0:00:00.000,0:00:01.976 Mimi ni msimuliaji wa hadithi 0:00:02.000,0:00:04.976 Ningependa kuwasimulia kidogo maisha yangu 0:00:05.000,0:00:09.976 juu ya kile ninachopenda kuita[br]"hatari ya simulizi moja" 0:00:10.746,0:00:13.976 Nilikulia mazingira ya chuo[br]kikuu magharibi mwa Nigeria 0:00:14.158,0:00:17.467 Mama yangu anasema nilianza kusoma[br]nikiwa na miaka miwili 0:00:17.491,0:00:20.507 japo nadhani miaka minne ni sahihi zaidi 0:00:21.753,0:00:23.564 Niliwahi sana kuanza kusoma 0:00:23.588,0:00:26.976 Nilisoma vitabu vya watoto vya Uingereza[br]na Marekani 0:00:27.706,0:00:29.976 Pia nilianza kuandika katika umri mdogo 0:00:30.000,0:00:33.976 Na nilipoanza kuandika,[br]nikiwa na takriban miaka saba, 0:00:34.000,0:00:36.048 hadithi za penseli na michoro ya rangi 0:00:36.072,0:00:39.604 ambazo mama yangu alilazimika kuzisoma, 0:00:39.628,0:00:43.196 niliandika hadithi[br]sawa na zile nilizokuwa nazisoma: 0:00:43.220,0:00:47.976 Wahusika wangu wote [br]walikuwa wazungu na wenye macho ya bluu. 0:00:48.000,0:00:50.307 Walicheza katika theluji. 0:00:50.331,0:00:52.418 Walikula matofaa 0:00:52.442,0:00:53.839 (Kicheko) 0:00:54.013,0:00:56.024 Na walizungumza sana kuhusu hali ya hewa, 0:00:56.048,0:00:58.176 jinsi ilivyo vizuri kuona jua limechomoza. 0:00:58.409,0:01:00.373 (Kicheko) 0:01:00.397,0:01:03.531 Yote haya,ingawa niliishi Nigeria. 0:01:03.555,0:01:05.333 Nilikuwa sijawahi kwenda nje ya Nigeria. 0:01:07.143,0:01:10.404 Hatukuwa na theluji, tulikula maembe. 0:01:10.428,0:01:12.276 Na hatukuzungumza kuhusu hali ya hewa, 0:01:12.300,0:01:13.976 sababu hakukuwa na haja ya kufanya hivyo. 0:01:14.269,0:01:16.976 Wahusika wangu pia[br]walikunywa sana bia ya tangawizi 0:01:17.000,0:01:19.381 kwa sababu wahusika [br]katika vitabu vya Uingereza 0:01:19.405,0:01:20.976 walikunywa bia ya tangawizi. 0:01:21.301,0:01:23.976 Ijapokuwa [br]sikuifahamu bia ya tangawizi 0:01:24.000,0:01:25.531 (Kicheko) 0:01:25.555,0:01:27.005 Na kwa miaka mingi baadaye 0:01:27.029,0:01:29.976 nilikuwa na shauku[br]ya kuonja bia ya tangawizi. 0:01:30.476,0:01:31.976 Lakini hiyo ni hadithi nyingine. 0:01:32.000,0:01:34.483 Ambacho hii inaonyesha,nafikiri[br] 0:01:34.507,0:01:37.361 Ni namna tulivyo wajinga na wanyonge 0:01:37.385,0:01:38.976 Tunapokabiliana na simulizi 0:01:39.000,0:01:40.385 hasa hasa kama watoto 0:01:41.639,0:01:45.409 Sababu nilisoma vitabu[br]vyenye wahusika wa kigeni 0:01:45.433,0:01:47.552 Nilikuwa nimeaminishwa kwamba vitabu 0:01:47.576,0:01:50.746 kwa asili lazima [br]viwe na wahusika wageni 0:01:50.770,0:01:54.489 Na vielezo kuhusu mambo ambayo[br]binafsi siyafahamu 0:01:55.600,0:01:58.219 Mambo yalibadilika[br]Nilipopata vitabu vya Afrika 0:01:59.000,0:02:00.976 havikuwepo kwa wingi 0:02:01.000,0:02:03.869 Na haikuwa rahisi kuvipata[br]kama vya kigeni[br] 0:02:03.893,0:02:06.976 Lakini sababu ya waandishi[br]kama Chinua Achebe na Camara Laye 0:02:07.000,0:02:10.976 Nilipata badiliko la akili[br]ninavyoiona fasihi 0:02:11.000,0:02:13.214 Niligundua kwamba watu kama mimi, 0:02:13.238,0:02:15.245 wasichana weusi 0:02:15.269,0:02:18.531 wenye nywele ngumu 0:02:18.555,0:02:20.365 pia wapo katika fasihi. 