0:00:04.653,0:00:07.421 Mwaka jana, nilipata gamba na upanga. 0:00:07.421,0:00:09.567 Nilikuta mbwa nikacheza nae. 0:00:09.567,0:00:11.675 Nilijenga nyumba na kutengeneza bustani. 0:00:11.675,0:00:14.584 Usiku ukaingia, na majitu yakawa kila[br]sehemu. 0:00:15.213,0:00:18.866 Kulikua na bwana mbaya[br]ambae nilianza kumuua. 0:00:18.866,0:00:21.592 Nilipokua tu ninakaribia kummaliza ... 0:00:21.592,0:00:22.611 (Miluzi) 0:00:22.611,0:00:24.482 "Mda wa kupanga mstari!" 0:00:24.482,0:00:26.721 Habari, jina langu ni Simon Link, 0:00:26.721,0:00:30.879 na ninaongelea kuhusu kwa nini watoto[br]wanatakiwa kuwa na mapumziko ya lisaa. 0:00:31.405,0:00:34.409 Unajua kua vinasaba vinabadilika[br]vinapopata mda wa kucheza? 0:00:34.409,0:00:39.489 Kati ya vinasaba 1,200 ambazo[br]wanasayansi wamechunguza, 0:00:39.489,0:00:43.761 moja ya tatu yao vimebadilika[br]vilipokua na nusu saa ya kucheza. 0:00:44.915,0:00:46.410 Tangu miaka ya 1800, 0:00:46.410,0:00:50.972 utafiti unaonyesha kua unajifunza[br]zaidi na haraka unapokuwa unacheza. 0:00:52.086,0:00:58.368 Kazi yenye mapumziko ni bora zaidi[br]kuliko kazi za mda mreeeeefu. 0:00:59.721,0:01:03.743 Baadhi ya kikundi kilitembelea[br]shule isiyokua na mapumziko. 0:01:04.264,0:01:06.866 Wakawauliza[br]wawe na mapumziko mara mbili kwa wiki 0:01:06.866,0:01:10.407 ili wawaangalie na kuona[br]jinsi walivyo. 0:01:10.412,0:01:14.782 Walikua wamekazia zaidi na watukutu kidogo[br]kwenye siku walizokua na mapumziko. 0:01:16.057,0:01:18.399 Mikazo inaathiri kujifunza na afya. 0:01:18.399,0:01:22.428 Kwa watoto wengi, haswa wale[br]wanaosemekana kukosa utulivu, 0:01:22.428,0:01:28.116 mapumziko ni nafasi ya kutumia nguvu[br]kwa namna yenye afya na inayofaa. 0:01:28.116,0:01:30.494 Mapumziko huunda maarifa ya kijamii. 0:01:30.494,0:01:34.916 Mapumziko yanaweza kua mda pekee wa siku[br]ambapo watoto wana nafasi 0:01:34.916,0:01:39.159 ya kupitia mahusiano na[br]mawasiliano ya ukweli. 0:01:39.634,0:01:43.399 Mwanga wa nje unasisimua[br]utoaji wa vitamini D, 0:01:43.399,0:01:48.933 ambapo tafiti nyingi zimeonyesha[br]kuongezeka kwa mafunzo ya kitaaluma. 0:01:50.167,0:01:55.023 Nje ni sehemu bora zaidi[br]kwa watoto kuchoma kalori, 0:01:55.023,0:02:00.237 kujaribu ujuzi wa dharura za kimwili,[br]na kupata furaha halisi ya kuzunguka. 0:02:01.492,0:02:06.572 Kulingana na Rae Pica, ambae ni mtaalamu[br]wa mazoezi ya mwili ya watoto, 0:02:06.572,0:02:08.314 mapumziko yanaweza kuwa ... 0:02:08.314,0:02:12.218 utafiti unaonyesha kua unajifunza ... 0:02:12.914,0:02:15.071 utafiti unaonyesha pia ... 0:02:16.526,0:02:17.530 kua ... 0:02:17.735,0:02:20.456 kunapokuwa na mazoezi ya mwili shuleni, 0:02:20.460,0:02:23.616 unakua na mazoezi ya mwili zaidi[br]ukiwa nyumbani, 0:02:23.624,0:02:27.720 na watoto ambao hawana hio[br]nafasi 0:02:27.720,0:02:30.491 kuwa na uwezo wa kufanya mazoezi[br]siku za shule 0:02:30.494,0:02:34.294 kawaida hawafidii[br]wakati wa masaa baada ya shule. 0:02:35.834,0:02:38.356 Kukimbia kunasaidia ubongo. 0:02:39.104,0:02:41.451 Kwa sababu ya maendeleo ya tafiti za[br]ubongo, 0:02:41.451,0:02:45.912 tunajua kua sehemu kubwa ya ubongo[br]inasisimka wakati wa mazoezi ya mwili 0:02:45.913,0:02:48.730 mara nyingi zaidi ya kukaa tu sehemu. 0:02:52.413,0:02:53.817 Sasa, simameni, 0:02:53.817,0:02:56.808 na mruke mara kumi nitakapowaambia. 0:03:04.433,0:03:05.443 Ruka! 0:03:05.443,0:03:09.453 Moja, mbili, tatu, nne, tano, 0:03:09.603,0:03:13.573 sita, saba, nane, tisa, kumi. 0:03:13.573,0:03:15.382 Sasa, kaeni chini. 0:03:20.985,0:03:25.232 Ninatafakari dunia ambayo kila mtoto[br]anapata mda wa kutosha wa kucheza. 0:03:25.232,0:03:26.917 Ninatumaini kua kama unawatoto, 0:03:26.917,0:03:30.175 utahakikisha kua hao watoto[br]wanapata mda mwingi wa kucheza. 0:03:30.175,0:03:31.177 Asanteni. 0:03:31.607,0:03:32.905 (Makofi)