0:00:00.837,0:00:03.104 Kila mtu achukue dakika kuangalia watu humu ndani, 0:00:03.104,0:00:05.823 jaribu kumtafuta mwenye wasiwasi kuliko wote 0:00:05.871,0:00:06.935 (Vicheko) 0:00:06.959,0:00:09.411 Sasa nionyeshe huyo mtu kwa kidole 0:00:09.435,0:00:10.470 (Vicheko) 0:00:10.494,0:00:11.853 Acha, natania, usinioneshe 0:00:11.877,0:00:12.996 (Vicheko) 0:00:13.020,0:00:14.889 Kama mwanasaikolojia, 0:00:14.913,0:00:16.795 Nimetumia muda mwingi katika mahali pa kazi, 0:00:16.819,0:00:19.249 na ninaiona hio paranoia kila mahali. 0:00:19.249,0:00:21.771 Paranoia inasababishwa na watu nawaita "wapokeaji." 0:00:21.815,0:00:24.148 Wapokeaji ni wabinafsi katika mahusiano. 0:00:24.172,0:00:26.573 Wanajali sana: utawahudumiaje wao. 0:00:26.582,0:00:28.233 Kinyume chao ni "watoaji" 0:00:28.257,0:00:31.017 Hawa ni watu ambao katika mahusiano yao, huuliza, 0:00:31.041,0:00:32.785 "Ni namna ipi naweza kukuhudumia?" 0:00:32.825,0:00:36.036 Ntawapa nafasi ya kutafakari tabia zenu. 0:00:36.060,0:00:38.013 Sote tumekuwa watoaji na wapokeaji katika nyakati mbalimbali. 0:00:38.037,0:00:41.053 Tabia yako ni namna unavyohusiana na watu mara nyingi, 0:00:41.077,0:00:42.235 bila ya kujifikiria 0:00:42.259,0:00:43.801 Nina jaribio fupi la kuwasaidia 0:00:43.825,0:00:46.324 kutambua kama wewe ni mtoaji au mpokeaji; 0:00:46.348,0:00:47.826 na mnaweza kulifanya sasa hivi. 0:00:47.850,0:00:49.289 [Tambua kama unajihusudu) 0:00:49.313,0:00:51.625 [Hatua ya 1: Chukua muda kujifikiria.] 0:00:51.649,0:00:52.752 (Vicheko) 0:00:52.776,0:00:54.076 [Hatua ya 2: Kama umeshaifikia hatua ya pili, haujihusudu.] 0:00:55.662,0:00:58.082 (Vicheko) 0:00:58.106,0:01:01.939 Hilo pekee nitasema leo bila ya data za kuthibitisha. 0:01:01.939,0:01:05.371 Ninaamani kama imekuchukua muda kuicheka hii katuni 0:01:05.395,0:01:07.822 tuwe na shaka kwamba wewe ni mpokeaji 0:01:07.846,0:01:08.911 (Vicheko) 0:01:08.935,0:01:10.967 Hakika wapokeaji wote sio wabinafsi 0:01:10.991,0:01:13.879 Baadhi ni watoaji waliotumika sana na kuchoka. 0:01:13.903,0:01:17.227 Pia kuna wapokeaji ambao hatutaongelea leo, 0:01:17.251,0:01:19.104 wale wagonjwa wa akili. 0:01:19.128,0:01:20.279 (Vicheko) 0:01:20.303,0:01:23.175 Nilitaka kuthibitisha uhalali wa pande hizi mbili, 0:01:23.199,0:01:26.008 hivyo nikatafiti zaidi ya watu 30,000 kwenye sekta 0:01:26.032,0:01:27.644 na tamaduni mbalimbali. 0:01:27.668,0:01:30.146 Nikakuta kwamba wengi[br]wako katikati - 0:01:30.170,0:01:31.636 kati ya kutoa na kupokea. 0:01:31.660,0:01:34.005 Hawa huchagua mtindo wa tatu "kulipiza." 