Swahili subtitles

← Chimamanda Adichie: Hatari ya simulizi moja

Get Embed Code
56 Languages

Showing Revision 23 created 09/22/2018 by Miriam Loivotoki Elisha.

 1. Mimi ni msimuliaji wa hadithi
 2. Ningependa kuwasimulia kidogo maisha yangu
 3. juu ya kile ninachopenda kuita
  "hatari ya simulizi moja"
 4. Nilikulia mazingira ya chuo
  kikuu magharibi mwa Nigeria
 5. Mama yangu anasema nilianza kusoma
  nikiwa na miaka miwili
 6. japo nadhani miaka minne ni sahihi zaidi
 7. Niliwahi sana kuanza kusoma
 8. Nilisoma vitabu vya watoto vya Uingereza
  na Marekani
 9. Pia nilianza kuandika katika umri mdogo

 10. Na nilipoanza kuandika,
  nikiwa na takriban miaka saba,
 11. hadithi za penseli na michoro ya rangi
 12. ambazo mama yangu alilazimika kuzisoma,
 13. niliandika hadithi
  sawa na zile nilizokuwa nazisoma:
 14. Wahusika wangu wote
  walikuwa wazungu na wenye macho ya bluu.
 15. Walicheza katika theluji.
 16. Walikula matofaa
 17. (Kicheko)

 18. Na walizungumza sana kuhusu hali ya hewa,

 19. jinsi ilivyo vizuri kuona jua limechomoza.
 20. (Kicheko)

 21. Yote haya,ingawa niliishi Nigeria.

 22. Nilikuwa sijawahi kwenda nje ya Nigeria.
 23. Hatukuwa na theluji, tulikula maembe.
 24. Na hatukuzungumza kuhusu hali ya hewa,
 25. sababu hakukuwa na haja ya kufanya hivyo.
 26. Wahusika wangu pia
  walikunywa sana bia ya tangawizi

 27. kwa sababu wahusika
  katika vitabu vya Uingereza
 28. walikunywa bia ya tangawizi.
 29. Ijapokuwa
  sikuifahamu bia ya tangawizi
 30. (Kicheko)

 31. Na kwa miaka mingi baadaye

 32. nilikuwa na shauku
  ya kuonja bia ya tangawizi.
 33. Lakini hiyo ni hadithi nyingine.
 34. Ambacho hii inaonyesha,nafikiri

 35. Ni namna tulivyo wajinga na wanyonge
 36. Tunapokabiliana na simulizi
 37. hasa hasa kama watoto
 38. Sababu nilisoma vitabu
  vyenye wahusika wa kigeni
 39. Nilikuwa nimeaminishwa kwamba vitabu
 40. kwa asili lazima
  viwe na wahusika wageni
 41. Na vielezo kuhusu mambo ambayo
  binafsi siyafahamu
 42. Mambo yalibadilika
  Nilipopata vitabu vya Afrika
 43. havikuwepo kwa wingi
 44. Na haikuwa rahisi kuvipata
  kama vya kigeni
 45. Lakini sababu ya waandishi
  kama Chinua Achebe na Camara Laye

 46. Nilipata badiliko la akili
  ninavyoiona fasihi
 47. Niligundua kwamba watu kama mimi,
 48. wasichana weusi
 49. wenye nywele ngumu
 50. pia wapo katika fasihi.
 51. Nilianza kuandika
  vitu nilivyovifahamu
 52. Nilikuwa navipenda hivyo vitabu
  vya Marekani na Uingereza

 53. Viliamsha fikra zangu
  Vilifunua vitu vipya.
 54. Lakini matokeo yasiyokusudiwa
 55. yalikuwa; sikufahamu kuwa
  watu kama mimi
 56. waweza kuwepo katika fasihi.
 57. hivyo ufumbuzi wa waandishi Waafrika:
 58. Uliniokoa na mtazamo mmoja
  juu ya vitabu
 59. Ninatoka kwenye familia
  ya kawaida

 60. Baba yangu alikuwa mhadhiri
 61. Mama yangu ni
  afisa wa utawala
 62. Kwa hiyo kama kawaida, tulikuwa na,
 63. mtumishi wa nyumbani
  anayetoka vijiji vya jirani
 64. Nilipokuwa na miaka nane
  tulipata mtumishi wa kiume
 65. Jina lake aliitwa Fide
 66. Mama alituambia kuwa familia
  yake ni masikini sana
 67. Mama alituma magimbi na mchele
  na nguo zetu za zamani kwa familia yao
 68. Na niliposhindwa kumaliza chakula
  mama alisema,
 69. "Maliza chakula! kuna watu
  ambao hawana chochote
 70. Niliwahurumia sana
  familia ya Fide
 71. Jumamosi moja tukaenda
  kijijini kwao kutembelea

