Return to Video

Je, wewe ni mtoaji au mpokeaji?

  • 0:01 - 0:03
    Kila mtu achukue dakika kuangalia watu humu ndani,
  • 0:03 - 0:06
    jaribu kumtafuta mwenye wasiwasi kuliko wote
  • 0:06 - 0:07
    (Vicheko)
  • 0:07 - 0:09
    Sasa nionyeshe huyo mtu kwa kidole
  • 0:09 - 0:10
    (Vicheko)
  • 0:10 - 0:12
    Acha, natania, usinioneshe
  • 0:12 - 0:13
    (Vicheko)
  • 0:13 - 0:15
    Kama mwanasaikolojia,
  • 0:15 - 0:17
    Nimetumia muda mwingi katika mahali pa kazi,
  • 0:17 - 0:19
    na ninaiona hio paranoia kila mahali.
  • 0:19 - 0:22
    Paranoia inasababishwa na watu nawaita "wapokeaji."
  • 0:22 - 0:24
    Wapokeaji ni wabinafsi katika mahusiano.
  • 0:24 - 0:27
    Wanajali sana: utawahudumiaje wao.
  • 0:27 - 0:28
    Kinyume chao ni "watoaji"
  • 0:28 - 0:31
    Hawa ni watu ambao katika mahusiano yao, huuliza,
  • 0:31 - 0:33
    "Ni namna ipi naweza kukuhudumia?"
  • 0:33 - 0:36
    Ntawapa nafasi ya kutafakari tabia zenu.
  • 0:36 - 0:38
    Sote tumekuwa watoaji na wapokeaji katika nyakati mbalimbali.
  • 0:38 - 0:41
    Tabia yako ni namna unavyohusiana na watu mara nyingi,
  • 0:41 - 0:42
    bila ya kujifikiria
  • 0:42 - 0:44
    Nina jaribio fupi la kuwasaidia
  • 0:44 - 0:46
    kutambua kama wewe ni mtoaji au mpokeaji;
  • 0:46 - 0:48
    na mnaweza kulifanya sasa hivi.
  • 0:48 - 0:49
    [Tambua kama unajihusudu)
  • 0:49 - 0:52
    [Hatua ya 1: Chukua muda kujifikiria.]
  • 0:52 - 0:53
    (Vicheko)
  • 0:53 - 0:54
    [Hatua ya 2: Kama umeshaifikia hatua ya pili, haujihusudu.]
  • 0:56 - 0:58
    (Vicheko)
  • 0:58 - 1:02
    Hilo pekee nitasema leo bila ya data za kuthibitisha.
  • 1:02 - 1:05
    Ninaamani kama imekuchukua muda kuicheka hii katuni
  • 1:05 - 1:08
    tuwe na shaka kwamba wewe ni mpokeaji
  • 1:08 - 1:09
    (Vicheko)
  • 1:09 - 1:11
    Hakika wapokeaji wote sio wabinafsi
  • 1:11 - 1:14
    Baadhi ni watoaji waliotumika sana na kuchoka.
  • 1:14 - 1:17
    Pia kuna wapokeaji ambao hatutaongelea leo,
  • 1:17 - 1:19
    wale wagonjwa wa akili.
  • 1:19 - 1:20
    (Vicheko)
  • 1:20 - 1:23
    Nilitaka kuthibitisha uhalali wa pande hizi mbili,
  • 1:23 - 1:26
    hivyo nikatafiti zaidi ya watu 30,000 kwenye sekta
  • 1:26 - 1:28
    na tamaduni mbalimbali.
  • 1:28 - 1:30
    Nikakuta kwamba wengi
    wako katikati -
  • 1:30 - 1:32
    kati ya kutoa na kupokea.
  • 1:32 - 1:34
    Hawa huchagua mtindo wa tatu "kulipiza."
  • 1:34 - 1:37
    Walipizaji huweka
    usawa kati kutoa na kupokea:
  • 1:37 - 1:41
    nipe nikupe --nitakusaidia ukinisaidia.
  • 1:41 - 1:43
    Inaonekana kama namna salama ya kuishi.
  • 1:43 - 1:46
    Ila, je, ni njia fanisi ya kuishi?
  • 1:46 - 1:49
    Jibu la hakika kwa swali hilo, ni
  • 1:49 - 1:50
    labda.
