[Script Info] Title: [Events] Format: Layer, Start, End, Style, Name, MarginL, MarginR, MarginV, Effect, Text Dialogue: 0,0:00:00.72,0:00:02.43,Default,,0000,0000,0000,,kwa jinsi gani uligundua shauku yako Dialogue: 0,0:00:02.43,0:00:03.53,Default,,0000,0000,0000,,ama kupata kazi yako? Dialogue: 0,0:00:03.72,0:00:04.93,Default,,0000,0000,0000,,Je, ulikutana nayo? Dialogue: 0,0:00:04.100,0:00:06.53,Default,,0000,0000,0000,,ama ilikua ni kufanya majaribio na kukosea? Dialogue: 0,0:00:06.86,0:00:09.98,Default,,0000,0000,0000,,Kama mtetezi wa haki za watoto,\NMarian Wright Edelman alisema, Dialogue: 0,0:00:10.57,0:00:13.08,Default,,0000,0000,0000,,¨Hauwezi ukawa usichokiona.¨ Dialogue: 0,0:00:13.57,0:00:15.79,Default,,0000,0000,0000,,Kwa bahati nzuri, sasa tunaishi katika\Nwakati Dialogue: 0,0:00:15.81,0:00:19.53,Default,,0000,0000,0000,,ambao teknolojia zinazojitokeza zaweza\Nkutusaidia kusuluhisha tatizo hili Dialogue: 0,0:00:19.53,0:00:21.19,Default,,0000,0000,0000,,Kwa miaka miwili iliyopita Dialogue: 0,0:00:21.19,0:00:23.57,Default,,0000,0000,0000,,nimekua nikikuza mpango wa ukweli\Nuliopanuliwa Dialogue: 0,0:00:23.57,0:00:27.10,Default,,0000,0000,0000,,unaowezesha wanafunzi wa shule za kati,\Nkutoka nchi nzima Dialogue: 0,0:00:27.10,0:00:30.08,Default,,0000,0000,0000,,kuchukua jukumu la mwanasaikolojia wa\Nbaharini Dialogue: 0,0:00:30.08,0:00:32.07,Default,,0000,0000,0000,,hata kama hawajawahi kuona bahari Dialogue: 0,0:00:33.43,0:00:36.08,Default,,0000,0000,0000,,kama mwanafunzi mmoja wa darasa la saba ambaye hivi\Nkaribuni amekamilisha programu yetu Dialogue: 0,0:00:36.08,0:00:38.100,Default,,0000,0000,0000,,alisema, ¨Niliweza kujiona ni\Nmwanasayansi, Dialogue: 0,0:00:38.100,0:00:40.83,Default,,0000,0000,0000,,kwa sababu nilifurahia mchezo huu.¨ Dialogue: 0,0:00:41.41,0:00:43.41,Default,,0000,0000,0000,,Maoni haya yalinisisimua sana Dialogue: 0,0:00:43.41,0:00:46.78,Default,,0000,0000,0000,,kwa sababu wanafunzi wachache sana hujiona\Nkama wanasayansi Dialogue: 0,0:00:47.45,0:00:53.12,Default,,0000,0000,0000,,Utafiti wa 2014 ulionyesha kuwa asilimia 57\Nya wanafunzi wa darasa la nane na tisa Dialogue: 0,0:00:53.12,0:00:55.28,Default,,0000,0000,0000,,walisema, ¨Sipendi sayansi¨ Dialogue: 0,0:00:55.76,0:00:58.17,Default,,0000,0000,0000,,Vivyo hivyo, pia katika 2014, Dialogue: 0,0:00:58.17,0:01:01.08,Default,,0000,0000,0000,,Nilikutana naye Mandë Holford,\Nmtaalamu wa kemia ya baharini Dialogue: 0,0:01:01.08,0:01:03.68,Default,,0000,0000,0000,,na Lindsay Portnoy, mwanasaikolojia wa\Nelimu. Dialogue: 0,0:01:04.56,0:01:06.66,Default,,0000,0000,0000,,Sote watatu tulishirikiana shauku Dialogue: 0,0:01:06.66,0:01:10.27,Default,,0000,0000,0000,,ya kuwafanya wanafunzi wavutiwe, na wawe\Nna starehe katika sayansi. Dialogue: 