WEBVTT 00:00:05.000 --> 00:00:08.000 Asante sana Chris. Kila mtu aliyekuja hapa 00:00:08.000 --> 00:00:12.000 alisema kuwa anaogopa. Sijui kama na mimi ninaogopa, 00:00:12.000 --> 00:00:16.000 lakini hii ni mara yangu ya kwanza kuhutubia hadhara kama hii. 00:00:16.000 --> 00:00:20.000 Na sina teknolojia yeyote ya kisasa kwa ajili yenu ili muweze kuiangalia. 00:00:20.000 --> 00:00:23.000 Hakuna kielezopicha, kwa hiyo itabidi mnivumilie. 00:00:23.000 --> 00:00:26.000 (Kicheko). NOTE Paragraph 00:00:26.000 --> 00:00:32.000 Ninachotaka kufanya asubuhi hii ni kuwasimulia hadithi kadhaa 00:00:32.000 --> 00:00:35.000 na kuongelea kuhusu Afrika iliyo tofauti. 00:00:35.000 --> 00:00:39.000 Tayari asubuhi hii kulikuwa na madokezo kuhusu Afrika 00:00:39.000 --> 00:00:44.000 unayoyasikia kila mara: Afrika ya VVU/UKIMWI, 00:00:44.000 --> 00:00:50.000 Afrika ya malaria, Afrika ya umaskini, Afrika ya migongano, 00:00:50.000 --> 00:00:53.000 na Afrika ya maafa. NOTE Paragraph 00:00:53.000 --> 00:00:57.000 Ingawa kuna ukweli kwamba mambo hayo yanatokea, 00:00:57.000 --> 00:01:01.000 kuna Afrika ambayo hamuisikii sana. 00:01:01.000 --> 00:01:05.000 Na saa nyingine nashangazwa na kujiuliza kwanini. 00:01:05.000 --> 00:01:09.000 Hii ni Afrika ambayo inabadilika, ambayo Chris ameidokezea. 00:01:09.000 --> 00:01:11.000 Hii ni Afrika yenye fursa. 00:01:11.000 --> 00:01:14.000 Hii ni Afrika ambayo watu wanataka kuchukua hatua juu ya 00:01:14.000 --> 00:01:16.000 maisha na uwezo wao. 00:01:16.000 --> 00:01:19.000 Na hii ndio Afrika ambayo watu wanatafuta kuingia ubia 00:01:19.000 --> 00:01:23.000 kufanya hivyo. Na hili haswa ndilo ninalotaka kuzungumzia leo. NOTE Paragraph 00:01:23.000 --> 00:01:25.000 Ningependa kuanza kwa kuwaambia 00:01:25.000 --> 00:01:27.000 habari kuhusu mabadiliko hayo Afrika. 00:01:28.000 --> 00:01:33.000 Mnamo 15 Septemba 2005, Bwana Diepreye Alamieyeseigha, 00:01:33.000 --> 00:01:37.000 Gavana wa jimbo moja lenye utajiri wa mafuta huko Nigeria, 00:01:37.000 --> 00:01:44.000 alikamatwa na Polisi wa mji wa London alipokuwa matembizini mjini London. 00:01:44.000 --> 00:01:49.000 Alikamatwa kwasababu kulikuwa na hamisho la kiasi cha dola za kimarekani milioni 8 00:01:49.000 --> 00:01:52.000 ambazo zilienda katika akaunti hewa 00:01:52.000 --> 00:01:55.000 ambazo alikuwa akizimiliki yeye pamoja na familia yake. 00:01:56.000 --> 00:01:58.000 Kukamatwa kwake kuliwezekana kwasababu kulikuwa na ushirikiano 00:01:58.000 --> 00:02:01.000 baina ya Polisi wa mji wa London 00:02:01.000 --> 00:02:04.000 na Tume ya Uhalifu wa Kiuchumi na Fedha ya Nigeria -- 00:02:04.000 --> 00:02:11.000 inayoongozwa na mtu wenye uwezo na ujasiri: Bwana Nuhu Ribadu. 00:02:11.000 --> 00:02:14.000 Alamieyeseigha alikamatwa mjini London. 00:02:14.000 --> 00:02:18.000 Kutokana na udhaifu, alifanikiwa kutoroka akiwa amevalia kama mwanamke 00:02:18.000 --> 00:02:21.000 na kukimbia kutoka London kurudi Nigeria ambako, 00:02:21.000 --> 00:02:25.000 kwa mujibu wa katiba, wale walio madarakani 00:02:25.000 --> 00:02:27.000 kama magavana, rais – kama ilivyo kwenye nchi nyingi -- 00:02:27.000 --> 00:02:32.000 wana kinga na hawawezi kushtakiwa. Lakini nini kilitokea: 00:02:32.000 --> 00:02:36.000 watu walikasirishwa sana na tabia hii na