1 00:00:05,000 --> 00:00:08,000 Asante sana Chris. Kila mtu aliyekuja hapa 2 00:00:08,000 --> 00:00:12,000 alisema kuwa anaogopa. Sijui kama na mimi ninaogopa, 3 00:00:12,000 --> 00:00:16,000 lakini hii ni mara yangu ya kwanza kuhutubia hadhara kama hii. 4 00:00:16,000 --> 00:00:20,000 Na sina teknolojia yeyote ya kisasa kwa ajili yenu ili muweze kuiangalia. 5 00:00:20,000 --> 00:00:23,000 Hakuna kielezopicha, kwa hiyo itabidi mnivumilie. 6 00:00:23,000 --> 00:00:26,000 (Kicheko). 7 00:00:26,000 --> 00:00:32,000 Ninachotaka kufanya asubuhi hii ni kuwasimulia hadithi kadhaa 8 00:00:32,000 --> 00:00:35,000 na kuongelea kuhusu Afrika iliyo tofauti. 9 00:00:35,000 --> 00:00:39,000 Tayari asubuhi hii kulikuwa na madokezo kuhusu Afrika 10 00:00:39,000 --> 00:00:44,000 unayoyasikia kila mara: Afrika ya VVU/UKIMWI, 11 00:00:44,000 --> 00:00:50,000 Afrika ya malaria, Afrika ya umaskini, Afrika ya migongano, 12 00:00:50,000 --> 00:00:53,000 na Afrika ya maafa. 13 00:00:53,000 --> 00:00:57,000 Ingawa kuna ukweli kwamba mambo hayo yanatokea, 14 00:00:57,000 --> 00:01:01,000 kuna Afrika ambayo hamuisikii sana. 15 00:01:01,000 --> 00:01:05,000 Na saa nyingine nashangazwa na kujiuliza kwanini. 16 00:01:05,000 --> 00:01:09,000 Hii ni Afrika ambayo inabadilika, ambayo Chris ameidokezea. 17 00:01:09,000 --> 00:01:11,000 Hii ni Afrika yenye fursa. 18 00:01:11,000 --> 00:01:14,000 Hii ni Afrika ambayo watu wanataka kuchukua hatua juu ya 19 00:01:14,000 --> 00:01:16,000 maisha na uwezo wao. 20 00:01:16,000 --> 00:01:19,000 Na hii ndio Afrika ambayo watu wanatafuta kuingia ubia 21 00:01:19,000 --> 00:01:23,000 kufanya hivyo. Na hili haswa ndilo ninalotaka kuzungumzia leo. 22 00:01:23,000 --> 00:01:25,000 Ningependa kuanza kwa kuwaambia 23 00:01:25,000 --> 00:01:27,000 habari kuhusu mabadiliko hayo Afrika. 24 00:01:28,000 --> 00:01:33,000 Mnamo 15 Septemba 2005, Bwana Diepreye Alamieyeseigha, 25 00:01:33,000 --> 00:01:37,000 Gavana wa jimbo moja lenye utajiri wa mafuta huko Nigeria, 26 00:01:37,000 --> 00:01:44,000 alikamatwa na Polisi wa mji wa London alipokuwa matembizini mjini London. 27 00:01:44,000 --> 00:01:49,000 Alikamatwa kwasababu kulikuwa na hamisho la kiasi cha dola za kimarekani milioni 8 28 00:01:49,000 --> 00:01:52,000 ambazo zilienda katika akaunti hewa 29 00:01:52,000 --> 00:01:55,000 ambazo alikuwa akizimiliki yeye pamoja na familia yake. 30 00:01:56,000 --> 00:01:58,000 Kukamatwa kwake kuliwezekana kwasababu kulikuwa na ushirikiano 31 00:01:58,000 --> 00:02:01,000 baina ya Polisi wa mji wa London 32 00:02:01,000 --> 00:02:04,000 na Tume ya Uhalifu wa Kiuchumi na Fedha ya Nigeria -- 33 00:02:04,000 --> 00:02:11,000 inayoongozwa na mtu wenye uwezo na ujasiri: Bwana Nuhu Ribadu. 34 00:02:11,000 --> 00:02:14,000 Alamieyeseigha alikamatwa mjini London. 35 00:02:14,000 --> 00:02:18,000 Kutokana na udhaifu, alifanikiwa kutoroka akiwa amevalia kama mwanamke 36 00:02:18,000 --> 00:02:21,000 na kukimbia kutoka London kurudi Nigeria ambako, 37 00:02:21,000 --> 00:02:25,000 kwa mujibu wa katiba, wale walio madarakani 38 00:02:25,000 --> 00:02:27,000 kama magavana, rais – kama ilivyo kwenye nchi nyingi -- 39 00:02:27,000 --> 00:02:32,000 wana kinga na hawawezi kushtakiwa. Lakini nini kilitokea: 40 00:02:32,000 --> 00:02:36,000 watu walikasirishwa sana na tabia hii na iliwezekana 41 00:02:36,000 --> 00:02:42,000 kwa sheria za jimbo lake kumvua madaraka. 