0,0:01:10.75,0:01:13.42,Default,,0000,0000,0000,,Tulifikiria juu ya jinsi\Ntunaweza kuwapa watoto Dialogue: 0,0:01:13.42,0:01:16.42,Default,,0000,0000,0000,,uzoefu wa kweli zaidi katika taaluma ya\Nkisayansi Dialogue: 0,0:01:16.42,0:01:18.03,Default,,0000,0000,0000,,Tulijadili utafiti huo; Dialogue: 0,0:01:18.03,0:01:22.20,Default,,0000,0000,0000,,ulionyesha kuwa wanafunzi walihisi vizuri\Nkuwa na uthubutu wakati wa kucheza michezo. Dialogue: 0,0:01:22.70,0:01:26.17,Default,,0000,0000,0000,,Basi sote watatu tulianzisha kampuni ya\Nmichezo ya kielimu Dialogue: 0,0:01:26.17,0:01:28.20,Default,,0000,0000,0000,,kuipa sayansi uhai Dialogue: 0,0:01:28.83,0:01:33.07,Default,,0000,0000,0000,,Ukweli halisi ulionekana kama njia ya bei\Nya chini ya kuongeza ufikiaji Dialogue: 0,0:01:33.48,0:01:36.21,Default,,0000,0000,0000,,Juu ya hayo, utafiti wa kitaalam\Numeonyesha Dialogue: 0,0:01:36.21,0:01:39.97,Default,,0000,0000,0000,,ukweli halisi unaweza kusababisha\Nkuongezeka kwa utunzaji wa kujifunza. Dialogue: 0,0:01:39.97,0:01:42.85,Default,,0000,0000,0000,,Hii ilikuwa kamili kwetu,\Nkama tulivyotaka kuwa mashuleni Dialogue: 0,0:01:42.85,0:01:45.76,Default,,0000,0000,0000,,ili tuweze kufikia\Nidadi kubwa ya wanafunzi kadiri iwezekanavyo, Dialogue: 0,0:01:45.76,0:01:48.99,Default,,0000,0000,0000,,haswa wanafunzi ambao wana uwakilishi mdogo katika sayansi Dialogue: 0,0:01:49.30,0:01:52.39,Default,,0000,0000,0000,,Kwa hivyo, tukiwa na ufadhili kutoka Mfuko wa Sayansi wa Kitaifa, Dialogue: 0,0:01:52.39,0:01:55.44,Default,,0000,0000,0000,,tulianza kukuza mpango wetu wa ukweli\Nuliopanuliwa Dialogue: 0,0:01:55.44,0:01:57.37,Default,,0000,0000,0000,,ulioleta pamoja ukweli halisi Dialogue: 0,0:01:57.40,0:01:59.46,Default,,0000,0000,0000,,na jarida la kibinafsi la kidijitali Dialogue: 0,0:01:59.77,0:02:02.08,Default,,0000,0000,0000,,Tulifanya kazi na waalimu tulipokua\Ntukiuendeleza Dialogue: 0,0:02:02.08,0:02:05.19,Default,,0000,0000,0000,,kuhakikisha kuwa utafaa bila shida \Nndani ya mitaala iliyopo Dialogue: 0,0:02:05.93,0:02:09.87,Default,,0000,0000,0000,,na kuwawezesha waalimu kutumia teknolojia\Nya kisasa madarasani mwao. Dialogue: 0,0:02:10.47,0:02:12.94,Default,,0000,0000,0000,,Tulibuni ukweli halisi wa Kadi ya Google, Dialogue: 0,0:02:12.94,0:02:15.24,Default,,0000,0000,0000,,ambao unahitaji simu janja tu Dialogue: 0,0:02:15.24,0:02:19.22,Default,,0000,0000,0000,,na kitazamaji cha VR cha dola 10\Nkilichotengenezwa kwa kadibodi. Dialogue: 0,0:02:19.55,0:02:21.48,Default,,0000,0000,0000,,kwa hivi vifaa vya kichwa visivyo ghali, Dialogue: 0,0:02:21.48,0:02:24.70,Default,,0000,0000,0000,,wanafunzi husafirishwa katika msafara\Nchini ya maji. Dialogue: 0,0:02:25.19,0:02:27.07,Default,,0000,0000,0000,,Wanafunzi hutumia jarida lao la kidijitali Dialogue: 