Kwanini umsome nyota wa bunilizi za sayansi Octavia E Butler?- Ayana Jamieson and Moya Bailey
-
0:08 - 0:10Baada ya vita ya nuklea vya kusikitisha
-
0:10 - 0:15Lilith Iyapo anaamka baada ya
miaka 250 ya mapumziko -
0:15 - 0:19kujikuta amezungukwa na kundi la
viumbe linaloitwa Oankali. -
0:19 - 0:22Hawa viumbe walioendelea sana
walitaka kubadilishana DNA -
0:22 - 0:23kwa kuzaliana na binadamu
-
0:23 - 0:28ili kila kinasaba cha kiumbe kisambae
na kiwe na nguvu kushinda kingine. -
0:28 - 0:32Njia pekee wanayotoa ni kinga ya uzazi
kwa jamii yote ya binadamu. -
0:32 - 0:35Je ubiinadamu utakubali kuingia kwenye
biolojia isiyojulikana, -
0:35 - 0:38au wang'ang'anie asili yao na wapotee?
-
0:38 - 0:41Maswali kama haya yamejaa kwenye
"Dawn" ya Olivia Butler, -
0:41 - 0:44ya kwanza kwenye simulizi yake ya utatu
ya "Lilith's Brood". -
0:44 - 0:47Msimuliaji anayeona mbali aliyebadilisha
bunilizi ya kisayansi, -
0:47 - 0:50Butler amejenga dunia za kustaajabisha
katika kazi yake -- -
0:50 - 0:53na kufumbua mafumbo
yanayotuweka macho usiku. -
0:53 - 0:55Alizaliwa mwaka 1947,
-
0:55 - 0:59Butler alikua na aibu na mpole akiishi
Pasadena, California. -
0:59 - 1:01Aliota hadithi akiwa na umri mdogo,
-
1:01 - 1:04na punde akaanza kuziandika hizi
fikra kwenye karatasi. -
1:04 - 1:07Na miaka kumi na mbili, alimuomba
mama yake mashine ya kuchapa -
1:07 - 1:12baada ya filamu ya bunilizi ya sayansi
iitwayo "Msichana Shetani kutoka Mars" -
1:12 - 1:14Kutokuvutiwa na alichokiona,
-
1:14 - 1:17Butler alijua angeweza kusimulia
simulizi nzuri zaidi. -
1:17 - 1:19Iliyojaa za bunilizi za sayansi
wanaume weupe mashujaa -
1:19 - 1:23wanaolipua viumbe au wanakua
wakombozi wa watu weusi. -
1:23 - 1:27Butler alitaka kuandika wahusika tofauti
kwa ajili ya watazamaji tofauti. -
1:27 - 1:31Alileta uelewa na kina kwenye
uwakilishaji wa uzoefu wao. -
1:31 - 1:32Kwa Butler,
-
1:32 - 1:36ubunifu haukua tu kwa kupanda mbegu
za bunilizi za sayansi-- -
1:36 - 1:41lakini pia njia ya kupona dunia isiyo na
haki kwa mapatano ya mtu mwenyewe. -
1:41 - 1:43Kazi yake huchukua sehemu
zenye mateso za duniani -
1:43 - 1:48kama ubaguaji unaotakana na rangi,
jinsia, hali au uwezo, -
1:48 - 1:52na kumkaribisha msomaji
kuzitafakari kwenye muktadha mpya. -
1:52 - 1:54Moja ya riwaya zake zinazopendwa,
-
1:54 - 1:55ya "Mithali ya Mpanzi,"
-
1:55 - 1:57Inafwata huu mpangilio.
-
1:57 - 2:00Inaelezea hadithi ya Lauren Oya Olamina
-
2:00 - 2:04akielekea njiani kupitia California ya
karibuni, iliyoharibiwa na tamaa ya jumla, -
2:04 - 2:07ukosefu wa haki, na uharibifu wa
mazingira. -
2:07 - 2:09Akipambana na huruma kubwa,
-
2:09 - 2:12au hali kwenye kitabu inayomfanya
asikie uchungu wa wenzie, -
2:12 - 2:14na mara chache, furaha yao.