iliwezekana 00:02:36.000 --> 00:02:42.000 kwa sheria za jimbo lake kumvua madaraka. NOTE Paragraph 00:02:43.000 --> 00:02:45.000 Leo, Alams – kama tumuitavyo kwa kifupi – yuko jela. 00:02:46.000 --> 00:02:51.000 Hii ni hadithi kuhusu ukweli kwamba watu wa Afrika 00:02:51.000 --> 00:02:56.000 hawako tayari tena kuvumilia rushwa kutoka kwa viongozi wao. 00:02:57.000 --> 00:03:02.000 Hii ni hadithi kuhusu ukweli kwamba watu wanataka rasilimali zao 00:03:02.000 --> 00:03:07.000 zidhibitiwe vizuri kwa manufaa yao, na sio kupelekwa sehemu 00:03:07.000 --> 00:03:10.000 ambako itawanufaisha mabwanyenye wachache. 00:03:10.000 --> 00:03:14.000 Kwa hiyo, unaposikia kuhusu Afrika ya rushwa -- 00:03:14.000 --> 00:03:18.000 rushwa kila mara – Ninataka mfahamu kuwa watu 00:03:18.000 --> 00:03:21.000 na serikali wanajitahidi sana kupambana na tatizo hili 00:03:21.000 --> 00:03:25.000 katika baadhi ya nchi, na kwamba mafanikio yanaanza kuonekana. NOTE Paragraph 00:03:25.000 --> 00:03:28.000 Inamaana kuwa tatizo limekwisha? Jibu ni hapana. 00:03:28.000 --> 00:03:32.000 Bado kuna safari ndefu, lakini pia kuna nia. 00:03:32.000 --> 00:03:36.000 Mafanikio yanaandikwa juu ya mapigano ya jambo hili muhimu. 00:03:36.000 --> 00:03:38.000 Kwa hiyo mnaposikia kuhusu rushwa, 00:03:38.000 --> 00:03:41.000 msifikiri kwamba hakuna linalotendeka kuhusu hili -- 00:03:41.000 --> 00:03:44.000 na kwamba hamuwezi kufanya kazi katika nchi yeyote Afrika 00:03:44.000 --> 00:03:47.000 kwasababu ya rushwa. Hiyo si kweli. 00:03:47.000 --> 00:03:53.000 Kuna nia ya kupambana na rushwa, na katika nchi nyingi, mapambano hayo yanaendelea 00:03:53.000 --> 00:03:57.000 na mafanikio yanaonekana. Katika nchi nyingine, kama yangu, 00:03:57.000 --> 00:04:00.000 ambako kumekuwa na historia ndefu ya kidikteta nchini Nigeria, 00:04:00.000 --> 00:04:04.000 mapambano bado yanaendelea, na bado tuna safari ndefu. NOTE Paragraph 00:04:04.000 --> 00:04:08.000 Ukweli wa mambo ni kwamba mapambano bado yanaendelea. 00:04:09.000 --> 00:04:11.000 Matokeo yanaonekana: 00:04:11.000 --> 00:04:15.000 tathmini huru ya Benki ya Dunia na mashirika mengine 00:04:15.000 --> 00:04:19.000 inaonyesha kuwa mwelekeo juu ya rushwa unapungua 00:04:19.000 --> 00:04:22.000 na utawala unarekebika. 00:04:22.000 --> 00:04:26.000 Utafiti uliofanywa na Tume ya Uchumi ya Afrika unaonyesha 00:04:26.000 --> 00:04:30.000 wazi mwelekeo mzuri wa utawala katika nchi 28 za Afrika. NOTE Paragraph 00:04:30.000 --> 00:04:32.000 Ngoja niseme kitu kimoja zaidi 00:04:32.000 --> 00:04:34.000 kabla sijamaliza kuzungumzia kuhusu utawala bora. 00:04:34.000 --> 00:04:37.000 Na ni kitu ambacho watu wanazungumzia kuhusu rushwa, rushwa. 00:04:37.000 --> 00:04:39.000 Kila mara wanapo zungumzia kuhusu hili 00:04:39.000 --> 00:04:41.000 mara moja unafikiria Afrika. 00:04:41.000 --> 00:04:45.000 Hiyo ndio picha: Nchi za Afrika. Lakini ngoja niseme hili: 00:04:45.000 --> 00:04:51.000 iwapo Alams alifanikiwa kuhamisha dola za kimarekani milioni 8 kwenye akaunti mjini London -- 00:04:53.000 --> 00:04:57.000 kama watu wengine waliochukukua pesa wakikadiria kuwa 00:04:57.000 --> 00:05:01.000 kati ya bilioni 20 na 40 za pesa za nchi zinazoendelea 00:05:01.000 --> 00:05:04.000 ziko nje ya nchi katika nchi zilizoendelea – kama wanaweza kufanyi hivi, 00:05:04.000 --> 00:05:07.000 hiyo ni nini? Hiyo siyo rushwa? 