0,0:02:27.07,0:02:28.59,Default,,0000,0000,0000,,kuandika maelezo yao, Dialogue: 0,0:02:28.59,0:02:30.02,Default,,0000,0000,0000,,kujibu maswali, Dialogue: 0,0:02:30.02,0:02:31.58,Default,,0000,0000,0000,,kujenga mifano Dialogue: 0,0:02:31.58,0:02:32.88,Default,,0000,0000,0000,,na kukuza nadharia. Dialogue: 0,0:02:33.40,0:02:36.84,Default,,0000,0000,0000,,Wanafunzi basi huenda katika ulimwengu wa kweli kujaribu nadharia zao Dialogue: 0,0:02:36.84,0:02:38.59,Default,,0000,0000,0000,,ili waone ikiwa ni sahihi, Dialogue: 0,0:02:38.59,0:02:40.18,Default,,0000,0000,0000,,kadiri wanasayansi waendavyo katika\Nnyanja za utafiti Dialogue: 0,0:02:40.18,0:02:41.83,Default,,0000,0000,0000,,katika kazi zao. Dialogue: 0,0:02:42.81,0:02:44.82,Default,,0000,0000,0000,,Wanafunzi wanaporudi kwa jarida lao la\Nkidijitali, Dialogue: 0,0:02:44.82,0:02:47.06,Default,,0000,0000,0000,,hushiriki uchunguzi wao, madai, Dialogue: 0,0:02:47.06,0:02:48.92,Default,,0000,0000,0000,,hoja na ushahidi. Dialogue: 0,0:02:49.40,0:02:53.99,Default,,0000,0000,0000,,Majibu ya wanafunzi yaliyoandikwa na\Nmwingiliano wa kawaida Dialogue: 0,0:02:53.99,0:02:55.80,Default,,0000,0000,0000,,zote husasishwa moja kwa moja Dialogue: 0,0:02:55.80,0:02:57.92,Default,,0000,0000,0000,,kwenye dashibodi ya tathmini ya mwalimu, Dialogue: 0,0:02:57.92,0:03:00.33,Default,,0000,0000,0000,,ili walimu waweze kufuata maendeleo yao Dialogue: 0,0:03:00.33,0:03:02.90,Default,,0000,0000,0000,,na wawasaidie kama inavyohitajika. Dialogue: 0,0:03:02.90,0:03:04.91,Default,,0000,0000,0000,,Ili kukupa hisia nzuri, nitakuonyesha Dialogue: 0,0:03:04.91,0:03:07.04,Default,,0000,0000,0000,,kidogo ya yale wanafunzi huona. Dialogue: 0,0:03:07.79,0:03:10.43,Default,,0000,0000,0000,,Huu ndio ukweli halisi wanapokuwa chini ya\Nmaji Dialogue: 0,0:03:10.43,0:03:13.37,Default,,0000,0000,0000,,wakiangalia mimea na wanyama. Dialogue: 0,0:03:14.45,0:03:16.94,Default,,0000,0000,0000,,Hii ni jarida la kidijitali\Nambapo wanaunda mifano yao Dialogue: 0,0:03:16.94,0:03:20.30,Default,,0000,0000,0000,,kulingana na data hii ya kawaida kuonyesha\Nwanachotarajia kuona. Dialogue: 0,0:03:21.42,0:03:24.16,Default,,0000,0000,0000,,Hapa, wanaunga mkono hiyo na taarifa za\Nubora. Dialogue: 0,0:03:24.16,0:03:27.08,Default,,0000,0000,0000,,Na hii ndio dashibodi ya ualimu\Ninayoonyesha maendeleo Dialogue: 0,0:03:27.08,0:03:30.81,Default,,0000,0000,0000,,na inawezesha [waalimu] kuona majibu ya\Nwanafunzi wanapoendelea. Dialogue: 0,0:03:32.72,0:03:34.72,Default,,0000,0000,0000,,Tulipokua tunaunda BioDive, Dialogue: 0,0:03:34.72,0:03:36.95,Default,,0000,0000,0000,,tulitaka sana kuzingatia ufikiaji, Dialogue: 0,0:03:36.95,0:03:41.09,Default,,0000,0000,0000,,kwa hivyo tuliijenga kuhitaji simu moja tu\Nkwa kila wanafunzi wanne. Dialogue: 0,0:03:41.09,0:03:44.88,Default,,0000,0000,0000,,Tulijua