[Script Info] Title: [Events] Format: Layer, Start, End, Style, Name, MarginL, MarginR, MarginV, Effect, Text Dialogue: 0,0:00:00.78,0:00:02.67,Default,,0000,0000,0000,,Kwa kadiri ninavyoweza kumbuka, Dialogue: 0,0:00:02.70,0:00:06.93,Default,,0000,0000,0000,,Tembo wa Afrika wamekuwa wakinijaza furaha mno. Dialogue: 0,0:00:07.53,0:00:11.07,Default,,0000,0000,0000,,Ni wanyama wakubwa zaidi wa nchi kavu na wanaonyonyesha waliopo hai nyakati hizi, Dialogue: 0,0:00:11.09,0:00:13.25,Default,,0000,0000,0000,,wakifikia hadi uzito wa tani saba, Dialogue: 0,0:00:13.28,0:00:16.51,Default,,0000,0000,0000,,wakiwa na urefu wa mita tatu na nusu kufikia mabega yao. Dialogue: 0,0:00:16.54,0:00:19.98,Default,,0000,0000,0000,,Wana uwezo wa kula chakula hadi kiasi cha kilo 400 kwa siku, Dialogue: 0,0:00:20.01,0:00:24.54,Default,,0000,0000,0000,,na wanasambaza mbegu muhimu za mimea kwa takribani maelfu ya kilomita Dialogue: 0,0:00:24.57,0:00:27.04,Default,,0000,0000,0000,,katika kipindi cha miaka 50 hadi 60 ya maisha yao. Dialogue: 0,0:00:27.53,0:00:31.86,Default,,0000,0000,0000,,Tembo jike ni kiini cha jamii yao iliyo karimu na ngumu kuielewa. Dialogue: 0,0:00:32.25,0:00:35.60,Default,,0000,0000,0000,,Hawa jike, viongozi imara hukuza watoto Dialogue: 0,0:00:35.62,0:00:38.69,Default,,0000,0000,0000,,na kuongoza njia katika kuzishinda changamoto zilizopo kwenye mbuga za Afrika Dialogue: 0,0:00:38.71,0:00:40.91,Default,,0000,0000,0000,,kutafuta chakula, maji na usalama. Dialogue: 0,0:00:41.55,0:00:43.40,Default,,0000,0000,0000,,Jamii zao ni ngumu kuzielewa, Dialogue: 0,0:00:43.42,0:00:45.72,Default,,0000,0000,0000,,bado hatujafanikiwa kuweza tambua Dialogue: 0,0:00:45.74,0:00:48.33,Default,,0000,0000,0000,,namna gani wanawasiliana, namna gani wanabadilishana maongezi, Dialogue: 0,0:00:48.36,0:00:49.98,Default,,0000,0000,0000,,namna gani wanatumia lugha zao. Dialogue: 0,0:00:50.01,0:00:54.08,Default,,0000,0000,0000,,Na hatuelewi kiundani namna gani wanatafuta njia katika uwanda, Dialogue: 0,0:00:54.10,0:00:57.05,Default,,0000,0000,0000,,kukumbuka njia zilizo salama katika kuvuka mto. Dialogue: 0,0:00:57.73,0:00:59.49,Default,,0000,0000,0000,,Nina uhakika kabisa kama nilivyo mimi, Dialogue: 0,0:00:59.51,0:01:03.24,Default,,0000,0000,0000,,wengi wenu mliomo humu mtakuwa na hisia chanya zinazofanana Dialogue: 0,0:01:03.27,0:01:05.67,Default,,0000,0000,0000,,kwa wanyama hawa maridadi kuliko wanyama wote. Dialogue: 0,0:01:06.12,0:01:08.54,Default,,0000,0000,0000,,Ni ngumu sana kutoangalia makala ya televisheni, Dialogue: 0,0:01:08.56,0:01:10.09,Default,,0000,0000,0000,,kujifunza kuhusu uwezo wao mkubwa wa akili Dialogue: 0,0:01:10.12,0:01:12.74,Default,,0000,0000,0000,,au, kama umeshawahi bahatika, kuwaona kwa macho yako Dialogue: 0,0:01:12.77,0:01:14.40,Default,,0000,0000,0000,,wakati ukitembelea mbuga. Dialogue: 0,0:01:15.08,0:01:16.53,Default,,0000,0000,0000,,Lakini najiuliza wangapi kati yenu Dialogue: 0,0:01:16.55,0:01:20.69,Default,,0000,0000,0000,,kiukweli kabisa, mmewahi kuwaogopa wanyama hawa. Dialogue: 0,0:01:22.48,0:01:24.74,Default,,0000,0000,0000,,Nilibahatika kukulia kusini mwa Afrika Dialogue: 0,0:01:24.77,0:01:26.24,Default,,0000,0000,0000,,wazazi wangu wakiwa ni walimu Dialogue: 0,0:01:26.26,0:01:29.32,Default,,0000,0000,0000,,waliokuwa na likizo ndefu lakini bajeti isiyomudu mambo mengi. Dialogue: 0,0:01:29.90,0:01:33.32,Default,,0000,0000,0000,,Na hivyo tulikuwa tukitumia gari yetu kuukuu aina ya Ford Cortina Estate, Dialogue: 0,0:01:33.34,0:01:35.37,Default,,0000,0000,0000,,na dada yangu, tutapakia mizigo nyuma ya gari, Dialogue: 0,0:01:35.40,0:01:38.22,Default,,0000,0000,0000,,tutabeba mahema na kwenda kuweka kambi katika mbuga