00:05:08.000 --> 00:05:12.000 Katika nchi hii, kama ukipokea vitu vya wizi, haushitakiwi? 00:05:13.000 --> 00:05:16.000 Kwa hiyo tukiongelea kuhusu aina hii ya rushwa, hebu pia tufikirie kuhusu 00:05:16.000 --> 00:05:19.000 nini kinatokea katika upande mwingine wa dunia -- 00:05:19.000 --> 00:05:23.000 ambako pesa hizo zinakwenda na nini kifanyike ili kuweza kuzuia hili. 00:05:23.000 --> 00:05:26.000 Kuna jambo ninalifanyia kazi kwa sasa, pamoja na Benki ya Dunia, 00:05:26.000 --> 00:05:29.000 kuhusu kurudisha rasilimali, tunajaribu tuwezalo 00:05:29.000 --> 00:05:32.000 kurudisha pesa ambazo zimepelekwa nje ya nchi -- 00:05:32.000 --> 00:05:35.000 pesa za nchi zinazoendelea -- ili ziweze kurudishwa. 00:05:35.000 --> 00:05:38.000 Kama tutaweza kurudisha dola bilioni 20 ambazo ziko nje, 00:05:38.000 --> 00:05:41.000 litakuwa jambo zuri sana kwa baadhi ya nchi hizi 00:05:41.000 --> 00:05:44.000 kuliko misaada yote ikiwekwa pamoja. 00:05:44.000 --> 00:05:51.000 (Makofi). NOTE Paragraph 00:05:51.000 --> 00:05:55.000 Kitu cha pili ninachotaka kuzungumzia ni nia ya mageuzi. 00:05:55.000 --> 00:05:59.000 Afrika, baada – wamechoka, tumechoka 00:05:59.000 --> 00:06:04.000 kuwa kitovu cha misaada kutoka kwa kila mtu. 00:06:04.000 --> 00:06:08.000 Tunashukuru, ila tunajua kuwa 00:06:08.000 --> 00:06:12.000 tunaweza kuchukua hatua juu ya uwezo wetu na kama tuna nia ya kufanya mabadiliko. 00:06:13.000 --> 00:06:17.000 Na kinachotokea katika nchi nyingi za Afrika sasa ni utambuzi kwamba 00:06:17.000 --> 00:06:21.000 hakuna anayeweza kufanya lolote ila sisi wenyewe. Ni lazima tufanye. 00:06:21.000 --> 00:06:25.000 Tunaweza kuwakaribisha washirika ambao wanaweza kutuunga mkono, lakini lazima tuanze wenyewe. 00:06:25.000 --> 00:06:28.000 Ni lazima turekebishe uchumi wetu, tubadilishe uongozi, 00:06:28.000 --> 00:06:34.000 tuwe na demokrasia zaidi, tuwe wazi kupokea mabadiliko na taarifa. NOTE Paragraph 00:06:34.000 --> 00:06:36.000 Na hiki ndicho tumeanza kukifanya 00:06:36.000 --> 00:06:39.000 katika mojawapo kati ya nchi kubwa kabisa katika bara, Nigeria. 00:06:39.000 --> 00:06:42.000 Hakika, kama hauko Nigeria, hauko Afrika. 00:06:42.000 --> 00:06:43.000 Ninataka kuwaambia kuwa. 00:06:43.000 --> 00:06:44.000 (Kicheko). 00:06:44.000 --> 00:06:46.000 Mmoja kati ya waafrika wanne walio kusini mwa jangwa la Sahara ni Mnigeria, 00:06:48.000 --> 00:06:53.000 na ina watu milioni 140 – watu wenye pilika -- 00:06:54.000 --> 00:06:58.000 lakini watu wenye kuvutia. Hauwezi kuchoka. 00:06:58.000 --> 00:06:59.000 (Kicheko). NOTE Paragraph 00:06:59.000 --> 00:07:01.000 Tulichoanza kufanya ni kujua kwamba 00:07:01.000 --> 00:07:03.000 tunaweza kuchukua hatua na kujibadili wenyewe. 00:07:04.000 --> 00:07:06.000 Na kwa msaada wa kiongozi 00:07:06.000 --> 00:07:09.000 ambaye alikuwa na nia, kwa wakati ule, ya kufanya mabadiliko, 00:07:09.000 --> 00:07:11.000 tunaandaa mpango madhubuti wa mabadiliko 00:07:11.000 --> 00:07:13.000 ambao tumeuandika wenyewe. 