zaidi, ni kwasababu tunataka kuondokana na mafuta Dialogue: 0,0:12:06.00,0:12:08.00,Default,,0000,0000,0000,,na kupanua wigo zaidi – na kuna fursa nyingi sana Dialogue: 0,0:12:08.00,0:12:11.00,Default,,0000,0000,0000,,katika nchi hii kubwa, kama ilivyo katika nchi nyingine za Afrika -- Dialogue: 0,0:12:13.00,0:12:16.00,Default,,0000,0000,0000,,kilichotia fora zaidi ni huu ukuaji haukutoka Dialogue: 0,0:12:16.00,0:12:19.00,Default,,0000,0000,0000,,kwenye sekta mafuta pekee, bali sekta nyingine pia. Dialogue: 0,0:12:19.00,0:12:22.00,Default,,0000,0000,0000,,Kilimo kilikuwa kwa wastani wa asilimi 8. Dialogue: 0,0:12:22.00,0:12:26.00,Default,,0000,0000,0000,,Sekta ya mawasiliano ilikuwa, makazi na ujenzi, Dialogue: 0,0:12:26.00,0:12:31.00,Default,,0000,0000,0000,,na ninaweza kuendelea zaidi na zaidi. Na hii ni kuwaonyesha kwamba Dialogue: 0,0:12:31.00,0:12:33.00,Default,,0000,0000,0000,,uchumi wako unaporekebishika, Dialogue: 0,0:12:33.00,0:12:37.00,Default,,0000,0000,0000,,fursa katika sekta nyingine zipo nyingi. Dialogue: 0,0:12:38.00,0:12:41.00,Default,,0000,0000,0000,,Tuna frusa katika kilimo, kama nilivyosema. Dialogue: 0,0:12:41.00,0:12:45.00,Default,,0000,0000,0000,,Tuna fursa katika madini. Tuna madini mengi Dialogue: 0,0:12:45.00,0:12:48.00,Default,,0000,0000,0000,,ambako hakuna mtu amewekeza katika utafutaji. Tumegundua Dialogue: 0,0:12:48.00,0:12:51.00,Default,,0000,0000,0000,,kuwa bila kuwa na sera sahihi za kuwezesha, Dialogue: 0,0:12:51.00,0:12:54.00,Default,,0000,0000,0000,,hilo halitawezekana. Sasa tuna sheria ya uchimbaji madini Dialogue: 0,0:12:54.00,0:12:57.00,Default,,0000,0000,0000,,ambayo inalinganishwa na sheria nyingine bora duniani. Dialogue: 0,0:12:58.00,0:13:00.00,Default,,0000,0000,0000,,Tuna fursa katika makazi na usimamizi wa majumba. Dialogue: 0,0:13:00.00,0:13:03.00,Default,,0000,0000,0000,,Kulikuwa hakuna chochote katika nchi ya watu milioni 140 -- Dialogue: 0,0:13:04.00,0:13:09.00,Default,,0000,0000,0000,,hakuna maduka makubwa kama myajuavyo hapa. Dialogue: 0,0:13:10.00,0:13:13.00,Default,,0000,0000,0000,,Hii inaweza kuwa fursa kwa mtu fulani Dialogue: 0,0:13:13.00,0:13:15.00,Default,,0000,0000,0000,,ambayo ilitia chachu ya kufikiria kwa watu. Dialogue: 0,0:13:16.00,0:13:19.00,Default,,0000,0000,0000,,Sasa tuna mazingira ambayo biashara katika maduka haya makubwa Dialogue: 0,0:13:19.00,0:13:22.00,Default,,0000,0000,0000,,yanapata faida mara nne ya ilivyokadiriwa. Dialogue: 0,0:13:23.00,0:13:26.00,Default,,0000,0000,0000,,Kwa hiyo mambo makubwa kwenye ujenzi, mali isiyohamishika, Dialogue: 0,0:13:26.00,0:13:28.00,Default,,0000,0000,0000,,Masoko ya rehani. Huduma za fedha Dialogue: 0,0:13:29.00,0:13:33.00,Default,,0000,0000,0000,,tulikuwa