Mwaka jana, nilipata gamba na upanga. Nilikuta mbwa nikacheza nae. Nilijenga nyumba na kutengeneza bustani. Usiku ukaingia, na majitu yakawa kila sehemu. Kulikua na bwana mbaya ambae nilianza kumuua. Nilipokua tu ninakaribia kummaliza ... (Miluzi) "Mda wa kupanga mstari!" Habari, jina langu ni Simon Link, na ninaongelea kuhusu kwa nini watoto wanatakiwa kuwa na mapumziko ya lisaa. Unajua kua vinasaba vinabadilika vinapopata mda wa kucheza? Kati ya vinasaba 1,200 ambazo wanasayansi wamechunguza, moja ya tatu yao vimebadilika vilipokua na nusu saa ya kucheza. Tangu miaka ya 1800, utafiti unaonyesha kua unajifunza zaidi na haraka unapokuwa unacheza. Kazi yenye mapumziko ni bora zaidi kuliko kazi za mda mreeeeefu. Baadhi ya kikundi kilitembelea shule isiyokua na mapumziko. Wakawauliza wawe na mapumziko mara mbili kwa wiki ili wawaangalie na kuona jinsi walivyo. Walikua wamekazia zaidi na watukutu kidogo kwenye siku walizokua na mapumziko. Mikazo inaathiri kujifunza na afya. Kwa watoto wengi, haswa wale wanaosemekana kukosa utulivu, mapumziko ni nafasi ya kutumia nguvu kwa namna yenye afya na inayofaa. Mapumziko huunda maarifa ya kijamii. Mapumziko yanaweza kua mda pekee wa siku ambapo watoto wana nafasi ya kupitia mahusiano na mawasiliano ya ukweli. Mwanga wa nje unasisimua utoaji wa vitamini D, ambapo tafiti nyingi zimeonyesha kuongezeka kwa mafunzo ya kitaaluma. Nje ni sehemu bora zaidi kwa watoto kuchoma kalori, kujaribu ujuzi wa dharura za kimwili, na kupata furaha halisi ya kuzunguka. Kulingana na Rae Pica, ambae ni mtaalamu wa mazoezi ya mwili ya watoto, mapumziko yanaweza kuwa ... utafiti unaonyesha kua unajifunza ... utafiti unaonyesha pia ... kua ... kunapokuwa na mazoezi ya mwili shuleni, unakua na mazoezi ya mwili zaidi ukiwa nyumbani, na watoto ambao hawana hio nafasi kuwa na uwezo wa kufanya mazoezi siku za shule kawaida hawafidii wakati wa masaa baada ya shule. Kukimbia kunasaidia ubongo. Kwa sababu ya maendeleo ya tafiti za ubongo, tunajua kua sehemu kubwa ya ubongo inasisimka wakati wa mazoezi ya mwili mara nyingi zaidi ya kukaa tu sehemu. Sasa, simameni, na mruke mara kumi nitakapowaambia. Ruka! Moja, mbili, tatu, nne, tano, sita, saba, nane, tisa, kumi. Sasa, kaeni chini. Ninatafakari dunia ambayo kila mtoto anapata mda wa kutosha wa kucheza. Ninatumaini kua kama unawatoto, utahakikisha kua hao watoto wanapata mda mwingi wa kucheza. Asanteni. (Makofi)