Jinsi ukweli halisi unawabadilisha wanafunzi kuwa wanasayansi
-
0:01 - 0:02kwa jinsi gani uligundua shauku yako
-
0:02 - 0:04ama kupata kazi yako?
-
0:04 - 0:05Je, ulikutana nayo?
-
0:05 - 0:07ama ilikua ni kufanya majaribio na kukosea?
-
0:07 - 0:10Kama mtetezi wa haki za watoto,
Marian Wright Edelman alisema, -
0:11 - 0:13¨Hauwezi ukawa usichokiona.¨
-
0:14 - 0:16Kwa bahati nzuri, sasa tunaishi katika
wakati -
0:16 - 0:20ambao teknolojia zinazojitokeza zaweza
kutusaidia kusuluhisha tatizo hili -
0:20 - 0:21Kwa miaka miwili iliyopita
-
0:21 - 0:24nimekua nikikuza mpango wa ukweli
uliopanuliwa -
0:24 - 0:27unaowezesha wanafunzi wa shule za kati,
kutoka nchi nzima -
0:27 - 0:30kuchukua jukumu la mwanasaikolojia wa
baharini -
0:30 - 0:32hata kama hawajawahi kuona bahari
-
0:33 - 0:36kama mwanafunzi mmoja wa darasa la saba ambaye hivi
karibuni amekamilisha programu yetu -
0:36 - 0:39alisema, ¨Niliweza kujiona ni
mwanasayansi, -
0:39 - 0:41kwa sababu nilifurahia mchezo huu.¨
-
0:41 - 0:43Maoni haya yalinisisimua sana
-
0:43 - 0:47kwa sababu wanafunzi wachache sana hujiona
kama wanasayansi -
0:47 - 0:53Utafiti wa 2014 ulionyesha kuwa asilimia 57
ya wanafunzi wa darasa la nane na tisa -
0:53 - 0:55walisema, ¨Sipendi sayansi¨
-
0:56 - 0:58Vivyo hivyo, pia katika 2014,
-
0:58 - 1:01Nilikutana naye Mandë Holford,
mtaalamu wa kemia ya baharini -
1:01 - 1:04na Lindsay Portnoy, mwanasaikolojia wa
elimu. -
1:05 - 1:07Sote watatu tulishirikiana shauku
-
1:07 - 1:10ya kuwafanya wanafunzi wavutiwe, na wawe
na starehe katika sayansi. -
1:11 - 1:13Tulifikiria juu ya jinsi
tunaweza kuwapa watoto -
1:13 - 1:16uzoefu wa kweli zaidi katika taaluma ya
kisayansi -
1:16 - 1:18Tulijadili utafiti huo;
-
1:18 - 1:22ulionyesha kuwa wanafunzi walihisi vizuri
kuwa na uthubutu wakati wa kucheza michezo. -
1:23 - 1:26Basi sote watatu tulianzisha kampuni ya
michezo ya kielimu -
1:26 - 1:28kuipa sayansi uhai
-
1:29 - 1:33Ukweli halisi ulionekana kama njia ya bei
ya chini ya kuongeza ufikiaji -
1:33 - 1:36Juu ya hayo, utafiti wa kitaalam
umeonyesha -
1:36 - 1:40ukweli halisi unaweza kusababisha
kuongezeka kwa utunzaji wa kujifunza. -
1:40 - 1:43Hii ilikuwa kamili kwetu,
kama tulivyotaka kuwa mashuleni -
1:43 - 1:46ili tuweze kufikia
idadi kubwa ya wanafunzi kadiri iwezekanavyo, -
1:46 - 1:49haswa wanafunzi ambao wana uwakilishi mdogo katika sayansi
-
1:49 - 1:52Kwa hivyo, tukiwa na ufadhili kutoka Mfuko wa Sayansi wa Kitaifa,
-
1:52 - 1:55tulianza kukuza mpango wetu wa ukweli
uliopanuliwa -
1:55 - 1:57ulioleta pamoja ukweli halisi
-
1:57 - 1:59na jarida la kibinafsi la kidijitali
-
2:00 - 2:02Tulifanya kazi na waalimu tulipokua
tukiuendeleza -
2:02 - 2:05kuhakikisha kuwa utafaa bila shida
ndani ya mitaala iliyopo -
2:06 - 2:10na kuwawezesha waalimu kutumia teknolojia
ya kisasa madarasani mwao. -
2:10 - 2:13Tulibuni ukweli halisi wa Kadi ya Google,
-
2:13 - 2:15ambao unahitaji simu janja tu
-
2:15 - 2:19na kitazamaji cha VR cha dola 10
kilichotengenezwa kwa kadibodi. -
2:20 - 2:21kwa hivi vifaa vya kichwa visivyo ghali,
-
2:21 - 2:25wanafunzi husafirishwa katika msafara
chini ya maji. -
2:25 - 2:27Wanafunzi hutumia jarida lao la kidijitali
-
2:27 - 2:29kuandika maelezo yao,
-
2:29 - 2:30kujibu maswali,
-
2:30 - 2:32kujenga mifano
-
2:32 - 2:33na kukuza nadharia.