0:01:34.029,0:01:37.374 Walipizaji huweka[br]usawa kati kutoa na kupokea: 0:01:37.398,0:01:40.716 nipe nikupe --nitakusaidia ukinisaidia. 0:01:40.740,0:01:43.121 Inaonekana kama namna salama ya kuishi. 0:01:43.145,0:01:46.329 Ila, je, ni njia fanisi ya kuishi? 0:01:46.353,0:01:48.817 Jibu la hakika kwa swali hilo, ni 0:01:48.841,0:01:49.999 labda. 0:01:50.023,0:01:51.249 (Vicheko) 0:01:51.273,0:01:53.452 Nimechunguza mashirika kadhaa, 0:01:53.476,0:01:54.651 maelfu ya watu. 0:01:54.675,0:01:58.227 Nmepima tija miongoni wahandisi. 0:01:58.251,0:02:00.606 (Vicheko) 0:02:00.630,0:02:03.599 Nimeangalia maksi ya wanafunzi wa udaktari 0:02:03.623,0:02:05.598 na hata mapato ya watu wa mauzo 0:02:05.622,0:02:07.068 (Vicheko) 0:02:07.092,0:02:08.744 Cha kushtua, ni 0:02:08.768,0:02:12.437 watoaji wanafanya vibaya kuliko wote, katika kila fani. 0:02:12.749,0:02:14.793 Wahandisi wanaofanya vibaya kazini 0:02:14.817,0:02:17.323 ndio wanaotoa fadhila kuliko wanapokea. 0:02:17.347,0:02:19.483 Wako makini kufanya kazi za watu wengine, 0:02:19.507,0:02:23.057 hata hawana muda au nguvu ya [br]kufanya kazi zao. 0:02:23.081,0:02:25.886 Katika udaktari, maksi za chini ni za 0:02:25.910,0:02:28.017 wanafunzi wanaokubaliana na kauli kama, 0:02:28.041,0:02:30.249 "Ninapenda kuwasaidia wengine," 0:02:31.068,0:02:33.292 ambacho inapendekeza umuamini zaidi daktari 0:02:33.316,0:02:36.395 ambaye hana lengo la kusaidia mtu yeyote. 0:02:36.419,0:02:37.446 (Vicheko) 0:02:37.470,0:02:39.828 Katika mauzo, mapato ya chini yanaokeana 0:02:39.852,0:02:41.547 miongoni mwa wauzaji wakarimu. 0:02:41.571,0:02:44.001 Niliongea na mmoja kati ya 0:02:44.025,0:02:45.632 wauzaji ambao ni watoaji. 0:02:45.656,0:02:48.214 Nikamuuliza, "Kwa nini[br]unafanya vibaya hivyo --" 0:02:48.238,0:02:49.779 Sikuuliza namna hiyo, lakini - 0:02:49.803,0:02:50.847 (Vicheko) 0:02:50.871,0:02:53.223 "Nini gharama ya ukarimu katika mauzo?" 0:02:53.247,0:02:56.513 Akasema, "Naam, ninawajali wateja wangu 0:02:56.537,0:02:59.299 kwamba kamwe siwezi kuwauzia bidhaa zetu ovyo. " 0:02:59.323,0:03:00.724 (Vicheko) 0:03:00.748,0:03:02.260 Hivyo, kwa faida yangu, 0:03:02.272,0:03:03.167 wangapi mnajitambua zaidi kama watoaji 0:03:03.247,0:03:04.672 kuliko wapokeaji au wanaolipizaji? 0:03:04.892,0:03:05.838 Inua mkono. 0:03:06.962,0:03:09.911 OK, ingekuwa zaidi kabla kuongelea hizi takwimu. 0:03:10.525,0:03:14.152 Lakini, kuna cha kushangaza[br]zaidi hapa, 0:03:14.176,0:03:17.472 kwa sababu watoaji mara nyingi[br]hujitoa wenyewe, 0:03:17.496,0:03:19.675 huyaboresha mashirika yao zaidi. 