42 00:02:43,000 --> 00:02:45,000 Leo, Alams – kama tumuitavyo kwa kifupi – yuko jela. 43 00:02:46,000 --> 00:02:51,000 Hii ni hadithi kuhusu ukweli kwamba watu wa Afrika 44 00:02:51,000 --> 00:02:56,000 hawako tayari tena kuvumilia rushwa kutoka kwa viongozi wao. 45 00:02:57,000 --> 00:03:02,000 Hii ni hadithi kuhusu ukweli kwamba watu wanataka rasilimali zao 46 00:03:02,000 --> 00:03:07,000 zidhibitiwe vizuri kwa manufaa yao, na sio kupelekwa sehemu 47 00:03:07,000 --> 00:03:10,000 ambako itawanufaisha mabwanyenye wachache. 48 00:03:10,000 --> 00:03:14,000 Kwa hiyo, unaposikia kuhusu Afrika ya rushwa -- 49 00:03:14,000 --> 00:03:18,000 rushwa kila mara – Ninataka mfahamu kuwa watu 50 00:03:18,000 --> 00:03:21,000 na serikali wanajitahidi sana kupambana na tatizo hili 51 00:03:21,000 --> 00:03:25,000 katika baadhi ya nchi, na kwamba mafanikio yanaanza kuonekana. 52 00:03:25,000 --> 00:03:28,000 Inamaana kuwa tatizo limekwisha? Jibu ni hapana. 53 00:03:28,000 --> 00:03:32,000 Bado kuna safari ndefu, lakini pia kuna nia. 54 00:03:32,000 --> 00:03:36,000 Mafanikio yanaandikwa juu ya mapigano ya jambo hili muhimu. 55 00:03:36,000 --> 00:03:38,000 Kwa hiyo mnaposikia kuhusu rushwa, 56 00:03:38,000 --> 00:03:41,000 msifikiri kwamba hakuna linalotendeka kuhusu hili -- 57 00:03:41,000 --> 00:03:44,000 na kwamba hamuwezi kufanya kazi katika nchi yeyote Afrika 58 00:03:44,000 --> 00:03:47,000 kwasababu ya rushwa. Hiyo si kweli. 59 00:03:47,000 --> 00:03:53,000 Kuna nia ya kupambana na rushwa, na katika nchi nyingi, mapambano hayo yanaendelea 60 00:03:53,000 --> 00:03:57,000 na mafanikio yanaonekana. Katika nchi nyingine, kama yangu, 61 00:03:57,000 --> 00:04:00,000 ambako kumekuwa na historia ndefu ya kidikteta nchini Nigeria, 62 00:04:00,000 --> 00:04:04,000 mapambano bado yanaendelea, na bado tuna safari ndefu. 63 00:04:04,000 --> 00:04:08,000 Ukweli wa mambo ni kwamba mapambano bado yanaendelea. 64 00:04:09,000 --> 00:04:11,000 Matokeo yanaonekana: 65 00:04:11,000 --> 00:04:15,000 tathmini huru ya Benki ya Dunia na mashirika mengine 66 00:04:15,000 --> 00:04:19,000 inaonyesha kuwa mwelekeo juu ya rushwa unapungua 67 00:04:19,000 --> 00:04:22,000 na utawala unarekebika. 68 00:04:22,000 --> 00:04:26,000 Utafiti uliofanywa na Tume ya Uchumi ya Afrika unaonyesha 69 00:04:26,000 --> 00:04:30,000 wazi mwelekeo mzuri wa utawala katika nchi 28 za Afrika. 70 00:04:30,000 --> 00:04:32,000 Ngoja niseme kitu kimoja zaidi 71 00:04:32,000 --> 00:04:34,000 kabla sijamaliza kuzungumzia kuhusu utawala bora. 72 00:04:34,000 --> 00:04:37,000 Na ni kitu ambacho watu wanazungumzia kuhusu rushwa, rushwa. 73 00:04:37,000 --> 00:04:39,000 Kila mara wanapo zungumzia kuhusu hili 74 00:04:39,000 --> 00:04:41,000 mara moja unafikiria Afrika. 75 00:04:41,000 --> 00:04:45,000 Hiyo ndio picha: Nchi za Afrika. Lakini ngoja niseme hili: 76 00:04:45,000 --> 00:04:51,000 iwapo Alams alifanikiwa kuhamisha dola za kimarekani milioni 8 kwenye akaunti mjini London -- 77 00:04:53,000 --> 00:04:57,000 kama watu wengine waliochukukua pesa wakikadiria kuwa 78 00:04:57,000 --> 00:05:01,000 kati ya bilioni 20 na 40 za pesa za nchi zinazoendelea 79 00:05:01,000 --> 00:05:04,000 ziko nje ya nchi katika nchi zilizoendelea – kama wanaweza kufanyi hivi, 80 00:05:04,000 --> 00:05:07,000 hiyo ni nini? Hiyo siyo rushwa? 