-
2:14 - 2:18Lauren anaanza safari na kundi la
wakimbizi kutafuta sehemu ya kupumzika. -
2:18 - 2:23Hapo, wanajaribu kuishi kutokana na dini
yake aliyoigundua, mbegu-dunia, -
2:23 - 2:25ambayo inategemea kanuni
-
2:25 - 2:28kua binadamu wanatakiwa wafuate
dunia inayobadilika kila mara. -
2:28 - 2:31Safari ya Lauren ina mizizi kwenye
uhalisi wa maisha- -
2:31 - 2:33California Prop 187,
-
2:33 - 2:37ambayo ilijaribu kuzuia wahamiaji bila
vibali haki za msingi za kibinadamu, -
2:37 - 2:39kabla ilionekana kutotambulika kwenye
katiba. -
2:39 - 2:43Butler siku zote aliweka habari
zinazoendelea kwenye uandishi wake. -
2:43 - 2:47Kwenye mwendelezo wake mwaka 1998 wa
"Mithali ya Mpanzi", "Mithali ya Talanta," -
2:47 - 2:49aliandika kuhusu mgombea uraisi
-
2:49 - 2:54anayewatawala Wamarekani kwa ukweli
taswira na "mikanda ya umeme." -
2:54 - 2:56Msemo wake? "Fanya Marekani bora tena."
-
2:56 - 2:58Wakati watu wakitambua utabiri wake,
-
2:58 - 3:02Butler alivutiwa pia na kufwatilia
tena historia. -
3:02 - 3:04Mfano
"Jamaa" inaelezea hadithi ya -
3:04 - 3:06mwanamke anayerudishwa nyuma
ya muda mara kwa mara -
3:06 - 3:09kwenye shamba la Maryland la mababu zake.
-
3:09 - 3:14Mwanzoni, anagundua kwamba kazi yake
ni kuokoa maisha ya mwananume mweupe -
3:14 - 3:16ambae atambaka nyanya yake.
-
3:16 - 3:20Asipomuokoa, yeye mweyewe
atasitishwa kuwepo -
3:20 - 3:23Haya matatizo makali yanamlazimisha Dana
kutazama majanga yanayoendelea -
3:23 - 3:27ya utumwa na ubakaji yanayowakabili
wanawake Weusi. -
3:27 - 3:29Na simulizi zake za wanawake
kuanzisha jumuiya mpya, -
3:29 - 3:32wasafiri wa mda wakishinda
fitina za kihistoria, -
3:32 - 3:34na viumbe tofauti kushabihiana,
-
3:34 - 3:39Butler alikuwa na ushawishi wa kushangaza
kwenye umaarufu unaokua wa Afrofuturism. -
3:39 - 3:40Hio ni harakati ya utamaduni
-
3:40 - 3:45ambapo waandishi na wasanii Weusi ambao
wanavutiwa na ya nyuma, sasa na ya mbele, -
3:45 - 3:50kutoa kazi zinazojumuisha mazingaombwe,
historia, teknolojia na mengine mengi. -
3:50 - 3:53Wakati Lauren anakuja kujifunza kwenye
"Mithali ya Mpanzi," -
3:53 - 3:55"Kila unachogusa unabadilisha.
-
3:55 - 3:58Kila unachobadilisha kinakubadilisha wewe.
-
3:58 - 4:01Ukweli pekee usiopinda ni Mabadiliko."
- Title:
- Kwanini umsome nyota wa bunilizi za sayansi Octavia E Butler?- Ayana Jamieson and Moya Bailey
- Speaker:
- Ayana Jamieson and Moya Bailey
- Description:
-
Angalia mafunzo yote: https//ed.ted.com/lessons/why-should-you-read-sci-fi-superstar-octavia-e-butler-ayana-jamieson-and-moya-bailey
Bunilizi za sayansi nyingi zinawahusisha wanaume weupe ambao wanaua viumbe au wanawaokoa watu wa rangi. Octavia E. Butler alijua angeweza kuhadithia simulizi nzuri zaidi. Alijenga dunia za kushangaza zenye watu wa kila aina, wenye mambo mbalimbali na ya kina kwenye majaribio yao. Ayana Jamieson na Moya Bailey wanazama kwenye kazi za mwanasimulizi mwenye maono aliyegeuza bunilizi za sayansi.
- Video Language:
- English
- Team:
- closed TED
- Project:
- TED-Ed
- Duration:
- 04:01
Nelson Simfukwe approved Swahili subtitles for Why should you read sci-fi superstar Octavia E. Butler? | ||
Doris Mangalu accepted Swahili subtitles for Why should you read sci-fi superstar Octavia E. Butler? | ||
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for Why should you read sci-fi superstar Octavia E. Butler? | ||
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for Why should you read sci-fi superstar Octavia E. Butler? | ||
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for Why should you read sci-fi superstar Octavia E. Butler? | ||
Julieth Mbeyella edited Swahili subtitles for Why should you read sci-fi superstar Octavia E. Butler? | ||
Julieth Mbeyella edited Swahili subtitles for Why should you read sci-fi superstar Octavia E. Butler? | ||
Julieth Mbeyella edited Swahili subtitles for Why should you read sci-fi superstar Octavia E. Butler? |