"Hatusongi mbele" kwenye maombolezo. Tunaendelea nayo mbele
-
0:01 - 0:03Mwaka 2014 ulikua ,mkubwa kwangu.
-
0:03 - 0:05Ulishawahi kuwa na hio,
-
0:05 - 0:07kama tu mwaka mkubwa, kama mwaka bango?
-
0:07 - 0:09Kwangu, ulienda hivi:
-
0:09 - 0:12Oktoba 3, nilipoteza ujauzito wangu wa
pili. -
0:12 - 0:15Halfu Oktoba 3, baba yangu alifariki kwa
saratani. -
0:15 - 0:18Halafu tena Novemba 25,
mme wangu Aaron alifariki -
0:18 - 0:21baada ya miaka mitatu
ya hatua ya nne ya glioblastoma, -
0:21 - 0:23ambalo ni neno la mbwembwe
la saratani ya ubongo. -
0:25 - 0:26Hivyo, nina vichekesho.
-
0:27 - 0:28(Kicheko)
-
0:28 - 0:32Watu wanapenda kunialika sehemu kila mara.
-
0:32 - 0:33Maingiano kibao.
-
0:33 - 0:36Kawaida, ninapoongelea
hiki kipindi cha maisha yangu, -
0:36 - 0:40majibu ninayopata kimsingi ni:
-
0:40 - 0:42(Mhemo)
-
0:42 - 0:43"Siwezi -- siwezi kufikiria."
-
0:45 - 0:47Lakini ninafikiri unaweza.
-
0:48 - 0:49Ninafikiri unaweza.
-
0:49 - 0:50Na ninafikiri kua unatakiwa
-
0:50 - 0:53kwa sababu, siku moja,
itakutokea wewe. -
0:53 - 0:58Labda sio hizi hasara kabisa
kwenye namna hii maalum au kwa kazi hii, -
0:58 - 0:59ila nimesema, nina vichekesho
-
0:59 - 1:03na utafiti nilioona
utakushangaza: -
1:03 - 1:06kila mtu unaempenda ana
nafasi asilimia 100 ya kufa. -
1:06 - 1:09(Kicheko)
-
1:09 - 1:11Na ndio maana ukaja TED.
-
1:11 - 1:13(Kicheko)
-
1:13 - 1:16(Makofi)
-
1:16 - 1:18Tangu hasara yote ilivyonitokea,
-
1:18 - 1:22nimefanya kazi kuongelea kuhusu kifo na
hasara, -
1:22 - 1:25sio yangu tu,
kwa sababu ni rahisi kukumbuka, -
1:25 - 1:29lakini hasara na mikasa
ambayo watu wengine wamepitia. -
1:29 - 1:31Ni sehemu, naweza kusema.
-
1:31 - 1:33(Kicheko)
-
1:33 - 1:36Ni sehemu ndogo, na natamani
ningekua na hela nyingi, lakini ... -
1:36 - 1:37(Kicheko)
-
1:37 - 1:41Nimeandika vitabu vya kuinua kweli,
-
1:41 - 1:44nikaendesha podikasti ya kuinua sana,
nikaanzaisha shirika lisilo la serikali. -
1:44 - 1:46Ninajaribu tu kufanya ninachoweza
-
1:46 - 1:49kufanya watu wengi zaidi wafarijike
kwenye hali zilizo ngumu, -
1:50 - 1:52na majonzi ni magumu sana.
-
1:52 - 1:56Ni magumu sana, haswa
kama ni majonzi ya mtu mwingine. -
1:57 - 2:02Basi sehemu ya hio kazi ni hili kundi
nililoanzisha na rafiki yangu Moe, -
2:02 - 2:03ambae pia ni mjane;
-
2:03 - 2:05tunaliita Chama cha Wajane Wadogo Wakali.
-
2:05 - 2:07(Kicheko)
-
2:07 - 2:09Na ni ukweli, tuna kadi za uwanachama
-
2:09 - 2:11na tisheti.