0:02:20.682,0:02:23.976 Nilianza kuandika [br]vitu nilivyovifahamu 0:02:24.737,0:02:27.976 Nilikuwa navipenda hivyo vitabu[br]vya Marekani na Uingereza 0:02:28.000,0:02:31.976 Viliamsha fikra zangu[br]Vilifunua vitu vipya. 0:02:32.000,0:02:33.976 Lakini matokeo yasiyokusudiwa 0:02:34.000,0:02:36.048 yalikuwa; sikufahamu kuwa[br]watu kama mimi 0:02:36.072,0:02:37.498 waweza kuwepo katika fasihi. 0:02:38.451,0:02:41.976 hivyo ufumbuzi wa waandishi Waafrika: 0:02:42.000,0:02:45.877 Uliniokoa na mtazamo mmoja[br]juu ya vitabu 0:02:47.000,0:02:49.976 Ninatoka kwenye familia[br]ya kawaida 0:02:50.000,0:02:51.976 Baba yangu alikuwa mhadhiri 0:02:52.385,0:02:54.068 Mama yangu ni[br]afisa wa utawala 0:02:55.369,0:02:58.171 Kwa hiyo kama kawaida, tulikuwa na, 0:02:58.195,0:03:02.544 mtumishi wa nyumbani[br]anayetoka vijiji vya jirani 0:03:03.182,0:03:06.468 Nilipokuwa na miaka nane[br]tulipata mtumishi wa kiume 0:03:07.102,0:03:08.356 Jina lake aliitwa Fide 0:03:09.658,0:03:13.959 Mama alituambia kuwa familia[br]yake ni masikini sana 0:03:15.000,0:03:19.976 Mama alituma magimbi na mchele[br]na nguo zetu za zamani kwa familia yao 0:03:20.000,0:03:22.620 Na niliposhindwa kumaliza chakula[br]mama alisema, 0:03:22.644,0:03:26.976 "Maliza chakula! kuna watu[br]ambao hawana chochote 0:03:27.000,0:03:30.976 Niliwahurumia sana[br]familia ya Fide 0:03:31.576,0:03:34.473 Jumamosi moja tukaenda[br]kijijini kwao kutembelea 0:03:34.497,0:03:37.976 na mama yake akatuonyesha[br]kikapu kizuri 0:03:38.000,0:03:40.976 kilichosukwa kwa ukili uliopakwa rangi[br]na kaka yake Fide 0:03:41.000,0:03:42.976 Nilishangaa 0:03:43.000,0:03:45.976 Sikudhani kuwa yeyote katika familia yake 0:03:46.000,0:03:48.976 angeweza kutengeneza chochote 0:03:49.000,0:03:51.976 yote niliyowahi kusikia kuhusu wao[br]ni namna walivyo masikini 0:03:52.000,0:03:56.467 Kwa hiyo ilikuwa haiwezekani kwangu[br]kuwaona tofauti na umasikini wao 0:03:57.143,0:03:59.514 umasikini wao ilikuwa[br]ni simulizi moja kwangu 0:04:01.000,0:04:03.524 baadaye niliwaza hili [br]nilipotoka Nigeria 0:04:03.548,0:04:06.230 Kwenda Marekani kusoma[br]chuo kikuu 0:04:06.341,0:04:07.674 Nilikuwa na miaka 19 0:04:08.421,0:04:11.198 Mmarekani niliyekuwa[br]naishi naye chumba kimoja alinishangaa 0:04:12.000,0:04:15.586 Aliuliza wapi nimefunza [br]kuzungumza kiingereza vizuri 0:04:15.610,0:04:17.698 Alishangaa nilipomwambia kuwa Nigeria 0:04:17.722,0:04:20.436 wanatumia kiingereza kama lugha ya taifa 0:04:21.753,0:04:25.976 Aliomba kusikiliza "nyimbo za kikabila" 0:04:26.000,0:04:27.976 na alipigwa butwaa vile vile 0:04:28.000,0:04:29.976 Nilipompa kanda yangu ya Mariah Carey 0:04:30.000,0:04:32.976 (kicheko) 0:04:33.000,0:04:36.693 Alidhani kuwa sifahamu[br]kutumia jiko la umeme 0:04:37.782,0:04:39.038 Kilichonishangaza mimi ni hiki 0:04:39.062,0:04:42.137 Alikuwa ananihurimia[br]hata kabla ya kuniona 0:04:42.528,0:04:45.976 Mtazamo wake mbovu,[br]kunihusu, kama Mwafrika, 0:04:46.000,0:04:49.036 Ulikuwa wa huruma ya kudhalilisha,[br]yenye kujali 0:04:50.000,0:04:53.496 Alikuwa na simulizi moja[br]kuhusu Afrika: 0:04:53.623,0:04:55.977 Simulizi ya majanga. 