1 00:00:00,778 --> 00:00:02,674 Kwa kadiri ninavyoweza kumbuka, 2 00:00:02,698 --> 00:00:06,933 Tembo wa Afrika wamekuwa wakinijaza furaha mno. 3 00:00:07,532 --> 00:00:11,069 Ni wanyama wakubwa zaidi wa nchi kavu na wanaonyonyesha waliopo hai nyakati hizi, 4 00:00:11,093 --> 00:00:13,252 wakifikia hadi uzito wa tani saba, 5 00:00:13,276 --> 00:00:16,514 wakiwa na urefu wa mita tatu na nusu kufikia mabega yao. 6 00:00:16,538 --> 00:00:19,982 Wana uwezo wa kula chakula hadi kiasi cha kilo 400 kwa siku, 7 00:00:20,006 --> 00:00:24,545 na wanasambaza mbegu muhimu za mimea kwa takribani maelfu ya kilomita 8 00:00:24,569 --> 00:00:27,036 katika kipindi cha miaka 50 hadi 60 ya maisha yao. 9 00:00:27,530 --> 00:00:31,863 Tembo jike ni kiini cha jamii yao iliyo karimu na ngumu kuielewa. 10 00:00:32,252 --> 00:00:35,601 Hawa jike, viongozi imara hukuza watoto 11 00:00:35,625 --> 00:00:38,688 na kuongoza njia katika kuzishinda changamoto zilizopo kwenye mbuga za Afrika 12 00:00:38,712 --> 00:00:40,912 kutafuta chakula, maji na usalama. 13 00:00:41,554 --> 00:00:43,395 Jamii zao ni ngumu kuzielewa, 14 00:00:43,419 --> 00:00:45,721 bado hatujafanikiwa kuweza tambua 15 00:00:45,745 --> 00:00:48,332 namna gani wanawasiliana, namna gani wanabadilishana maongezi, 16 00:00:48,356 --> 00:00:49,982 namna gani wanatumia lugha zao. 17 00:00:50,006 --> 00:00:54,077 Na hatuelewi kiundani namna gani wanatafuta njia katika uwanda, 18 00:00:54,101 --> 00:00:57,050 kukumbuka njia zilizo salama katika kuvuka mto. 19 00:00:57,728 --> 00:00:59,486 Nina uhakika kabisa kama nilivyo mimi, 20 00:00:59,510 --> 00:01:03,244 wengi wenu mliomo humu mtakuwa na hisia chanya zinazofanana 21 00:01:03,268 --> 00:01:05,668 kwa wanyama hawa maridadi kuliko wanyama wote. 22 00:01:06,117 --> 00:01:08,537 Ni ngumu sana kutoangalia makala ya televisheni, 23 00:01:08,561 --> 00:01:10,094 kujifunza kuhusu uwezo wao mkubwa wa akili 24 00:01:10,118 --> 00:01:12,744 au, kama umeshawahi bahatika, kuwaona kwa macho yako 25 00:01:12,768 --> 00:01:14,402 wakati ukitembelea mbuga. 26 00:01:15,085 --> 00:01:16,529 Lakini najiuliza wangapi kati yenu 27 00:01:16,553 --> 00:01:20,694 kiukweli kabisa, mmewahi kuwaogopa wanyama hawa. 28 00:01:22,482 --> 00:01:24,744 Nilibahatika kukulia kusini mwa Afrika 29 00:01:24,768 --> 00:01:26,236 wazazi wangu wakiwa ni walimu 30 00:01:26,260 --> 00:01:29,315 waliokuwa na likizo ndefu lakini bajeti isiyomudu mambo mengi. 