81 00:05:08,000 --> 00:05:12,000 Katika nchi hii, kama ukipokea vitu vya wizi, haushitakiwi? 82 00:05:13,000 --> 00:05:16,000 Kwa hiyo tukiongelea kuhusu aina hii ya rushwa, hebu pia tufikirie kuhusu 83 00:05:16,000 --> 00:05:19,000 nini kinatokea katika upande mwingine wa dunia -- 84 00:05:19,000 --> 00:05:23,000 ambako pesa hizo zinakwenda na nini kifanyike ili kuweza kuzuia hili. 85 00:05:23,000 --> 00:05:26,000 Kuna jambo ninalifanyia kazi kwa sasa, pamoja na Benki ya Dunia, 86 00:05:26,000 --> 00:05:29,000 kuhusu kurudisha rasilimali, tunajaribu tuwezalo 87 00:05:29,000 --> 00:05:32,000 kurudisha pesa ambazo zimepelekwa nje ya nchi -- 88 00:05:32,000 --> 00:05:35,000 pesa za nchi zinazoendelea -- ili ziweze kurudishwa. 89 00:05:35,000 --> 00:05:38,000 Kama tutaweza kurudisha dola bilioni 20 ambazo ziko nje, 90 00:05:38,000 --> 00:05:41,000 litakuwa jambo zuri sana kwa baadhi ya nchi hizi 91 00:05:41,000 --> 00:05:44,000 kuliko misaada yote ikiwekwa pamoja. 92 00:05:44,000 --> 00:05:51,000 (Makofi). 93 00:05:51,000 --> 00:05:55,000 Kitu cha pili ninachotaka kuzungumzia ni nia ya mageuzi. 94 00:05:55,000 --> 00:05:59,000 Afrika, baada – wamechoka, tumechoka 95 00:05:59,000 --> 00:06:04,000 kuwa kitovu cha misaada kutoka kwa kila mtu. 96 00:06:04,000 --> 00:06:08,000 Tunashukuru, ila tunajua kuwa 97 00:06:08,000 --> 00:06:12,000 tunaweza kuchukua hatua juu ya uwezo wetu na kama tuna nia ya kufanya mabadiliko. 98 00:06:13,000 --> 00:06:17,000 Na kinachotokea katika nchi nyingi za Afrika sasa ni utambuzi kwamba 99 00:06:17,000 --> 00:06:21,000 hakuna anayeweza kufanya lolote ila sisi wenyewe. Ni lazima tufanye. 100 00:06:21,000 --> 00:06:25,000 Tunaweza kuwakaribisha washirika ambao wanaweza kutuunga mkono, lakini lazima tuanze wenyewe. 101 00:06:25,000 --> 00:06:28,000 Ni lazima turekebishe uchumi wetu, tubadilishe uongozi, 102 00:06:28,000 --> 00:06:34,000 tuwe na demokrasia zaidi, tuwe wazi kupokea mabadiliko na taarifa. 103 00:06:34,000 --> 00:06:36,000 Na hiki ndicho tumeanza kukifanya 104 00:06:36,000 --> 00:06:39,000 katika mojawapo kati ya nchi kubwa kabisa katika bara, Nigeria. 105 00:06:39,000 --> 00:06:42,000 Hakika, kama hauko Nigeria, hauko Afrika. 106 00:06:42,000 --> 00:06:43,000 Ninataka kuwaambia kuwa. 107 00:06:43,000 --> 00:06:44,000 (Kicheko). 108 00:06:44,000 --> 00:06:46,000 Mmoja kati ya waafrika wanne walio kusini mwa jangwa la Sahara ni Mnigeria, 109 00:06:48,000 --> 00:06:53,000 na ina watu milioni 140 – watu wenye pilika -- 110 00:06:54,000 --> 00:06:58,000 lakini watu wenye kuvutia. Hauwezi kuchoka. 111 00:06:58,000 --> 00:06:59,000 (Kicheko). 112 00:06:59,000 --> 00:07:01,000 Tulichoanza kufanya ni kujua kwamba 113 00:07:01,000 --> 00:07:03,000 tunaweza kuchukua hatua na kujibadili wenyewe. 114 00:07:04,000 --> 00:07:06,000 Na kwa msaada wa kiongozi 115 00:07:06,000 --> 00:07:09,000 ambaye alikuwa na nia, kwa wakati ule, ya kufanya mabadiliko, 116 00:07:09,000 --> 00:07:11,000 tunaandaa mpango madhubuti wa mabadiliko 117 00:07:11,000 --> 00:07:13,000 ambao tumeuandika wenyewe. 118 00:07:13,000 --> 00:07:16,000 Si Shirika la Kimataifa la Fedha. Wala Benki ya Dunia, 119 00:07:16,000 --> 00:07:19,000 ambako nilifanya kazi kwa miaka 21 na kufikia cheo cha makamu wa rais. 120 00:07:20,000 --> 00:07:22,000 Hakuna mtu anaweza kukufanyia. Inabidi ufanye mwenyewe. 