Safari yangu ya Ncha ya Kaskazini na kuendelea | Jade Hameister | TEDxMelbourne
-
0:07 - 0:12Vipi kama mabinti duniani kote
-
0:13 - 0:16wangehamasishwa kuwa zaidi
-
0:16 - 0:18badala ya kuwekwa chini?
-
0:19 - 0:23Vipi kama mkazo ukahama
-
0:23 - 0:26kutoka kwa jinsi tunavyoonekana
-
0:26 - 0:30mpaka uwezekano wa tunachoweza kufanya?
-
0:31 - 0:34Kama binti mdogo, ninaishi kwenye dunia
-
0:34 - 0:39ambayo mara kwa mara ninashambuliwa
na ujumbe wa kunitaka niwe duni, -
0:40 - 0:45nile kidogo, nivae kidogo, niwe mwembamba,
-
0:45 - 0:48kunyweza matarajio yangu yaweze kutoshea,
-
0:49 - 0:52kumngoja Mfalme wangu anayevutia
aje kuniokoa, -
0:52 - 0:55au kuepuka shughuli ambazo ni za wavulana
-
0:55 - 0:58kwa sababu sina nguvu ya kutosha au niliye imara.
-
0:59 - 1:03Huu ujumbe ulichochea
hofu na wasiwasi. -
1:03 - 1:05Ninabaki kufikiria mara zote
-
1:05 - 1:09kama nina uwezo wa kutosha
au nikae tu kwenye usalama -
1:09 - 1:12ili nisiishie
kuonekana mpuuzi. -
1:13 - 1:14Lakini fikiria
-
1:15 - 1:18kama wanawake wote kwenye
nchi fulani -
1:18 - 1:22wakachukua hatua moja mbele
upande wa kiasi cha kuamini -
1:22 - 1:24kwenye uwezo wao.
-
1:24 - 1:28Matumaini ya nchi hiyo
yatakuaje mbeleni? -
1:29 - 1:33Sasa fikiria kama mabinti
wote wa hii dunia -
1:33 - 1:36wangechukua hatua hiyo hiyo mbele
kwenye kufikiri kwao -
1:36 - 1:38kwa ni nini kinawezekana kwao.
-
1:39 - 1:43Matumaini ya huko mbeleni yatakuaje
kwa dunia yetu kwa kila mtu? -
1:43 - 1:46Hayo ni mawazo ya kijasiri.
-
1:47 - 1:53Na hata hivyo, ni raha zaidi
kujaribu kuwa zaidi kuliko kuwa chini. -
1:54 - 1:57Aprili mwaka huu, nikiwa na miaka 14,
-
1:57 - 2:00nilikua mdogo wa wote -
mwanaume, au mwanamke - kwenye historia -
2:00 - 2:04kuteleza kuelekea Ncha ya Kaskazini
kutoka popote nje ya Digrii ya Mwisho. -
2:04 - 2:05(Makofi)
-
2:05 - 2:06Asanteni.
-
2:06 - 2:08(Makofi)
-
2:08 - 2:10Asanteni.
-
2:11 - 2:15Ilikua pia safari ndefu zaidi kuelekea
kwenye Ncha na mwanamke yoyote duniani -
2:15 - 2:17kwenye miaka miwili iliyopita.
-
2:17 - 2:19(Makofi)
-
2:19 - 2:20Asanteni.
-
2:22 - 2:28Nilisukuma sledi iliyokuwa nzito kama
mimi, kwenye umbali zaidi ya kilomita 150 -
2:28 - 2:32kama ilivyopimwa kwenye mstari ulionyooka
kutoka kwenye Ncha, kwa kuteleza, -
2:32 - 2:34kwenye halijoto ya chini ya digrii 30.
