-
Hamjambo. Kipindi hiki kinawajieni kutoka
Ohio
-
ambako kwa maeneo mengine watu wanasubiri
kwenye foleni ndefu ili kupiga kura.
-
Wiki chache tu zilizopita, hapa katika
Jimbo la Buckeye,
-
kura zisizo sahihi zilipatikana kwa
wapiga kura 50,000 wa Franklin County.
-
Rais alisema ulikuwa uchaguzi wa ulaghai,
usiodhibitika na wa hila.
-
Kaunti iliarifu kuwa ilikuwa hitilafu
kubwa
-
ambayo walikuwa wanajitahidi
kushughulikia.
-
Tunaona simulizi kama hizi kote nchini.
-
"Kisanduku kisicho rasmi cha kura,"
-
"Kebo iliyokatwa ilizima tovuti ya
wapiga kura wa Virginia,"
-
"Mashine za kupiga kura wazi kwa
wadukuzi wa Kirusi,"
-
kila siku na mada mpya ya habari.
-
Msimu wa uchaguzi wa mwaka huu ni
muhimu zaidi kwa 2020.
-
Unawezaje kupita taarifa hizi zisizo
sahihi?
-
Hujambo, mimi ni Hari Sreenivasan.
Karibu kwa Take On Fake
-
ambapo tunafichua madai ambayo
huenda umeona au hata kushiriki mtandaoni.
-
Uchaguzi umekaribia.
-
Kuna hatari kubwa.
-
Pia kuna taarifa nyingi za kupotosha.
-
Wiki chache zilizopita,
-
tulizungumza na mwanahabari aliyefichua
hadithi tatu tofauti kuhusu upigaji kura
-
katika majimbo matatu tofauti:
Illinois, California na Washington.
-
Kuna balagha na madai mengi ya uongo
na ya kupotosha kuhusu mchakato huo.
-
Nafikiri ni muhimu zaidi kuwa sisi,
kama wanaohakikisha ukweli,
-
lakini pia kila Mwamerika apinge madai
hayo ambayo hayajahakikishwa
-
kwa sababu yanadhoofisha demokrasia
yetu mwisho wa siku.
-
Mwanahabari Angelo Fichera kutoka
FactCheck.org
-
alituonyesha mojawapo ya hadithi zake,
kuhusu vitambulisho bandia huko Illinois.
-
Chapisho kwenye Facebook liliripoti kuliwa
na karibu vitambulisho 20,000 bandia
-
na kuwa vyote vilihusishwa na usajili
wa kidemokrasia wa wapiga kura.
-
Kwa hivyo hawa ndio watu ambao -
-
wangejisajili kwa njia haramu ili kupiga
kura kwa kutumia leseni hizi za udereva?
-
Hilo ndilo lilikuwa athari.
-
Hivyo jambo la kwanza ambalo ningefanya
ni kutafuta maandishi hayo kwenye Google.
-
Na katika hali hii, nilielekezwa kwa
tovuti ya kipindi cha mazunguzo cha redio
-
ambayo ilitumia karibu maandishi
sawa kama mada yake.
-
Kwa hivyo nilitazama makala hayo kubaini
iwapo ushahidi wowote wa dai hili upo
-
kuwa vitambulisho vilihusishwa na
usajili wa wapiga kura.
-
Ukiangalia simulizi kwa karibu
na kutafuta maelezo yoyote,
-
utagundua kuwa hakukuwa na
uthibitishaji wa madai hayo
-
kuwa simulizi linataja idara ya Forodha
na Ulinzi wa Mipaka ya Marekani
-
na inahusisha maelezo kuhusu vitambulisho
bandia na shirika hilo la serikali.
-
Kwa hivyo nilifanya utafutaji kwa kutumia
nambari mahususi za vitambulisho bandia
-
na Idara ya Forodha ya Ulinzi wa Mipaka,
-
na niliona hati kwa wanahabari iliyotolewa
na shirika hilo mwishoni mwa Julai.
-
Hamna mahali kulikotajwa
vitambulisho bandia
-
vinavyohusishwa na usajili wa wapiga
kura, ulaghai wa kura.
-
Yote waliyosema ni kuwa ilikuwa inalenga
wanafunzi wa umri wa chuo
-
katika majimbo ya karibu.
-
Sawa, nikiwa nimewahi kupitia chuo,
-
Nafikiri kuna uwezekano kuwa kuna
soko kubwa ya wanafunzi
-
ambao huenda wanajaribu kuingia katika
vilabu kwa kutumia vitambulisho bandia.