0:04:56.412,0:04:57.698 Kwenye simulizi hii moja, 0:04:57.722,0:05:01.976 Hakukuwa na uwezekano wa Mwafrika[br]kufanana naye kwa namna yeyote, 0:05:02.000,0:05:04.976 Hakukuwa na uwezekano wa hisia[br]ngumu zaidi ya huruma, 0:05:05.000,0:05:08.976 Hakukuwa na uwezekano wa ushirikiano[br]kama binadamu walio sawa. 0:05:09.000,0:05:11.123 Lazima niseme kuwa[br]kabla ya kwenda Marekani, 0:05:11.147,0:05:13.428 Sikuwa nikijitambua kwa undani[br]kama Mwafrika. 0:05:14.000,0:05:16.976 Lakini Marekani, popote Afrika ilipotajwa,[br]watu walinigeukia. 0:05:17.000,0:05:19.746 Bila kujali kuwa sifahamu chochote[br]kuhusu nchi kama Namibia. 0:05:21.000,0:05:23.096 Lakini nilikuja kuupokea[br]huu utambulisho mpya, 0:05:23.120,0:05:25.976 Na kwa namna nyingi sasa [br]ninajitazama kama Mwafrika. 0:05:26.000,0:05:29.976 Ijapokuwa bado ninakasirishwa sana[br]pale Afrika inapoelezewa kama ni nchi 0:05:30.000,0:05:33.976 Mfano wa karibu, ni safari yangu ya ndege 0:05:34.000,0:05:35.285 Kutoka Lagos hivi juzi, 0:05:35.309,0:05:38.191 Ambapo kulikuwa na tangazo 0:05:38.215,0:05:42.976 Kuhusu kazi ya kujitolea kule[br]"India, Afika na nchi nyingine" 0:05:43.000,0:05:44.317 Kicheko 0:05:44.476,0:05:47.976 Baada ya kuishi Marekani kama Mwafrica 0:05:48.000,0:05:51.174 Nikaanza kuelewa mwitikio wa [br]niliyekuwa naishi naye chumba kimoja 0:05:52.000,0:05:54.025 kama sikukulia Nigeria 0:05:54.049,0:05:57.190 Na kama kila nilichofahamu kuhusu Afrika [br]kilitokana na picha maarufu 0:05:57.214,0:06:02.386 Mimi pia ningedhani kuwa Africa ni mahali[br]penye mandhari nzuri, 0:06:02.410,0:06:03.976 Wanyama wa kupendeza, 0:06:04.000,0:06:05.976 na watu wasioeleweka, 0:06:06.000,0:06:09.631 wapiganao vita visivyo na maana,[br]wanaokufa na umasikini na UKIMWI 0:06:09.655,0:06:11.976 wasioweza kujisemea 0:06:12.000,0:06:16.155 wanaosubiri kusaidiwa na[br]mtu mweupe, mgeni mwenye ukarimu 0:06:16.928,0:06:19.097 Ningewaona waafrika[br]kwa namna ile ambayo mimi, 0:06:19.121,0:06:21.824 nilipokuwa mtoto,[br]niliiona familia ya Fide 0:06:23.000,0:06:26.976 Hii simulizi moja kuhusu Afrika[br]nadhani inatokana na fasihi za magharibi 0:06:27.000,0:06:31.976 Sasa, huu ni msemo kutoka katika uandishi[br]wa mfanyabiashara wa London aitwaye John Lok, 0:06:32.000,0:06:34.976 aliyesafiri kwa maji kuelekea [br]Afrika magharibi mwaka 1561 0:06:35.000,0:06:38.663 na aliweka hazina ya kuvutia [br]kutokana na safari yake. 0:06:40.203,0:06:43.976 Baada ya kuwaita Waafrika weusi kama[br]" hayawani wasio na nyumba," 0:06:44.000,0:06:47.976 aliandika,"Pia kuna watu wasio na vichwa, 0:06:48.000,0:06:51.968 midomo na macho yao[br]yapo katika vifua vyao." 0:06:53.000,0:06:55.096 Sasa, nilicheka kila [br]nikisoma haya maneno. 0:06:55.120,0:06:58.500 Na lazima mtu [br]atakubaliana na fikira za John Lok. 0:06:59.373,0:07:01.239 Lakini kipi ni muhimu [br]kuhusu uandishi wake 0:07:01.263,0:07:02.976 ni kwamba inawakilisha mwanzo 0:07:03.000,0:07:05.976 wa utamaduni wa kuelezea hadithi [br]za Afrika kwa Magharibi: 0:07:06.000,0:07:09.367 Utamaduni wa kusini mwa jangwa la Sahara[br]kama sehemu isiyofaa, 0:07:09.479,0:07:11.634 yenye utofauti, yenye kiza, 0:07:11.658,0:07:16.976 ya watu ambao, kutokana na maneno ya[br]mshairi bora aitwaye Rudyard Kipling, 0:07:17.000,0:07:18.941 ni "nusu shetani, nusu watoto." 