Mimi ni msimuliaji wa hadithi Ningependa kuwasimulia kidogo maisha yangu juu ya kile ninachopenda kuita "hatari ya simulizi moja" Nilikulia mazingira ya chuo kikuu magharibi mwa Nigeria Mama yangu anasema nilianza kusoma nikiwa na miaka miwili japo nadhani miaka minne ni sahihi zaidi Niliwahi sana kuanza kusoma Nilisoma vitabu vya watoto vya Uingereza na Marekani Pia nilianza kuandika katika umri mdogo Na nilipoanza kuandika, nikiwa na takriban miaka saba, hadithi za penseli na michoro ya rangi ambazo mama yangu alilazimika kuzisoma, niliandika hadithi sawa na zile nilizokuwa nazisoma: Wahusika wangu wote walikuwa wazungu na wenye macho ya bluu. Walicheza katika theluji. Walikula matofaa (Kicheko) Na walizungumza sana kuhusu hali ya hewa, jinsi ilivyo vizuri kuona jua limechomoza. (Kicheko) Yote haya,ingawa niliishi Nigeria. Nilikuwa sijawahi kwenda nje ya Nigeria. Hatukuwa na theluji, tulikula maembe. Na hatukuzungumza kuhusu hali ya hewa, sababu hakukuwa na haja ya kufanya hivyo. Wahusika wangu pia walikunywa sana bia ya tangawizi kwa sababu wahusika katika vitabu vya Uingereza walikunywa bia ya tangawizi. Ijapokuwa sikuifahamu bia ya tangawizi (Kicheko) Na kwa miaka mingi baadaye nilikuwa na shauku ya kuonja bia ya tangawizi. Lakini hiyo ni hadithi nyingine. Ambacho hii inaonyesha,nafikiri Ni namna tulivyo wajinga na wanyonge Tunapokabiliana na simulizi hasa hasa kama watoto Sababu nilisoma vitabu vyenye wahusika wa kigeni Nilikuwa nimeaminishwa kwamba vitabu kwa asili lazima viwe na wahusika wageni Na vielezo kuhusu mambo ambayo binafsi siyafahamu Mambo yalibadilika Nilipopata vitabu vya Afrika havikuwepo kwa wingi Na haikuwa rahisi kuvipata kama vya kigeni Lakini sababu ya waandishi kama Chinua Achebe na Camara Laye Nilipata badiliko la akili ninavyoiona fasihi Niligundua kwamba watu kama mimi, wasichana weusi wenye nywele ngumu pia wapo katika fasihi. Nilianza kuandika vitu nilivyovifahamu Nilikuwa navipenda hivyo vitabu vya Marekani na Uingereza Viliamsha fikra zangu Vilifunua vitu vipya. Lakini matokeo yasiyokusudiwa yalikuwa; sikufahamu kuwa watu kama mimi waweza kuwepo katika fasihi. hivyo ufumbuzi wa waandishi Waafrika: Uliniokoa na mtazamo mmoja juu ya vitabu Ninatoka kwenye familia ya kawaida Baba yangu alikuwa mhadhiri Mama yangu ni afisa wa utawala Kwa hiyo kama kawaida, tulikuwa na, mtumishi wa nyumbani anayetoka vijiji vya jirani Nilipokuwa na miaka nane tulipata mtumishi wa kiume Jina lake aliitwa Fide Mama alituambia kuwa familia yake ni masikini sana Mama alituma magimbi na mchele na nguo zetu za zamani kwa familia yao Na niliposhindwa kumaliza chakula mama alisema, "Maliza chakula! kuna watu ambao hawana chochote Niliwahurumia sana familia ya Fide Jumamosi moja tukaenda kijijini kwao kutembelea na mama yake akatuonyesha kikapu kizuri kilichosukwa kwa ukili uliopakwa rangi na kaka yake Fide Nilishangaa Sikudhani kuwa yeyote katika familia yake angeweza kutengeneza chochote yote niliyowahi kusikia kuhusu wao ni namna walivyo masikini Kwa hiyo ilikuwa haiwezekani kwangu kuwaona tofauti na umasikini wao umasikini wao ilikuwa ni simulizi moja kwangu baadaye niliwaza hili nilipotoka Nigeria Kwenda Marekani kusoma chuo kikuu Nilikuwa na miaka 19 Mmarekani niliyekuwa