Baada ya vita ya nuklea vya kusikitisha Lilith Iyapo anaamka baada ya miaka 250 ya mapumziko kujikuta amezungukwa na kundi la viumbe linaloitwa Oankali. Hawa viumbe walioendelea sana walitaka kubadilishana DNA kwa kuzaliana na binadamu ili kila kinasaba cha kiumbe kisambae na kiwe na nguvu kushinda kingine. Njia pekee wanayotoa ni kinga ya uzazi kwa jamii yote ya binadamu. Je ubiinadamu utakubali kuingia kwenye biolojia isiyojulikana, au wang'ang'anie asili yao na wapotee? Maswali kama haya yamejaa kwenye "Dawn" ya Olivia Butler, ya kwanza kwenye simulizi yake ya utatu ya "Lilith's Brood". Msimuliaji anayeona mbali aliyebadilisha bunilizi ya kisayansi, Butler amejenga dunia za kustaajabisha katika kazi yake -- na kufumbua mafumbo yanayotuweka macho usiku. Alizaliwa mwaka 1947, Butler alikua na aibu na mpole akiishi Pasadena, California. Aliota hadithi akiwa na umri mdogo, na punde akaanza kuziandika hizi fikra kwenye karatasi. Na miaka kumi na mbili, alimuomba mama yake mashine ya kuchapa baada ya filamu ya bunilizi ya sayansi iitwayo "Msichana Shetani kutoka Mars" Kutokuvutiwa na alichokiona, Butler alijua angeweza kusimulia simulizi nzuri zaidi. Iliyojaa za bunilizi za sayansi wanaume weupe mashujaa wanaolipua viumbe au wanakua wakombozi wa watu weusi. Butler alitaka kuandika wahusika tofauti kwa ajili ya watazamaji tofauti. Alileta uelewa na kina kwenye uwakilishaji wa uzoefu wao. Kwa Butler, ubunifu haukua tu kwa kupanda mbegu za bunilizi za sayansi-- lakini pia njia ya kupona dunia isiyo na haki kwa mapatano ya mtu mwenyewe. Kazi yake huchukua sehemu zenye mateso za duniani kama ubaguaji unaotakana na rangi, jinsia, hali au uwezo, na kumkaribisha msomaji kuzitafakari kwenye muktadha mpya. Moja ya riwaya zake zinazopendwa, ya "Mithali ya Mpanzi," Inafwata huu mpangilio. Inaelezea hadithi ya Lauren Oya Olamina akielekea njiani kupitia California ya karibuni, iliyoharibiwa na tamaa ya jumla, ukosefu wa haki, na uharibifu wa mazingira. Akipambana na huruma kubwa, au hali kwenye kitabu inayomfanya asikie uchungu wa wenzie, na mara chache, furaha yao. Lauren anaanza safari na kundi la wakimbizi kutafuta sehemu ya kupumzika. Hapo, wanajaribu kuishi kutokana na dini yake aliyoigundua, mbegu-dunia, ambayo inategemea kanuni kua binadamu wanatakiwa wafuate dunia inayobadilika kila mara. Safari ya Lauren ina mizizi kwenye uhalisi wa maisha- California Prop 187, ambayo ilijaribu kuzuia wahamiaji bila vibali haki za msingi za kibinadamu, kabla ilionekana kutotambulika kwenye katiba. Butler siku zote aliweka habari zinazoendelea kwenye uandishi wake. Kwenye mwendelezo wake mwaka 1998 wa "Mithali ya Mpanzi", "Mithali ya Talanta," aliandika kuhusu mgombea uraisi anayewatawala Wamarekani kwa ukweli taswira na "mikanda ya umeme." Msemo wake? "Fanya Marekani bora tena." Wakati watu wakitambua utabiri wake, Butler alivutiwa pia na kufwatilia tena historia. Mfano "Jamaa" inaelezea hadithi ya mwanamke anayerudishwa nyuma ya muda mara kwa mara kwenye shamba la Maryland la mababu zake. Mwanzoni, anagundua kwamba kazi yake ni kuokoa maisha ya mwananume mweupe ambae atambaka nyanya yake. Asipomuokoa, yeye mweyewe atasitishwa kuwepo Haya matatizo makali yanamlazimisha Dana kutazama majanga yanayoendelea ya utumwa na ubakaji yanayowakabili wanawake Weusi. Na simulizi zake za wanawake kuanzisha jumuiya mpya, wasafiri wa mda wakishinda fitina za kihistoria, na viumbe tofauti kushabihiana, Butler alikuwa na ushawishi wa kushangaza kwenye umaarufu unaokua wa Afrofuturism. Hio ni harakati ya utamaduni ambapo waandishi na wasanii Weusi ambao wanavutiwa na ya nyuma, sasa na ya mbele, kutoa kazi zinazojumuisha mazingaombwe, historia, teknolojia na mengine mengi. Wakati Lauren anakuja kujifunza kwenye "Mithali ya Mpanzi," "Kila unachogusa unabadilisha. Kila unachobadilisha kinakubadilisha wewe. Ukweli pekee usiopinda ni Mabadiliko."