pia jinsi kazi ya sayansi inavyoshirikisha, Dialogue: 0,0:03:44.88,0:03:47.42,Default,,0000,0000,0000,,kwa hivyo tuliunda uzoefu kutatuliwa tu Dialogue: 0,0:03:47.42,0:03:49.33,Default,,0000,0000,0000,,kupitia kushirikiana Dialogue: 0,0:03:49.33,0:03:53.22,Default,,0000,0000,0000,,kwani kila mwanafunzi ni mtaalam katika\Neneo tofauti la kijiografia. Dialogue: 0,0:03:53.59,0:03:56.89,Default,,0000,0000,0000,,Kwa kuzingatia kwamba akili za watoto hawa\Nbado inaendelea kukua, Dialogue: 0,0:03:56.89,0:04:00.85,Default,,0000,0000,0000,,tulipunguza kila uzoefu kudumu kiwango\Nkisichozidi dakika mbili. Dialogue: 0,0:04:00.85,0:04:05.30,Default,,0000,0000,0000,,Na mwishowe, kwa sababu tunajua umuhimu\Nwa kudhihirishwa mara kwa mara Dialogue: 0,0:04:05.30,0:04:06.87,Default,,0000,0000,0000,,ili kufahamu maarifa Dialogue: 0,0:04:06.87,0:04:10.57,Default,,0000,0000,0000,,tuliunda BioDive ifanyike zaidi ya vipindi\Nvya darasa tano. Dialogue: 0,0:04:11.52,0:04:14.99,Default,,0000,0000,0000,,Tulianza majaribio ya BioDive mnamo 2017 Dialogue: 0,0:04:14.99,0:04:17.83,Default,,0000,0000,0000,,katika shule 20 huko New York na New Jersey. Dialogue: 0,0:04:17.83,0:04:20.62,Default,,0000,0000,0000,,Tulitaka kuona wanafunzi walipokuwa\Nwakitumia teknolojia hii mpya. Dialogue: 0,0:04:21.47,0:04:23.91,Default,,0000,0000,0000,,Mnamo mwaka wa 2019, sasa, Dialogue: 0,0:04:23.91,0:04:27.61,Default,,0000,0000,0000,,tunafanya majaribio katika majimbo 26 kwa\Nsasa. Dialogue: 0,0:04:27.100,0:04:30.78,Default,,0000,0000,0000,,Tulichosikia kutoka kwa waalimu\Nambao wamefundisha kwa kutumia programu yetu: Dialogue: 0,0:04:30.78,0:04:34.49,Default,,0000,0000,0000,,"Ilikuwa njia nzuri ya kuonyesha mienendo ya bahari\Nbila anasa ya kuwa huko hasa Dialogue: 0,0:04:34.49,0:04:35.88,Default,,0000,0000,0000,,kwa kuwa tupo Ohio. " Dialogue: 0,0:04:35.88,0:04:36.89,Default,,0000,0000,0000,,(Kicheko) Dialogue: 0,0:04:36.89,0:04:38.40,Default,,0000,0000,0000,,"Ni ya kushangaza sana." Dialogue: 0,0:04:38.40,0:04:40.72,Default,,0000,0000,0000,,"Wanafunzi walishiriki kabisa." Dialogue: 0,0:04:41.05,0:04:44.33,Default,,0000,0000,0000,,Lakini kinachotupa tumaini ni tunachosikia\Nkutoka kwa wanafunzi Dialogue: 0,0:04:44.80,0:04:46.91,Default,,0000,0000,0000,,"Nilipenda jinsi ilivyoonekana kana kwamba\Nnilikuwa pale." Dialogue: 0,0:04:46.91,0:04:49.39,Default,,0000,0000,0000,,"Ina maingiliano na ni njia nzuri ya\Nkufurahia unapojifunza." Dialogue: 0,0:04:49.39,0:04:52.91,Default,,0000,0000,0000,,"Ilinipa mifano ya kweli ya jinsi viumbe\Nhawa wanavyoonekana. " Dialogue: 0,0:04:53.65,0:04:58.16,Default,,0000,0000,0000,,"Nilijiona kama mwanasayansi\Nkwa sababu inaonekana kufurahisha sana. " Dialogue: 0,0:04:58.77,0:05:01.27,Default,,0000,0000,0000,,Maoni yetu hayakuwa mazuri kila