Pfizer pekee. Wakijaribu kunipa Johnson & Johnson, Nitawaambia wanipe COVID badala yake. Msimulizi: Mtandao unaonekana kujua ni chanjo zipi hasa ni bora zaidi na mbaya zaidi. M: Moderna? Zaidi kama ya kawaida, wastani. Hatufanyi wastani. Mira Frike: Wanadamu hupenda kulinganisha. Si ajabu tunafanya hivyo pia na chanjo za COVID-19. Tatizo ni kwamba huwezi kulinganisha chanjo kwa urahisi. Na kufanya hivyo yaweza hata kuwa na madhara katika janga. N: Sisi hujishughulisha kuangalia nambari hizi - viwango vya ufanisi - kwa sababu vinapima uwezekano wako wa kupata COVID-19 baada ya kupewa chanjo. MF: Tatizo ni kwamba nambari hizi hazikutengenezwa ziwe sawa. Badala yake, huamuliwa kulingana na wakati na mahali majaribio ya ufanisi yalifanyika. Carlos Guzmán: Nadhani ulinganisho wa ufanisi wa chanjo nje ya muktadha inaweza kusababisha matokeo potovu sana. Kuna tofauti kuu katikati ya watu wanofanyiwa utafiti, kwa mfano; umri, jinsia, mazingira, hali zilizopo awali. N: Je, majaribio ya ufanisi hufanyaje kazi? Washiriki hugawanywa katika vikundi viwili. Kundi moja hupata chanjo; nyingine, placebo. Kisha wanaendelea na maisha yao kama kawaida. Baada ya muda fulani, watafiti wanahesabu wangapi kati yao waliugua COVID-19. Ikiwa washiriki wote ambao waliugua alitoka kwa kikundi cha placebo, na sufuri kutoka kwa kikundi cha chanjo, chanjo itakuwa na ufanisi 100%. Na ikiwa ni idadi sawa ya watu kutoka kwa vikundi vyote viwili waliugua, ufanisi wa chanjo itakuwa sufuri kwa sababu hatari ya kuambukizwa haikubadilika na chanjo. Lakini uwezekano wa washiriki kupata ugonjwa wakati wa majaribio inalingana na jumla ya kiwango cha maambukizi katika mazingira yao. CG: Pia kuna tofauti katika suala la uwepo au kutokuwepo kwa lahaja ya virusi ambayo hupigwa kwa ufanisi mdogo au mwingi na kingamwili zinazochochewa na aina ya protini ya virusi vya asili vya SARS-CoV-2 ambayo ilijumuishwa katika chanjo za sasa. MF: Kwa hivyo wakati tunafikiria tunajua ni chanjo gani bora, maoni yetu kwa kweli yameathiriwa na sababu za kimazingira. N: Hebu tuangalie mfano. Majaribio ya Moderna na Pfizer yalifanyika zaidi nchini Marekani na kabla ya kuwasili kwa aina za anuwai zaidi za kuambukiza, kama ile ya kutoka Uingereza au Afrika Kusini. Majaribio ya AstraZeneca na Johnson & Johnson, kwa upande mwingine, yalifanyika baadaye au katika nchi ambazo anuwai zaidi za kuambukiza ziliibuka na zikawa zaidi katika maambukizi. MF: Hivyo viwango vya ufanisi haitakuwa sawa kabisa katika mazingira halisi ya ulimwengu, na inaweza kubadilika kwa wakati. CG: Kwa mfano, hivi majuzi tuna ripoti kutoka Qatar, ambapo 50% na 45% ya maambukizi yanasababishwa na lahaja ya Afrika Kusini na Uingereza. Utafiti huu ulituonyesha kuwa ufanisi wa chanjo ya BioNTech/Pfizer hupungua hadi 89% na 75% kwa maambukizi yanayosababishwa na lahaja ya Uingereza na Afrika Kusini. MF: Lakini labda kumekuwa na urekebishaji