naishi naye chumba kimoja alinishangaa Aliuliza wapi nimefunza kuzungumza kiingereza vizuri Alishangaa nilipomwambia kuwa Nigeria wanatumia kiingereza kama lugha ya taifa Aliomba kusikiliza "nyimbo za kikabila" na alipigwa butwaa vile vile Nilipompa kanda yangu ya Mariah Carey (kicheko) Alidhani kuwa sifahamu kutumia jiko la umeme Kilichonishangaza mimi ni hiki Alikuwa ananihurimia hata kabla ya kuniona Mtazamo wake mbovu, kunihusu, kama Mwafrika, Ulikuwa wa huruma ya kudhalilisha, yenye kujali Alikuwa na simulizi moja kuhusu Afrika: Simulizi ya majanga. Kwenye simulizi hii moja, Hakukuwa na uwezekano wa Mwafrika kufanana naye kwa namna yeyote, Hakukuwa na uwezekano wa hisia ngumu zaidi ya huruma, Hakukuwa na uwezekano wa ushirikiano kama binadamu walio sawa. Lazima niseme kuwa kabla ya kwenda Marekani, Sikuwa nikijitambua kwa undani kama Mwafrika. Lakini Marekani, popote Afrika ilipotajwa, watu walinigeukia. Bila kujali kuwa sifahamu chochote kuhusu nchi kama Namibia. Lakini nilikuja kuupokea huu utambulisho mpya, Na kwa namna nyingi sasa ninajitazama kama Mwafrika. Ijapokuwa bado ninakasirishwa sana pale Afrika inapoelezewa kama ni nchi Mfano wa karibu, ni safari yangu ya ndege Kutoka Lagos hivi juzi, Ambapo kulikuwa na tangazo Kuhusu kazi ya kujitolea kule "India, Afika na nchi nyingine" Kicheko Baada ya kuishi Marekani kama Mwafrica Nikaanza kuelewa mwitikio wa niliyekuwa naishi naye chumba kimoja kama sikukulia Nigeria Na kama kila nilichofahamu kuhusu Afrika kilitokana na picha maarufu Mimi pia ningedhani kuwa Africa ni mahali penye mandhari nzuri, Wanyama wa kupendeza, na watu wasioeleweka, wapiganao vita visivyo na maana, wanaokufa na umasikini na UKIMWI wasioweza kujisemea wanaosubiri kusaidiwa na mtu mweupe, mgeni mwenye ukarimu Ningewaona waafrika kwa namna ile ambayo mimi, nilipokuwa mtoto, niliiona familia ya Fide Hii simulizi moja kuhusu Afrika nadhani inatokana na fasihi za magharibi Sasa, huu ni msemo kutoka katika uandishi wa mfanyabiashara wa London aitwaye John Lok, aliyesafiri kwa maji kuelekea Afrika magharibi mwaka 1561 na aliweka hazina ya kuvutia kutokana na safari yake. Baada ya kuwaita Waafrika weusi kama " hayawani wasio na nyumba," aliandika,"Pia kuna watu wasio na vichwa, midomo na macho yao yapo katika vifua vyao." Sasa, nilicheka kila nikisoma haya maneno. Na lazima mtu atakubaliana na fikira za John Lok. Lakini kipi ni muhimu kuhusu uandishi wake ni kwamba inawakilisha mwanzo wa utamaduni wa kuelezea hadithi za Afrika kwa Magharibi: Utamaduni wa kusini mwa jangwa la Sahara kama sehemu isiyofaa, yenye utofauti, yenye kiza, ya watu ambao, kutokana na maneno ya mshairi bora aitwaye Rudyard Kipling, ni "nusu shetani, nusu watoto." Hivyo, nilianza kuelewa kwamba mwanafunzi Mmarekani ninayeshirikiana nae chumba lazima katika maisha yake atakuwa ameona na kusikia namna mbalimbali za hii hadithi moja, kama ilivyo kwa profesa, ambaye aliwahi niambia kuwa riwaya yangu haikuwa "na uhalisia wa Kiafrika," Sasa, nilikubaliana na kuchanganua kwamba kulikuwa na baadhi ya vitu ambavyo si sawa katika riwaya hii, na kuwa nilifeli katika maeneo mbalimbali, lakini sikufiria kwamba ilifeli katika kutekeleza uhalisia wake wa Kiafrika. Kiukweli, sikufahamu uhalisia