-
2:33 - 2:37Wanafunzi basi huenda katika ulimwengu wa kweli kujaribu nadharia zao
-
2:37 - 2:39ili waone ikiwa ni sahihi,
-
2:39 - 2:40kadiri wanasayansi waendavyo katika
nyanja za utafiti -
2:40 - 2:42katika kazi zao.
-
2:43 - 2:45Wanafunzi wanaporudi kwa jarida lao la
kidijitali, -
2:45 - 2:47hushiriki uchunguzi wao, madai,
-
2:47 - 2:49hoja na ushahidi.
-
2:49 - 2:54Majibu ya wanafunzi yaliyoandikwa na
mwingiliano wa kawaida -
2:54 - 2:56zote husasishwa moja kwa moja
-
2:56 - 2:58kwenye dashibodi ya tathmini ya mwalimu,
-
2:58 - 3:00ili walimu waweze kufuata maendeleo yao
-
3:00 - 3:03na wawasaidie kama inavyohitajika.
-
3:03 - 3:05Ili kukupa hisia nzuri, nitakuonyesha
-
3:05 - 3:07kidogo ya yale wanafunzi huona.
-
3:08 - 3:10Huu ndio ukweli halisi wanapokuwa chini ya
maji -
3:10 - 3:13wakiangalia mimea na wanyama.
-
3:14 - 3:17Hii ni jarida la kidijitali
ambapo wanaunda mifano yao -
3:17 - 3:20kulingana na data hii ya kawaida kuonyesha
wanachotarajia kuona. -
3:21 - 3:24Hapa, wanaunga mkono hiyo na taarifa za
ubora. -
3:24 - 3:27Na hii ndio dashibodi ya ualimu
inayoonyesha maendeleo -
3:27 - 3:31na inawezesha [waalimu] kuona majibu ya
wanafunzi wanapoendelea. -
3:33 - 3:35Tulipokua tunaunda BioDive,
-
3:35 - 3:37tulitaka sana kuzingatia ufikiaji,
-
3:37 - 3:41kwa hivyo tuliijenga kuhitaji simu moja tu
kwa kila wanafunzi wanne. -
3:41 - 3:45Tulijua pia jinsi kazi ya sayansi inavyoshirikisha,
-
3:45 - 3:47kwa hivyo tuliunda uzoefu kutatuliwa tu
-
3:47 - 3:49kupitia kushirikiana
-
3:49 - 3:53kwani kila mwanafunzi ni mtaalam katika
eneo tofauti la kijiografia. -
3:54 - 3:57Kwa kuzingatia kwamba akili za watoto hawa
bado inaendelea kukua, -
3:57 - 4:01tulipunguza kila uzoefu kudumu kiwango
kisichozidi dakika mbili. -
4:01 - 4:05Na mwishowe, kwa sababu tunajua umuhimu
wa kudhihirishwa mara kwa mara -
4:05 - 4:07ili kufahamu maarifa
-
4:07 - 4:11tuliunda BioDive ifanyike zaidi ya vipindi
vya darasa tano. -
4:12 - 4:15Tulianza majaribio ya BioDive mnamo 2017
-
4:15 - 4:18katika shule 20 huko New York na New Jersey.
-
4:18 - 4:21Tulitaka kuona wanafunzi walipokuwa
wakitumia teknolojia hii mpya. -
4:21 - 4:24Mnamo mwaka wa 2019, sasa,
-
4:24 - 4:28tunafanya majaribio katika majimbo 26 kwa
sasa. -
4:28 - 4:31Tulichosikia kutoka kwa waalimu
ambao wamefundisha kwa kutumia programu yetu: -
4:31 - 4:34"Ilikuwa njia nzuri ya kuonyesha mienendo ya bahari
bila anasa ya kuwa huko hasa -
4:34 - 4:36kwa kuwa tupo Ohio. "
-
4:36 - 4:37(Kicheko)
-
4:37 - 4:38"Ni ya kushangaza sana."