-
2:11 - 2:15Na pale mtu wako akifariki,
mmeo, mke, mchumba, -
2:15 - 2:17hatujali kabisa kama ulikua kwenye ndoa,
-
2:17 - 2:20marafiki zako na familia yako
watakua tu wanaangalia -
2:20 - 2:22kwa marafiki wa marafiki
wa marafiki wa marafiki -
2:22 - 2:25mpaka wapate mtu
ambae amepitia hali inayofanana, -
2:25 - 2:27halafu watawasukuma
mje pamoja -
2:27 - 2:32ili muongee miongoni mwenu na msiwe
na masikitiko kwa watu wengine. -
2:32 - 2:34(Kicheko)
-
2:34 - 2:35Basi ndicho tunachofanya.
-
2:35 - 2:39Ni mfululizo tu wa makundi madogo,
-
2:39 - 2:42ambapo wanaume, wanawake, mashoga, wa
kawaida, wanandoa, wenye wenza, -
2:43 - 2:47wanaweza kuongelea kuhusu mtu wao
aliyekufa, -
2:47 - 2:48na kusema vile vitu
-
2:48 - 2:52ambavyo mtu mwingine kwenye maisha yao
hayuko tayari kuvisikia bado. -
2:52 - 2:54Eneo kubwa la mazungumzo.
-
2:54 - 2:56Kama, "Mme wangu alikufa wiki mbili
zilizopita, -
2:56 - 2:58siwezi kuacha kufikiria kuhusu
ngono, ni kawaida?" -
2:58 - 3:00Ndio.
-
3:00 - 3:02"Je kama ni mmoja wa
Property Brothers?" -
3:02 - 3:03Kawaida kidogo, ila nitaikubali.
-
3:03 - 3:06(Kicheko)
-
3:07 - 3:11Vitu kama, "Ona, nikiwa hadharani na
nikaona wazee wanashikana mikono, -
3:11 - 3:13wenzi ambao ni wazi wamekua
pamoja kwa miongo, -
3:13 - 3:16halafu ninawaangalia na kuwaza
-
3:16 - 3:18vitu vyote ambavyo wamepitia
pamoja, -
3:18 - 3:20vitu vizuri na vitu vibaya,
-
3:20 - 3:23ugomvi waliokuanao
kuhusu nani wa kutoa taka ... -
3:23 - 3:26nakuta tu moyo umejawa na hasira."
-
3:26 - 3:27(Kicheko)
-
3:27 - 3:29Na huo mfano ni wa pekee kwangu.
-
3:30 - 3:33Mazungumzo mengi ambayo
tunakuwa nayo kwenye kundi -
3:33 - 3:35yanaweza na yanakaa miongoni mwetu,
-
3:35 - 3:37lakini kuna vitu tunavyoviongelea
-
3:37 - 3:40ambavyo duniani --
dunia ambayo iko karibu na majonzi -
3:40 - 3:42ila bado haijapigwa na majonzi
-
3:42 - 3:44inaweza kweli kunufaika kusikia.
-
3:44 - 3:45Na kama huwezi kusema,
-
3:45 - 3:50ninavutiwa/uwezo tu wa
masomo yabbsiyo ya kisayansi, -
3:50 - 3:52nilienda kwenye
Chama cha Wajane Wadogo Wakali -
3:52 - 3:57na kusema, "Habari, marafiki, unakumbuka
mtu wako alivyokufa?" Walikumbuka. -
3:57 - 3:59"Unakumbuka vitu vyote watu
walikuambia?" -
3:59 - 4:00"Ah, ndio."
-
4:00 - 4:02"Ni vipi ulivyovichukia zaidi?"
-
4:02 - 4:05Nilipata maoni mengi, majibu mengi,
watu wanasema vitu vingi, -
4:05 - 4:08lakini viwili vilisimama juu haraka sana.
-
4:09 - 4:10"Kusonga mbele."
-
4:12 - 4:14Sasa, tangu 2014,
-
4:14 - 4:18nitakuambia nilifunga ndoa tena na
mwanaume mzuri kweli aitwae Matthew, -
4:18 - 4:21tuna watoto wanne
kwenye familia yetu iliyochanganyika, -
4:21 - 4:25tuniashi kwenye viunga
vya Minneapolis, Minnesota, Marekani. -
4:25 - 4:26Tuna mbwa aliyeokolewa.
-
4:26 - 4:28(Kicheko)
-
4:28 - 4:29ninaendesha gari la familia,
-
4:29 - 4:32kama la aina ambayo milango inafunguka
bila hata kuigusa. -
4:32 - 4:33(Kicheko)
-
4:33 - 4:36Kama, "mezhure" yoyte, maisha ni mazuri.