 72. na mama yake akatuonyesha
  kikapu kizuri
 73. kilichosukwa kwa ukili uliopakwa rangi
  na kaka yake Fide
 74. Nilishangaa
 75. Sikudhani kuwa yeyote katika familia yake
 76. angeweza kutengeneza chochote
 77. yote niliyowahi kusikia kuhusu wao
  ni namna walivyo masikini
 78. Kwa hiyo ilikuwa haiwezekani kwangu
  kuwaona tofauti na umasikini wao
 79. umasikini wao ilikuwa
  ni simulizi moja kwangu
 80. baadaye niliwaza hili
  nilipotoka Nigeria

 81. Kwenda Marekani kusoma
  chuo kikuu
 82. Nilikuwa na miaka 19
 83. Mmarekani niliyekuwa
  naishi naye chumba kimoja alinishangaa
 84. Aliuliza wapi nimefunza
  kuzungumza kiingereza vizuri
 85. Alishangaa nilipomwambia kuwa Nigeria
 86. wanatumia kiingereza kama lugha ya taifa
 87. Aliomba kusikiliza "nyimbo za kikabila"
 88. na alipigwa butwaa vile vile
 89. Nilipompa kanda yangu ya Mariah Carey
 90. (kicheko)

 91. Alidhani kuwa sifahamu
  kutumia jiko la umeme

 92. Kilichonishangaza mimi ni hiki

 93. Alikuwa ananihurimia
  hata kabla ya kuniona
 94. Mtazamo wake mbovu,
  kunihusu, kama Mwafrika,
 95. Ulikuwa wa huruma ya kudhalilisha,
  yenye kujali
 96. Alikuwa na simulizi moja
  kuhusu Afrika:
 97. Simulizi ya majanga.
 98. Kwenye simulizi hii moja,
 99. Hakukuwa na uwezekano wa Mwafrika
  kufanana naye kwa namna yeyote,
 100. Hakukuwa na uwezekano wa hisia
  ngumu zaidi ya huruma,
 101. Hakukuwa na uwezekano wa ushirikiano
  kama binadamu walio sawa.
 102. Lazima niseme kuwa
  kabla ya kwenda Marekani,

 103. Sikuwa nikijitambua kwa undani
  kama Mwafrika.
 104. Lakini Marekani, popote Afrika ilipotajwa,
  watu walinigeukia.
 105. Bila kujali kuwa sifahamu chochote
  kuhusu nchi kama Namibia.
 106. Lakini nilikuja kuupokea
  huu utambulisho mpya,
 107. Na kwa namna nyingi sasa
  ninajitazama kama Mwafrika.
 108. Ijapokuwa bado ninakasirishwa sana
  pale Afrika inapoelezewa kama ni nchi
 109. Mfano wa karibu, ni safari yangu ya ndege
 110. Kutoka Lagos hivi juzi,
 111. Ambapo kulikuwa na tangazo
 112. Kuhusu kazi ya kujitolea kule
  "India, Afika na nchi nyingine"
 113. Kicheko

 114. Baada ya kuishi Marekani kama Mwafrica

 115. Nikaanza kuelewa mwitikio wa
  niliyekuwa naishi naye chumba kimoja
 116. kama sikukulia Nigeria
 117. Na kama kila nilichofahamu kuhusu Afrika
  kilitokana na picha maarufu
 118. Mimi pia ningedhani kuwa Africa ni mahali
  penye mandhari nzuri,
 119. Wanyama wa kupendeza,
 120. na watu wasioeleweka,
 121. wapiganao vita visivyo na maana,
  wanaokufa na umasikini na UKIMWI
 122. wasioweza kujisemea
 123. wanaosubiri kusaidiwa na
  mtu mweupe, mgeni mwenye ukarimu
 124. Ningewaona waafrika
  kwa namna ile ambayo mimi,
 125. nilipokuwa mtoto,
  niliiona familia ya Fide
 126. Hii simulizi moja kuhusu Afrika
  nadhani inatokana na fasihi za magharibi

 127. Sasa, huu ni msemo kutoka katika uandishi
  wa mfanyabiashara wa London aitwaye John Lok,
 128. aliyesafiri kwa maji kuelekea
  Afrika magharibi mwaka 1561
 129. na aliweka hazina ya kuvutia
  kutokana na safari yake.
 130. Baada ya kuwaita Waafrika weusi kama
  " hayawani wasio na nyumba,"
 131. aliandika,"Pia kuna watu wasio na vichwa,
 132. midomo na macho yao
  yapo katika vifua vyao."
 133. Sasa, nilicheka kila
  nikisoma haya maneno.