-
2:36 - 2:36Kilomita mia na hamsini zinaweza kuonekana si mbaya sana,
-
2:38 - 2:41mpaka uelewe mazingira ya
huko juu kwenye Bahari ya Aktiki. -
2:42 - 2:46Tusingeweza kupata njia kuzungukia
au juu ya maeneo yaliyoganda -
2:46 - 2:50amapo barafu ya bahari iligongana
kutengeneza kifusi cha barafu, -
2:50 - 2:54na mara nyingine, hiki kifusi cha barafu
kinaweza kua kuta urefu wa mita baadhi kwenda juu. -
2:55 - 2:58Tulitakiwa kutafuta njia kuzungukia
mwelekezo wa maji ya wazi, -
2:58 - 3:00ambapo barafu ya bahari
ilipasuka. -
3:00 - 3:03Pale tuliposhindwa,
ilitubidi kujenga daraja na sledi zetu, -
3:03 - 3:06au mtu angeogelea
akiwa na suti ya kuzama, -
3:06 - 3:10wakati wengine tulivutwa kwenye
chelezo iliyotengenezwa na sledi zetu. -
3:11 - 3:14Tulikua tunasafiri kwenye bahari ya barafu
inayoelea, -
3:14 - 3:17hivyo mikondo ya bahari
ilikua inatufanya tupoteze mwelekeo, -
3:17 - 3:20mara nyingi tulisikia barafu
bahari ikimeguka chini yetu -
3:20 - 3:22na tukawaza kama
tungeangukia -
3:22 - 3:24chini kwenye bahari iliyoganda.
-
3:24 - 3:26Pia tulizipita nyayo za dubu wanaoishi barafuni,
-
3:26 - 3:29na tulikaa macho usiku
tukiwasikilizia, -
3:29 - 3:31sio kwamba tungelala vizuri hata hivyo,
-
3:31 - 3:34kama ilivyo ni mwangaza masaa-24 huko juu
huu mda wa mwaka. -
3:35 - 3:37Na mimi sio mtelezaji pia.
-
3:38 - 3:42Nilijifunza tu kuteleza mwaka uliopita,
kwenye safari ya siku tatu ya New Zealand. -
3:42 - 3:43(Kicheko)
-
3:44 - 3:46Hakuna barafu nyingi ninapoishi
-
3:46 - 3:49hivyo nilijifunza karibu kila siku
kwa zaidi ya mwaka kabla, -
3:49 - 3:53ikiwemo kuburuza matairi kila mahali,
ambayo ilikua karibu sana na ukweli. -
3:55 - 3:59Hivyo, unaweza fikiria,
mwendo ulikua taratibu na mgumu. -
4:00 - 4:05Licha ya malengelenge kadhaa, nilipoteza
hisia kwenye ncha za vidole vyangu, -
4:05 - 4:06ambayo hatimaye ilirudi
-
4:06 - 4:09baada ya ngozi yote kufa
na kumenyeka. -
4:10 - 4:15Na mbaya ya yote, nilipata jamidi
kwenye paja langu la juu na makalio -
4:15 - 4:18kwa kujifunua kwenye baridi
ya kuganda na upepo -
4:18 - 4:20kila mara nilipoenda chooni.
-
4:20 - 4:22(Kicheko)
-
4:22 - 4:24Lakini nilipenda.
-
4:25 - 4:28Ilikua ni uzoefu mzuri kabisa la maisha
yangu mpaka sasa, -
4:28 - 4:32na nilipenda sana hii sehemu nzuri
lakini dhaifu ya dunia yetu. -
4:33 - 4:37Na kwa jinsi nilivyotaka kurudi nyumbani
na kuona familia yangu na marafiki, -
4:37 - 4:39nilisikitika sana kuondoka.
-
4:40 - 4:44Aprili ijayo, mpango wangu ni kuteleza
kilomita 540 katikati ya Greenland -
4:44 - 4:46nitapokuwa na miaka 15,
-
4:46 - 4:48halafu, mwishoni mwa mwaka ujao,
-
4:48 - 4:53niteleze kilomita 1,170 kutoka kwenye
pwani ya Antaktika mpaka Ncha ya Kusini, -
4:53 - 4:55na mda huo, nitakua na miaka 16.
-
4:56 - 4:59Nikiweza kufika huko,
pembeni ya rekodi chache ndogo, -
4:59 - 5:02nitakua mtu mdogo wa wote
kuteleza kwenye Ncha zote mbili -
5:02 - 5:04na kukamilisha Polar Hat Trick.
-
5:06 - 5:09Nini nilichojifunza kwenye maisha
yangu mafupi mpaka sasa -
5:09 - 5:11ambacho kitafaa kuwashirikisha?