-
4:36 - 4:39Sijawahi pia kusema "mezhure,"
sijawahi hata mara moja kuisema hivyo. -
4:39 - 4:45(Kicheko)
-
4:45 - 4:46Sijui hata imetokea wapi.
-
4:46 - 4:48(Kicheko)
-
4:48 - 4:51Sijawahi kusikia mtu yeyote
akiisema hivyo. -
4:51 - 4:53Inaonekana kama inapaswa kusemwa hivyo,
-
4:53 - 4:55na ndio sababu lugha ya Kiingereza
ni mbovu, basi ... -
4:55 - 4:56(Kicheko)
-
4:56 - 4:58Ninavutiwa sana na mtu
ambae anaiongea -
4:58 - 5:01kuongezea kwenye lugha
inayoeleweka -- kazi nzuri. -
5:01 - 5:03(Kicheko)
-
5:03 - 5:05Lakini, kwa vyovote vile ...
-
5:05 - 5:06(Kicheko)
-
5:06 - 5:11Kwa vyovyote vile, maisha ni mazuri
sana sana, lakini "sijasonga mbele." -
5:12 - 5:15Sijasonga mbele,
na siupendi kabisa huo msemo, -
5:15 - 5:17na ninaelewa kwanini wengine hawaupendi.
-
5:17 - 5:18Kwa sababu unachosema
-
5:18 - 5:23ni kua maisha na kifo cha Aaron
na upendo ni wakati tu -
5:23 - 5:27ambao nauweza kuuacha nyuma yangu --
na kua napaswa kufanya hivyo. -
5:27 - 5:31Na ninapoongelea kuhusu Aaron,
ninaingia kirahisi kwenye hali halisi, -
5:31 - 5:33na nimewaza kweli kua hio inanifanya
wa ajabu. -
5:33 - 5:36Halafu nikagundua kua kila mtu anafanya
hivyo. -
5:37 - 5:41Na sio kwa sababu tuna kana
au kwa sababu tunasahau, -
5:41 - 5:43ni kwa sababu watu
tunaowapenda, tuliowapoteza, -
5:43 - 5:45bado ni halisi kwetu sisi.
-
5:47 - 5:49Basi, ninaposema, "Oh, Aaron ni ..."
-
5:50 - 5:53Ni kwa sababu Aaron bado yupo.
-
5:54 - 5:56Na sio kwa namna
alivyokua kabla. -
5:56 - 5:57iliyokua bora zaidi,
-
5:57 - 6:01na sio namna ambayo watu wa kanisani
wanavyojaribu kuniambia anavyokua. -
6:01 - 6:04ni kua tu amezimika,
-
6:05 - 6:08na hivyo yupo sasa kwangu.
-
6:09 - 6:10Hapa,
-
6:10 - 6:12yupo hapa kwenye kazi ninayofanya,
-
6:12 - 6:15kwenye mtoto tulionae pamoja,
-
6:15 - 6:17kwenye hawa watoto wengine watatu
ninaolea, -
6:17 - 6:20ambao hawajawahi kunuona,
ambao hawana DNA yake, -
6:20 - 6:23lakini wapo kwenye maisha yangu tu
kwa sababu nilikuwa na Aaron -
6:23 - 6:25na kwa sababu nilimpoteza Aaron.
-
6:26 - 6:29Yupo nami kwenye ndoa yangu na Matthew,
-
6:29 - 6:32kwa sababu maisha na upendo na kifo cha
Aaron -
6:32 - 6:35vimenifanya kua mtu ambae
Matthew angetaka kuoa. -
6:35 - 6:39Hivyo sijasonga mbele kutoka kwa Aaron,
-
6:39 - 6:42nimesonga mbele na yeye.
-
6:45 - 6:51(Makofi)
-
6:51 - 6:56Tulisambaza majivu ya Aaron
kwenye mto aupendao huko Minnesota, -
6:56 - 6:57na pale begi lilipokua tupu --
-
6:57 - 7:02kwa sababu ukiwa umechomwa,
unatoshea kwenye mfuko wa plastiki -- -
7:02 - 7:05kulikua na majibu bado
yamebaki kwenye vidole vyangu. -
7:05 - 7:08Na ningeingiza tu mikono yangu kwenye
maji na kuisuuza, -
7:08 - 7:11lakini badala lake, nililamba mikono
yangu, -
7:12 - 7:15kwa sababu niliogopa kupoteza zaidi
ya nilichopoteza zaidi, -
7:15 - 7:19na nilitamani sana kuhakikisha kua
atakua ni sehemu yangu daima. -
7:20 - 7:22Lakini bila shaka atakua.
