Return to Video

Watoto wanahitaji mapumziko | Simon Link | TEDxAmanaAcademy

  • 0:05 - 0:07
    Mwaka jana, nilipata gamba na upanga.
  • 0:07 - 0:10
    Nilikuta mbwa nikacheza nae.
  • 0:10 - 0:12
    Nilijenga nyumba na kutengeneza bustani.
  • 0:12 - 0:15
    Usiku ukaingia, na majitu yakawa kila
    sehemu.
  • 0:15 - 0:19
    Kulikua na bwana mbaya
    ambae nilianza kumuua.
  • 0:19 - 0:22
    Nilipokua tu ninakaribia kummaliza ...
  • 0:22 - 0:23
    (Miluzi)
  • 0:23 - 0:24
    "Mda wa kupanga mstari!"
  • 0:24 - 0:27
    Habari, jina langu ni Simon Link,
  • 0:27 - 0:31
    na ninaongelea kuhusu kwa nini watoto
    wanatakiwa kuwa na mapumziko ya lisaa.
  • 0:31 - 0:34
    Unajua kua vinasaba vinabadilika
    vinapopata mda wa kucheza?
  • 0:34 - 0:39
    Kati ya vinasaba 1,200 ambazo
    wanasayansi wamechunguza,
  • 0:39 - 0:44
    moja ya tatu yao vimebadilika
    vilipokua na nusu saa ya kucheza.
  • 0:45 - 0:46
    Tangu miaka ya 1800,
  • 0:46 - 0:51
    utafiti unaonyesha kua unajifunza
    zaidi na haraka unapokuwa unacheza.
  • 0:52 - 0:58
    Kazi yenye mapumziko ni bora zaidi
    kuliko kazi za mda mreeeeefu.
  • 1:00 - 1:04
    Baadhi ya kikundi kilitembelea
    shule isiyokua na mapumziko.
  • 1:04 - 1:07
    Wakawauliza
    wawe na mapumziko mara mbili kwa wiki
  • 1:07 - 1:10
    ili wawaangalie na kuona
    jinsi walivyo.
  • 1:10 - 1:15
    Walikua wamekazia zaidi na watukutu kidogo
    kwenye siku walizokua na mapumziko.
  • 1:16 - 1:18
    Mikazo inaathiri kujifunza na afya.
  • 1:18 - 1:22
    Kwa watoto wengi, haswa wale
    wanaosemekana kukosa utulivu,
  • 1:22 - 1:28
    mapumziko ni nafasi ya kutumia nguvu
    kwa namna yenye afya na inayofaa.
  • 1:28 - 1:30
    Mapumziko huunda maarifa ya kijamii.
  • 1:30 - 1:35
    Mapumziko yanaweza kua mda pekee wa siku
    ambapo watoto wana nafasi
  • 1:35 - 1:39
    ya kupitia mahusiano na
    mawasiliano ya ukweli.
  • 1:40 - 1:43
    Mwanga wa nje unasisimua
    utoaji wa vitamini D,
  • 1:43 - 1:49
    ambapo tafiti nyingi zimeonyesha
    kuongezeka kwa mafunzo ya kitaaluma.
  • 1:50 - 1:55
    Nje ni sehemu bora zaidi
    kwa watoto kuchoma kalori,
  • 1:55 - 2:00
    kujaribu ujuzi wa dharura za kimwili,
    na kupata furaha halisi ya kuzunguka.
  • 2:01 - 2:07
    Kulingana na Rae Pica, ambae ni mtaalamu
    wa mazoezi ya mwili ya watoto,
  • 2:07 - 2:08
    mapumziko yanaweza kuwa ...
  • 2:08 - 2:12
    utafiti unaonyesha kua unajifunza ...
  • 2:13 - 2:15
    utafiti unaonyesha pia ...
  • 2:17 - 2:18
    kua ...
  • 2:18 - 2:20
    kunapokuwa na mazoezi ya mwili shuleni,
  • 2:20 - 2:24
    unakua na mazoezi ya mwili zaidi
    ukiwa nyumbani,
  • 2:24 - 2:28
    na watoto ambao hawana hio
    nafasi
  • 2:28 - 2:30
    kuwa na uwezo wa kufanya mazoezi
    siku za shule
  • 2:30 - 2:34
    kawaida hawafidii
    wakati wa masaa baada ya shule.
  • 2:36 - 2:38
    Kukimbia kunasaidia ubongo.
  • 2:39 - 2:41
    Kwa sababu ya maendeleo ya tafiti za
    ubongo,
  • 2:41 - 2:46
    tunajua kua sehemu kubwa ya ubongo
    inasisimka wakati wa mazoezi ya mwili
  • 2:46 - 2:49
    mara nyingi zaidi ya kukaa tu sehemu.
  • 2:52 - 2:54
    Sasa, simameni,
  • 2:54 - 2:57
    na mruke mara kumi nitakapowaambia.
  • 3:04 - 3:05
    Ruka!
  • 3:05 - 3:09
    Moja, mbili, tatu, nne, tano,
  • 3:10 - 3:14
    sita, saba, nane, tisa, kumi.
  • 3:14 - 3:15
    Sasa, kaeni chini.
  • 3:21 - 3:25
    Ninatafakari dunia ambayo kila mtoto
    anapata mda wa kutosha wa kucheza.
  • 3:25 - 3:27
    Ninatumaini kua kama unawatoto,
  • 3:27 - 3:30
    utahakikisha kua hao watoto
    wanapata mda mwingi wa kucheza.
  • 3:30 - 3:31
    Asanteni.
  • 3:32 - 3:33
    (Makofi)
Title:
Watoto wanahitaji mapumziko | Simon Link | TEDxAmanaAcademy
Description:

Simon Link yuko darasa la tatu Shule ya Amana. Anapenda chokoleti, pipi na kujifunza kuhusu historia za tamaduni nyingine. Anapenda kukimbia na kucheza wakati wa mapumziko. Simon anaamini wanafunzi wanapaswa kua na mda mrefu zaidi wa mapumziko na mda wa mazoezi kwenye siku. Hili wazo linaungana na la Utoaji wa Mfumo wa Kujifunza wa Uelewa Mkuu, na Jukumu la Kujifunza.

Maongezi haya yametolewa kwenye tukio la TEDx kutumia mfumo wa mikutano ya TED yakiwa yameandaliwa kipekee na jamii. Jifunze zaidi kupitia https://www.ted.com/tedx

more » « less
Video Language:
English
Team:
closed TED
Project:
TEDxTalks
Duration:
03:39

Swahili subtitles

Revisions