121 00:07:22,000 --> 00:07:26,000 Tukaandaa mpango ambao kwanza, utafanya: kuiondoa serikali 122 00:07:26,000 --> 00:07:30,000 kwenye shughuli zisizo na manufaa -- zisizoihusu -- 123 00:07:30,000 --> 00:07:32,000 Serikali haitakiwi kufanya biashara 124 00:07:32,000 --> 00:07:33,000 ya uzalishaji na utoaji huduma 125 00:07:33,000 --> 00:07:36,000 kwasababu haina ufanisi na haina ujuzi. 126 00:07:36,000 --> 00:07:40,000 Kwa hiyo tuliamua kubinafsisha mashirika yetu mengi. 127 00:07:40,000 --> 00:07:44,000 (Makofi). 128 00:07:45,000 --> 00:07:49,000 Sisi -- matokeo yake, tuliamua kuwa na soko huria. 129 00:07:49,000 --> 00:07:52,000 Unaweza kuamini kuwa kabla ya mabadiliko haya -- 130 00:07:52,000 --> 00:07:56,000 ambayo yalianza mwishoni mwa mwaka 2003, wakati nilipoondoka Washington 131 00:07:56,000 --> 00:07:58,000 kwenda kushika nafasi ya Waziri wa Fedha -- 132 00:08:00,000 --> 00:08:04,000 tulikuwa na kampuni ya simu ambayo iliweza kutoa huduma za simu za mezani 133 00:08:04,000 --> 00:08:09,000 4,500 katika historia yake ya miaka 30? 134 00:08:09,000 --> 00:08:11,000 (Kicheko). 135 00:08:11,000 --> 00:08:14,000 Kuwa na simu katika nchi yangu lilikuwa ni jambo la kifahari sana. 136 00:08:14,000 --> 00:08:16,000 Usingeweza kupata. Ilibidi uhonge. 137 00:08:16,000 --> 00:08:18,000 Ilibidi ufanye kila uwezalo ili kupata simu. 138 00:08:18,000 --> 00:08:21,000 Rais Obasanjo aliunga mkono na kuzindua 139 00:08:21,000 --> 00:08:25,000 kulegezwa kwa masharti katika sekta ya mawasiliano 140 00:08:26,000 --> 00:08:34,000 tumepanda kutoka simu 4,500 za mezani kufikia simu milioni 32 zenye GSM, na zinaongezeka. 141 00:08:34,000 --> 00:08:39,000 Soko la mawasiliano la Nigeria ni la pili kwa ukuaji duniani kote,♪ 142 00:08:39,000 --> 00:08:44,000 ikiwa imetanguliwa na China. Tunapata uwekezaji wa takriban dola bilioni 1 kwa mwaka 143 00:08:44,000 --> 00:08:50,000 katika mawasiliano. Na hakuna mtu anayejua, isipokuwa kwa wajanja wachache. 144 00:08:50,000 --> 00:08:53,000 (Kicheko). 145 00:08:53,000 --> 00:08:57,000 Wajanja wa kwanza kuja 146 00:08:57,000 --> 00:08:59,000 walikuwa ni kampuni ya MTN ya Afrika Kusini. 147 00:08:59,000 --> 00:09:03,000 Katika miaka mitatu niliyokuwa Waziri wa Fedha, 148 00:09:03,000 --> 00:09:06,000 wamepata wastani wa dola milioni 360 kwa mwaka. 149 00:09:08,000 --> 00:09:14,000 milioni 360 katika soko – katika nchi ambayo ni maskini, 150 00:09:14,000 --> 00:09:18,000 yenye wastani wa pato la taifa chini ya dola 500. 151 00:09:19,000 --> 00:09:21,000 Kwahiyo soko lipo hapo. 152 00:09:21,000 --> 00:09:24,000 Walilifanya hili siri, lakini baadae wengine nao walianza kujua. 153 00:09:25,000 --> 00:09:28,000 Wanageria wenyewe walianzisha 154 00:09:28,000 --> 00:09:30,000 makampuni ya mawasiliano ya simu zisizotumia waya 155 00:09:30,000 --> 00:09:32,000 na wengine kama watatu wane hivi wameingia. 156 00:09:32,000 --> 00:09:35,000 Lakini bado kuna soko kubwa sana, 157 00:09:35,000 --> 00:09:38,000 na watu hawajui kuhusu hili, au hawataki kujua. 158 00:09:40,000 --> 00:09:42,000 Kwa hiyo ubinafsishaji ni jambo mojawapo tulilofanya. 159 00:09:43,000 --> 00:09:49,000 Kitu kingine tulichofanya ni kusimamia vizuri masuala yetu ya fedha. 160 00:09:50,000 --> 00:09:52,000 Kwasababu hakuna atakayekusaidia na kukuongoza 161 00:09:53,000 --> 00:09:56,000 iwapo hudhibiti fedha zako vizuri. 