mbalimbali Dialogue: 0,0:01:38.24,0:01:39.50,Default,,0000,0000,0000,,kusini mwa Afrika Dialogue: 0,0:01:39.52,0:01:42.98,Default,,0000,0000,0000,,Ilikuwa ni kama hisia inayokaribia na ya mbinguni, kwa mtafiti mdogo wa wanyama ninaechipukia kama mimi. Dialogue: 0,0:01:43.40,0:01:45.75,Default,,0000,0000,0000,,Lakini nakumbuka hata katika umri ule mdogo Dialogue: 0,0:01:45.77,0:01:49.43,Default,,0000,0000,0000,,ambapo niliona senyenge ndefu za umeme zilizozunguka mbuga Dialogue: 0,0:01:49.45,0:01:50.71,Default,,0000,0000,0000,,zikileta mgawanyiko. Dialogue: 0,0:01:51.08,0:01:53.75,Default,,0000,0000,0000,,Hakika, ziliwazuia tembo kuishi na jamii, Dialogue: 0,0:01:53.78,0:01:57.20,Default,,0000,0000,0000,,lakini pia zilizuia jamii kuweza fika katika mapori. Dialogue: 0,0:01:58.24,0:02:01.63,Default,,0000,0000,0000,,Ilikuwa ni changamoto sana katika umri ule mdogo. Dialogue: 0,0:02:02.13,0:02:05.36,Default,,0000,0000,0000,,Ilikuwa ni mpaka nilipohamia Kenya nikiwa na umri wa miaka 14, Dialogue: 0,0:02:05.38,0:02:10.10,Default,,0000,0000,0000,,Nilipoweza kukutana na sehemu za pori zilizo kubwa ndani ya Afrika Mashariki. Dialogue: 0,0:02:10.12,0:02:13.88,Default,,0000,0000,0000,,Na hapa sasa ninahisi kweli, binafsi, Dialogue: 0,0:02:13.90,0:02:15.19,Default,,0000,0000,0000,,nipo nyumbani. Dialogue: 0,0:02:15.90,0:02:19.58,Default,,0000,0000,0000,,Nimeishi miaka mingi ya furaha, nikiwatafiti tembo nikiwa ndani ya hema, Dialogue: 0,0:02:19.61,0:02:21.62,Default,,0000,0000,0000,,katika mbuga ya taifa ya Samburu, Dialogue: 0,0:02:21.64,0:02:25.88,Default,,0000,0000,0000,,chini ya uangalizi wa Profesa Fritz Vollrath na Iain Douglas-Hamilton, Dialogue: 0,0:02:25.90,0:02:30.54,Default,,0000,0000,0000,,nikisomea shahada ya uzamivu na kuelewa mambo mengi magumu ya jamii za tembo. Dialogue: 0,0:02:31.79,0:02:35.73,Default,,0000,0000,0000,,Lakini sasa, katika jukumu langu nikiwa kama mkuu wa programu ya uwepo tembo na binadamu pamoja Dialogue: 0,0:02:35.75,0:02:37.08,Default,,0000,0000,0000,,kwa ajili ya mradi wa Okoa Tembo, Dialogue: 0,0:02:37.10,0:02:41.22,Default,,0000,0000,0000,,tunaona mabadiliko mengi yakitokea haraka Dialogue: 0,0:02:41.24,0:02:45.44,Default,,0000,0000,0000,,ambayo yanachochea mabadiliko katika programu zetu za utafiti. Dialogue: 0,0:02:45.46,0:02:48.96,Default,,0000,0000,0000,,Hatuwezi tena tukakaa na kuelewa jamii za tembo Dialogue: 0,0:02:48.98,0:02:51.78,Default,,0000,0000,0000,,au kujifunza namna za kuzuia biashara ya pembe za tembo, Dialogue: 0,0:02:51.81,0:02:54.24,Default,,0000,0000,0000,,ambayo inatisha na bado inaendelea. Dialogue: 0,0:02:54.27,0:02:57.02,Default,,0000,0000,0000,,Tunahitajika kubadili rasilimali zetu zaidi na zaidi Dialogue: 0,0:02:57.05,0:03:01.19,Default,,0000,0000,0000,,tukiangazia matatizo yanajitokeza katika migogoro ya binadamu na tembo, Dialogue: 0,0:03:01.21,0:03:04.79,Default,,0000,0000,0000,,pale binadamu na tembo wanapogombania nafasi na rasilimali. Dialogue: 0,0:03:05.54,0:03:07.58,Default,,0000,0000,0000,,Ni hivi karibuni katika miaka ya 1970 Dialogue: 0,0:03:07.61,0:03:11.90,Default,,0000,0000,0000,,ambapo tulikuwa na tembo takribani milioni 1.2 wakizunguka Afrika. Dialogue: 0,0:03:11.93,0:03:16.66,Default,,0000,0000,0000,,Leo hii, tuna takaribani tembo 400,000 waliosalia. Dialogue: 0,0:03:17.09,0:03:21.36,Default,,0000,0000,0000,,Na katika wakati huo huo, jamii ya binadamu imeongezeka mara nne, Dialogue: 0,0:03:21.39,0:03:23.70,Default,,0000,0000,0000,,na ardhi inagawanywa katika kasi Dialogue: 0,0:03:23.73,0:03:26.26,Default,,0000,0000,0000,,ambayo ni ngumu kwenda nayo. Dialogue: 0,0:03:26.67,0:03:30.36,Default,,0000,0000,0000,,Mara nyingi, tembo hawa wanaohama huishia