0:03:20.345,0:03:23.112 Tuna ushahidi mwingi -- 0:03:23.136,0:03:26.869 tafiti nyingi kuhusu tabia za watoaji 0:03:26.893,0:03:29.030 katika timu au shirika -- 0:03:29.054,0:03:32.140 na zaidi watu wanavyosaidiana, kufundisha 0:03:32.164,0:03:33.317 wengine na kushauriana, 0:03:33.341,0:03:36.118 ndivyo huboresha mashirika katika kila kipimo: 0:03:36.142,0:03:38.973 faida, kuridhisha wateja, kuvutia[br]wafanyakazi - 0:03:38.997,0:03:40.842 hata hupunguza gharama za uendeshaji. 0:03:41.407,0:03:42.407 Hivyo watoaji hutumia muda mwingi 0:03:42.407,0:03:44.299 kusaidia wengine 0:03:44.299,0:03:45.506 na kuboresha timu, 0:03:45.530,0:03:48.006 kwa bahati mbaya, wanajikuta kwenye hasara. 0:03:48.030,0:03:49.698 Nataka kuzungumzia namna ya 0:03:49.722,0:03:53.043 kujenga utamaduni ambapo watoaji wanafanikiwa. 0:03:53.564,0:03:56.584 Hivyo nilijiuliza kama watoaji sio [br]watekelezaji bora, 0:03:56.608,0:03:58.436 wapi ni watekelezaji bora? 0:03:59.438,0:04:02.088 Nitanza na habari njema:[br]siyo wapokeaji. 0:04:02.112,0:04:03.112 Wapokeaji hupanda haraka 0:04:03.112,0:04:05.791 lakini pia huanguka upesi maofisini. 0:04:05.791,0:04:07.888 Na huanguka katika mikono ya walipizaji. 0:04:07.912,0:04:08.912 Kama mlipizaji, 0:04:08.912,0:04:11.356 unafuata sheria ya "jicho kwa jicho" - ndiyo haki. 0:04:11.356,0:04:12.776 Hivyo unapokutana na mpokeaji, 0:04:12.800,0:04:14.669 unalifanya jukumu lako 0:04:14.693,0:04:16.735 kumuadhibu mpokeaji, kumtia adabu. 0:04:16.759,0:04:17.773 (Vicheko) 0:04:17.797,0:04:19.422 Na hivyo haki hutolewa. 0:04:20.108,0:04:22.078 Naam, watu wengi ni walipizaji. 0:04:22.102,0:04:23.686 Ina maana, kama wewe ni mpokeaji, 0:04:23.710,0:04:25.690 hatimaye, balaa hukupata; 0:04:25.714,0:04:27.352 Kwendako mema, hurudi mema. 0:04:27.376,0:04:28.982 Hivyo hitimisho lenye mantiki ni: 0:04:29.006,0:04:31.871 walipizaji ndio wafanyakazi bora. 0:04:31.895,0:04:33.413 Lakini, hapana, siyo. 0:04:33.437,0:04:36.287 Katika kila fani, kila shirika, nimechunguza, 0:04:36.311,0:04:38.473 watoaji, tena, ndio wenye matokeo bora. 0:04:39.651,0:04:42.809 Tuangalie baadhi ya takwimu nimekusanya, za mapato 0:04:42.833,0:04:43.986 ya watu wa mauzo. 0:04:44.010,0:04:46.665 Unachoona ni kwamba watoaji wako katika vikomo vyote. 0:04:46.689,0:04:49.907 Wengi wao huleta mapato ya chini, 0:04:49.931,0:04:51.397 lakini pia mapato ya juu. 0:04:51.421,0:04:54.025 Mwelekeo huo ni kweli pia kwenye tija za wahandisi 0:04:54.049,0:04:55.440 na maksi za wanafunzi wa udaktari. 