00:07:13.000 --> 00:07:16.000 Si Shirika la Kimataifa la Fedha. Wala Benki ya Dunia, 00:07:16.000 --> 00:07:19.000 ambako nilifanya kazi kwa miaka 21 na kufikia cheo cha makamu wa rais. 00:07:20.000 --> 00:07:22.000 Hakuna mtu anaweza kukufanyia. Inabidi ufanye mwenyewe. NOTE Paragraph 00:07:22.000 --> 00:07:26.000 Tukaandaa mpango ambao kwanza, utafanya: kuiondoa serikali 00:07:26.000 --> 00:07:30.000 kwenye shughuli zisizo na manufaa -- zisizoihusu -- 00:07:30.000 --> 00:07:32.000 Serikali haitakiwi kufanya biashara 00:07:32.000 --> 00:07:33.000 ya uzalishaji na utoaji huduma 00:07:33.000 --> 00:07:36.000 kwasababu haina ufanisi na haina ujuzi. 00:07:36.000 --> 00:07:40.000 Kwa hiyo tuliamua kubinafsisha mashirika yetu mengi. 00:07:40.000 --> 00:07:44.000 (Makofi). 00:07:45.000 --> 00:07:49.000 Sisi -- matokeo yake, tuliamua kuwa na soko huria. 00:07:49.000 --> 00:07:52.000 Unaweza kuamini kuwa kabla ya mabadiliko haya -- 00:07:52.000 --> 00:07:56.000 ambayo yalianza mwishoni mwa mwaka 2003, wakati nilipoondoka Washington 00:07:56.000 --> 00:07:58.000 kwenda kushika nafasi ya Waziri wa Fedha -- 00:08:00.000 --> 00:08:04.000 tulikuwa na kampuni ya simu ambayo iliweza kutoa huduma za simu za mezani 00:08:04.000 --> 00:08:09.000 4,500 katika historia yake ya miaka 30? 00:08:09.000 --> 00:08:11.000 (Kicheko). NOTE Paragraph 00:08:11.000 --> 00:08:14.000 Kuwa na simu katika nchi yangu lilikuwa ni jambo la kifahari sana. 00:08:14.000 --> 00:08:16.000 Usingeweza kupata. Ilibidi uhonge. 00:08:16.000 --> 00:08:18.000 Ilibidi ufanye kila uwezalo ili kupata simu. 00:08:18.000 --> 00:08:21.000 Rais Obasanjo aliunga mkono na kuzindua 00:08:21.000 --> 00:08:25.000 kulegezwa kwa masharti katika sekta ya mawasiliano 00:08:26.000 --> 00:08:34.000 tumepanda kutoka simu 4,500 za mezani kufikia simu milioni 32 zenye GSM, na zinaongezeka. 00:08:34.000 --> 00:08:39.000 Soko la mawasiliano la Nigeria ni la pili kwa ukuaji duniani kote,♪ 00:08:39.000 --> 00:08:44.000 ikiwa imetanguliwa na China. Tunapata uwekezaji wa takriban dola bilioni 1 kwa mwaka 00:08:44.000 --> 00:08:50.000 katika mawasiliano. Na hakuna mtu anayejua, isipokuwa kwa wajanja wachache. 00:08:50.000 --> 00:08:53.000 (Kicheko). NOTE Paragraph 00:08:53.000 --> 00:08:57.000 Wajanja wa kwanza kuja 00:08:57.000 --> 00:08:59.000 walikuwa ni kampuni ya MTN ya Afrika Kusini. 00:08:59.000 --> 00:09:03.000 Katika miaka mitatu niliyokuwa Waziri wa Fedha, 00:09:03.000 --> 00:09:06.000 wamepata wastani wa dola milioni 360 kwa mwaka. 00:09:08.000 --> 00:09:14.000 milioni 360 katika soko – katika nchi ambayo ni maskini, 00:09:14.000 --> 00:09:18.000 yenye wastani wa pato la taifa chini ya dola 500. 00:09:19.000 --> 00:09:21.000 Kwahiyo soko lipo hapo. 00:09:21.000 --> 00:09:24.000 Walilifanya hili siri, lakini baadae wengine nao walianza kujua. 00:09:25.000 --> 00:09:28.000 Wanageria wenyewe walianzisha 00:09:28.000 --> 00:09:30.000 makampuni ya mawasiliano ya simu zisizotumia waya 00:09:30.000 --> 00:09:32.000 na wengine kama watatu wane hivi wameingia. 00:09:32.000 --> 00:09:35.000 Lakini bado kuna soko kubwa sana, 00:09:35.000 --> 00:09:38.000 na watu hawajui kuhusu hili, au hawataki kujua. 00:09:40.000 --> 00:09:42.000 Kwa hiyo ubinafsishaji ni jambo mojawapo tulilofanya. NOTE Paragraph 00:09:43.000 --> 00:09:49.000 Kitu kingine tulichofanya ni kusimamia vizuri masuala yetu ya fedha. 