0:07:20.211,0:07:22.976 Hivyo, nilianza kuelewa kwamba mwanafunzi[br]Mmarekani ninayeshirikiana nae chumba 0:07:23.000,0:07:24.976 lazima katika maisha yake 0:07:25.000,0:07:28.976 atakuwa ameona na kusikia [br]namna mbalimbali za hii hadithi moja, 0:07:29.000,0:07:30.976 kama ilivyo kwa profesa, 0:07:31.000,0:07:34.766 ambaye aliwahi niambia kuwa [br]riwaya yangu haikuwa "na uhalisia wa Kiafrika," 0:07:35.869,0:07:37.560 Sasa, nilikubaliana na kuchanganua 0:07:37.584,0:07:40.679 kwamba kulikuwa na baadhi ya vitu [br]ambavyo si sawa katika riwaya hii, 0:07:40.703,0:07:43.976 na kuwa nilifeli katika maeneo mbalimbali, 0:07:44.000,0:07:46.239 lakini sikufiria kwamba ilifeli 0:07:46.263,0:07:48.976 katika kutekeleza [br]uhalisia wake wa Kiafrika. 0:07:49.000,0:07:52.706 Kiukweli, sikufahamu [br]uhalisia wa Kiafrika ni upi. 0:07:54.000,0:07:58.396 Profesa alinielezza kwamba wahusika kwenye riwaya[br]walikuwa wanafanana mno kama yeye, 0:07:58.420,0:08:00.396 msomi aliye katika maisha ya kati. 0:08:00.420,0:08:02.522 Wahusika wangu waliendesha magari. 0:08:02.546,0:08:04.976 Hawakuwa wanashinda na njaa. 0:08:05.000,0:08:07.927 Kwa hiyo hawakuwa Waafrika halisi. 0:08:09.000,0:08:11.976 Lakini niongeze haraka-haraka [br]kwamba najisikia hatia 0:08:12.000,0:08:14.070 katika swali la la hadithi iliyo moja. 0:08:15.000,0:08:17.991 Miaka michache iliyopita, [br]nilitembelea Mexico nikitokea Marekani. 0:08:19.000,0:08:21.667 Hali ya kisiasa nchini Marekani [br]wakati huo ilikuwa tete, 0:08:21.691,0:08:24.976 kulikuwa na majadiliano yanayoendelea [br]kuhusu uhamiaji. 0:08:25.000,0:08:26.976 Na, mara kwa mara hutokea Marekani, 0:08:27.000,0:08:29.976 neno uhamiaji likaja kuwa [br]linahusishwa na watu wenye asili ya Mexico. 0:08:30.698,0:08:32.631 Kulikuwa na hadithi ndefu [br]kuhusu Wamexico 0:08:32.655,0:08:35.976 kama watu wanaonyonya mfumo wa afya, 0:08:36.000,0:08:37.976 wanajipenyeza kwenye mipaka, 0:08:38.000,0:08:40.465 wanakamatwa kwenye mipaka,[br]vitu kama hivyo. 0:08:42.163,0:08:45.976 Nakumbuka siku ya kwanza nilipokuwa natembea[br]eneo liitwalo Guadalajara, 0:08:46.000,0:08:47.976 nikiwaangalia watu wakielekea makazini, 0:08:48.000,0:08:49.976 wakitengeneza tortilla maeneo ya sokoni, 0:08:50.000,0:08:51.973 wakivuta sigara, wakicheka. 0:08:53.195,0:08:55.976 Nakumbuka kwa mara ya kwanza [br]nilipatwa na mshangao kidogo. 0:08:56.000,0:08:58.976 Kisha, nikagubikwa na aibu. 0:08:59.341,0:09:03.976 Nikatambua ya kwamba nimezama sana katika habari zinazoelezea watu wa Mexico 0:09:04.000,0:09:06.000 ambao wamekuwa jambo katika akili yangu, 0:09:06.024,0:09:07.849 wahamiaji duni, 0:09:08.769,0:09:11.191 nilidanganyika katika hadithi moja[br]ya watu wa Mexico 0:09:11.215,0:09:13.722 na sikuweza kujisikia aibu zaidi. 0:09:14.071,0:09:16.618 Kwa hiyo hiyo ndiyo[br]namna ya kutengeneza hadithi moja. 0:09:16.642,0:09:18.976 kuwaeleza watu kama jambo moja, 0:09:19.000,0:09:20.976 kama jambo moja tu, 0:09:21.000,0:09:22.976 tena na tena, 0:09:23.000,0:09:24.515 na hivyo ndivyo watakavyokuwa. 0:09:25.793,0:09:28.239 Haiwezekani kuongelea kuhusu hadithi moja 0:09:28.263,0:09:29.952 bila kuongelea kuhusu uwezo ya mamlaka. 