0:04:55.464,0:04:58.071 Watoaji wana uwakilishi mkubwa[br]chini na juu 0:04:58.095,0:05:00.177 katika kila kipimo cha mafanikio. 0:05:00.201,0:05:01.503 Hivyo swali ni: 0:05:01.527,0:05:04.936 Jinsi gani tunaweza kujenga dunia[br]ambapo watoaji hufanikiwa? 0:05:04.960,0:05:07.783 Nitazungumzi jinsi ya kufanya hivyo, sio tu katika biashara, 0:05:07.807,0:05:09.638 ila katika taasisi mbalimbali 0:05:09.662,0:05:10.955 na hata serikalini. 0:05:10.979,0:05:12.185 Mko tiyari? 0:05:12.209,0:05:13.395 (Makofi) 0:05:13.419,0:05:16.411 Ningewaambia hata hivyo, ila asante kwa shauku. 0:05:16.435,0:05:17.458 (Vicheko) 0:05:17.482,0:05:19.326 Kitu cha kwanza muhimu 0:05:19.350,0:05:22.097 ni kutambua kwamba watoaji ni watu muhimu, 0:05:22.121,0:05:24.555 ila tusipoangalia, tutawakatisha tamaa. 0:05:24.579,0:05:27.069 Hivyo, tunabidi kuwalinda watoaji miongoni mwetu 0:05:27.093,0:05:31.233 Nimejifunza mengi kutoka kwa mwanamitandao bora wa Fortune. 0:05:32.993,0:05:34.343 Ni huyo mtu, sio paka 0:05:34.367,0:05:35.527 (Vicheko) 0:05:35.551,0:05:37.307 Anaitwa Adamu Rifkin. 0:05:37.331,0:05:39.543 Yeye ni mwekezaji mahiri. 0:05:39.567,0:05:42.361 Hutumia muda mwingi akisaidia wengine. 0:05:42.385,0:05:44.721 Siri yake ya mafanikio ni kutoa dakika tano za fadhila. 0:05:45.261,0:05:47.920 Adamu alisema, "Huhitaji kuwa Mama Teresa or Gandhi 0:05:47.944,0:05:49.127 kuwa mtoaji. 0:05:49.151,0:05:51.654 Unabidi utafute njia ndogondogo tu 0:05:51.678,0:05:53.035 za kushika maisha ya watu." 0:05:53.083,0:05:55.426 Kama kuwatambulisha watu wawili 0:05:55.426,0:05:57.861 wanaoweza kufaidika kwa kujuana. 0:05:57.921,0:06:00.771 Inaweza kuwa kutoa maarifa yako[br]au kutoa maoni. 0:06:01.002,0:06:03.314 Au hata kusema kitu kama, 0:06:04.078,0:06:05.307 "Unajua, 0:06:05.331,0:06:06.831 nitajaribu kumtambua mtu 0:06:06.855,0:06:09.884 ambaye kazi yake hakujatambuliwa. " 0:06:10.422,0:06:12.716 Hizo dakika tano za fadhila ni muhimu 0:06:12.756,0:06:13.756 kusaidia watoaji kujiwekea mipaka 0:06:13.756,0:06:15.962 na kujihami. 0:06:15.962,0:06:17.407 Jambo la pili la msingi 0:06:17.431,0:06:19.899 katika kujenga utamaduni ambapo watoaji wanafanikiwa, 0:06:19.923,0:06:22.848 ni kuhamasisha utamaduni wa kutafuta msaada; 0:06:22.872,0:06:24.052 ambapo watu huuliza na huomba kusaidiwa. 0:06:24.536,0:06:27.205 Hii inaweza kuwaogopesha baadhi yenu. 0:06:27.229,0:06:30.268 [katika mahusiano yako, ni lazima uwe mtoaji daima?] 