Kwa kadiri ninavyoweza kumbuka,
Tembo wa Afrika wamekuwa wakinijaza furaha mno.
Ni wanyama wakubwa zaidi wa nchi kavu na wanaonyonyesha waliopo hai nyakati hizi,
wakifikia hadi uzito wa tani saba,
wakiwa na urefu wa mita tatu na nusu kufikia mabega yao.
Wana uwezo wa kula chakula hadi kiasi cha kilo 400 kwa siku,
na wanasambaza mbegu muhimu za mimea kwa takribani maelfu ya kilomita
katika kipindi cha miaka 50 hadi 60 ya maisha yao.
Tembo jike ni kiini cha jamii yao iliyo karimu na ngumu kuielewa.
Hawa jike, viongozi imara hukuza watoto
na kuongoza njia katika kuzishinda changamoto zilizopo kwenye mbuga za Afrika
kutafuta chakula, maji na usalama.
Jamii zao ni ngumu kuzielewa,
bado hatujafanikiwa kuweza tambua
namna gani wanawasiliana, namna gani wanabadilishana maongezi,
namna gani wanatumia lugha zao.
Na hatuelewi kiundani namna gani wanatafuta njia katika uwanda,
kukumbuka njia zilizo salama katika kuvuka mto.
Nina uhakika kabisa kama nilivyo mimi,
wengi wenu mliomo humu mtakuwa na hisia chanya zinazofanana
kwa wanyama hawa maridadi kuliko wanyama wote.
Ni ngumu sana kutoangalia makala ya televisheni,
kujifunza kuhusu uwezo wao mkubwa wa akili
au, kama umeshawahi bahatika, kuwaona kwa macho yako
wakati ukitembelea mbuga.
Lakini najiuliza wangapi kati yenu
kiukweli kabisa, mmewahi kuwaogopa wanyama hawa.
Nilibahatika kukulia kusini mwa Afrika
wazazi wangu wakiwa ni walimu
waliokuwa na likizo ndefu lakini bajeti isiyomudu mambo mengi.
Na hivyo tulikuwa tukitumia gari yetu kuukuu aina ya Ford Cortina Estate,
na dada yangu, tutapakia mizigo nyuma ya gari,
tutabeba mahema na kwenda kuweka kambi katika mbuga mbalimbali
kusini mwa Afrika
Ilikuwa ni kama hisia inayokaribia na ya mbinguni, kwa mtafiti mdogo wa wanyama ninaechipukia kama mimi.
Lakini nakumbuka hata katika umri ule mdogo
ambapo niliona senyenge ndefu za umeme zilizozunguka mbuga
zikileta mgawanyiko.
Hakika, ziliwazuia tembo kuishi na jamii,
lakini pia zilizuia jamii kuweza fika katika mapori.
Ilikuwa ni changamoto sana katika umri ule mdogo.
Ilikuwa ni mpaka nilipohamia Kenya nikiwa na umri wa miaka 14,
Nilipoweza kukutana na sehemu za pori zilizo kubwa ndani ya Afrika Mashariki.
Na hapa sasa ninahisi kweli, binafsi,
nipo nyumbani.
Nimeishi miaka mingi ya furaha, nikiwatafiti tembo nikiwa ndani ya hema,
katika mbuga ya taifa ya Samburu,
chini ya uangalizi wa Profesa Fritz Vollrath na Iain Douglas-Hamilton,
nikisomea shahada ya uzamivu na kuelewa mambo mengi magumu ya jamii za tembo.
Lakini sasa, katika jukumu langu nikiwa kama mkuu wa programu ya uwepo tembo na binadamu pamoja
kwa ajili ya mradi wa Okoa Tembo,
tunaona mabadiliko mengi yakitokea haraka
ambayo yanachochea mabadiliko katika programu zetu za utafiti.
Hatuwezi tena tukakaa na kuelewa jamii za tembo
au kujifunza namna za kuzuia biashara ya pembe za tembo,
ambayo inatisha na bado inaendelea.
Tunahitajika kubadili rasilimali zetu zaidi na zaidi
tukiangazia matatizo yanajitokeza katika migogoro ya binadamu na tembo,
pale binadamu na tembo wanapogombania nafasi na rasilimali.
Ni hivi karibuni katika miaka ya 1970
ambapo tulikuwa na tembo takribani milioni 1.2 wakizunguka Afrika.
