Namna gani nyuki wanaweza kuleta amani kati ya tembo na binadamu
-
0:01 - 0:03Kwa kadiri ninavyoweza kumbuka,
-
0:03 - 0:07Tembo wa Afrika wamekuwa wakinijaza furaha mno.
-
0:08 - 0:11Ni wanyama wakubwa zaidi wa nchi kavu na wanaonyonyesha waliopo hai nyakati hizi,
-
0:11 - 0:13wakifikia hadi uzito wa tani saba,
-
0:13 - 0:17wakiwa na urefu wa mita tatu na nusu kufikia mabega yao.
-
0:17 - 0:20Wana uwezo wa kula chakula hadi kiasi cha kilo 400 kwa siku,
-
0:20 - 0:25na wanasambaza mbegu muhimu za mimea kwa takribani maelfu ya kilomita
-
0:25 - 0:27katika kipindi cha miaka 50 hadi 60 ya maisha yao.
-
0:28 - 0:32Tembo jike ni kiini cha jamii yao iliyo karimu na ngumu kuielewa.
-
0:32 - 0:36Hawa jike, viongozi imara hukuza watoto
-
0:36 - 0:39na kuongoza njia katika kuzishinda changamoto zilizopo kwenye mbuga za Afrika
-
0:39 - 0:41kutafuta chakula, maji na usalama.
-
0:42 - 0:43Jamii zao ni ngumu kuzielewa,
-
0:43 - 0:46bado hatujafanikiwa kuweza tambua
-
0:46 - 0:48namna gani wanawasiliana, namna gani wanabadilishana maongezi,
-
0:48 - 0:50namna gani wanatumia lugha zao.
-
0:50 - 0:54Na hatuelewi kiundani namna gani wanatafuta njia katika uwanda,
-
0:54 - 0:57kukumbuka njia zilizo salama katika kuvuka mto.
-
0:58 - 0:59Nina uhakika kabisa kama nilivyo mimi,
-
1:00 - 1:03wengi wenu mliomo humu mtakuwa na hisia chanya zinazofanana
-
1:03 - 1:06kwa wanyama hawa maridadi kuliko wanyama wote.
-
1:06 - 1:09Ni ngumu sana kutoangalia makala ya televisheni,
-
1:09 - 1:10kujifunza kuhusu uwezo wao mkubwa wa akili
-
1:10 - 1:13au, kama umeshawahi bahatika, kuwaona kwa macho yako
-
1:13 - 1:14wakati ukitembelea mbuga.
-
1:15 - 1:17Lakini najiuliza wangapi kati yenu
-
1:17 - 1:21kiukweli kabisa, mmewahi kuwaogopa wanyama hawa.
-
1:22 - 1:25Nilibahatika kukulia kusini mwa Afrika
-
1:25 - 1:26wazazi wangu wakiwa ni walimu
-
1:26 - 1:29waliokuwa na likizo ndefu lakini bajeti isiyomudu mambo mengi.
-
1:30 - 1:33Na hivyo tulikuwa tukitumia gari yetu kuukuu aina ya Ford Cortina Estate,
-
1:33 - 1:35na dada yangu, tutapakia mizigo nyuma ya gari,
-
1:35 - 1:38tutabeba mahema na kwenda kuweka kambi katika mbuga mbalimbali
-
1:38 - 1:40kusini mwa Afrika
-
1:40 - 1:43Ilikuwa ni kama hisia inayokaribia na ya mbinguni, kwa mtafiti mdogo wa wanyama ninaechipukia kama mimi.
-
1:43 - 1:46Lakini nakumbuka hata katika umri ule mdogo
-
1:46 - 1:49ambapo niliona senyenge ndefu za umeme zilizozunguka mbuga
-
1:49 - 1:51zikileta mgawanyiko.
-
1:51 - 1:54Hakika, ziliwazuia tembo kuishi na jamii,
-
1:54 - 1:57lakini pia zilizuia jamii kuweza fika katika mapori.
-
1:58 - 2:02Ilikuwa ni changamoto sana katika umri ule mdogo.
-
2:02 - 2:05Ilikuwa ni mpaka nilipohamia Kenya nikiwa na umri wa miaka 14,
-
2:05 - 2:10Nilipoweza kukutana na sehemu za pori zilizo kubwa ndani ya Afrika Mashariki.
-
2:10 - 2:14Na hapa sasa ninahisi kweli, binafsi,
-
2:14 - 2:15nipo nyumbani.