-
4:38 - 4:41"Wanafunzi walishiriki kabisa."
-
4:41 - 4:44Lakini kinachotupa tumaini ni tunachosikia
kutoka kwa wanafunzi -
4:45 - 4:47"Nilipenda jinsi ilivyoonekana kana kwamba
nilikuwa pale." -
4:47 - 4:49"Ina maingiliano na ni njia nzuri ya
kufurahia unapojifunza." -
4:49 - 4:53"Ilinipa mifano ya kweli ya jinsi viumbe
hawa wanavyoonekana. " -
4:54 - 4:58"Nilijiona kama mwanasayansi
kwa sababu inaonekana kufurahisha sana. " -
4:59 - 5:01Maoni yetu hayakuwa mazuri kila wakati.
-
5:02 - 5:03Tulipoanza kukuza,
-
5:03 - 5:05tulianza kwa kuwauliza wanafunzi
-
5:05 - 5:07walichokipenda,
-
5:07 - 5:08kile wasichokipenda
-
5:08 - 5:10na kile walichokipata kinawachanganya.
-
5:10 - 5:13Mwishowe tulianza kuuliza walichokua
nahamu ya kufanya. -
5:14 - 5:17Maoni yao yakatupa vitu halisi vya kujenga
ndani -
5:17 - 5:21ili kuwa na uhakika kuwa tunajumuisha
sauti za wanafunzi katika tulichokibuni. -
5:22 - 5:26Kwa jumla, kile tumejifunza ni kwamba huu
ni mwanzo wa jukwaa mpya -
5:26 - 5:29la kuwapa wanafunzi sauti na umiliki
-
5:29 - 5:32katika kuamua jinsi wanataka kuwa na athari
-
5:32 - 5:33katika kazi zao.
-
5:34 - 5:35Tulilenga sayansi,
-
5:35 - 5:37kwa sababu twafahamu kuwa twawahitaji wanasayansi
-
5:37 - 5:40ili kutusaidia kutatua hali yetu ya sasa na
changamoto za baadaye. -
5:41 - 5:45Lakini ukweli halisi unaweza kusaidia
wanafunzi katika eneo lolote. -
5:45 - 5:49Tunawezaje kuwasaidia wanafunzi katika
kutafuta tamaa zao zote -
5:49 - 5:53kwa uzoefu huu wa kufungua jicho na nafasi
za kujifunza kutoka kwa vyanzo vya msingi? -
5:53 - 5:57Tunaweza kuunda... VR za vifaa vya kichwa
visivyo ghali -
5:58 - 6:01ambazo zinawaruhusu wazame katika fasihi
ya mdomo -
6:01 - 6:03au katika wakati mgumu wa historia ya wanadamu?
-
6:03 - 6:07Ukweli uliopanuliwa una uwezo
wakubadilisha mwelekeo -
6:07 - 6:09wa maisha ya watoto wetu
-
6:09 - 6:11na uwaongoze kwenye kazi hawakuwahi
kufikiria -
6:12 - 6:15kwa kuwapa nafasi ya kuona ni nini
wanaweza wakawa. -
6:15 - 6:16Asanteni
-
6:16 - 6:18(Makofi)
- Title:
- Jinsi ukweli halisi unawabadilisha wanafunzi kuwa wanasayansi
- Speaker:
- Jessica Ochoa Hendrix
- Description:
-
Kwa kutumia ukweli halisi wa bei ya chini, mwanaharakati wa elimu Jessica Ochoa Hendrix amesaidia kuleta sayansi katika shule kote Amerika. Katika mazungumzo haya ya haraka, anaelezea jinsi uzoefu wa VR alivyokua unawaalika wanafunzi kuchunguza mazingira ya chini ya maji kana kwamba ni biolojia ya baharini - na kujiona katika kazi zingine ambazo labda hawangefikiria.
- Video Language:
- English
- Team:
closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 06:34
![]() |
Joachim Mangilima approved Swahili subtitles for How virtual reality turns students into scientists | |
![]() |
Joachim Mangilima accepted Swahili subtitles for How virtual reality turns students into scientists | |
![]() |
Joachim Mangilima edited Swahili subtitles for How virtual reality turns students into scientists | |
![]() |
Sundie Murugi edited Swahili subtitles for How virtual reality turns students into scientists | |
![]() |
Sundie Murugi edited Swahili subtitles for How virtual reality turns students into scientists |