31 00:01:29,898 --> 00:01:33,318 Na hivyo tulikuwa tukitumia gari yetu kuukuu aina ya Ford Cortina Estate, 32 00:01:33,342 --> 00:01:35,374 na dada yangu, tutapakia mizigo nyuma ya gari, 33 00:01:35,398 --> 00:01:38,215 tutabeba mahema na kwenda kuweka kambi katika mbuga mbalimbali 34 00:01:38,239 --> 00:01:39,501 kusini mwa Afrika 35 00:01:39,525 --> 00:01:42,977 Ilikuwa ni kama hisia inayokaribia na ya mbinguni, kwa mtafiti mdogo wa wanyama ninaechipukia kama mimi. 36 00:01:43,398 --> 00:01:45,747 Lakini nakumbuka hata katika umri ule mdogo 37 00:01:45,771 --> 00:01:49,429 ambapo niliona senyenge ndefu za umeme zilizozunguka mbuga 38 00:01:49,453 --> 00:01:50,712 zikileta mgawanyiko. 39 00:01:51,077 --> 00:01:53,752 Hakika, ziliwazuia tembo kuishi na jamii, 40 00:01:53,776 --> 00:01:57,204 lakini pia zilizuia jamii kuweza fika katika mapori. 41 00:01:58,236 --> 00:02:01,632 Ilikuwa ni changamoto sana katika umri ule mdogo. 42 00:02:02,133 --> 00:02:05,355 Ilikuwa ni mpaka nilipohamia Kenya nikiwa na umri wa miaka 14, 43 00:02:05,379 --> 00:02:10,101 Nilipoweza kukutana na sehemu za pori zilizo kubwa ndani ya Afrika Mashariki. 44 00:02:10,125 --> 00:02:13,879 Na hapa sasa ninahisi kweli, binafsi, 45 00:02:13,903 --> 00:02:15,188 nipo nyumbani. 46 00:02:15,902 --> 00:02:19,585 Nimeishi miaka mingi ya furaha, nikiwatafiti tembo nikiwa ndani ya hema, 47 00:02:19,609 --> 00:02:21,615 katika mbuga ya taifa ya Samburu, 48 00:02:21,639 --> 00:02:25,876 chini ya uangalizi wa Profesa Fritz Vollrath na Iain Douglas-Hamilton, 49 00:02:25,900 --> 00:02:30,535 nikisomea shahada ya uzamivu na kuelewa mambo mengi magumu ya jamii za tembo. 50 00:02:31,791 --> 00:02:35,729 Lakini sasa, katika jukumu langu nikiwa kama mkuu wa programu ya uwepo tembo na binadamu pamoja 51 00:02:35,753 --> 00:02:37,078 kwa ajili ya mradi wa Okoa Tembo, 52 00:02:37,102 --> 00:02:41,218 tunaona mabadiliko mengi yakitokea haraka 53 00:02:41,242 --> 00:02:45,440 ambayo yanachochea mabadiliko katika programu zetu za utafiti. 54 00:02:45,464 --> 00:02:48,956 Hatuwezi tena tukakaa na kuelewa jamii za tembo 55 00:02:48,980 --> 00:02:51,782 au kujifunza namna za kuzuia biashara ya pembe za tembo, 56 00:02:51,806 --> 00:02:54,244 ambayo inatisha na bado inaendelea. 57 00:02:54,268 --> 00:02:57,022 Tunahitajika kubadili rasilimali zetu zaidi na zaidi 58 00:02:57,046 --> 00:03:01,188 tukiangazia matatizo yanajitokeza katika migogoro ya binadamu na tembo, 59 00:03:01,212 --> 00:03:04,791 pale binadamu na tembo wanapogombania nafasi na rasilimali. 60 00:03:05,536 --> 00:03:07,585 Ni hivi karibuni katika miaka ya 1970 61 00:03:07,609 --> 00:03:11,902 ambapo tulikuwa na tembo takribani milioni 1.2 wakizunguka Afrika. 62 00:03:11,926 --> 00:03:16,664 Leo hii, tuna takaribani tembo 400,000 waliosalia. 63 00:03:17,093 --> 00:03:21,363 Na katika wakati huo huo, jamii ya binadamu imeongezeka mara nne, 64 00:03:21,387 --> 00:03:23,704 na ardhi inagawanywa katika kasi 65 00:03:23,728 --> 00:03:26,261 ambayo ni ngumu kwenda nayo. 66 00:03:26,673 --> 00:03:30,355 Mara nyingi, tembo hawa wanaohama huishia katika jamii za binadamu, 67 00:03:30,379 --> 00:03:31,673 wakitafuta maji na chakula 68 00:03:31,697 --> 00:03:34,252 lakini huishia kuvunja pipa za maji 69 00:03:34,276 --> 00:03:35,433 wakivunja mabomba 70 00:03:35,457 --> 00:03:38,387 na, pia, huvunja maghala ya chakula. 