na Benki 89. Nyingi hazifanyi biashara iliyokusudiwa. Dialogue: 0,0:13:33.00,0:13:37.00,Default,,0000,0000,0000,,Tulizizatiti kutoka 89 kufikia Benki 25 kwa Dialogue: 0,0:13:37.00,0:13:42.00,Default,,0000,0000,0000,,waongeze mtaji wao -- gawio la mtaji. Dialogue: 0,0:13:42.00,0:13:47.00,Default,,0000,0000,0000,,Ilikuwa kutoka dola milioni 25 mpaka dola milioni 150. Dialogue: 0,0:13:47.00,0:13:51.00,Default,,0000,0000,0000,,Benki, Benki hizi sasa zimejizatiti na kuimarishwa Dialogue: 0,0:13:51.00,0:13:55.00,Default,,0000,0000,0000,,mfumo wa Benki umevutia wamekezaji wengi kutoka nje. Dialogue: 0,0:13:55.00,0:13:59.00,Default,,0000,0000,0000,,Benki ya Barclays kutoka Uingereza inaingiza milioni 500. Dialogue: 0,0:13:59.00,0:14:03.00,Default,,0000,0000,0000,,Standard Chartered imeingiza milioni 140. Dialogue: 0,0:14:03.00,0:14:06.00,Default,,0000,0000,0000,,Ninaweza kuendelea zaidi. Dola zaidi na zaidi, ndani ya mfumo. Dialogue: 0,0:14:06.00,0:14:08.00,Default,,0000,0000,0000,,Tunafanya hivyo hivyo kwenye sekta ya bima. Dialogue: 0,0:14:08.00,0:14:11.00,Default,,0000,0000,0000,,Kwa hiyo kwenye huduma za fedha, kuna fursa kubwa zaidi. Dialogue: 0,0:14:11.00,0:14:17.00,Default,,0000,0000,0000,,Kwenye utalii, katika nchi nyingi za Kiafrika, ni fursa kubwa. Dialogue: 0,0:14:17.00,0:14:20.00,Default,,0000,0000,0000,,Na hii ndiyo sababu kubwa ya kuwa watu wengi wanaifahamu Afrika Mashariki kwa: Dialogue: 0,0:14:21.00,0:14:24.00,Default,,0000,0000,0000,,wanyama pori, tembo na kadhalika. Dialogue: 0,0:14:24.00,0:14:26.00,Default,,0000,0000,0000,,Lakini kusimimamia soko la utalii ili Dialogue: 0,0:14:26.00,0:14:29.00,Default,,0000,0000,0000,,liweze kuwanufaisha watu ni muhimu sana. Dialogue: 0,0:14:30.00,0:14:33.00,Default,,0000,0000,0000,,Sasa ninachojaribu kusema ni nini? Najaribu kuwaambia Dialogue: 0,0:14:33.00,0:14:36.00,Default,,0000,0000,0000,,kuna wimbi jipya katika bara. Dialogue: 0,0:14:36.00,0:14:41.00,Default,,0000,0000,0000,,Wimbi la uwazi na demokrasia ambapo tangu mwaka 2000, Dialogue: 0,0:14:41.00,0:14:43.00,Default,,0000,0000,0000,,zaidi ya theluthi mbili ya nchi za Afrika zimefanya Dialogue: 0,0:14:43.00,0:14:45.00,Default,,0000,0000,0000,,uchaguzi wa kidemokrasia wa vyama vingi. Dialogue: 0,0:14:46.00,0:14:49.00,Default,,0000,0000,0000,,Si zote zilikuwa kamilifu, au zitakuwa, Dialogue: 0,0:14:49.00,0:14:51.00,Default,,0000,0000,0000,,lakini mwelekeo uko wazi. Dialogue: 0,0:14:51.00,0:14:55.00,Default,,0000,0000,0000,,Ninajaribu kuwaelezea kwamba toka miaka mitatu iliyopita Dialogue: 0,0:14:55.00,0:14:58.00,Default,,0000,0000,0000,,wastani wa ukuaji wa uchumi katika bara umeongezeka Dialogue: 0,0:14:58.00,0:15:02.00,Default,,0000,0000,0000,,kutoka karibu asilimia 