162 00:09:56,000 --> 00:10:00,000 Na Nigeria, ikiwa na sekta ya mafuta, ilikuwa na sifa 163 00:10:00,000 --> 00:10:05,000 ya rushwa na kutosimamia vizuri masuala ya fedha za umma. 164 00:10:05,000 --> 00:10:09,000 Je tulijaribu kufanya nini? Tulianzisha sheria ya fedha 165 00:10:10,000 --> 00:10:12,000 ambayo ilitenganisha bajeti yetu na bei ya mafuta. 166 00:10:12,000 --> 00:10:16,000 Zamani tulikuwa tumezoea kubajeti kutokana na kipato ambacho tulikipata kutokana na mafuta, 167 00:10:16,000 --> 00:10:21,000 kwasababu mafuta ndiyo sekta kuu ya mapato 168 00:10:21,000 --> 00:10:24,000 katika uchumi: asilimia 70 ya mapato yetu yanatokana na mafuta. 169 00:10:24,000 --> 00:10:28,000 Tulitenganisha hilo, na tulipofanya hivyo tulianza kubajeti 170 00:10:28,000 --> 00:10:31,000 kwa bei ambayo ilikuwa chini kidogo ya bei ya mafuta 171 00:10:31,000 --> 00:10:35,000 na kuhifadhi chochote cha ziada juu ya bei hiyo. 172 00:10:36,000 --> 00:10:39,000 Hatukuweza kujua kama tungeweza kufanikisha, ilikuwa ni utata sana.® 173 00:10:39,000 --> 00:10:42,000 Lakini kitu ambacho kilitokea haraka ilikuwa ni mabadiliko 174 00:10:42,000 --> 00:10:45,000 ambayo yalikuwepo kwa maendeleo yetu ya uchumi -- 175 00:10:45,000 --> 00:10:49,000 ambapo, hata kama bei ya mafuta ingekuwa juu, tungekuwa haraka sana. 176 00:10:49,000 --> 00:10:51,000 Wakati zilipoanguka, tulianguka. 177 00:10:51,000 --> 00:10:55,000 Na tulikuwa tunashindwa kulipia chochote, hata mishahara, katika uchumi. 178 00:10:56,000 --> 00:11:00,000 Hii ilisawazisha. Tuliweza kuweka akiba, kabla sijaondoka, 179 00:11:00,000 --> 00:11:06,000 dola bilioni 27. Ambapo – hii ilienda kwenye hazina yetu -- 180 00:11:06,000 --> 00:11:10,000 wakati nilipofika mwaka 2003, tulikuwa na dola billion 7 kwenye akiba. 181 00:11:11,000 --> 00:11:14,000 Na wakati naondoka, tulikuwa na karibu dola bilioni 30. Na 182 00:11:14,000 --> 00:11:17,000 tunavyoongea sasa, tuna dola bilioni 40 kwenye akiba 183 00:11:18,000 --> 00:11:22,000 hii ni kutokana na usimamizi mzuri wa fedha zetu. 184 00:11:23,000 --> 00:11:26,000 Hii inasaidia kutuliza uchumi wetu, kuufanya uwe imara. 185 00:11:26,000 --> 00:11:29,000 Thamani ya fedha yetu ilikuwa ikibadilika kila mara 186 00:11:29,000 --> 00:11:33,000 kwa sasa ipo angalau imara na kusimamiwa, ili wafanyabiashara 187 00:11:33,000 --> 00:11:38,000 wawe na uhakika wa bei katika uchumi. 188 00:11:40,000 --> 00:11:44,000 Tuliweza kudhibiti mfumuko bei kutoka asilimia 28 mpaka karibu asilimia 11. 189 00:11:46,000 --> 00:11:52,000 Na pato letu la taifa liliongezeka kutoka wastani wa asilimia 2.3 kwa muongo uliopita 190 00:11:52,000 --> 00:11:55,000 mpaka kufikia asilimia 6.5 sasa. 191 00:11:56,000 --> 00:11:59,000 Kwa hiyo mabadiliko yote tuliyoweza kufanya 192 00:11:59,000 --> 00:12:02,000 yameweza kuonekana kwa vitendo ambavyo vinaweza kuonekana katika uchumi. 193 00:12:02,000 --> 00:12:06,000 Na kitu cha muhimu zaidi, ni kwasababu tunataka kuondokana na mafuta 194 00:12:06,000 --> 00:12:08,000 na kupanua wigo zaidi – na kuna fursa nyingi sana 195 00:12:08,000 --> 00:12:11,000 katika nchi hii kubwa, kama ilivyo katika nchi nyingine za Afrika -- 196 00:12:13,000 --> 00:12:16,000 kilichotia fora zaidi ni huu ukuaji haukutoka 197 00:12:16,000 --> 00:12:19,000 kwenye sekta mafuta pekee, bali sekta nyingine pia. 198 00:12:19,000 --> 00:12:22,000 Kilimo kilikuwa kwa wastani wa asilimi 8. 