1 00:00:07,062 --> 00:00:12,313 Vipi kama mabinti duniani kote 2 00:00:13,419 --> 00:00:15,554 wangehamasishwa kuwa zaidi 3 00:00:16,210 --> 00:00:17,633 badala ya kuwekwa chini? 4 00:00:19,227 --> 00:00:22,751 Vipi kama mkazo ukahama 5 00:00:23,471 --> 00:00:25,593 kutoka kwa jinsi tunavyoonekana 6 00:00:26,473 --> 00:00:29,690 mpaka uwezekano wa tunachoweza kufanya? 7 00:00:31,220 --> 00:00:34,100 Kama binti mdogo, ninaishi kwenye dunia 8 00:00:34,340 --> 00:00:38,853 ambayo mara kwa mara ninashambuliwa na ujumbe wa kunitaka niwe duni, 9 00:00:39,823 --> 00:00:44,728 nile kidogo, nivae kidogo, niwe mwembamba, 10 00:00:45,188 --> 00:00:48,241 kunyweza matarajio yangu yaweze kutoshea, 11 00:00:48,571 --> 00:00:51,871 kumngoja Mfalme wangu anayevutia aje kuniokoa, 12 00:00:52,141 --> 00:00:55,070 au kuepuka shughuli ambazo ni za wavulana 13 00:00:55,071 --> 00:00:57,963 kwa sababu sina nguvu ya kutosha au niliye imara. 14 00:00:58,983 --> 00:01:02,700 Huu ujumbe ulichochea hofu na wasiwasi. 15 00:01:02,701 --> 00:01:05,069 Ninabaki kufikiria mara zote 16 00:01:05,071 --> 00:01:09,200 kama nina uwezo wa kutosha au nikae tu kwenye usalama 17 00:01:09,201 --> 00:01:11,863 ili nisiishie kuonekana mpuuzi. 18 00:01:12,803 --> 00:01:14,292 Lakini fikiria 19 00:01:14,852 --> 00:01:18,110 kama wanawake wote kwenye nchi fulani 20 00:01:18,350 --> 00:01:21,630 wakachukua hatua moja mbele upande wa kiasi cha kuamini 21 00:01:21,631 --> 00:01:23,811 kwenye uwezo wao. 22 00:01:24,341 --> 00:01:28,283 Matumaini ya nchi hiyo yatakuaje mbeleni? 23 00:01:29,073 --> 00:01:32,828 Sasa fikiria kama mabinti wote wa hii dunia 24 00:01:32,829 --> 00:01:35,660 wangechukua hatua hiyo hiyo mbele kwenye kufikiri kwao 25 00:01:35,661 --> 00:01:38,341 kwa ni nini kinawezekana kwao. 26 00:01:38,701 --> 00:01:43,321 Matumaini ya huko mbeleni yatakuaje kwa dunia yetu kwa kila mtu? 27 00:01:43,322 --> 00:01:46,150 Hayo ni mawazo ya kijasiri. 28 00:01:46,610 --> 00:01:52,561 Na hata hivyo, ni raha zaidi kujaribu kuwa zaidi kuliko kuwa chini. 29 00:01:54,211 --> 00:01:57,141 Aprili mwaka huu, nikiwa na miaka 14, 30 00:01:57,142 --> 00:02:00,430 nilikua mdogo wa wote - mwanaume, au mwanamke - kwenye historia 31 00:02:00,431 --> 00:02:03,920 kuteleza kuelekea Ncha ya Kaskazini kutoka popote nje ya Digrii ya Mwisho. 32 00:02:03,921 --> 00:02:05,071 (Makofi) 33 00:02:05,072 --> 00:02:06,091 Asanteni. 34 00:02:06,092 --> 00:02:07,671 (Makofi) 35 00:02:08,392 --> 00:02:09,812 Asanteni. 36 00:02:11,132 --> 00:02:14,905 Ilikua pia safari ndefu zaidi kuelekea kwenye Ncha na mwanamke yoyote duniani 37 00:02:14,906 --> 00:02:16,805 kwenye miaka miwili iliyopita. 