wa Kiafrika ni upi. Profesa alinielezza kwamba wahusika kwenye riwaya walikuwa wanafanana mno kama yeye, msomi aliye katika maisha ya kati. Wahusika wangu waliendesha magari. Hawakuwa wanashinda na njaa. Kwa hiyo hawakuwa Waafrika halisi. Lakini niongeze haraka-haraka kwamba najisikia hatia katika swali la la hadithi iliyo moja. Miaka michache iliyopita, nilitembelea Mexico nikitokea Marekani. Hali ya kisiasa nchini Marekani wakati huo ilikuwa tete, kulikuwa na majadiliano yanayoendelea kuhusu uhamiaji. Na, mara kwa mara hutokea Marekani, neno uhamiaji likaja kuwa linahusishwa na watu wenye asili ya Mexico. Kulikuwa na hadithi ndefu kuhusu Wamexico kama watu wanaonyonya mfumo wa afya, wanajipenyeza kwenye mipaka, wanakamatwa kwenye mipaka, vitu kama hivyo. Nakumbuka siku ya kwanza nilipokuwa natembea eneo liitwalo Guadalajara, nikiwaangalia watu wakielekea makazini, wakitengeneza tortilla maeneo ya sokoni, wakivuta sigara, wakicheka. Nakumbuka kwa mara ya kwanza nilipatwa na mshangao kidogo. Kisha, nikagubikwa na aibu. Nikatambua ya kwamba nimezama sana katika habari zinazoelezea watu wa Mexico ambao wamekuwa jambo katika akili yangu, wahamiaji duni, nilidanganyika katika hadithi moja ya watu wa Mexico na sikuweza kujisikia aibu zaidi. Kwa hiyo hiyo ndiyo namna ya kutengeneza hadithi moja. kuwaeleza watu kama jambo moja, kama jambo moja tu, tena na tena, na hivyo ndivyo watakavyokuwa. Haiwezekani kuongelea kuhusu hadithi moja bila kuongelea kuhusu uwezo ya mamlaka. Kuna neno, neno la lugha ya Igbo, ambalo huwa naliwaza kila nikifikiria mfumo wa mamlaka wa dunia, na hili "nkali". Ni nomino ambayo inatafsiriwa kama "kuwa juu zaidi ya mwigine." Kama ulivyo ulimwengu wa kiuchumi na kisiasa, hadithi pia huelezwa kwa kanuni ya nkali: Zinaelezwaje, nani anaelezea, wakati gani zilielezwa, hadithi ngapi zinaelezwa, haya yote yanategemea sana nguvu ya mamlaka. Mamlaka ni uwezo sio tu wa kueleza hadithi ya kuhusu mtu mwingine, lakini kuifanya iwe hadithi mahususi kuhusu mtu huyo. Mshairi wa Kipalestina Mourid Barghouti aliandika kwamba kama unataka kuwaondoa watu, njia rahisi ya kufanya hivyo ni kuelezea hadithi yao na kuanza na, "pili." Anza hadithi na mishale ya waliokuwa wakazi halisi wa Amerika, na sio baada ya kufika kwa Waingereza, na utakuwa na hadithi tofauti nyingine kabisa. Anza na hadithi kuhusu kuanguka kwa dola za Kiafrika, na sio dola za Kiafrika zilizotokana na ukoloni, na utakuwa na hadithi tofauti kabisa. Hivi karibun nilitoa hotuba katika chuo ambapo mwanafunzi aliniambia kwamba ilikuwa ni aibu kwamba wanaume wa Kinigeria walikuwa wanyanyasaji kama alivyo muhusika ambaye ni baba katika riwaya yangu. Nikamwambia nimesoma riwaya iitwayo "Mwendawazimu wa Kiamerika" -- (Kicheko) -- na kwamba ilikuwa aibu kwamba vijana wadogo wa Kiamerika walikuwa wauaji waliokubuhu. (Kicheko) (Makofi) Sasa, kiukweli nilisema hili kutokana na kukerwa. (Kicheko) Lakini isingeweza kutokea kwangu kuwaza kwamba kwa sababu nimesoma riwaya ambayo muhusika ni muuaji wa kufululiza kwamba kwa kiasi fulani wanawakilisha Wamarekani wote. Hii si kwamba mimi ni mtu bora kuliko yule mwanafunzi, lakini kwa sababu ya utamaduni na nguvu ya uchumi wa Marekani, Nilikuwa nina hadithi nyingi za Marekani. Nilisoma