71 00:03:38,411 --> 00:03:40,344 Ni changamoto kubwa mno. 72 00:03:40,968 --> 00:03:42,491 Unaweza fikiria hatari 73 00:03:42,515 --> 00:03:46,108 ya tembo akiwa anavunja paa la nyumba yako ya udongo 74 00:03:46,132 --> 00:03:47,428 usiku wa manane 75 00:03:47,452 --> 00:03:49,516 na kuwatupa watoto wako pembeni 76 00:03:49,540 --> 00:03:53,958 anaposogeza mkonga, akitafuta chakula katika giza? 77 00:03:54,585 --> 00:03:57,315 Tembo hawa wanakanyaga na kula mazao, 78 00:03:57,339 --> 00:03:59,605 na hii inaondoa 79 00:03:59,629 --> 00:04:02,561 uvumilivu ambao watu wamekuwa nao kwa tembo. 80 00:04:03,046 --> 00:04:06,847 Na cha kusikitisha, tunawapoteza wanyama hawa ndani ya siku 81 00:04:06,871 --> 00:04:09,855 na, katika baadhi ya nchi, ndani ya saa -- 82 00:04:09,879 --> 00:04:11,260 si tu kwa ajili kupata pembe za ndovu 83 00:04:11,284 --> 00:04:13,895 lakini mgogoro huu unaokua haraka kati ya binadamu na tembo 84 00:04:13,919 --> 00:04:16,585 wanapogombania nafasi na rasilimali. 85 00:04:16,950 --> 00:04:18,156 Ni changamoto kubwa mno. 86 00:04:18,180 --> 00:04:21,141 Namaanisha, unawezaje kupambana na tembo wa tani saba, 87 00:04:21,165 --> 00:04:23,242 ambao kwa kawaida huja katika makundi ya tembo 10 au 12, 88 00:04:23,266 --> 00:04:25,720 katika mashamba madogo ya kijijini 89 00:04:25,744 --> 00:04:27,252 unapokuwa unaongelea watu 90 00:04:27,276 --> 00:04:30,371 ambao wanaishi katika ufukara? 91 00:04:30,395 --> 00:04:31,796 Hawana bajeti kubwa. 92 00:04:31,820 --> 00:04:34,759 Unawezaje kusuluhisha? 93 00:04:35,157 --> 00:04:38,760 Pengine, labda suala laweza kuwa hivi, unaweza anza kujenga senyenge ya umeme, 94 00:04:38,784 --> 00:04:40,522 na hili linatokea Afrika kote, 95 00:04:40,546 --> 00:04:42,156 tunaliona likitokea zaidi na zaidi. 96 00:04:42,180 --> 00:04:45,822 Lakini wanagawanya maeneo na kufunga njia. 97 00:04:45,846 --> 00:04:49,251 Na ninakueleza, hawa tembo hawajali zaidi kuhusu hili, 98 00:04:49,275 --> 00:04:52,164 iwapo watazuia shimo muhimu la maji 99 00:04:52,188 --> 00:04:53,371 ambapo wanahitaji maji, 100 00:04:53,395 --> 00:04:56,103 au kuna jike linalovutia upande wa pili. 101 00:04:56,127 --> 00:04:58,658 Haichukui muda kuvunja nguzo mojawapo ya senyenge. 102 00:04:58,682 --> 00:05:00,738 Na mara panapotokea mwanya katika senyenge, 103 00:05:00,762 --> 00:05:02,428 wanarudi tena, wanaongea na wenzao na ghafla wote wanapita kwenda upande wa pili, 104 00:05:02,452 --> 00:05:04,335 na mwishoni wote wanakuwa wamepita, 105 00:05:04,359 --> 00:05:07,857 na sasa unao tembo 12 katika upande jamii ya binadamu inapoishi. 