00:09:50.000 --> 00:09:52.000 Kwasababu hakuna atakayekusaidia na kukuongoza 00:09:53.000 --> 00:09:56.000 iwapo hudhibiti fedha zako vizuri. 00:09:56.000 --> 00:10:00.000 Na Nigeria, ikiwa na sekta ya mafuta, ilikuwa na sifa 00:10:00.000 --> 00:10:05.000 ya rushwa na kutosimamia vizuri masuala ya fedha za umma. 00:10:05.000 --> 00:10:09.000 Je tulijaribu kufanya nini? Tulianzisha sheria ya fedha 00:10:10.000 --> 00:10:12.000 ambayo ilitenganisha bajeti yetu na bei ya mafuta. 00:10:12.000 --> 00:10:16.000 Zamani tulikuwa tumezoea kubajeti kutokana na kipato ambacho tulikipata kutokana na mafuta, 00:10:16.000 --> 00:10:21.000 kwasababu mafuta ndiyo sekta kuu ya mapato 00:10:21.000 --> 00:10:24.000 katika uchumi: asilimia 70 ya mapato yetu yanatokana na mafuta. 00:10:24.000 --> 00:10:28.000 Tulitenganisha hilo, na tulipofanya hivyo tulianza kubajeti 00:10:28.000 --> 00:10:31.000 kwa bei ambayo ilikuwa chini kidogo ya bei ya mafuta 00:10:31.000 --> 00:10:35.000 na kuhifadhi chochote cha ziada juu ya bei hiyo. 00:10:36.000 --> 00:10:39.000 Hatukuweza kujua kama tungeweza kufanikisha, ilikuwa ni utata sana.® 00:10:39.000 --> 00:10:42.000 Lakini kitu ambacho kilitokea haraka ilikuwa ni mabadiliko 00:10:42.000 --> 00:10:45.000 ambayo yalikuwepo kwa maendeleo yetu ya uchumi -- 00:10:45.000 --> 00:10:49.000 ambapo, hata kama bei ya mafuta ingekuwa juu, tungekuwa haraka sana. 00:10:49.000 --> 00:10:51.000 Wakati zilipoanguka, tulianguka. 00:10:51.000 --> 00:10:55.000 Na tulikuwa tunashindwa kulipia chochote, hata mishahara, katika uchumi. 00:10:56.000 --> 00:11:00.000 Hii ilisawazisha. Tuliweza kuweka akiba, kabla sijaondoka, 00:11:00.000 --> 00:11:06.000 dola bilioni 27. Ambapo – hii ilienda kwenye hazina yetu -- 00:11:06.000 --> 00:11:10.000 wakati nilipofika mwaka 2003, tulikuwa na dola billion 7 kwenye akiba. 00:11:11.000 --> 00:11:14.000 Na wakati naondoka, tulikuwa na karibu dola bilioni 30. Na 00:11:14.000 --> 00:11:17.000 tunavyoongea sasa, tuna dola bilioni 40 kwenye akiba 00:11:18.000 --> 00:11:22.000 hii ni kutokana na usimamizi mzuri wa fedha zetu. 00:11:23.000 --> 00:11:26.000 Hii inasaidia kutuliza uchumi wetu, kuufanya uwe imara. NOTE Paragraph 00:11:26.000 --> 00:11:29.000 Thamani ya fedha yetu ilikuwa ikibadilika kila mara 00:11:29.000 --> 00:11:33.000 kwa sasa ipo angalau imara na kusimamiwa, ili wafanyabiashara 00:11:33.000 --> 00:11:38.000 wawe na uhakika wa bei katika uchumi. 00:11:40.000 --> 00:11:44.000 Tuliweza kudhibiti mfumuko bei kutoka asilimia 28 mpaka karibu asilimia 11. 00:11:46.000 --> 00:11:52.000 Na pato letu la taifa liliongezeka kutoka wastani wa asilimia 2.3 kwa muongo uliopita 00:11:52.000 --> 00:11:55.000 mpaka kufikia asilimia 6.5 sasa. 00:11:56.000 --> 00:11:59.000 Kwa hiyo mabadiliko yote tuliyoweza kufanya 00:11:59.000 --> 00:12:02.000 yameweza kuonekana kwa vitendo ambavyo vinaweza kuonekana katika uchumi. NOTE Paragraph 00:12:02.000 --> 00:12:06.000 Na kitu cha muhimu zaidi, ni kwasababu tunataka kuondokana na mafuta 00:12:06.000 --> 00:12:08.000 na kupanua wigo zaidi – na kuna fursa nyingi sana 00:12:08.000 --> 00:12:11.000 katika nchi hii kubwa, kama ilivyo katika nchi nyingine za Afrika -- 00:12:13.000 --> 00:12:16.000 kilichotia fora zaidi ni huu ukuaji haukutoka 00:12:16.000 --> 00:12:19.000 kwenye sekta mafuta pekee, bali sekta nyingine pia. 00:12:19.000 --> 00:12:22.000 Kilimo kilikuwa kwa wastani wa asilimi 8. 