katika jamii za binadamu, Dialogue: 0,0:03:30.38,0:03:31.67,Default,,0000,0000,0000,,wakitafuta maji na chakula Dialogue: 0,0:03:31.70,0:03:34.25,Default,,0000,0000,0000,,lakini huishia kuvunja pipa za maji Dialogue: 0,0:03:34.28,0:03:35.43,Default,,0000,0000,0000,,wakivunja mabomba Dialogue: 0,0:03:35.46,0:03:38.39,Default,,0000,0000,0000,,na, pia, huvunja maghala ya chakula. Dialogue: 0,0:03:38.41,0:03:40.34,Default,,0000,0000,0000,,Ni changamoto kubwa mno. Dialogue: 0,0:03:40.97,0:03:42.49,Default,,0000,0000,0000,,Unaweza fikiria hatari Dialogue: 0,0:03:42.52,0:03:46.11,Default,,0000,0000,0000,,ya tembo akiwa anavunja paa la nyumba yako ya udongo Dialogue: 0,0:03:46.13,0:03:47.43,Default,,0000,0000,0000,,usiku wa manane Dialogue: 0,0:03:47.45,0:03:49.52,Default,,0000,0000,0000,,na kuwatupa watoto wako pembeni Dialogue: 0,0:03:49.54,0:03:53.96,Default,,0000,0000,0000,,anaposogeza mkonga, akitafuta chakula katika giza? Dialogue: 0,0:03:54.58,0:03:57.32,Default,,0000,0000,0000,,Tembo hawa wanakanyaga na kula mazao, Dialogue: 0,0:03:57.34,0:03:59.60,Default,,0000,0000,0000,,na hii inaondoa Dialogue: 0,0:03:59.63,0:04:02.56,Default,,0000,0000,0000,,uvumilivu ambao watu wamekuwa nao kwa tembo. Dialogue: 0,0:04:03.05,0:04:06.85,Default,,0000,0000,0000,,Na cha kusikitisha, tunawapoteza wanyama hawa ndani ya siku Dialogue: 0,0:04:06.87,0:04:09.86,Default,,0000,0000,0000,,na, katika baadhi ya nchi, ndani ya saa -- Dialogue: 0,0:04:09.88,0:04:11.26,Default,,0000,0000,0000,,si tu kwa ajili kupata pembe za ndovu Dialogue: 0,0:04:11.28,0:04:13.90,Default,,0000,0000,0000,,lakini mgogoro huu unaokua haraka kati ya binadamu na tembo Dialogue: 0,0:04:13.92,0:04:16.58,Default,,0000,0000,0000,,wanapogombania nafasi na rasilimali. Dialogue: 0,0:04:16.95,0:04:18.16,Default,,0000,0000,0000,,Ni changamoto kubwa mno. Dialogue: 0,0:04:18.18,0:04:21.14,Default,,0000,0000,0000,,Namaanisha, unawezaje kupambana na tembo wa tani saba, Dialogue: 0,0:04:21.16,0:04:23.24,Default,,0000,0000,0000,,ambao kwa kawaida huja katika makundi ya tembo 10 au 12, Dialogue: 0,0:04:23.27,0:04:25.72,Default,,0000,0000,0000,,katika mashamba madogo ya kijijini Dialogue: 0,0:04:25.74,0:04:27.25,Default,,0000,0000,0000,,unapokuwa unaongelea watu Dialogue: 0,0:04:27.28,0:04:30.37,Default,,0000,0000,0000,,ambao wanaishi katika ufukara? Dialogue: 0,0:04:30.40,0:04:31.80,Default,,0000,0000,0000,,Hawana bajeti kubwa. Dialogue: 0,0:04:31.82,0:04:34.76,Default,,0000,0000,0000,,Unawezaje kusuluhisha? Dialogue: 0,0:04:35.16,0:04:38.76,Default,,0000,0000,0000,,Pengine, labda suala laweza kuwa hivi, unaweza anza kujenga senyenge ya umeme, Dialogue: 0,0:04:38.78,0:04:40.52,Default,,0000,0000,0000,,na hili linatokea Afrika kote, Dialogue: 0,0:04:40.55,0:04:42.16,Default,,0000,0000,0000,,tunaliona likitokea zaidi na zaidi. Dialogue: 0,0:04:42.18,0:04:45.82,Default,,0000,0000,0000,,Lakini wanagawanya maeneo na kufunga njia. Dialogue: 0,0:04:45.85,0:04:49.25,Default,,0000,0000,0000,,Na ninakueleza, hawa tembo hawajali zaidi kuhusu hili, Dialogue: 0,0:04:49.28,0:04:52.16,Default,,0000,0000,0000,,iwapo watazuia shimo muhimu la maji Dialogue: 0,0:04:52.19,0:04:53.37,Default,,0000,0000,0000,,ambapo wanahitaji maji, Dialogue: 0,0:04:53.40,0:04:56.10,Default,,0000,0000,0000,,au kuna jike linalovutia upande wa pili. Dialogue: 0,0:04:56.13,0:04:58.66,Default,,0000,0000,0000,,Haichukui muda kuvunja nguzo mojawapo ya senyenge. Dialogue: 0,0:04:58.68,0:05:00.74,Default,,0000,0000,0000,,Na mara panapotokea mwanya katika senyenge, Dialogue: 0,0:05:00.76,0:05:02.43,Default,,0000,0000,0000,,wanarudi tena, wanaongea na wenzao na ghafla wote wanapita kwenda upande wa pili, Dialogue: 