106 00:05:07,881 --> 00:05:10,032 Na upo katika hatari kwelikweli. 107 00:05:10,056 --> 00:05:13,575 Watu hujaribu kuja na namna mbalimbali za senyenge za umeme. 108 00:05:14,421 --> 00:05:17,334 Hata hivyo, tembo hawa hawafikiri sana kuhusu hilo. 109 00:05:17,761 --> 00:05:20,710 (Kicheko) 110 00:05:22,687 --> 00:05:27,439 Kwa hiyo badala ya kuwa na hizi senyenge ngumu, zilizo na umeme, 111 00:05:27,463 --> 00:05:31,124 ambazo zinaleta mgawanyo wa tembo na binadamu kuhama, 112 00:05:31,148 --> 00:05:33,757 lazima kuwepo na namna nyingine ya kutazamia changamoto hii. 113 00:05:33,781 --> 00:05:36,616 Ninaangazia zaidi katika njia ambayo ni ya jumla na iliyo ya asili 114 00:05:36,640 --> 00:05:39,520 ili kuwatenganisha wanadamu na tembo pale inapohitajika. 115 00:05:40,180 --> 00:05:41,823 Kwa urahisi kuongea na watu, 116 00:05:41,847 --> 00:05:44,109 kuongea na wafugaji wa vijijini kaskazini mwa Kenya 117 00:05:44,133 --> 00:05:46,680 ambao wana uzoefu mkubwa wa porini, 118 00:05:46,704 --> 00:05:50,680 tuligundua hii hadithi ya kwamba walikuwapo tembo ambao hawali majani ya miti 119 00:05:50,704 --> 00:05:52,570 ambayo ina mizinga ya nyuki. 120 00:05:52,594 --> 00:05:54,611 Sasa hii ilikuwa ni hadithi ya kuvutia. 121 00:05:54,635 --> 00:05:56,643 Tembo walipokuwa wakila katika miti, 122 00:05:56,667 --> 00:06:00,270 walivunja matawi na pengine kuharibu mizinga ya nyuki. 123 00:06:00,294 --> 00:06:03,651 Na wale nyuki watakimbia kutoka katika makazi yao 124 00:06:03,675 --> 00:06:05,347 na kuwang'ata tembo. 125 00:06:05,371 --> 00:06:06,958 Sasa kama tembo watang'atwa, 126 00:06:06,982 --> 00:06:09,625 pengine watakumbuka kwamba mti huu ni hatari 127 00:06:09,649 --> 00:06:11,839 na hawatorudi sehemu ile. 128 00:06:11,863 --> 00:06:15,316 Inaonekana kwamba haiwezekani kung'atwa katika ngozi yao nene -- 129 00:06:15,340 --> 00:06:17,706 ngozi ya tembo ni takribani sentimeta mbili. 130 00:06:17,730 --> 00:06:20,494 Lakini inaonekana nyuki huwang'ata katika sehemu ambazo zina maji maji, 131 00:06:20,518 --> 00:06:24,505 kuzunguka macho, nyuma ya masikio, katika mdomo, juu ya mkonga. 132 00:06:24,946 --> 00:06:28,183 Unaweza kuona kwamba watakumbuka kwa urahisi zaidi. 133 00:06:28,207 --> 00:06:31,073 Na si kwamba wanaogopa kung'atwa mara moja. 134 00:06:31,097 --> 00:06:34,065 Nyuki wa Afrika wana uwezo wa ajabu: 135 00:06:34,089 --> 00:06:36,864 waking'ata sehemu, hutoa kemikali iitwayo pheromone 136 00:06:36,888 --> 00:06:40,103 ambayo huchochea nyuki wengine kung'ata sehemu hiyo hiyo. 137 00:06:40,127 --> 00:06:42,458 Kwa si mng'ato mmoja wanaoogopa -- 138 00:06:42,492 --> 00:06:44,364 lakini pengine ming'ato takribani elfu ya nyuki, 139 00:06:44,388 --> 00:06:47,493 kuja kung'ata sehemu hiyo hiyo -- hicho ndicho wanachoogopa. 