Jinsi gani habari za uongo huleta madhara ya kweli
-
0:01 - 0:04Nataka niwaambie kisa
kuhusu msichana mmoja. -
0:05 - 0:07Lakini siwezi kuwaambia jina lake halisi.
-
0:07 - 0:09Hivyo tufanye kumuita Hadiza.
-
0:10 - 0:11Hadiza ana miaka 20.
-
0:12 - 0:13Ana aibu,
-
0:13 - 0:16lakini ana tabasamu zuri
ambalo hufanya uso wake kung'aa -
0:17 - 0:19Lakini yuko katika maumivu wakati wote.
-
0:21 - 0:24Na anaweza kuwa
mtu wa matibabu maisha yake yote. -
0:25 - 0:27Je wataka kujua kwa nini?
-
0:28 - 0:31Hadiza ni msichana wa Chibok,
-
0:31 - 0:34na mnamo Aprili 14, 2014, alitekwa
-
0:34 - 0:36na magaidi wa Boko Haram.
-
0:36 - 0:39Ingawa alijaribu kutoroka,
-
0:39 - 0:42kwa kuruka toka kwenye gari lililokuwa limebeba wasichana.
-
0:42 - 0:46Lakini alipotua chini, alivunjika miguu yako yote miwili,
-
0:46 - 0:49na alihitaji kutambaa kwa tumbo kujificha kichakani.
-
0:49 - 0:53Aliniambia aliogopa sana
kuwa Boko Haram wangeweza kumrudia. -
0:54 - 0:58Alikuwa mmoja wa wasichana 57 waliotoroka
kwa kuruka toka kwenye magari siku ile. -
0:58 - 1:01Kisa hiki, hakika, kilisambaa kama mawimbi
-
1:01 - 1:02duniani kote.
-
1:02 - 1:06Watu kama Michelle Obama,
Malala na wengine -
1:06 - 1:08walitoa sauti zao wakipinga,
-
1:08 - 1:11na wakati huo huo --
nilikuwa nikiishi London wati huo -
1:11 - 1:16Nilitumwa kutoka London kwenda Abuja
kupata habari za Jukwaa la Uchumi Duniani -
1:16 - 1:18ambapo Naijeria ilikuwa mwenyeji
kwa mara ya kwanza -
1:19 - 1:23Lakini nilipofika, ilikuwa dhahiri
kwamba kulikuwa na habari moja tu mjini. -
1:24 - 1:26Tuliiiweka serikali kwenye shinikizo.
-
1:26 - 1:28Tuliuliza maswali magumu
juu ya nini wanafanya -
1:28 - 1:30kuwarudisha wasichana hawa.
-
1:30 - 1:32Ilieleweka hakika,
-
1:32 - 1:35hawakuwa na furaha juu ya maswali yetu,
-
1:35 - 1:39na tuseme tu tulipata mgao mzuri
wa "ukweli mbadala". -
1:39 - 1:41(Kicheko)
-
1:41 - 1:45Wanaijeria wenye ushawishi mkubwa
walikuwa wakituambia wakati ule -
1:45 - 1:47kuwa tulikuwa washamba.
-
1:47 - 1:50hatukuelewa hali ya siasa ya Naijeria.
-
1:51 - 1:53Lakini pia walituambia
-
1:53 - 1:56kuwa habari ya wasichana wa Chibok
-
1:56 - 1:57illikuwa mzaha.
-
1:58 - 2:01Cha kusikitisha ni kuwa
habari hii ya mzaha imedumu -
2:01 - 2:03na bado kuna watu Naijeria leo
-
2:03 - 2:06wanaoamini
wasichana wa Chibok hawakutekwa. -
2:07 - 2:09Bado, nilikuwa nikiongea na watu kama hawa
-
2:10 - 2:12wazazi wenye huzuni kubwa,
-
2:12 - 2:16ambao walituambia
siku Boko Haram waliwateka binti zao, -
2:16 - 2:21walikimbia mpaka Msitu wa Sambisa
wakifukuza magari laliyobeba binti zao. -
2:21 - 2:25Wao walikuwa na mapanga kama silaha,
lakini walilazimika kurudi -
2:25 - 2:26sababu Boko Haram walikuwa na bunduki.