 134. Na lazima mtu
  atakubaliana na fikira za John Lok.
 135. Lakini kipi ni muhimu
  kuhusu uandishi wake
 136. ni kwamba inawakilisha mwanzo
 137. wa utamaduni wa kuelezea hadithi
  za Afrika kwa Magharibi:
 138. Utamaduni wa kusini mwa jangwa la Sahara
  kama sehemu isiyofaa,
 139. yenye utofauti, yenye kiza,
 140. ya watu ambao, kutokana na maneno ya
  mshairi bora aitwaye Rudyard Kipling,
 141. ni "nusu shetani, nusu watoto."
 142. Hivyo, nilianza kuelewa kwamba mwanafunzi
  Mmarekani ninayeshirikiana nae chumba

 143. lazima katika maisha yake
 144. atakuwa ameona na kusikia
  namna mbalimbali za hii hadithi moja,
 145. kama ilivyo kwa profesa,
 146. ambaye aliwahi niambia kuwa
  riwaya yangu haikuwa "na uhalisia wa Kiafrika,"
 147. Sasa, nilikubaliana na kuchanganua
 148. kwamba kulikuwa na baadhi ya vitu
  ambavyo si sawa katika riwaya hii,
 149. na kuwa nilifeli katika maeneo mbalimbali,
 150. lakini sikufiria kwamba ilifeli
 151. katika kutekeleza
  uhalisia wake wa Kiafrika.
 152. Kiukweli, sikufahamu
  uhalisia wa Kiafrika ni upi.
 153. Profesa alinielezza kwamba wahusika kwenye riwaya
  walikuwa wanafanana mno kama yeye,
 154. msomi aliye katika maisha ya kati.
 155. Wahusika wangu waliendesha magari.
 156. Hawakuwa wanashinda na njaa.
 157. Kwa hiyo hawakuwa Waafrika halisi.
 158. Lakini niongeze haraka-haraka
  kwamba najisikia hatia

 159. katika swali la la hadithi iliyo moja.
 160. Miaka michache iliyopita,
  nilitembelea Mexico nikitokea Marekani.
 161. Hali ya kisiasa nchini Marekani
  wakati huo ilikuwa tete,
 162. kulikuwa na majadiliano yanayoendelea
  kuhusu uhamiaji.
 163. Na, mara kwa mara hutokea Marekani,
 164. neno uhamiaji likaja kuwa
  linahusishwa na watu wenye asili ya Mexico.
 165. Kulikuwa na hadithi ndefu
  kuhusu Wamexico
 166. kama watu wanaonyonya mfumo wa afya,
 167. wanajipenyeza kwenye mipaka,
 168. wanakamatwa kwenye mipaka,
  vitu kama hivyo.
 169. Nakumbuka siku ya kwanza nilipokuwa natembea
  eneo liitwalo Guadalajara,

 170. nikiwaangalia watu wakielekea makazini,
 171. wakitengeneza tortilla maeneo ya sokoni,
 172. wakivuta sigara, wakicheka.
 173. Nakumbuka kwa mara ya kwanza
  nilipatwa na mshangao kidogo.
 174. Kisha, nikagubikwa na aibu.
 175. Nikatambua ya kwamba nimezama sana katika habari zinazoelezea watu wa Mexico
 176. ambao wamekuwa jambo katika akili yangu,
 177. wahamiaji duni,
 178. nilidanganyika katika hadithi moja
  ya watu wa Mexico
 179. na sikuweza kujisikia aibu zaidi.
 180. Kwa hiyo hiyo ndiyo
  namna ya kutengeneza hadithi moja.