140 00:06:47,961 --> 00:06:49,596 Na hivyo, mama mzuri 141 00:06:49,620 --> 00:06:52,548 huwaepusha mbali watoto zake na hatari hiyo. 142 00:06:52,572 --> 00:06:54,509 tembo wadogo wana ngozi nyembamba, 143 00:06:54,533 --> 00:06:56,572 na inapelekea uwezekano wa kuweza kung'atwa 144 00:06:56,596 --> 00:06:58,463 katika ngozi zao nyembamba. 145 00:06:58,950 --> 00:07:02,442 Hivyo kwa ajili ya shahada ya uzamivu, nilipata changamoto hii isiyo kawaida 146 00:07:02,466 --> 00:07:03,848 katika kujaribu kutafuta namna 147 00:07:03,872 --> 00:07:07,819 namna gani tembo na nyuki wa Afrika wanaweza kuwa pamoja, 148 00:07:07,843 --> 00:07:10,716 wakati nadharia inasema hawawezi changamana kabisa. 149 00:07:10,740 --> 00:07:12,772 Niliwezaje kufanyia utafiti hili suala? 150 00:07:12,796 --> 00:07:16,776 Sasa, nilirekodi mlio wa nyuki wa Afrika waliokasirishwa, 151 00:07:16,800 --> 00:07:20,220 na nikauchezesha karibu na tembo waliopumzika chini ya miti 152 00:07:20,244 --> 00:07:21,939 kupitia spika isiyotumia waya, 153 00:07:21,963 --> 00:07:26,442 hivyo ingenipelekea kuelewa namna gani wangeitikia kama kungekuwepo na nyuki pori katika eneo lile. 154 00:07:26,466 --> 00:07:29,553 Na ilitokea kwamba waliitikia katika namna ya kustaajabu 155 00:07:29,577 --> 00:07:31,844 kutokana na sauti ile ya nyuki pori. 156 00:07:32,990 --> 00:07:36,617 Hapa sasa, sauti ya nyuki ikisikika katika kundi hili la tembo. 157 00:07:36,641 --> 00:07:39,362 Utaona masikio yao yanaenda juu, yanatoka nje, 158 00:07:39,386 --> 00:07:41,839 wanageuza vichwa vyao kila pande, 159 00:07:41,863 --> 00:07:44,601 tembo mmoja anachezesha mkonga wake akijaribu kunusa. 160 00:07:45,050 --> 00:07:48,082 Kuna tembo mmoja anayempiga mtoto katika ardhi 161 00:07:48,106 --> 00:07:50,765 akimueleza asimame kwa vile kuna hatari. 162 00:07:51,210 --> 00:07:53,829 Na tembo mmoja anarudi nyuma, 163 00:07:53,853 --> 00:07:57,903 na baada ya muda mfupi familia yote ya tembo inakimbia kumfata 164 00:07:57,927 --> 00:08:01,126 kwenye nyika katika wingu la vumbi. 165 00:08:01,150 --> 00:08:02,854 (Sauti ya nyuki wakilia) 166 00:08:08,394 --> 00:08:09,679 (Sauti ya nyuki inafikia ukingoni) 167 00:08:09,703 --> 00:08:14,028 Nimefanya utafiti huu mara nyingi sana, 168 00:08:14,052 --> 00:08:16,703 na tembo hukimbia. 169 00:08:16,727 --> 00:08:18,479 Si tu kukimbia, 170 00:08:18,503 --> 00:08:20,590 Lakini hujichafua pale wanapokimbia, 171 00:08:20,614 --> 00:08:22,947 ili kuweza kuwafukuzza nyuki kutoka hewani. 