0,0:05:02.45,0:05:04.34,Default,,0000,0000,0000,,na mwishoni wote wanakuwa wamepita, Dialogue: 0,0:05:04.36,0:05:07.86,Default,,0000,0000,0000,,na sasa unao tembo 12 katika upande jamii ya binadamu inapoishi. Dialogue: 0,0:05:07.88,0:05:10.03,Default,,0000,0000,0000,,Na upo katika hatari kwelikweli. Dialogue: 0,0:05:10.06,0:05:13.58,Default,,0000,0000,0000,,Watu hujaribu kuja na namna mbalimbali za senyenge za umeme. Dialogue: 0,0:05:14.42,0:05:17.33,Default,,0000,0000,0000,,Hata hivyo, tembo hawa hawafikiri sana kuhusu hilo. Dialogue: 0,0:05:17.76,0:05:20.71,Default,,0000,0000,0000,,(Kicheko) Dialogue: 0,0:05:22.69,0:05:27.44,Default,,0000,0000,0000,,Kwa hiyo badala ya kuwa na hizi senyenge ngumu, zilizo na umeme, Dialogue: 0,0:05:27.46,0:05:31.12,Default,,0000,0000,0000,,ambazo zinaleta mgawanyo wa tembo na binadamu kuhama, Dialogue: 0,0:05:31.15,0:05:33.76,Default,,0000,0000,0000,,lazima kuwepo na namna nyingine ya kutazamia changamoto hii. Dialogue: 0,0:05:33.78,0:05:36.62,Default,,0000,0000,0000,,Ninaangazia zaidi katika njia ambayo ni ya jumla na iliyo ya asili Dialogue: 0,0:05:36.64,0:05:39.52,Default,,0000,0000,0000,,ili kuwatenganisha wanadamu na tembo pale inapohitajika. Dialogue: 0,0:05:40.18,0:05:41.82,Default,,0000,0000,0000,,Kwa urahisi kuongea na watu, Dialogue: 0,0:05:41.85,0:05:44.11,Default,,0000,0000,0000,,kuongea na wafugaji wa vijijini kaskazini mwa Kenya Dialogue: 0,0:05:44.13,0:05:46.68,Default,,0000,0000,0000,,ambao wana uzoefu mkubwa wa porini, Dialogue: 0,0:05:46.70,0:05:50.68,Default,,0000,0000,0000,,tuligundua hii hadithi ya kwamba walikuwapo tembo ambao hawali majani ya miti Dialogue: 0,0:05:50.70,0:05:52.57,Default,,0000,0000,0000,,ambayo ina mizinga ya nyuki. Dialogue: 0,0:05:52.59,0:05:54.61,Default,,0000,0000,0000,,Sasa hii ilikuwa ni hadithi ya kuvutia. Dialogue: 0,0:05:54.64,0:05:56.64,Default,,0000,0000,0000,,Tembo walipokuwa wakila katika miti, Dialogue: 0,0:05:56.67,0:06:00.27,Default,,0000,0000,0000,,walivunja matawi na pengine kuharibu mizinga ya nyuki. Dialogue: 0,0:06:00.29,0:06:03.65,Default,,0000,0000,0000,,Na wale nyuki watakimbia kutoka katika makazi yao Dialogue: 0,0:06:03.68,0:06:05.35,Default,,0000,0000,0000,,na kuwang'ata tembo. Dialogue: 0,0:06:05.37,0:06:06.96,Default,,0000,0000,0000,,Sasa kama tembo watang'atwa, Dialogue: 0,0:06:06.98,0:06:09.62,Default,,0000,0000,0000,,pengine watakumbuka kwamba mti huu ni hatari Dialogue: 0,0:06:09.65,0:06:11.84,Default,,0000,0000,0000,,na hawatorudi sehemu ile. Dialogue: 0,0:06:11.86,0:06:15.32,Default,,0000,0000,0000,,Inaonekana kwamba haiwezekani kung'atwa katika ngozi yao nene -- Dialogue: 0,0:06:15.34,0:06:17.71,Default,,0000,0000,0000,,ngozi ya tembo ni takribani sentimeta mbili. Dialogue: 0,0:06:17.73,0:06:20.49,Default,,0000,0000,0000,,Lakini inaonekana nyuki huwang'ata katika sehemu ambazo zina maji maji, Dialogue: 0,0:06:20.52,0:06:24.50,Default,,0000,0000,0000,,kuzunguka macho, nyuma ya masikio, katika mdomo, juu ya mkonga. Dialogue: 0,0:06:24.95,0:06:28.18,Default,,0000,0000,0000,,Unaweza kuona kwamba watakumbuka kwa urahisi zaidi. Dialogue: 0,0:06:28.21,0:06:31.07,Default,,0000,0000,0000,,Na si kwamba wanaogopa kung'atwa mara moja. Dialogue: 0,0:06:31.10,0:06:34.06,Default,,0000,0000,0000,,Nyuki wa Afrika wana uwezo wa ajabu: Dialogue: 0,0:06:34.09,0:06:36.86,Default,,0000,0000,0000,,waking'ata sehemu, hutoa kemikali iitwayo pheromone Dialogue: 0,0:06:36.89,0:06:40.10,Default,,0000,0000,0000,,ambayo huchochea nyuki wengine kung'ata sehemu hiyo hiyo. Dialogue: 0,0:06:40.13,0:06:42.46,Default,,0000,0000,0000,,Kwa si mng'ato mmoja wanaoogopa -- Dialogue: 0,0:06:42.49,0:06:44.36,Default,,0000,0000,0000,,lakini pengine ming'ato takribani