0:06:30.292,0:06:31.316 (Vicheko) 0:06:31.340,0:06:33.071 Utakachogundua katika watoaji waliofanikiwa 0:06:33.095,0:06:36.215 ni wanatambua kwamba ni sawa[br]kuwa mpokeaji pia. 0:06:36.754,0:06:39.617 Kama unamiliki shirika,[br]tunaweza kukurahisishia. 0:06:39.641,0:06:41.938 Tunaweza kurahishia watu kuomba msaada. 0:06:41.962,0:06:44.034 Mimi na wenzangu tulifanya utafiti katika mahospitali. 0:06:44.058,0:06:47.260 Tuligundua wauguzi katika baadhi za wadi 0:06:47.284,0:06:49.535 waliomba kusaidiwa, kuliko wadi nyingine. 0:06:49.559,0:06:52.905 Kilichozitofautisha wadi ambazo 0:06:52.929,0:06:54.080 kuomba msaada ilikuwa kawaida, ni kulikuwa 0:06:54.104,0:06:56.479 na muuguzi mmoja ambaye kazi yake 0:06:56.503,0:06:58.534 ni kuwasaidia wengine katika kitengo. 0:06:58.558,0:06:59.939 Msaada ulipohitajika, wauguzi walisema, 0:06:59.963,0:07:03.620 "Sio aibu kuomba msaada - 0:07:03.644,0:07:05.024 bali tabia inayohamasishwa." 0:07:06.263,0:07:09.089 Kutafuta msaada ni muhimu[br]katika kuwalinda, 0:07:09.113,0:07:10.512 pia kwa ajili ya ustawi wa watoaji. 0:07:10.536,0:07:13.468 Na kuhamisisha tabia za watoaji, 0:07:13.492,0:07:15.371 kwa sababu takwimu zinaonyesha kwamba 0:07:15.371,0:07:18.129 asilimia 75 hadi 90 ya utoaji 0:07:18.129,0:07:19.504 huanzia na ombi. 0:07:19.714,0:07:21.249 Lakini watu wengi hawaulizi. 0:07:21.433,0:07:23.458 Wanahofia kuonekana hawajui, 0:07:23.528,0:07:25.796 hawajui wageukia wapi, wanaogopa kuwasumbua wenzao. 0:07:26.084,0:07:28.671 Ikiwa kamwe hakuna anayeomba msaada, 0:07:28.721,0:07:30.763 utakuwa na watoaji wengi waliokatishwa tamaa, 0:07:30.763,0:07:32.706 ambao wangependa kuchangia kwa kusaidia, 0:07:32.730,0:07:34.896 laiti wangejua nani anahitaji msaada na kwa namna gani. 0:07:35.413,0:07:37.211 Lakini jambo muhimu zaidi kama 0:07:37.235,0:07:39.711 unataka kujenga utamaduni[br]ambapo watoaji wanafanikiwa, 0:07:39.735,0:07:42.537 ni kuwa mwangalifu kuhusu nani[br]unaweka kwenye timu yako. 0:07:42.561,0:07:45.577 Kama unataka utamaduni[br]wa ukarimu na uzalishaji, 0:07:45.601,0:07:47.573 unapaswa kuajiri watoaji. 0:07:47.597,0:07:51.267 Lakini nilishangaa kugundua kwamba hiyo haikuwa sahihi -- 0:07:51.715,0:07:54.190 mapungufu ya mpokeaji 0:07:54.214,0:07:57.083 ni mara mbili au mara tatu[br]zaidi kuliko manufaa ya mtoaji. 0:07:57.530,0:07:58.680 Ifiikirie hivi: 0:07:58.704,0:08:00.368 tunda moja baya linaweza kuharibu kikapu chote, 0:08:00.392,0:08:03.218 lakini yai moja nzuri haliwezi kuboresha dazeni nzima. 0:08:03.942,0:08:05.494 Sijui hii ina maana gani-- 0:08:05.518,0:08:06.637 (Vicheko) 0:08:06.661,0:08:08.034 Lakini natumaini mnaelewa. 