 181. kuwaeleza watu kama jambo moja,
 182. kama jambo moja tu,
 183. tena na tena,
 184. na hivyo ndivyo watakavyokuwa.
 185. Haiwezekani kuongelea kuhusu hadithi moja

 186. bila kuongelea kuhusu uwezo ya mamlaka.
 187. Kuna neno, neno la lugha ya Igbo,
 188. ambalo huwa naliwaza kila nikifikiria
  mfumo wa mamlaka wa dunia,
 189. na hili "nkali".
 190. Ni nomino ambayo inatafsiriwa kama
  "kuwa juu zaidi ya mwigine."
 191. Kama ulivyo ulimwengu wa
  kiuchumi na kisiasa,
 192. hadithi pia huelezwa kwa kanuni ya nkali:
 193. Zinaelezwaje, nani anaelezea,
 194. wakati gani zilielezwa,
  hadithi ngapi zinaelezwa,
 195. haya yote yanategemea sana
  nguvu ya mamlaka.
 196. Mamlaka ni uwezo sio tu wa kueleza
  hadithi ya kuhusu mtu mwingine,

 197. lakini kuifanya iwe hadithi mahususi
  kuhusu mtu huyo.
 198. Mshairi wa Kipalestina
  Mourid Barghouti aliandika
 199. kwamba kama unataka kuwaondoa watu,
 200. njia rahisi ya kufanya hivyo
  ni kuelezea hadithi yao
 201. na kuanza na, "pili."
 202. Anza hadithi na mishale
  ya waliokuwa wakazi halisi wa Amerika,
 203. na sio baada ya kufika kwa Waingereza,
 204. na utakuwa na hadithi tofauti nyingine kabisa.
 205. Anza na hadithi kuhusu
  kuanguka kwa dola za Kiafrika,
 206. na sio dola za Kiafrika
  zilizotokana na ukoloni,
 207. na utakuwa na hadithi tofauti kabisa.
 208. Hivi karibun nilitoa hotuba katika chuo

 209. ambapo mwanafunzi aliniambia
  kwamba ilikuwa ni aibu
 210. kwamba wanaume wa Kinigeria
  walikuwa wanyanyasaji
 211. kama alivyo muhusika
  ambaye ni baba katika riwaya yangu.
 212. Nikamwambia nimesoma riwaya
  iitwayo "Mwendawazimu wa Kiamerika" --
 213. (Kicheko)

 214. -- na kwamba ilikuwa aibu

 215. kwamba vijana wadogo wa Kiamerika
  walikuwa wauaji waliokubuhu.
 216. (Kicheko)

 217. (Makofi)

 218. Sasa, kiukweli nilisema hili
  kutokana na kukerwa.

 219. (Kicheko)

 220. Lakini isingeweza kutokea kwangu kuwaza

 221. kwamba kwa sababu nimesoma riwaya
  ambayo muhusika ni muuaji wa kufululiza
 222. kwamba kwa kiasi fulani
  wanawakilisha Wamarekani wote.
 223. Hii si kwamba mimi
  ni mtu bora kuliko yule mwanafunzi,
 224. lakini kwa sababu ya utamaduni
  na nguvu ya uchumi wa Marekani,
 225. Nilikuwa nina hadithi nyingi za Marekani.
 226. Nilisoma Tyler na Updike
  na Steinbeck na Gaitskill.
 227. Sikuwa na hadithi moja ya Marekani.
 228. Nilipojifunza, miaka kadhaa iliyopita,

 229. kwamba waandishi wanategemewa kuwa na maisha ya utotoni ambayo siyo ya furaha
 230. ili kuja kufanikiwa baadaye,
 231. Nilianza kuwaza ni namna gani naweza buni
  vitu vibaya ambavyo wazazi wangu walinifanyia.
 232. (Kicheko)

 233. Lakini ukweli ni kwamba nilikuwa na maisha ya utoto ambayo yalikuwa ya furaha sana,

 234. yaliyojaa vicheko na upendo,
  katika familia iliyo na ukaribu sana.
 235. Lakini pia nilikuwa na mababu
  waliofia kwenye kambi za wakimbizi.

 236. Binamu yangu Polle alifariki
  sababu hakupata matibabu yanayostahili.
 237. Mmoja wa rafiki zangu,Okoloma,
  alifariki kwenye ajali ya ndege
 238. kwa sababu gari zetu za zimamoto
  hazikuwa na maji.
 239. Nimekulia katika serikali ya kijeshi
  ambayo ni kandamizi
 240. ambayo haikujali elimu,
 241. kwa muda mwingine,
  wazazi walikuwa hawalipwi mishahara.
 242. Hivyo, kama mtoto, nilianza kuona jamu hakuna mezani wakati wa kupata kifungua kinywa,
 243. kisha siagi nayo ikakosekana,
 244. kisha mkate ukawa ghali sana,
 245. kisha maziwa yakapungua.
 246. Na katika yote, hali ya hofu ya kisiasa
 247. ikaingilia maisha yetu,
 248. Na hadithi zote hizi zimenitengeneza mimi wa leo.

