-
Pfizer pekee.
-
Wakijaribu kunipa Johnson & Johnson,
Nitawaambia wanipe COVID badala yake.
-
Msimulizi: Mtandao unaonekana kujua
ni chanjo zipi hasa ni bora zaidi
-
na mbaya zaidi.
-
M: Moderna?
-
Zaidi kama ya kawaida,
wastani.
-
Hatufanyi wastani.
-
Mira Frike: Wanadamu hupenda
kulinganisha.
-
Si ajabu tunafanya hivyo pia
na chanjo za COVID-19.
-
Tatizo ni kwamba huwezi
kulinganisha chanjo kwa urahisi.
-
Na kufanya hivyo yaweza hata
kuwa na madhara katika janga.
-
N: Sisi hujishughulisha
kuangalia nambari hizi -
-
viwango vya ufanisi -
-
kwa sababu vinapima
uwezekano wako wa kupata COVID-19
-
baada ya kupewa chanjo.
-
MF: Tatizo ni kwamba nambari hizi
hazikutengenezwa ziwe sawa.
-
Badala yake, huamuliwa kulingana
na wakati na mahali
-
majaribio ya ufanisi yalifanyika.
-
Carlos Guzmán: Nadhani
ulinganisho wa ufanisi wa chanjo
-
nje ya muktadha inaweza kusababisha
matokeo potovu sana.
-
Kuna tofauti kuu katikati ya watu
wanofanyiwa utafiti,
-
kwa mfano; umri, jinsia,
mazingira, hali zilizopo awali.
-
N: Je, majaribio ya ufanisi
hufanyaje kazi?
-
Washiriki hugawanywa
katika vikundi viwili.
-
Kundi moja hupata chanjo;
nyingine, placebo.
-
Kisha wanaendelea na maisha yao
kama kawaida.
-
Baada ya muda fulani,
-
watafiti wanahesabu
wangapi kati yao waliugua COVID-19.
-
Ikiwa washiriki wote ambao waliugua
alitoka kwa kikundi cha placebo,
-
na sufuri kutoka kwa kikundi cha chanjo,
-
chanjo itakuwa na ufanisi 100%.
-
Na ikiwa ni idadi sawa ya watu
kutoka kwa vikundi vyote viwili waliugua,
-
ufanisi wa chanjo itakuwa sufuri
-
kwa sababu hatari ya kuambukizwa
haikubadilika na chanjo.
-
Lakini uwezekano wa washiriki
kupata ugonjwa wakati wa majaribio
-
inalingana na jumla ya kiwango
cha maambukizi katika mazingira yao.
-
CG: Pia kuna tofauti katika suala la
uwepo au kutokuwepo kwa lahaja ya virusi
-
ambayo hupigwa kwa ufanisi mdogo
au mwingi na kingamwili
-
zinazochochewa na aina ya protini
ya virusi vya asili vya SARS-CoV-2
-
ambayo ilijumuishwa
katika chanjo za sasa.
-
MF: Kwa hivyo wakati tunafikiria
tunajua ni chanjo gani bora,
-
maoni yetu kwa kweli yameathiriwa
na sababu za kimazingira.
-
N: Hebu tuangalie mfano.
-
Majaribio ya Moderna na Pfizer
yalifanyika zaidi nchini Marekani
-
na kabla ya kuwasili kwa aina
za anuwai zaidi za kuambukiza,
-
kama ile ya kutoka Uingereza au Afrika Kusini.
-
Majaribio ya AstraZeneca na Johnson & Johnson,
kwa upande mwingine,
-
yalifanyika baadaye
-
au katika nchi
-
ambazo anuwai zaidi za kuambukiza ziliibuka
na zikawa zaidi katika maambukizi.
-
MF: Hivyo viwango vya ufanisi
haitakuwa sawa kabisa
-
katika mazingira halisi ya ulimwengu,
-
na inaweza kubadilika kwa wakati.
-
CG: Kwa mfano, hivi majuzi
tuna ripoti kutoka Qatar,
-
ambapo 50% na 45% ya maambukizi
-
yanasababishwa na lahaja ya
Afrika Kusini na Uingereza.
-
Utafiti huu ulituonyesha kuwa ufanisi wa
chanjo ya BioNTech/Pfizer
-
hupungua hadi 89% na 75%
kwa maambukizi yanayosababishwa
-
na lahaja ya Uingereza na Afrika Kusini.