-
2:27 - 2:31Kwa miaka miwili, pasipo kuepukika,
ajenda za habari zilisonga mbele, -
2:31 - 2:33na kwa miaka miwili,
-
2:33 - 2:36hatukusikia sana
kuhusu wasichana wa Chibok. -
2:36 - 2:38Kila moja alidhania wamekwishakufa.
-
2:38 - 2:40Lakini Aprili mwaka jana,
-
2:40 - 2:42niliweza kupata video hii.
-
2:43 - 2:45Hii ni picha-mnato toka kwenye video
-
2:45 - 2:48ambayo Boko Haram walirekodi
kama ushahidi kuwa wako hai, -
2:49 - 2:51na kupitia chanzo kimoja,
nilipata video hii. -
2:52 - 2:54Lakini kabla sijaichapisha,
-
2:54 - 2:57Nilihitaji kusafiri
kwenda kaskazini mashariki mwa Naijeria -
2:57 - 2:59kuzungumza na wazazi, kuihakikisha.
-
2:59 - 3:03Sikuhitaji kusubiri sana
kupata uthibitisho. -
3:04 - 3:07Mmoja wa wamama,
alipoangalia hiyo video, aliniambia -
3:07 - 3:10kama angeweza kuifika ndani ya kompyuta
-
3:10 - 3:14na kumvuta na kumtoa nje mtoto wake
kutoka kwenye kompyuta, -
3:14 - 3:15angefanya hivyo.
-
3:16 - 3:19Kwa wale kati yenu ambao ni wazazi,
kama mimi, katika wasikilizaji. -
3:19 - 3:22Mnaweza tu kufikiria uchungu
-
3:22 - 3:24ambao yule mama aliusikia
-
3:26 - 3:32Video hii iliendelea hadi kuanzisha
mjadala wa mazungumzo na Boko Haram. -
3:32 - 3:36Na seneta mmoja wa Kinaijeria aliniambia
kuwa kwa sababu ya video hii -
3:36 - 3:38waliingia katika yale mazungumzo,
-
3:38 - 3:42kwa sababu muda mrefu walidhani
wasichana wa Chibok walishakufa. -
3:43 - 3:47Wasichana 21 waliachiwa huru
mwezi Oktoba mwaka jana. -
3:47 - 3:51Cha kusikitisha, karibu 200 kati yao
bado hawajapatikana. -
3:52 - 3:56Ni lazima nikiri,
sijawa mwangalizi niliyependelea -
3:56 - 3:57kuzungumzia habari hii.
-
3:57 - 4:01Nakuwa na hasira ninapofikiria
juu ya fursa zinazopotea -
4:02 - 4:03kuwaokoa wasichana hawa.
-
4:03 - 4:07Nakuwa na hasira ninapofikiria
juu ya kile wazazi wameniambia, -
4:07 - 4:10kuwa ingekuwa mabinti hawa
ni wa matajiri na wenye nguvu, -
4:10 - 4:12wangepatikana mapema zaidi.
-
4:14 - 4:16Na nina hasira
-
4:16 - 4:18kwamba simulizi la mzaha
-
4:18 - 4:20ambalo naamini hakika
-
4:20 - 4:22limesababisha kuchelewa;
-
4:22 - 4:25lilikuwa ni sehemu ya sababu
ya ucheleweshwaji wa kurudi kwao. -
4:27 - 4:31Hii inaonesha kwangu
hatari kubwa ya habari za uongo. -
4:31 - 4:33Nini twaweza kufanya juu ya hili?