-
5:12 - 5:17Nimejifunza kua ujumbe wote ule
niliopokea kila siku kuwa chini hazifai. -
5:18 - 5:21Nimejifunza kua kwa kupanua ndoto zangu
-
5:21 - 5:24inashindikana kufikiria kuhusu
kuwa mdogo. -
5:25 - 5:28Badala ya kuangalia jinsi tunavyoonekana,
-
5:28 - 5:31tuangalie ni nini miili yetu na
akili zetu zinaweza kufanya -
5:31 - 5:33na kugundua uwezekano wa ajabu
-
5:33 - 5:37ambao unauwezo wa na unaweza
kuchangia kwenye hii dunia. -
5:38 - 5:42Hakuna kibaya na kutaka
kuboresha umbo lako, -
5:42 - 5:46lakini tatizo ni pale watu wanapojitolea
uwezo wao au afya zao -
5:46 - 5:47ili tu waingie kwenye
-
5:47 - 5:50kwenye kiwango flani cha muonekano
unaoundwa na watu wengine. -
5:51 - 5:54Tuifanye iwe kuhusu nini
unachofanya na sio jinsi unavyoonekana. -
5:55 - 5:56Ukifikiria kuhusu hilo,
-
5:56 - 6:00kinachochekesha kuhusu akaunti
nyingi za mitandao ya kijamii za mazoezi -
6:00 - 6:02ni kua zinatuma picha za wenyewe
-
6:02 - 6:06wakisimama mbele ya kioo
bila kufanya chochote. -
6:06 - 6:07(Kicheko)
-
6:07 - 6:08Hio haileti hamasa.
-
6:08 - 6:11Hio inajaribu tu kufanya sisi
wengine tujiskie vibaya. -
6:11 - 6:13Nafikiri inaleta hamasa zaidi
-
6:13 - 6:16kuona picha na video za watu
wakifanya kitu kabisa. -
6:16 - 6:17Asanteni.
-
6:17 - 6:18(Makofi)
-
6:22 - 6:24Hivyo tunabadilishaje vitu?
-
6:24 - 6:26Tunahamishaje malengo yetu?
-
6:27 - 6:31Kwa mimi, ninapoona wanawake wengine
wakisonga mbele licha ya hofu, -
6:31 - 6:33ninajifunza kinachowezekana.
-
6:33 - 6:36Kuna mifano mizuri
-
6:36 - 6:39ya wanawake kwenye historia
wakichagua kuwa zaidi. -
6:40 - 6:42Lakini kama ilivyo ajabu kwangu
-
6:42 - 6:45kwa wasichana wanaoweza kufanya kazi
ya muda huku wakisoma -
6:45 - 6:47kusaidia familia zao;
-
6:47 - 6:50wasichana wanaosimama kwa
kile wanachoamini; -
6:50 - 6:52wasichana wanaoamka kukiwa giza kila
asubuhi, -
6:52 - 6:55kujizoeza, kuwa bora katika
mchezo wanaopenda; -
6:56 - 7:00wasichana wanaokaa macho usiku kusoma kwa
bidii kufanikiwa kwenye elimu yao; -
7:01 - 7:06msichana yeyote anaekataa kukubali na
ujumbe wa kuwa chini. -
7:07 - 7:12Hivyo, kama wewe ni mzazi wangu, ndugu
yangu, mwalimu wangu, au kocha wangu, -
7:12 - 7:13basi ninaongea na wewe.
-
7:14 - 7:19Msiwe mnanilinda sana kwa sababu
tu mimi ni msichana. -
7:19 - 7:21Nihamasishe nifanye vitu vingi
-
7:21 - 7:25kwenye kukimbiza ndoto
ambazo ni muhimu kwangu na sio kwako. -
7:26 - 7:27Udada -
-
7:28 - 7:30tusherehekee mafanikio
ya marafiki zetu. -
7:30 - 7:32Tusiwashushe chini!
-
7:32 - 7:36Nimeshangazwa na msaada
niliopokea kwa marafiki zangu. -
7:36 - 7:39Lakini muhimu kuliko yote,
ni lazima kuanza na sisi wenyewe. -
7:41 - 7:44Sisi ni adui wetu wakubwa.
-
7:45 - 7:47Tunatakiwa kutoka nje ya njia zetu
wenyewe -
7:47 - 7:51na kuacha kujali sana kuhusu
nini wengine wanafikiri. -
7:51 - 7:55Ukweli ni kwamba kila mtu
anawasiwasi kuhusu -
7:55 - 7:57nini kila mtu anawaza kuhusu wao.
-
7:57 - 8:01Tunahitaji kuangalia kwenye
tunachotaka kwa ajili yetu -
8:01 - 8:03kwenye mstari na thamani zetu binafsi
-
8:03 - 8:07sio hizo za wazazi, marafiki, au
shule tunazokwenda. -
8:07 - 8:10Usifanye kwa wengine, fanya kwa ajili yako.
