1 00:00:00,000 --> 00:00:02,468 Hamjambo. Kipindi hiki kinawajieni kutoka Ohio 2 00:00:02,468 --> 00:00:07,682 ambako kwa maeneo mengine watu wanasubiri kwenye foleni ndefu ili kupiga kura. 3 00:00:07,762 --> 00:00:10,930 Wiki chache tu zilizopita, hapa katika Jimbo la Buckeye, 4 00:00:10,930 --> 00:00:16,380 kura zisizo sahihi zilipatikana kwa wapiga kura 50,000 wa Franklin County. 5 00:00:16,634 --> 00:00:20,534 Rais alisema ulikuwa uchaguzi wa ulaghai, usiodhibitika na wa hila. 6 00:00:20,966 --> 00:00:23,110 Kaunti iliarifu kuwa ilikuwa hitilafu kubwa 7 00:00:23,110 --> 00:00:25,253 ambayo walikuwa wanajitahidi kushughulikia. 8 00:00:25,253 --> 00:00:27,777 Tunaona simulizi kama hizi kote nchini. 9 00:00:27,777 --> 00:00:29,778 "Kisanduku kisicho rasmi cha kura," 10 00:00:29,778 --> 00:00:32,637 "Kebo iliyokatwa ilizima tovuti ya wapiga kura wa Virginia," 11 00:00:32,645 --> 00:00:35,179 "Mashine za kupiga kura wazi kwa wadukuzi wa Kirusi," 12 00:00:35,279 --> 00:00:37,284 kila siku na mada mpya ya habari. 13 00:00:37,284 --> 00:00:40,683 Msimu wa uchaguzi wa mwaka huu ni muhimu zaidi kwa 2020. 14 00:00:40,683 --> 00:00:43,672 Unawezaje kupita taarifa hizi zisizo sahihi? 15 00:00:44,124 --> 00:00:46,890 Hujambo, mimi ni Hari Sreenivasan. Karibu kwa Take On Fake 16 00:00:46,900 --> 00:00:50,856 ambapo tunafichua madai ambayo huenda umeona au hata kushiriki mtandaoni. 17 00:00:50,856 --> 00:00:52,758 Uchaguzi umekaribia. 18 00:00:52,758 --> 00:00:54,166 Kuna hatari kubwa. 19 00:00:54,166 --> 00:00:56,263 Pia kuna taarifa nyingi za kupotosha. 20 00:00:56,263 --> 00:00:57,386 Wiki chache zilizopita, 21 00:00:57,496 --> 00:01:01,405 tulizungumza na mwanahabari aliyefichua hadithi tatu tofauti kuhusu upigaji kura 22 00:01:01,435 --> 00:01:05,382 katika majimbo matatu tofauti: Illinois, California na Washington. 23 00:01:05,385 --> 00:01:11,247 Kuna balagha na madai mengi ya uongo na ya kupotosha kuhusu mchakato huo. 24 00:01:11,404 --> 00:01:14,741 Nafikiri ni muhimu zaidi kuwa sisi, kama wanaohakikisha ukweli, 25 00:01:14,741 --> 00:01:21,510 lakini pia kila Mwamerika apinge madai hayo ambayo hayajahakikishwa 26 00:01:21,643 --> 00:01:25,549 kwa sababu yanadhoofisha demokrasia yetu mwisho wa siku. 27 00:01:25,549 --> 00:01:28,150 Mwanahabari Angelo Fichera kutoka FactCheck.org 28 00:01:28,150 --> 00:01:31,969 alituonyesha mojawapo ya hadithi zake, kuhusu vitambulisho bandia huko Illinois. 29 00:01:32,269 --> 00:01:36,237 Chapisho kwenye Facebook liliripoti kuliwa na karibu vitambulisho 20,000 bandia 30 00:01:36,237 --> 00:01:40,541 na kuwa vyote vilihusishwa na usajili wa kidemokrasia wa wapiga kura. 31 00:01:40,541 --> 00:01:42,986 Kwa hivyo hawa ndio watu ambao - 32 00:01:43,256 --> 00:01:47,149 wangejisajili kwa njia haramu ili kupiga kura kwa kutumia leseni hizi za udereva? 33 00:01:47,209 --> 00:01:48,580 Hilo ndilo lilikuwa athari. 34 00:01:48,620 --> 00:01:54,333 Hivyo jambo la kwanza ambalo ningefanya ni kutafuta maandishi hayo kwenye Google. 