0:00:00.000,0:00:04.000 KIla kitu kinahusiana na kingine 0:00:04.000,0:00:07.000 Kama muhindi, nilikuzwa kujua hili 0:00:07.000,0:00:09.000 Sisi ni kabila dogo la wavuvi 0:00:09.000,0:00:12.000 Katika ncha ya kusini mashariki mwa kisiwa cha Long 0:00:12.000,0:00:15.000 karibu na mji wa Southampton katika jiji la New York. 0:00:15.000,0:00:18.000 Nilipokuwa msichana mdogo, 0:00:18.000,0:00:23.000 Babu yangu alinichukua kukaa naye juani katika wakati wa majira ya joto. 0:00:23.000,0:00:27.000 Hakukuwa na mawingu angani. 0:00:27.000,0:00:30.000 na baada ya muda mfupi nikaanza kutoka jasho. 0:00:30.000,0:00:33.000 na akanionyesha angani na kusema, 0:00:33.000,0:00:36.000 "Angalia,unaona kile? 0:00:36.000,0:00:38.000 Ile ni sehemu yako kule juu. 0:00:38.000,0:00:41.000 Yale ni maji yako yanayosaidia kutengeneza mawingu 0:00:41.000,0:00:46.000 yanayokuwa mvua inayonywesha mimea 0:00:46.000,0:00:49.000 ambayo inalisha wanyama." 0:00:49.000,0:00:52.000 katika utafiti wangu wa mambo haya 0:00:52.000,0:00:57.000 ambayo yanaonyesha uhusiano katika maisha, 0:00:57.000,0:01:00.000 Nilianza kukimbiza vimbunga mwaka 2008 0:01:00.000,0:01:03.000 baada ya binti yangu kusema, " Mama, ni lazima ufanye hivyo." 0:01:03.000,0:01:10.000 siku tatu baadaye,nikiendesha gari kwa kasi sana, 0:01:10.000,0:01:17.000 nikajikuta nafuatilia aina moja ya wingu kubwa sana, 0:01:17.000,0:01:21.000 lenye uwezo wa kutengeneza mvua ua mawe kubwa 0:01:21.000,0:01:23.000 na vimbunga vya ajabu, 0:01:23.000,0:01:30.000 ingawa ni asilimia mbili tu hufanya hivyo. 0:01:30.000,0:01:35.000 mawingu haya yanaweza kuwa makubwa sana, mpaka maili 50 kwa upana 0:01:35.000,0:01:39.000 na yanaweza yakaenda mpaka futi 65,000 juu angani. 0:01:39.000,0:01:41.000 yanaweza yakawa makubwa sana kiasi cha kuzuia mwanga wa mchana, 0:01:41.000,0:01:46.000 kufanya ukisimama chini yake kuwa peusi sana. 0:01:46.000,0:01:49.000 Kukimbiza vimbunga ni kitu chenye mguso wa kipekee. 0:01:49.000,0:01:53.000 unakuta kuna upepo mnyevu wa joto unaopuliza mgongoni kwako 0:01:53.000,0:02:00.000 haufu ya mchanga,ngano na majani. 0:02:00.000,0:02:04.000 halafu pia kuna rangi mbalimbali katika mawingu 0:02:04.000,0:02:09.000 ya mvua ya mawe, ya kijani na bluu. 0:02:09.000,0:02:12.000 nimejifunza kuiheshimu radi. 0:02:12.000,0:02:14.000 Nywele zangu zilikuwa hazijajikunja ziko moja kwa moja. 0:02:14.000,0:02:16.000 (vicheko) 0:02:16.000,0:02:17.000 ninatania. 0:02:17.000,0:02:19.000 (vicheko) 0:02:19.000,0:02:23.000 kinachonifurahisha mimi kuhusu vimbunga hivi 0:02:23.000,0:02:27.000 ni jinsi vinavyotembea,vinavyozunguka, 0:02:27.000,0:02:31.000 na mawingu yenye vitu kama miale ya moto. 0:02:31.000,0:02:34.000 yanakuwa ni madude yanayotisha huku yakipendeza pia. 0:02:34.000,0:02:36.000 ninapoyapiga picha, 0:02:36.000,0:02:40.000 nashindwa kujizuia kukumbuka mafundisho ya babu yangu. 0:02:40.000,0:02:42.000 na ninasimama chini yake, 0:02:42.000,0:02:44.000 naona sio tu wingu, 0:02:44.000,0:02:47.000 lakini na kuelewa pia nina bahati ya kushuhudia 0:02:47.000,0:02:51.000 nguvu zile zile ,mchakato ule ule, katika hali ndogo 0:02:51.000,0:02:58.000 ambavyo vilitengeneza anga letu,mfumo wa jua,jua letu 0:02:58.000,0:03:02.000 na hata sayari hii. 0:03:02.000,0:03:05.000 na mahusiano yote yangu. Asante sana. 0:03:05.000,0:03:07.000 (Shangwe)