  • 1:50 - 1:51
    (Vicheko)
  • 1:51 - 1:53
    Nimechunguza mashirika kadhaa,
  • 1:53 - 1:55
    maelfu ya watu.
  • 1:55 - 1:58
    Nmepima tija miongoni wahandisi.
  • 1:58 - 2:01
    (Vicheko)
  • 2:01 - 2:04
    Nimeangalia maksi ya wanafunzi wa udaktari
  • 2:04 - 2:06
    na hata mapato ya watu wa mauzo
  • 2:06 - 2:07
    (Vicheko)
  • 2:07 - 2:09
    Cha kushtua, ni
  • 2:09 - 2:12
    watoaji wanafanya vibaya kuliko wote, katika kila fani.
  • 2:13 - 2:15
    Wahandisi wanaofanya vibaya kazini
  • 2:15 - 2:17
    ndio wanaotoa fadhila kuliko wanapokea.
  • 2:17 - 2:19
    Wako makini kufanya kazi za watu wengine,
  • 2:20 - 2:23
    hata hawana muda au nguvu ya
    kufanya kazi zao.
  • 2:23 - 2:26
    Katika udaktari, maksi za chini ni za
  • 2:26 - 2:28
    wanafunzi wanaokubaliana na kauli kama,
  • 2:28 - 2:30
    "Ninapenda kuwasaidia wengine,"
  • 2:31 - 2:33
    ambacho inapendekeza umuamini zaidi daktari
  • 2:33 - 2:36
    ambaye hana lengo la kusaidia mtu yeyote.
  • 2:36 - 2:37
    (Vicheko)
  • 2:37 - 2:40
    Katika mauzo, mapato ya chini yanaokeana
  • 2:40 - 2:42
    miongoni mwa wauzaji wakarimu.
  • 2:42 - 2:44
    Niliongea na mmoja kati ya
  • 2:44 - 2:46
    wauzaji ambao ni watoaji.
  • 2:46 - 2:48
    Nikamuuliza, "Kwa nini
    unafanya vibaya hivyo --"
  • 2:48 - 2:50
    Sikuuliza namna hiyo, lakini -
  • 2:50 - 2:51
    (Vicheko)
  • 2:51 - 2:53
    "Nini gharama ya ukarimu katika mauzo?"
  • 2:53 - 2:57
    Akasema, "Naam, ninawajali wateja wangu
  • 2:57 - 2:59
    kwamba kamwe siwezi kuwauzia bidhaa zetu ovyo. "
  • 2:59 - 3:01
    (Vicheko)
  • 3:01 - 3:02
    Hivyo, kwa faida yangu,
  • 3:02 - 3:03
    wangapi mnajitambua zaidi kama watoaji
  • 3:03 - 3:05
    kuliko wapokeaji au wanaolipizaji?
  • 3:05 - 3:06
    Inua mkono.
  • 3:07 - 3:10
    OK, ingekuwa zaidi kabla kuongelea hizi takwimu.
  • 3:11 - 3:14
    Lakini, kuna cha kushangaza
    zaidi hapa,
  • 3:14 - 3:17
    kwa sababu watoaji mara nyingi
    hujitoa wenyewe,
  • 3:17 - 3:20
    huyaboresha mashirika yao zaidi.
  • 3:20 - 3:23
    Tuna ushahidi mwingi --
  • 3:23 - 3:27
    tafiti nyingi kuhusu tabia za watoaji
  • 3:27 - 3:29
    katika timu au shirika --
  • 3:29 - 3:32
    na zaidi watu wanavyosaidiana, kufundisha
  • 3:32 - 3:33
    wengine na kushauriana,
  • 3:33 - 3:36
    ndivyo huboresha mashirika katika kila kipimo:
  • 3:36 - 3:39
    faida, kuridhisha wateja, kuvutia
    wafanyakazi -
  • 3:39 - 3:41
    hata hupunguza gharama za uendeshaji.
  • 3:41 - 3:42
    Hivyo watoaji hutumia muda mwingi
  • 3:42 - 3:44
    kusaidia wengine
  • 3:44 - 3:46
    na kuboresha timu,
  • 3:46 - 3:48
    kwa bahati mbaya, wanajikuta kwenye hasara.
  • 3:48 - 3:50
    Nataka kuzungumzia namna ya
  • 3:50 - 3:53
    kujenga utamaduni ambapo watoaji wanafanikiwa.
  • 3:54 - 3:57
    Hivyo nilijiuliza kama watoaji sio
    watekelezaji bora,
  • 3:57 - 3:58
    wapi ni watekelezaji bora?