38 00:02:17,445 --> 00:02:18,584 (Makofi) 39 00:02:18,585 --> 00:02:19,865 Asanteni. 40 00:02:21,675 --> 00:02:27,963 Nilisukuma sledi iliyokuwa nzito kama mimi, kwenye umbali zaidi ya kilomita 150 41 00:02:27,964 --> 00:02:31,560 kama ilivyopimwa kwenye mstari ulionyooka kutoka kwenye Ncha, kwa kuteleza, 42 00:02:31,561 --> 00:02:33,784 kwenye halijoto ya chini ya digrii 30. 43 00:02:36,116 --> 00:02:36,366 Kilomita mia na hamsini zinaweza kuonekana si mbaya sana, 44 00:02:37,794 --> 00:02:41,268 mpaka uelewe mazingira ya huko juu kwenye Bahari ya Aktiki. 45 00:02:42,428 --> 00:02:46,383 Tusingeweza kupata njia kuzungukia au juu ya maeneo yaliyoganda 46 00:02:46,384 --> 00:02:49,544 amapo barafu ya bahari iligongana kutengeneza kifusi cha barafu, 47 00:02:49,545 --> 00:02:54,196 na mara nyingine, hiki kifusi cha barafu kinaweza kua kuta urefu wa mita baadhi kwenda juu. 48 00:02:55,066 --> 00:02:58,067 Tulitakiwa kutafuta njia kuzungukia mwelekezo wa maji ya wazi, 49 00:02:58,068 --> 00:02:59,646 ambapo barafu ya bahari ilipasuka. 50 00:03:00,386 --> 00:03:03,224 Pale tuliposhindwa, ilitubidi kujenga daraja na sledi zetu, 51 00:03:03,225 --> 00:03:05,986 au mtu angeogelea akiwa na suti ya kuzama, 52 00:03:05,987 --> 00:03:09,958 wakati wengine tulivutwa kwenye chelezo iliyotengenezwa na sledi zetu. 53 00:03:11,428 --> 00:03:13,929 Tulikua tunasafiri kwenye bahari ya barafu inayoelea, 54 00:03:13,930 --> 00:03:17,169 hivyo mikondo ya bahari ilikua inatufanya tupoteze mwelekeo, 55 00:03:17,170 --> 00:03:19,909 mara nyingi tulisikia barafu bahari ikimeguka chini yetu 56 00:03:19,910 --> 00:03:22,069 na tukawaza kama tungeangukia 57 00:03:22,070 --> 00:03:24,029 chini kwenye bahari iliyoganda. 58 00:03:24,030 --> 00:03:26,081 Pia tulizipita nyayo za dubu wanaoishi barafuni, 59 00:03:26,082 --> 00:03:28,791 na tulikaa macho usiku tukiwasikilizia, 60 00:03:28,792 --> 00:03:30,749 sio kwamba tungelala vizuri hata hivyo, 61 00:03:30,750 --> 00:03:34,251 kama ilivyo ni mwangaza masaa-24 huko juu huu mda wa mwaka. 62 00:03:35,231 --> 00:03:37,023 Na mimi sio mtelezaji pia. 63 00:03:37,553 --> 00:03:41,645 Nilijifunza tu kuteleza mwaka uliopita, kwenye safari ya siku tatu ya New Zealand. 64 00:03:41,646 --> 00:03:42,922 (Kicheko) 65 00:03:43,672 --> 00:03:45,721 Hakuna barafu nyingi ninapoishi 66 00:03:45,722 --> 00:03:49,121 hivyo nilijifunza karibu kila siku kwa zaidi ya mwaka kabla, 67 00:03:49,122 --> 00:03:53,242 ikiwemo kuburuza matairi kila mahali, ambayo ilikua karibu sana na ukweli. 68 00:03:55,043 --> 00:03:59,483 Hivyo, unaweza fikiria, mwendo ulikua taratibu na mgumu. 