0:09:31.496,0:09:33.244 Kuna neno, neno la lugha ya Igbo, 0:09:33.268,0:09:36.919 ambalo huwa naliwaza kila nikifikiria [br]mfumo wa mamlaka wa dunia, 0:09:36.943,0:09:38.133 na hili "nkali". 0:09:38.332,0:09:42.976 Ni nomino ambayo inatafsiriwa kama [br]"kuwa juu zaidi ya mwigine." 0:09:43.554,0:09:46.482 Kama ulivyo ulimwengu wa[br]kiuchumi na kisiasa, 0:09:46.506,0:09:50.976 hadithi pia huelezwa kwa kanuni ya nkali: 0:09:51.000,0:09:52.976 Zinaelezwaje, nani anaelezea, 0:09:53.000,0:09:56.237 wakati gani zilielezwa,[br]hadithi ngapi zinaelezwa, 0:09:56.261,0:09:58.468 haya yote yanategemea sana [br]nguvu ya mamlaka. 0:10:00.000,0:10:03.143 Mamlaka ni uwezo sio tu wa kueleza[br]hadithi ya kuhusu mtu mwingine, 0:10:03.167,0:10:06.976 lakini kuifanya iwe hadithi mahususi[br]kuhusu mtu huyo. 0:10:07.000,0:10:09.096 Mshairi wa Kipalestina[br]Mourid Barghouti aliandika 0:10:09.120,0:10:11.976 kwamba kama unataka kuwaondoa watu, 0:10:12.000,0:10:14.976 njia rahisi ya kufanya hivyo [br]ni kuelezea hadithi yao 0:10:15.000,0:10:17.230 na kuanza na, "pili." 0:10:18.484,0:10:22.382 Anza hadithi na mishale[br]ya waliokuwa wakazi halisi wa Amerika, 0:10:22.406,0:10:24.976 na sio baada ya kufika kwa Waingereza, 0:10:25.000,0:10:27.977 na utakuwa na hadithi tofauti nyingine kabisa. 0:10:28.001,0:10:32.433 Anza na hadithi kuhusu [br]kuanguka kwa dola za Kiafrika, 0:10:32.457,0:10:35.976 na sio dola za Kiafrika [br]zilizotokana na ukoloni, 0:10:36.000,0:10:38.742 na utakuwa na hadithi tofauti kabisa. 0:10:40.000,0:10:41.976 Hivi karibun nilitoa hotuba katika chuo 0:10:42.000,0:10:45.785 ambapo mwanafunzi aliniambia [br]kwamba ilikuwa ni aibu 0:10:45.809,0:10:48.928 kwamba wanaume wa Kinigeria [br]walikuwa wanyanyasaji 0:10:48.952,0:10:50.896 kama alivyo muhusika [br]ambaye ni baba katika riwaya yangu. 0:10:52.000,0:10:55.976 Nikamwambia nimesoma riwaya [br]iitwayo "Mwendawazimu wa Kiamerika" -- 0:10:56.000,0:10:57.976 (Kicheko) 0:10:58.000,0:10:59.976 -- na kwamba ilikuwa aibu 0:11:00.000,0:11:02.976 kwamba vijana wadogo wa Kiamerika [br]walikuwa wauaji waliokubuhu. 0:11:03.000,0:11:06.976 (Kicheko) 0:11:07.000,0:11:12.976 (Makofi) 0:11:13.000,0:11:15.976 Sasa, kiukweli nilisema hili [br]kutokana na kukerwa. 0:11:16.000,0:11:17.976 (Kicheko) 0:11:18.000,0:11:20.191 Lakini isingeweza kutokea kwangu kuwaza 0:11:20.215,0:11:23.976 kwamba kwa sababu nimesoma riwaya [br]ambayo muhusika ni muuaji wa kufululiza 0:11:24.000,0:11:27.976 kwamba kwa kiasi fulani [br]wanawakilisha Wamarekani wote. 0:11:28.000,0:11:30.976 Hii si kwamba mimi [br]ni mtu bora kuliko yule mwanafunzi, 0:11:31.000,0:11:33.976 lakini kwa sababu ya utamaduni [br]na nguvu ya uchumi wa Marekani, 0:11:34.000,0:11:35.976 Nilikuwa nina hadithi nyingi za Marekani. 0:11:36.000,0:11:39.976 Nilisoma Tyler na Updike [br]na Steinbeck na Gaitskill. 0:11:40.000,0:11:42.560 Sikuwa na hadithi moja ya Marekani. 0:11:43.671,0:11:45.377 Nilipojifunza, miaka kadhaa iliyopita, 0:11:45.401,0:11:49.742 kwamba waandishi wanategemewa kuwa na maisha ya utotoni ambayo siyo ya furaha 0:11:49.766,0:11:51.976 ili kuja kufanikiwa baadaye, 0:11:52.000,0:11:56.000 Nilianza kuwaza ni namna gani naweza buni [br]vitu vibaya ambavyo wazazi wangu walinifanyia. 