  • 3:59 - 4:02
    Nitanza na habari njema:
    siyo wapokeaji.
  • 4:02 - 4:03
    Wapokeaji hupanda haraka
  • 4:03 - 4:06
    lakini pia huanguka upesi maofisini.
  • 4:06 - 4:08
    Na huanguka katika mikono ya walipizaji.
  • 4:08 - 4:09
    Kama mlipizaji,
  • 4:09 - 4:11
    unafuata sheria ya "jicho kwa jicho" - ndiyo haki.
  • 4:11 - 4:13
    Hivyo unapokutana na mpokeaji,
  • 4:13 - 4:15
    unalifanya jukumu lako
  • 4:15 - 4:17
    kumuadhibu mpokeaji, kumtia adabu.
  • 4:17 - 4:18
    (Vicheko)
  • 4:18 - 4:19
    Na hivyo haki hutolewa.
  • 4:20 - 4:22
    Naam, watu wengi ni walipizaji.
  • 4:22 - 4:24
    Ina maana, kama wewe ni mpokeaji,
  • 4:24 - 4:26
    hatimaye, balaa hukupata;
  • 4:26 - 4:27
    Kwendako mema, hurudi mema.
  • 4:27 - 4:29
    Hivyo hitimisho lenye mantiki ni:
  • 4:29 - 4:32
    walipizaji ndio wafanyakazi bora.
  • 4:32 - 4:33
    Lakini, hapana, siyo.
  • 4:33 - 4:36
    Katika kila fani, kila shirika, nimechunguza,
  • 4:36 - 4:38
    watoaji, tena, ndio wenye matokeo bora.
  • 4:40 - 4:43
    Tuangalie baadhi ya takwimu nimekusanya, za mapato
  • 4:43 - 4:44
    ya watu wa mauzo.
  • 4:44 - 4:47
    Unachoona ni kwamba watoaji wako katika vikomo vyote.
  • 4:47 - 4:50
    Wengi wao huleta mapato ya chini,
  • 4:50 - 4:51
    lakini pia mapato ya juu.
  • 4:51 - 4:54
    Mwelekeo huo ni kweli pia kwenye tija za wahandisi
  • 4:54 - 4:55
    na maksi za wanafunzi wa udaktari.
  • 4:55 - 4:58
    Watoaji wana uwakilishi mkubwa
    chini na juu
  • 4:58 - 5:00
    katika kila kipimo cha mafanikio.
  • 5:00 - 5:02
    Hivyo swali ni:
  • 5:02 - 5:05
    Jinsi gani tunaweza kujenga dunia
    ambapo watoaji hufanikiwa?
  • 5:05 - 5:08
    Nitazungumzi jinsi ya kufanya hivyo, sio tu katika biashara,
  • 5:08 - 5:10
    ila katika taasisi mbalimbali
  • 5:10 - 5:11
    na hata serikalini.
  • 5:11 - 5:12
    Mko tiyari?
  • 5:12 - 5:13
    (Makofi)
  • 5:13 - 5:16
    Ningewaambia hata hivyo, ila asante kwa shauku.
  • 5:16 - 5:17
    (Vicheko)
  • 5:17 - 5:19
    Kitu cha kwanza muhimu
  • 5:19 - 5:22
    ni kutambua kwamba watoaji ni watu muhimu,
  • 5:22 - 5:25
    ila tusipoangalia, tutawakatisha tamaa.
  • 5:25 - 5:27
    Hivyo, tunabidi kuwalinda watoaji miongoni mwetu
  • 5:27 - 5:31
    Nimejifunza mengi kutoka kwa mwanamitandao bora wa Fortune.
  • 5:33 - 5:34
    Ni huyo mtu, sio paka
  • 5:34 - 5:36
    (Vicheko)
  • 5:36 - 5:37
    Anaitwa Adamu Rifkin.
  • 5:37 - 5:40
    Yeye ni mwekezaji mahiri.
  • 5:40 - 5:42
    Hutumia muda mwingi akisaidia wengine.
  • 5:42 - 5:45
    Siri yake ya mafanikio ni kutoa dakika tano za fadhila.
  • 5:45 - 5:48
    Adamu alisema, "Huhitaji kuwa Mama Teresa or Gandhi
  • 5:48 - 5:49
    kuwa mtoaji.