-
Sijui iwapo upigaji kura ni jambo ambalo
wanajaribu kufanya, lakini ...
-
Huko Illinois, iwapo mtu atajaribu
kujisajili,
-
watakagua nambari hizo dhidi ya nambari
walizo nazo katika hifadhidata zao,
-
kwa hivyo mikakati ya usalama imewekwa
-
ili kuzuia aina hiyo ya
usajili wa ulaghai wa wapiga kura.
-
Lakini hilo silo tukio pekee la
maelezo ya kupotosha kuhusu uchaguzi
-
ambalo Angelo alifichua hivi majuzi.
-
Tweet iliyosambaa ilidai kulikuwa na
zaidi ya kura 1,000 za barua pepe
-
zilizopatikana kwenye bomba la taka
katika jimbo la California.
-
Lakini kupitia utafutaji wa maneno
muhimu, Angelo aligundua kuwa
-
picha hiyo ilionyesha bahasha mpya
kutoka kwa uchaguzi wa kati wa 2018,
-
na zilikuwa zimetupwa kwa njia haramu.
-
Kaunti ya Sonoma pia ilibainisha kuwa
wakati wa kutolewa kwa tweet hivyo,
-
kura za 2020 bado hazikuwa zimetumwa.
-
Simulizi la tatu - hili kutoka jimbo la
Washington - picha inayodai
-
maelfu ya Wanademokrasia wa Seattle wame
kutana kutaka upigaji kura wa barua pepe
-
kwa sababu ni hatari kupiga kura
moja kwa moja.
-
Ili kufichua hili, Angelo alifanya
utafutaji kwa kutumia picha
-
na akagundua kuwa picha hii haikuhusiana
kabisa na mchakato wa kupiga kura.
-
Picha hii ilitoka kwa maandamano ya
Black Lives Matter miezi 2 awali.
-
Tukirejelea tweet hiyo halisi,
-
utagunduaa kuwa mchapishaji halisi ni
akaunti inayoitwa Walter Cronkite.
-
Sote tunafahamu kuwa Walter Cronkite
alikuwa mwanahabari aliyeheshimiwa
-
ambayo mara nyingi alirejelewa kuwa mtu
anayeaminika zaidi nchini Marekani.
-
Kweli, "alikuwa" kwa sababu alifariki
miaka 11 iliyopita.
-
Kwa hivyo hii si tweet kutoka kwa
Walter Cronkite halisi.
-
Akaunti inatoa taarifa hapo,
-
lakini iwapo unapitia tu simu yako,
-
huenda usielewe hilo mara moja.
-
Huenda ukaona jina Walter Cronkite
-
na uamini tweet hiyo zaidi kuliko
inayohitajika
-
Ukiwa na maelezo haya ya kupotosha;
-
wahakikishaji wa ukweli kama Angelo
wanafanya nini ili kuandaa?
-
Tunakuwa makini zaidi
-
na kuwa tayari kukabili kitakachokuwa
maelezo mengi ya kupotosha,
-
lakini tunahitaji usaidizi wa umma, pia,
-
ili kuripoti mambo kwa wanaohakikisha
ukweli.
-
Tuna barua pepe.
tuna akaunti za mitandao jamii.
-
Na iwapo watu wana maswali,
tungependa kuwasaidia.
-
Kitakachofanyika katika siku
chache zijazo,
-
kitatuhitaji tutulie
-
inapofika kwa mada, tweets na
machapisho yanayotutisha na kutukasirisha.
-
Iwapo historia ni kiashirio chochote,
-
maelezo ya kupotosha kuhusu
uchaguzi yatakuwa kila mahali.
-
Kwa hivyo ni jukumu letu kuchunguza
zaidi na kutafuta vyanzo vinavyoaminika.
-
Hadi wakati mwingine.
-
Usisambaze habari bandia.
Kuwa wa kweli.
-
Mimi ni Hari Sreenivasan na hii ni
Take on Fake.
-
Asante kwa kutazama.
-
Tungependa kupata maoni yako.
-
Shiriki simulizi au mpango wako
wa kupiga kura katika maoni hapa chini.
-
Je, ulipiga kura kupitia barua pepe?
-
Je, unapanga kupiga mwenyewe?
-
Je, wewe ni mpigaji kura wa mapema
ambaye bado anasubiri kwenye foleni?
-
Kipindi chetu cha mwisho cha msimu
hakitakuja hadi baada ya uchaguzi.
-
Kwa hivyo tutaonana baada ya uchaguzi.