Zungumza na Moyo I Marleen Laschet I TEDxTrondheim
-
0:09 - 0:15Takriban watu milioni mia tatu sitini na tano hutumia Kiingereza kama lugha ya mama
-
0:17 - 0:21Wengine zaidi ya bilioni mbili husoma na kutumia Kiingeereza
-
0:21 - 0:23kama lugha ya pili au ya tatu
-
0:24 - 0:26Kama wewe ni mzungumzaji wa Kiingereza
-
0:26 - 0:32unayosema yanaeleweka kwa watu takriban bilioni mbili unusu
-
0:32 - 0:37Kutakuwa na haja gani kusomea lugha yeyote ingine ya kigeni?
-
0:37 - 0:41Si itakuwa tu kupoteza mda?
-
0:41 - 0:45Nelson Mandela alikashifiwa vikali
-
0:45 - 0:49na waafrika kusini kwa kuongea Afrikaans
-
0:50 - 0:51Alijibu hivi,
-
0:51 - 0:55"Unapomuongelesha mtu kwa lugha anayoifahamu
-
0:56 - 0:58hilo halisahau.
-
0:59 - 1:02Unapomuongelesha mtu kwa lugha ya mama
-
1:03 - 1:04hilo huenda moyoni mwake."
-
1:05 - 1:07Hivyo jambo ni hili:
-
1:07 - 1:09Ukitaka kumshawishi mtu
-
1:09 - 1:12lenga moyo wake uongeapo.
-
1:13 - 1:15Mapapa wanajua hili.
-
1:15 - 1:19John Paul wa pili afahamu lugha kumi vyema
-
1:19 - 1:22na kadhaa zingine alizijua kimsingi.
-
1:23 - 1:27Popote alipoenda, alisalimia wenyeji
-
1:27 - 1:31akitumia yale maneno aliyojua kwa lugha zao asili;
-
1:31 - 1:36na hapo ndipo umaarufu wake ulipotokea.
-
1:37 - 1:40Walio na akina mama wakwe wa ugenini
-
1:40 - 1:43au akina mama wakwe wa ugenini watarajiwa, wanalijua hili, pia.
-
1:44 - 1:46Wanaweza kuongea Kiingereza wakiwa na wapenzi wao,
-
1:46 - 1:51lakini wakitaka kuwa na maelewano na mama wa msichana,
-
1:51 - 1:55vijana hujitolea kujifunza lugha za kushangaza,
-
1:55 - 1:57hata Kiholanzi.
-
1:57 - 1:59(Vicheko)
-
1:59 - 2:01Na hili husaidia.
-
2:02 - 2:03Kwa nini?
-
2:04 - 2:09Kwa vile, lugha zetu asili huambatana kwa karibu na
-
2:09 - 2:13utu wetu na kujitambulisha kwetu.
-
2:13 - 2:18Historia yetu yote imeota mizizi,
-
2:18 - 2:21na kulowa ndani ya lugha zetu asili.
-
2:21 - 2:28Kuna makumbusho na hisia zilizounganika na maneno, muonekano,
-
2:29 - 2:32hata kwa sarufi tulizokua nazo.
-
2:33 - 2:37Hivyo, unapojifunza lugha ya mwengine,
-
2:37 - 2:40unajifahamisha kuwa una nia halisi
-
2:40 - 2:44kwa maisha yao, kwa utu wao.
-
2:45 - 2:48Ni mama mkwe yupi hatafurahia?
-
2:49 - 2:53Unaposikia lugha yako unaskia kuungika.
-
2:54 - 2:56Unaposafiri,
-
2:56 - 3:00na umekuwa ukiongea lugha ya kigeni kwa siku au wiki kadhaa,
-
3:01 - 3:03wakati unapoabiri ndege
-
3:03 - 3:06na msaidizi kwa ndege akusalimie kwa lugha yako asili,
-
3:06 - 3:08unafahamu basi unaenda nyumbani.
-
3:10 - 3:14Kama lugha asili zingekuwa na harufu,
-
3:14 - 3:19nadhani zingenukia kama kuki,
-
3:19 - 3:21na kama supu ya kuku ya kurariji,
-
3:22 - 3:24na kama marashi ya nyanya -
-
3:25 - 3:28labda kidogo kama kifukuzi nondo.
