0:00:01.072,0:00:03.880 Nataka niwaambie kisa [br]kuhusu msichana mmoja. 0:00:04.515,0:00:06.627 Lakini siwezi kuwaambia jina lake halisi. 0:00:07.015,0:00:08.928 Hivyo tufanye kumuita Hadiza. 0:00:09.561,0:00:11.050 Hadiza ana miaka 20. 0:00:11.639,0:00:12.790 Ana aibu, 0:00:12.814,0:00:16.048 lakini ana tabasamu zuri [br]ambalo hufanya uso wake kung'aa 0:00:16.959,0:00:18.889 Lakini yuko katika maumivu wakati wote. 0:00:20.643,0:00:24.117 Na anaweza kuwa [br]mtu wa matibabu maisha yake yote. 0:00:25.046,0:00:26.551 Je wataka kujua kwa nini? 0:00:27.964,0:00:30.821 Hadiza ni msichana wa Chibok, 0:00:30.845,0:00:34.078 na mnamo Aprili 14, 2014, alitekwa 0:00:34.102,0:00:35.726 na magaidi wa Boko Haram. 0:00:36.470,0:00:38.979 Ingawa alijaribu kutoroka, 0:00:39.003,0:00:42.200 kwa kuruka toka kwenye gari lililokuwa limebeba wasichana. 0:00:42.224,0:00:45.517 Lakini alipotua chini, alivunjika miguu yako yote miwili, 0:00:45.541,0:00:48.961 na alihitaji kutambaa kwa tumbo kujificha kichakani. 0:00:48.985,0:00:53.063 Aliniambia aliogopa sana [br]kuwa Boko Haram wangeweza kumrudia. 0:00:53.704,0:00:58.331 Alikuwa mmoja wa wasichana 57 waliotoroka [br]kwa kuruka toka kwenye magari siku ile. 0:00:58.355,0:01:00.896 Kisa hiki, hakika, kilisambaa kama mawimbi 0:01:00.920,0:01:02.292 duniani kote. 0:01:02.316,0:01:05.586 Watu kama Michelle Obama, [br]Malala na wengine 0:01:05.610,0:01:07.702 walitoa sauti zao wakipinga, 0:01:07.726,0:01:10.987 na wakati huo huo -- [br]nilikuwa nikiishi London wati huo 0:01:11.011,0:01:15.654 Nilitumwa kutoka London kwenda Abuja [br]kupata habari za Jukwaa la Uchumi Duniani 0:01:15.678,0:01:18.100 ambapo Naijeria ilikuwa mwenyeji[br]kwa mara ya kwanza 0:01:18.655,0:01:22.719 Lakini nilipofika, ilikuwa dhahiri [br]kwamba kulikuwa na habari moja tu mjini. 0:01:23.909,0:01:25.754 Tuliiiweka serikali kwenye shinikizo. 0:01:25.778,0:01:28.340 Tuliuliza maswali magumu [br]juu ya nini wanafanya 0:01:28.364,0:01:29.855 kuwarudisha wasichana hawa. 0:01:30.379,0:01:32.103 Ilieleweka hakika, 0:01:32.127,0:01:34.934 hawakuwa na furaha juu ya maswali yetu, 0:01:34.958,0:01:38.707 na tuseme tu tulipata mgao mzuri [br]wa "ukweli mbadala". 0:01:38.731,0:01:41.412 (Kicheko) 0:01:41.436,0:01:44.634 Wanaijeria wenye ushawishi mkubwa [br]walikuwa wakituambia wakati ule 0:01:44.658,0:01:46.655 kuwa tulikuwa washamba. 0:01:46.679,0:01:49.883 hatukuelewa hali ya siasa ya Naijeria. 0:01:50.900,0:01:52.995 Lakini pia walituambia 0:01:53.019,0:01:55.627 kuwa habari ya wasichana wa Chibok 0:01:55.651,0:01:56.836 illikuwa mzaha. 