-
2:16 - 2:20Nimeishi miaka mingi ya furaha, nikiwatafiti tembo nikiwa ndani ya hema,
-
2:20 - 2:22katika mbuga ya taifa ya Samburu,
-
2:22 - 2:26chini ya uangalizi wa Profesa Fritz Vollrath na Iain Douglas-Hamilton,
-
2:26 - 2:31nikisomea shahada ya uzamivu na kuelewa mambo mengi magumu ya jamii za tembo.
-
2:32 - 2:36Lakini sasa, katika jukumu langu nikiwa kama mkuu wa programu ya uwepo tembo na binadamu pamoja
-
2:36 - 2:37kwa ajili ya mradi wa Okoa Tembo,
-
2:37 - 2:41tunaona mabadiliko mengi yakitokea haraka
-
2:41 - 2:45ambayo yanachochea mabadiliko katika programu zetu za utafiti.
-
2:45 - 2:49Hatuwezi tena tukakaa na kuelewa jamii za tembo
-
2:49 - 2:52au kujifunza namna za kuzuia biashara ya pembe za tembo,
-
2:52 - 2:54ambayo inatisha na bado inaendelea.
-
2:54 - 2:57Tunahitajika kubadili rasilimali zetu zaidi na zaidi
-
2:57 - 3:01tukiangazia matatizo yanajitokeza katika migogoro ya binadamu na tembo,
-
3:01 - 3:05pale binadamu na tembo wanapogombania nafasi na rasilimali.
-
3:06 - 3:08Ni hivi karibuni katika miaka ya 1970
-
3:08 - 3:12ambapo tulikuwa na tembo takribani milioni 1.2 wakizunguka Afrika.
-
3:12 - 3:17Leo hii, tuna takaribani tembo 400,000 waliosalia.
-
3:17 - 3:21Na katika wakati huo huo, jamii ya binadamu imeongezeka mara nne,
-
3:21 - 3:24na ardhi inagawanywa katika kasi
-
3:24 - 3:26ambayo ni ngumu kwenda nayo.
-
3:27 - 3:30Mara nyingi, tembo hawa wanaohama huishia katika jamii za binadamu,
-
3:30 - 3:32wakitafuta maji na chakula
-
3:32 - 3:34lakini huishia kuvunja pipa za maji
-
3:34 - 3:35wakivunja mabomba
-
3:35 - 3:38na, pia, huvunja maghala ya chakula.
-
3:38 - 3:40Ni changamoto kubwa mno.
-
3:41 - 3:42Unaweza fikiria hatari
-
3:43 - 3:46ya tembo akiwa anavunja paa la nyumba yako ya udongo
-
3:46 - 3:47usiku wa manane
-
3:47 - 3:50na kuwatupa watoto wako pembeni
-
3:50 - 3:54anaposogeza mkonga, akitafuta chakula katika giza?
-
3:55 - 3:57Tembo hawa wanakanyaga na kula mazao,
-
3:57 - 4:00na hii inaondoa
-
4:00 - 4:03uvumilivu ambao watu wamekuwa nao kwa tembo.
-
4:03 - 4:07Na cha kusikitisha, tunawapoteza wanyama hawa ndani ya siku
-
4:07 - 4:10na, katika baadhi ya nchi, ndani ya saa --
-
4:10 - 4:11si tu kwa ajili kupata pembe za ndovu
-
4:11 - 4:14lakini mgogoro huu unaokua haraka kati ya binadamu na tembo
-
4:14 - 4:17wanapogombania nafasi na rasilimali.
-
4:17 - 4:18Ni changamoto kubwa mno.
-
4:18 - 4:21Namaanisha, unawezaje kupambana na tembo wa tani saba,
-
4:21 - 4:23ambao kwa kawaida huja katika makundi ya tembo 10 au 12,
-
4:23 - 4:26katika mashamba madogo ya kijijini
-
4:26 - 4:27unapokuwa unaongelea watu
-
4:27 - 4:30ambao wanaishi katika ufukara?
-
4:30 - 4:32Hawana bajeti kubwa.
-
4:32 - 4:35Unawezaje kusuluhisha?
-
4:35 - 4:39Pengine, labda suala laweza kuwa hivi, unaweza anza kujenga senyenge ya umeme,
-
4:39 - 4:41na hili linatokea Afrika kote,
-
4:41 - 4:42tunaliona likitokea zaidi na zaidi.
-
4:42 - 4:46Lakini wanagawanya maeneo na kufunga njia.