 249. Lakini kusisitiza katika hizi hadithi hasi
 250. ni kuongeza uzoefu wangu
 251. na kuachana na hadithi nyinginezo nyingi ambazo zimenitengeneza mimi.
 252. Hadithi moja hutengeneza tabaka,
 253. na tatizo la tabaka
  si kwamba hazina kweli,
 254. lakini hazijakamilika.
 255. Hufanya hadithi moja kuwa hadithi pekee.
 256. Hakika, Afrika ni bara
  ambalo limejaa majanga:

 257. Kuna majanga yaliyo makubwa,
  kama ubakaji wa kutisha nchini Congo
 258. na wa kudidimiza,
 259. kama ukweli kwamba watu 5000 wanaomba
  nafasi moja ya kazi nchini Nigeria.
 260. Lakini kuna hadithi nyingine
  ambazo hazihusiani na majanga,
 261. na ni muhimu sana, ni namna kuziongelea.
 262. Wakati wote nimekuwa nikihisi haiwezekani

 263. kujiunga kwa utaratibu na sehemu au mtu
 264. bila kuhusiana na hadithi zote
  za mahala pale au mtu huyo.
 265. Madhara ya hadithi moja ni kwamba:
 266. Hunyang'anya watu wa heshima.
 267. Hufanya utambuzi wetu
  wa usawa wa kibinadamu kuwa mgumu.
 268. Husisitiza ni jinsi gani tulivyo tofauti
  kuliko vile tulivyo sawa.
 269. Inakuwaje wakati
  kabla ya safari yangu ya Mexico,

 270. Ningefatilia majadiliano ya uhamiaji
  kutoka pande zote,
 271. upande wa Marekani na wa Mexico?
 272. Ingekuwaje kama mama yangu angeniambia
  familia ya Fide ilikuwa masikini
 273. na ya wachapakazi?
 274. Inakuwaje kama tungekuwa
  na mtandao wa televisheni wa Kiafrika
 275. ambao unarusha vipindi
  vya hadithi za Afrika duniani kote?
 276. Kitu ambacho muandishi wa Kinigeria Chinua Achebe
  anaita "usawa wa hadithi."
 277. Inakuweaje kama mwanafunzi niliyeishi naye chumba kimoja angefahamu kuhusu mchapishaji wangu wa Kinigeria,

 278. Muhtar Bakare,
 279. mtu wa kipekee ambaye
  aliacha kazi ya benki
 280. na kufuata ndoto zake
  na kuanzisha nyumba ya uchapishaji
 281. Sasa, hekima iliyozoeleka ilikuwa kwamba
  Wanigeria huwa hawasomi fasihi.
 282. Yeye alikataa.
 283. Alihisi kwamba watu
  ambao wanaweza kusoma, wangesoma,
 284. kama ungefanya kazi ya fasihi iwe katika bei nafuu na kupatikana kiurahisi.
 285. Muda mfupi baada ya kuchapisha
  riwaya yangu ya kwanza,

 286. Nilikwenda kwenye kituo cha televisheni
  kilichopo Lagos kwa ajili ya mahojiano,
 287. na mwanamke ambaye anafanya kazi pale kama karani alinifata na kusema,
 288. "Nimependa sana riwaya yako.
  Sijapenda mwishoni mwake.
 289. Sasa, ni lazima uandike muendelezo
  na hiki ndicho kitatokea ..."
 290. (Kicheko)

 291. Na alipoendelea kunielezea
  kipi cha kuandika kwenye muendelezo.

 292. Si kwamba nilivutiwa tu,
  lakini pia nilisisimka.
 293. Huyu ni mwanamke, mmoja wa watu wengi
  wa kawaida waliopo Nigeria,
 294. ambao hawakutakiwa kuwa wasomaji.
 295. Si kwamba alisoma tu kitabu,
 296. lakini pia alikimiliki
 297. na aliona ana haki kuaniambia
  kitu cha kuandika katika muendelezo.
 298. Sasa, ingekuwaje kama mwanafunzi niishiye nae chumba kimoja angejua kuhusu rafiki yangu Funmi Lyanda,