elfu ya nyuki, Dialogue: 0,0:06:44.39,0:06:47.49,Default,,0000,0000,0000,,kuja kung'ata sehemu hiyo hiyo -- hicho ndicho wanachoogopa. Dialogue: 0,0:06:47.96,0:06:49.60,Default,,0000,0000,0000,,Na hivyo, mama mzuri Dialogue: 0,0:06:49.62,0:06:52.55,Default,,0000,0000,0000,,huwaepusha mbali watoto zake na hatari hiyo. Dialogue: 0,0:06:52.57,0:06:54.51,Default,,0000,0000,0000,,tembo wadogo wana ngozi nyembamba, Dialogue: 0,0:06:54.53,0:06:56.57,Default,,0000,0000,0000,,na inapelekea uwezekano wa kuweza kung'atwa Dialogue: 0,0:06:56.60,0:06:58.46,Default,,0000,0000,0000,,katika ngozi zao nyembamba. Dialogue: 0,0:06:58.95,0:07:02.44,Default,,0000,0000,0000,,Hivyo kwa ajili ya shahada ya uzamivu, nilipata changamoto hii isiyo kawaida Dialogue: 0,0:07:02.47,0:07:03.85,Default,,0000,0000,0000,,katika kujaribu kutafuta namna Dialogue: 0,0:07:03.87,0:07:07.82,Default,,0000,0000,0000,,namna gani tembo na nyuki wa Afrika wanaweza kuwa pamoja, Dialogue: 0,0:07:07.84,0:07:10.72,Default,,0000,0000,0000,,wakati nadharia inasema hawawezi changamana kabisa. Dialogue: 0,0:07:10.74,0:07:12.77,Default,,0000,0000,0000,,Niliwezaje kufanyia utafiti hili suala? Dialogue: 0,0:07:12.80,0:07:16.78,Default,,0000,0000,0000,,Sasa, nilirekodi mlio wa nyuki wa Afrika waliokasirishwa, Dialogue: 0,0:07:16.80,0:07:20.22,Default,,0000,0000,0000,,na nikauchezesha karibu na tembo waliopumzika chini ya miti Dialogue: 0,0:07:20.24,0:07:21.94,Default,,0000,0000,0000,,kupitia spika isiyotumia waya, Dialogue: 0,0:07:21.96,0:07:26.44,Default,,0000,0000,0000,,hivyo ingenipelekea kuelewa namna gani wangeitikia kama kungekuwepo na nyuki pori katika eneo lile. Dialogue: 0,0:07:26.47,0:07:29.55,Default,,0000,0000,0000,,Na ilitokea kwamba waliitikia katika namna ya kustaajabu Dialogue: 0,0:07:29.58,0:07:31.84,Default,,0000,0000,0000,,kutokana na sauti ile ya nyuki pori. Dialogue: 0,0:07:32.99,0:07:36.62,Default,,0000,0000,0000,,Hapa sasa, sauti ya nyuki ikisikika katika kundi hili la tembo. Dialogue: 0,0:07:36.64,0:07:39.36,Default,,0000,0000,0000,,Utaona masikio yao yanaenda juu, yanatoka nje, Dialogue: 0,0:07:39.39,0:07:41.84,Default,,0000,0000,0000,,wanageuza vichwa vyao kila pande, Dialogue: 0,0:07:41.86,0:07:44.60,Default,,0000,0000,0000,,tembo mmoja anachezesha mkonga wake akijaribu kunusa. Dialogue: 0,0:07:45.05,0:07:48.08,Default,,0000,0000,0000,,Kuna tembo mmoja anayempiga mtoto katika ardhi Dialogue: 0,0:07:48.11,0:07:50.76,Default,,0000,0000,0000,,akimueleza asimame kwa vile kuna hatari. Dialogue: 0,0:07:51.21,0:07:53.83,Default,,0000,0000,0000,,Na tembo mmoja anarudi nyuma, Dialogue: 0,0:07:53.85,0:07:57.90,Default,,0000,0000,0000,,na baada ya muda mfupi familia yote ya tembo inakimbia kumfata Dialogue: 0,0:07:57.93,0:08:01.13,Default,,0000,0000,0000,,kwenye nyika katika wingu la vumbi. Dialogue: 0,0:08:01.15,0:08:02.85,Default,,0000,0000,0000,,(Sauti ya nyuki wakilia) Dialogue: 0,0:08:08.39,0:08:09.68,Default,,0000,0000,0000,,(Sauti ya nyuki inafikia ukingoni) Dialogue: 0,0:08:09.70,0:08:14.03,Default,,0000,0000,0000,,Nimefanya utafiti huu mara nyingi sana, Dialogue: 0,0:08:14.05,0:08:16.70,Default,,0000,0000,0000,,na tembo hukimbia. Dialogue: 0,0:08:16.73,0:08:18.48,Default,,0000,0000,0000,,Si tu kukimbia, Dialogue: 0,0:08:18.50,0:08:20.59,Default,,0000,0000,0000,,Lakini hujichafua pale wanapokimbia, Dialogue: 0,0:08:20.61,0:08:22.95,Default,,0000,0000,0000,,ili kuweza kuwafukuzza nyuki kutoka hewani. Dialogue: 0,0:08:23.51,0:08:26.99,Default,,0000,0000,0000,,Na tuliweka vipaza sauti vya kunasa mawimbi ya chini ya sauti kuwazunguka tembo Dialogue: 0,0:08:27.02,0:08:28.77,Default,,0000,0000,0000,,tukiwa tunafanya utafiti huu. Dialogue: 