00:12:22.000 --> 00:12:26.000 Sekta ya mawasiliano ilikuwa, makazi na ujenzi, 00:12:26.000 --> 00:12:31.000 na ninaweza kuendelea zaidi na zaidi. Na hii ni kuwaonyesha kwamba 00:12:31.000 --> 00:12:33.000 uchumi wako unaporekebishika, 00:12:33.000 --> 00:12:37.000 fursa katika sekta nyingine zipo nyingi. NOTE Paragraph 00:12:38.000 --> 00:12:41.000 Tuna frusa katika kilimo, kama nilivyosema. 00:12:41.000 --> 00:12:45.000 Tuna fursa katika madini. Tuna madini mengi 00:12:45.000 --> 00:12:48.000 ambako hakuna mtu amewekeza katika utafutaji. Tumegundua 00:12:48.000 --> 00:12:51.000 kuwa bila kuwa na sera sahihi za kuwezesha, 00:12:51.000 --> 00:12:54.000 hilo halitawezekana. Sasa tuna sheria ya uchimbaji madini 00:12:54.000 --> 00:12:57.000 ambayo inalinganishwa na sheria nyingine bora duniani. 00:12:58.000 --> 00:13:00.000 Tuna fursa katika makazi na usimamizi wa majumba. 00:13:00.000 --> 00:13:03.000 Kulikuwa hakuna chochote katika nchi ya watu milioni 140 -- 00:13:04.000 --> 00:13:09.000 hakuna maduka makubwa kama myajuavyo hapa. 00:13:10.000 --> 00:13:13.000 Hii inaweza kuwa fursa kwa mtu fulani 00:13:13.000 --> 00:13:15.000 ambayo ilitia chachu ya kufikiria kwa watu. 00:13:16.000 --> 00:13:19.000 Sasa tuna mazingira ambayo biashara katika maduka haya makubwa 00:13:19.000 --> 00:13:22.000 yanapata faida mara nne ya ilivyokadiriwa. NOTE Paragraph 00:13:23.000 --> 00:13:26.000 Kwa hiyo mambo makubwa kwenye ujenzi, mali isiyohamishika, 00:13:26.000 --> 00:13:28.000 Masoko ya rehani. Huduma za fedha 00:13:29.000 --> 00:13:33.000 tulikuwa na Benki 89. Nyingi hazifanyi biashara iliyokusudiwa. 00:13:33.000 --> 00:13:37.000 Tulizizatiti kutoka 89 kufikia Benki 25 kwa 00:13:37.000 --> 00:13:42.000 waongeze mtaji wao -- gawio la mtaji. 00:13:42.000 --> 00:13:47.000 Ilikuwa kutoka dola milioni 25 mpaka dola milioni 150. 00:13:47.000 --> 00:13:51.000 Benki, Benki hizi sasa zimejizatiti na kuimarishwa 00:13:51.000 --> 00:13:55.000 mfumo wa Benki umevutia wamekezaji wengi kutoka nje. 00:13:55.000 --> 00:13:59.000 Benki ya Barclays kutoka Uingereza inaingiza milioni 500. 00:13:59.000 --> 00:14:03.000 Standard Chartered imeingiza milioni 140. 00:14:03.000 --> 00:14:06.000 Ninaweza kuendelea zaidi. Dola zaidi na zaidi, ndani ya mfumo. NOTE Paragraph 00:14:06.000 --> 00:14:08.000 Tunafanya hivyo hivyo kwenye sekta ya bima. 00:14:08.000 --> 00:14:11.000 Kwa hiyo kwenye huduma za fedha, kuna fursa kubwa zaidi. 00:14:11.000 --> 00:14:17.000 Kwenye utalii, katika nchi nyingi za Kiafrika, ni fursa kubwa. 00:14:17.000 --> 00:14:20.000 Na hii ndiyo sababu kubwa ya kuwa watu wengi wanaifahamu Afrika Mashariki kwa: 00:14:21.000 --> 00:14:24.000 wanyama pori, tembo na kadhalika. 00:14:24.000 --> 00:14:26.000 Lakini kusimimamia soko la utalii ili 00:14:26.000 --> 00:14:29.000 liweze kuwanufaisha watu ni muhimu sana. NOTE Paragraph 00:14:30.000 --> 00:14:33.000 Sasa ninachojaribu kusema ni nini? Najaribu kuwaambia 00:14:33.000 --> 00:14:36.000 kuna wimbi jipya katika bara. 00:14:36.000 --> 00:14:41.000 Wimbi la uwazi na demokrasia ambapo tangu mwaka 2000, 00:14:41.000 --> 00:14:43.000 zaidi ya theluthi mbili ya nchi za Afrika zimefanya 00:14:43.000 --> 00:14:45.000 uchaguzi wa kidemokrasia wa vyama vingi. 