69 00:04:00,483 --> 00:04:04,704 Licha ya malengelenge kadhaa, nilipoteza hisia kwenye ncha za vidole vyangu, 70 00:04:04,705 --> 00:04:06,182 ambayo hatimaye ilirudi 71 00:04:06,183 --> 00:04:09,043 baada ya ngozi yote kufa na kumenyeka. 72 00:04:09,703 --> 00:04:14,961 Na mbaya ya yote, nilipata jamidi kwenye paja langu la juu na makalio 73 00:04:14,962 --> 00:04:18,233 kwa kujifunua kwenye baridi ya kuganda na upepo 74 00:04:18,233 --> 00:04:20,322 kila mara nilipoenda chooni. 75 00:04:20,322 --> 00:04:21,743 (Kicheko) 76 00:04:21,744 --> 00:04:24,423 Lakini nilipenda. 77 00:04:24,983 --> 00:04:27,954 Ilikua ni uzoefu mzuri kabisa la maisha yangu mpaka sasa, 78 00:04:27,955 --> 00:04:31,982 na nilipenda sana hii sehemu nzuri lakini dhaifu ya dunia yetu. 79 00:04:32,632 --> 00:04:36,672 Na kwa jinsi nilivyotaka kurudi nyumbani na kuona familia yangu na marafiki, 80 00:04:36,673 --> 00:04:38,815 nilisikitika sana kuondoka. 81 00:04:39,735 --> 00:04:44,454 Aprili ijayo, mpango wangu ni kuteleza kilomita 540 katikati ya Greenland 82 00:04:44,455 --> 00:04:45,639 nitapokuwa na miaka 15, 83 00:04:46,089 --> 00:04:48,004 halafu, mwishoni mwa mwaka ujao, 84 00:04:48,005 --> 00:04:52,714 niteleze kilomita 1,170 kutoka kwenye pwani ya Antaktika mpaka Ncha ya Kusini, 85 00:04:52,715 --> 00:04:54,795 na mda huo, nitakua na miaka 16. 86 00:04:55,805 --> 00:04:59,294 Nikiweza kufika huko, pembeni ya rekodi chache ndogo, 87 00:04:59,295 --> 00:05:02,104 nitakua mtu mdogo wa wote kuteleza kwenye Ncha zote mbili 88 00:05:02,105 --> 00:05:04,025 na kukamilisha Polar Hat Trick. 89 00:05:05,935 --> 00:05:08,676 Nini nilichojifunza kwenye maisha yangu mafupi mpaka sasa 90 00:05:08,677 --> 00:05:10,693 ambacho kitafaa kuwashirikisha? 91 00:05:11,673 --> 00:05:17,172 Nimejifunza kua ujumbe wote ule niliopokea kila siku kuwa chini hazifai. 92 00:05:18,257 --> 00:05:20,906 Nimejifunza kua kwa kupanua ndoto zangu 93 00:05:20,907 --> 00:05:24,077 inashindikana kufikiria kuhusu kuwa mdogo. 94 00:05:24,937 --> 00:05:27,595 Badala ya kuangalia jinsi tunavyoonekana, 95 00:05:27,596 --> 00:05:30,856 tuangalie ni nini miili yetu na akili zetu zinaweza kufanya 96 00:05:30,857 --> 00:05:32,998 na kugundua uwezekano wa ajabu 97 00:05:32,998 --> 00:05:37,168 ambao unauwezo wa na unaweza kuchangia kwenye hii dunia. 98 00:05:38,018 --> 00:05:41,566 Hakuna kibaya na kutaka kuboresha umbo lako, 99 00:05:41,567 --> 00:05:46,106 lakini tatizo ni pale watu wanapojitolea uwezo wao au afya zao 100 00:05:46,107 --> 00:05:47,485 ili tu waingie kwenye 101 00:05:47,486 --> 00:05:50,386 kwenye kiwango flani cha muonekano unaoundwa na watu wengine. 102 00:05:50,676 --> 00:05:53,997 Tuifanye iwe kuhusu nini unachofanya na sio jinsi unavyoonekana. 