  • 5:49 - 5:52
    Unabidi utafute njia ndogondogo tu
  • 5:52 - 5:53
    za kushika maisha ya watu."
  • 5:53 - 5:55
    Kama kuwatambulisha watu wawili
  • 5:55 - 5:58
    wanaoweza kufaidika kwa kujuana.
  • 5:58 - 6:01
    Inaweza kuwa kutoa maarifa yako
    au kutoa maoni.
  • 6:01 - 6:03
    Au hata kusema kitu kama,
  • 6:04 - 6:05
    "Unajua,
  • 6:05 - 6:07
    nitajaribu kumtambua mtu
  • 6:07 - 6:10
    ambaye kazi yake hakujatambuliwa. "
  • 6:10 - 6:13
    Hizo dakika tano za fadhila ni muhimu
  • 6:13 - 6:14
    kusaidia watoaji kujiwekea mipaka
  • 6:14 - 6:16
    na kujihami.
  • 6:16 - 6:17
    Jambo la pili la msingi
  • 6:17 - 6:20
    katika kujenga utamaduni ambapo watoaji wanafanikiwa,
  • 6:20 - 6:23
    ni kuhamasisha utamaduni wa kutafuta msaada;
  • 6:23 - 6:24
    ambapo watu huuliza na huomba kusaidiwa.
  • 6:25 - 6:27
    Hii inaweza kuwaogopesha baadhi yenu.
  • 6:27 - 6:30
    [katika mahusiano yako, ni lazima uwe mtoaji daima?]
  • 6:30 - 6:31
    (Vicheko)
  • 6:31 - 6:33
    Utakachogundua katika watoaji waliofanikiwa
  • 6:33 - 6:36
    ni wanatambua kwamba ni sawa
    kuwa mpokeaji pia.
  • 6:37 - 6:40
    Kama unamiliki shirika,
    tunaweza kukurahisishia.
  • 6:40 - 6:42
    Tunaweza kurahishia watu kuomba msaada.
  • 6:42 - 6:44
    Mimi na wenzangu tulifanya utafiti katika mahospitali.
  • 6:44 - 6:47
    Tuligundua wauguzi katika baadhi za wadi
  • 6:47 - 6:50
    waliomba kusaidiwa, kuliko wadi nyingine.
  • 6:50 - 6:53
    Kilichozitofautisha wadi ambazo
  • 6:53 - 6:54
    kuomba msaada ilikuwa kawaida, ni kulikuwa
  • 6:54 - 6:56
    na muuguzi mmoja ambaye kazi yake
  • 6:57 - 6:59
    ni kuwasaidia wengine katika kitengo.
  • 6:59 - 7:00
    Msaada ulipohitajika, wauguzi walisema,
  • 7:00 - 7:04
    "Sio aibu kuomba msaada -
  • 7:04 - 7:05
    bali tabia inayohamasishwa."
  • 7:06 - 7:09
    Kutafuta msaada ni muhimu
    katika kuwalinda,
  • 7:09 - 7:11
    pia kwa ajili ya ustawi wa watoaji.
  • 7:11 - 7:13
    Na kuhamisisha tabia za watoaji,
  • 7:13 - 7:15
    kwa sababu takwimu zinaonyesha kwamba
  • 7:15 - 7:18
    asilimia 75 hadi 90 ya utoaji
  • 7:18 - 7:20
    huanzia na ombi.
  • 7:20 - 7:21
    Lakini watu wengi hawaulizi.
  • 7:21 - 7:23
    Wanahofia kuonekana hawajui,
  • 7:24 - 7:26
    hawajui wageukia wapi, wanaogopa kuwasumbua wenzao.
  • 7:26 - 7:29
    Ikiwa kamwe hakuna anayeomba msaada,
  • 7:29 - 7:31
    utakuwa na watoaji wengi waliokatishwa tamaa,
  • 7:31 - 7:33
    ambao wangependa kuchangia kwa kusaidia,
  • 7:33 - 7:35
    laiti wangejua nani anahitaji msaada na kwa namna gani.
  • 7:35 - 7:37
    Lakini jambo muhimu zaidi kama
  • 7:37 - 7:40
    unataka kujenga utamaduni
    ambapo watoaji wanafanikiwa,
  • 7:40 - 7:43
    ni kuwa mwangalifu kuhusu nani
    unaweka kwenye timu yako.
  • 7:43 - 7:46
    Kama unataka utamaduni
    wa ukarimu na uzalishaji,
  • 7:46 - 7:48
    unapaswa kuajiri watoaji.