199 00:12:22,000 --> 00:12:26,000 Sekta ya mawasiliano ilikuwa, makazi na ujenzi, 200 00:12:26,000 --> 00:12:31,000 na ninaweza kuendelea zaidi na zaidi. Na hii ni kuwaonyesha kwamba 201 00:12:31,000 --> 00:12:33,000 uchumi wako unaporekebishika, 202 00:12:33,000 --> 00:12:37,000 fursa katika sekta nyingine zipo nyingi. 203 00:12:38,000 --> 00:12:41,000 Tuna frusa katika kilimo, kama nilivyosema. 204 00:12:41,000 --> 00:12:45,000 Tuna fursa katika madini. Tuna madini mengi 205 00:12:45,000 --> 00:12:48,000 ambako hakuna mtu amewekeza katika utafutaji. Tumegundua 206 00:12:48,000 --> 00:12:51,000 kuwa bila kuwa na sera sahihi za kuwezesha, 207 00:12:51,000 --> 00:12:54,000 hilo halitawezekana. Sasa tuna sheria ya uchimbaji madini 208 00:12:54,000 --> 00:12:57,000 ambayo inalinganishwa na sheria nyingine bora duniani. 209 00:12:58,000 --> 00:13:00,000 Tuna fursa katika makazi na usimamizi wa majumba. 210 00:13:00,000 --> 00:13:03,000 Kulikuwa hakuna chochote katika nchi ya watu milioni 140 -- 211 00:13:04,000 --> 00:13:09,000 hakuna maduka makubwa kama myajuavyo hapa. 212 00:13:10,000 --> 00:13:13,000 Hii inaweza kuwa fursa kwa mtu fulani 213 00:13:13,000 --> 00:13:15,000 ambayo ilitia chachu ya kufikiria kwa watu. 214 00:13:16,000 --> 00:13:19,000 Sasa tuna mazingira ambayo biashara katika maduka haya makubwa 215 00:13:19,000 --> 00:13:22,000 yanapata faida mara nne ya ilivyokadiriwa. 216 00:13:23,000 --> 00:13:26,000 Kwa hiyo mambo makubwa kwenye ujenzi, mali isiyohamishika, 217 00:13:26,000 --> 00:13:28,000 Masoko ya rehani. Huduma za fedha 218 00:13:29,000 --> 00:13:33,000 tulikuwa na Benki 89. Nyingi hazifanyi biashara iliyokusudiwa. 219 00:13:33,000 --> 00:13:37,000 Tulizizatiti kutoka 89 kufikia Benki 25 kwa 220 00:13:37,000 --> 00:13:42,000 waongeze mtaji wao -- gawio la mtaji. 221 00:13:42,000 --> 00:13:47,000 Ilikuwa kutoka dola milioni 25 mpaka dola milioni 150. 222 00:13:47,000 --> 00:13:51,000 Benki, Benki hizi sasa zimejizatiti na kuimarishwa 223 00:13:51,000 --> 00:13:55,000 mfumo wa Benki umevutia wamekezaji wengi kutoka nje. 224 00:13:55,000 --> 00:13:59,000 Benki ya Barclays kutoka Uingereza inaingiza milioni 500. 225 00:13:59,000 --> 00:14:03,000 Standard Chartered imeingiza milioni 140. 226 00:14:03,000 --> 00:14:06,000 Ninaweza kuendelea zaidi. Dola zaidi na zaidi, ndani ya mfumo. 227 00:14:06,000 --> 00:14:08,000 Tunafanya hivyo hivyo kwenye sekta ya bima. 228 00:14:08,000 --> 00:14:11,000 Kwa hiyo kwenye huduma za fedha, kuna fursa kubwa zaidi. 229 00:14:11,000 --> 00:14:17,000 Kwenye utalii, katika nchi nyingi za Kiafrika, ni fursa kubwa. 230 00:14:17,000 --> 00:14:20,000 Na hii ndiyo sababu kubwa ya kuwa watu wengi wanaifahamu Afrika Mashariki kwa: 231 00:14:21,000 --> 00:14:24,000 wanyama pori, tembo na kadhalika. 232 00:14:24,000 --> 00:14:26,000 Lakini kusimimamia soko la utalii ili 233 00:14:26,000 --> 00:14:29,000 liweze kuwanufaisha watu ni muhimu sana. 234 00:14:30,000 --> 00:14:33,000 Sasa ninachojaribu kusema ni nini? Najaribu kuwaambia 235 00:14:33,000 --> 00:14:36,000 kuna wimbi jipya katika bara. 236 00:14:36,000 --> 00:14:41,000 Wimbi la uwazi na demokrasia ambapo tangu mwaka 2000, 237 00:14:41,000 --> 00:14:43,000 zaidi ya theluthi mbili ya nchi za Afrika zimefanya 238 00:14:43,000 --> 00:14:45,000 uchaguzi wa kidemokrasia wa vyama vingi. 