0:11:56.024,0:11:57.976 (Kicheko) 0:11:58.000,0:12:01.976 Lakini ukweli ni kwamba nilikuwa na maisha ya utoto ambayo yalikuwa ya furaha sana, 0:12:02.000,0:12:04.976 yaliyojaa vicheko na upendo,[br]katika familia iliyo na ukaribu sana. 0:12:05.000,0:12:08.211 Lakini pia nilikuwa na mababu [br]waliofia kwenye kambi za wakimbizi. 0:12:08.750,0:12:12.976 Binamu yangu Polle alifariki [br]sababu hakupata matibabu yanayostahili. 0:12:13.000,0:12:15.976 Mmoja wa rafiki zangu,Okoloma, [br]alifariki kwenye ajali ya ndege 0:12:16.000,0:12:18.976 kwa sababu gari zetu za zimamoto [br]hazikuwa na maji. 0:12:19.000,0:12:21.976 Nimekulia katika serikali ya kijeshi[br]ambayo ni kandamizi 0:12:22.000,0:12:23.976 ambayo haikujali elimu, 0:12:24.000,0:12:26.976 kwa muda mwingine,[br]wazazi walikuwa hawalipwi mishahara. 0:12:27.000,0:12:30.977 Hivyo, kama mtoto, nilianza kuona jamu hakuna mezani wakati wa kupata kifungua kinywa, 0:12:31.001,0:12:33.498 kisha siagi nayo ikakosekana, 0:12:33.522,0:12:35.976 kisha mkate ukawa ghali sana, 0:12:36.000,0:12:37.871 kisha maziwa yakapungua. 0:12:39.000,0:12:42.657 Na katika yote, hali ya hofu ya kisiasa 0:12:42.681,0:12:44.363 ikaingilia maisha yetu, 0:12:45.823,0:12:47.960 Na hadithi zote hizi zimenitengeneza mimi wa leo. 0:12:48.457,0:12:51.976 Lakini kusisitiza katika hizi hadithi hasi 0:12:52.000,0:12:54.976 ni kuongeza uzoefu wangu 0:12:55.000,0:12:58.664 na kuachana na hadithi nyinginezo nyingi ambazo zimenitengeneza mimi. 0:12:59.394,0:13:01.976 Hadithi moja hutengeneza tabaka, 0:13:02.000,0:13:06.976 na tatizo la tabaka [br]si kwamba hazina kweli, 0:13:07.000,0:13:08.976 lakini hazijakamilika. 0:13:09.357,0:13:11.960 Hufanya hadithi moja kuwa hadithi pekee. 0:13:13.000,0:13:15.572 Hakika, Afrika ni bara [br]ambalo limejaa majanga: 0:13:15.596,0:13:18.976 Kuna majanga yaliyo makubwa,[br]kama ubakaji wa kutisha nchini Congo 0:13:19.000,0:13:20.626 na wa kudidimiza, 0:13:20.650,0:13:25.150 kama ukweli kwamba watu 5000 wanaomba [br]nafasi moja ya kazi nchini Nigeria. 0:13:26.000,0:13:29.563 Lakini kuna hadithi nyingine [br]ambazo hazihusiani na majanga, 0:13:29.587,0:13:32.976 na ni muhimu sana, ni namna kuziongelea. 0:13:33.000,0:13:34.976 Wakati wote nimekuwa nikihisi haiwezekani 0:13:35.000,0:13:37.976 kujiunga kwa utaratibu na sehemu au mtu 0:13:38.000,0:13:41.976 bila kuhusiana na hadithi zote[br]za mahala pale au mtu huyo. 0:13:42.000,0:13:45.580 Madhara ya hadithi moja ni kwamba: 0:13:45.604,0:13:47.561 Hunyang'anya watu wa heshima. 0:13:48.332,0:13:51.976 Hufanya utambuzi wetu[br]wa usawa wa kibinadamu kuwa mgumu. 0:13:52.000,0:13:56.164 Husisitiza ni jinsi gani tulivyo tofauti [br]kuliko vile tulivyo sawa. 0:13:57.000,0:13:59.489 Inakuwaje wakati[br]kabla ya safari yangu ya Mexico, 0:13:59.513,0:14:02.976 Ningefatilia majadiliano ya uhamiaji [br]kutoka pande zote, 0:14:03.000,0:14:04.976 upande wa Marekani na wa Mexico? 0:14:05.000,0:14:08.976 Ingekuwaje kama mama yangu angeniambia [br]familia ya Fide ilikuwa masikini 0:14:09.000,0:14:10.976 na ya wachapakazi? 