0:01:58.265,0:02:00.965 Cha kusikitisha ni kuwa [br]habari hii ya mzaha imedumu 0:02:00.989,0:02:03.279 na bado kuna watu Naijeria leo 0:02:03.303,0:02:06.066 wanaoamini [br]wasichana wa Chibok hawakutekwa. 0:02:06.931,0:02:09.494 Bado, nilikuwa nikiongea na watu kama hawa 0:02:10.401,0:02:12.106 wazazi wenye huzuni kubwa, 0:02:12.130,0:02:16.184 ambao walituambia [br]siku Boko Haram waliwateka binti zao, 0:02:16.208,0:02:20.782 walikimbia mpaka Msitu wa Sambisa [br]wakifukuza magari laliyobeba binti zao. 0:02:20.806,0:02:24.534 Wao walikuwa na mapanga kama silaha, [br]lakini walilazimika kurudi 0:02:24.558,0:02:26.407 sababu Boko Haram walikuwa na bunduki. 0:02:27.345,0:02:31.008 Kwa miaka miwili, pasipo kuepukika, [br]ajenda za habari zilisonga mbele, 0:02:31.032,0:02:32.762 na kwa miaka miwili, 0:02:32.786,0:02:35.945 hatukusikia sana [br]kuhusu wasichana wa Chibok. 0:02:35.969,0:02:37.838 Kila moja alidhania wamekwishakufa. 0:02:38.233,0:02:40.220 Lakini Aprili mwaka jana, 0:02:40.244,0:02:42.449 niliweza kupata video hii. 0:02:43.036,0:02:44.776 Hii ni picha-mnato toka kwenye video 0:02:44.800,0:02:47.914 ambayo Boko Haram walirekodi [br]kama ushahidi kuwa wako hai, 0:02:48.923,0:02:51.467 na kupitia chanzo kimoja, [br]nilipata video hii. 0:02:52.109,0:02:53.646 Lakini kabla sijaichapisha, 0:02:53.670,0:02:56.695 Nilihitaji kusafiri [br]kwenda kaskazini mashariki mwa Naijeria 0:02:56.719,0:02:58.786 kuzungumza na wazazi, kuihakikisha. 0:02:59.317,0:03:02.694 Sikuhitaji kusubiri sana [br]kupata uthibitisho. 0:03:03.630,0:03:06.960 Mmoja wa wamama, [br]alipoangalia hiyo video, aliniambia 0:03:06.984,0:03:09.684 kama angeweza kuifika ndani ya kompyuta 0:03:09.708,0:03:13.727 na kumvuta na kumtoa nje mtoto wake [br]kutoka kwenye kompyuta, 0:03:13.751,0:03:15.157 angefanya hivyo. 0:03:16.203,0:03:19.425 Kwa wale kati yenu ambao ni wazazi, [br]kama mimi, katika wasikilizaji. 0:03:19.449,0:03:22.277 Mnaweza tu kufikiria uchungu 0:03:22.301,0:03:23.760 ambao yule mama aliusikia 0:03:25.601,0:03:32.155 Video hii iliendelea hadi kuanzisha [br]mjadala wa mazungumzo na Boko Haram. 0:03:32.179,0:03:36.147 Na seneta mmoja wa Kinaijeria aliniambia [br]kuwa kwa sababu ya video hii 0:03:36.171,0:03:38.164 waliingia katika yale mazungumzo, 0:03:38.188,0:03:41.694 kwa sababu muda mrefu walidhani [br]wasichana wa Chibok walishakufa. 0:03:42.639,0:03:47.341 Wasichana 21 waliachiwa huru [br]mwezi Oktoba mwaka jana. 0:03:47.365,0:03:50.933 Cha kusikitisha, karibu 200 kati yao [br]bado hawajapatikana. 