35 00:01:54,333 --> 00:01:58,631 Na katika hali hii, nilielekezwa kwa tovuti ya kipindi cha mazunguzo cha redio 36 00:01:58,631 --> 00:02:02,795 ambayo ilitumia karibu maandishi sawa kama mada yake. 37 00:02:02,795 --> 00:02:07,114 Kwa hivyo nilitazama makala hayo kubaini iwapo ushahidi wowote wa dai hili upo 38 00:02:07,114 --> 00:02:09,900 kuwa vitambulisho vilihusishwa na usajili wa wapiga kura. 39 00:02:09,910 --> 00:02:14,132 Ukiangalia simulizi kwa karibu na kutafuta maelezo yoyote, 40 00:02:14,132 --> 00:02:17,499 utagundua kuwa hakukuwa na uthibitishaji wa madai hayo 41 00:02:17,499 --> 00:02:20,885 kuwa simulizi linataja idara ya Forodha na Ulinzi wa Mipaka ya Marekani 42 00:02:20,885 --> 00:02:26,242 na inahusisha maelezo kuhusu vitambulisho bandia na shirika hilo la serikali. 43 00:02:26,242 --> 00:02:30,143 Kwa hivyo nilifanya utafutaji kwa kutumia nambari mahususi za vitambulisho bandia 44 00:02:30,143 --> 00:02:32,480 na Idara ya Forodha ya Ulinzi wa Mipaka, 45 00:02:32,480 --> 00:02:38,886 na niliona hati kwa wanahabari iliyotolewa na shirika hilo mwishoni mwa Julai. 46 00:02:38,933 --> 00:02:41,918 Hamna mahali kulikotajwa vitambulisho bandia 47 00:02:41,918 --> 00:02:45,770 vinavyohusishwa na usajili wa wapiga kura, ulaghai wa kura. 48 00:02:45,770 --> 00:02:50,113 Yote waliyosema ni kuwa ilikuwa inalenga wanafunzi wa umri wa chuo 49 00:02:50,113 --> 00:02:51,624 katika majimbo ya karibu. 50 00:02:51,624 --> 00:02:54,074 Sawa, nikiwa nimewahi kupitia chuo, 51 00:02:54,564 --> 00:03:00,547 Nafikiri kuna uwezekano kuwa kuna soko kubwa ya wanafunzi 52 00:03:00,547 --> 00:03:04,256 ambao huenda wanajaribu kuingia katika vilabu kwa kutumia vitambulisho bandia. 53 00:03:04,316 --> 00:03:08,636 Sijui iwapo upigaji kura ni jambo ambalo wanajaribu kufanya, lakini ... 54 00:03:08,684 --> 00:03:12,005 Huko Illinois, iwapo mtu atajaribu kujisajili, 55 00:03:12,005 --> 00:03:16,282 watakagua nambari hizo dhidi ya nambari walizo nazo katika hifadhidata zao, 56 00:03:16,306 --> 00:03:18,476 kwa hivyo mikakati ya usalama imewekwa 57 00:03:18,476 --> 00:03:23,010 ili kuzuia aina hiyo ya usajili wa ulaghai wa wapiga kura. 58 00:03:23,010 --> 00:03:26,278 Lakini hilo silo tukio pekee la maelezo ya kupotosha kuhusu uchaguzi 59 00:03:26,408 --> 00:03:28,175 ambalo Angelo alifichua hivi majuzi. 60 00:03:28,195 --> 00:03:31,668 Tweet iliyosambaa ilidai kulikuwa na zaidi ya kura 1,000 za barua pepe 61 00:03:31,668 --> 00:03:34,707 zilizopatikana kwenye bomba la taka katika jimbo la California. 62 00:03:34,717 --> 00:03:37,793 Lakini kupitia utafutaji wa maneno muhimu, Angelo aligundua kuwa 63 00:03:37,813 --> 00:03:41,588 picha hiyo ilionyesha bahasha mpya kutoka kwa uchaguzi wa kati wa 2018, 64 00:03:41,998 --> 00:03:45,970 na zilikuwa zimetupwa kwa njia haramu. 65 00:03:46,860 --> 00:03:50,379 Kaunti ya Sonoma pia ilibainisha kuwa wakati wa kutolewa kwa tweet hivyo, 66 00:03:50,379 --> 00:03:53,489 kura za 2020 bado hazikuwa zimetumwa. 67 00:03:53,579 --> 00:03:56,978 Simulizi la tatu - hili kutoka jimbo la Washington - picha inayodai 68 00:03:56,988 --> 00:04:00,791 maelfu ya Wanademokrasia wa Seattle wame kutana kutaka upigaji kura wa barua pepe 69 00:04:00,791 --> 00:04:03,629 kwa sababu ni hatari kupiga kura moja kwa moja. 70 00:04:03,907 --> 00:04:07,176 Ili kufichua hili, Angelo alifanya utafutaji kwa kutumia picha 71 00:04:07,176 --> 00:04:11,737 na akagundua kuwa picha hii haikuhusiana kabisa na mchakato wa kupiga kura. 72 00:04:11,793 --> 00:04:15,880 Picha hii ilitoka kwa maandamano ya Black Lives Matter miezi 2 awali. 