0:14:11.000,0:14:13.096 Inakuwaje kama tungekuwa[br]na mtandao wa televisheni wa Kiafrika 0:14:13.120,0:14:16.976 ambao unarusha vipindi [br]vya hadithi za Afrika duniani kote? 0:14:17.000,0:14:21.331 Kitu ambacho muandishi wa Kinigeria Chinua Achebe[br]anaita "usawa wa hadithi." 0:14:21.355,0:14:25.331 Inakuweaje kama mwanafunzi niliyeishi naye chumba kimoja angefahamu kuhusu mchapishaji wangu wa Kinigeria, 0:14:25.355,0:14:26.976 Muhtar Bakare, 0:14:27.000,0:14:29.048 mtu wa kipekee ambaye [br]aliacha kazi ya benki 0:14:29.072,0:14:31.977 na kufuata ndoto zake [br]na kuanzisha nyumba ya uchapishaji 0:14:32.001,0:14:35.688 Sasa, hekima iliyozoeleka ilikuwa kwamba [br]Wanigeria huwa hawasomi fasihi. 0:14:35.712,0:14:36.966 Yeye alikataa. 0:14:36.990,0:14:40.076 Alihisi kwamba watu [br]ambao wanaweza kusoma, wangesoma, 0:14:40.100,0:14:43.976 kama ungefanya kazi ya fasihi iwe katika bei nafuu na kupatikana kiurahisi. 0:14:44.666,0:14:46.976 Muda mfupi baada ya kuchapisha[br]riwaya yangu ya kwanza, 0:14:47.000,0:14:49.976 Nilikwenda kwenye kituo cha televisheni [br]kilichopo Lagos kwa ajili ya mahojiano, 0:14:50.000,0:14:53.191 na mwanamke ambaye anafanya kazi pale kama karani alinifata na kusema, 0:14:53.215,0:14:55.976 "Nimependa sana riwaya yako. [br]Sijapenda mwishoni mwake. 0:14:56.000,0:14:59.239 Sasa, ni lazima uandike muendelezo [br]na hiki ndicho kitatokea ..." 0:14:59.263,0:15:01.977 (Kicheko) 0:15:02.001,0:15:04.977 Na alipoendelea kunielezea [br]kipi cha kuandika kwenye muendelezo. 0:15:05.564,0:15:07.976 Si kwamba nilivutiwa tu, [br]lakini pia nilisisimka. 0:15:08.000,0:15:10.976 Huyu ni mwanamke, mmoja wa watu wengi [br]wa kawaida waliopo Nigeria, 0:15:11.000,0:15:13.003 ambao hawakutakiwa kuwa wasomaji. 0:15:13.901,0:15:15.525 Si kwamba alisoma tu kitabu, 0:15:15.549,0:15:17.358 lakini pia alikimiliki 0:15:17.382,0:15:20.485 na aliona ana haki kuaniambia [br]kitu cha kuandika katika muendelezo. 0:15:21.580,0:15:24.976 Sasa, ingekuwaje kama mwanafunzi niishiye nae chumba kimoja angejua kuhusu rafiki yangu Funmi Lyanda, 0:15:25.000,0:15:27.976 mwanamke jasiri ambaye anaongoza [br]kipindi cha televisheni Lagos, 0:15:28.000,0:15:31.000 na anadhamiria kuelezea hadithi [br]ambazo tunapendelea kuzisahau? 0:15:31.695,0:15:34.976 Inakuwaje kama mwenzangu [br]angetambua kuhusu upasuaji wa moyo 0:15:35.000,0:15:37.976 ambao ulifanyika wiki iliyopita [br]jijini Lagos? 0:15:38.000,0:15:41.976 Inakuwaje angefahamu [br]kuhusu muziki wa kisasa kwa Kinigeria, 0:15:42.000,0:15:44.976 watu wenye vipaji wanaoimba [br]katika lugha za Kiingereza na pijini, 0:15:45.000,0:15:46.976 na Kiigbo na Kiyoruba na Kiijo, 0:15:47.000,0:15:50.976 wakichanganya ushawishi [br]kutoka kwa Jay Z hadi kwa Fela 0:15:51.000,0:15:53.182 kwenda kwa Bob Marley na babu zao. 0:15:54.000,0:15:56.239 Inakuwaje kama angejua [br]kuhusu wakili mwanamke 0:15:56.263,0:15:59.976 ambaye hivi karibuni alienda mahakamani nchini Nigeria kuipa changamoto sheria isiyo na maana 0:16:00.000,0:16:02.976 ambayo inawataka wanawake [br]kupewa ruhusa na waume zao 0:16:03.000,0:16:05.976 kabla ya kutengeneza hati mpya ya kusafiria? 