103 00:05:54,837 --> 00:05:56,485 Ukifikiria kuhusu hilo, 104 00:05:56,486 --> 00:06:00,227 kinachochekesha kuhusu akaunti nyingi za mitandao ya kijamii za mazoezi 105 00:06:00,228 --> 00:06:02,278 ni kua zinatuma picha za wenyewe 106 00:06:02,279 --> 00:06:05,749 wakisimama mbele ya kioo bila kufanya chochote. 107 00:06:05,750 --> 00:06:06,868 (Kicheko) 108 00:06:06,869 --> 00:06:08,258 Hio haileti hamasa. 109 00:06:08,259 --> 00:06:11,003 Hio inajaribu tu kufanya sisi wengine tujiskie vibaya. 110 00:06:11,113 --> 00:06:12,940 Nafikiri inaleta hamasa zaidi 111 00:06:12,941 --> 00:06:16,110 kuona picha na video za watu wakifanya kitu kabisa. 112 00:06:16,111 --> 00:06:17,231 Asanteni. 113 00:06:17,232 --> 00:06:18,452 (Makofi) 114 00:06:21,692 --> 00:06:23,580 Hivyo tunabadilishaje vitu? 115 00:06:23,860 --> 00:06:26,249 Tunahamishaje malengo yetu? 116 00:06:26,759 --> 00:06:30,757 Kwa mimi, ninapoona wanawake wengine wakisonga mbele licha ya hofu, 117 00:06:30,758 --> 00:06:32,920 ninajifunza kinachowezekana. 118 00:06:33,390 --> 00:06:35,850 Kuna mifano mizuri 119 00:06:35,851 --> 00:06:39,151 ya wanawake kwenye historia wakichagua kuwa zaidi. 120 00:06:39,571 --> 00:06:41,822 Lakini kama ilivyo ajabu kwangu 121 00:06:41,823 --> 00:06:44,801 kwa wasichana wanaoweza kufanya kazi ya muda huku wakisoma 122 00:06:44,802 --> 00:06:46,542 kusaidia familia zao; 123 00:06:46,822 --> 00:06:49,840 wasichana wanaosimama kwa kile wanachoamini; 124 00:06:49,841 --> 00:06:52,082 wasichana wanaoamka kukiwa giza kila asubuhi, 125 00:06:52,083 --> 00:06:55,083 kujizoeza, kuwa bora katika mchezo wanaopenda; 126 00:06:55,593 --> 00:07:00,315 wasichana wanaokaa macho usiku kusoma kwa bidii kufanikiwa kwenye elimu yao; 127 00:07:01,045 --> 00:07:05,856 msichana yeyote anaekataa kukubali na ujumbe wa kuwa chini. 128 00:07:07,335 --> 00:07:11,524 Hivyo, kama wewe ni mzazi wangu, ndugu yangu, mwalimu wangu, au kocha wangu, 129 00:07:11,525 --> 00:07:13,313 basi ninaongea na wewe. 130 00:07:14,443 --> 00:07:19,039 Msiwe mnanilinda sana kwa sababu tu mimi ni msichana. 131 00:07:19,339 --> 00:07:21,137 Nihamasishe nifanye vitu vingi 132 00:07:21,137 --> 00:07:25,010 kwenye kukimbiza ndoto ambazo ni muhimu kwangu na sio kwako. 133 00:07:26,060 --> 00:07:27,348 Udada - 134 00:07:27,668 --> 00:07:30,495 tusherehekee mafanikio ya marafiki zetu. 135 00:07:30,496 --> 00:07:32,157 Tusiwashushe chini! 136 00:07:32,158 --> 00:07:35,529 Nimeshangazwa na msaada niliopokea kwa marafiki zangu. 137 00:07:35,829 --> 00:07:39,499 Lakini muhimu kuliko yote, ni lazima kuanza na sisi wenyewe. 138 00:07:40,608 --> 00:07:44,149 Sisi ni adui wetu wakubwa. 