2.5 mpaka asilimia 5 kwa mwaka. Dialogue: 0,0:15:02.00,0:15:06.00,Default,,0000,0000,0000,,Hii ni bora zaidi ya ufanisi wa nchi nyingi za OECD. Dialogue: 0,0:15:07.00,0:15:11.00,Default,,0000,0000,0000,,Kwahiyo ni wazi kwamba mambo yanabadilika. Dialogue: 0,0:15:11.00,0:15:13.00,Default,,0000,0000,0000,,Migogoro imepungua barani; Dialogue: 0,0:15:14.00,0:15:16.00,Default,,0000,0000,0000,,kutoka migogoro 12 kwa muongo uliopita, Dialogue: 0,0:15:16.00,0:15:18.00,Default,,0000,0000,0000,,kufikia migogoro mitatu au minne, Dialogue: 0,0:15:18.00,0:15:21.00,Default,,0000,0000,0000,,Mojawapo ya migogoro mibaya zaidi, kwa hakika, ni ule wa Darfur. Dialogue: 0,0:15:21.00,0:15:24.00,Default,,0000,0000,0000,,Na kama ujuavyo, kuna athari kwa majirani, iwapo Dialogue: 0,0:15:24.00,0:15:26.00,Default,,0000,0000,0000,,kuna jambo linatokea upande mmoja wa bara, Dialogue: 0,0:15:26.00,0:15:29.00,Default,,0000,0000,0000,,inaonekana kama bara zima limeathirika. Dialogue: 0,0:15:29.00,0:15:32.00,Default,,0000,0000,0000,,Lakini ni vema muelewe kwamba hili bara -- Dialogue: 0,0:15:32.00,0:15:38.00,Default,,0000,0000,0000,,ni bara lenye nchi nyingi na si nchi moja. Dialogue: 0,0:15:38.00,0:15:40.00,Default,,0000,0000,0000,,Na iwapo tuna migogoro mitatu minne hivi, Dialogue: 0,0:15:40.00,0:15:43.00,Default,,0000,0000,0000,,ina maana kuwa kuna fursa nyingi za kuwekeza Dialogue: 0,0:15:43.00,0:15:50.00,Default,,0000,0000,0000,,katika uchumi ulio imara, unaokua na wenye kusisimua Dialogue: 0,0:15:50.00,0:15:53.00,Default,,0000,0000,0000,,ambako kuna fursa nyingi sana. Dialogue: 0,0:15:54.00,0:15:58.00,Default,,0000,0000,0000,,Ningependa kutoa dokezo moja kuhusu uwekezaji huu. Dialogue: 0,0:15:59.00,0:16:01.00,Default,,0000,0000,0000,,Namna nzuri ya kuisaidia Afrika sasa Dialogue: 0,0:16:02.00,0:16:05.00,Default,,0000,0000,0000,,ni kuwasaidia waweze kusimama wenyewe. Dialogue: 0,0:16:05.00,0:16:09.00,Default,,0000,0000,0000,,Na namna nzuri ya kufanya hivyo ni kusaidia kuleta ajira. Dialogue: 0,0:16:10.00,0:16:14.00,Default,,0000,0000,0000,,Hakuna tatizo katika kupambana na malaria na kuwekeza pesa kwenye hilo Dialogue: 0,0:16:14.00,0:16:18.00,Default,,0000,0000,0000,,na kuokoa maisha ya watoto. Sina maana hiyo. Hilo ni sawa. Dialogue: 0,0:16:19.00,0:16:23.00,Default,,0000,0000,0000,,Lakini fikiria tofauti itakayokuwa kwenye familia: iwapo wazazi wanaweza kuwa na ajira Dialogue: 0,0:16:23.00,0:16:25.00,Default,,0000,0000,0000,,na wakahakikisha watoto wao wanakwenda shule, Dialogue: 0,0:16:25.00,0:16:28.00,Default,,0000,0000,0000,,kwamba wanaweza kununua dawa za kupambana na magonjwa wao wenyewe. Dialogue: 0,0:16:28.00,0:16:32.00,Default,,0000,0000,0000,,Kama tunaweza kuwekeza kwenye maeneo