-
MF: Lakini labda kumekuwa na urekebishaji
mwingi sana juu ya ufanisi wakati huu wote.
-
N: Ufanisi kwa kawaida ni kipimo
kwa matokeo bora zaidi iwezekanavyo:
-
hakuna dalili hata kidogo.
-
Badala yake, tunaweza kuangalia|
jinsi chanjo zinazuia kulazwa hospitalini
-
na kifo kutoka na COVID-19,
kwa sababu chanjo hizi zote hufanya hivyo vizuri.
-
MF: Sasa kuna kipengele kingine
ambayo huathiri jinsi tunavyohukumu chanjo:
-
madhara.
-
N: Taarifa za kuganda kwa damu
zimetengeneza vichwa vya habari
-
na kuwatia watu wasiwasi.
-
EU pia iliamua
isihuishe mikataba yake
-
na AstraZeneca na Johnson & Johnson.
-
Hii yote inaweza kutoa hisia kwamba
chanjo zingine ni mbaya zaidi kuliko zingine.
-
MF: Lakini tena, si rahisi hivyo
-
kwa sababu hatari ya kila mtu binafsi
ya kuambukizwa
-
huathiri tathmini ya
jinsi kila chanjo ina manufaa.
-
N: Hebu tuangalie mfano
na chanjo ya AstraZeneca
-
na kuchukua viwango vya wastani vya
maambukizi kuwa kesi 55 kwa laki moja.
-
Kati ya watu 100,000
walio chini ya umri wa miaka 29,
-
ni wawili tu wataadhirika na ganda la nadra
la damu baada ya chanjo ya AstraZeneca,
-
lakini hakuna ambaye angehitaji uangalizi mahututi
kutokana na maambukizi ya COVID-19.
-
Lakini mtu zaidi ya miaka 60
-
ana uwezekano mkubwa zaidi wa kuishia
katika uangalizi maalum na COVID-19
-
na uwezekano mdogo wa kuadhirika na
ganda la nadra la damu.
-
MF: Ndio maana baadhi ya serikali
zinapendekeza chanjo cha AstraZeneca
-
tu kwa watu wenye umri wa miaka 60+.
-
Lakini tathmini hii inabadilika
ikiwa viwango vya maambukizi ni vya juu.
-
N: Wacha tuangalie hesabu sawa
lakini kwa viwango vya juu vya maambukizi.
-
Hapa, kesi 401 kwa laki moja.
-
Sasa kila mtu ana uwezekano mkubwa wa kuishia
katika uangalizi maalum kutokana na COVID-19
-
kuliko kuganda kwa damu
baada ya chanjo.
-
Katika hali hii, faida ya kupata
chanjo ya AstraZeneca
-
inazidi hatari ya kuganda kwa damu
kwa makundi yote ya umri.
-
CG: Na bila shaka,
-
kwa uingiliaji wa kuzuia
unaolenga watu wenye afya, kama chanjo,
-
ni muhimu
-
kwamba usawa wa hatari na faida
-
inakubalika kwa watu tofauti,
vikundi au hata watu binafsi.
-
MF: Je, kuna baadhi ya chanjo
mbaya zaidi kuliko zingine?
-
Tukiangalia tu madhara,
-
zingine hufanya vizuri zaidi,
-
angalau kutokana na kile
tunachojua hadi sasa.
-
Lakini hiyo ni kipengele kimoja tu
-
na isiwe pekee tunayozingatia.
-
CG: Nadhani suala kuu
-
ni kwamba chanjo au mpango
wa chanjo bora zaidi
-
ni ule unaoturuhusu
kuzuia magonjwa na kifo.
-
Na bila shaka, kupunguza matokeo
moja kwa moja na yasiyo ya moja kwa moja -
-
matokeo mabaya -
-
juu ya uharibifu mbaya.
-
MF: Chanjo yoyote iliyopokea
idhini ya dharura kutoka kwa WHO
-
hulinda dhidi ya visa vikali vya COVID-19.
-
Zinazuia vifo na kusaidia
kumaliza janga hili.
-
N: Hivyo, ikiwa chanjo ni chache,
-
kuna hoja nzuri sana kuchukua
chochote kinachopatikana kwetu,
-
kwa sababu ikiwa tunasisitiza
kupata chanjo maalum,
-
tunaweza kurefusha janga hili zima,
-
na hilo linaweza kugharimu maisha.
-
Manukuu na Maurício Kakuei Tanaka
Mapitio ya Carol Wang
-
-