 299. mwanamke jasiri ambaye anaongoza
  kipindi cha televisheni Lagos,
 300. na anadhamiria kuelezea hadithi
  ambazo tunapendelea kuzisahau?
 301. Inakuwaje kama mwenzangu
  angetambua kuhusu upasuaji wa moyo
 302. ambao ulifanyika wiki iliyopita
  jijini Lagos?
 303. Inakuwaje angefahamu
  kuhusu muziki wa kisasa kwa Kinigeria,
 304. watu wenye vipaji wanaoimba
  katika lugha za Kiingereza na pijini,
 305. na Kiigbo na Kiyoruba na Kiijo,
 306. wakichanganya ushawishi
  kutoka kwa Jay Z hadi kwa Fela
 307. kwenda kwa Bob Marley na babu zao.
 308. Inakuwaje kama angejua
  kuhusu wakili mwanamke

 309. ambaye hivi karibuni alienda mahakamani nchini Nigeria kuipa changamoto sheria isiyo na maana
 310. ambayo inawataka wanawake
  kupewa ruhusa na waume zao
 311. kabla ya kutengeneza hati mpya ya kusafiria?
 312. Inakuwaje kama angefahamu kuhusu Nollywood,
 313. iliyojawa na watu wabunifu wanaotengeneza filamu ingawaje kuna changamoto nyingi za kiufundi,
 314. filamu ambazo ni maarufu sana
 315. ambazo ni mfano mzuri unaoonyesha Wanigeria wanatumia kile wanachotengeneza?
 316. Inakuwaje kama angefahamu
  kuhusu msusi wangu bora kabisa,
 317. ambaye ameanza biashara yake mwenyewe
  akiuza nywele za kuongezea?
 318. Au kuhusu mamilioni ya Wanigeria wengine ambao huanza biashara na muda mwingine kuanguka,
 319. lakini huendelea kukuza azma yao?
 320. Muda wote nikiwa nyumbani hukutana

 321. na vyanzo vya kila wakati vya kukwaza
  kwa Wanigeria wengi:
 322. miundombinu yetu mibovu,
  serikali iliyoanguka,
 323. lakini pia kwa ustahimilivu mkubwa
 324. wa watu ambao hufanikiwa,
  bila ya kutegemea serikali,
 325. bila yenyewe kabisa.
 326. Huwa natoa mafunzo ya uandishi
  kila kipindi cha joto jijini Lagos,
 327. na huwa inanishangaza
  kwa namna gani watu wengi hujiunga,
 328. namna ambavyo watu wengi wana shauku ya kuandika,
 329. ili kueleza hadithi.
 330. Mimi na mchapishaji wa kitabu changu
  tumeanzisha taasisi isiyo ya kibiashara

 331. inayofahamika kama Farafina Trust,
 332. na tuna ndoto kubwa ya kujenga maktaba
 333. na kukarabati maktaba ambazo tayari zipo
 334. na kutoa vitabu kwa shule za majimboni
 335. ambazo hazina vitabu katika maktaba zao,
 336. na kuandaa mafunzo mengi mno,
 337. katika kuandika na kusoma,
 338. kwa watu wote ambao wana shauku
  ya kuelezea hadithi zetu nyingi.
 339. Hadithi zina maana.

 340. Hadithi nyingi zina maana.
 341. Haidithi zimekuwa
  zikitumika kupokonya na kukejeli,
 342. lakini hadithi zinaweza tumika
  kuhamasisha na kuleta ubinadamu.
 343. Hadithi zinaweza kuvunja heshima ya watu,
 344. lakini hadithi zinaweza
  kurudisha heshima iliyopotea.
 345. Mwandishi wa Kimarekani
  Alice Walker aliandika

 346. kuhusu ndugu zake wanaotokea Kusini
  ambao walihamia Kaskazini.
 347. Aliwaonyesha kitabu kuhusu
 348. maisha ya Kusini ambayo wameyaacha nyuma.
 349. "Walikaa, na wakakisoma kitabu,
 350. nisikilize mimi soma kitabu,
  na raha ya dunia utaipata tena."
 351. Ningependelea kumalizia na hili wazo:

 352. Kwamba pale tunapokataa hadithi moja,
 353. tunapogundua kwamba hakuna hadithi moja
 354. kuhusu sehemu yoyote,
 355. huwa tunarejesha Furaha.
 356. Asante.

 357. (Makofi)