ambayo nyinyi wenyewe mnapata faida Dialogue: 0,0:16:32.00,0:16:37.00,Default,,0000,0000,0000,,wakati huo huo mkitengeneza ajira na kuwasaidia watu wasimame wenyewe, Dialogue: 0,0:16:37.00,0:16:42.00,Default,,0000,0000,0000,,hii siyo fursa nzuri? Hii si ndiyo njia ya kufuata? Dialogue: 0,0:16:42.00,0:16:45.00,Default,,0000,0000,0000,,Na nataka kusema jambo kuhusu watu bora zaidi wa kuwawekezea Dialogue: 0,0:16:45.00,0:16:47.00,Default,,0000,0000,0000,,katika bara hili ni wanawake. Dialogue: 0,0:16:48.00,0:16:55.00,Default,,0000,0000,0000,,(Makofi). Dialogue: 0,0:16:55.00,0:17:00.00,Default,,0000,0000,0000,,Nina CD hapa. Samahani sikusema kwa wakati muafaka. Dialogue: 0,0:17:00.00,0:17:02.00,Default,,0000,0000,0000,,Lakini, ningependa mngekuwa mmeiangalia. Dialogue: 0,0:17:02.00,0:17:05.00,Default,,0000,0000,0000,,Inasema, "Afrika: Iko wazi kwa Biashara." Dialogue: 0,0:17:06.00,0:17:09.00,Default,,0000,0000,0000,,Na video hii imeshinda tuzo Dialogue: 0,0:17:09.00,0:17:11.00,Default,,0000,0000,0000,,kama makala bora ya mwaka. Dialogue: 0,0:17:11.00,0:17:13.00,Default,,0000,0000,0000,,Elewa kwamba mwanamke aliyetengeneza makala hii Dialogue: 0,0:17:13.00,0:17:18.00,Default,,0000,0000,0000,,atakuwa Tanzania, ambako watakuwa na kongamano mwezi Juni. Dialogue: 0,0:17:19.00,0:17:24.00,Default,,0000,0000,0000,,Lakini hii inakuonyesha kwamba Waafrika, na hususani wanawake wa Afrika, ambao Dialogue: 0,0:17:24.00,0:17:29.00,Default,,0000,0000,0000,,pamoja na matatizo yote wameweza kuanzisha biashara, nyingine ni za kiwango cha kimataifa. Dialogue: 0,0:17:29.00,0:17:32.00,Default,,0000,0000,0000,,Mmoja kati ya wanawake katika video hii, Adenike Ogunlesi, Dialogue: 0,0:17:32.00,0:17:34.00,Default,,0000,0000,0000,,anashona nguo za watoto Dialogue: 0,0:17:34.00,0:17:39.00,Default,,0000,0000,0000,,kitu ambacho alianza kama kujifurahisha na ikakua na kuwa biashara. Dialogue: 0,0:17:39.00,0:17:42.00,Default,,0000,0000,0000,,Akichanganya vitambaa vya Kiafrika ambavyo tunavyo, Dialogue: 0,0:17:43.00,0:17:44.00,Default,,0000,0000,0000,,na vitambaa vingine kutoka sehemu nyingine. Dialogue: 0,0:17:44.00,0:17:49.00,Default,,0000,0000,0000,,Na hivyo, atatengeneza suruali kwa kutumia vitambaa vizito, Dialogue: 0,0:17:49.00,0:17:53.00,Default,,0000,0000,0000,,ikiwa imechanganywa na vitambaa vya kiafrika. Ni ubunifu mzuri sana. Dialogue: 0,0:17:55.00,0:17:58.00,Default,,0000,0000,0000,,Amefikai hatua ambapo anapata zabuni kutoka Wal-Mart. Dialogue: 0,0:17:59.00,0:18:00.00,Default,,0000,0000,0000,,(Kicheko). Dialogue: 0,0:18:01.00,0:18:03.00,Default,,0000,0000,0000,,Kwa nguo 10,000 Dialogue: 0,0:18:04.00,0:18:08.00,Default,,0000,0000,0000,,Kwa hiyo hii inawaonyesha kuwa tuna watu wenye uwezo wa