Leo hii, tuna takaribani tembo 400,000 waliosalia.
Na katika wakati huo huo, jamii ya binadamu imeongezeka mara nne,
na ardhi inagawanywa katika kasi
ambayo ni ngumu kwenda nayo.
Mara nyingi, tembo hawa wanaohama huishia katika jamii za binadamu,
wakitafuta maji na chakula
lakini huishia kuvunja pipa za maji
wakivunja mabomba
na, pia, huvunja maghala ya chakula.
Ni changamoto kubwa mno.
Unaweza fikiria hatari
ya tembo akiwa anavunja paa la nyumba yako ya udongo
usiku wa manane
na kuwatupa watoto wako pembeni
anaposogeza mkonga, akitafuta chakula katika giza?
Tembo hawa wanakanyaga na kula mazao,
na hii inaondoa
uvumilivu ambao watu wamekuwa nao kwa tembo.
Na cha kusikitisha, tunawapoteza wanyama hawa ndani ya siku
na, katika baadhi ya nchi, ndani ya saa --
si tu kwa ajili kupata pembe za ndovu
lakini mgogoro huu unaokua haraka kati ya binadamu na tembo
wanapogombania nafasi na rasilimali.
Ni changamoto kubwa mno.
Namaanisha, unawezaje kupambana na tembo wa tani saba,
ambao kwa kawaida huja katika makundi ya tembo 10 au 12,
katika mashamba madogo ya kijijini
unapokuwa unaongelea watu
ambao wanaishi katika ufukara?
Hawana bajeti kubwa.
Unawezaje kusuluhisha?
Pengine, labda suala laweza kuwa hivi, unaweza anza kujenga senyenge ya umeme,
na hili linatokea Afrika kote,
tunaliona likitokea zaidi na zaidi.
Lakini wanagawanya maeneo na kufunga njia.
Na ninakueleza, hawa tembo hawajali zaidi kuhusu hili,
iwapo watazuia shimo muhimu la maji
ambapo wanahitaji maji,
au kuna jike linalovutia upande wa pili.
Haichukui muda kuvunja nguzo mojawapo ya senyenge.
Na mara panapotokea mwanya katika senyenge,
wanarudi tena, wanaongea na wenzao na ghafla wote wanapita kwenda upande wa pili,
na mwishoni wote wanakuwa wamepita,
na sasa unao tembo 12 katika upande jamii ya binadamu inapoishi.
Na upo katika hatari kwelikweli.
Watu hujaribu kuja na namna mbalimbali za senyenge za umeme.
Hata hivyo, tembo hawa hawafikiri sana kuhusu hilo.
(Kicheko)
Kwa hiyo badala ya kuwa na hizi senyenge ngumu, zilizo na umeme,
ambazo zinaleta mgawanyo wa tembo na binadamu kuhama,
lazima kuwepo na namna nyingine ya kutazamia changamoto hii.
Ninaangazia zaidi katika njia ambayo ni ya jumla na iliyo ya asili
ili kuwatenganisha wanadamu na tembo pale inapohitajika.
Kwa urahisi kuongea na watu,
kuongea na wafugaji wa vijijini kaskazini mwa Kenya
ambao wana uzoefu mkubwa wa porini,
tuligundua hii hadithi ya kwamba walikuwapo tembo ambao hawali majani ya miti
ambayo ina mizinga ya nyuki.
Sasa hii ilikuwa ni hadithi ya kuvutia.
Tembo walipokuwa wakila katika miti,
walivunja matawi na pengine kuharibu mizinga ya nyuki.
Na wale nyuki watakimbia kutoka katika makazi yao
na kuwang'ata tembo.
Sasa kama tembo watang'atwa,
pengine watakumbuka kwamba mti huu ni hatari
na hawatorudi sehemu ile.
Inaonekana kwamba haiwezekani kung'atwa katika ngozi yao nene --
ngozi ya tembo ni takribani sentimeta mbili.
Lakini inaonekana nyuki huwang'ata katika sehemu ambazo zina maji maji,
kuzunguka macho, nyuma ya masikio, katika mdomo, juu ya mkonga.
Unaweza kuona kwamba watakumbuka kwa urahisi zaidi.
Na si kwamba wanaogopa kung'atwa mara moja.
Nyuki wa Afrika wana uwezo wa ajabu:
waking'ata sehemu, hutoa kemikali iitwayo pheromone
ambayo huchochea nyuki wengine kung'ata sehemu hiyo hiyo.