wakati. Dialogue: 0,0:05:01.74,0:05:03.50,Default,,0000,0000,0000,,Tulipoanza kukuza, Dialogue: 0,0:05:03.50,0:05:05.43,Default,,0000,0000,0000,,tulianza kwa kuwauliza wanafunzi Dialogue: 0,0:05:05.43,0:05:06.56,Default,,0000,0000,0000,,walichokipenda, Dialogue: 0,0:05:06.56,0:05:07.66,Default,,0000,0000,0000,,kile wasichokipenda Dialogue: 0,0:05:07.66,0:05:09.74,Default,,0000,0000,0000,,na kile walichokipata kinawachanganya. Dialogue: 0,0:05:09.74,0:05:13.32,Default,,0000,0000,0000,,Mwishowe tulianza kuuliza walichokua\Nnahamu ya kufanya. Dialogue: 0,0:05:13.91,0:05:17.47,Default,,0000,0000,0000,,Maoni yao yakatupa vitu halisi vya kujenga\Nndani Dialogue: 0,0:05:17.47,0:05:21.14,Default,,0000,0000,0000,,ili kuwa na uhakika kuwa tunajumuisha\Nsauti za wanafunzi katika tulichokibuni. Dialogue: 0,0:05:22.02,0:05:26.35,Default,,0000,0000,0000,,Kwa jumla, kile tumejifunza ni kwamba huu\Nni mwanzo wa jukwaa mpya Dialogue: 0,0:05:26.35,0:05:29.38,Default,,0000,0000,0000,,la kuwapa wanafunzi sauti na umiliki Dialogue: 0,0:05:29.38,0:05:31.70,Default,,0000,0000,0000,,katika kuamua jinsi wanataka kuwa na athari Dialogue: 0,0:05:31.70,0:05:33.16,Default,,0000,0000,0000,,katika kazi zao. Dialogue: 0,0:05:33.61,0:05:35.06,Default,,0000,0000,0000,,Tulilenga sayansi, Dialogue: 0,0:05:35.06,0:05:36.76,Default,,0000,0000,0000,,kwa sababu twafahamu kuwa twawahitaji wanasayansi Dialogue: 0,0:05:36.76,0:05:39.93,Default,,0000,0000,0000,,ili kutusaidia kutatua hali yetu ya sasa na\Nchangamoto za baadaye. Dialogue: 0,0:05:40.54,0:05:44.61,Default,,0000,0000,0000,,Lakini ukweli halisi unaweza kusaidia\Nwanafunzi katika eneo lolote. Dialogue: 0,0:05:44.61,0:05:49.22,Default,,0000,0000,0000,,Tunawezaje kuwasaidia wanafunzi katika\Nkutafuta tamaa zao zote Dialogue: 0,0:05:49.22,0:05:53.02,Default,,0000,0000,0000,,kwa uzoefu huu wa kufungua jicho na nafasi\Nza kujifunza kutoka kwa vyanzo vya msingi? Dialogue: 0,0:05:53.02,0:05:57.30,Default,,0000,0000,0000,,Tunaweza kuunda... VR za vifaa vya kichwa\Nvisivyo ghali Dialogue: 0,0:05:57.88,0:06:00.55,Default,,0000,0000,0000,,ambazo zinawaruhusu wazame katika fasihi\Nya mdomo Dialogue: 0,0:06:00.55,0:06:02.92,Default,,0000,0000,0000,,au katika wakati mgumu wa historia ya wanadamu? Dialogue: 0,0:06:03.25,0:06:07.20,Default,,0000,0000,0000,,Ukweli uliopanuliwa una uwezo\Nwakubadilisha mwelekeo Dialogue: 0,0:06:07.20,0:06:08.90,Default,,0000,0000,0000,,wa maisha ya watoto wetu Dialogue: 0,0:06:08.90,0:06:11.48,Default,,0000,0000,0000,,na uwaongoze kwenye kazi hawakuwahi\Nkufikiria Dialogue: 0,0:06:11.93,0:06:15.34,Default,,0000,0000,0000,,kwa kuwapa nafasi ya kuona ni nini\Nwanaweza wakawa. Dialogue: 0,0:06:15.34,0:06:16.25,Default,,0000,0000,0000,,Asanteni Dialogue: 0,0:06:16.25,0:06:17.51,Default,,0000,0000,0000,,(Makofi)