Tyler na Updike na Steinbeck na Gaitskill. Sikuwa na hadithi moja ya Marekani. Nilipojifunza, miaka kadhaa iliyopita, kwamba waandishi wanategemewa kuwa na maisha ya utotoni ambayo siyo ya furaha ili kuja kufanikiwa baadaye, Nilianza kuwaza ni namna gani naweza buni vitu vibaya ambavyo wazazi wangu walinifanyia. (Kicheko) Lakini ukweli ni kwamba nilikuwa na maisha ya utoto ambayo yalikuwa ya furaha sana, yaliyojaa vicheko na upendo, katika familia iliyo na ukaribu sana. Lakini pia nilikuwa na mababu waliofia kwenye kambi za wakimbizi. Binamu yangu Polle alifariki sababu hakupata matibabu yanayostahili. Mmoja wa rafiki zangu,Okoloma, alifariki kwenye ajali ya ndege kwa sababu gari zetu za zimamoto hazikuwa na maji. Nimekulia katika serikali ya kijeshi ambayo ni kandamizi ambayo haikujali elimu, kwa muda mwingine, wazazi walikuwa hawalipwi mishahara. Hivyo, kama mtoto, nilianza kuona jamu hakuna mezani wakati wa kupata kifungua kinywa, kisha siagi nayo ikakosekana, kisha mkate ukawa ghali sana, kisha maziwa yakapungua. Na katika yote, hali ya hofu ya kisiasa ikaingilia maisha yetu, Na hadithi zote hizi zimenitengeneza mimi wa leo. Lakini kusisitiza katika hizi hadithi hasi ni kuongeza uzoefu wangu na kuachana na hadithi nyinginezo nyingi ambazo zimenitengeneza mimi. Hadithi moja hutengeneza tabaka, na tatizo la tabaka si kwamba hazina kweli, lakini hazijakamilika. Hufanya hadithi moja kuwa hadithi pekee. Hakika, Afrika ni bara ambalo limejaa majanga: Kuna majanga yaliyo makubwa, kama ubakaji wa kutisha nchini Congo na wa kudidimiza, kama ukweli kwamba watu 5000 wanaomba nafasi moja ya kazi nchini Nigeria. Lakini kuna hadithi nyingine ambazo hazihusiani na majanga, na ni muhimu sana, ni namna kuziongelea. Wakati wote nimekuwa nikihisi haiwezekani kujiunga kwa utaratibu na sehemu au mtu bila kuhusiana na hadithi zote za mahala pale au mtu huyo. Madhara ya hadithi moja ni kwamba: Hunyang'anya watu wa heshima. Hufanya utambuzi wetu wa usawa wa kibinadamu kuwa mgumu. Husisitiza ni jinsi gani tulivyo tofauti kuliko vile tulivyo sawa. Inakuwaje wakati kabla ya safari yangu ya Mexico, Ningefatilia majadiliano ya uhamiaji kutoka pande zote, upande wa Marekani na wa Mexico? Ingekuwaje kama mama yangu angeniambia familia ya Fide ilikuwa masikini na ya wachapakazi? Inakuwaje kama tungekuwa na mtandao wa televisheni wa Kiafrika ambao unarusha vipindi vya hadithi za Afrika duniani kote? Kitu ambacho muandishi wa Kinigeria Chinua Achebe anaita "usawa wa hadithi." Inakuweaje kama mwanafunzi niliyeishi naye chumba kimoja angefahamu kuhusu mchapishaji wangu wa Kinigeria, Muhtar Bakare, mtu wa kipekee ambaye aliacha kazi ya benki na kufuata ndoto zake na kuanzisha nyumba ya uchapishaji Sasa, hekima iliyozoeleka ilikuwa kwamba Wanigeria huwa hawasomi fasihi. Yeye alikataa. Alihisi kwamba watu ambao wanaweza kusoma, wangesoma, kama ungefanya kazi ya fasihi iwe katika bei nafuu na kupatikana kiurahisi. Muda mfupi baada ya kuchapisha riwaya yangu ya kwanza, Nilikwenda kwenye kituo cha televisheni kilichopo Lagos kwa ajili ya mahojiano, na mwanamke ambaye anafanya kazi pale kama karani alinifata na kusema, "Nimependa sana riwaya yako. Sijapenda mwishoni mwake. Sasa, ni lazima uandike muendelezo na