Kwa si mng'ato mmoja wanaoogopa --
lakini pengine ming'ato takribani elfu ya nyuki,
kuja kung'ata sehemu hiyo hiyo -- hicho ndicho wanachoogopa.
Na hivyo, mama mzuri
huwaepusha mbali watoto zake na hatari hiyo.
tembo wadogo wana ngozi nyembamba,
na inapelekea uwezekano wa kuweza kung'atwa
katika ngozi zao nyembamba.
Hivyo kwa ajili ya shahada ya uzamivu, nilipata changamoto hii isiyo kawaida
katika kujaribu kutafuta namna
namna gani tembo na nyuki wa Afrika wanaweza kuwa pamoja,
wakati nadharia inasema hawawezi changamana kabisa.
Niliwezaje kufanyia utafiti hili suala?
Sasa, nilirekodi mlio wa nyuki wa Afrika waliokasirishwa,
na nikauchezesha karibu na tembo waliopumzika chini ya miti
kupitia spika isiyotumia waya,
hivyo ingenipelekea kuelewa namna gani wangeitikia kama kungekuwepo na nyuki pori katika eneo lile.
Na ilitokea kwamba waliitikia katika namna ya kustaajabu
kutokana na sauti ile ya nyuki pori.
Hapa sasa, sauti ya nyuki ikisikika katika kundi hili la tembo.
Utaona masikio yao yanaenda juu, yanatoka nje,
wanageuza vichwa vyao kila pande,
tembo mmoja anachezesha mkonga wake akijaribu kunusa.
Kuna tembo mmoja anayempiga mtoto katika ardhi
akimueleza asimame kwa vile kuna hatari.
Na tembo mmoja anarudi nyuma,
na baada ya muda mfupi familia yote ya tembo inakimbia kumfata
kwenye nyika katika wingu la vumbi.
(Sauti ya nyuki wakilia)
(Sauti ya nyuki inafikia ukingoni)
Nimefanya utafiti huu mara nyingi sana,
na tembo hukimbia.
Si tu kukimbia,
Lakini hujichafua pale wanapokimbia,
ili kuweza kuwafukuzza nyuki kutoka hewani.
Na tuliweka vipaza sauti vya kunasa mawimbi ya chini ya sauti kuwazunguka tembo
tukiwa tunafanya utafiti huu.
Na tukagundua kwamba wanawasiliana katika sauti za mawimbi ya chini wakinguruma
wakijaribu kuambiana kuhusu hatari ya nyuki
na kukaa mbali na eneo lile.
Hivyo ugunduzi huu wa tabia
ulitasaidia kuelewa namna gani tembo wanaitikia
wanaposikia au kuwaona nyuki.
Hii ilinisaidia kutengeneza ubunifu mpya wa senyenge ya mizinga ya nyuki,
ambayo kwa sasa tunajenga katika mashamba madogo ya kati ya ekari moja hadi mbili
katika sehemu ambazo zina tatizo hili kwa kiasi kikubwa
ambapo binadamu na tembo hugombania nafasi.
Senyenge hizi za mizinga ya nyuki ni rahisi sana.
Tunatumia mizinga 12 ya mizinga 12 mingine bandia
ili kulinda ekari moja ya shamba.
Sasa mzinga bandia ni kipande cha mbao
ambacho hukatwa katika mraba, kupakwa rangi ya njano
na kuning'inizwa katika mizinga halisi.
Kimsingi tunawapumbaza tembo
kwamba kuna mizinga ya nyuki mingi kuliko iliyopo.
Na hata hivyo, inaokoa nusu gharama ya senyenge.
Kwa hivyo kuna mzinga halisi na ulio bandia
na mzinga halisi tena ukifatiwa na ulio wa bandia,
kila mita 10 kuzunguka mpaka wa nje.
Inashikiliwa na nguzo
na kivuli cha paa ili kulinda nyuki,
na imeunganishwa na kipande cha kawaida cha waya,
ambacho kinazunguka kwenye shamba lote, kikiunganisha mizinga.
Hivyo kama tembo atajaribu kuingia katika shamba,
atakwepa mizinga ya nyuki katika namna yoyote ile,
lakini atajaribu kusukuma katika mzinga halisi na bandia,
kusababisha mizinga yote kutikisika pale waya unapogonga mzinga.
