Picha kutoka kwa mkimbiza vimbunga
-
0:00 - 0:04KIla kitu kinahusiana na kingine
-
0:04 - 0:07Kama muhindi, nilikuzwa kujua hili
-
0:07 - 0:09Sisi ni kabila dogo la wavuvi
-
0:09 - 0:12Katika ncha ya kusini mashariki mwa kisiwa cha Long
-
0:12 - 0:15karibu na mji wa Southampton katika jiji la New York.
-
0:15 - 0:18Nilipokuwa msichana mdogo,
-
0:18 - 0:23Babu yangu alinichukua kukaa naye juani katika wakati wa majira ya joto.
-
0:23 - 0:27Hakukuwa na mawingu angani.
-
0:27 - 0:30na baada ya muda mfupi nikaanza kutoka jasho.
-
0:30 - 0:33na akanionyesha angani na kusema,
-
0:33 - 0:36"Angalia,unaona kile?
-
0:36 - 0:38Ile ni sehemu yako kule juu.
-
0:38 - 0:41Yale ni maji yako yanayosaidia kutengeneza mawingu
-
0:41 - 0:46yanayokuwa mvua inayonywesha mimea
-
0:46 - 0:49ambayo inalisha wanyama."
-
0:49 - 0:52katika utafiti wangu wa mambo haya
-
0:52 - 0:57ambayo yanaonyesha uhusiano katika maisha,
-
0:57 - 1:00Nilianza kukimbiza vimbunga mwaka 2008
-
1:00 - 1:03baada ya binti yangu kusema, " Mama, ni lazima ufanye hivyo."
-
1:03 - 1:10siku tatu baadaye,nikiendesha gari kwa kasi sana,
-
1:10 - 1:17nikajikuta nafuatilia aina moja ya wingu kubwa sana,
-
1:17 - 1:21lenye uwezo wa kutengeneza mvua ua mawe kubwa
-
1:21 - 1:23na vimbunga vya ajabu,
-
1:23 - 1:30ingawa ni asilimia mbili tu hufanya hivyo.
-
1:30 - 1:35mawingu haya yanaweza kuwa makubwa sana, mpaka maili 50 kwa upana
-
1:35 - 1:39na yanaweza yakaenda mpaka futi 65,000 juu angani.
-
1:39 - 1:41yanaweza yakawa makubwa sana kiasi cha kuzuia mwanga wa mchana,
-
1:41 - 1:46kufanya ukisimama chini yake kuwa peusi sana.
-
1:46 - 1:49Kukimbiza vimbunga ni kitu chenye mguso wa kipekee.
-
1:49 - 1:53unakuta kuna upepo mnyevu wa joto unaopuliza mgongoni kwako
-
1:53 - 2:00haufu ya mchanga,ngano na majani.
-
2:00 - 2:04halafu pia kuna rangi mbalimbali katika mawingu
-
2:04 - 2:09ya mvua ya mawe, ya kijani na bluu.
-
2:09 - 2:12nimejifunza kuiheshimu radi.
-
2:12 - 2:14Nywele zangu zilikuwa hazijajikunja ziko moja kwa moja.
-
2:14 - 2:16(vicheko)
-
2:16 - 2:17ninatania.
-
2:17 - 2:19(vicheko)
-
2:19 - 2:23kinachonifurahisha mimi kuhusu vimbunga hivi
-
2:23 - 2:27ni jinsi vinavyotembea,vinavyozunguka,
-
2:27 - 2:31na mawingu yenye vitu kama miale ya moto.
-
2:31 - 2:34yanakuwa ni madude yanayotisha huku yakipendeza pia.
-
2:34 - 2:36ninapoyapiga picha,
-
2:36 - 2:40nashindwa kujizuia kukumbuka mafundisho ya babu yangu.
-
2:40 - 2:42na ninasimama chini yake,
-
2:42 - 2:44naona sio tu wingu,
-
2:44 - 2:47lakini na kuelewa pia nina bahati ya kushuhudia
-
2:47 - 2:51nguvu zile zile ,mchakato ule ule, katika hali ndogo
-
2:51 - 2:58ambavyo vilitengeneza anga letu,mfumo wa jua,jua letu
-
2:58 - 3:02na hata sayari hii.
-
3:02 - 3:05na mahusiano yote yangu. Asante sana.
-
3:05 - 3:07(Shangwe)
- Title:
- Picha kutoka kwa mkimbiza vimbunga
- Speaker:
- Camille Seaman
- Description:
-
Mpiga picha,Camille Seaman amekuwa akikimbiza vimbunga kwa miaka 5. katika mazungumzo haya anaonyesha picha za kupendeza sana za vishindi za mbingu.
- Video Language:
- English
- Team:
- closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 03:26
Ivana Korom edited Swahili subtitles for Photos from a storm chaser | ||
Joachim Mangilima approved Swahili subtitles for Photos from a storm chaser | ||
Nelson Simfukwe accepted Swahili subtitles for Photos from a storm chaser | ||
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for Photos from a storm chaser | ||
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for Photos from a storm chaser | ||
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for Photos from a storm chaser |