-
3:29 - 3:34Hii inaweza kuwa sababu lugha zilizotungwa,
-
3:34 - 3:40kama Esperanto, hazijasambaa kama ilivyotarajiwa.
-
3:41 - 3:44Ziwe zimetungwa kiujanja namna gani,
-
3:44 - 3:47na rahisi kushika,
-
3:48 - 3:53hakuna nchi yeyote imewahi pitisha lugha ya kutungwa kama lugha asili.
-
3:54 - 3:59Wala kama lugha ya kigeni kufunzwa
-
3:59 - 4:03kwa mkabala mkubwa, kwa kipindi kirefu,
-
4:03 - 4:05ingawa hilo limejaribiwa.
-
4:06 - 4:12Lakini, licha ya matatizo yanayokumba lugha asili -
-
4:12 - 4:15kama makosa ya kutataniisha,
-
4:15 - 4:20tofauti ya uandishi na matamko,
-
4:20 - 4:25wakati mwengine ugumu wa fasaha -
-
4:26 - 4:27lakini licha ya hayo yote,
-
4:28 - 4:34tunaona bora kujifunza lugha zilizochipuka katikati ya watu.
-
4:36 - 4:40Lugha zilizotungwa hulenga akili.
-
4:41 - 4:45Lugha asili zina mnuso wa kuki.
-
4:46 - 4:52Kwa Nelson Mandela, kujifunza Afrikaans ilikuwa inalenga "kutambua adui."
-
4:52 - 4:57Alisema, "Unahitaji kujua lugha yao, na shauku zao,
-
4:57 - 5:00na matarajio, na uoga wao, kama unataka kuwashinda."
-
5:01 - 5:04Alifanya hilo. Lilifaulu.
-
5:05 - 5:08Lakini si wakati wote maadui wanapohusika, ama?
-
5:09 - 5:12Hii inafaa kutumika kwa uhusiano wote wa kibinaadamu.
-
5:13 - 5:18Na siwezi sema kuwa akina mama wakwe ni maadui -
-
5:18 - 5:19ki ufafanuzi.
-
5:20 - 5:23Takriban miaka saba au nane zilizopita,
-
5:23 - 5:26nilikuwa nasafiri Poland na familia yangu.
-
5:27 - 5:31Maduka yalikuwa karibu kufungwa na tulihitaji kununua chakula.
-
5:32 - 5:36Mwishowe, tulipata duka kubwa upande wa pili wa barabara.
-
5:37 - 5:42Njia pekee tungefikia duka hilo kabla kufungwa ilikuwa kugeuza gari pasipo pa kugeuka.
-
5:42 - 5:43Hivyo ndivyo nilivyofanya.
-
5:44 - 5:47Hilo lilikuwa hatari.
-
5:48 - 5:50Ilikuwa haramu kwa kweli.
-
5:52 - 5:58Nilipoegesha gari, hata kabla niziime injini -
-
5:58 - 6:00- niliskia sauti ya kubisha.
-
6:01 - 6:06Hivyo nikateremsha dirisha, na jozi mbili za macho zikatokea.
-
6:08 - 6:12Kila jozi la macho lilikuwa la polisi.
-
6:13 - 6:18Sasa, siwezi jigamba naelewa lugha ya Polish vyema
-
6:18 - 6:19kwa nyakati nzuri,
-
6:20 - 6:24lakini nyakati zilizopita niliweza kuendeleza mazungumzo.
-
6:24 - 6:28Lakini kwa mazingara yale, na dhamiri ya hatia,
-
6:29 - 6:32jicho kwa jicho na polisi, wakiwa na sare halisi,
-
6:33 - 6:38kila neno la Polish nililokuwa nikijua liliniponyoka.
-
6:40 - 6:44Na bado, sikufikiria hata kwa mda,
-
6:45 - 6:48kujaribu kusuluhisha tatizo nikitumia Kiingereza.
-
6:49 - 6:53Kiingereza nadhani kingenipatia upeo wa juu kilugha,
-
6:54 - 6:57lakini labda ingefanya polisi kuwa na wasiwasi.
