1 00:00:04,653 --> 00:00:07,421 Mwaka jana, nilipata gamba na upanga. 2 00:00:07,421 --> 00:00:09,567 Nilikuta mbwa nikacheza nae. 3 00:00:09,567 --> 00:00:11,675 Nilijenga nyumba na kutengeneza bustani. 4 00:00:11,675 --> 00:00:14,584 Usiku ukaingia, na majitu yakawa kila sehemu. 5 00:00:15,213 --> 00:00:18,866 Kulikua na bwana mbaya ambae nilianza kumuua. 6 00:00:18,866 --> 00:00:21,592 Nilipokua tu ninakaribia kummaliza ... 7 00:00:21,592 --> 00:00:22,611 (Miluzi) 8 00:00:22,611 --> 00:00:24,482 "Mda wa kupanga mstari!" 9 00:00:24,482 --> 00:00:26,721 Habari, jina langu ni Simon Link, 10 00:00:26,721 --> 00:00:30,879 na ninaongelea kuhusu kwa nini watoto wanatakiwa kuwa na mapumziko ya lisaa. 11 00:00:31,405 --> 00:00:34,409 Unajua kua vinasaba vinabadilika vinapopata mda wa kucheza? 12 00:00:34,409 --> 00:00:39,489 Kati ya vinasaba 1,200 ambazo wanasayansi wamechunguza, 13 00:00:39,489 --> 00:00:43,761 moja ya tatu yao vimebadilika vilipokua na nusu saa ya kucheza. 14 00:00:44,915 --> 00:00:46,410 Tangu miaka ya 1800, 15 00:00:46,410 --> 00:00:50,972 utafiti unaonyesha kua unajifunza zaidi na haraka unapokuwa unacheza. 16 00:00:52,086 --> 00:00:58,368 Kazi yenye mapumziko ni bora zaidi kuliko kazi za mda mreeeeefu. 17 00:00:59,721 --> 00:01:03,743 Baadhi ya kikundi kilitembelea shule isiyokua na mapumziko. 18 00:01:04,264 --> 00:01:06,866 Wakawauliza wawe na mapumziko mara mbili kwa wiki 19 00:01:06,866 --> 00:01:10,407 ili wawaangalie na kuona jinsi walivyo. 20 00:01:10,412 --> 00:01:14,782 Walikua wamekazia zaidi na watukutu kidogo kwenye siku walizokua na mapumziko. 21 00:01:16,057 --> 00:01:18,399 Mikazo inaathiri kujifunza na afya. 22 00:01:18,399 --> 00:01:22,428 Kwa watoto wengi, haswa wale wanaosemekana kukosa utulivu, 23 00:01:22,428 --> 00:01:28,116 mapumziko ni nafasi ya kutumia nguvu kwa namna yenye afya na inayofaa. 24 00:01:28,116 --> 00:01:30,494 Mapumziko huunda maarifa ya kijamii. 25 00:01:30,494 --> 00:01:34,916 Mapumziko yanaweza kua mda pekee wa siku ambapo watoto wana nafasi 26 00:01:34,916 --> 00:01:39,159 ya kupitia mahusiano na mawasiliano ya ukweli. 27 00:01:39,634 --> 00:01:43,399 Mwanga wa nje unasisimua utoaji wa vitamini D, 28 00:01:43,399 --> 00:01:48,933 ambapo tafiti nyingi zimeonyesha kuongezeka kwa mafunzo ya kitaaluma. 29 00:01:50,167 --> 00:01:55,023 Nje ni sehemu bora zaidi kwa watoto kuchoma kalori, 30 00:01:55,023 --> 00:02:00,237 kujaribu ujuzi wa dharura za kimwili, na kupata furaha halisi ya kuzunguka. 31 00:02:01,492 --> 00:02:06,572 Kulingana na Rae Pica, ambae ni mtaalamu wa mazoezi ya mwili ya watoto, 32 00:02:06,572 --> 00:02:08,314 mapumziko yanaweza kuwa ... 33 00:02:08,314 --> 00:02:12,218 utafiti unaonyesha kua unajifunza ... 34 00:02:12,914 --> 00:02:15,071 utafiti unaonyesha pia ... 35 00:02:16,526 --> 00:02:17,530 kua ... 36 00:02:17,735 --> 00:02:20,456 kunapokuwa na mazoezi ya mwili shuleni, 37 00:02:20,460 --> 00:02:23,616 unakua na mazoezi ya mwili zaidi ukiwa nyumbani, 38 00:02:23,624 --> 00:02:27,720 na watoto ambao hawana hio nafasi 39 00:02:27,720 --> 00:02:30,491 kuwa na uwezo wa kufanya mazoezi siku za shule 40 00:02:30,494 --> 00:02:34,294 kawaida hawafidii wakati wa masaa baada ya shule. 41 00:02:35,834 --> 00:02:38,356 Kukimbia kunasaidia ubongo. 42 00:02:39,104 --> 00:02:41,451 Kwa sababu ya maendeleo ya tafiti za ubongo, 43 00:02:41,451 --> 00:02:45,912 tunajua kua sehemu kubwa ya ubongo inasisimka wakati wa mazoezi ya mwili 44 00:02:45,913 --> 00:02:48,730 mara nyingi zaidi ya kukaa tu sehemu. 45 00:02:52,413 --> 00:02:53,817 Sasa, simameni, 46 00:02:53,817 --> 00:02:56,808 na mruke mara kumi nitakapowaambia. 47 00:03:04,433 --> 00:03:05,443 Ruka! 48 00:03:05,443 --> 00:03:09,453 Moja, mbili, tatu, nne, tano, 49 00:03:09,603 --> 00:03:13,573 sita, saba, nane, tisa, kumi. 50 00:03:13,573 --> 00:03:15,382 Sasa, kaeni chini. 51 00:03:20,985 --> 00:03:25,232 Ninatafakari dunia ambayo kila mtoto anapata mda wa kutosha wa kucheza. 52 00:03:25,232 --> 00:03:26,917 Ninatumaini kua kama unawatoto, 53 00:03:26,917 --> 00:03:30,175 utahakikisha kua hao watoto wanapata mda mwingi wa kucheza. 54 00:03:30,175 --> 00:03:31,177 Asanteni. 55 00:03:31,607 --> 00:03:32,905 (Makofi)