-
7:23 - 7:27Kwa sababu unapomuona mtu wako
akijijaza na sumu kwa miaka mitatu, -
7:27 - 7:30ili tu aweze kuishi
zaidi kidogo na wewe, -
7:30 - 7:32hilo linakaa na wewe.
-
7:33 - 7:38Unapomuangalia akififia kutoka kwenye
mtu mwenye afya siku mliokutana -
7:38 - 7:39kuwa sifuri, hiyo inakaa na wewe.
-
7:39 - 7:42Unapomuangalia mwanao,
amba hata bado hana miaka miwili, -
7:42 - 7:45akienda kitandani kwa baba yake
siku ya mwisho ya maisha yake, -
7:45 - 7:47kama vile anajua kinachofuata
masaa machache, -
7:47 - 7:52na kusema, "Nakupenda. Nimemaliza.
Kwaheri." -
7:54 - 7:56Hiyo inakaa na wewe.
-
7:57 - 8:02Kama tu unapopenda,
hatimae, unapopenda kweli -
8:02 - 8:04mtu anaekuelewa na kukuona
-
8:04 - 8:08na unaona pia, "Mungu wangu,
nimekua nikikosea mda wote huu. -
8:08 - 8:12Upendo sio mashindano au
kipindi cha televisheni -- ni ukimya sana, -
8:12 - 8:16ni huu uzi usioonekana wa utulivu
unatuunganisha wawili -
8:16 - 8:18hata kama kila kitu kina vurugu,
-
8:18 - 8:21vitu vinapoenda vibaya,
hata kama akiondoka." -
8:22 - 8:25Hio inakaa na wewe.
-
8:27 - 8:28Tulikua tunafanya hivi --
-
8:28 - 8:31mikono yangu ilikua na
baridi na yeye ana joto, -
8:31 - 8:34nilichukua mikono yangu ya barafu
na kuisukuma ndani ya shati lake ... -
8:35 - 8:37kuikandamiza kwenye mwili wake mkali.
-
8:37 - 8:39(Kicheko)
-
8:39 - 8:42Na alikua hapendi kabisa,
-
8:42 - 8:43(Kicheko)
-
8:43 - 8:44lakini alinipenda,
-
8:44 - 8:49na alivyokufa,
nililala kitandani na Aaron -
8:49 - 8:52na nikaweka mikono yangu chini yake
-
8:53 - 8:56na nikahisi joto lake.
-
8:58 - 9:02Na sikuweza hata kusema kama
mikono yangu ilikua na baridi, -
9:02 - 9:03lakini ninaweza kuwaambia
-
9:03 - 9:06kua nilijua ilikua mara ya mwisho
ningeweza kufanya hivyo. -
9:08 - 9:11Na hio kumbukumbu
itakua ya kusikitisha daima. -
9:12 - 9:14Hio kumbukumbu itauma daima.
-
9:14 - 9:17Hata kama nikiwa na miaka 600
na ni hologramu tu. -
9:17 - 9:19(Kicheko)
-
9:20 - 9:26Kama tu kumbukumbu ya kukutana nae
itanifanya nicheke daima. -
9:28 - 9:30Maombolezo hayatokei kwenye huu
utupu, -
9:30 - 9:36yanatokea pamoja na na ikichanganyika
na hisia zote hizi nyingine. -
9:38 - 9:43Hivyo, nikakutana na Matthew, mme wangu wa
sasa -- -
9:43 - 9:44ambae hapendi hicho cheo,
-
9:44 - 9:48(Kicheko)
-
9:49 - 9:50lakini ni sawa kabisa.
-
9:50 - 9:53(Kicheko)
-
9:54 - 9:56Nilikutana na Matthew, na ...
-
9:58 - 10:01kulikua na hii pumzi ya wazi ya faraja
kati ya watu wanaonipenda, -
10:01 - 10:03kama, "Imekwisha!
-
10:05 - 10:06Ameweza.
-
10:07 - 10:10Amepata mwisho mzuri,
tunaweza kurudi nyumbani sasa. -
10:10 - 10:12Na tumefanya vizuri."