-
8:10 - 8:17Kuendeleza tunachoamini kinawezekana,
tunatakiwa kuwa na ujasiri,. -
8:17 - 8:22Tunatakiwa tujiandae na tuwe tayari
kushindwa. -
8:23 - 8:26Usingoje mpaka ufikiri unaweza
kufanya kitu vizuri, -
8:26 - 8:28anza tu.
-
8:29 - 8:32Nilikua tayari ninateleza mara moja
kwenye maisha yangu kabla, -
8:32 - 8:35halafu nikajaribu kuteleza kwenye Ncha ya
Kusini, -
8:35 - 8:37ambayo ni raha sana
nikiwaza kuhusu hilo. -
8:37 - 8:38(Kicheko)
-
8:38 - 8:44Nimejaribu kukojoa kwa kusimama kutumia
mpare wa kukojoa kwenye digrii 20 chini -
8:44 - 8:46na nikashindwa vibaya sana.
-
8:46 - 8:47(Kicheko)
-
8:48 - 8:49Nikatumia siku iliyobaki
-
8:49 - 8:53nikiteleza kwenye suruali iliyojaa
mkojo wangu mwenyewe ulioganda. -
8:53 - 8:55(Kicheko)
-
8:56 - 8:59Ujasiri sio kutokuwepo kwa hofu
-
9:00 - 9:02lakini nia ya kuchukua hatua
-
9:02 - 9:05licha ya uwepo wa
hofu au kutojiamini. -
9:06 - 9:10Bila ujiasiri, maisha yetu yanabaki
madogo. -
9:11 - 9:14Hivyo tujitoe kuchukua hatua
moja mbele -
9:14 - 9:17kwenye mawazo yetu na matarajio yetu
-
9:17 - 9:21kwenye nini kinawezekana
kwa mabinti kupata. -
9:21 - 9:24Tuchunguze maisha yetu mara kwa mara
-
9:24 - 9:28kua tunalenga kwenye nini tunaweza
kufanya na sio jinsi tunavyoonekana. -
9:29 - 9:32Hizo hatua zote ndogo zitaleta maana
karibuni, -
9:32 - 9:36na tutaendeleza kwa pamoja nini
kinachowezekana kwa mabinti -
9:36 - 9:39na matokeo yake,
kwa mustakabali wa dunia yetu, -
9:39 - 9:40Asanteni.
-
9:40 - 9:42(Makofi)
- Title:
- Safari yangu ya Ncha ya Kaskazini na kuendelea | Jade Hameister | TEDxMelbourne
- Description:
-
Maongezi haya yametolewa kwenye tukio la TEDx kutumia mfumo wa mikutano ya TED yakiwa yameandaliwa kipekee na jamii. Jifunze zaidi kupitia https://www.ted.com/tedx
Jade Hameister akiwa na miaka 14 tu alikua mtu mdogo wa wote kuteleza kwenye Ncha ya Kaskazini kutokea kokote nje ya Digrii ya Mwisho. Jade anataka mabinti wadogo ku #kuzauwezekano na kuwachochea na kuwawezesha kutenda zaidi na kukimbiza ndoto zao.
Jade sasa ameamua kuwa mtu mdogo wa wote kukamilisha "Polar Hat Trick," inayohusisha Ncha ya Kaskazini, Kukatiza Greenland, na Ncha ya Kusini, njia yote kutoka pwani. Anaamini kuwa na akili ya kijasiri inamaanisha kujiandaa kupinga fikra zilizopitwa na wakati, kukumbana na hatari, na kukubali kushindwa kama uwezekano.
- Video Language:
- English
- Team:
closed TED
- Project:
- TEDxTalks
- Duration:
- 10:07
![]() |
Nelson Simfukwe approved Swahili subtitles for More than we appear | Jade Hameister | TEDxMelbourne | |
![]() |
Nelson Simfukwe accepted Swahili subtitles for More than we appear | Jade Hameister | TEDxMelbourne | |
![]() |
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for More than we appear | Jade Hameister | TEDxMelbourne | |
![]() |
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for More than we appear | Jade Hameister | TEDxMelbourne | |
![]() |
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for More than we appear | Jade Hameister | TEDxMelbourne | |
![]() |
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for More than we appear | Jade Hameister | TEDxMelbourne | |
![]() |
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for More than we appear | Jade Hameister | TEDxMelbourne | |
![]() |
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for More than we appear | Jade Hameister | TEDxMelbourne |