172 00:08:23,511 --> 00:08:26,991 Na tuliweka vipaza sauti vya kunasa mawimbi ya chini ya sauti kuwazunguka tembo 173 00:08:27,015 --> 00:08:28,768 tukiwa tunafanya utafiti huu. 174 00:08:28,792 --> 00:08:32,443 Na tukagundua kwamba wanawasiliana katika sauti za mawimbi ya chini wakinguruma 175 00:08:32,467 --> 00:08:34,403 wakijaribu kuambiana kuhusu hatari ya nyuki 176 00:08:34,427 --> 00:08:36,493 na kukaa mbali na eneo lile. 177 00:08:37,038 --> 00:08:38,664 Hivyo ugunduzi huu wa tabia 178 00:08:38,688 --> 00:08:41,188 ulitasaidia kuelewa namna gani tembo wanaitikia 179 00:08:41,212 --> 00:08:43,561 wanaposikia au kuwaona nyuki. 180 00:08:43,585 --> 00:08:47,704 Hii ilinisaidia kutengeneza ubunifu mpya wa senyenge ya mizinga ya nyuki, 181 00:08:47,728 --> 00:08:51,204 ambayo kwa sasa tunajenga katika mashamba madogo ya kati ya ekari moja hadi mbili 182 00:08:51,228 --> 00:08:53,941 katika sehemu ambazo zina tatizo hili kwa kiasi kikubwa 183 00:08:53,965 --> 00:08:56,609 ambapo binadamu na tembo hugombania nafasi. 184 00:08:57,260 --> 00:08:59,349 Senyenge hizi za mizinga ya nyuki ni rahisi sana. 185 00:08:59,373 --> 00:09:02,625 Tunatumia mizinga 12 ya mizinga 12 mingine bandia 186 00:09:02,649 --> 00:09:05,045 ili kulinda ekari moja ya shamba. 187 00:09:05,069 --> 00:09:07,363 Sasa mzinga bandia ni kipande cha mbao 188 00:09:07,387 --> 00:09:09,625 ambacho hukatwa katika mraba, kupakwa rangi ya njano 189 00:09:09,649 --> 00:09:11,307 na kuning'inizwa katika mizinga halisi. 190 00:09:11,331 --> 00:09:13,276 Kimsingi tunawapumbaza tembo 191 00:09:13,300 --> 00:09:16,125 kwamba kuna mizinga ya nyuki mingi kuliko iliyopo. 192 00:09:16,149 --> 00:09:18,990 Na hata hivyo, inaokoa nusu gharama ya senyenge. 193 00:09:19,014 --> 00:09:20,671 Kwa hivyo kuna mzinga halisi na ulio bandia 194 00:09:20,695 --> 00:09:22,442 na mzinga halisi tena ukifatiwa na ulio wa bandia, 195 00:09:22,466 --> 00:09:24,942 kila mita 10 kuzunguka mpaka wa nje. 196 00:09:24,966 --> 00:09:26,601 Inashikiliwa na nguzo 197 00:09:26,625 --> 00:09:28,745 na kivuli cha paa ili kulinda nyuki, 198 00:09:28,769 --> 00:09:31,921 na imeunganishwa na kipande cha kawaida cha waya, 199 00:09:31,945 --> 00:09:34,379 ambacho kinazunguka kwenye shamba lote, kikiunganisha mizinga. 200 00:09:34,403 --> 00:09:36,859 Hivyo kama tembo atajaribu kuingia katika shamba, 201 00:09:36,883 --> 00:09:38,729 atakwepa mizinga ya nyuki katika namna yoyote ile, 202 00:09:38,753 --> 00:09:42,059 lakini atajaribu kusukuma katika mzinga halisi na bandia, 203 00:09:42,083 --> 00:09:45,423 kusababisha mizinga yote kutikisika pale waya unapogonga mzinga. 204 00:09:45,447 --> 00:09:47,408 Na tunajua kutokana na utafiti wetu, 205 00:09:47,432 --> 00:09:50,347 hii itasababisha tembo kukimbia mbali na eneo lile -- 206 00:09:50,371 --> 00:09:54,108 na pia kukumbuka kutokurudi eneo lile ambalo ni hatari. 207 00:09:54,132 --> 00:09:55,863 Nyuki watatoka kwenye mizinga, 208 00:09:55,887 --> 00:09:58,481 na kuwafukuza tembo. 