-
Mnamo Agosti 4, kulikuwa na mlipuko mkubwa
kwenye bandari ya Beirut, Lebanon.
-
(Milipuko)
-
Simu za rununu zilinasa mlipuko huo
kutoka karibu kila pembe.
-
Video zilisambaa kupitia mitandao ya kijamii
na
majukwaa ya ujumbe karibu mara moja.
-
Baadhi zilikuwa halisi, baadhi ziliendeshwa
-
Chache zilionekana kuonyesha kombora
kugonga kabla ya mlipuko huo.
-
(Milipuko)
-
Video hizi zilibadilishwa
-
Mwandishi wa habari mchunguzi Emmanuelle Saliba
-
alipopokea moja ya video hizo
kutoka kwa chanzo huko Beirut,
-
alijua lazima aende kazini.
-
Kama mwandishi wa habari mchunguzaji,
-
jukumu langu ni kujaribu kujua
nini kilisababisha mlipuko katika kesi hii.
-
Kwa hivyo niliwasiliana na mtu
ambaye ana biashara katika bandari la Beirut.
-
Familia yake imekuwa
ikifanya kazi huko kwa miaka 40.
-
Na katika mabadilishano haya alisema:
"Wacha nikutumie video."
-
"Nadhani kombora lilisababisha mlipuko huo."
-
Tayari nilikuwa na shauku sana
-
kwa sababu nilikuwa nimeona baadhi kwa urahisi
video zinazoweza kufichulika huko nje.
-
Kwa hivyo tunachoangalia hapa ni video ya kwanza iliyotoka ambayo ilibadilishwa.
-
Kinachovutia katika kesi hii ni -
-
ni video halisi ya shahidi.
-
kwa hivyo kweli tunaliona tukio hilo,
-
lakini kile mtu huyo alifanya ni
iliongeza kombora.
-
Na nitawaonyesha video halisi, ambayo ni hii.
-
(Gari yapiga honi)
-
(Milipuko)
-
Kikubwa kizuri sasa kuhusu kinacho endelea mtandaoni
-
ni kuwa punde tu video iliyo badilishwa inapotokea,
-
kuna waandishi wa habari wengi
ambao wamefunzwa kufanya hivi,
-
kuwa kwa kasi zinafichuliwa.
-
Kwa hivyo mwenzangu katika BBC ambaye anaangazia
juu ya habari za uongo, alifichua hili.
-
Na tupo sote, ingawaje tunafanyia kazi kampuni tofauti,
-
sote tunaangalia kazi za wenzetu na kusaidiana.
-
Kwa hiyo nilikuwa na hilo kichwani wakati
Nilikuwa nazungumza na chanzo changu,
-
na nikafikiri, "Wajua, tumesha ifichua video hii.
-
Nina shaka sana kuhusu hili."
-
"Nitumie."
-
Alinitumia kwa njia ya WhatsApp na yeye
alisema aliipata kutoka kwa marafiki na familia.
-
Unajua, fikiria biashara yake imeharibiwa, wanataka majibu.
-
Wanataka kujua ni nini kilisababisha mlipuko huo.
-
Niliangalia video
na ni video ya infrared.
-
Nitakuonyesha toleo
ambayo iko hapa, ambayo bado inaishi kwenye Twitter.
-
Nitakuchezea ili uone.
-
(Milipuko)
-
Unaweza kuona kuwa hizi ni video mbili
ambazo zimehaririwa pamoja
-
kuifanya ionekane kama
ni shoti moja mfululizo.
-
Lakini kwa kuiangalia tu,
mtu yeyote angeweza kuona kuwa
-
zimechukuliwa kutoka pembe mbili tofauti.
-
Pia kuna safu hii ya picha ya joto
ambayo ni ya ajabu kidogo,
-
ukizingatia hiyo video
kamera huanguka kwenye sakafu
-
na unaweza kuona ilichukuliwa na mwanadamu.