-
10:12 - 10:15Na hio hadithi inafaa hata
hata kwangu, -
10:15 - 10:18na nikawaza labda nimeipata
hio pia, lakini haikua hivyo. -
10:18 - 10:21Nilipata sura nyingine.
-
10:21 - 10:25Na ni sura nzuri sana --
nakupenda, mpenzi -- -
10:25 - 10:27ni sura nzuri sana.
-
10:27 - 10:31Tena haswahaswa mwanzoni,
ilikua kama ulimwengu mbadala, -
10:31 - 10:34au moja ya vile vitabu ya zamani vya
"chagua shani yako" vya miaka ya 80 -
10:34 - 10:36ambapo kuna mistari miwili sambamba.
-
10:36 - 10:38Nikafungua moyo wangu kwa
Matthew, -
10:38 - 10:42na ubongo wangu ukawa,
"Ungependa kumfikiria Aaron? -
10:42 - 10:46Kama zamani, sasa, mbeleni,
ingia tu huko," na nilifanya hivyo. -
10:47 - 10:50Na ghafla,
hiyo mistari miwili ilifunguka kwa pamoja, -
10:50 - 10:54na kupendana na Matthew kumenisaidia
sana kugundua ukubwa -
10:54 - 10:56wa nilichopoteza Aaron alivyofariki.
-
10:58 - 10:59Na ilivyo muhimu,
-
10:59 - 11:03ilinisaidia kugundua kua upendo wangu
kwa Aaron -
11:03 - 11:05na maombolezo yangu kwa Aaron,
-
11:05 - 11:09na upendo wangu kwa Matthew,
sio nguvu za kupishana. -
11:11 - 11:13Ni sehemu tu za uzi mmoja
-
11:14 - 11:16Ni vitu sawa sawa.
-
11:18 - 11:21Wazazi wangu wangesemaje?
-
11:21 - 11:23Mimi sio wa pekee.
-
11:24 - 11:25(Kicheko)
-
11:25 - 11:27Walikua na watoto wanne,
walikua kama ... wa kweli. -
11:27 - 11:29(Kicheko)
-
11:29 - 11:31Lakini mimi sio, mimi sio wa pekee.
-
11:31 - 11:33Ninajua hilo, ninajua vizuri
-
11:33 - 11:35kua siku nzima, kila siku
duniani kote, -
11:35 - 11:37vitu vibaya vinatokea.
-
11:37 - 11:38Kila mara.
-
11:38 - 11:40Kama nilivyosema, mtu mcheshi.
-
11:40 - 11:43Lakini vitu vibaya vinatokea,
-
11:43 - 11:49watu wanapata hasara za kina na mbaya
kila siku. -
11:49 - 11:52Na kama sehemu ya kazi yangu,
-
11:52 - 11:53hii podikasti ya ajabu niliyonayo,
-
11:53 - 11:55kuna mda ninaongea na watu
-
11:55 - 11:58kuhusu kitu kibaya
kilichowahi kuwatokea. -
11:58 - 12:01Na saa nyingine, hio ni
kupotelewa na mpendwa, -
12:01 - 12:05mara nyingine siku, wiki miaka
au miongo iliyopita. -
12:06 - 12:09Na hawa watu ninaowahoji,
-
12:09 - 12:11hawajajifungia wenyewe
kwenye hii hasara -
12:11 - 12:14na kuifanya sehemu kuu ya maisha yao.
-
12:14 - 12:18Wameishi, dunia zao
zimeendelea kuzunguka. -
12:19 - 12:23Lakini wanaongea na mimi,
mgeni kabisa, -
12:23 - 12:25kuhusu mtu wanaempenda aliyekufa,
-
12:25 - 12:28kwa sababu hivi ndivyo vitu tunavyopitia
-
12:28 - 12:33vinavyotuonyesha na kutufanya
kama tu wale wenye furaha. -
12:33 - 12:35Na kama ilivyo ya kudumu.
-
12:37 - 12:39Baadae baada ya kupata kadi yako
ya mwisho ya huruma -
12:39 - 12:41au pishi la moto la mwisho.