0:03:51.691,0:03:55.888 Ni lazima nikiri, [br]sijawa mwangalizi niliyependelea 0:03:55.912,0:03:57.098 kuzungumzia habari hii. 0:03:57.122,0:04:00.930 Nakuwa na hasira ninapofikiria [br]juu ya fursa zinazopotea 0:04:02.232,0:04:03.421 kuwaokoa wasichana hawa. 0:04:03.445,0:04:07.345 Nakuwa na hasira ninapofikiria [br]juu ya kile wazazi wameniambia, 0:04:07.369,0:04:10.143 kuwa ingekuwa mabinti hawa [br]ni wa matajiri na wenye nguvu, 0:04:10.167,0:04:12.328 wangepatikana mapema zaidi. 0:04:14.281,0:04:16.289 Na nina hasira 0:04:16.313,0:04:18.241 kwamba simulizi la mzaha 0:04:18.265,0:04:20.143 ambalo naamini hakika 0:04:20.167,0:04:22.279 limesababisha kuchelewa; 0:04:22.303,0:04:25.292 lilikuwa ni sehemu ya sababu [br]ya ucheleweshwaji wa kurudi kwao. 0:04:26.680,0:04:31.195 Hii inaonesha kwangu [br]hatari kubwa ya habari za uongo. 0:04:31.219,0:04:32.811 Nini twaweza kufanya juu ya hili? 0:04:33.883,0:04:35.800 Kuna watu werevu sana, 0:04:35.824,0:04:38.283 wahandisi werevu huko Google na Facebook, 0:04:38.307,0:04:43.372 wanaojaribu kutumia tekinolojia [br]kuzuia kusambaa kwa habari za uongo. 0:04:43.396,0:04:48.147 Lakini zaidi ya hapo, nafikiri [br]kila mmoja hapa -- wewe na mimi -- 0:04:48.171,0:04:50.358 tuna nafasi ya kushiriki katika hilo. 0:04:50.382,0:04:52.675 Sisi ndio tunaoshirikishana maudhui 0:04:52.699,0:04:55.210 Sisi ndio tunaoshirikishana [br]habari mitandaoni 0:04:55.234,0:04:57.421 Nyakati za leo, sisi sote ni wachapishaji, 0:04:58.535,0:05:01.026 na tuna jukumu. 0:05:01.050,0:05:03.360 Katika kazi yangu kama mwanahabari, 0:05:03.384,0:05:05.412 Ninaangalia, ninathibitisha, 0:05:05.436,0:05:08.717 Ninaamini hisia zangu, [br]lakini nauliza maswali magumu. 0:05:09.620,0:05:12.496 Kwa nini huyu mtu ananiambia habari hii? 0:05:12.520,0:05:16.019 Nini atakachokipata [br]kwa kunishirikisha taarifa hii? 0:05:16.043,0:05:17.851 Je, ana ajenda ya siri? 0:05:18.682,0:05:24.173 Ninaamini kabisa kuwa wote tunatakiwa [br]kuanza kuuliza maswali magumu zaidi 0:05:24.197,0:05:26.507 kwa taarifa tunazozipata mtandaoni. 0:05:29.673,0:05:35.404 Utafiti unaonesha kwamba kati yetu [br]kuna wasiosoma zaidi ya vichwa vya habari 0:05:35.428,0:05:37.531 kabla ya kushirikisha habari. 0:05:37.555,0:05:39.094 Nani hapa amefanya hivyo? 0:05:39.944,0:05:41.279 Najua mimi nimefanya. 0:05:42.435,0:05:43.794 Lakini ingekuwaje kama 0:05:45.295,0:05:49.504 tungeacha kuchukua taarifa tuipatayo jinsi ionekanavyo kijuujuu? 0:05:50.250,0:05:53.823 vipi kama tutasimama na kufikiria athari 0:05:53.847,0:05:56.296 za taarifa ambazo tunazisambaza 0:05:56.320,0:05:59.531 na uwezo wake wa kuchochea vurugu na chuki? 0:06:00.595,0:06:05.130 Vipi kama tutasimama na kufikiria juu ya athari kwenye maisha halisi 0:06:05.154,0:06:07.002 za taarifa tunazoshirikishana? 0:06:08.105,0:06:09.905 Ahsanteni sana kwa kunisikiliza. 0:06:09.929,0:06:13.423 (Makofi na vifijo)