-
4:46 - 4:49Na ninakueleza, hawa tembo hawajali zaidi kuhusu hili,
-
4:49 - 4:52iwapo watazuia shimo muhimu la maji
-
4:52 - 4:53ambapo wanahitaji maji,
-
4:53 - 4:56au kuna jike linalovutia upande wa pili.
-
4:56 - 4:59Haichukui muda kuvunja nguzo mojawapo ya senyenge.
-
4:59 - 5:01Na mara panapotokea mwanya katika senyenge,
-
5:01 - 5:02wanarudi tena, wanaongea na wenzao na ghafla wote wanapita kwenda upande wa pili,
-
5:02 - 5:04na mwishoni wote wanakuwa wamepita,
-
5:04 - 5:08na sasa unao tembo 12 katika upande jamii ya binadamu inapoishi.
-
5:08 - 5:10Na upo katika hatari kwelikweli.
-
5:10 - 5:14Watu hujaribu kuja na namna mbalimbali za senyenge za umeme.
-
5:14 - 5:17Hata hivyo, tembo hawa hawafikiri sana kuhusu hilo.
-
5:18 - 5:21(Kicheko)
-
5:23 - 5:27Kwa hiyo badala ya kuwa na hizi senyenge ngumu, zilizo na umeme,
-
5:27 - 5:31ambazo zinaleta mgawanyo wa tembo na binadamu kuhama,
-
5:31 - 5:34lazima kuwepo na namna nyingine ya kutazamia changamoto hii.
-
5:34 - 5:37Ninaangazia zaidi katika njia ambayo ni ya jumla na iliyo ya asili
-
5:37 - 5:40ili kuwatenganisha wanadamu na tembo pale inapohitajika.
-
5:40 - 5:42Kwa urahisi kuongea na watu,
-
5:42 - 5:44kuongea na wafugaji wa vijijini kaskazini mwa Kenya
-
5:44 - 5:47ambao wana uzoefu mkubwa wa porini,
-
5:47 - 5:51tuligundua hii hadithi ya kwamba walikuwapo tembo ambao hawali majani ya miti
-
5:51 - 5:53ambayo ina mizinga ya nyuki.
-
5:53 - 5:55Sasa hii ilikuwa ni hadithi ya kuvutia.
-
5:55 - 5:57Tembo walipokuwa wakila katika miti,
-
5:57 - 6:00walivunja matawi na pengine kuharibu mizinga ya nyuki.
-
6:00 - 6:04Na wale nyuki watakimbia kutoka katika makazi yao
-
6:04 - 6:05na kuwang'ata tembo.
-
6:05 - 6:07Sasa kama tembo watang'atwa,
-
6:07 - 6:10pengine watakumbuka kwamba mti huu ni hatari
-
6:10 - 6:12na hawatorudi sehemu ile.
-
6:12 - 6:15Inaonekana kwamba haiwezekani kung'atwa katika ngozi yao nene --
-
6:15 - 6:18ngozi ya tembo ni takribani sentimeta mbili.
-
6:18 - 6:20Lakini inaonekana nyuki huwang'ata katika sehemu ambazo zina maji maji,
-
6:21 - 6:25kuzunguka macho, nyuma ya masikio, katika mdomo, juu ya mkonga.
-
6:25 - 6:28Unaweza kuona kwamba watakumbuka kwa urahisi zaidi.
-
6:28 - 6:31Na si kwamba wanaogopa kung'atwa mara moja.
-
6:31 - 6:34Nyuki wa Afrika wana uwezo wa ajabu:
-
6:34 - 6:37waking'ata sehemu, hutoa kemikali iitwayo pheromone
-
6:37 - 6:40ambayo huchochea nyuki wengine kung'ata sehemu hiyo hiyo.
-
6:40 - 6:42Kwa si mng'ato mmoja wanaoogopa --
-
6:42 - 6:44lakini pengine ming'ato takribani elfu ya nyuki,
-
6:44 - 6:47kuja kung'ata sehemu hiyo hiyo -- hicho ndicho wanachoogopa.
-
6:48 - 6:50Na hivyo, mama mzuri
-
6:50 - 6:53huwaepusha mbali watoto zake na hatari hiyo.
-
6:53 - 6:55tembo wadogo wana ngozi nyembamba,
-
6:55 - 6:57na inapelekea uwezekano wa kuweza kung'atwa
-
6:57 - 6:58katika ngozi zao nyembamba.