-
12:42 - 12:44Kama, hatuangalii watu
wanaotuzunguka -
12:44 - 12:48wakipitia furaha na maajabu ya maisha
na kuwaambia "wasonge mbele", ndio? -
12:48 - 12:52Hatutumi kadi ambazo zinasema
"Hongera kwa mtoto mzuri," -
12:52 - 12:55halafu, miaka mitano baadae, tunawaza,
"Sherehe nyingine ya kuzaliwa? Acha hizo." -
12:55 - 12:57(Kicheko)
-
12:57 - 12:59Ndio, tunaelewa, ana miaka mitano.
-
12:59 - 13:00(Kicheko)
-
13:00 - 13:01Wow.
-
13:01 - 13:03(Kicheko)
-
13:04 - 13:06Lakini maombolezo ni moja ya vile vitu,
-
13:06 - 13:10kama kupenda au kuwa na mtoto
au kuangalia "The Wire" kwenye HBO, -
13:10 - 13:14ambapo hauelewi
mpaka upate, mpaka ufanye. -
13:15 - 13:21Na punde unavyofanya,
punde ni mpenzi wako au mtoto wako, -
13:21 - 13:26punde ni maombolezo yako
na uko mstari wa mbele kwenye msiba, -
13:26 - 13:27unaelewa.
-
13:27 - 13:31Unaelewa unachopitia sio
sehemu ya mda, -
13:31 - 13:33sio mfupa kua utajirudi,
-
13:33 - 13:36lakini kua umeguswa na kitu kikali.
-
13:37 - 13:38Kitu kisichotibika.
-
13:38 - 13:41Hakiui, lakini saa nyingine
yanakua kama yanaweza. -
13:43 - 13:47Na kama hatuwezi kuzuia miongoni mwetu,
-
13:47 - 13:48nini tunaweza kufanya?
-
13:51 - 13:55Nini tunaweza kufanya zaidi ya
kukumbushiana -
13:55 - 13:58kua vitu vingine havirekebishiki,
-
13:58 - 14:01na sio kila kidonda kinapaswa kupona.
-
14:02 - 14:06Tunahitajiana kukumbuka,
-
14:06 - 14:07kusaidiana kukumbuka,
-
14:07 - 14:10kua maombolezo ni hisia ya mambo mengi.
-
14:10 - 14:16Kua unaweza na utakua na huzuni, na
furaha; utaomboleza na kupenda -
14:16 - 14:19kwenye mwaka au wiki au pumzi hio hio.
-
14:21 - 14:27Tunahitaji kukumbuka kua mtu anaeomboleza
ataenda kucheka na kutabasamu tena. -
14:27 - 14:31Wakibahatika,
wanaweza hata kupenda tena. -
14:32 - 14:35Lakini ndio, hakika
wataenda kusonga mbele. -
14:36 - 14:39Lakini hiyo haimaanishi kua
wameendelea mbele. -
14:40 - 14:41Asanteni.
-
14:41 - 14:48(Makofi)
- Title:
- "Hatusongi mbele" kwenye maombolezo. Tunaendelea nayo mbele
- Speaker:
- Nora Mclnerny
- Description:
-
Kwenye maongezi ambayo yanapishana kwa kusikitisha na kuchekesha, mwandishi na mwanapodikasti Nora Mclnerny anashirikisha busara yake iliyopatikana kwa shida kuhusu maisha na kifo. Mtazamo wake wa wazi kwenye kitu ambacho, kwa kweli, kitatuathiri wote, ambacho ni huru na ni kigumu. Kwa nguvu zaidi, anatusisitizia kubadili jinsi tunavyoona maombolezo. "Mtu anaeomboleza ataenda kucheka na kutabasamu tena," anasema. "Wataenda kusonga mbele. Lakini haimaanishi wameendelea mbele."
- Video Language:
- English
- Team:
- closed TED
- Project:
- TEDTalks
- Duration:
- 15:05
Nelson Simfukwe approved Swahili subtitles for We don't "move on" from grief. We move forward with it | ||
Julieth Mbeyella accepted Swahili subtitles for We don't "move on" from grief. We move forward with it | ||
Julieth Mbeyella edited Swahili subtitles for We don't "move on" from grief. We move forward with it | ||
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for We don't "move on" from grief. We move forward with it | ||
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for We don't "move on" from grief. We move forward with it | ||
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for We don't "move on" from grief. We move forward with it | ||
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for We don't "move on" from grief. We move forward with it | ||
Doris Mangalu edited Swahili subtitles for We don't "move on" from grief. We move forward with it |