239 00:14:46,000 --> 00:14:49,000 Si zote zilikuwa kamilifu, au zitakuwa, 240 00:14:49,000 --> 00:14:51,000 lakini mwelekeo uko wazi. 241 00:14:51,000 --> 00:14:55,000 Ninajaribu kuwaelezea kwamba toka miaka mitatu iliyopita 242 00:14:55,000 --> 00:14:58,000 wastani wa ukuaji wa uchumi katika bara umeongezeka 243 00:14:58,000 --> 00:15:02,000 kutoka karibu asilimia 2.5 mpaka asilimia 5 kwa mwaka. 244 00:15:02,000 --> 00:15:06,000 Hii ni bora zaidi ya ufanisi wa nchi nyingi za OECD. 245 00:15:07,000 --> 00:15:11,000 Kwahiyo ni wazi kwamba mambo yanabadilika. 246 00:15:11,000 --> 00:15:13,000 Migogoro imepungua barani; 247 00:15:14,000 --> 00:15:16,000 kutoka migogoro 12 kwa muongo uliopita, 248 00:15:16,000 --> 00:15:18,000 kufikia migogoro mitatu au minne, 249 00:15:18,000 --> 00:15:21,000 Mojawapo ya migogoro mibaya zaidi, kwa hakika, ni ule wa Darfur. 250 00:15:21,000 --> 00:15:24,000 Na kama ujuavyo, kuna athari kwa majirani, iwapo 251 00:15:24,000 --> 00:15:26,000 kuna jambo linatokea upande mmoja wa bara, 252 00:15:26,000 --> 00:15:29,000 inaonekana kama bara zima limeathirika. 253 00:15:29,000 --> 00:15:32,000 Lakini ni vema muelewe kwamba hili bara -- 254 00:15:32,000 --> 00:15:38,000 ni bara lenye nchi nyingi na si nchi moja. 255 00:15:38,000 --> 00:15:40,000 Na iwapo tuna migogoro mitatu minne hivi, 256 00:15:40,000 --> 00:15:43,000 ina maana kuwa kuna fursa nyingi za kuwekeza 257 00:15:43,000 --> 00:15:50,000 katika uchumi ulio imara, unaokua na wenye kusisimua 258 00:15:50,000 --> 00:15:53,000 ambako kuna fursa nyingi sana. 259 00:15:54,000 --> 00:15:58,000 Ningependa kutoa dokezo moja kuhusu uwekezaji huu. 260 00:15:59,000 --> 00:16:01,000 Namna nzuri ya kuisaidia Afrika sasa 261 00:16:02,000 --> 00:16:05,000 ni kuwasaidia waweze kusimama wenyewe. 262 00:16:05,000 --> 00:16:09,000 Na namna nzuri ya kufanya hivyo ni kusaidia kuleta ajira. 263 00:16:10,000 --> 00:16:14,000 Hakuna tatizo katika kupambana na malaria na kuwekeza pesa kwenye hilo 264 00:16:14,000 --> 00:16:18,000 na kuokoa maisha ya watoto. Sina maana hiyo. Hilo ni sawa. 265 00:16:19,000 --> 00:16:23,000 Lakini fikiria tofauti itakayokuwa kwenye familia: iwapo wazazi wanaweza kuwa na ajira 266 00:16:23,000 --> 00:16:25,000 na wakahakikisha watoto wao wanakwenda shule, 267 00:16:25,000 --> 00:16:28,000 kwamba wanaweza kununua dawa za kupambana na magonjwa wao wenyewe. 268 00:16:28,000 --> 00:16:32,000 Kama tunaweza kuwekeza kwenye maeneo ambayo nyinyi wenyewe mnapata faida 269 00:16:32,000 --> 00:16:37,000 wakati huo huo mkitengeneza ajira na kuwasaidia watu wasimame wenyewe, 270 00:16:37,000 --> 00:16:42,000 hii siyo fursa nzuri? Hii si ndiyo njia ya kufuata? 271 00:16:42,000 --> 00:16:45,000 Na nataka kusema jambo kuhusu watu bora zaidi wa kuwawekezea 272 00:16:45,000 --> 00:16:47,000 katika bara hili ni wanawake. 273 00:16:48,000 --> 00:16:55,000 (Makofi). 274 00:16:55,000 --> 00:17:00,000 Nina CD hapa. Samahani sikusema kwa wakati muafaka. 275 00:17:00,000 --> 00:17:02,000 Lakini, ningependa mngekuwa mmeiangalia. 276 00:17:02,000 --> 00:17:05,000 Inasema, "Afrika: Iko wazi kwa Biashara." 277 00:17:06,000 --> 00:17:09,000 Na video hii imeshinda tuzo 278 00:17:09,000 --> 00:17:11,000 kama makala bora ya mwaka. 