KIla kitu kinahusiana na kingine
Kama muhindi, nilikuzwa kujua hili
Sisi ni kabila dogo la wavuvi
Katika ncha ya kusini mashariki mwa kisiwa cha Long
karibu na mji wa Southampton katika jiji la New York.
Nilipokuwa msichana mdogo,
Babu yangu alinichukua kukaa naye juani katika wakati wa majira ya joto.
Hakukuwa na mawingu angani.
na baada ya muda mfupi nikaanza kutoka jasho.
na akanionyesha angani na kusema,
"Angalia,unaona kile?
Ile ni sehemu yako kule juu.
Yale ni maji yako yanayosaidia kutengeneza mawingu
yanayokuwa mvua inayonywesha mimea
ambayo inalisha wanyama."
katika utafiti wangu wa mambo haya
ambayo yanaonyesha uhusiano katika maisha,
Nilianza kukimbiza vimbunga mwaka 2008
baada ya binti yangu kusema, " Mama, ni lazima ufanye hivyo."
siku tatu baadaye,nikiendesha gari kwa kasi sana,
nikajikuta nafuatilia aina moja ya wingu kubwa sana,
lenye uwezo wa kutengeneza mvua ua mawe kubwa
na vimbunga vya ajabu,
ingawa ni asilimia mbili tu hufanya hivyo.
mawingu haya yanaweza kuwa makubwa sana, mpaka maili 50 kwa upana
na yanaweza yakaenda mpaka futi 65,000 juu angani.
yanaweza yakawa makubwa sana kiasi cha kuzuia mwanga wa mchana,
kufanya ukisimama chini yake kuwa peusi sana.
Kukimbiza vimbunga ni kitu chenye mguso wa kipekee.
unakuta kuna upepo mnyevu wa joto unaopuliza mgongoni kwako
haufu ya mchanga,ngano na majani.
halafu pia kuna rangi mbalimbali katika mawingu
ya mvua ya mawe, ya kijani na bluu.
nimejifunza kuiheshimu radi.
Nywele zangu zilikuwa hazijajikunja ziko moja kwa moja.
(vicheko)
ninatania.
(vicheko)
kinachonifurahisha mimi kuhusu vimbunga hivi
ni jinsi vinavyotembea,vinavyozunguka,
na mawingu yenye vitu kama miale ya moto.
yanakuwa ni madude yanayotisha huku yakipendeza pia.
ninapoyapiga picha,
nashindwa kujizuia kukumbuka mafundisho ya babu yangu.
na ninasimama chini yake,
naona sio tu wingu,
lakini na kuelewa pia nina bahati ya kushuhudia
nguvu zile zile ,mchakato ule ule, katika hali ndogo
ambavyo vilitengeneza anga letu,mfumo wa jua,jua letu
na hata sayari hii.
na mahusiano yote yangu. Asante sana.
(Shangwe)