0,0:08:28.79,0:08:32.44,Default,,0000,0000,0000,,Na tukagundua kwamba wanawasiliana katika sauti za mawimbi ya chini wakinguruma Dialogue: 0,0:08:32.47,0:08:34.40,Default,,0000,0000,0000,,wakijaribu kuambiana kuhusu hatari ya nyuki Dialogue: 0,0:08:34.43,0:08:36.49,Default,,0000,0000,0000,,na kukaa mbali na eneo lile. Dialogue: 0,0:08:37.04,0:08:38.66,Default,,0000,0000,0000,,Hivyo ugunduzi huu wa tabia Dialogue: 0,0:08:38.69,0:08:41.19,Default,,0000,0000,0000,,ulitasaidia kuelewa namna gani tembo wanaitikia Dialogue: 0,0:08:41.21,0:08:43.56,Default,,0000,0000,0000,,wanaposikia au kuwaona nyuki. Dialogue: 0,0:08:43.58,0:08:47.70,Default,,0000,0000,0000,,Hii ilinisaidia kutengeneza ubunifu mpya wa senyenge ya mizinga ya nyuki, Dialogue: 0,0:08:47.73,0:08:51.20,Default,,0000,0000,0000,,ambayo kwa sasa tunajenga katika mashamba madogo ya kati ya ekari moja hadi mbili Dialogue: 0,0:08:51.23,0:08:53.94,Default,,0000,0000,0000,,katika sehemu ambazo zina tatizo hili kwa kiasi kikubwa Dialogue: 0,0:08:53.96,0:08:56.61,Default,,0000,0000,0000,,ambapo binadamu na tembo hugombania nafasi. Dialogue: 0,0:08:57.26,0:08:59.35,Default,,0000,0000,0000,,Senyenge hizi za mizinga ya nyuki ni rahisi sana. Dialogue: 0,0:08:59.37,0:09:02.62,Default,,0000,0000,0000,,Tunatumia mizinga 12 ya mizinga 12 mingine bandia Dialogue: 0,0:09:02.65,0:09:05.04,Default,,0000,0000,0000,,ili kulinda ekari moja ya shamba. Dialogue: 0,0:09:05.07,0:09:07.36,Default,,0000,0000,0000,,Sasa mzinga bandia ni kipande cha mbao Dialogue: 0,0:09:07.39,0:09:09.62,Default,,0000,0000,0000,,ambacho hukatwa katika mraba, kupakwa rangi ya njano Dialogue: 0,0:09:09.65,0:09:11.31,Default,,0000,0000,0000,,na kuning'inizwa katika mizinga halisi. Dialogue: 0,0:09:11.33,0:09:13.28,Default,,0000,0000,0000,,Kimsingi tunawapumbaza tembo Dialogue: 0,0:09:13.30,0:09:16.12,Default,,0000,0000,0000,,kwamba kuna mizinga ya nyuki mingi kuliko iliyopo. Dialogue: 0,0:09:16.15,0:09:18.99,Default,,0000,0000,0000,,Na hata hivyo, inaokoa nusu gharama ya senyenge. Dialogue: 0,0:09:19.01,0:09:20.67,Default,,0000,0000,0000,,Kwa hivyo kuna mzinga halisi na ulio bandia Dialogue: 0,0:09:20.70,0:09:22.44,Default,,0000,0000,0000,,na mzinga halisi tena ukifatiwa na ulio wa bandia, Dialogue: 0,0:09:22.47,0:09:24.94,Default,,0000,0000,0000,,kila mita 10 kuzunguka mpaka wa nje. Dialogue: 0,0:09:24.97,0:09:26.60,Default,,0000,0000,0000,,Inashikiliwa na nguzo Dialogue: 0,0:09:26.62,0:09:28.74,Default,,0000,0000,0000,,na kivuli cha paa ili kulinda nyuki, Dialogue: 0,0:09:28.77,0:09:31.92,Default,,0000,0000,0000,,na imeunganishwa na kipande cha kawaida cha waya, Dialogue: 0,0:09:31.94,0:09:34.38,Default,,0000,0000,0000,,ambacho kinazunguka kwenye shamba lote, kikiunganisha mizinga. Dialogue: 0,0:09:34.40,0:09:36.86,Default,,0000,0000,0000,,Hivyo kama tembo atajaribu kuingia katika shamba, Dialogue: 0,0:09:36.88,0:09:38.73,Default,,0000,0000,0000,,atakwepa mizinga ya nyuki katika namna yoyote ile, Dialogue: 0,0:09:38.75,0:09:42.06,Default,,0000,0000,0000,,lakini atajaribu kusukuma katika mzinga halisi na bandia, Dialogue: 0,0:09:42.08,0:09:45.42,Default,,0000,0000,0000,,kusababisha mizinga yote kutikisika pale waya unapogonga mzinga. Dialogue: 0,0:09:45.45,0:09:47.41,Default,,0000,0000,0000,,Na tunajua kutokana na utafiti wetu, Dialogue: 0,0:09:47.43,0:09:50.35,Default,,0000,0000,0000,,hii itasababisha tembo kukimbia mbali na eneo lile -- Dialogue: 0,0:09:50.37,0:09:54.11,Default,,0000,0000,0000,,na pia kukumbuka kutokurudi eneo lile ambalo ni hatari. Dialogue: 0,0:09:54.13,0:09:55.86,Default,,0000,0000,0000,,Nyuki watatoka kwenye mizinga, Dialogue: 0,0:09:55.89,0:09:58.48,Default,,0000,0000,0000,,na kuwafukuza tembo. Dialogue: 