73 00:04:17,853 --> 00:04:20,167 Tukirejelea tweet hiyo halisi, 74 00:04:20,167 --> 00:04:24,088 utagunduaa kuwa mchapishaji halisi ni akaunti inayoitwa Walter Cronkite. 75 00:04:24,088 --> 00:04:27,519 Sote tunafahamu kuwa Walter Cronkite alikuwa mwanahabari aliyeheshimiwa 76 00:04:27,709 --> 00:04:31,756 ambayo mara nyingi alirejelewa kuwa mtu anayeaminika zaidi nchini Marekani. 77 00:04:31,756 --> 00:04:34,786 Kweli, "alikuwa" kwa sababu alifariki miaka 11 iliyopita. 78 00:04:34,796 --> 00:04:37,524 Kwa hivyo hii si tweet kutoka kwa Walter Cronkite halisi. 79 00:04:37,524 --> 00:04:39,085 Akaunti inatoa taarifa hapo, 80 00:04:39,085 --> 00:04:42,100 lakini iwapo unapitia tu simu yako, 81 00:04:42,100 --> 00:04:44,649 huenda usielewe hilo mara moja. 82 00:04:45,099 --> 00:04:46,919 Huenda ukaona jina Walter Cronkite 83 00:04:46,919 --> 00:04:50,428 na uamini tweet hiyo zaidi kuliko inayohitajika 84 00:04:50,899 --> 00:04:52,746 Ukiwa na maelezo haya ya kupotosha; 85 00:04:52,926 --> 00:04:55,988 wahakikishaji wa ukweli kama Angelo wanafanya nini ili kuandaa? 86 00:04:55,988 --> 00:04:58,743 Tunakuwa makini zaidi 87 00:04:58,743 --> 00:05:03,231 na kuwa tayari kukabili kitakachokuwa maelezo mengi ya kupotosha, 88 00:05:03,231 --> 00:05:07,118 lakini tunahitaji usaidizi wa umma, pia, 89 00:05:07,118 --> 00:05:09,718 ili kuripoti mambo kwa wanaohakikisha ukweli. 90 00:05:09,718 --> 00:05:12,178 Tuna barua pepe. tuna akaunti za mitandao jamii. 91 00:05:12,178 --> 00:05:14,692 Na iwapo watu wana maswali, tungependa kuwasaidia. 92 00:05:14,792 --> 00:05:16,851 Kitakachofanyika katika siku chache zijazo, 93 00:05:16,866 --> 00:05:19,582 kitatuhitaji tutulie 94 00:05:19,582 --> 00:05:24,710 inapofika kwa mada, tweets na machapisho yanayotutisha na kutukasirisha. 95 00:05:24,740 --> 00:05:26,841 Iwapo historia ni kiashirio chochote, 96 00:05:26,851 --> 00:05:29,635 maelezo ya kupotosha kuhusu uchaguzi yatakuwa kila mahali. 97 00:05:29,735 --> 00:05:35,006 Kwa hivyo ni jukumu letu kuchunguza zaidi na kutafuta vyanzo vinavyoaminika. 98 00:05:35,006 --> 00:05:36,039 Hadi wakati mwingine. 99 00:05:36,039 --> 00:05:37,909 Usisambaze habari bandia. Kuwa wa kweli. 100 00:05:37,989 --> 00:05:40,302 Mimi ni Hari Sreenivasan na hii ni Take on Fake. 101 00:05:40,347 --> 00:05:41,422 Asante kwa kutazama. 102 00:05:42,112 --> 00:05:43,547 Tungependa kupata maoni yako. 103 00:05:43,627 --> 00:05:47,021 Shiriki simulizi au mpango wako wa kupiga kura katika maoni hapa chini. 104 00:05:47,061 --> 00:05:48,816 Je, ulipiga kura kupitia barua pepe? 105 00:05:48,946 --> 00:05:50,368 Je, unapanga kupiga mwenyewe? 106 00:05:50,514 --> 00:05:53,922 Je, wewe ni mpigaji kura wa mapema ambaye bado anasubiri kwenye foleni? 107 00:05:54,136 --> 00:05:58,112 Kipindi chetu cha mwisho cha msimu hakitakuja hadi baada ya uchaguzi. 108 00:05:58,352 --> 00:06:00,236 Kwa hivyo tutaonana baada ya uchaguzi.