0:08:08.058,0:08:11.380 Yani-- weka hata mpokeaji mmoja kwenye timu, 0:08:11.404,0:08:14.258 na utaona kwamba watoaji[br]wataacha kusaidia. 0:08:14.648,0:08:17.578 Watasema, "Nimezungukwa[br]na rundo la nyoka na papa. 0:08:17.602,0:08:18.968 Kwa nini mimi nichangie? " 0:08:18.992,0:08:20.968 Wakati, ukiweka mtoaji mmoja kwenye timu, 0:08:20.992,0:08:23.114 huwezi kupata mlipuko wa ukarimu. 0:08:23.138,0:08:24.559 Mara nyingi zaidi, watu hufikiri, 0:08:24.583,0:08:26.721 "Afadhali! Huyo anaweza kufanya kazi yetu yote." 0:08:27.077,0:08:29.823 Hivyo, ufanisi katika kuajiri na kujenga timu 0:08:29.847,0:08:31.983 haihusishi kuleta pamoja watoaji tu; 0:08:32.007,0:08:34.221 ila pia kuwatoa wapokeaji nje ya shirika. 0:08:35.036,0:08:36.187 Ukifanikiwa, 0:08:36.211,0:08:38.153 utabakiza watoaji na walipizaji. 0:08:38.177,0:08:39.542 Watoaji watakuwa wakarimu 0:08:39.566,0:08:42.200 kwa sababu hawana wasiwasi[br]kuhusu kupokea fadhila. 0:08:42.224,0:08:45.337 Na uzuri wa walipizaji ni kwamba wanafuata musuada uliopo. 0:08:45.361,0:08:48.129 Hivyo ni jinsi gani utamtambua mpokeaji, mapema? 0:08:48.745,0:08:51.632 Sio rahisi kumtambua mpokeaji 0:08:51.656,0:08:53.482 hasa kufuata tu hisia zetu za mwanzo. 0:08:53.506,0:08:55.814 Kuna tabia ambayo hutupotosha . 0:08:55.838,0:08:57.143 Inaitwa wito upendezi, 0:08:57.167,0:08:58.167 kati ya vipimo vikuu vya hulka 0:08:58.167,0:08:59.812 miongoni mwa tamaduni mbalimbali. 0:08:59.812,0:09:03.102 Watu wapendezi ni wakarimu, wema, wanyenyekevu. 0:09:03.321,0:09:05.112 Utawakuta wengi wao Kanada -- 0:09:05.136,0:09:06.739 (Vicheko) 0:09:06.763,0:09:10.260 Ambapo kulikuwa na shindano la kitaifa 0:09:10.284,0:09:13.314 la kutafuta kauli mbiu mpya ya Kanada[br]kwa kujaza tashbihi, 0:09:13.338,0:09:14.913 "Mkanada kama ..." 0:09:14.937,0:09:17.021 Nilidhani kauli mbiu itakayoshinda ingekuwa, 0:09:17.045,0:09:19.516 "Mkanada kama maple syrup,"[br]au, "... Hoki ya barafuni ." 0:09:19.540,0:09:22.525 Lakini, hapana. Kura zilichagua kauli mbiu mpya kuwa - 0:09:22.549,0:09:23.710 na siwatanii -- 0:09:23.734,0:09:26.165 "Mkanada kama iwezekanavyo,[br]katika mazingira haya. " 0:09:26.189,0:09:29.402 (Vicheko) 0:09:30.020,0:09:32.391 Sasa kwa wale ambao ni wapendezi, 0:09:32.415,0:09:33.808 au labda ni wakanada kidogo 0:09:33.832,0:09:35.205 mtaielewa upesi. 0:09:35.229,0:09:37.046 Ninawezaje kusema kuwa mimi ni aina moja pekee 0:09:37.070,0:09:39.896 wakati daima ninajibadilisha kuridhisha wengine? 0:09:40.400,0:09:42.223 Watu nongwa hujaribu mara chache zaidi. 