0,0:09:58.50,0:10:01.97,Default,,0000,0000,0000,,Mizinga hii tunaifatilia kwa kufunga kamera Dialogue: 0,0:10:01.100,0:10:04.36,Default,,0000,0000,0000,,ili kutusaidia kuelewa namna gani tembo wanaitikia Dialogue: 0,0:10:04.38,0:10:05.58,Default,,0000,0000,0000,,katika nyakati za usiku, Dialogue: 0,0:10:05.61,0:10:07.87,Default,,0000,0000,0000,,ambapo ni muda uharibifu wa mazao hutokea sana. Dialogue: 0,0:10:07.89,0:10:10.22,Default,,0000,0000,0000,,Katika mashamba darasa yetu tuligundua Dialogue: 0,0:10:10.24,0:10:12.96,Default,,0000,0000,0000,,kwamba tunafukuza asilimia 80 ya tembo Dialogue: 0,0:10:12.98,0:10:15.47,Default,,0000,0000,0000,,kutoweza kuingia katika shamba. Dialogue: 0,0:10:15.97,0:10:20.72,Default,,0000,0000,0000,,Na nyuki husaidia uchavushaji katika eneo lile. Dialogue: 0,0:10:20.74,0:10:24.41,Default,,0000,0000,0000,,Hivyo tunafakiwa kupunguza sana uharibifu wa mazao na idadi ya tembo wanaoshambulia mashamba Dialogue: 0,0:10:24.43,0:10:27.10,Default,,0000,0000,0000,,na kuongeza mazao kutokana na uchavushaji Dialogue: 0,0:10:27.12,0:10:29.79,Default,,0000,0000,0000,,ambao nyuki wanaufanya kwenye mazao. Dialogue: 0,0:10:30.58,0:10:33.26,Default,,0000,0000,0000,,Nguvu ya senyenge za mizinga ya nyuki ni muhimu sana -- Dialogue: 0,0:10:33.28,0:10:35.20,Default,,0000,0000,0000,,koloni zinatakiwa kuwa imara. Dialogue: 0,0:10:35.22,0:10:38.17,Default,,0000,0000,0000,,Hivyo tunajaribu kuwasaidia wakulima kukuza mazao yanasaidia uchavushaji Dialogue: 0,0:10:38.20,0:10:40.22,Default,,0000,0000,0000,,ili kuweza kukuza mizinga yao, Dialogue: 0,0:10:40.24,0:10:41.87,Default,,0000,0000,0000,,kuongeza nguvu ya nyuki zao Dialogue: 0,0:10:41.90,0:10:44.77,Default,,0000,0000,0000,,na, hivyo, kutengeneza asali bora zaidi. Dialogue: 0,0:10:44.79,0:10:48.93,Default,,0000,0000,0000,,Asali hii ina thamani kubwa kama kipato cha ziada kwa wakulima. Dialogue: 0,0:10:49.24,0:10:51.28,Default,,0000,0000,0000,,Ni mbadala wa sukari wenye afya, Dialogue: 0,0:10:51.30,0:10:53.01,Default,,0000,0000,0000,,na kwa jamii yetu, Dialogue: 0,0:10:53.04,0:10:55.55,Default,,0000,0000,0000,,ni zawadi yenye thamani sana kumpa mama mkwe, Dialogue: 0,0:10:55.58,0:10:57.46,Default,,0000,0000,0000,,ambapo inakuwa kama tunu. Dialogue: 0,0:10:57.49,0:10:59.62,Default,,0000,0000,0000,,(Kicheko) Dialogue: 0,0:10:59.94,0:11:01.61,Default,,0000,0000,0000,,Sasa tunaweka asali hii kwenye chupa, Dialogue: 0,0:11:01.63,0:11:05.73,Default,,0000,0000,0000,,na tumeipa asali hii jina la Asali Rafiki kwa Tembo. Dialogue: 0,0:11:05.76,0:11:06.91,Default,,0000,0000,0000,,Ni jina la kufurahisha, Dialogue: 0,0:11:06.93,0:11:09.12,Default,,0000,0000,0000,,lakini pia limeleta usikivu katika mradi wetu Dialogue: 0,0:11:09.15,0:11:11.55,Default,,0000,0000,0000,,na kusaidia kuelewa ni kipi tunachojaribu kufanya Dialogue: 0,0:11:11.58,0:11:12.73,Default,,0000,0000,0000,,ili kuokoa tembo. Dialogue: 0,0:11:12.75,0:11:14.50,Default,,0000,0000,0000,,Tunafanya kazi na wakina mama wengi sana Dialogue: 0,0:11:14.52,0:11:17.10,Default,,0000,0000,0000,,katika sehemu 60 zilzo na migogoro ya binadamu na tembo Dialogue: 0,0:11:17.13,0:11:19.63,Default,,0000,0000,0000,,katika nchi 19 zilizopo Afrika na Asia Dialogue: 0,0:11:19.66,0:11:21.69,Default,,0000,0000,0000,,kujenga senyenge hizi za mizinga, Dialogue: 0,0:11:21.71,0:11:24.14,Default,,0000,0000,0000,,tukifanya kazi kwa ukaribu na wakulima wengi Dialogue: 0,0:11:24.16,0:11:26.44,Default,,0000,0000,0000,,lakini hasa kwa sasa na wakulima wanawake, Dialogue: 0,0:11:26.47,0:11:29.59,Default,,0000,0000,0000,,kuwasaidia kuishi maisha yenye amani na tembo. Dialogue: 0,0:11:29.62,0:11:33.06,Default,,0000,0000,0000,,Moja ya vitu tunavyojaribu