  • 7:48 - 7:51
    Lakini nilishangaa kugundua kwamba hiyo haikuwa sahihi --
  • 7:52 - 7:54
    mapungufu ya mpokeaji
  • 7:54 - 7:57
    ni mara mbili au mara tatu
    zaidi kuliko manufaa ya mtoaji.
  • 7:58 - 7:59
    Ifiikirie hivi:
  • 7:59 - 8:00
    tunda moja baya linaweza kuharibu kikapu chote,
  • 8:00 - 8:03
    lakini yai moja nzuri haliwezi kuboresha dazeni nzima.
  • 8:04 - 8:05
    Sijui hii ina maana gani--
  • 8:06 - 8:07
    (Vicheko)
  • 8:07 - 8:08
    Lakini natumaini mnaelewa.
  • 8:08 - 8:11
    Yani-- weka hata mpokeaji mmoja kwenye timu,
  • 8:11 - 8:14
    na utaona kwamba watoaji
    wataacha kusaidia.
  • 8:15 - 8:18
    Watasema, "Nimezungukwa
    na rundo la nyoka na papa.
  • 8:18 - 8:19
    Kwa nini mimi nichangie? "
  • 8:19 - 8:21
    Wakati, ukiweka mtoaji mmoja kwenye timu,
  • 8:21 - 8:23
    huwezi kupata mlipuko wa ukarimu.
  • 8:23 - 8:25
    Mara nyingi zaidi, watu hufikiri,
  • 8:25 - 8:27
    "Afadhali! Huyo anaweza kufanya kazi yetu yote."
  • 8:27 - 8:30
    Hivyo, ufanisi katika kuajiri na kujenga timu
  • 8:30 - 8:32
    haihusishi kuleta pamoja watoaji tu;
  • 8:32 - 8:34
    ila pia kuwatoa wapokeaji nje ya shirika.
  • 8:35 - 8:36
    Ukifanikiwa,
  • 8:36 - 8:38
    utabakiza watoaji na walipizaji.
  • 8:38 - 8:40
    Watoaji watakuwa wakarimu
  • 8:40 - 8:42
    kwa sababu hawana wasiwasi
    kuhusu kupokea fadhila.
  • 8:42 - 8:45
    Na uzuri wa walipizaji ni kwamba wanafuata musuada uliopo.
  • 8:45 - 8:48
    Hivyo ni jinsi gani utamtambua mpokeaji, mapema?
  • 8:49 - 8:52
    Sio rahisi kumtambua mpokeaji
  • 8:52 - 8:53
    hasa kufuata tu hisia zetu za mwanzo.
  • 8:54 - 8:56
    Kuna tabia ambayo hutupotosha .
  • 8:56 - 8:57
    Inaitwa wito upendezi,
  • 8:57 - 8:58
    kati ya vipimo vikuu vya hulka
  • 8:58 - 9:00
    miongoni mwa tamaduni mbalimbali.
  • 9:00 - 9:03
    Watu wapendezi ni wakarimu, wema, wanyenyekevu.
  • 9:03 - 9:05
    Utawakuta wengi wao Kanada --
  • 9:05 - 9:07
    (Vicheko)
  • 9:07 - 9:10
    Ambapo kulikuwa na shindano la kitaifa
  • 9:10 - 9:13
    la kutafuta kauli mbiu mpya ya Kanada
    kwa kujaza tashbihi,
  • 9:13 - 9:15
    "Mkanada kama ..."
  • 9:15 - 9:17
    Nilidhani kauli mbiu itakayoshinda ingekuwa,
  • 9:17 - 9:20
    "Mkanada kama maple syrup,"
    au, "... Hoki ya barafuni ."
  • 9:20 - 9:23
    Lakini, hapana. Kura zilichagua kauli mbiu mpya kuwa -
  • 9:23 - 9:24
    na siwatanii --
  • 9:24 - 9:26
    "Mkanada kama iwezekanavyo,
    katika mazingira haya. "
  • 9:26 - 9:29
    (Vicheko)
  • 9:30 - 9:32
    Sasa kwa wale ambao ni wapendezi,
  • 9:32 - 9:34
    au labda ni wakanada kidogo
  • 9:34 - 9:35
    mtaielewa upesi.