0:09:42.247,0:09:45.184 Hawa, wana mashaka, ni wakasoaji, ni changamoto 0:09:45.208,0:09:48.262 na ndio wenye kwenda kusoma sheria. 0:09:48.286,0:09:49.429 (Vicheko) 0:09:49.453,0:09:52.108 Hiyo sio utani; ni kweli kama kanuni. 0:09:52.132,0:09:53.191 (Vicheko) 0:09:53.215,0:09:55.764 daima nildhani watu wapendezi ni watoaji 0:09:55.788,0:09:57.735 na watu nongwa ni wapokeaji. 0:09:57.759,0:09:59.189 Nilipofanya utafiti, 0:09:59.213,0:10:02.326 nilistaajabu kukuta hakuna uhusiano katika sifa hizo, 0:10:02.350,0:10:05.009 kwa sababu tabia ya upendezi au nongwa 0:10:05.033,0:10:06.196 ni gamba la nje tu: 0:10:06.220,0:10:08.161 Je, watu wanajisikiaje baada ya kuzungumza na wewe? 0:10:08.185,0:10:10.877 Wakati kutoa na kupokea inategemea nia yako: 0:10:10.901,0:10:13.793 Je, maadili yako ni yapi?[br]Je, nia yako kwa wengine ni ipi? 0:10:13.817,0:10:16.009 Kama unataka kusoma watu kwa usahihi, 0:10:16.033,0:10:19.550 utataka kuwepo katika chumba wakati kila mshauri anasubiri, 0:10:19.574,0:10:20.739 kupata picha halisi. 0:10:20.763,0:10:24.371 (Vicheko) 0:10:25.321,0:10:27.655 Ni rahisi kuwatambua watoaji wapendezi: 0:10:27.679,0:10:30.313 wao husema ndiyo kwa kila kitu. 0:10:31.740,0:10:34.613 Wapokeaji nongwa wanatambulika kirahisi pia, 0:10:34.637,0:10:38.544 ingawa unaweza kuwaita[br]kwa jina tofauti kidogo. 0:10:38.568,0:10:40.432 (Vicheko) 0:10:41.828,0:10:43.900 Tunasahau makundi mengine mbili. 0:10:43.924,0:10:47.259 Kuna watoaji nongwa[br]katika mashirika. 0:10:47.283,0:10:49.924 Hawa wanaonekana wagumu kwa nje 0:10:49.948,0:10:52.486 lakini hujali sana maslahi ya wengine. 0:10:53.089,0:10:54.452 Au kama mhandisi anavyoiweka, 0:10:54.476,0:10:56.082 "Ah, watoaji nongwa ni - 0:10:56.082,0:10:57.502 kama mtu mwenye kiolesura kibaya cha mtumiaji 0:10:57.586,0:11:00.006 lakini mfumo mzuri." 0:11:00.006,0:11:01.292 (Vicheko) 0:11:01.316,0:11:02.687 Kama inawasaidia. 0:11:02.711,0:11:03.951 (Vicheko) 0:11:04.424,0:11:07.927 Watoaji nongwa hawathaminiwi katika mashirika yetu, 0:11:07.951,0:11:10.543 kwa sababu huotoa changamoto 0:11:10.567,0:11:13.173 ambazo watu hawataki kusikia[br]hata kama tunahizitaji. 0:11:13.197,0:11:15.685 Tunahitaji kuwathamini zaidi[br]watu hawa 0:11:15.709,0:11:17.497 badala ya kuwapuuza, 0:11:17.521,0:11:19.265 na kusema, "Eh, wanakera, 0:11:19.289,0:11:20.786 lazima awe mpokeaji nongwa." 0:11:21.849,0:11:24.608 Kundi jingine hatari tunasahau ni- 0:11:24.632,0:11:27.314 mpokeaji mpendezi, pia anajulikana kama muigizaji. 