00:14:46.000 --> 00:14:49.000 Si zote zilikuwa kamilifu, au zitakuwa, 00:14:49.000 --> 00:14:51.000 lakini mwelekeo uko wazi. 00:14:51.000 --> 00:14:55.000 Ninajaribu kuwaelezea kwamba toka miaka mitatu iliyopita 00:14:55.000 --> 00:14:58.000 wastani wa ukuaji wa uchumi katika bara umeongezeka 00:14:58.000 --> 00:15:02.000 kutoka karibu asilimia 2.5 mpaka asilimia 5 kwa mwaka. 00:15:02.000 --> 00:15:06.000 Hii ni bora zaidi ya ufanisi wa nchi nyingi za OECD. 00:15:07.000 --> 00:15:11.000 Kwahiyo ni wazi kwamba mambo yanabadilika. NOTE Paragraph 00:15:11.000 --> 00:15:13.000 Migogoro imepungua barani; 00:15:14.000 --> 00:15:16.000 kutoka migogoro 12 kwa muongo uliopita, 00:15:16.000 --> 00:15:18.000 kufikia migogoro mitatu au minne, 00:15:18.000 --> 00:15:21.000 Mojawapo ya migogoro mibaya zaidi, kwa hakika, ni ule wa Darfur. 00:15:21.000 --> 00:15:24.000 Na kama ujuavyo, kuna athari kwa majirani, iwapo 00:15:24.000 --> 00:15:26.000 kuna jambo linatokea upande mmoja wa bara, 00:15:26.000 --> 00:15:29.000 inaonekana kama bara zima limeathirika. 00:15:29.000 --> 00:15:32.000 Lakini ni vema muelewe kwamba hili bara -- 00:15:32.000 --> 00:15:38.000 ni bara lenye nchi nyingi na si nchi moja. 00:15:38.000 --> 00:15:40.000 Na iwapo tuna migogoro mitatu minne hivi, 00:15:40.000 --> 00:15:43.000 ina maana kuwa kuna fursa nyingi za kuwekeza 00:15:43.000 --> 00:15:50.000 katika uchumi ulio imara, unaokua na wenye kusisimua 00:15:50.000 --> 00:15:53.000 ambako kuna fursa nyingi sana. 00:15:54.000 --> 00:15:58.000 Ningependa kutoa dokezo moja kuhusu uwekezaji huu. NOTE Paragraph 00:15:59.000 --> 00:16:01.000 Namna nzuri ya kuisaidia Afrika sasa 00:16:02.000 --> 00:16:05.000 ni kuwasaidia waweze kusimama wenyewe. 00:16:05.000 --> 00:16:09.000 Na namna nzuri ya kufanya hivyo ni kusaidia kuleta ajira. 00:16:10.000 --> 00:16:14.000 Hakuna tatizo katika kupambana na malaria na kuwekeza pesa kwenye hilo 00:16:14.000 --> 00:16:18.000 na kuokoa maisha ya watoto. Sina maana hiyo. Hilo ni sawa. 00:16:19.000 --> 00:16:23.000 Lakini fikiria tofauti itakayokuwa kwenye familia: iwapo wazazi wanaweza kuwa na ajira 00:16:23.000 --> 00:16:25.000 na wakahakikisha watoto wao wanakwenda shule, 00:16:25.000 --> 00:16:28.000 kwamba wanaweza kununua dawa za kupambana na magonjwa wao wenyewe. 00:16:28.000 --> 00:16:32.000 Kama tunaweza kuwekeza kwenye maeneo ambayo nyinyi wenyewe mnapata faida 00:16:32.000 --> 00:16:37.000 wakati huo huo mkitengeneza ajira na kuwasaidia watu wasimame wenyewe, 00:16:37.000 --> 00:16:42.000 hii siyo fursa nzuri? Hii si ndiyo njia ya kufuata? 00:16:42.000 --> 00:16:45.000 Na nataka kusema jambo kuhusu watu bora zaidi wa kuwawekezea 00:16:45.000 --> 00:16:47.000 katika bara hili ni wanawake. 00:16:48.000 --> 00:16:55.000 (Makofi). NOTE Paragraph 00:16:55.000 --> 00:17:00.000 Nina CD hapa. Samahani sikusema kwa wakati muafaka. 00:17:00.000 --> 00:17:02.000 Lakini, ningependa mngekuwa mmeiangalia. 00:17:02.000 --> 00:17:05.000 Inasema, "Afrika: Iko wazi kwa Biashara." 00:17:06.000 --> 00:17:09.000 Na video hii imeshinda tuzo 00:17:09.000 --> 00:17:11.000 kama makala bora ya mwaka. 