mwingi sana juu ya ufanisi wakati huu wote. N: Ufanisi kwa kawaida ni kipimo kwa matokeo bora zaidi iwezekanavyo: hakuna dalili hata kidogo. Badala yake, tunaweza kuangalia| jinsi chanjo zinazuia kulazwa hospitalini na kifo kutoka na COVID-19, kwa sababu chanjo hizi zote hufanya hivyo vizuri. MF: Sasa kuna kipengele kingine ambayo huathiri jinsi tunavyohukumu chanjo: madhara. N: Taarifa za kuganda kwa damu zimetengeneza vichwa vya habari na kuwatia watu wasiwasi. EU pia iliamua isihuishe mikataba yake na AstraZeneca na Johnson & Johnson. Hii yote inaweza kutoa hisia kwamba chanjo zingine ni mbaya zaidi kuliko zingine. MF: Lakini tena, si rahisi hivyo kwa sababu hatari ya kila mtu binafsi ya kuambukizwa huathiri tathmini ya jinsi kila chanjo ina manufaa. N: Hebu tuangalie mfano na chanjo ya AstraZeneca na kuchukua viwango vya wastani vya maambukizi kuwa kesi 55 kwa laki moja. Kati ya watu 100,000 walio chini ya umri wa miaka 29, ni wawili tu wataadhirika na ganda la nadra la damu baada ya chanjo ya AstraZeneca, lakini hakuna ambaye angehitaji uangalizi mahututi kutokana na maambukizi ya COVID-19. Lakini mtu zaidi ya miaka 60 ana uwezekano mkubwa zaidi wa kuishia katika uangalizi maalum na COVID-19 na uwezekano mdogo wa kuadhirika na ganda la nadra la damu. MF: Ndio maana baadhi ya serikali zinapendekeza chanjo cha AstraZeneca tu kwa watu wenye umri wa miaka 60+. Lakini tathmini hii inabadilika ikiwa viwango vya maambukizi ni vya juu. N: Wacha tuangalie hesabu sawa lakini kwa viwango vya juu vya maambukizi. Hapa, kesi 401 kwa laki moja. Sasa kila mtu ana uwezekano mkubwa wa kuishia katika uangalizi maalum kutokana na COVID-19 kuliko kuganda kwa damu baada ya chanjo. Katika hali hii, faida ya kupata chanjo ya AstraZeneca inazidi hatari ya kuganda kwa damu kwa makundi yote ya umri. CG: Na bila shaka, kwa uingiliaji wa kuzuia unaolenga watu wenye afya, kama chanjo, ni muhimu kwamba usawa wa hatari na faida inakubalika kwa watu tofauti, vikundi au hata watu binafsi. MF: Je, kuna baadhi ya chanjo mbaya zaidi kuliko zingine? Tukiangalia tu madhara, zingine hufanya vizuri zaidi, angalau kutokana na kile tunachojua hadi sasa. Lakini hiyo ni kipengele kimoja tu na isiwe pekee tunayozingatia. CG: Nadhani suala kuu ni kwamba chanjo au mpango wa chanjo bora zaidi ni ule unaoturuhusu kuzuia magonjwa na kifo. Na bila shaka, kupunguza matokeo moja kwa moja na yasiyo ya moja kwa moja - matokeo mabaya - juu ya uharibifu mbaya. MF: Chanjo yoyote iliyopokea idhini ya dharura kutoka kwa WHO hulinda dhidi ya visa vikali vya COVID-19. Zinazuia vifo na kusaidia kumaliza janga hili. N: Hivyo, ikiwa chanjo ni chache, kuna hoja nzuri sana kuchukua chochote kinachopatikana kwetu, kwa sababu ikiwa tunasisitiza kupata chanjo maalum, tunaweza kurefusha janga hili zima, na hilo linaweza kugharimu maisha. Manukuu na Maurício Kakuei Tanaka Mapitio ya Carol Wang