-
Ni binadamu gani ana kamera ya infrared?
-
Hii gia ni ya kitaalamu.
-
Haki. Video inatetemeka.
-
Hakuna picha za usalama ambazo zingetoka hivyo haraka
-
kutokana na nguvu ya mlipuko huo.
-
Kwa hivyo unaanza tu, kama,
kuunganisha mambo haya pamoja.
-
Nilitambua shoti hii ya kwanza
-
na nilijua kuwa ilichukuliwa
na mhariri wa mitandao ya kijamii
-
ambaye kwa kweli alikuwa ardhini,
ambaye anafanya kazi CNN.
-
Na hii hapa video asili.
-
Unaona, haina kichujio hicho.
-
Na unapoicheza,
-
(Milipuko)
-
unaweza kuona kwamba hakuna kombora
ambayo inapita angani na kugonga.
-
Kwa hivyo hiyo iliongezwa.
-
Nilizungumza naye na akasema,
-
"Ndio, video yangu ilichukuliwa, ikabadilishwa.
-
Na niliendelea kupata barua pepe hizi zote
kuhusu kombora linalodhaniwa kwenye video yangu"
-
ambayo unaweza kuona haipo.
-
Na haraka baadaye, Twitter
kweli iliweka tukio
-
ili kuonyesha kwamba wachunguzi wa ukweli walikuwa wamehitimisha
-
kwamba video ya mlipuko wa Beirut ilibadilishwa na ni pamoja na kombora bandia.
-
Na walionyesha tweet yangu
na thread yangu niliyoifanya
-
na pia waliunganisha waandishi wengine wachache
-
ambao pia wamekuwa wakifanya kazi sawa ya ufichuzi.
-
Kwa hivyo ni muhimu kwetu kuwa wepesi kabisa kukataa haya
-
na kuyafichua haraka
-
nakuonyesha watu jinsi tunavyoifanya, sio?
-
Ni rahisi kusema ni halisi.
-
lakini tunahitaji watu kuelewa kwanini na ni vipi sio halisi.
-
Kwa hivyo kweli nilimwandikia
nikaziweka hatua zangu, nikasema,
-
"Hivi ndivyo ninavyojua sio halisi."
-
Na yeye akasema, "Sawa,
hiyo ni nzuri sana kujua.
-
Nitawaambia marafiki zangu
na familia yangu."
-
Na ni jambo linalosaidia sana, nadhani kama wewe ni
mtu binafsi, kuunda orodha
-
na waandishi wa habari hawa tofauti,
-
ili uweze kuwafuatilia wakati habari zinapochipuka.
-
Jenga jumuiya yako ndogo ya wataalam
unaoamini, ambao wamethibitishwa,
-
na kwa njia hiyo unaweza kuona
kwamba kile unachotaka kushiriki
-
kweli kilionekana hapa
kama kitu ambacho hupaswi kufanya.
-
Hasa.
-
Mlipuko wa Agosti 4 katika
Beirut ulikuwa wenye kuangamiza.
-
Maisha yalipotea.
Maelfu walijeruhiwa.
-
Mabilioni ya dola ya uharibifu yalifanyika.
-
Sote tulitaka kujua jinsi hii ilifanyika.
-
Tulipata maelezo mara moja.
-
Lakini habari za kuaminika huchukua muda.
-
Kwa hivyo tunafanya nini wakati habari
husafiri haraka kuliko ukweli?
-
Unda orodha kama Emmanuelle anavyo pendekeza.
-
Tafuta waandishi wa habari unao waamini na kuwafuata.
-
Halafu habari kubwa inapochipuka -
-
na ikiwa 2020 imetufundisha chochote,
hakika itachipuka -
-
utajua tayari kwenda kwa nani.
-
Mpaka wakati ujao. Iweke kweli.
Usieneze habari za uwongo.
-
Mimi ni Hari Sreenivasan
na hii ni Take On Fake.
-
Asante kwa kutazama.
-
-
-
-
-