-
6:58 - 7:01Hivyo, niliaminisha kubaki na lugha ya Polish.
-
7:02 - 7:03Kivipi?
-
7:04 - 7:09Ile kona yangu finyu ya lugha ya Polish ilikuwa imezima
-
7:10 - 7:12isipokuwa jambo moja.
-
7:13 - 7:18Kulikuwa na jambo moja nililokuwa nimelirudia mara nyingi
-
7:18 - 7:21hata ningeweza kulikariri nikiwa usingizini.
-
7:23 - 7:25Lilikuwa ni shairi la watoto,
-
7:28 - 7:30lililohusu chura mgonjwa.
-
7:30 - 7:32(Vicheko)
-
7:33 - 7:35Hilo ndilo nililokuwa nalo.
-
7:35 - 7:40Najua lilikuwa jambo la ajabu kufanya, lakini nilitoa kelele:
-
7:40 - 7:43(Polish) "Chura mmoja alisikia udhaifu
-
7:43 - 7:46hivyo akaenda kwa daktari na akasema ni mgonjwa.
-
7:46 - 7:50Daktari akavalia miwani yake kwa sababu alikuwa kazeeka."
-
7:52 - 7:54Niliwatazama polisi.
-
7:54 - 7:56Na walikuwa wakiniangalia kwa mshangao.
-
7:56 - 7:58(Vicheko)
-
7:59 - 8:02Nakumbuka kama mmoja wao alikuna kichwa.
-
8:03 - 8:05Alafu wote wakatabasamu.
-
8:06 - 8:07Wakatabasamu.
-
8:07 - 8:11Na hilo, kwa upande wake, likaniweka hali shwari,
-
8:11 - 8:14shwari hadi maneno machache husika yaliyopotea
-
8:14 - 8:17yangeweza kurudi akilini mwangu.
-
8:17 - 8:20Ningeweza kugugumiza sentensi chache kama,
-
8:20 - 8:23"Pole sana, nilikuwa nahitaji chakula, sitawahi kurudia hilo tena."
-
8:25 - 8:26Waliniachilia bila adhabu.
-
8:27 - 8:32Nilipokuwa nakimbia ndani ya duka, waliita, "maneno kwa lugha ya Polish!"
-
8:32 - 8:34"Uwe na safari njema!"
-
8:35 - 8:39Si lengo langu kuwashurutisha kujifunza lugha za kigeni
-
8:39 - 8:43ndio msafiri pande zote za dunia, mvunje sheria na muepuke bila adhabu.
-
8:45 - 8:49Lakini tukio hili linaonyesha vile maneno machache,
-
8:50 - 8:54ingawa rahisi au ya kijinga, maneno machache tu,
-
8:54 - 8:58yanawezaenda moja kwa moja ndani ya moyo na kuuyeyusha.
-
8:59 - 9:02Ijapo kuwa, kulikuwa na wimbo mbadala wa ule wa chura mgonjwa.
-
9:02 - 9:04Lilikuwa jambo moja nililolijua vyema sana:
-
9:06 - 9:07wimbo wa kunywa.
-
9:07 - 9:09(Kicheko)
-
9:09 - 9:11Labda hilo halingenipatia tabasamu
-
9:12 - 9:14labda safari hadi kituo cha polisi
-
9:14 - 9:16kwa uchunguzi wa damu.
-
9:18 - 9:21Si lazima ujifunze lugha nyingi,
-
9:21 - 9:24na si lazima uzijue kwa undani.
-
9:24 - 9:26Ujuzi kidogo unaweza kuwa wa manufaa makubwa.
-
9:27 - 9:30Maneno kumi yanalengayo moyoni yanaweza kuwa na athari kubwa
-
9:30 - 9:33kuliko maneno alfu moja yalengayo akili.
-
9:35 - 9:39Unaweza kuchagua kutumia Kiingereza na kukutana katikati.
-
9:40 - 9:45Lakini pia unaweza chagua kuwa yule mtu avukaye kigezo kilicho katikati
-
9:45 - 9:49na kukutana na swahiba wako au mpinzani wako, yeyote yule,
-
9:49 - 9:50kutana nao kwa maskani yao.