279 00:17:11,000 --> 00:17:13,000 Elewa kwamba mwanamke aliyetengeneza makala hii 280 00:17:13,000 --> 00:17:18,000 atakuwa Tanzania, ambako watakuwa na kongamano mwezi Juni. 281 00:17:19,000 --> 00:17:24,000 Lakini hii inakuonyesha kwamba Waafrika, na hususani wanawake wa Afrika, ambao 282 00:17:24,000 --> 00:17:29,000 pamoja na matatizo yote wameweza kuanzisha biashara, nyingine ni za kiwango cha kimataifa. 283 00:17:29,000 --> 00:17:32,000 Mmoja kati ya wanawake katika video hii, Adenike Ogunlesi, 284 00:17:32,000 --> 00:17:34,000 anashona nguo za watoto 285 00:17:34,000 --> 00:17:39,000 kitu ambacho alianza kama kujifurahisha na ikakua na kuwa biashara. 286 00:17:39,000 --> 00:17:42,000 Akichanganya vitambaa vya Kiafrika ambavyo tunavyo, 287 00:17:43,000 --> 00:17:44,000 na vitambaa vingine kutoka sehemu nyingine. 288 00:17:44,000 --> 00:17:49,000 Na hivyo, atatengeneza suruali kwa kutumia vitambaa vizito, 289 00:17:49,000 --> 00:17:53,000 ikiwa imechanganywa na vitambaa vya kiafrika. Ni ubunifu mzuri sana. 290 00:17:55,000 --> 00:17:58,000 Amefikai hatua ambapo anapata zabuni kutoka Wal-Mart. 291 00:17:59,000 --> 00:18:00,000 (Kicheko). 292 00:18:01,000 --> 00:18:03,000 Kwa nguo 10,000 293 00:18:04,000 --> 00:18:08,000 Kwa hiyo hii inawaonyesha kuwa tuna watu wenye uwezo wa kufanya mambo. 294 00:18:08,000 --> 00:18:13,000 Wanawake wana juhudi, wako makini; wanachapa kazi. 295 00:18:13,000 --> 00:18:15,000 Naweza kuendelea kwa kutoa mifano: 296 00:18:15,000 --> 00:18:19,000 Beatrice Gakuba wa Rwanda, alifungua biashara ya maua 297 00:18:19,000 --> 00:18:24,000 na sasa anayasafirisha kwenye mnada wa udachi huko Amsterdam kila asubuhi, 298 00:18:24,000 --> 00:18:28,000 na ameajiri wanawake na wanaume takriban 200 kumsaidia kazi. 299 00:18:29,000 --> 00:18:33,000 Hata hivyo, wengi wao, wana kiu ya kupata mtaji wa kupanua biashara zao, 300 00:18:34,000 --> 00:18:37,000 kwasababu hakuna anayeamini nje ya nchi zetu 301 00:18:37,000 --> 00:18:42,000 tunaweza kufanya mambo ya maana. Hakuna mtu anayefikiria kwa mtazamo wa masoko. 302 00:18:42,000 --> 00:18:45,000 Hakuna anyefikiria kuna fursa 303 00:18:45,000 --> 00:18:48,000 Nimesimama hapa kuwaambia wale waliochelewa jahazi kwa sasa, 304 00:18:48,000 --> 00:18:50,000 watalikosa milele. 305 00:18:50,000 --> 00:18:56,000 Kwa hiyo iwapo unataka kuwa Afrika, fikiria kuwekeza. 306 00:18:57,000 --> 00:19:03,000 Wafikirie akina Beatrice, wafikirie kina Adenike wa dunia hii. 307 00:19:03,000 --> 00:19:06,000 ambao wanafanya mambo makubwa ambayo yanawasogeza 308 00:19:06,000 --> 00:19:09,000 katika uchumi wa dunia, wakati huo huo wakihakikisha 309 00:19:09,000 --> 00:19:12,000 wanawake wenzao na wanaume wanapata ajira. 310 00:19:12,000 --> 00:19:14,000 na kwamba watoto katika familia hizo wanapata elimu 311 00:19:14,000 --> 00:19:17,000 kwa sababu wazazi wao wanapata kipato cha kuridhisha 312 00:19:18,000 --> 00:19:22,000 Kwa hiyo nina wakaribisha kuja kutafuta fursa 313 00:19:23,000 --> 00:19:27,000 Mtakapo kwenda Tanzania, sikilizeni kwa makini, 314 00:19:27,000 --> 00:19:31,000 kwasababu nina hakika mtasikia kuhusu fursa mbalimbali zilizopo 315 00:19:31,000 --> 00:19:36,000 ili muweze kushiriki katika kufanya mambo mazuri 316 00:19:36,000 --> 00:19:41,000 kwa bara hili, kwa watu wake na kwenu wenyewe 317 00:19:41,000 --> 00:19:42,000 Asanteni sana. 318 00:19:42,000 --> 00:19:50,000 (Makofi)