hiki ndicho kitatokea ..." (Kicheko) Na alipoendelea kunielezea kipi cha kuandika kwenye muendelezo. Si kwamba nilivutiwa tu, lakini pia nilisisimka. Huyu ni mwanamke, mmoja wa watu wengi wa kawaida waliopo Nigeria, ambao hawakutakiwa kuwa wasomaji. Si kwamba alisoma tu kitabu, lakini pia alikimiliki na aliona ana haki kuaniambia kitu cha kuandika katika muendelezo. Sasa, ingekuwaje kama mwanafunzi niishiye nae chumba kimoja angejua kuhusu rafiki yangu Funmi Lyanda, mwanamke jasiri ambaye anaongoza kipindi cha televisheni Lagos, na anadhamiria kuelezea hadithi ambazo tunapendelea kuzisahau? Inakuwaje kama mwenzangu angetambua kuhusu upasuaji wa moyo ambao ulifanyika wiki iliyopita jijini Lagos? Inakuwaje angefahamu kuhusu muziki wa kisasa kwa Kinigeria, watu wenye vipaji wanaoimba katika lugha za Kiingereza na pijini, na Kiigbo na Kiyoruba na Kiijo, wakichanganya ushawishi kutoka kwa Jay Z hadi kwa Fela kwenda kwa Bob Marley na babu zao. Inakuwaje kama angejua kuhusu wakili mwanamke ambaye hivi karibuni alienda mahakamani nchini Nigeria kuipa changamoto sheria isiyo na maana ambayo inawataka wanawake kupewa ruhusa na waume zao kabla ya kutengeneza hati mpya ya kusafiria? Inakuwaje kama angefahamu kuhusu Nollywood, iliyojawa na watu wabunifu wanaotengeneza filamu ingawaje kuna changamoto nyingi za kiufundi, filamu ambazo ni maarufu sana ambazo ni mfano mzuri unaoonyesha Wanigeria wanatumia kile wanachotengeneza? Inakuwaje kama angefahamu kuhusu msusi wangu bora kabisa, ambaye ameanza biashara yake mwenyewe akiuza nywele za kuongezea? Au kuhusu mamilioni ya Wanigeria wengine ambao huanza biashara na muda mwingine kuanguka, lakini huendelea kukuza azma yao? Muda wote nikiwa nyumbani hukutana na vyanzo vya kila wakati vya kukwaza kwa Wanigeria wengi: miundombinu yetu mibovu, serikali iliyoanguka, lakini pia kwa ustahimilivu mkubwa wa watu ambao hufanikiwa, bila ya kutegemea serikali, bila yenyewe kabisa. Huwa natoa mafunzo ya uandishi kila kipindi cha joto jijini Lagos, na huwa inanishangaza kwa namna gani watu wengi hujiunga, namna ambavyo watu wengi wana shauku ya kuandika, ili kueleza hadithi. Mimi na mchapishaji wa kitabu changu tumeanzisha taasisi isiyo ya kibiashara inayofahamika kama Farafina Trust, na tuna ndoto kubwa ya kujenga maktaba na kukarabati maktaba ambazo tayari zipo na kutoa vitabu kwa shule za majimboni ambazo hazina vitabu katika maktaba zao, na kuandaa mafunzo mengi mno, katika kuandika na kusoma, kwa watu wote ambao wana shauku ya kuelezea hadithi zetu nyingi. Hadithi zina maana. Hadithi nyingi zina maana. Haidithi zimekuwa zikitumika kupokonya na kukejeli, lakini hadithi zinaweza tumika kuhamasisha na kuleta ubinadamu. Hadithi zinaweza kuvunja heshima ya watu, lakini hadithi zinaweza kurudisha heshima iliyopotea. Mwandishi wa Kimarekani Alice Walker aliandika kuhusu ndugu zake wanaotokea Kusini ambao walihamia Kaskazini. Aliwaonyesha kitabu kuhusu maisha ya Kusini ambayo wameyaacha nyuma. "Walikaa, na wakakisoma kitabu, nisikilize mimi soma kitabu, na raha ya dunia utaipata tena." Ningependelea kumalizia na hili wazo: Kwamba pale tunapokataa hadithi moja, tunapogundua kwamba hakuna hadithi moja kuhusu sehemu yoyote, huwa tunarejesha Furaha. Asante. (Makofi)