-
4:34 - 4:36Kuna watu werevu sana,
-
4:36 - 4:38wahandisi werevu huko Google na Facebook,
-
4:38 - 4:43wanaojaribu kutumia tekinolojia
kuzuia kusambaa kwa habari za uongo. -
4:43 - 4:48Lakini zaidi ya hapo, nafikiri
kila mmoja hapa -- wewe na mimi -- -
4:48 - 4:50tuna nafasi ya kushiriki katika hilo.
-
4:50 - 4:53Sisi ndio tunaoshirikishana maudhui
-
4:53 - 4:55Sisi ndio tunaoshirikishana
habari mitandaoni -
4:55 - 4:57Nyakati za leo, sisi sote ni wachapishaji,
-
4:59 - 5:01na tuna jukumu.
-
5:01 - 5:03Katika kazi yangu kama mwanahabari,
-
5:03 - 5:05Ninaangalia, ninathibitisha,
-
5:05 - 5:09Ninaamini hisia zangu,
lakini nauliza maswali magumu. -
5:10 - 5:12Kwa nini huyu mtu ananiambia habari hii?
-
5:13 - 5:16Nini atakachokipata
kwa kunishirikisha taarifa hii? -
5:16 - 5:18Je, ana ajenda ya siri?
-
5:19 - 5:24Ninaamini kabisa kuwa wote tunatakiwa
kuanza kuuliza maswali magumu zaidi -
5:24 - 5:27kwa taarifa tunazozipata mtandaoni.
-
5:30 - 5:35Utafiti unaonesha kwamba kati yetu
kuna wasiosoma zaidi ya vichwa vya habari -
5:35 - 5:38kabla ya kushirikisha habari.
-
5:38 - 5:39Nani hapa amefanya hivyo?
-
5:40 - 5:41Najua mimi nimefanya.
-
5:42 - 5:44Lakini ingekuwaje kama
-
5:45 - 5:50tungeacha kuchukua taarifa tuipatayo jinsi ionekanavyo kijuujuu?
-
5:50 - 5:54vipi kama tutasimama na kufikiria athari
-
5:54 - 5:56za taarifa ambazo tunazisambaza
-
5:56 - 6:00na uwezo wake wa kuchochea vurugu na chuki?
-
6:01 - 6:05Vipi kama tutasimama na kufikiria juu ya athari kwenye maisha halisi
-
6:05 - 6:07za taarifa tunazoshirikishana?
-
6:08 - 6:10Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.
-
6:10 - 6:13(Makofi na vifijo)
- Title:
- Jinsi gani habari za uongo huleta madhara ya kweli
- Speaker:
- Stephanie Busari
- Description:
-
Mnamo Aprili 14, 2014, shirika la kigaidi la Boko Haram liliteka zaidi ya wasichana wa shule 200 kutoka mji wa Chibok, Naijeria. Duniani kote, uhalifu huu ulifanywa mfano kwa kauli mbiu ya #BringBackOurGirls yaani "Rejesha Wasichana Wetu" -- lakini ndani ya Naijeria, maafisa wa serikali waliita uhalifu huu kuwa ni mzaha, kusababisha utata na kuchelewesha jitihada zozote za kuwakomboa wasichana hawa. Katika zungumzo hili shupavu, mwanahabari Stephanie Busari anaelekezea janga la Chibok kueleza hatari kubwa ya habari za uongo na nini tunaweza kufanya kuzizuia.
- Video Language:
- English
- Team:
closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 06:26
![]() |
Joachim Mangilima approved Swahili subtitles for How fake news does real harm | |
![]() |
Joachim Mangilima accepted Swahili subtitles for How fake news does real harm | |
![]() |
Clarence Bitegeko edited Swahili subtitles for How fake news does real harm | |
![]() |
Clarence Bitegeko edited Swahili subtitles for How fake news does real harm | |
![]() |
Clarence Bitegeko edited Swahili subtitles for How fake news does real harm |