-
9:50 - 9:52Kuongea lugha ya mwengine haikufanyi kuwa dhaifu,
-
9:52 - 9:55inadhibitisha una nguvu.
-
9:55 - 9:57Ni yule aliye na ujasiri, na afanyaye juhudi za kuvuka vigezo
-
9:58 - 10:04anayeibuka mshindi mwishowe.
-
10:05 - 10:07Usiogope kufanya makosa. Makosa yanadhihirisha ubinadamu.
-
10:08 - 10:12Na kando na haya, kuna la ziada:
-
10:13 - 10:17Ukifanya makosa huko nje,
-
10:18 - 10:21unatoa fursa kwa wenzako kukusaidia, kukujia na kukutana nawe.
-
10:21 - 10:26Na kwa njia hii, utangamano utakaokuwa umeanzisha utakuwa wenye nguvu.
-
10:26 - 10:32Hivyo, wataka kueleweka
-
10:33 - 10:37au wataka kutangamana?
-
10:38 - 10:40Jameni tuendelee kujifunza na kukitumia Kiingereza.
-
10:42 - 10:47Ndivyo tutangamane na walio na lugha tofauti za kiasilia, kama tunavyofanya hapa TEDx.
-
10:48 - 10:53Kiingereza ni kigezo muhimu cha kueneza ujuzi,
-
10:54 - 10:58kwa mikutano ya kimataifa ya kujadili shida za kimataifa
-
10:58 - 11:04Juu ya yote, Kiingereza ni barabara kuu kufikia mioyo milioni mia tatu sitini na tano.
-
11:05 - 11:10Kwa watu mia tatu sitini na tano, lugha ya Kiingereza yanukia kuki.
-
11:11 - 11:17Lakini mbona ukomee hapo?
-
11:19 - 11:21Mbona usiongeze jitihada
-
11:22 - 11:25na kujifunza angalau lugha moja geni?
-
11:25 - 11:28Kuna ladha kadhaa za kuki.
-
11:29 - 11:32Twendeni na tuonje moja mpya.
-
11:32 - 11:34Asante.
-
11:35 - 11:36(Makofi)
-
11:36 - 11:38(Makofi)
- Title:
- Zungumza na Moyo I Marleen Laschet I TEDxTrondheim
- Description:
-
Hotuba hii ilitolewa katika jumuiko la TEDx kwa kutumia maelezo ya jumuiko la TED lakini lililopangwa na jamii kwa kujitegemea. Jifunze zaidi katika http://ted.com/tedx
Inahusika na utamu wa lugha na vile chura mgonjwa anavyoweza kukukoa.
Marleen ni mtaalamu wa lugha na mawasiliano aliye na hamu ya kuhadithi na lugha.
Katika wavuti wake ya kusihirisha, anahadithia furaha na manufaa ya kufahamu lugha zaidi ya moja na tofauti za kitamaduni. Msingi wa hadithi kwenye wavuti wake ni maisha yake kama mjuzi na mtumizi wa lugha kadhaa na ufahamu wa utamaduni na ujuzi wa lugha.
- Video Language:
- English
- Team:
closed TED
- Project:
- TEDxTalks
- Duration:
- 11:56
![]() |
Joachim Mangilima approved Swahili subtitles for Speak to the heart | Marleen Laschet | TEDxTrondheim | |
![]() |
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for Speak to the heart | Marleen Laschet | TEDxTrondheim | |
![]() |
Joachim Mangilima accepted Swahili subtitles for Speak to the heart | Marleen Laschet | TEDxTrondheim | |
![]() |
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for Speak to the heart | Marleen Laschet | TEDxTrondheim | |
![]() |
David Mvoi edited Swahili subtitles for Speak to the heart | Marleen Laschet | TEDxTrondheim | |
![]() |
David Mvoi edited Swahili subtitles for Speak to the heart | Marleen Laschet | TEDxTrondheim | |
![]() |
David Mvoi edited Swahili subtitles for Speak to the heart | Marleen Laschet | TEDxTrondheim | |
![]() |
David Mvoi edited Swahili subtitles for Speak to the heart | Marleen Laschet | TEDxTrondheim |