0:11:28.444,0:11:30.509 Huyu ni mtu mwema akiwa mbele yako, 0:11:30.533,0:11:32.513 na ukigeuka hukuchoma. 0:11:32.537,0:11:33.869 (Vicheko) 0:11:34.537,0:11:37.771 Napenda kuwakamata[br]hawa watu katika usahili 0:11:37.795,0:11:39.067 kwa kuuliza swali, 0:11:39.091,0:11:41.053 "Je, unaweza kunipa majina ya watu wanne 0:11:41.077,0:11:43.446 ambao umewasaidia kimsingi kazini?" 0:11:44.424,0:11:46.317 Wapokeaji watakupa hayo majina manne, 0:11:46.341,0:11:49.038 na wote watakuwa na mafinikio zaidi kuliko wao, 0:11:49.062,0:11:50.062 kwa sababu wapokeaji ni wastadi katika kunyenyekea 0:11:50.062,0:11:52.957 wakuu wao na kudharau walio chini. 0:11:52.957,0:11:56.357 Watoaji wanajua zaidi majina ya watu chini ya uongozi wao, 0:11:56.381,0:11:57.927 ambao hawana mamlaka mingi, 0:11:57.951,0:11:59.323 ambao hawana mchango muhimu kwao. 0:11:59.723,0:12:02.897 Hakika, tunafahamu kuwa tunajifunza mengi kuhusu tabia ya mtu 0:12:02.921,0:12:05.476 kwa kumuangalia anavyohusiana na mhudumu 0:12:05.500,0:12:06.663 au dereva wa Uber. 0:12:07.319,0:12:08.585 Hivyo tukifanya yote vizuri, 0:12:08.609,0:12:10.693 kama tutatoa wapokeaji katika mashirika, 0:12:10.717,0:12:12.629 kama tutaweza kuwahakikishia usalama wanaoomba msaada, 0:12:12.653,0:12:14.667 kama tutaweza kuwalinda watoaji wasichoke 0:12:14.691,0:12:17.918 na kuwawezesha kutimiza malengo yao 0:12:17.942,0:12:20.098 na pia kusaidia watu wengine, 0:12:20.122,0:12:21.122 tunaweza kubadilisha mtizamo wa watu 0:12:21.122,0:12:23.053 wanavyotizama mafanikio. 0:12:23.053,0:12:26.405 Badala ya kuona ni mashindano, 0:12:26.429,0:12:29.969 watu watatambua mafanikio kama mchango kijumuiya zaidi. 0:12:30.761,0:12:33.122 Naamini kuwa njia kuu ya kufanikiwa 0:12:33.146,0:12:35.016 ni kuwasaidia watu wengine wafanikiwe. 0:12:35.040,0:12:36.711 Na kama tunaweza kusambaza imani hio, 0:12:36.735,0:12:39.386 tunaweza kweli kuigeuza paranoia. 0:12:39.410,0:12:40.573 Kuna jina kwa ajili hiyo 0:12:40.597,0:12:42.033 inaitwa "pronoia." 0:12:43.025,0:12:44.722 Pronoia ni imani kwamba 0:12:44.746,0:12:47.346 wengine wanapanga mema kwa ajili yako. 0:12:47.370,0:12:48.893 (Vicheko) 0:12:50.908,0:12:53.461 Kwamba wanakuzunguka 0:12:53.485,0:12:56.401 na kuimba sifa zako. 0:12:57.647,0:13:01.456 Uzuri wa utamaduni wa watoaji[br]ni kwamba hio sio njozi, 0:13:01.480,0:13:02.714 huo ndio uhalisia. 0:13:03.697,0:13:06.273 Ningependa kuishi kwenye dunia ambayo watoaji wanafanikiwa. 0:13:06.297,0:13:08.613 Natumaini nyote mtanisaidia kujenga ulimwengu huo. 0:13:08.653,0:13:09.383 Asanteni. 0:13:09.893,0:13:10.473 (Makofi)