0:16:06.000,0:16:08.976 Inakuwaje kama angefahamu kuhusu Nollywood, 0:16:09.000,0:16:13.380 iliyojawa na watu wabunifu wanaotengeneza filamu ingawaje kuna changamoto nyingi za kiufundi, 0:16:13.404,0:16:14.976 filamu ambazo ni maarufu sana 0:16:15.000,0:16:19.976 ambazo ni mfano mzuri unaoonyesha Wanigeria wanatumia kile wanachotengeneza? 0:16:20.000,0:16:23.286 Inakuwaje kama angefahamu [br]kuhusu msusi wangu bora kabisa, 0:16:23.310,0:16:26.976 ambaye ameanza biashara yake mwenyewe [br]akiuza nywele za kuongezea? 0:16:27.000,0:16:30.976 Au kuhusu mamilioni ya Wanigeria wengine ambao huanza biashara na muda mwingine kuanguka, 0:16:31.000,0:16:33.938 lakini huendelea kukuza azma yao? 0:16:35.000,0:16:36.976 Muda wote nikiwa nyumbani hukutana 0:16:37.000,0:16:39.976 na vyanzo vya kila wakati vya kukwaza [br]kwa Wanigeria wengi: 0:16:40.000,0:16:43.444 miundombinu yetu mibovu, [br]serikali iliyoanguka, 0:16:43.468,0:16:45.523 lakini pia kwa ustahimilivu mkubwa 0:16:45.547,0:16:48.976 wa watu ambao hufanikiwa,[br]bila ya kutegemea serikali, 0:16:49.000,0:16:50.261 bila yenyewe kabisa. 0:16:51.373,0:16:53.976 Huwa natoa mafunzo ya uandishi [br]kila kipindi cha joto jijini Lagos, 0:16:54.000,0:16:56.976 na huwa inanishangaza [br]kwa namna gani watu wengi hujiunga, 0:16:57.000,0:16:59.976 namna ambavyo watu wengi wana shauku ya kuandika, 0:17:00.000,0:17:01.386 ili kueleza hadithi. 0:17:02.275,0:17:05.298 Mimi na mchapishaji wa kitabu changu [br]tumeanzisha taasisi isiyo ya kibiashara 0:17:05.322,0:17:06.976 inayofahamika kama Farafina Trust, 0:17:07.000,0:17:09.976 na tuna ndoto kubwa ya kujenga maktaba 0:17:10.000,0:17:12.143 na kukarabati maktaba ambazo tayari zipo 0:17:12.167,0:17:14.976 na kutoa vitabu kwa shule za majimboni 0:17:15.000,0:17:17.096 ambazo hazina vitabu katika maktaba zao, 0:17:17.120,0:17:19.501 na kuandaa mafunzo mengi mno, 0:17:19.525,0:17:20.976 katika kuandika na kusoma, 0:17:21.000,0:17:24.199 kwa watu wote ambao wana shauku [br]ya kuelezea hadithi zetu nyingi. 0:17:24.326,0:17:25.976 Hadithi zina maana. 0:17:26.000,0:17:27.976 Hadithi nyingi zina maana. 0:17:28.000,0:17:31.976 Haidithi zimekuwa [br]zikitumika kupokonya na kukejeli, 0:17:32.000,0:17:35.976 lakini hadithi zinaweza tumika [br]kuhamasisha na kuleta ubinadamu. 0:17:36.642,0:17:38.976 Hadithi zinaweza kuvunja heshima ya watu, 0:17:39.000,0:17:42.703 lakini hadithi zinaweza [br]kurudisha heshima iliyopotea. 0:17:44.000,0:17:46.048 Mwandishi wa Kimarekani [br]Alice Walker aliandika 0:17:46.072,0:17:49.976 kuhusu ndugu zake wanaotokea Kusini[br]ambao walihamia Kaskazini. 0:17:50.000,0:17:51.976 Aliwaonyesha kitabu kuhusu 0:17:52.000,0:17:54.068 maisha ya Kusini ambayo wameyaacha nyuma. 0:17:55.592,0:17:58.976 "Walikaa, na wakakisoma kitabu, 0:17:59.000,0:18:04.528 nisikilize mimi soma kitabu,[br]na raha ya dunia utaipata tena." 0:18:05.579,0:18:08.441 Ningependelea kumalizia na hili wazo: 0:18:08.465,0:18:10.976 Kwamba pale tunapokataa hadithi moja, 0:18:11.000,0:18:13.976 tunapogundua kwamba hakuna hadithi moja 0:18:14.000,0:18:16.441 kuhusu sehemu yoyote, 0:18:16.465,0:18:17.976 huwa tunarejesha Furaha. 0:18:18.695,0:18:19.817 Asante. 0:18:19.841,0:18:22.841 (Makofi)