  • 9:35 - 9:37
    Ninawezaje kusema kuwa mimi ni aina moja pekee
  • 9:37 - 9:40
    wakati daima ninajibadilisha kuridhisha wengine?
  • 9:40 - 9:42
    Watu nongwa hujaribu mara chache zaidi.
  • 9:42 - 9:45
    Hawa, wana mashaka, ni wakasoaji, ni changamoto
  • 9:45 - 9:48
    na ndio wenye kwenda kusoma sheria.
  • 9:48 - 9:49
    (Vicheko)
  • 9:49 - 9:52
    Hiyo sio utani; ni kweli kama kanuni.
  • 9:52 - 9:53
    (Vicheko)
  • 9:53 - 9:56
    daima nildhani watu wapendezi ni watoaji
  • 9:56 - 9:58
    na watu nongwa ni wapokeaji.
  • 9:58 - 9:59
    Nilipofanya utafiti,
  • 9:59 - 10:02
    nilistaajabu kukuta hakuna uhusiano katika sifa hizo,
  • 10:02 - 10:05
    kwa sababu tabia ya upendezi au nongwa
  • 10:05 - 10:06
    ni gamba la nje tu:
  • 10:06 - 10:08
    Je, watu wanajisikiaje baada ya kuzungumza na wewe?
  • 10:08 - 10:11
    Wakati kutoa na kupokea inategemea nia yako:
  • 10:11 - 10:14
    Je, maadili yako ni yapi?
    Je, nia yako kwa wengine ni ipi?
  • 10:14 - 10:16
    Kama unataka kusoma watu kwa usahihi,
  • 10:16 - 10:20
    utataka kuwepo katika chumba wakati kila mshauri anasubiri,
  • 10:20 - 10:21
    kupata picha halisi.
  • 10:21 - 10:24
    (Vicheko)
  • 10:25 - 10:28
    Ni rahisi kuwatambua watoaji wapendezi:
  • 10:28 - 10:30
    wao husema ndiyo kwa kila kitu.
  • 10:32 - 10:35
    Wapokeaji nongwa wanatambulika kirahisi pia,
  • 10:35 - 10:39
    ingawa unaweza kuwaita
    kwa jina tofauti kidogo.
  • 10:39 - 10:40
    (Vicheko)
  • 10:42 - 10:44
    Tunasahau makundi mengine mbili.
  • 10:44 - 10:47
    Kuna watoaji nongwa
    katika mashirika.
  • 10:47 - 10:50
    Hawa wanaonekana wagumu kwa nje
  • 10:50 - 10:52
    lakini hujali sana maslahi ya wengine.
  • 10:53 - 10:54
    Au kama mhandisi anavyoiweka,
  • 10:54 - 10:56
    "Ah, watoaji nongwa ni -
  • 10:56 - 10:58
    kama mtu mwenye kiolesura kibaya cha mtumiaji
  • 10:58 - 11:00
    lakini mfumo mzuri."
  • 11:00 - 11:01
    (Vicheko)
  • 11:01 - 11:03
    Kama inawasaidia.
  • 11:03 - 11:04
    (Vicheko)
  • 11:04 - 11:08
    Watoaji nongwa hawathaminiwi katika mashirika yetu,
  • 11:08 - 11:11
    kwa sababu huotoa changamoto
  • 11:11 - 11:13
    ambazo watu hawataki kusikia
    hata kama tunahizitaji.
  • 11:13 - 11:16
    Tunahitaji kuwathamini zaidi
    watu hawa
  • 11:16 - 11:17
    badala ya kuwapuuza,
  • 11:18 - 11:19
    na kusema, "Eh, wanakera,
  • 11:19 - 11:21
    lazima awe mpokeaji nongwa."
  • 11:22 - 11:25
    Kundi jingine hatari tunasahau ni-
  • 11:25 - 11:27
    mpokeaji mpendezi, pia anajulikana kama muigizaji.
  • 11:28 - 11:31
    Huyu ni mtu mwema akiwa mbele yako,
  • 11:31 - 11:33
    na ukigeuka hukuchoma.
  • 11:33 - 11:34
    (Vicheko)
  • 11:35 - 11:38
    Napenda kuwakamata
    hawa watu katika usahili
  • 11:38 - 11:39
    kwa kuuliza swali,
  • 11:39 - 11:41
    "Je, unaweza kunipa majina ya watu wanne
  • 11:41 - 11:43
    ambao umewasaidia kimsingi kazini?"
