Mnamo Agosti 4, kulikuwa na mlipuko mkubwa kwenye bandari ya Beirut, Lebanon. (Milipuko) Simu za rununu zilinasa mlipuko huo kutoka karibu kila pembe. Video zilisambaa kupitia mitandao ya kijamii na majukwaa ya ujumbe karibu mara moja. Baadhi zilikuwa halisi, baadhi ziliendeshwa Chache zilionekana kuonyesha kombora kugonga kabla ya mlipuko huo. (Milipuko) Video hizi zilibadilishwa Mwandishi wa habari mchunguzi Emmanuelle Saliba alipopokea moja ya video hizo kutoka kwa chanzo huko Beirut, alijua lazima aende kazini. Kama mwandishi wa habari mchunguzaji, jukumu langu ni kujaribu kujua nini kilisababisha mlipuko katika kesi hii. Kwa hivyo niliwasiliana na mtu ambaye ana biashara katika bandari la Beirut. Familia yake imekuwa ikifanya kazi huko kwa miaka 40. Na katika mabadilishano haya alisema: "Wacha nikutumie video." "Nadhani kombora lilisababisha mlipuko huo." Tayari nilikuwa na shauku sana kwa sababu nilikuwa nimeona baadhi kwa urahisi video zinazoweza kufichulika huko nje. Kwa hivyo tunachoangalia hapa ni video ya kwanza iliyotoka ambayo ilibadilishwa. Kinachovutia katika kesi hii ni - ni video halisi ya shahidi. kwa hivyo kweli tunaliona tukio hilo, lakini kile mtu huyo alifanya ni iliongeza kombora. Na nitawaonyesha video halisi, ambayo ni hii. (Gari yapiga honi) (Milipuko) Kikubwa kizuri sasa kuhusu kinacho endelea mtandaoni ni kuwa punde tu video iliyo badilishwa inapotokea, kuna waandishi wa habari wengi ambao wamefunzwa kufanya hivi, kuwa kwa kasi zinafichuliwa. Kwa hivyo mwenzangu katika BBC ambaye anaangazia juu ya habari za uongo, alifichua hili. Na tupo sote, ingawaje tunafanyia kazi kampuni tofauti, sote tunaangalia kazi za wenzetu na kusaidiana. Kwa hiyo nilikuwa na hilo kichwani wakati Nilikuwa nazungumza na chanzo changu, na nikafikiri, "Wajua, tumesha ifichua video hii. Nina shaka sana kuhusu hili." "Nitumie." Alinitumia kwa njia ya WhatsApp na yeye alisema aliipata kutoka kwa marafiki na familia. Unajua, fikiria biashara yake imeharibiwa, wanataka majibu. Wanataka kujua ni nini kilisababisha mlipuko huo. Niliangalia video na ni video ya infrared. Nitakuonyesha toleo ambayo iko hapa, ambayo bado inaishi kwenye Twitter. Nitakuchezea ili uone. (Milipuko) Unaweza kuona kuwa hizi ni video mbili ambazo zimehaririwa pamoja kuifanya ionekane kama ni shoti moja mfululizo. Lakini kwa kuiangalia tu, mtu yeyote angeweza kuona kuwa zimechukuliwa kutoka pembe mbili tofauti. Pia kuna safu hii ya picha ya joto ambayo ni ya ajabu kidogo, ukizingatia hiyo video kamera huanguka kwenye sakafu na unaweza kuona ilichukuliwa na mwanadamu. Ni binadamu gani ana kamera ya infrared? Hii gia ni ya kitaalamu. Haki. Video inatetemeka. Hakuna picha za usalama ambazo zingetoka hivyo haraka kutokana na nguvu ya mlipuko huo. Kwa hivyo unaanza tu, kama, kuunganisha mambo haya pamoja. Nilitambua shoti hii ya kwanza na nilijua kuwa ilichukuliwa na mhariri wa mitandao ya kijamii ambaye kwa kweli alikuwa ardhini, ambaye anafanya kazi CNN. Na hii hapa video asili. Unaona, haina kichujio hicho. Na unapoicheza, (Milipuko) unaweza kuona kwamba hakuna kombora ambayo inapita angani na kugonga. Kwa hivyo hiyo iliongezwa. Nilizungumza naye na akasema, "Ndio, video yangu ilichukuliwa, ikabadilishwa. Na niliendelea kupata barua pepe hizi zote kuhusu kombora linalodhaniwa kwenye video yangu" ambayo unaweza kuona haipo. Na haraka baadaye, Twitter kweli iliweka tukio ili kuonyesha kwamba wachunguzi wa ukweli walikuwa wamehitimisha kwamba video ya mlipuko wa Beirut ilibadilishwa na ni pamoja na kombora bandia. Na walionyesha tweet yangu na thread yangu niliyoifanya na pia waliunganisha waandishi wengine wachache ambao pia wamekuwa wakifanya kazi sawa ya ufichuzi. Kwa hivyo ni muhimu kwetu kuwa wepesi kabisa kukataa haya na kuyafichua haraka nakuonyesha watu jinsi tunavyoifanya, sio? Ni rahisi kusema ni halisi. lakini tunahitaji watu kuelewa kwanini na ni vipi sio halisi. Kwa hivyo kweli nilimwandikia nikaziweka hatua zangu, nikasema, "Hivi ndivyo ninavyojua sio halisi." Na yeye akasema, "Sawa, hiyo ni nzuri sana kujua. Nitawaambia marafiki zangu na familia yangu." Na ni jambo linalosaidia sana, nadhani kama wewe ni mtu binafsi, kuunda orodha na waandishi wa habari hawa tofauti, ili uweze kuwafuatilia wakati habari zinapochipuka. Jenga jumuiya yako ndogo ya wataalam unaoamini, ambao wamethibitishwa, na kwa njia hiyo unaweza kuona kwamba kile unachotaka kushiriki kweli kilionekana hapa kama kitu ambacho hupaswi kufanya. Hasa. Mlipuko wa Agosti 4 katika Beirut ulikuwa wenye kuangamiza. Maisha yalipotea. Maelfu walijeruhiwa. Mabilioni ya dola ya uharibifu yalifanyika. Sote tulitaka kujua jinsi hii ilifanyika. Tulipata maelezo mara moja. Lakini habari za kuaminika huchukua muda. Kwa hivyo tunafanya nini wakati habari husafiri haraka kuliko ukweli? Unda orodha kama Emmanuelle anavyo pendekeza. Tafuta waandishi wa habari unao waamini na kuwafuata. Halafu habari kubwa inapochipuka - na ikiwa 2020 imetufundisha chochote, hakika itachipuka - utajua tayari kwenda kwa nani. Mpaka wakati ujao. Iweke kweli. Usieneze habari za uwongo. Mimi ni Hari Sreenivasan na hii ni Take On Fake. Asante kwa kutazama.