-
6:59 - 7:02Hivyo kwa ajili ya shahada ya uzamivu, nilipata changamoto hii isiyo kawaida
-
7:02 - 7:04katika kujaribu kutafuta namna
-
7:04 - 7:08namna gani tembo na nyuki wa Afrika wanaweza kuwa pamoja,
-
7:08 - 7:11wakati nadharia inasema hawawezi changamana kabisa.
-
7:11 - 7:13Niliwezaje kufanyia utafiti hili suala?
-
7:13 - 7:17Sasa, nilirekodi mlio wa nyuki wa Afrika waliokasirishwa,
-
7:17 - 7:20na nikauchezesha karibu na tembo waliopumzika chini ya miti
-
7:20 - 7:22kupitia spika isiyotumia waya,
-
7:22 - 7:26hivyo ingenipelekea kuelewa namna gani wangeitikia kama kungekuwepo na nyuki pori katika eneo lile.
-
7:26 - 7:30Na ilitokea kwamba waliitikia katika namna ya kustaajabu
-
7:30 - 7:32kutokana na sauti ile ya nyuki pori.
-
7:33 - 7:37Hapa sasa, sauti ya nyuki ikisikika katika kundi hili la tembo.
-
7:37 - 7:39Utaona masikio yao yanaenda juu, yanatoka nje,
-
7:39 - 7:42wanageuza vichwa vyao kila pande,
-
7:42 - 7:45tembo mmoja anachezesha mkonga wake akijaribu kunusa.
-
7:45 - 7:48Kuna tembo mmoja anayempiga mtoto katika ardhi
-
7:48 - 7:51akimueleza asimame kwa vile kuna hatari.
-
7:51 - 7:54Na tembo mmoja anarudi nyuma,
-
7:54 - 7:58na baada ya muda mfupi familia yote ya tembo inakimbia kumfata
-
7:58 - 8:01kwenye nyika katika wingu la vumbi.
-
8:01 - 8:03(Sauti ya nyuki wakilia)
-
8:08 - 8:10(Sauti ya nyuki inafikia ukingoni)
-
8:10 - 8:14Nimefanya utafiti huu mara nyingi sana,
-
8:14 - 8:17na tembo hukimbia.
-
8:17 - 8:18Si tu kukimbia,
-
8:19 - 8:21Lakini hujichafua pale wanapokimbia,
-
8:21 - 8:23ili kuweza kuwafukuzza nyuki kutoka hewani.
-
8:24 - 8:27Na tuliweka vipaza sauti vya kunasa mawimbi ya chini ya sauti kuwazunguka tembo
-
8:27 - 8:29tukiwa tunafanya utafiti huu.
-
8:29 - 8:32Na tukagundua kwamba wanawasiliana katika sauti za mawimbi ya chini wakinguruma
-
8:32 - 8:34wakijaribu kuambiana kuhusu hatari ya nyuki
-
8:34 - 8:36na kukaa mbali na eneo lile.
-
8:37 - 8:39Hivyo ugunduzi huu wa tabia
-
8:39 - 8:41ulitasaidia kuelewa namna gani tembo wanaitikia
-
8:41 - 8:44wanaposikia au kuwaona nyuki.
-
8:44 - 8:48Hii ilinisaidia kutengeneza ubunifu mpya wa senyenge ya mizinga ya nyuki,
-
8:48 - 8:51ambayo kwa sasa tunajenga katika mashamba madogo ya kati ya ekari moja hadi mbili
-
8:51 - 8:54katika sehemu ambazo zina tatizo hili kwa kiasi kikubwa
-
8:54 - 8:57ambapo binadamu na tembo hugombania nafasi.
-
8:57 - 8:59Senyenge hizi za mizinga ya nyuki ni rahisi sana.
-
8:59 - 9:03Tunatumia mizinga 12 ya mizinga 12 mingine bandia
-
9:03 - 9:05ili kulinda ekari moja ya shamba.
-
9:05 - 9:07Sasa mzinga bandia ni kipande cha mbao
-
9:07 - 9:10ambacho hukatwa katika mraba, kupakwa rangi ya njano
-
9:10 - 9:11na kuning'inizwa katika mizinga halisi.
-
9:11 - 9:13Kimsingi tunawapumbaza tembo
-
9:13 - 9:16kwamba kuna mizinga ya nyuki mingi kuliko iliyopo.
-
9:16 - 9:19Na hata hivyo, inaokoa nusu gharama ya senyenge.