209 00:09:58,505 --> 00:10:01,974 Mizinga hii tunaifatilia kwa kufunga kamera 210 00:10:01,998 --> 00:10:04,355 ili kutusaidia kuelewa namna gani tembo wanaitikia 211 00:10:04,379 --> 00:10:05,584 katika nyakati za usiku, 212 00:10:05,608 --> 00:10:07,870 ambapo ni muda uharibifu wa mazao hutokea sana. 213 00:10:07,894 --> 00:10:10,218 Katika mashamba darasa yetu tuligundua 214 00:10:10,242 --> 00:10:12,958 kwamba tunafukuza asilimia 80 ya tembo 215 00:10:12,982 --> 00:10:15,466 kutoweza kuingia katika shamba. 216 00:10:15,966 --> 00:10:20,720 Na nyuki husaidia uchavushaji katika eneo lile. 217 00:10:20,744 --> 00:10:24,410 Hivyo tunafakiwa kupunguza sana uharibifu wa mazao na idadi ya tembo wanaoshambulia mashamba 218 00:10:24,434 --> 00:10:27,097 na kuongeza mazao kutokana na uchavushaji 219 00:10:27,121 --> 00:10:29,791 ambao nyuki wanaufanya kwenye mazao. 220 00:10:30,585 --> 00:10:33,258 Nguvu ya senyenge za mizinga ya nyuki ni muhimu sana -- 221 00:10:33,282 --> 00:10:35,197 koloni zinatakiwa kuwa imara. 222 00:10:35,221 --> 00:10:38,173 Hivyo tunajaribu kuwasaidia wakulima kukuza mazao yanasaidia uchavushaji 223 00:10:38,197 --> 00:10:40,221 ili kuweza kukuza mizinga yao, 224 00:10:40,245 --> 00:10:41,872 kuongeza nguvu ya nyuki zao 225 00:10:41,896 --> 00:10:44,767 na, hivyo, kutengeneza asali bora zaidi. 226 00:10:44,791 --> 00:10:48,926 Asali hii ina thamani kubwa kama kipato cha ziada kwa wakulima. 227 00:10:49,244 --> 00:10:51,276 Ni mbadala wa sukari wenye afya, 228 00:10:51,300 --> 00:10:53,014 na kwa jamii yetu, 229 00:10:53,038 --> 00:10:55,553 ni zawadi yenye thamani sana kumpa mama mkwe, 230 00:10:55,577 --> 00:10:57,465 ambapo inakuwa kama tunu. 231 00:10:57,489 --> 00:10:59,616 (Kicheko) 232 00:10:59,942 --> 00:11:01,607 Sasa tunaweka asali hii kwenye chupa, 233 00:11:01,631 --> 00:11:05,734 na tumeipa asali hii jina la Asali Rafiki kwa Tembo. 234 00:11:05,758 --> 00:11:06,909 Ni jina la kufurahisha, 235 00:11:06,933 --> 00:11:09,123 lakini pia limeleta usikivu katika mradi wetu 236 00:11:09,147 --> 00:11:11,552 na kusaidia kuelewa ni kipi tunachojaribu kufanya 237 00:11:11,576 --> 00:11:12,728 ili kuokoa tembo. 238 00:11:12,752 --> 00:11:14,498 Tunafanya kazi na wakina mama wengi sana 239 00:11:14,522 --> 00:11:17,103 katika sehemu 60 zilzo na migogoro ya binadamu na tembo 240 00:11:17,127 --> 00:11:19,634 katika nchi 19 zilizopo Afrika na Asia 241 00:11:19,658 --> 00:11:21,688 kujenga senyenge hizi za mizinga, 242 00:11:21,712 --> 00:11:24,138 tukifanya kazi kwa ukaribu na wakulima wengi 243 00:11:24,162 --> 00:11:26,442 lakini hasa kwa sasa na wakulima wanawake, 244 00:11:26,466 --> 00:11:29,592 kuwasaidia kuishi maisha yenye amani na tembo. 