139 00:07:44,579 --> 00:07:46,638 Tunatakiwa kutoka nje ya njia zetu wenyewe 140 00:07:46,639 --> 00:07:50,680 na kuacha kujali sana kuhusu nini wengine wanafikiri. 141 00:07:51,090 --> 00:07:54,661 Ukweli ni kwamba kila mtu anawasiwasi kuhusu 142 00:07:54,662 --> 00:07:57,041 nini kila mtu anawaza kuhusu wao. 143 00:07:57,431 --> 00:08:00,570 Tunahitaji kuangalia kwenye tunachotaka kwa ajili yetu 144 00:08:00,571 --> 00:08:03,221 kwenye mstari na thamani zetu binafsi 145 00:08:03,222 --> 00:08:06,728 sio hizo za wazazi, marafiki, au shule tunazokwenda. 146 00:08:06,729 --> 00:08:09,714 Usifanye kwa wengine, fanya kwa ajili yako. 147 00:08:10,494 --> 00:08:16,655 Kuendeleza tunachoamini kinawezekana, tunatakiwa kuwa na ujasiri,. 148 00:08:17,425 --> 00:08:21,836 Tunatakiwa tujiandae na tuwe tayari kushindwa. 149 00:08:22,756 --> 00:08:26,255 Usingoje mpaka ufikiri unaweza kufanya kitu vizuri, 150 00:08:26,256 --> 00:08:28,026 anza tu. 151 00:08:28,546 --> 00:08:32,283 Nilikua tayari ninateleza mara moja kwenye maisha yangu kabla, 152 00:08:32,284 --> 00:08:34,544 halafu nikajaribu kuteleza kwenye Ncha ya Kusini, 153 00:08:34,784 --> 00:08:37,365 ambayo ni raha sana nikiwaza kuhusu hilo. 154 00:08:37,366 --> 00:08:38,486 (Kicheko) 155 00:08:38,486 --> 00:08:43,583 Nimejaribu kukojoa kwa kusimama kutumia mpare wa kukojoa kwenye digrii 20 chini 156 00:08:43,585 --> 00:08:45,635 na nikashindwa vibaya sana. 157 00:08:45,636 --> 00:08:47,006 (Kicheko) 158 00:08:47,526 --> 00:08:48,933 Nikatumia siku iliyobaki 159 00:08:48,934 --> 00:08:53,126 nikiteleza kwenye suruali iliyojaa mkojo wangu mwenyewe ulioganda. 160 00:08:53,127 --> 00:08:54,555 (Kicheko) 161 00:08:55,845 --> 00:08:59,024 Ujasiri sio kutokuwepo kwa hofu 162 00:08:59,644 --> 00:09:02,076 lakini nia ya kuchukua hatua 163 00:09:02,406 --> 00:09:05,373 licha ya uwepo wa hofu au kutojiamini. 164 00:09:06,163 --> 00:09:09,677 Bila ujiasiri, maisha yetu yanabaki madogo. 165 00:09:10,747 --> 00:09:14,203 Hivyo tujitoe kuchukua hatua moja mbele 166 00:09:14,204 --> 00:09:17,023 kwenye mawazo yetu na matarajio yetu 167 00:09:17,024 --> 00:09:20,645 kwenye nini kinawezekana kwa mabinti kupata. 168 00:09:21,205 --> 00:09:23,545 Tuchunguze maisha yetu mara kwa mara 169 00:09:23,546 --> 00:09:27,805 kua tunalenga kwenye nini tunaweza kufanya na sio jinsi tunavyoonekana. 170 00:09:28,885 --> 00:09:31,925 Hizo hatua zote ndogo zitaleta maana karibuni, 171 00:09:31,926 --> 00:09:36,482 na tutaendeleza kwa pamoja nini kinachowezekana kwa mabinti 172 00:09:36,483 --> 00:09:39,376 na matokeo yake, kwa mustakabali wa dunia yetu, 173 00:09:39,376 --> 00:09:40,409 Asanteni. 174 00:09:40,409 --> 00:09:41,799 (Makofi)