-
9:19 - 9:21Kwa hivyo kuna mzinga halisi na ulio bandia
-
9:21 - 9:22na mzinga halisi tena ukifatiwa na ulio wa bandia,
-
9:22 - 9:25kila mita 10 kuzunguka mpaka wa nje.
-
9:25 - 9:27Inashikiliwa na nguzo
-
9:27 - 9:29na kivuli cha paa ili kulinda nyuki,
-
9:29 - 9:32na imeunganishwa na kipande cha kawaida cha waya,
-
9:32 - 9:34ambacho kinazunguka kwenye shamba lote, kikiunganisha mizinga.
-
9:34 - 9:37Hivyo kama tembo atajaribu kuingia katika shamba,
-
9:37 - 9:39atakwepa mizinga ya nyuki katika namna yoyote ile,
-
9:39 - 9:42lakini atajaribu kusukuma katika mzinga halisi na bandia,
-
9:42 - 9:45kusababisha mizinga yote kutikisika pale waya unapogonga mzinga.
-
9:45 - 9:47Na tunajua kutokana na utafiti wetu,
-
9:47 - 9:50hii itasababisha tembo kukimbia mbali na eneo lile --
-
9:50 - 9:54na pia kukumbuka kutokurudi eneo lile ambalo ni hatari.
-
9:54 - 9:56Nyuki watatoka kwenye mizinga,
-
9:56 - 9:58na kuwafukuza tembo.
-
9:59 - 10:02Mizinga hii tunaifatilia kwa kufunga kamera
-
10:02 - 10:04ili kutusaidia kuelewa namna gani tembo wanaitikia
-
10:04 - 10:06katika nyakati za usiku,
-
10:06 - 10:08ambapo ni muda uharibifu wa mazao hutokea sana.
-
10:08 - 10:10Katika mashamba darasa yetu tuligundua
-
10:10 - 10:13kwamba tunafukuza asilimia 80 ya tembo
-
10:13 - 10:15kutoweza kuingia katika shamba.
-
10:16 - 10:21Na nyuki husaidia uchavushaji katika eneo lile.
-
10:21 - 10:24Hivyo tunafakiwa kupunguza sana uharibifu wa mazao na idadi ya tembo wanaoshambulia mashamba
-
10:24 - 10:27na kuongeza mazao kutokana na uchavushaji
-
10:27 - 10:30ambao nyuki wanaufanya kwenye mazao.
-
10:31 - 10:33Nguvu ya senyenge za mizinga ya nyuki ni muhimu sana --
-
10:33 - 10:35koloni zinatakiwa kuwa imara.
-
10:35 - 10:38Hivyo tunajaribu kuwasaidia wakulima kukuza mazao yanasaidia uchavushaji
-
10:38 - 10:40ili kuweza kukuza mizinga yao,
-
10:40 - 10:42kuongeza nguvu ya nyuki zao
-
10:42 - 10:45na, hivyo, kutengeneza asali bora zaidi.
-
10:45 - 10:49Asali hii ina thamani kubwa kama kipato cha ziada kwa wakulima.
-
10:49 - 10:51Ni mbadala wa sukari wenye afya,
-
10:51 - 10:53na kwa jamii yetu,
-
10:53 - 10:56ni zawadi yenye thamani sana kumpa mama mkwe,
-
10:56 - 10:57ambapo inakuwa kama tunu.
-
10:57 - 11:00(Kicheko)
-
11:00 - 11:02Sasa tunaweka asali hii kwenye chupa,
-
11:02 - 11:06na tumeipa asali hii jina la Asali Rafiki kwa Tembo.
-
11:06 - 11:07Ni jina la kufurahisha,
-
11:07 - 11:09lakini pia limeleta usikivu katika mradi wetu
-
11:09 - 11:12na kusaidia kuelewa ni kipi tunachojaribu kufanya
-
11:12 - 11:13ili kuokoa tembo.
-
11:13 - 11:14Tunafanya kazi na wakina mama wengi sana
-
11:15 - 11:17katika sehemu 60 zilzo na migogoro ya binadamu na tembo
-
11:17 - 11:20katika nchi 19 zilizopo Afrika na Asia
-
11:20 - 11:22kujenga senyenge hizi za mizinga,
-
11:22 - 11:24tukifanya kazi kwa ukaribu na wakulima wengi
-
11:24 - 11:26lakini hasa kwa sasa na wakulima wanawake,
-
11:26 - 11:30kuwasaidia kuishi maisha yenye amani na tembo.