kufanya ni kutengeneza mifumo ya machaguo Dialogue: 0,0:11:33.08,0:11:36.23,Default,,0000,0000,0000,,ili kuishi katika amani na hawa tembo wakubwa. Dialogue: 0,0:11:36.25,0:11:38.40,Default,,0000,0000,0000,,Moja ya masuala hayo ni kujaribu kuwafanya wakulima, Dialogue: 0,0:11:38.43,0:11:39.65,Default,,0000,0000,0000,,na wanawake kwa ujumla. Dialogue: 0,0:11:39.67,0:11:41.86,Default,,0000,0000,0000,,kuwaza kwa upana kuhusu ni mazao gani wanayopanda Dialogue: 0,0:11:41.89,0:11:43.19,Default,,0000,0000,0000,,katika mashamba yao. Dialogue: 0,0:11:43.21,0:11:44.86,Default,,0000,0000,0000,,Hivyo tunatazamia kupanda mazao Dialogue: 0,0:11:44.88,0:11:47.76,Default,,0000,0000,0000,,ambayo tembo hawahitaji kula, kama pilipili, Dialogue: 0,0:11:47.79,0:11:50.06,Default,,0000,0000,0000,,tangawizi, moringa, alizeti. Dialogue: 0,0:11:50.08,0:11:53.31,Default,,0000,0000,0000,,Na hakika, nyuki na mizinga ya nyuki hupenda mazao haya pia, Dialogue: 0,0:11:53.33,0:11:55.12,Default,,0000,0000,0000,,kwa sababu yana maua mazuri. Dialogue: 0,0:11:55.14,0:11:57.83,Default,,0000,0000,0000,,Moja ya mazao haya ni zao lenye miiba liitwalo katani -- Dialogue: 0,0:11:57.86,0:11:59.73,Default,,0000,0000,0000,,hapa mnalifahamu kama jute. Dialogue: 0,0:12:00.08,0:12:02.59,Default,,0000,0000,0000,,Na mmea huu unaweza kuchanwa Dialogue: 0,0:12:02.62,0:12:04.96,Default,,0000,0000,0000,,na kugeuzwa katika bidhaa ya kufumia. Dialogue: 0,0:12:04.98,0:12:07.05,Default,,0000,0000,0000,,Tunashirikiana na wanawake hawa Dialogue: 0,0:12:07.08,0:12:09.74,Default,,0000,0000,0000,,ambao wanaishi kila siku na changamoto ya tembo Dialogue: 0,0:12:09.77,0:12:12.74,Default,,0000,0000,0000,,kutumia mmea huu kufumia vikapu Dialogue: 0,0:12:12.76,0:12:15.31,Default,,0000,0000,0000,,kujitengenezea kipato. Dialogue: 0,0:12:15.70,0:12:18.18,Default,,0000,0000,0000,,Tumeanza ujenzi wiki tatu zilizopita Dialogue: 0,0:12:18.20,0:12:20.24,Default,,0000,0000,0000,,wa kituo cha biashara cha kinamama Dialogue: 0,0:12:20.26,0:12:22.58,Default,,0000,0000,0000,,ambapo tutakuwa tukishirikiana na wanawake hawa Dialogue: 0,0:12:22.60,0:12:24.12,Default,,0000,0000,0000,,si tu kama wataalamu wa utunzaji nyuki Dialogue: 0,0:12:24.14,0:12:25.80,Default,,0000,0000,0000,,lakini kama wasuka vikapu maridadi; Dialogue: 0,0:12:25.82,0:12:28.93,Default,,0000,0000,0000,,watachakata mafuta ya pilipili, alizeti Dialogue: 0,0:12:28.96,0:12:30.90,Default,,0000,0000,0000,,kutengeneza ving'arisha midomo na asali, Dialogue: 0,0:12:30.93,0:12:34.17,Default,,0000,0000,0000,,na tupo mahala katika safari yetu ili kusaidia hawa wakulima Dialogue: 0,0:12:34.20,0:12:38.59,Default,,0000,0000,0000,,kuishi katika miradi rafiki iliyo bora Dialogue: 0,0:12:38.62,0:12:40.46,Default,,0000,0000,0000,,katika kuishi na tembo. Dialogue: 0,0:12:40.48,0:12:42.20,Default,,0000,0000,0000,,Hivyo ikiwa ni tembo Dialogue: 0,0:12:42.23,0:12:45.29,Default,,0000,0000,0000,,au akinamama au watafiti kama mimi, Dialogue: 0,0:12:45.32,0:12:47.90,Default,,0000,0000,0000,,Nawaona wanawake wakija mstari wa mbele sasa Dialogue: 0,0:12:47.93,0:12:51.97,Default,,0000,0000,0000,,kuwaza tofauti na kwa ufasaha kuhusu changamoto tunazokutana nazo. Dialogue: 0,0:12:52.48,0:12:54.04,Default,,0000,0000,0000,,Tukiwa na ubunifu zaidi, Dialogue: 0,0:12:54.06,0:12:57.50,Default,,0000,0000,0000,,na pengine kuweza kujaliana, Dialogue: 0,0:12:57.53,0:13:00.94,Default,,0000,0000,0000,,Ninaamini tunaweza kutoka katika migogoro na tembo Dialogue: 0,0:13:00.97,0:13:02.91,Default,,0000,0000,0000,,na kuweza kuishi nao kwa uhalisia. Dialogue: 0,0:13:03.34,0:13:04.50,Default,,0000,0000,0000,,Asante. Dialogue: 0,0:13:04.52,0:13:10.61,Default,,0000,0000,0000,,(Makofi)