245 00:11:29,616 --> 00:11:33,060 Moja ya vitu tunavyojaribu kufanya ni kutengeneza mifumo ya machaguo 246 00:11:33,084 --> 00:11:36,228 ili kuishi katika amani na hawa tembo wakubwa. 247 00:11:36,252 --> 00:11:38,403 Moja ya masuala hayo ni kujaribu kuwafanya wakulima, 248 00:11:38,427 --> 00:11:39,649 na wanawake kwa ujumla. 249 00:11:39,673 --> 00:11:41,863 kuwaza kwa upana kuhusu ni mazao gani wanayopanda 250 00:11:41,887 --> 00:11:43,188 katika mashamba yao. 251 00:11:43,212 --> 00:11:44,860 Hivyo tunatazamia kupanda mazao 252 00:11:44,884 --> 00:11:47,764 ambayo tembo hawahitaji kula, kama pilipili, 253 00:11:47,788 --> 00:11:50,061 tangawizi, moringa, alizeti. 254 00:11:50,085 --> 00:11:53,308 Na hakika, nyuki na mizinga ya nyuki hupenda mazao haya pia, 255 00:11:53,332 --> 00:11:55,117 kwa sababu yana maua mazuri. 256 00:11:55,141 --> 00:11:57,831 Moja ya mazao haya ni zao lenye miiba liitwalo katani -- 257 00:11:57,855 --> 00:11:59,728 hapa mnalifahamu kama jute. 258 00:12:00,075 --> 00:12:02,591 Na mmea huu unaweza kuchanwa 259 00:12:02,615 --> 00:12:04,956 na kugeuzwa katika bidhaa ya kufumia. 260 00:12:04,980 --> 00:12:07,052 Tunashirikiana na wanawake hawa 261 00:12:07,076 --> 00:12:09,742 ambao wanaishi kila siku na changamoto ya tembo 262 00:12:09,766 --> 00:12:12,735 kutumia mmea huu kufumia vikapu 263 00:12:12,759 --> 00:12:15,307 kujitengenezea kipato. 264 00:12:15,696 --> 00:12:18,180 Tumeanza ujenzi wiki tatu zilizopita 265 00:12:18,204 --> 00:12:20,235 wa kituo cha biashara cha kinamama 266 00:12:20,259 --> 00:12:22,577 ambapo tutakuwa tukishirikiana na wanawake hawa 267 00:12:22,601 --> 00:12:24,117 si tu kama wataalamu wa utunzaji nyuki 268 00:12:24,141 --> 00:12:25,799 lakini kama wasuka vikapu maridadi; 269 00:12:25,823 --> 00:12:28,934 watachakata mafuta ya pilipili, alizeti 270 00:12:28,958 --> 00:12:30,903 kutengeneza ving'arisha midomo na asali, 271 00:12:30,927 --> 00:12:34,171 na tupo mahala katika safari yetu ili kusaidia hawa wakulima 272 00:12:34,195 --> 00:12:38,592 kuishi katika miradi rafiki iliyo bora 273 00:12:38,616 --> 00:12:40,456 katika kuishi na tembo. 274 00:12:40,480 --> 00:12:42,203 Hivyo ikiwa ni tembo 275 00:12:42,227 --> 00:12:45,291 au akinamama au watafiti kama mimi, 276 00:12:45,315 --> 00:12:47,905 Nawaona wanawake wakija mstari wa mbele sasa 277 00:12:47,929 --> 00:12:51,974 kuwaza tofauti na kwa ufasaha kuhusu changamoto tunazokutana nazo. 278 00:12:52,481 --> 00:12:54,037 Tukiwa na ubunifu zaidi, 279 00:12:54,061 --> 00:12:57,505 na pengine kuweza kujaliana, 280 00:12:57,529 --> 00:13:00,942 Ninaamini tunaweza kutoka katika migogoro na tembo 281 00:13:00,966 --> 00:13:02,913 na kuweza kuishi nao kwa uhalisia. 282 00:13:03,341 --> 00:13:04,500 Asante. 283 00:13:04,524 --> 00:13:10,611 (Makofi)