Na tunajua kutokana na utafiti wetu,
hii itasababisha tembo kukimbia mbali na eneo lile --
na pia kukumbuka kutokurudi eneo lile ambalo ni hatari.
Nyuki watatoka kwenye mizinga,
na kuwafukuza tembo.
Mizinga hii tunaifatilia kwa kufunga kamera
ili kutusaidia kuelewa namna gani tembo wanaitikia
katika nyakati za usiku,
ambapo ni muda uharibifu wa mazao hutokea sana.
Katika mashamba darasa yetu tuligundua
kwamba tunafukuza asilimia 80 ya tembo
kutoweza kuingia katika shamba.
Na nyuki husaidia uchavushaji katika eneo lile.
Hivyo tunafakiwa kupunguza sana uharibifu wa mazao na idadi ya tembo wanaoshambulia mashamba
na kuongeza mazao kutokana na uchavushaji
ambao nyuki wanaufanya kwenye mazao.
Nguvu ya senyenge za mizinga ya nyuki ni muhimu sana --
koloni zinatakiwa kuwa imara.
Hivyo tunajaribu kuwasaidia wakulima kukuza mazao yanasaidia uchavushaji
ili kuweza kukuza mizinga yao,
kuongeza nguvu ya nyuki zao
na, hivyo, kutengeneza asali bora zaidi.
Asali hii ina thamani kubwa kama kipato cha ziada kwa wakulima.
Ni mbadala wa sukari wenye afya,
na kwa jamii yetu,
ni zawadi yenye thamani sana kumpa mama mkwe,
ambapo inakuwa kama tunu.
(Kicheko)
Sasa tunaweka asali hii kwenye chupa,
na tumeipa asali hii jina la Asali Rafiki kwa Tembo.
Ni jina la kufurahisha,
lakini pia limeleta usikivu katika mradi wetu
na kusaidia kuelewa ni kipi tunachojaribu kufanya
ili kuokoa tembo.
Tunafanya kazi na wakina mama wengi sana
katika sehemu 60 zilzo na migogoro ya binadamu na tembo
katika nchi 19 zilizopo Afrika na Asia
kujenga senyenge hizi za mizinga,
tukifanya kazi kwa ukaribu na wakulima wengi
lakini hasa kwa sasa na wakulima wanawake,
kuwasaidia kuishi maisha yenye amani na tembo.
Moja ya vitu tunavyojaribu kufanya ni kutengeneza mifumo ya machaguo
ili kuishi katika amani na hawa tembo wakubwa.
Moja ya masuala hayo ni kujaribu kuwafanya wakulima,
na wanawake kwa ujumla.
kuwaza kwa upana kuhusu ni mazao gani wanayopanda
katika mashamba yao.
Hivyo tunatazamia kupanda mazao
ambayo tembo hawahitaji kula, kama pilipili,
tangawizi, moringa, alizeti.
Na hakika, nyuki na mizinga ya nyuki hupenda mazao haya pia,
kwa sababu yana maua mazuri.
Moja ya mazao haya ni zao lenye miiba liitwalo katani --
hapa mnalifahamu kama jute.
Na mmea huu unaweza kuchanwa
na kugeuzwa katika bidhaa ya kufumia.
Tunashirikiana na wanawake hawa
ambao wanaishi kila siku na changamoto ya tembo
kutumia mmea huu kufumia vikapu
kujitengenezea kipato.
Tumeanza ujenzi wiki tatu zilizopita
wa kituo cha biashara cha kinamama
ambapo tutakuwa tukishirikiana na wanawake hawa
si tu kama wataalamu wa utunzaji nyuki
lakini kama wasuka vikapu maridadi;
watachakata mafuta ya pilipili, alizeti
kutengeneza ving'arisha midomo na asali,
na tupo mahala katika safari yetu ili kusaidia hawa wakulima
kuishi katika miradi rafiki iliyo bora
katika kuishi na tembo.
Hivyo ikiwa ni tembo
au akinamama au watafiti kama mimi,
Nawaona wanawake wakija mstari wa mbele sasa
kuwaza tofauti na kwa ufasaha kuhusu changamoto tunazokutana nazo.
Tukiwa na ubunifu zaidi,
na pengine kuweza kujaliana,
Ninaamini tunaweza kutoka katika migogoro na tembo
na kuweza kuishi nao kwa uhalisia.
Asante.
(Makofi)