kufanya mambo. Dialogue: 0,0:18:08.00,0:18:13.00,Default,,0000,0000,0000,,Wanawake wana juhudi, wako makini; wanachapa kazi. Dialogue: 0,0:18:13.00,0:18:15.00,Default,,0000,0000,0000,,Naweza kuendelea kwa kutoa mifano: Dialogue: 0,0:18:15.00,0:18:19.00,Default,,0000,0000,0000,,Beatrice Gakuba wa Rwanda, alifungua biashara ya maua Dialogue: 0,0:18:19.00,0:18:24.00,Default,,0000,0000,0000,,na sasa anayasafirisha kwenye mnada wa udachi huko Amsterdam kila asubuhi, Dialogue: 0,0:18:24.00,0:18:28.00,Default,,0000,0000,0000,,na ameajiri wanawake na wanaume takriban 200 kumsaidia kazi. Dialogue: 0,0:18:29.00,0:18:33.00,Default,,0000,0000,0000,,Hata hivyo, wengi wao, wana kiu ya kupata mtaji wa kupanua biashara zao, Dialogue: 0,0:18:34.00,0:18:37.00,Default,,0000,0000,0000,,kwasababu hakuna anayeamini nje ya nchi zetu Dialogue: 0,0:18:37.00,0:18:42.00,Default,,0000,0000,0000,,tunaweza kufanya mambo ya maana. Hakuna mtu anayefikiria kwa mtazamo wa masoko. Dialogue: 0,0:18:42.00,0:18:45.00,Default,,0000,0000,0000,,Hakuna anyefikiria kuna fursa Dialogue: 0,0:18:45.00,0:18:48.00,Default,,0000,0000,0000,,Nimesimama hapa kuwaambia wale waliochelewa jahazi kwa sasa, Dialogue: 0,0:18:48.00,0:18:50.00,Default,,0000,0000,0000,,watalikosa milele. Dialogue: 0,0:18:50.00,0:18:56.00,Default,,0000,0000,0000,,Kwa hiyo iwapo unataka kuwa Afrika, fikiria kuwekeza. Dialogue: 0,0:18:57.00,0:19:03.00,Default,,0000,0000,0000,,Wafikirie akina Beatrice, wafikirie kina Adenike wa dunia hii. Dialogue: 0,0:19:03.00,0:19:06.00,Default,,0000,0000,0000,,ambao wanafanya mambo makubwa ambayo yanawasogeza Dialogue: 0,0:19:06.00,0:19:09.00,Default,,0000,0000,0000,,katika uchumi wa dunia, wakati huo huo wakihakikisha Dialogue: 0,0:19:09.00,0:19:12.00,Default,,0000,0000,0000,,wanawake wenzao na wanaume wanapata ajira. Dialogue: 0,0:19:12.00,0:19:14.00,Default,,0000,0000,0000,,na kwamba watoto katika familia hizo wanapata elimu Dialogue: 0,0:19:14.00,0:19:17.00,Default,,0000,0000,0000,,kwa sababu wazazi wao wanapata kipato cha kuridhisha Dialogue: 0,0:19:18.00,0:19:22.00,Default,,0000,0000,0000,,Kwa hiyo nina wakaribisha kuja kutafuta fursa Dialogue: 0,0:19:23.00,0:19:27.00,Default,,0000,0000,0000,,Mtakapo kwenda Tanzania, sikilizeni kwa makini, Dialogue: 0,0:19:27.00,0:19:31.00,Default,,0000,0000,0000,,kwasababu nina hakika mtasikia kuhusu fursa mbalimbali zilizopo Dialogue: 0,0:19:31.00,0:19:36.00,Default,,0000,0000,0000,,ili muweze kushiriki katika kufanya mambo mazuri Dialogue: 0,0:19:36.00,0:19:41.00,Default,,0000,0000,0000,,kwa bara hili, kwa watu wake na kwenu wenyewe Dialogue: 0,0:19:41.00,0:19:42.00,Default,,0000,0000,0000,,Asanteni sana. Dialogue: 0,0:19:42.00,0:19:50.00,Default,,0000,0000,0000,,(Makofi)