00:17:11.000 --> 00:17:13.000 Elewa kwamba mwanamke aliyetengeneza makala hii 00:17:13.000 --> 00:17:18.000 atakuwa Tanzania, ambako watakuwa na kongamano mwezi Juni. 00:17:19.000 --> 00:17:24.000 Lakini hii inakuonyesha kwamba Waafrika, na hususani wanawake wa Afrika, ambao 00:17:24.000 --> 00:17:29.000 pamoja na matatizo yote wameweza kuanzisha biashara, nyingine ni za kiwango cha kimataifa. NOTE Paragraph 00:17:29.000 --> 00:17:32.000 Mmoja kati ya wanawake katika video hii, Adenike Ogunlesi, 00:17:32.000 --> 00:17:34.000 anashona nguo za watoto 00:17:34.000 --> 00:17:39.000 kitu ambacho alianza kama kujifurahisha na ikakua na kuwa biashara. 00:17:39.000 --> 00:17:42.000 Akichanganya vitambaa vya Kiafrika ambavyo tunavyo, 00:17:43.000 --> 00:17:44.000 na vitambaa vingine kutoka sehemu nyingine. 00:17:44.000 --> 00:17:49.000 Na hivyo, atatengeneza suruali kwa kutumia vitambaa vizito, 00:17:49.000 --> 00:17:53.000 ikiwa imechanganywa na vitambaa vya kiafrika. Ni ubunifu mzuri sana. 00:17:55.000 --> 00:17:58.000 Amefikai hatua ambapo anapata zabuni kutoka Wal-Mart. 00:17:59.000 --> 00:18:00.000 (Kicheko). 00:18:01.000 --> 00:18:03.000 Kwa nguo 10,000 00:18:04.000 --> 00:18:08.000 Kwa hiyo hii inawaonyesha kuwa tuna watu wenye uwezo wa kufanya mambo. NOTE Paragraph 00:18:08.000 --> 00:18:13.000 Wanawake wana juhudi, wako makini; wanachapa kazi. 00:18:13.000 --> 00:18:15.000 Naweza kuendelea kwa kutoa mifano: 00:18:15.000 --> 00:18:19.000 Beatrice Gakuba wa Rwanda, alifungua biashara ya maua 00:18:19.000 --> 00:18:24.000 na sasa anayasafirisha kwenye mnada wa udachi huko Amsterdam kila asubuhi, 00:18:24.000 --> 00:18:28.000 na ameajiri wanawake na wanaume takriban 200 kumsaidia kazi. 00:18:29.000 --> 00:18:33.000 Hata hivyo, wengi wao, wana kiu ya kupata mtaji wa kupanua biashara zao, 00:18:34.000 --> 00:18:37.000 kwasababu hakuna anayeamini nje ya nchi zetu 00:18:37.000 --> 00:18:42.000 tunaweza kufanya mambo ya maana. Hakuna mtu anayefikiria kwa mtazamo wa masoko. 00:18:42.000 --> 00:18:45.000 Hakuna anyefikiria kuna fursa 00:18:45.000 --> 00:18:48.000 Nimesimama hapa kuwaambia wale waliochelewa jahazi kwa sasa, 00:18:48.000 --> 00:18:50.000 watalikosa milele. NOTE Paragraph 00:18:50.000 --> 00:18:56.000 Kwa hiyo iwapo unataka kuwa Afrika, fikiria kuwekeza. 00:18:57.000 --> 00:19:03.000 Wafikirie akina Beatrice, wafikirie kina Adenike wa dunia hii. 00:19:03.000 --> 00:19:06.000 ambao wanafanya mambo makubwa ambayo yanawasogeza 00:19:06.000 --> 00:19:09.000 katika uchumi wa dunia, wakati huo huo wakihakikisha 00:19:09.000 --> 00:19:12.000 wanawake wenzao na wanaume wanapata ajira. 00:19:12.000 --> 00:19:14.000 na kwamba watoto katika familia hizo wanapata elimu 00:19:14.000 --> 00:19:17.000 kwa sababu wazazi wao wanapata kipato cha kuridhisha NOTE Paragraph 00:19:18.000 --> 00:19:22.000 Kwa hiyo nina wakaribisha kuja kutafuta fursa 00:19:23.000 --> 00:19:27.000 Mtakapo kwenda Tanzania, sikilizeni kwa makini, 00:19:27.000 --> 00:19:31.000 kwasababu nina hakika mtasikia kuhusu fursa mbalimbali zilizopo 00:19:31.000 --> 00:19:36.000 ili muweze kushiriki katika kufanya mambo mazuri 00:19:36.000 --> 00:19:41.000 kwa bara hili, kwa watu wake na kwenu wenyewe NOTE Paragraph 00:19:41.000 --> 00:19:42.000 Asanteni sana. 00:19:42.000 --> 00:19:50.000 (Makofi)