Baada ya vita ya nuklea vya kusikitisha
Lilith Iyapo anaamka baada ya
miaka 250 ya mapumziko
kujikuta amezungukwa na kundi la
viumbe linaloitwa Oankali.
Hawa viumbe walioendelea sana
walitaka kubadilishana DNA
kwa kuzaliana na binadamu
ili kila kinasaba cha kiumbe kisambae
na kiwe na nguvu kushinda kingine.
Njia pekee wanayotoa ni kinga ya uzazi
kwa jamii yote ya binadamu.
Je ubiinadamu utakubali kuingia kwenye
biolojia isiyojulikana,
au wang'ang'anie asili yao na wapotee?
Maswali kama haya yamejaa kwenye
"Dawn" ya Olivia Butler,
ya kwanza kwenye simulizi yake ya utatu
ya "Lilith's Brood".
Msimuliaji anayeona mbali aliyebadilisha
bunilizi ya kisayansi,
Butler amejenga dunia za kustaajabisha
katika kazi yake --
na kufumbua mafumbo
yanayotuweka macho usiku.
Alizaliwa mwaka 1947,
Butler alikua na aibu na mpole akiishi
Pasadena, California.
Aliota hadithi akiwa na umri mdogo,
na punde akaanza kuziandika hizi
fikra kwenye karatasi.
Na miaka kumi na mbili, alimuomba
mama yake mashine ya kuchapa
baada ya filamu ya bunilizi ya sayansi
iitwayo "Msichana Shetani kutoka Mars"
Kutokuvutiwa na alichokiona,
Butler alijua angeweza kusimulia
simulizi nzuri zaidi.
Iliyojaa za bunilizi za sayansi
wanaume weupe mashujaa
wanaolipua viumbe au wanakua
wakombozi wa watu weusi.
Butler alitaka kuandika wahusika tofauti
kwa ajili ya watazamaji tofauti.
Alileta uelewa na kina kwenye
uwakilishaji wa uzoefu wao.
Kwa Butler,
ubunifu haukua tu kwa kupanda mbegu
za bunilizi za sayansi--
lakini pia njia ya kupona dunia isiyo na
haki kwa mapatano ya mtu mwenyewe.
Kazi yake huchukua sehemu
zenye mateso za duniani
kama ubaguaji unaotakana na rangi,
jinsia, hali au uwezo,
na kumkaribisha msomaji
kuzitafakari kwenye muktadha mpya.
Moja ya riwaya zake zinazopendwa,
ya "Mithali ya Mpanzi,"
Inafwata huu mpangilio.
Inaelezea hadithi ya Lauren Oya Olamina
akielekea njiani kupitia California ya
karibuni, iliyoharibiwa na tamaa ya jumla,
ukosefu wa haki, na uharibifu wa
mazingira.
Akipambana na huruma kubwa,
au hali kwenye kitabu inayomfanya
asikie uchungu wa wenzie,
na mara chache, furaha yao.
Lauren anaanza safari na kundi la
wakimbizi kutafuta sehemu ya kupumzika.
Hapo, wanajaribu kuishi kutokana na dini
yake aliyoigundua, mbegu-dunia,
ambayo inategemea kanuni
kua binadamu wanatakiwa wafuate
dunia inayobadilika kila mara.
Safari ya Lauren ina mizizi kwenye
uhalisi wa maisha-
California Prop 187,
ambayo ilijaribu kuzuia wahamiaji bila
vibali haki za msingi za kibinadamu,
kabla ilionekana kutotambulika kwenye
katiba.
Butler siku zote aliweka habari
zinazoendelea kwenye uandishi wake.
Kwenye mwendelezo wake mwaka 1998 wa
"Mithali ya Mpanzi", "Mithali ya Talanta,"
aliandika kuhusu mgombea uraisi
anayewatawala Wamarekani kwa ukweli
taswira na "mikanda ya umeme."
Msemo wake? "Fanya Marekani bora tena."
Wakati watu wakitambua utabiri wake,
Butler alivutiwa pia na kufwatilia
tena historia.
Mfano
"Jamaa" inaelezea hadithi ya
mwanamke anayerudishwa nyuma
ya muda mara kwa mara
kwenye shamba la Maryland la mababu zake.
Mwanzoni, anagundua kwamba kazi yake
ni kuokoa maisha ya mwananume mweupe
ambae atambaka nyanya yake.
Asipomuokoa, yeye mweyewe
atasitishwa kuwepo
Haya matatizo makali yanamlazimisha Dana
kutazama majanga yanayoendelea
ya utumwa na ubakaji yanayowakabili
wanawake Weusi.
Na simulizi zake za wanawake
kuanzisha jumuiya mpya,
wasafiri wa mda wakishinda
fitina za kihistoria,
na viumbe tofauti kushabihiana,
Butler alikuwa na ushawishi wa kushangaza
kwenye umaarufu unaokua wa Afrofuturism.
Hio ni harakati ya utamaduni
ambapo waandishi na wasanii Weusi ambao
wanavutiwa na ya nyuma, sasa na ya mbele,
kutoa kazi zinazojumuisha mazingaombwe,
historia, teknolojia na mengine mengi.
Wakati Lauren anakuja kujifunza kwenye
"Mithali ya Mpanzi,"
"Kila unachogusa unabadilisha.
Kila unachobadilisha kinakubadilisha wewe.
Ukweli pekee usiopinda ni Mabadiliko."