-
11:30 - 11:33Moja ya vitu tunavyojaribu kufanya ni kutengeneza mifumo ya machaguo
-
11:33 - 11:36ili kuishi katika amani na hawa tembo wakubwa.
-
11:36 - 11:38Moja ya masuala hayo ni kujaribu kuwafanya wakulima,
-
11:38 - 11:40na wanawake kwa ujumla.
-
11:40 - 11:42kuwaza kwa upana kuhusu ni mazao gani wanayopanda
-
11:42 - 11:43katika mashamba yao.
-
11:43 - 11:45Hivyo tunatazamia kupanda mazao
-
11:45 - 11:48ambayo tembo hawahitaji kula, kama pilipili,
-
11:48 - 11:50tangawizi, moringa, alizeti.
-
11:50 - 11:53Na hakika, nyuki na mizinga ya nyuki hupenda mazao haya pia,
-
11:53 - 11:55kwa sababu yana maua mazuri.
-
11:55 - 11:58Moja ya mazao haya ni zao lenye miiba liitwalo katani --
-
11:58 - 12:00hapa mnalifahamu kama jute.
-
12:00 - 12:03Na mmea huu unaweza kuchanwa
-
12:03 - 12:05na kugeuzwa katika bidhaa ya kufumia.
-
12:05 - 12:07Tunashirikiana na wanawake hawa
-
12:07 - 12:10ambao wanaishi kila siku na changamoto ya tembo
-
12:10 - 12:13kutumia mmea huu kufumia vikapu
-
12:13 - 12:15kujitengenezea kipato.
-
12:16 - 12:18Tumeanza ujenzi wiki tatu zilizopita
-
12:18 - 12:20wa kituo cha biashara cha kinamama
-
12:20 - 12:23ambapo tutakuwa tukishirikiana na wanawake hawa
-
12:23 - 12:24si tu kama wataalamu wa utunzaji nyuki
-
12:24 - 12:26lakini kama wasuka vikapu maridadi;
-
12:26 - 12:29watachakata mafuta ya pilipili, alizeti
-
12:29 - 12:31kutengeneza ving'arisha midomo na asali,
-
12:31 - 12:34na tupo mahala katika safari yetu ili kusaidia hawa wakulima
-
12:34 - 12:39kuishi katika miradi rafiki iliyo bora
-
12:39 - 12:40katika kuishi na tembo.
-
12:40 - 12:42Hivyo ikiwa ni tembo
-
12:42 - 12:45au akinamama au watafiti kama mimi,
-
12:45 - 12:48Nawaona wanawake wakija mstari wa mbele sasa
-
12:48 - 12:52kuwaza tofauti na kwa ufasaha kuhusu changamoto tunazokutana nazo.
-
12:52 - 12:54Tukiwa na ubunifu zaidi,
-
12:54 - 12:58na pengine kuweza kujaliana,
-
12:58 - 13:01Ninaamini tunaweza kutoka katika migogoro na tembo
-
13:01 - 13:03na kuweza kuishi nao kwa uhalisia.
-
13:03 - 13:04Asante.
-
13:05 - 13:11(Makofi)
- Title:
- Namna gani nyuki wanaweza kuleta amani kati ya tembo na binadamu
- Speaker:
- Lucy King
- Description:
-
Jaribu kutafakari kuamka usiku wa manane huku tembo akivunja paa la nyumba yako akitafuta chakula. Huu ni uhalisia katika baadhi ya jamii barani Afrika ambapo, mapori yanavyozidi kupungua, binadamu na tembo wanaanza kugombania nafasi na rasilimali. Katika hotuba hii ya kusisimua, mtaalamu wa wanyama Lucy King anatushirikisha katika utatuzi katika mgogoro unaokua: senyenge zinazotengenezwa kutokana na mizinga ya nyuki ambazo zinawafanya tembo kutoharibu mazao shambani na kuongeza kipato kwa wakulima.
- Video Language:
- English
- Team:
closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 13:10
![]() |
Joachim Mangilima approved Swahili subtitles for How bees can keep the peace between elephants and humans | |
![]() |
Joachim Mangilima accepted Swahili subtitles for How bees can keep the peace between elephants and humans | |
![]() |
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for How bees can keep the peace between elephants and humans | |
![]() |
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for How bees can keep the peace between elephants and humans | |
![]() |
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for How bees can keep the peace between elephants and humans | |
![]() |
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for How bees can keep the peace between elephants and humans | |
![]() |
Nelson Simfukwe edited Swahili subtitles for How bees can keep the peace between elephants and humans |