Mwaka jana, nilipata gamba na upanga.
Nilikuta mbwa nikacheza nae.
Nilijenga nyumba na kutengeneza bustani.
Usiku ukaingia, na majitu yakawa kila
sehemu.
Kulikua na bwana mbaya
ambae nilianza kumuua.
Nilipokua tu ninakaribia kummaliza ...
(Miluzi)
"Mda wa kupanga mstari!"
Habari, jina langu ni Simon Link,
na ninaongelea kuhusu kwa nini watoto
wanatakiwa kuwa na mapumziko ya lisaa.
Unajua kua vinasaba vinabadilika
vinapopata mda wa kucheza?
Kati ya vinasaba 1,200 ambazo
wanasayansi wamechunguza,
moja ya tatu yao vimebadilika
vilipokua na nusu saa ya kucheza.
Tangu miaka ya 1800,
utafiti unaonyesha kua unajifunza
zaidi na haraka unapokuwa unacheza.
Kazi yenye mapumziko ni bora zaidi
kuliko kazi za mda mreeeeefu.
Baadhi ya kikundi kilitembelea
shule isiyokua na mapumziko.
Wakawauliza
wawe na mapumziko mara mbili kwa wiki
ili wawaangalie na kuona
jinsi walivyo.
Walikua wamekazia zaidi na watukutu kidogo
kwenye siku walizokua na mapumziko.
Mikazo inaathiri kujifunza na afya.
Kwa watoto wengi, haswa wale
wanaosemekana kukosa utulivu,
mapumziko ni nafasi ya kutumia nguvu
kwa namna yenye afya na inayofaa.
Mapumziko huunda maarifa ya kijamii.
Mapumziko yanaweza kua mda pekee wa siku
ambapo watoto wana nafasi
ya kupitia mahusiano na
mawasiliano ya ukweli.
Mwanga wa nje unasisimua
utoaji wa vitamini D,
ambapo tafiti nyingi zimeonyesha
kuongezeka kwa mafunzo ya kitaaluma.
Nje ni sehemu bora zaidi
kwa watoto kuchoma kalori,
kujaribu ujuzi wa dharura za kimwili,
na kupata furaha halisi ya kuzunguka.
Kulingana na Rae Pica, ambae ni mtaalamu
wa mazoezi ya mwili ya watoto,
mapumziko yanaweza kuwa ...
utafiti unaonyesha kua unajifunza ...
utafiti unaonyesha pia ...
kua ...
kunapokuwa na mazoezi ya mwili shuleni,
unakua na mazoezi ya mwili zaidi
ukiwa nyumbani,
na watoto ambao hawana hio
nafasi
kuwa na uwezo wa kufanya mazoezi
siku za shule
kawaida hawafidii
wakati wa masaa baada ya shule.
Kukimbia kunasaidia ubongo.
Kwa sababu ya maendeleo ya tafiti za
ubongo,
tunajua kua sehemu kubwa ya ubongo
inasisimka wakati wa mazoezi ya mwili
mara nyingi zaidi ya kukaa tu sehemu.
Sasa, simameni,
na mruke mara kumi nitakapowaambia.
Ruka!
Moja, mbili, tatu, nne, tano,
sita, saba, nane, tisa, kumi.
Sasa, kaeni chini.
Ninatafakari dunia ambayo kila mtoto
anapata mda wa kutosha wa kucheza.
Ninatumaini kua kama unawatoto,
utahakikisha kua hao watoto
wanapata mda mwingi wa kucheza.
Asanteni.
(Makofi)