  • 11:44 - 11:46
    Wapokeaji watakupa hayo majina manne,
  • 11:46 - 11:49
    na wote watakuwa na mafinikio zaidi kuliko wao,
  • 11:49 - 11:50
    kwa sababu wapokeaji ni wastadi katika kunyenyekea
  • 11:50 - 11:53
    wakuu wao na kudharau walio chini.
  • 11:53 - 11:56
    Watoaji wanajua zaidi majina ya watu chini ya uongozi wao,
  • 11:56 - 11:58
    ambao hawana mamlaka mingi,
  • 11:58 - 11:59
    ambao hawana mchango muhimu kwao.
  • 12:00 - 12:03
    Hakika, tunafahamu kuwa tunajifunza mengi kuhusu tabia ya mtu
  • 12:03 - 12:05
    kwa kumuangalia anavyohusiana na mhudumu
  • 12:06 - 12:07
    au dereva wa Uber.
  • 12:07 - 12:09
    Hivyo tukifanya yote vizuri,
  • 12:09 - 12:11
    kama tutatoa wapokeaji katika mashirika,
  • 12:11 - 12:13
    kama tutaweza kuwahakikishia usalama wanaoomba msaada,
  • 12:13 - 12:15
    kama tutaweza kuwalinda watoaji wasichoke
  • 12:15 - 12:18
    na kuwawezesha kutimiza malengo yao
  • 12:18 - 12:20
    na pia kusaidia watu wengine,
  • 12:20 - 12:21
    tunaweza kubadilisha mtizamo wa watu
  • 12:21 - 12:23
    wanavyotizama mafanikio.
  • 12:23 - 12:26
    Badala ya kuona ni mashindano,
  • 12:26 - 12:30
    watu watatambua mafanikio kama mchango kijumuiya zaidi.
  • 12:31 - 12:33
    Naamini kuwa njia kuu ya kufanikiwa
  • 12:33 - 12:35
    ni kuwasaidia watu wengine wafanikiwe.
  • 12:35 - 12:37
    Na kama tunaweza kusambaza imani hio,
  • 12:37 - 12:39
    tunaweza kweli kuigeuza paranoia.
  • 12:39 - 12:41
    Kuna jina kwa ajili hiyo
  • 12:41 - 12:42
    inaitwa "pronoia."
  • 12:43 - 12:45
    Pronoia ni imani kwamba
  • 12:45 - 12:47
    wengine wanapanga mema kwa ajili yako.
  • 12:47 - 12:49
    (Vicheko)
  • 12:51 - 12:53
    Kwamba wanakuzunguka
  • 12:53 - 12:56
    na kuimba sifa zako.
  • 12:58 - 13:01
    Uzuri wa utamaduni wa watoaji
    ni kwamba hio sio njozi,
  • 13:01 - 13:03
    huo ndio uhalisia.
  • 13:04 - 13:06
    Ningependa kuishi kwenye dunia ambayo watoaji wanafanikiwa.
  • 13:06 - 13:09
    Natumaini nyote mtanisaidia kujenga ulimwengu huo.
  • 13:09 - 13:09
    Asanteni.
  • 13:10 - 13:10
    (Makofi)
Title:
Je, wewe ni mtoaji au mpokeaji?
Speaker:
Adam Grant
Description:

Katika kila mahali pa kazi, kuna aina tatu za msingi za watu: watoaji, wapokeaji na walipizaji. Mwanasaikoloji Adam Grant anazifafanua hizi nafsi tatu na anatoa mikakati ya kukuza utamaduni wa ukarimu na jinsi ya kuwaepuka wafanyakazi wabinafsi kuchukua zaidi kuliko sehemu yao.

more » « less
Video Language:
English
Team:
closed TED
Project:
TEDTalks
Duration:
13:28
Joachim Mangilima approved Swahili subtitles for Are you a giver or a taker?
Joachim Mangilima accepted Swahili subtitles for Are you a giver or a taker?
Sophia Mwema edited Swahili subtitles for Are you a giver or a taker?
Sophia Mwema edited Swahili subtitles for Are you a giver or a taker?
Sophia Mwema edited Swahili subtitles for Are you a giver or a taker?
Sophia Mwema edited Swahili subtitles for Are you a giver or a taker?
Sophia Mwema edited Swahili subtitles for Are you a giver or a taker?
Sophia Mwema edited Swahili subtitles for Are you a giver or a taker?
Show all

Swahili subtitles

Revisions